50-01
Kanisa limekuwa likikua
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, " Idadi ya watu kanisani duniani kote imekuwa ikiongezeka" au, " Idadi ya waamini katika Yesu imekuwa ikiongezeka."
Wakati wa mwisho wa dunia
Sentensi hii inamaanisha, "kabla tu ya mwisho wa dunia kufika" au, "katika siku za mwisho za dunia hii."
50-02
Mwisho utakuja
Hii inaweza kutafsiriwa kama, " Mwisho wa dunia hii utakuja" au, "mwisho wa dunia hii utatokea" au, "dunia hii ya sasa itafikia mwisho
50-03
Kufanya wanafunzi
Hii inamaana, wasaidie watu wafanyike wanafunzi wangu."
Mashamba yamekomaa kwa mavuno
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "wako tayari kuletwa kwa Mungu kama vile mashamba yalivyotayari kwa mavuno" au, "wako tayari kukusanywa na kuletwa Kwa Mungu kama vile mashamba ambayo mazao yake yameiva na kuwa tayari kukusanywa."
Mashamba
Katika maelezo , "Mashamba" yanawakilisha watu wa duniani.
Kuiva
"Iva" Hii inawakilisha jambo la kuwa tayari kumwamini Yesu.
Mavuno
"Mavuno" Hii inawakilisha kazi ya kuwaleta watu kwa Mungu kw kuwafundisha kuhusu Yesu.
50-04
Si mkuu kuliko
Hii ni, " si wa muhimu kuliko" au, "katika hali hii, "si kutendewa vizuri zaidi kuliko."
Kwa sababu yangu
Hii ni, " kwasababu mnanitii mimi" au, kwa sababu mnawafundisha watu kuhusu mimi" au, " kwasababu ninyi ni watu wa miliki yangu."
Katika dunia hii
Hii ninaweza pia kutafsiriwa kama, "katika wakati huu wa kuishi."
Baki mwaminifu kwangu
Hii ni, "Endelea kuwa mtiifu kwangu."
Hadi mwisho
Hii ni, "mpaka mwisho wa maisha yako."
Atawaokoa
Hii inamaanisha wokovu wa ki roho zaidi zsana kuliko kuokolewa ki mwili kutokakatika hali ya kudhurika. imekwisha semwa kwamba waamini wengi watauwawa au kuteswa.
50-05
Mbegu njema
Mbegu hizi zilikuwa ni mbegu za ngano. Kama aina hii ya mbegu haijulikani katika lugha ya eneo lako ni vema kutumia neno la jumla lenye kumaanisha "mbegu." Kama hakuna neno la jumla, itakuwa lazima kuchagua aina ya mbegu inayo fahamika na kusema, kwa mfano, "mbegu njema kama mpunga."
Mbegu za magugu
Mbegu za magugu ambazo zilipandwa zingelikua na kuwa kama nyasi marefu lakini zisingeweza kuliwa.zilikuwa hazifai.
Ngano
Hii ni, "mbegu za ngano." Ngano ni aina ya mbegu ambazo hukua na kuwa kama nyasi ndefu. Zina mbegu ambazo watu huzitumia kwa chakula.
50-06
Adui atakuwa lazima amepanda
Kama ikiwezekana tafsiri jambo hili kwa njia ambayo itaonesha msemaji hakuona hili likitendeka.
50-07
Mtang'oa na ngano pamoja
Hii ni kwamba, "mnaweza kung'oa ngano kwa bahati mbaya pia." Itakuwa jambo gumu kutofautisha ngano ambayo haijakomaa na magugu, na kung'oa magugu bila kung'oa ngano.
Hadi mavuno
Hii ni, "Hadi wakati ambao ngano itakuwa tayari kuvunwa" au, "hadi pale ambapo ngano imekomaa vya kutosha kuvunwa."
Ngano
Hii ni, "mbegu za ngano zilizo vunwa."
