14-01
nguzo ya Wingu
Ona ni jinsi gani unaweza kutafsiriwa huu msemo katika (12-1)
14-03
Ondoa
Hii inaweza kutafsiriwa kama, 'wapate kutoka nje ya nchi' au, 'kuwaondoa wao kwenye nchi.
msifanye amani pamoja nao
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Msiishi kwa amani miongoni mwao au pamoja nao" au, " haukuahidi kuishi kwa amani pamoja nao".
msioane nao
Mungu hakutaka mtu yeyote wa Israeli kuoana na Mkanaani.
mtaabudu miungu yao
Kama Waisraeli wakiwa marafiki na Wakanaani na hawakuharibu sanamu zao, wataweza kujaribiwa na kuabudu sanamu badala ya Mungu. Unaweza kusema, "itakuwa mwisho wao kuabudu" ili kuweka wazi kwamba hii itapelekea au itasababishwa na kuishi karibu na Wakanaani na kujifunza njia zao.
14-04
kupeleleza Nchi
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kwa siri kupata taarifa kuhusu nchi" au, "siri kujifunza kuhusu nchi". Sehemu ya kazi ya wapelelezi ilikuwa kujua ni aina gani ya chakula nchi inaweza kuzalisha.
peleleza Kanaani
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kwa siri kupata taarifa kuhusu watu wa Kanaani" au, kwa siri kujifunza kuhusu Wakanaani".
ili kuona kama walikuwa na nguvu au dhaifu
Walitaka kujua kama Wakanaani wamejiandaa kupigana nao. Hii inaweza kutafsiriwa kama, "ili kujua ni nguvu ya kiasi gani majeshi ya Mkanaani walikuwa nayo"
14-05
walirudi
Walirudi ambapo wengine wa Waisraeli walikuwa wakisubiri nje kidogo ya mpaka wa Kanani.
Miji ina nguvu sana
mji ulikuwa na ukuta imara unaoizunguka, hivyo itakuwa vigumu sana kwa Waisraeli kuwashambulia
watu wana maumbo makubwa
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "watu ni kama majitu ukilinganisha na sisi!" au, "watu ni warefu sana na wenye nguvu kuliko tulivyo!"
14-06
watu wa Kanaani
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "watu ambao wanaishi Kanaani" au, "Wakanaani."
kwa hakika tutashinda.! Mungu atatupigania
Kuonyesha uhusiano kati ya kauli hizi mbili, inaweza kuwa muhimu kusema, 'kwa hakika tunaweza kuwashinda kwa sababu Mungu atatupigania!'
Mungu atatupigania
Hii inaweza kutafsiriwa kama: "Mungu atapambana pamoja nasi na kutusaidia kuwashinda wao! ' Hii inaonesha wazi kwamba Waisraeli pia watapigana dhidi ya Wakanaani.
14-07
kwa nini ulituleta sisi
Hili sio swali halisi. Ni njia kwamba baadhi ya lugha hutumia kusema, 'hukupaswa kutuleta sisi.'
mahali hapa pa ovyo
Wao waliichukulia Kanaani kuwa 'ovyo' kwa sababu wao walidhani ilikuwa hatari kwamba wangeweza wote kuuawa.
badala ya kuuawa katika vita na wake zetu na watoto kufanywa watumwa
Hii inaweza kutafsiriwa kama, 'Kama sisi tukipigana na hao Wakanaani, na kutuua wanaume na kuwalazimisha wake zetu na watoto kuwa watumwa wao.'
14-08
alikuja
Mungu hakuonekana kama mtu, lakini alikuja kwa njia nyingine ambayo ilioesha utukufu wake na nguvu.
Kutangatanga Jangwani
Mungu angeweza kuwaongoza watu katika jangwa bila mwelekeo maalumu mpaka watu wazima ambao walimwasi wafe.
14-09
walitenda Dhambi
Inaweza kuwa muhimu kuongeza, 'walikuwa wamefanya dhambi kwa kutotii amri za Mungu za kuwashinda watu wa Kanaani.'
Musa aliwaonya wao wasiende
Hii ina maana kwamba Musa aliwaambia wasiende kupigana na Wakanaani kwasababu wangekuwa katika hatari kama wangefanya hivyo.
