Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

19-01

Kupitia Historia ya

Msemo huu una maana kuwa Mungu alituma manabii wengi katika nyakati nyingi tofauti kupitia miaka yote ambayo Israeli na Yuda walikuwepo.

Waisraeli

Hii inaweza kuwa imetafsiriwa hapa kama, "Falme za Israeli na Yuda."Vizazi vyote vya Yakobo kujumlisha wote katika ufalme wa Yuda, waliendelea kuitwa "Waisraeli."

19-02

Mpaka nisema hivyo

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Mpaka niamuru mvua na umande kuja tena."

Hii ilimkasirisha sana Ahabu

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Wakati Ahabu alisikia kile Eliya alichosema,alikuwa na hasira sana."

19-03

Porini

Hili ni eneo porini mahali ambapo pana watu wachache. Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "jangwa" au "vichakani."

Ukame

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "upungufu wa mvua." Ukame huu ulikuwa matokeo ya tamko la Eliya kwamba kungekuwa na mvua.

19-04

Nchi jirani

Hii inaonyesha nchi ile ilikuwa karibu, au inayoshirikiana mpaka na Israeli.

Njaa

Kwa kweli inaweza kutafsiriwa kama, "njaa iliyosababishwa na ukame."

Alimtunza

Hii ina maana walimpa mahali kwa kukaa katika nyumba yao na walimpa chakula.Haina maana kuwa alikuwa mgonjwa.

Mungu aliwapatia...haikupungukiwa kamwe

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Mungu alitunza chombo chao cha unga na chupa yao ya mafuta visipungukiwe," au "Mungu alisababisha... kutopungukiwa kamwe."

chombo cha unga

Hii inaonyesha kuwa chombo cha udongo ambacho mjane alitunza unga wake.

Chupa ya mafuta

Katika Israeli, mafuta ya mzeituni yalitumika kwa kupikia.Hii inawezakutafasiriwa kama, "chupa ya mafuta ya kupikia. "Mjane alitumia unga na mafuta kwa kutengeneza mkate.

19-05

Ongea na Ahabu kwasababu alikuwa anakwenda kutuma

Hii inaweza kutafasiriwa kama. "Mwambie Ahabu kwamba Mungu alikuwa anakwenda kutuma"

Msababishaji wa matatizo

Hii inamaanisha, "Wewe ni msababishaji wa matatizo!" Ahabu alikuwa ana mlaumu Eliya kwa kusababisha matatizo kwa kumwambia mfalme kuwa alikuwa anafanya mabaya na pia kwa kuzuia mvua.

Umemutelekeza Yahwe

Kwamba Ahabu aliwaongoza Israeli kuacha kumwabudu na kumtii Yawhe

Mlima wa Karmeli

Mlima wa Karmeli ni jina la mlima uliokuwa kaskazini mwa Israeli. Una urefu wa mita 500.

19-06

Mlima wa Karmeli

Ni jina la mlima uliokuwa kaskazini mwa Israeli.

Kama Yahwe ni Mungu...Kama Baali ni Mungu

Hii haina maana kwamba Eliya alikuwa hana maamuzi. Alifahamu kuwa Yahwe ni Mungu hakika. Alitaka watu kuelewa kwamba wakati wana wanaabudu miungu ya uongo, wanamkataa Yahwe kama Mungu wa kweli pekee.Tafasiri hii inaonyesha kuwa watu wanapaswa kufanya uchaguzi.

Kwa muda gani mta...

Hili si swali halisi liulizwalo kwa maelezo. Eliya alikuwa anawaonya Waisraeli kwa kugeuka geuka na kubadilika mawazo yao kuhusu labda watamtumikia Mungu au Baal. Lugha zingine zinapaswa kueleza hii kama maelezo kama vile "Msibadilishe mawazo yenu juu ya nani mtamwabudu"

19-07

Anayejibu kwa moto

Hii ni "Ambaye kwa miujiza hutuma moto ili kuteketeza dhabihu."

