18-01
Aliomba hekima
Hii inaweza kutafasiriwa kama, " alimuomba Mungu ampe hekima."
18-02
Alikuwemo ndani ya Hekalu
inamaanisha kuwa, " alikuwemo ndani ya hekalu kwa namna ya pekee." Hata hivyo Mungu alikuwepo kila mahali mda wote, alijidhihirisha mwenyewe kwa hali ya upekee kwa watu ndani ya hekalu.
Na watu wake
inaweza kutafasiriwa kama, " katikati ya watu wake" au " kati ya watu wake."
18-03
Waliileta miungu yao pamoja na nao.
Walileta sanamu zao na namna zao za kuziabudu sanam huko israel.
18-04
Kama adhabu ya Selemani kwa sababu ya kukosa uaminifu, aliahidi kuligawa
inamaanisha ya kuwa, "kumuadhibu Selemani kwa kukosa uaminifu, Hivyo Mungu akasema ataligawa taifa"
18-05
Kumthibitisha yeye kama Mfalme
Inamaana ya kuwa, " kumwambia ya kuwa walifurahia yeye kuwa Mfalme na wangefanya kila alichokisema."
18-06
Kujibu kwa upumbavu
jibu la Rehoboam lilikuwa la ukali, na ilisababisha watu kumgeuka yeye.
18-07
Makabila ya taifa la israel
Kila uzao wa watoto wa Yakobo ulifanyika kuwa "kabila" au kikundi kikubwa cha familia katika taifa la israel. Kila mmoja katika israel alikuwa sehemu ya makabila kumi na mbili.
Yalimuasi Rehoboamu
inamaana ya kuwa, "walikataa kumfata Rehoboam kama Mfalme wao." inaweza ikasaidia kuanza sentensi hii kama, "kwa hiyo" au, "kwa sababu hiyo" au " kwa sababu alichokisema Rehoboamu."
Walibaki kuwa waaminifu kwake
inamaanisha ya kuwa, " waliendelea kwa waaminifu kwake" au waliendelea kumuunga mkono kama Mfalme."
18-08
Walikaa na kuutengeneza ufalme wao.
inaweza kutafasiriwa kama, " walianzisha" au "kujenga" sentensi hii pia inaweza ikatafasiriwa kama, " walijitenga mbali na yale makabila mawili na wakakaa(wakaishi) kazikazini mwa nchi. na wakaiita nchi yao Israel."
18-09
Alisababisha watu watende dhambi
Hii ingeweza kutafasiriwa kama, " kuwafanya watu watende dhambi" au " aliwapelekea watu dhambini," Rehoboamu aliwapelekea watu dhambini kwa kutengeneza sanamu kwa ajili ya wao kuabudu."
Badala ya wao kumwabudu Mungu...Yuda.
Inaweza kutafasiriwa kama, "ilikusudi wasimwabudu Mungu" au " badala ya kwenda kwenye ufalme wa Yuda kwa ajili ya kumwabudu Mungu kwenye hekalu."
18-10
Yuda na Israel
Watu wa Yuda na Israel, wote walikuwa ni uzao wa Yakobo na sehemu ya watu wa Mungu. Hata hivyo, hawakumtii Mungu
18-11
Waisrael
Hapa " waisrael" inarejea watu walioishi kazikazini mwa ufalme wa israel, sio kwa watu waliokuwa wakiishi kusini mwa ufalme wa Yuda.
18-12
Kafara ya watoto
Waliwauwa watoto na kuwafanya kafara kwa miungu yao.
18-13
Alitawala kwa haki
inamaanisha ya kuwa alitawala kutokana na Sheria za Mungu. inaweza kutafasirwa kama, " walipotawala, walifanya yaliyokuwa sahihi."
Rushwa
Inaweza kutafasiriwa kama, "walifanya yasiyosahihi ilikusudi kujipatia waliyokuwa wakiyahitaji."