Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

05-01

bado hakuwa na mtoto

bila mtoto, Abramu hakuwa na uzao wa kumfanya yeye kuwa taifa kubwa.

Amuoe naye pia

Abramu angemchukua Hagai kuwa mke wake wa pili, lakini Hagai asingekuwa mke halali wa Abramu kama alivyokuwa Sarai. Bado alikuwa mtumishi wa Sarai.

upate mtoto kwa ajili yangu

Kwa kuwa Hagai alikuwa mtumishi wa Sarai, basi Sarai angehesabiwa kuwa ndiye mama wa mtoto ambaye angezaliwa.

05-02

ameolewa

Hagai akawa suria wa Abramu - mke wa pili kisheria. Lakini Hagai bado alikuwa mtumishi wa Sarai.

alimuonea Hagai wivu

Sarai alimuonea Hagai wivu kwa sababu alipata mtoto na yeye asingeweza kupata mtoto.

05-03

baba wa mataifa mengi

Abramu angekuwa na uzao mkubwa na wangekuwa na ardhi yao na kujiongoza wenyewe.

Nitakuwa Mungu wao

Njia nyngine ya kusema hili ni, "Nitakuwa kwao Mungu watakayemwabudu."

kila mtu mme katika familia

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kila kijana na mwanaume katika familia yako."

05-04

mtoto wa ahadi

Isaka alikuwa mtoto ambaye Mungu aliwaahidia Sarai na Abramu. Na pia atakuwa mtoto ambaye Abramu atapata uzao mwingi kwake

Nitafanya agano langu na yeye

Hili litakuwa agano sawa na lile ambalo Mungu alifanya na Abramu.

baba wa wengi

Kama Mungu alivyoahidi, Abrahamu atakuwa baba wa watu wengi ambao pia watakuwa mataifa mengi.

Binti wa mfalme

Majina ya Sarai na Hagai yote yalikuwa na maana sawa yaani "Binti wa mfalme."

05-05

wanaume wote wa nyumbani kwake

Hii ina maana ya wanaume na wavulana wote ambao Abrahamu aliwatunza pamoja na watumishi wake wote wa kiume, wadogo kwa wakubwa.

05-06

Mungu aliijaribu imani ya Abrahamu

Mungu alitaka Abrahamu aoneshe ya kuwa amejitoa kikamilifu kwa kwake, na kwamba angetii chochote ambacho Mungu angemwambia.

Muue

Mungu hakutaka sadaka ya kutekezwa ya mtu. Mungu alitaka kuona ya kuwa Abrahamu alimpenda Mungu zaidi kuliko mtoto wake.

alijiandaa kutoa sadaka ya kuteketezwa

Abrahamu alijiandaa kumtoa mwanae kuwa sadaka ya kuteketezwa. Mungu alimzuia kabla hajamuua kijana wake.

05-07

alitembea kwenda eneo la kutolea sadaka

Mungu alimwagiza Abrahamu akamtoe Isaka sadaka juu ya mlima maalumu ambao ulikuwa umbali wa mwendo wa siku tatu kutoka alikokuwa anaishi.

kuni kwa ajili ya sadaka

Kawaida, kondoo aliuawa kwa ajili ya sadaka na kuwekwa juu ya kuni ili kwamba kuni na sadaka viungue pamoja.

mwanakondoo

mwanakondoo au mbuzi ndiyo walikuwa wanyama wanaostahili kwa sadaka.

atajipatia

Yawezekana Abrahamu aliamini kuwa Isaka ndiye alikuwa badala ya "mwanakondoo" ambaye Mungu alimpatia. Hata hivyo Mungu alitimiza maneno ya Abrahamu kwa kumpatia mwanakondoo kwa ajili ya sadaka.

05-08

kumuua kijana wake

Mungu hakutaka sadaka ya binadamu bali alimpima Abrahamu kujua imani yake.

Acha? usimdhuru kijana!

Mungu alimlinda Isaka na akamkinga Abrahamu asimdhuru.

unaniogopa

Abrahamu alimwogopa Mungu. Hii ilijumuisha heshima na uchaji wa Mungu. Kwa sababu ya mambo hayo, alimtii Mungu.

kijana wako wa pekee

Ishimaeli pia alikuwa mtoto wa Abrahamu, lakini Isaka ndiye alikuwa mtoto wa Abrahamu na Sarai. Agano la Mungu na Abrahamu lilikuwa juu ya Isaka.

05-09

Mwanambuzi

Mwanambuzi ni mbuzi dume.

Mungu alimpatia mwanambuzi

Kwa muda muafaka, Mungu alimleta mwanambuzi aliyenaswa kwenye kichaka.

05-10

Mwanao wa pekee

Isaka ndiye alikuwa mtoto pekee wa Abrahamu na Sarai.

nyota za angani

uzao wa Abrahamu ungekuwa kama nyota angani, hauhesabiki

familia zote duniani

neno "familia" hapa linamaanisha kundi fulani la watu duniani, licha ya wazazi na watoto.

umebarikiwa kupitia familia yako

hapa familia ina maana ya uzao mkubwa ambao Abrahamu angepewa.