Mungu kweli

Ina maanisha Mungu mmoja na wa kweli tu

19-08

Waliomba kwa Baal

Manabii wa Baali walimwomba Baali kutuma moto juu ya ng'ombe waliyemwandaa kama dhabihu.

Walipaza sauti

Walipaza au kumwita kwa nguvu Baali

Walijikata wao wenyewe kwa visu

Walijijeruhi wao wenyewe kwa visu kama kuonyesha maombi yao kwa Baali, tarajio kwamba hii ingelimsukuma kuwasikia.

Hakukuwa na jibu

Hakukuwa na majibu ya aina yote kwa kupaza sauti kwao,na hakuna moto ulikuja kuteketeza dhabihu.

19-10

tuoneshe

Ni kwamba "tuthibitishie"au "jioneshe kwetu.

mimi ni mtumishi wako

Hii inaweza kutafsiriwa kama, " Wewe umenipa mamlaka ya kukutumikia na kufanya vitu hivi."

Nijibu

Hili ni "Jibu kwa maombi yangu" au "tuma moto ule nimeomba kwako."

Hawa watu watajua

Hii inaweza kutafsiriwa kama "Watu hawa wataona na kuelewa."

19-11

anguka kutoka angani

Hii inaweza kutafsiriwa kama "gafla ulikuja chini kutoka angani."

shuka ardhini

Walianguka chini au walipiga magoti juu ya ardhi. Wamliogopa Yahwe kwa sababu waliona nguvu zake. Walijua kwamba Mungu wa kweli tu anaweza kufanya vile na walisujudu chini kumheshimu na kumwabudu.

Yahweh ni Mungu

Hii inamaanisha kwamba walielewa kuwa Yahweh ni Mungu pekee, si mmoja wa miungu wengine.

19-12

toroka

Manabii wa Baali walijaribu kukimbia mbali baada ya mungu wao kuthibitishwa kuwa mungu wa uongo.

kamatwa

Hii ni kuchukuliwa na kushikiliwa

19-13

Wingu likawa jeusi

Hii ni, "Anga likawa jeusi sana" Mawingu mazito ya mvua yalifunika anga, ilifanya kuonekana giza la kijivu au jeusi.

Ukame

Hii ni, "kipindi kirefu kisicho na mvua."

19-14

Kamanda adui

Naamani alikuwa kamanda wa jeshi moja la nchi adui za Israeli.

Alikuwa amekwisha sikia Elisha

Hii ina maanisha kwamba wale watu walikwisha mwambia Naamani kuwa Elisha alikuwa anaweza kufanya miujiza.

Alikwenda na kumuuliza Elisha

Maana yake, "Alikwenda kumwona Elisha na kumuuliza." Naamani alipaswa kwenda Israeli kumtafuta Elisha na kumuuliza kufanya hivi.

19-15

Ungeliacha kufanya hivyo, itaonekana kama ni upumbavu

Naamani asingefanya kile Elisha alisema kwasababu alifahamu kwamba kuoga peke yake kusingeliponya ugonjwa wake.

Alibadirisha mawazo yake

Hii ni, "aliamua kufanya kile Elisha alimwambia kufanya."

19-16

Anza kuonyesha haki na huruma

Hii inaweza kutafsiriwa kama,"anza kuwa na haki na huruma" au "anza kuonyesha haki na huruma."

19-17

Kisima kikavu

Kisima hakikuwa na maji yoyote ndani yake, lakini bado kina matope chini . Hii inaweza kutafsiriwa kama " kisima tupu."

Alikuwa na huruma kwake

Hii ina maana alikuwa aina yaYeremia na alimsaidia

19-18

Aliendelea kuongea kwa niaba ya Mungu

Hii ni "aliendelea kuwaambia watu kile Mungu alitaka kuwaambia,"

ahidiwa kwamba masihi wa Mungu angekuja

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Kwamba Mungu aliwaahidi kuwa Masihi angekuja kuokoa watu wake."