Galani
Hii inamaanisha nyumba ambayo mbegu za ngano zinapovunwa zinahifadhiwa na kutunzwa. inaweza pia kuitwa gala.
50-08
Watu wa ufalme wa Mungu
Hii inaweza kutafsiriwa kama, " watu wanaoishi chini ya mamlaka ya Mungu" au, "watu ambao wametii mamlaka ya utawala wa Mungu" au, "watu ambao wataishi pamoja na Mungu katika ufalme wake."
50-09
Watu wa milikiya mwovu
Hii ni, Ambao wanamtii mwovu" au, "ambao wanatawaliwa na mwovu."
Mwovu
Hili ni jina lingine la shetani. Linaweza kutafsiriwa kama,"shetani" ingawa jina mwovu linaeleza hasa tabia yake.
Ibilisi
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, " shetani"
Inawakilisha mwisho wa dunia
Hii ni, " inawakilisha jambo ambalo litatokea kwa watu mwisho wa dunia."
Wavunaji
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, " watua ambao wanavuna mbegu zilizo komaa au zilizo iva" au, "wafanyakazi ambao wanakusanya mbegu zilizo iva."
50-10
Wa miliki ya ibilisi
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "anaye mtii shetani, au, "anaye tawaliwa na shetani," hawa ni wale wasio mwamini Yesu ila wakifuata njia mbaya za ibilisi.
Moto wa hasira
Huu ni moto ambao ni mkali sana, "moto unao unguza," au, " moto mkubwa.
Wenye haki
Hawa ni wale watu ambao ni miliki ya Masihi
Wata ng'aa kama jua
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, " hali ya kuwa katika utukufu kama jua" au, " kuonesha wema usio na waa kama jua linavyo onesha mwanga mkali."
50-11
aliondoka
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "aliiacha dunia" au, "aliondoka kurudi mbinguni."
Atakuja katika mawingu katika anga
Hii ni, " Mawingu katika anga yatamzunguka wakati atakapo kuja" au, "Mawingu ya angani yata mbeba."
Wakati Yesu atakaporudi
Hii ni, " Wakati Yesu atakapo rudi duniani."
Kutana naye angani
Hii ni, "Kuungana naye katika anga." wale ambao wameamini watapaa juu kuwa karibu na Yesu wakati atakapokuwa angani.
50-12
Salia hai
Hii ni, "ambao watakuwa hai wakati Yesu atakaporudi,"
50-13
Taji
Taji hii inawakilisha zawadi yetu kwa kumwamini Yesu na kumtumikia katika maisha haya
Timilifu
Hii, "iliyo kamilifu" au "Jumla"
50-14
Kulia na kusaga meno katika mateso
Tazama tafsiri ya simulizi ya 50 -10
50-15
Ufalme wake
Hiiinaweza pia kutafsiriwa kama, "utawala wa kiovu wa shetani kwa watu" au, "mambo yote maovu afanyayo ana watu waovu anao wadhibiti."
Badala ya
Hii ni, "badala ya."
50-16
Kuleta dhambi humu
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "alisababisha dhami kuingia."
Mbingu mpya
Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, mbingu mpya, au, nchi mpya," Inarejea katika mfumo mpya wa nyota na kila kitu katika anga.
Nchi mpya
Nchi hii ya sasa ambayo tunakaa itatoweshwa nakuwekwa nyingine mpya iliyoboreshwa.
50-17
Atafuta kila chozi
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kukomesha huzuni zote" au, "kufanya matatizo yote kuisha" au, " kuondoa huzuni zote watu walizo nazo."
Hakutakuwa na mateso, huzuni, kilio, uovu, maumivu, au, kifo."
Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "watu hawatapata mateso tena, huzuni, kilio, mambo mauvu, kuhisi maumivu, au, kufa."
Atatawala katika ufalme wake kwa amani na haki
Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "utawala wa haki juu ya watu wake, kwa njia ambayo inaleta amani."