02-01
bustani
Ni sehemu maalum yenye kila aina ya miti na mimea ambayo Mungu aliandaa kwa Adamu na Hawa kufurahia na kula mahali hapo.
kuongea na Mungu
Neno "kuongea" ni kama lile la kuongea na mtu. Mungu huenda alivaa sura ya mwanadamu ili aweze kuongea na mwanaume na mwanamke kwani kifunguu hii kilionyesha kuwa waliongea uso kwa uso.
haya
Ni hisia inayokuja kwa kujua kuwa tumefanya dhambi au tumepungukiwa kwa namna fulani.
02-02
mwerevu
Mjanja na mwerevu, mwenye nia ya kudanganya.
nyoka
Ni mnyama wa ardhini mrefu, asiye na miguu anayetembea kwa kutambaa kwa tumbo lake. Hataivyo katika historia hii ilidhihirika kwamba nyoka ni Shetani, hataivyo kwenye kipengele hii haitajulikana hivyo.
Je, ni kweli Mungu alikuambia
Nyoka alimuuliza mwanamke kama ni kweli Mungu aliwaambia wasile katika mti wowote ndani ya bustani. Lakini alikuwa akijifanya hajui Mungu alisema nini kwa sababu alitaka kujenga shaka kwenye ufahamu wa mwanamke. Alitaka yeye aweke ulizo au shaka juu ya wema wa Mungu.
matunda ya mti wowote
Aina zote za matunda kutoka kwa kila aina ya mti ndani ya bustani.
02-03
matunda
Hatufahamu ilikuwa ni aina gani ya matunda. Tunafahamu tu kwamba ni tunda lililokuwa kwenye mti. Kwa hapa yafaa kutumia neno la jumla la tunda na siyo tunda fulani maalum.
mti wa ujuzi wa mema na mabaya
Mwanamke alijua kwa hakika kuwa hawaruhusiwi kula matunda kutoka katika mti huo ambao utawafanya wajue mema na mabaya.
mtakufa
Tumia neno lako la kawaida ya kufa, ni hali ya kufikia uko kwa maisha haya ya kimwili. usikwepe neno hili kwa sababu wazo la kifo linatisha.
02-04
kama Mungu
Mwanaume na mwanamke tayari wamefanywa kwa namna na sura ya Mungu. Nyoka anashauri kuwa mwanamke atakuwa kama Mungu zaidi kama akijua mabaya. Hata hivyo Mungu hakukusudia yeye kuwa na ufahamu huu.
kujua mema na mabaya
Kujua kwa njia ya uzoefu mambo yaliyo mema na mambo yaliyo mabaya, au kuwa na uwezo wa kujua kuwa jambo ni jema au baya.
02-05
hekima
Mwanamke alitamani kuwa na uelewa na ufahamu kama nyoka anavyoonekana kuwa nayo, na kama aliyonayo Mungu.
aliyekuwa pamoja naye
Hii ni habari muhimu kwani inaonyesha kuwa mwanaume alikuwepo wakati hawa anafanya maamuzi ya kula tunda.
02-06
mara macho yao yakafunguliwa
Hii inaweza kutafsiriwa kuwa "waliona vitu kwa namna ya tofauti." Inaonyesha kuwa walijua kitu kwa mara ya kwanza. Katika lugha yenu unaweza kuwa na namna vyingine ya kuelezea hali hii.
wakagundua kwamba walikuwa uchi
Baada ya Mwanaume na Mwanamke kutokumtii Mungu, waliona aibu kwa kuwa uchi. Ndiyo maana walijaribu kujifunika miili yao kwa kuvaa majani ya miti.
kuficha miili yao
Mwanaume na mwanamke walijaribu kujifunika kwa kutumia majani ili kujificha mbele za Mungu.
02-07
Mungu akitembea
Inaonekana kuwa Mungu alikuja mara kwa mara kuwatembelea Mwanaume na Mwanamke bustanini. Hatufahamu hili lilionekanaje. Kama inawezekana ni vizuri kutumia neno linalotumika kuelezea mtu anapotembea.
Uko wapi?
