Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

41-01

viongozi wa Kiyahudi wasioamini

Hawa ni, "viongozi wa kiyahudi ambao hawakuamini."

Yule Muongo, Yesu, alisema

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "huyo mwanaume Yesu , alidanganya na kusema," walikataa kuamini kwamba Yesu aliwaambia ukweli kuhusu yeye kuwa mwana wa Mungu.

amefufuka kutoka katika wafu

Hii ni kwamba, " amerudi tena kuwa hai au kuishi, au, "amekuwa mzima tena."

41-02

wakaweka

Hii ni kwamba, " viongozi wa dini na maaskari walimweka."

Muhuri kwenye jiwe

Waliweka kitu laini kama udongo mfinyanzi au nta kati ya jiwe na kaburi na wakalitia alama kwa kutumia muhuri maalumu. Kama mtu angelitoa jiwe, kile kitu laini kingelikatika na kuonesha kuwa mtu ameingia kaburini. Jambo hili pia linaweza kutafsiriwa pia kama, "alama katika jiwe kuzuia watu wasilihamishe."

41-03

Wayahudi hawakuruhusiwa

Sheria za siku ya sabato hazikuruhusu myahudi kutembea umbali mrefu au kufanya aina nyingine ya kazi.

marashi ya maziko.

Hii inamaanisha vile viungo vyenye harufu nzuri , marashi ambavyo viliwekwa kwenye maiti ya mtu kuzuia harufu mbaya. Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "viungo vyenye marashi" au, "mafuta yenye manukato" au, "mimea yenye manukato, au harufu nzuri."

41-04

tetemeko kubwa

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "tetemeko lenye nguvu" au, "mtikisiko wa nguvu wa ardhi." Lugha zingine zingependelea kutumia neno hili kama, "ardhi ilianza kutetemeka kwa nguvu."

ambaye mng'ao wake ulikuwa kama mng'ao wa mwanga wa radi

Hii ni kwamba, " ambaye mwonekano wake ulikuwa unang'aa kama radi."

Walianguka chini na kuwa kama watu waliokufa.

Hawakuwa wamekufa, lakini hawakuweza kutembea, kama vile watu waliokufa wasivyoweza kutembea. Ili kufanya jambo hili lieleweke zaidi, ni kwamba jambo hili inaweza kutafsiriwa kama, " walianguka chini kwa ghafla na hawakuweza kutembea."

41-05

Msiogope

Hii ni kwamba, "acheni kuogopa" malaika aliyeng'aa kama radi alikuwa na mwonekano wa kuogopesha!

Amefufuka kutoka katika wafu

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "amerudi tena kuwa hai."

41-07

Walijawa na hofu na furaha kuu

Hii ni, kupata hisia za hofu pamoja na furaha kuu."

habari njema.

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, " Habari njema kuwa sasa Yesu yuko hai tena." Hii habari njema inamaanisha ukweli kwamba Yesu amefufuka katika wafu.

41-08

Mtaniona

Hii ni kwamba, " mtaniona" au, "mtakutana na mimi."