Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

27-01

Siku moja

Hii sentensi inatoa utangulizi wa tukio ambalo lilitokea wakati ulio pita, ingawa halizungumzi muda maalumu. Lugha nyingi zinz nzmnz hii ya kuanza kusimulia simulizi ambayo ni kweli.

Mwalimu wa mambo ya sheria ya kiyahudi

Huyu ni mtu aliye fundishwa na kujifunza sheria za kiyahudi ambazo Mungu aliwapatia Israel paoja na zile sheria za kiyahudi.

Kumjaribu

Hii ni kuona kama, Yesu angeliweza kutoa jibu zuri."

Kurithi uzima wa milele

Hii ni "kuwa na maisha pamoja na Mungu milele" au , "ili kwamba Mungu anipatie maisha pamoja naye milele" au, kupokea uzima wa milele kutoka kwa Mungu." Mwalimu wa mambo ya sheria alikuwa anauliza jinsi gani angelistahili kupokea uzima wa milele kama urithi kutoka kwa Mungu baba.

Uzima wa milele

Hii inamaanisha maisha ya milele pamoja na Mungu baada ya mwili wa kuharibika kufa.

Nini kimeandikwa katika sheria ya Mungu?

Hii ni. "Nini kimeandikwa katika sheria ya Mungu kuhusu hili?Yesu aliuliza swali hili kwa sababu alitaka mtu huyu afikiri kuhusu nini hasa sheria ya Mungu inafundisha.

27-02

Mwalimu wa mambo ya sheria

Huyu ni mtu aliye soma na kufundishwa sheria za Mungu walizopewa waisrael pamoja na sheia zingine za kiyahudi.

Mpende Bwana Mungu wako

Unaweza kuchagua kusema, "Tunapaswakumpenda Bwana Mungu wetu," Hakikisha kuwa haita someka kuwa mtu yule alikuwa amamwamrisha Yesu. Badala yake ananukuu nini ambacho sheria ya Mungu inawataka watu wafanye.

Kwa moyo wako, nafsi, nguvu, na akili

Hii ni kumaanisha "utu wote wa mtu" kila sehemu ya utu wako" katika baadhi ya lugha hii inaweza kutafsiriwa kama, "kwa ini lako, kwa pumzi zako kwa nguvu zako, na kwa mawazo yako." mtazamo si katika kila sehemu hizi, isipokuwa sisi katika utu wetu wote. tumia dhana katika lugha yako ambayo itafanya ieleweke kuwa ni mtu kwa ujumla wake.

Moyo

Hii ni sehemu ya mtu ambayo ina utashi na hisia

Nafsi

Nafsi inamaanisha ile sehemu isiyo na mwili, sehemu ya kiroho ya mtu.

Nguvu

Nguvu inamaanisha mwili halisi pamoja na uwezo wake wote.

Akili

Akili inamaanisha sehemu ya mtu ambayo hufikiri, hupanga, na kutengeneza mawazo.

Jirani

Neno "Jirani" kwa kawaida humaanisha mtu anayeishi karibu nasi. Kwa wayahudi walitumia neno hili si tu kwa mtu aliye karibu, bali kwa ndugu, mgeni au adui.

Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe

Hii inamaana, "mpende jirani yako kwa kiwango kilekile unachojipenda wewe mwenyewe."

27-03

Mwalimu wa mambo ya sheria

Huyu ni mtu aliye soma na kufundishwa sheria za Mungu walizopewa waisrael pamoja na sheia zingine za kiyahudi.

Jirani yangu ni nani?

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "unamaana gani unaposema jirani?" au. "ni watu gani ni majirani zangu?" Alijua kuwa hakuwapenda kila mtu, naalikuwa anauliza ni watu gani alihitajika kuwapenda.

27-04

Mtaalam wa sheria

Huyu ni mtu aliye soma na kufundishwa sheria za Mungu walizopewa waisrael pamoja na sheia zingine za kiyahudi.

Kutoka Yerusalem kwenda Yeriko

Kwa baadhi ya lugha unaweza kutafsiri hii kama, "kutoka katika mji wa Yerusalem kwenda mjiwa Yeriko" au, "kutoka mji wa Yerusalem hadi mji wa Yeriko."

27-05

kilakitu alichokuwa nacho

Hii ni kwamba, " kilakitu alichokuwa nacho, pamoja na nguo alizokuwa amevaa."

27-06

Alipita katika barabara hiyo

Hii ni kwamba, "ilitokea akipita katika njia ile." kwa lugha zingine inaweza kulazimika kutumia neno kama," kusafiri" badala ya kupita au kutembea kwa kuwa kuhani alikuwa hatembei tu barabarani lakini alikuwa anasafiri kwenda mji mwingine.

Hakumjali

Hii ni kwamba, "Hakumsaidia mtu yule" au alionesha kutohusika kwa shida ya mtu yule."

Aliendelea kwenda

Hii ni kwamba, "Aliendelea kusafiri barabarani."

27-07

alipita barabara hiyohiyo

Hii ni kwamba, Alikuwa anasafiri kwenye barabara hiyo hiyo

Walawi walikuwa kabila la Wayahudi

Hii ni, "Walawi walikuwa wanatokana nakabila ya Waisrael ya Lawi" au, Walawi walikuwa wanatokana na waisrael katika ukoo wa Lawi."

Bila kujali

Hii ni kwamba, "Hakumsaidia."

27-08

pita barabara

Hii ni, kusafiri" Hawa watu walikuwa wanasafiri kutoka katika mji mmoja kwenda mwingine. hakikisha kwamba isionekane kwamba walikuwa wanazungukazunguka tu.

27-09

Punda wake

Hakikisha kuwa neno wake inamaanisha Msamaria.

Nyumba ya wageni

Hii ni," Mahali wageni wanafika kulala" hii ni sehemu ambayo wasafiri wangeweza kupata chakula na kupumzika usiku.

Mahali ambapo alimuhudumia

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "Mahali ambapo aliendelea kumuhudumia."

27-10

aliendelea na safari yake

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Aliendelea kuafiri na kufika mwisho wa safari yake."

Mwangalizi

Huyi ni mtu "ambaye alisimamia." Inaweza kuwa kwamba mtu huyu pia alikuwa anamiliki sehemu ya kulala wageni.

Kumtunza

Kwa lugha zingine ingependelewa kusema, "Tafadhari mtunze" ili kwamba ijulikane wazi kuwa hilimlilikuwa ni ombi la kumsihi, na si amri.

Kulipa zaidi gharama hizo

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "kukulipa tena" au, "kulipa tena fedha hiyo" au, "kuilipa"

27-11

Mwalimu wa sheria

Huyu ni "mtaalamu wa sheria katika sheria ya kiyahudi."

Watu watatu

watu watatu walikuwa ni, Kuhani, Mlawi, na Msamalia.

Jirani

Yesu anatumia neno "Jirani" katikaile maana pana, "Jirani" inamaanisha mtu yeyote tunayekutana naye akiwa anahitaji msaada wetu.

Alikuwa jirani

Hii inweza pia kutafsiriwa kama, "Aliye kuwa na tabia za jirani" au, "Alikuwa rafiki" au, "alifanya kwa upendo".

Nenda na ufanye

Hii ni kwamba,, "wewe pia nenda ukafanye hivyo" au, "sasa lazima ufanye." Yesu alikuwa anamwamrisha mtaalamu wa sheria kufanya kama msamalia alivyo fanya.

Fanya hivyo

Hii ni kwamba, "Wapende wengine hata wale ambao ni adui zako." hakikisha tu kwamba isomeke kuwa inamaanisha kumsaidia mtu aliye umizwa.