Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

07-01

Alipenda kukaa nyumbani ... alipenda kuwinda

Lugha nyingine hutumia neno "kupenda" ambavyo ni tofauti na ilivyotumika hapa, "Rebeka alimpenda Yakobo." Kwa mfano hii inaweza kutafasiriwa kama "alipenda kukaa nyumbani" ... "alipenda kuwinda" au "alipendelea kukaa nyumbani" ... "alipendelea kuwinda."

Nyumbani

Maelezo haya yanaelezea ni eneo ambalo familia wanaishi. Yakobo alipenda kukaa karibu na hema sehemu walipoishi. Lugha nyingine zina maelezo ya kipekee juu ya "nyumba."

Rebeka alimpenda Yakobo, ila Isaka alimpenda Esau.

Hii inaweza kutafasiriwa kama "Rebeka alimpenda sana Yakobo na Isaka alimpenda sana Esau." Hii haimaanishi kuwa Rebeka na Isaka hawakumpenda mtoto mwingine lakini kila mzazi alikua naupendeleo wake.

07-02

Nipe mimi sehemu ya chakula ... nipe mimi haki zako

lugha nyingine zingependelea kutumia maneno mawili tofauti kwenye neno "nipe." Hii pia hutumika kama "Esau alimpa ... Yakobo alimpa" kwenye sentensi mbili za mwisho.

Haki kama mtoto mkubwa

Kutokana na desturi, kwa kuwa Esau alikua mtoto mkubwa, alipaswa kupokea mara mbili ya utajiri wa baba yake endapo baba yao atafariki. Ykobo alitafta njia ya kuchukua haki za mtoto wa kwanza toka kwa Esau.

07-03

Akampa baraka zake

Ilikua desturi kwa baba kuelezea shauku zao juu ya mambo mema yatakayotokea kwa watoto wao. Kwa kawaida mtoto mkubwa anapokea ahadi nzuri. Isaka alitaka baraka zaidi zitokee kwa Esau.

Alimdanganya kwa hila

Neno "hila" inamaanisha kufanya jambo kwa ajili ya kumdanganya mtu. Rebeka alikuja na mpango wa kumlaghai Isaka ampe Yakobo baraka ya pekee badala ya Esau.

Kuigiza

Neno "kuigiza" linaonesha namna ambavyo Yakobo alimdanganya baba yake (aliyekua na uwezo mdogo wa kuona kutokana na umri wake kuwa mkubwa).

Ngozi ya mbuzi

Manyoya yaliyopo katika ngozi ya mbuzi yalingemfanya Yakobo aonekane kama Esau.

07-04

Yakobo akaja kwa Isaka

Kwenye lugha zingine inaweza kuwa na uhalisia zaidi kwa kusema "Jakobo alikwenda kwa Isaka."

Alidhani kuwa ni Esau.

Alidhani kuwa mtu aliyemshika na kusikia harufu yake alikua Esau.

07-05

Haki kama mtoto wa kwanza

Yakobo alitafta namna ya kupata sehemu kubwa ya mali ya baba yake iliyotakiwa kwenda kwa Esau kama mtoto wa kwanza.

Baraka yake.

Yakobo pia alimlaghai baba yao katika kumpa yeye ahadi ya utajiri wa baraka ya kipekee ambayo Isaka alikusudia kumpa Esau.

07-06

Mpango ya Esau

Mpango wa Esau ulikua ni kumuua Yakobo baada ya kifo cha baba yake.

Rebeka na Isaka wakamtuma Yakobo.

Rebeka alitaka kumlinda Yakobo toka kwa Esau hivyo akaongea na Isaka juu ya kumtuma yakobo aende zake.

kwenda mbali kuishi na ndugu zake

Hii ilikua sehemu ile ile ambayo Rebeka aliishi kipindi ambacho mtumwa wa Ibrahamu alimchukua kuwa mke wa Isaka. Kuliweka hili wazi unaweza kuongeza kuwa "ndugu wa ardhi ile ile alipokua akiishi." Arhi ile ilikua mashariki, umbali wa maili mamia.

Ndugu zake

hii inaweza kutafsairikwa kama "ndugu zao" Kwa kuwa kaka yake na Abraham alikua babu yake na Rebeka, ndugu zake na Rebeka pia walikua ndugu wa Isaka.

07-07

Utajiri

Hii inajumuisha pesa, kundi kubwa ya wanyama na vyote alivyomiliki.

07-08

Baada ya miaka ishirini.

Yakobo aliishi miaka ishirini kwenye nchi aliyotoka mama yake. Kama hiyo haijaeleweka unaweza kusema "Baada ya miaka ishirini akiishi katika nchi ambayo ndugu zake waliishi pia."

07-09

Mtumishi wako Yakobo

Yakobo hakika hakua mtumishi wa Esau. lakini alimwambia watumishi wake kusema hivi kwa sababu alitaka kumuonyesha Esau kuwa alimwendea kwa unyenyekevu na heshima ili Esau asiendelee kua na hasira juu yake.

07-10

Waliishi kwa amani

Hii inaelezea kuwa Esau na Yakobo hawakukasirikiana na kugombana wao kwa wao.

Wakamzika

Hii inaweza kumaanisha kuwa walichimba shimo kwenye ardhi wakauweka mwili wa Isaka na kufunika shimo hilo kwa kutumia udongo au jiwe. au inaweza kumaanisha kuwa waliuweka mwili wa Isaka kwenye pango na kufunika sehemu ya wazi.

Agano la ahadi

Hizi ni ahadi alizozifanya Mungu kwenye agano lake na Ibrahamu.

Ikapita toka kwa Isaka kwenda kwa Yakobo

Ahadi zilizotoka kwa Ibrahamu kwenda kwa mwanawe Isaka na sasa twenda kwa Yakobo mtoto wa Isaka. Esau hakuzipokea ahadi.