Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

43-01

Alirudi mbinguni

Hii ni, "alirudi mbinguni."

Walibakia Yerusalem

Hii ni kwamba, " walisalia Yerusalem kwa muda." hawakukaa pale kabisa.

43-02

Pentekoste

"Pentekoste" maana yake ni siku ya hamsini. " Unaweza kutumia neno "pentekoste " katika tafsiri yako na kuacha kifungu kieleze maana yake. au unaweza kutumia neno ambalo linamaanisha. "siku 50."

Walisherehekea mavuno ya ngano

Wayahudi walifikiri Mungu katika mavuno ya ngano kwa njia ya kuleta sadaka pamoja na kusherehekea kwa kula chakula maalumu. Ngano ni zao la nafaka; unaweza kutumia neno la jumla linalo maanisha nafaka. hii ilifanyika katika mwezi Mei; mazao mengine yalikuwa yamevunwa kwa kipindi kingine cha mwaka.

Mwaka huu

Hii ni mkwamba, katika mwaka ambao Yesu alikufa."

43-03

Sauti kama ya upepo mkali

Hii ni, "sauti ambayo upepo mkali unatengeneza" au, " sauti ambayo inatengenezwa na upepo wakati unapovuma kwa nguvu."

Kujazwa na Roho Mtakatifu

Hii ni , "hali ya kpewa nguvu na Roho Mtakatifu" au, nguvu itokayo kwa Roho Mtakatifu."

Katika lugha zingine

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "katika lugha zingine zaidi ya ile ya kwao" au, "katika lugha ngeni" au, " waamini hawakujua lugha hizi hadi pale Roho Mtakatifu alipowapa uwezo wa kuziongea.Hakikisha kwamba neno lililo tumika kutafsiri "lugha" linamaanisha lugha ambazo watu wanazungumza na kuzielewa.

43-04

Umati

Hii inaweza kutafsiriwa kama, " kundi la watu au, "kundi kubwa la watu."

Kazi za Mungu za kushangaza

Hii inaweza kutafsiriwa kama, " mambo ya ajabu ambayo Mungu amefanya."

43-05

Waliwashutumu wanafunzi kuwa wamelewa

Hii pia inaweza pia kutafsiriwa kama, " walisema kuwa wanafunzi walikuwa wamelewa."

Yoeli

Yoeli alikuwa nabii katika Israel ambaye aliishi miaka mamia kabla mambo haya hayajatokea.

Sku za mwisho

Hii inamaana , Siku za mwisho kabala ya mwisho wa dunia."

Nitawamwagieni Roho wangu

Hii inaweza kueleweka katika hali ya , " kutoa kwa ukarimu Roho wangu kwa watu"au, " kusababisha Roho wangu kuwajaza nguvu kwa ukamilifu watu."

Roho wangu

Hii ni, Roho Mtakatifu wangu."

43-06

Watu wa Israel

Kwa lugha zingine ni vema kusema, Watu wa Israel" kwa kuwa ni wazi kuwa hiiinajumuisha wanaume na wanawake. hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "ndugu zangu waisrael" au, " ndugu zangu wayahudi" ili kuweka wazi kwamba Petro alikuwa pia myahudi na kwamba alikuwa miongoni mwa " watu wa Israel."

Mlimsulibisha

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, " mlisababisha asulibiwe" au, " kwa sababu yenu alisulibiwa." Kwa uhalisia, wayahudi hawa kumgongelea misumari Yesu pale msalabani. Ingawaje, viongozi wa wayahudi walisababisha ahukumiwe na watu wengi katika kusanyiko walipiga kelele asulibiwe.

43-07

Hii inatimiliza unabii unaosema

Njia nyingine ya kutafsiri hii inaweza kuwa, hii ilisababisha haya kutimilika kwa yale ambayo mmoja wa manabii alisema zamani za kale."

Wewe hutamwacha mtakatifu wako

"Wewe" na "wako" inamaanisha Mungu baba. ili kuweka wazi, hii inaweza kutafsiriwa kama, " wewe" Mungu hatakuacha." Lugha zingine zaweza kuwa na njia maalumu ya kueleza mtu, kama vile "wewe, Mungu"

Kuoza kaburini

Hii inamaana "kuoza ndani ya kaburi" hii dhihirisha ukweli kwamba Yesu hakubakia kaburini kwa muda mrefu na ni njia nyingine ya kusema kwamba hakubakia mfu, lakini alifufuka na kuwa hai tena.

Alimfufua Yesu kuwa hai tena

Hii ni kwamba, " alimfanya Yesu kuwa hai tena."

43-08

Yesu sasaametukuzwa

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "Yesu sasa ameinuliwa juu" au, " Yesu sasa amepandishwa juu" au, " Mungu amemtukuza Yesu."

Mkono wa kuume/ mkono wa kulia wa

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "nafasi ya muhimu sana" au, mali pa heshima ya juu baada ya."

Sababisha

Hii ni, " kuwezesha waamini kufanya" au, " kuwapatia watu hawa uwezo wa kufanya."

43-09

Lakini mfahamu kwa uhakika kwamba

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, " lakini unaweza kujua kuwa ni kweli kwamba" au, " unaweza kuwa na uhakika kwamba."

43-10

Walivutiwa sana

Hii ni kwamba, "walihangaishwa" au, walijisikia huzuni wakati waliposikia." kuvutiwa ni kupata hisia kali.

Ndugu/ kaka

Hii ilikuwa ni njia ya kawaida kwa myahudi kumwita myahudi mwenzake. Inaweza pia kutafsiriwa kama, "marafiki."

43-11

Kwa jina la

Sentensi hii inamaana mbili, " kwa mamlaka ya" na, " chini ya mamlaka ya" fikiri kutafsiri neno "jina" kwa uhalisia ikiwa itaeleweka kwa jinsi hii katika lugha yako.

Kristo

Hili ni jina ambalo maana yake ni "Masihi" inaweza kutafsiriwa kama, " mpakwa mafuta" au, "aliye teuliwa" badala ya kutoa maana, tafsiri zingine zinaweza kuchagua kuhifadhi neno "Kristo" na kuliandika kwa kutumia herufi ambazo zina sauti ya lugha yao.

Yesu Kristo

Kwa kuwa "Kristo" ni cheo mahali hapa, baadhi ya watafsiri wanaweza kuchagua kubadilisha mpangilio na kusema, " Kristo Yesu" na mipangilio yote miwili inatumika katika Biblia.

43-13

Mtazamo mzuri juu yao

Hii ni kwamba, " alikuwa na mtazamo chanya juu yao."