38-01
Karne nyingi zilizopita
Hii ni, "mamia ya miaka iliyopita" au, "muda mrefu kabla."
38-02
Mtunza mfuko wa fedha za mitume
Hii ni, "wajibika kutunza fedha za mitume" au, "kuwajibika kusimamia mfuko ambao ulikuwa na fedha za mitume na matumizi yake."
Alipenda fedha
Hii ni, "alithamini sana fedha" au, alitaka pesa." Baadhi ya lugha zisingelitumia neno lililo sawa na linaloweza kutumika kwa "kupenda watu."
38-03
Vipande thelathini vya fedha
Kila kipande au sarafu ilikuwa na thamani ya posho ya siku nne.
38-04
Alisherekea
Hii ni, "alikuwa akisherehe"
Alichukua mkate
Hii ingelikuwa inatafsirika kama, "alichukua kipande cha mkate." au " akachukua mkate."
Akauvunja
Baadhi ya lugha zitasema, "akaugawanya vipande" au, "akaugawa nusu yake" au, "akaugawa sehemu yake"
Umetolewa kwa ajili yenu
Hii inaweza kutafsiriwa kwamba, "ambao umetolewa kwaajili yenu"
Fanya hivyo kwa kunikumbuka mimi
Hii ni, "Fanya hivi ikiwa ni njia ya kukukumbusha ambayo Mimi nafanya kwaajili yako." Yesu alikuwa anarejelea kuhusu kifo chake, ambacho kingelitokea karibuni.
38-05
kikombe
Hiki ni, "kikombe cha mvinyo" au, "kikombe kilichojaa kinywaji kilichotengenezwa kwa mzabibu"
Kunywa hiki
Hii ni, "kunywa ambacho kimo katika kikombe hiki" au, "kunywa kutoka katika kikombe hiki." Kunywa katika kikombe chenye zabibu iliyokuwa imetengenezwa ikiwa na rangi nyekundu sana.
Damu ya agano jipya
Hii ingelitafsiriwa kama, "damu inayofanya agano liwezekane." au "damu ambayo ni msingi wa agano jipya."
Imemwagwa
Hii ingelitafsiriwa kama, "itatoka mwilini mwangu" au, "nitatokwa damu."
Kwaajili ya msamaha wa dhambi
Hii ni, "kusudi kwamba Mungu aweze kusamehe dhambi zote za watu kikamilifu."
Nikumbuke
Hii ni, "sherehekea kwa ajili yangu" au, "niadhimisheni." Inaweza pia kutafsiriwa kama, "hasa inayolenga kwangu" au, "jikumbusheni kuhusu mimi."
38-06
Kumpa kipande cha mkate
Hii ni, "kukabidhi kipande cha mkate"
Ni msaliti
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "atanisaliti" au, "yeye ndiye atakaye nisaliti."
38-07
Shetani alimwingia
Hii ni, "shetani alimwingia" au, "akajawa na shetani."
Yuda aliondoka na akaenda
Lugha nyingine inaweza kupendelea kusema, "Yuda alikiacha chakula na akaenda." au, "Yuda aliondoka ndani na akaenda nje."
38-08
Mlima wa Mizeituni
Hili ni jina mlima uliofunikwa na miti ya mizeituni, nje tu ya jiji la Yerusalemu. Pia inaweza kutafsiriwa kama, "mlima wenye miti ya mizeituni."
kuniacha
Hii ni, "kunitenga mimi" au, "kuniacha."
Imeandikwa
Hiyo ni, "Imeandikwa kwenye neno la Mungu" au, "imeandikwa katika maandiko" au, "Mmoja wa manabii aliandika." Pia inawezekana kusema, kilichoandikwa kitatokea." au, "itatimia kama ilivyoandikwa." Unabii huu unarejelea kifo cha Yesu na wafuasi wake kukimbia.
Nitampiga
Hii ni, "Nitaua"
mchungaji na kondoo wote
Usitumie jina la Yesu katika nukuu hii kwa sababu nabii aliyeandika mwanzoni hangelijua jina la mchungaji. Pia usirejelee wanafunzi kuwa ni wanafunzi. Inafaa sana kutumia maneno yenye maana ya "mchungaji" na "kondoo" unapotafsiri.
watatawanyika
Hii ni, "kwenda huko na huko kwa uelekeo tofauti"
38-09
Sitakuacha
.........
Kuwa nanyi wote
Hii ni, "kuwatawala kikamilifu" au, "anataka ninyi mtumike kwake kikamilifu." Neno wewe au "ninyi" ni wingi katika kauli hii. Maneno haya "wewe" na "yako" yanayofuata yako katika umoja.
Imani yako haitashindwa
Hii ni, "kwamba hutaacha kuniamini"
Kabla jogoo hajawika
Kwa kawaida jogoo huwika kabla ya kuanza siku mpya. Kama hiyo haijaeleweka , itasaidia kusema, "kabla ya kuwika jogoo mapema kesho" au, "kabla hajawika jogoo kesho asubuhi."
38-10
Kukukana
Hii ni, "nakujua lakini nakana" au, "mimi mwanafunzi wako halafu nakana" au "nakukataa"
38-11
Sehemu inayoitwa Gethmane
Hii ingeliweza kutafsiriwa, "eneo jirani lililoitwa Gethsemane" au, au "sehemu iliyoitwa Gethsemane chini ya Mlima wa Mizeituni."
Kuingia majaribuni
Hii ni, "wasingetenda dhambi walipojaribiwa" au, "Wasingeliingia kwenye majaribu yaliyokuwa yanaelekea kuwapata."
Peke yake
Hii ingetafsiriwa kama "yeye tu."
38-12
Kunywea kikombe cha mateso
Hii ni, "kupitia amateso haya" au, "kuteseka kwa kinachokaribia kutokea" au, "kuvumilia haya mateso."
Mapenzi yako yafanyike
maelezo haya yanamaanisha, "fanya ambacho umepanga" au, "fanya unachohitaji kufanya."
38-13
Kila baada ya maombi
Hii ni, "Kila wakati Yesu aliomba maombi hayo." Hii inarejelea zile mara tatu aliomba kama ilivyotajwa
38-14
Akaja
Lugha zingine zitapendelea kusema, "akaenda"
Salaam
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "habari" au, "amani" au, "Habari za mchana."
Ishara
Hiki ni, "kiashiria."
Unanisaliti mimi kwa busu
Hii ni, "ni hakika unakwenda kunisaliti mimi kwa busu?" Yesu hatafuti jibu kwenye swali hili. Hivyo lugha zingine zingelitafsiri kama ifuatavyo: "unanisaliti kwa kunibusu!" au, "unafanya usaliti mbaya wa kunibusu kabisa."
38-15
Ikawa askari walimkamata Yesu
Hii ni, "wakati askari walikuwa wakimkamata Yesu."
Aliuvuta upanga wake
Hii ni, "kutoa upanga kutoka mahali alipokuwa ameuweka."
Lazima nimtii Baba yangu
Hii ni, "Sitafanya hivyo kwa sababu lazima nitii mapenzi ya Baba yangu, niko tayari kukamatwa."