47-01
kutangaza
Hiyo ina maana kwamba, "kufundisha" au, "kuhubiri."
mfanyabiashara
Hii ingeweza kutafsiriwa kama, "muuzaji" au, "mmiliki wa biashara" au, "mwenye biashara."
47-02
aliufungua moyo wa Lidia
Hii ina maana kwamba, "alimwezesha Lidia"
yeye na familia yake walibatizwa
Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "walimbatiza Lidia na familia yake."
hivyo wakakaa naye yeye na familia yake
Hii ilikuwa desturi ya kawaida siku zile kwa watu kuwakarimu wageni nyumbani mwao. Kulikuwa hakuna nia mbaya kinyume cha maadili katika kufanya hivi.
47-03
waliomtumikisha
katika hili, hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "wamiliki wake" au, "watu wanaommiliki"
kama mtambuzi
Hiyo ina maana kwamba. "ni kama mtu anaye waambia watu yale ambayo yangewatokea katika siku zao za usoni."
47-04
njia ya kupata wokovu
Hiyo ina maana kwamba, "ni jinsi unaweza kuokoka" au, " jinsi gani Mungu anaokoa watu" au. "Mpango wa Mungu kuwaokoa watu"
47-05
siku moja
Hii sentensi inatambulisha tukio ambalo limetokea huko nyumba, lakini haisemi ni wakati gani hasa. Lugha nyingi zinanamna kama hiyo ya kuanza kuhadithia hadithi.
aligeuka kwake
Hii ina maana kwamba, "aligeuka na kumwangalia"
kwa Jina la Yesu
Hiyo ina maana kwamba, "kwa mamlaka ya Yesu." Kwa sababu ya mamlaka ya Yesu, Paulo aliweza kuamuru pepo kuondoka.
toka ndani yake
Hiyo ina maana kwamba, "muache" au, "nenda mbali naye"
47-06
bila ya pepo
Hiyo ina maana kwamba. "bila ya nguvu kutoka kwa pepo" au, "sasa kwamba hakuwa na pepo."
wakati ujao
Hiyo ina maana kwamba, "mambo yatakayowatokea katika wakati ujao."
Hii ilimaanisha kwamba
Hii ingeweza pia kutafsiriwa kama, "Kwa sababu ya hili" au, "Kwahiyo."
47-07
kuwatia
Hiyo ina maana kwamba, "kuwaweka."
47-08
usiku wa manane
Hii ingeweza kutafsiriwa kama, "usiku sana" au, "alfajiri mapema sana." Hii ilikuwa wakati ilipokuwa giza kabisa huko nje, ambapo watu kwa kawaida wanakuwa wamelala."
wakiimba nyimbo za kumsifu Mungu
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kumsifu Mungu kwa kuimba" au, "kuimba nyimbo za kumsifu Mungu" au, "kuimba nyimbo ambazo zinampa Mungu sifa."
47-09
kuwa wazi
Hiyo ina maana kwamba, "kutokufungwa na ghafla kuwa wazi kabisa."
kuanguka
Hiyo ni maana kwamba, "ghafla ilitoka" au, "ghafla ikajitenga hivyo wafungwa wakawa wamefunguliwa."
47-10
Askari mlinzi wa wafungwa
Hiyo ina maana kwamba, "afisa mwangalizi wa gereza."
Sisi
Baadhi ya lugha zinaliangalia neno "sisi" kimaalum kabisa ambayo haimhusishi mtu anayeongeleshwa. Hapa "sisi" haimuhusishi askari mlinzi wa wafungwa, ni Paulo tu pamoja na wafungwa wengine.
47-11
kusalimika
Hii ingeweza kutafsiriwa pia kama, "ili niweze kuokoka kutoka katika dhambi zangu" au "ili kwamba Mungu aniokoe kutoka katika dhambi zangu." Swali linahusu wokovu kutoka katika kuadhibiwa na Mungu aliyesababisha tetemeko.
Mwamini Yesu, Bwana mkubwa.
Hii inaelezwa kwa wote wawili yaani askari mlinzi wa gereza pamoja na familia yake, ambao wote walikuja kuamini na kubatizwa. Baadhi ya lugha zingetumika kuonyesha kwamba Paulo anaongea na kundi.
wewe na watu wa nyumbani mwako mtapata wokovu.
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Mungu atawaokoa wewe na familia yako kutoka katika adhabu ya milele kwa sababu ya dhambi zenu." Hakikisha kwamba wokovu unaoongelewa hapa ni wakiroho, na si wa kimwili.
47-13
viongozi wa mji
Hii inaelezea juu ya, "maafisa wa mji" au, "mamlaka ya mji."
Injili ya Yesu iliendelea kuenea
Hiyo ina maana kwamba, "Watu katika maeneo mengi zaidi walikuwa wakisikiliza habari njema kuhusu Yesu."
Kanisa liliendelea kukua
Hiyo ina maana kwamba, "watu wengi zaidi walikuwa wanakuwa sehemu ya kanisa" au, "watu wengi zaidi na zaidi walikuwa wakimwamini Yesu."