Mungu hakuwa pamoja nao
Kwa maneno mengine, Mungu hakuwa pamoja nao ili kuwasaidia. Kwa sababu ya kutotii kwao, Mungu aliwaacha Waisraeli bila uwepo wake, ulinzi na nguvu.
lakini hawakutaka kumsikiliza
Hawakumtii Musa. Wakaenda kuwashambulia Wakanaani.
14-10
Mungu hakuenenda pamoja nao katika vita hii
Kwa maneno mengine, Mungu hakuwasaidia katika vita hii.
wakarudi kutoka Kanaani
Waliondoka Kanaani na kurudi nyikani ambapo walikuwako kabla.
walitangatanga Jangwani
Waliishi katika jangwa, na kwa pamoja walisogea kutoka sehemu moja hadi nyingine , ardhi kavu, kutafuta chakula na maji kwa ajili yao wenyewe na wanyama wao.
14-11
Mungu aliwahudumia
Hii inaweza kutafsiriwa kama, 'Mungu aliwapa kila kitu walichohitaji kwa chakula, maji, na maladhi.'
mkate kutoka mbinguni, ulioitwa 'mana'
Hiki ni chakula aina ya mkate mwembamba ulishuka kutoka mbinguni mara moja kwenye majani kama umande. Uliitwa 'mana'. Karibu kila siku watu waliipata hii 'mana' na kuipika kama chakula chao.
Pia alituma makundi ya kware
Njia nyingine ya kusema hii itakuwa, 'Yeye pia alisababishwa idadi kubwa ya kware kuruka katika kambi yao.' Kama kware ni hawajulikani, tumia neno tofauti sawa na aina ya ndege inayoweza kutumika. Au inaweza kutafsiriwa kama, 'idadi kubwa ya ndege.'
Kambi yao
mahali ambapo Waisraeli waliweka hema zao kulala paliitwa 'kambi'. Ilikuwa ni kama mji na mahema badala ya majengo.
14-12
kimiujiza akawapa maji kutoka kwenye mwamba
Hii inaweza kutafsiriwa kama, 'kwa kufanya kitu ambacho Mungu tu anaweza kufanya, alifanya maji kumwagika kutoka kwenye mwamba hivyo watu na wanyama wakaweza kunywa.'
Lakini pamoja na yote hayo
Hii inaweza kutafsiriwa kama, 'Lakini, hata kama Mungu aliwapatia chakula, maji, mavazi, na kila kitu ambacho walihitaji.'
Hata hivyo
Hii inaweza kutafsiriwa kama, 'Japokuwa Waisraeli walilalamika na kunung'unika dhidi yake.'
Mungu bado alikuwa mwaminifu kwa ahadi zake
Hii inaweza kutafsiriwa hivi, 'Mungu aliendelea kufanya kama alivyomwambia Abrahamu, Isaka na Yakobo kuwa angefanya.' Alitoa kiza chao kama walivyohitaji hivyo kwamba wanaweza kuishi na kuwa taifa kubwa na hatimaye kumiliki nchi ya Kanaani.
14-13
Musa hakumheshimu Mungu
Hii inaweza kutafsiriwa, 'Musa kutomtii Mungu' au, 'Musa kutomheshimu Mungu.' Mungu alikuwa na njia maalumu ambayo alitaka Musa kuonesha watu uwezo wa Mungu kwa ajili yao. Wakati Musa akiacha kumtii Mungu kwa kufanya hivyo kwa njia tofauti alionesha ukosefu wa heshima kwa Mungu.
kwa kupiga mwamba mara mbili kwa fimbo baaada ya kuzungumza nao.
Hii inaweza kutafsiriwa kama, 'Musa hakuongea na mwamba; yeye aliupiga mara mbili kwa fimbo. '
14-14
waliokuwa wameasi dhidi ya Mungu
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "ambaye alikataa kumtii Mungu alipowaambia waende katika nchi ya ahadi".
watu
Yaani, watoto wa kizazi kilichokufa.
siku moja
Hii ina maana, 'wakati fulani katika siku zijazo.'
Nabii mwingine kama Musa
Kama Musa, mtu huyu atakuwa Muisraeli, atakayeweza kusema maneno ya Mungu kwa watu, nae ataweza kuwaongoza watu.
14-15
waliomboleza kwa siku thelathini
Kwa muda wa siku thelathini watu wote wa Israeli wlilia na kuonesha kuwa walikuwa wakisikitika sana kwamba Musa alikuwa amekufa.