Mungu tayari alijua majibu ya swali hilo. Kusudi la swali hili ni kumfanya mwanume na mwanamke waeleze kwanini wanajificha.
02-08
Nani aliyekuambia kuwa uko uchi?
Au "Ulijuaje kuwa uko uchi?" Mungu tayari alijua majibu ya maswali yote. Kwa kuuliza maswali na kufuatilia alikuwa anampa Adamu nafasi ya kukiri dhambi yake ya kutokutii. Kuwa uchi siyo dhambi kwani Mungu aliwaumba hivyo. Ufahamu wao juu ya kuwa uchi ndiyo tatizo. Aibu yao ilionyesha kuwa walikuwa wametenda dhambi.
amenipa tunda
Mwanaume alimlaumu mwanake badala ya kutubu kwa kutokutii na kuwajibika kwa kutokumtii Mungu.
ulifanya nini?
Au "Kwanini umefanya haya?" Mungu tayari alijua majibu ya swali hilo. Kwa kuuliza swali hili, alikuwa akimpa nafasi mwanamke akubali kosa lake. Pia Mungu alimaanisha kuwa asingefanya kile alichokifanya.
Nyoka alinidanganya
Nyoka alinidanganya au alinipotosha. Nyoka alimuambia uongo. Usitumie neno linaloonyesha kama vile alimlogo au kuwa alimpa kitu kilichompofusha macho au kumfanya akili yake achanganyikiwe na kuamua bila yeye kujua. Mwanamke alimlaumu nyoka badala ya kutubu kosa lake la kutotii na kukubali kuwajibika kwa kutomtii Mungu.
02-09
Umelaaniwa
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "Nimekulaani wewe" au "Tatizo baya litakujia." Usitumie neno lenye kuashiria uchawi.
mtakuwa maadui
Mwanamke atamchukia nyoka na nyoka atamchukia mwanamke. Na uzao wa mwanamke utachukia uzao wa nyoka na uzao wa nyoka utachukia uzao wa mwanamke.
uzao wa mwanamke
Inamaanisha moja wa uzao wake.
utakuponda kichwa
Uzao wa mwanamke utaharibu (kuuwa) uzao wa nyoka.
utamgonga kisigino
Uzao wa nyoka utamjeruhi uzao wa mwanamke kwenye kisigino.
02-10
nitaongeza uchungu wakati wa kuzaa kwako
Huenda lugha nyingine zinahitaji kueleea hii kama kitenzi. Unaweza kusema, "Nitakufanya usikie uchungu mkubwa wakati wa kujifungua."
02-11
ardhi imelaaniwa
Kama adhabu kwa kutokutii kwa Adamu, ardhi haitatoa tena matunda. Itampasa Adamu kufanya kazi kwa nguvu nyingi ili apate chakula ya kula.
utakufa
Mwisho wa adhabu yao ni kifo. Kifo cha kiroho ni utengano wa sisi na Mungu. Kifo cha kimwili ni utengano na miili yetu.
utarudi katika uchafu
Mungu alimtengeneza Adamu katika mavumbi au uchafu na kumpa maisha. Kwa sababu ya dhambi, maisha yake yatachukuliwa kutoka kwake na mwili wake utaoza na kurudia kwenye uchafu tena.
Hawa, yenye kumaanisha "mtoa maisha"
Mungu alimpa uhai Adamu na Hawa, na uhai huo walipewa vizazi vyote kwa njia ya kuzaliwa (kuzaliwa kwa watoto).
Mama wawatu wote
Hii inamaana kuwa atakuwa mama wa kwanza kwa vizazi vyote vya watu. Lugha nyingine zinasema "atakuwa bibi" wa watu wote e
02-12
kama sisi kwa kujua mema na mabaya
Maneno haya, yanaonyesha namna mpya ambayo Adamu na Hawa watakuwa kama Mungu. Kwasababu wamefanya dhambi, wanajua mabaya na wanaweza kufanya. Unaweza kusema "kwasababu sasa wanajua mema na mabaya."
tunda
Ni aina ya tunda ambayo haukujulishwa au kuelezwa, kwa hiyo yafaa itafsiriwe kama tunda.
mti wa uzima
Huu ni mti halisi wenye matunda.