Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

10-01

Kwa Farao

Inaweza kuwa wazi kusema "kwenye nyumba ya kifalme ya Farao ili kuongea naye."

Mungu wa Israeli

Inaweza kutafasiriwa kuwa "Mungu aliyewachagua waisraeli kuwa watu wake" au "Mungu aliyewaongoza wana wa israeli" au "Mungu anayeabudiwa na wana wa Israeli"

Waache watu wangu waende

Njia nyingine ya kusema hivi yaweza kuwa "Waruhusu watu wangu wawe huru kuondoka" au "waachie watu wangu wawe huru kuondoka Misri"

Kusikiliza

Hii inaweza kutafasiriwa kama "tilia maanani" au "kutii."

10-02

Watu

Hii inamaanisha watu wa Israeli pia unaweza kuwaita "waisraeli"

Mapigo hatari kumi

Pigo ni kitu kibaya sana au cha kutisha ambacho kinaweza kutokea kwa mtu au kwa kitu fulani. Pigo mara nyingi ni kitu ambacho kinaathiri watu wengi au eneo kubwa. Neno lingine la "pigo" laweza kuwa "majanga."

miungu yote ya Misri

Inaweza kuelezewa zaidi kwa kusema "miungu yote ambayo watu wa misri waliiabudu" watu wa Misri waliabudu miungu mingi ya uongo. Hii miungu ya uongo ni roho ambayo Mungu wa Israeli aliziumba au hazikuwepo kabisa.

10-03

Akabadili mto Nile kuwa damu.

Kwenye lugha nyingine tunaweza kusema "akabadili maji ya mto Nile kuwa damu" Badala ya maji kwenye mto kulikuwa na damu, hivyo samaki walikufa na watu walikosa maji ya kunywa.

10-04

Mungu akatuma Vyura wengi Misri yote

Hii inaweza kutafasiriwa kuwa "Mungu alisababisha vyura wengi sana kutokea katika maeneo yote ya Misri"

Akaufanya Moyo wake kuwa mgumu

Alikuwa msumbufu tena na akakataa kumtii Mungu.

10-05

Mungu alituma pigo

Hii inaweza kutafasiriwa kuwa "Mungu alisababisha kuwepo kwa mapigo" au "Mungu alisababisha mapigo (mbu) yaje juu ya nchi ya Misri.

Mbu

Hawa walikuwa wadogo , wanaon'gata na kuruka katika makundi makubwa, walikuwa wakiwaudhi na walitua juu ya watu na wanyama wa Misri.

Nzi

Hawa walikuwa wadudu wakubwa zaidi ambao walikua wanaudhi na wenye kuharibu. Walikuwa wengi sana wakafunika kilakitu ikiwemo nyumba za Wamisri.

kuufanya moyo wake mgumu

Angalia maelezo katika 10-4.

10-06

Wanyama wa shambani

Hii inaelezea wanyama wakubwa ambao Wana wa Israeli walitumia katika kuwasaidia kazi zao, mfano wa wanyama hao ni Farasi, punda, ngamia, ng'ombe, kondoo na mbuzi.

Moyo ulikua mgumu

Angalia maelezo katika 10-4.

10-07

Mungu akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu

Mungu akasababisha Farao akaendelea kuwa msumbufu.

10-08

Baada ya hapo

Hii inamaanisha kuwa baada ya Mungu kusababisha maumivu ya majipu juu ya ngozi za wana wa Israeli.

Mungu alituma mvua ya Mawe

Mungu alisababisha mvua ya mawe kuanguka toka angani.

Mvua ya mawe

Mvua ya mawe ni vipande vya barafu vinavyoanguka toka kwenye anga mvua ikiwa inanyesha. Vipande hivi vinaweza kuwa vikubwa au vidogo. Vipande vikubwa vinaweza kusababisa maumivu au kuua vikianguka.

Ninyi mwaweza kwenda

Neno "wewe" linamuelezea Musa, Haruni na wana wa Israeli.

10-09

Miyoyo migumu

Angalia maelezo katika 10-4.

10-10

Kundi la nzige

Nzige ni panzi ambao huruka kwa pamoja katika kundi au makundi makubwa na huweza kuharibu eneo kubwa la mimea na mazao ya chakula kwa kuyala.

Mvua ya mawe

Mvua ya mawe ni vipande vya barafu vinavyoshuka kutoka kwenye mawingi mvua ikiwa inanyesha.

10-11

Mungu akatuma giza

Mungu alisababisha giza kutanda juu ya Misri. Kwa maneno mengine Mungu aliondoa mwanga sehemu hii ya Misri.

Giza lililodumu kwa siku tatu

Giza hili lilikua giza nene zaidi ya giza la usiku na liliendelea kuwa giza nene kwa siku tatu.

10-12

Haya mapigo tisa

Hii inamaanisha "majanga haya tisa ambayo yalisababishwa na Mungu"

Kwa kuwa Farao hakusikiliza

Hii inaweza kutafasiriwa kama "Kwa kuwa Farao hakufanya yale aliyoambiwa na Mungu ayafanye" au "kwa kuwa Farao hakumtii Mungu"

Hii ingeweza kubadili nia ya Farao

Njia nyingine ya kusema haya ni "Hili pigo la mwisho litamfanya Farao abadili mtazamo wake juu ya Mungu hatimaye aliwacha wana wa Israeli waende.