39-01
usiku wa manane
Kauli hii inamaanisha, "usiku ukiwa katikati" au, "usiku ukiwa umeendelea sana"
kumhoji
Hii ni, "kumuuliza Yesu maswali kujaribu kutafuta jambo ambalo wangemtuhumu Yesu kuwa ni mkosaji "
39-02
Walimshitaki Yesu
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "walishandaa kikao kumtuhumu Yesu kuwa anakosa." kwa kawaida mashitaka yanafanyika ili kubaini kama mtu anahatia au kosa kwenye uhalifu uliotokea. Katika hili viongozi walidhamiria kufanya Yesu aonekane anahatia.
Walisema uongo juu ya mtu
Hii ni, "shuhudia uongo dhidi yake" au, "kulazimisha mashitaka kwamba huyu anamakosa"
Kauli zao hazikuoana
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "walisema mambo juu ya Yesu ambayo yalikuwa yanatofautiana" au "hoja za mashahidi walizosema juu ya Yesu zilipingana."
Kuwa na hatia kwa kitu chochote
Hii ni, "kwamba yeye alikuwa nakosa lolote."
39-03
Hatimaye
Hii ni, "Baada ya kukosa uthibitisho wowote dhidi yake" au, "Baada ya kushindwa kuthibitisha kwamba alikuwa na hatia."
39-04
Mimi ndiye
Hii ni, "Mimi ndiye kama ulivyosema" au, "Mimi ndiye masihi na Mwana wa Mungu." "Mimi ndiye " pia ni jina la Mungu. Kwa kurahisisha, "Mimi ndiye" Pia Yesu alikuwa anasema kwamba yeye ni Mungu. Kama inawezekana tafsiri ili kwamba watu waone ulinganifu kati jibu la Yesu na jina la Mungu.
Keti pamoja na Mungu
Hii ingelitafsiriwa kama, "kutawala pamoja na Mungu." Kwa sababu Mungu ni mtawala wa vyote, Watu wanamzungumzia kama ameketi kwenye kiti cha enzi mbinguni. Kwa kusema hivyo atakuwa alikuwa pamoja na Mungu, Yesu alikiri kwamba alikuwa na mamlaka ya kutawala pamoja na Baba.
Kaketi pamoja na Mungu na akishuka kutoka mbinguni
Hii inatafsiriwa kama, "kakaa karibu na Mungu halafu akishuka kutoka mbinguni"
Alichana mavazi yake kwa hasira
Wayahudi wangelichana nguo kuonesha huzuni au hasira. Ikiwa kuchana nguo inamaanisha kitu kingine kwenye lugha yako, unaweza kuweka sentensi mbadala kama vile, "alikuwa na hasira sana."
Hukumu yenu ni ipi?
Hii ni, "Uamzi wenu ni upi?" au, "Tuambie umeamuaje: Anahatia au kosa?" Kuhani mkuu alitaka viongozi wa dini wamhukumu Yesu kwa kukiri kuwa sawa na Mungu.
39-05
Walimfunika machon Yesu
Hii ni, "Walimfunika macho Yesu ili kwamba asiweze kuona"
walimtemea mate
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kumtusi kwa kumtemea mate" au "Kumtemea mate kwa kusema alikwa hanafaida." Hii ilikuwa njia yakuonesha kumdharau mtu.
39-06
Alikana
Hii inaweza kutafsiriwa kuwa, "alisema kwamba si kweli" au, "alisema kwamba hakuwa pamoja na Yesu" au, alisema, Hapana. "Hiyo siyo kweli"
Petro akakana tena
Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Petro alikana kumjua Yesu mara ya pili" au, "Petro akasema kwa mara nyingine hakuwa pamoja na Yesu"
Mnatokea Galilaya
Hii hii inaweza kutafsiriwa kama, "ni Wagalilaya." Watu wangelisema kutokana na Yesu na Petro walivyowaambia kwamba walitokea mkoa wa Galilaya.
39-07
Kaapa
Hii ni, "kasema kwa msisitizo" au, "kasema kwa kukazia sana."
Mungu anilaani kama namjua mtu huyu
Hii ni laana inayoonesha kwamba, "Mungu alete au asababishe madhara kama unachosema ni kweli" au "Mungu anilaani kama ninawadanganya!" kwa namna hiyo Petro alikuwa anakazia alikuwa hamjui Yesu. Pia alikuwa anarejelea kwa Yesu kama, "mtu huyu" ili ieleweke kama hamjui.
Akawika jogoo
"Kuwika" ni sauti anayoitoa jogoo
39-08
Alilia kwa uchungu
Hii ni, "kulia, kwa hisia kali sana" au, "kulia, kwa hisia na majuto"
Msaliti
Hii ni, "ambaye alimkana Yesu" au, "ambaye aliwasaidia viongozi wamkamate Yesu"
Alimhukumu Yesu kufa
Hii ni, "alisema kwamba Yesu alikuwa na hatia ni lazima afe"
39-09
Utawala wa Kirumi
Hii ni, "afisa wa utawala wa Kirumi." Utawala wa Kirumi ulimteua Pilato kutawala mkoa wa uyahudi katika Israeli.
Ahukumiwe kuuawa
Kama mtawala, Pilato alikuwa na mamlaka kumhukumu Yesu kifo na kuidhinisha auawe msalabani, au kumwacha huru. Viongozi wa kidini wa Kiyahudi hawakuwa na mamlaka kuruhusu mtu afe.
39-10
Umesema hivyo
Hii ni, "Umesema sahihi kabisa" au, kweli umepatia
Ufalme wangu siyo ufalme wa kidunia
Hii ni, "Ufalme wangu siyo kama falme za kidunia.
Watumishi wangu wangepigana kwaajili yangu
Hii ni, "wanafunzi wangu wangepigana kunilinda" ili kwamba niimarishe ufalme wangu.
Hunisikiliza
Hii ingetafsiriwa kama, "husikia mafundisho yangu na hunitii." Siyo tu kusikiliza maneno ya Yesu lakini pia kufanya kile anachosema.
Ukweli ni nini?
Hii ni, "Inawezekana yeyote kujua ukweli ni nini?"
39-11
Sioni hatia kwa mtu huyu
Hii ni, "sijapata hatia kwa mtu huyu" au, "Nimefanya uchunguzi kwa mtu huyu na sioni kama kosa alilofanya."
Hana hatia
Hii ni, "Hajatenda kosa lolote!?"
39-12
Ghasia
Hii ni, "wakafanya fujo wakiwa na hasira."
Aliwakubalia
Pilato hakutaka kumuua Yesu kwa sababu aliamini kwamba Yesu hakuwa na hatia. Lakini alilazimishwa kuwaambia askari kumsulibisha Yesu kwa sababu ya kuhofia makutano. Kama inawezekana, tafsiri kauli hii kwa namna ambayo itaonesha wasiwasi wake.
Vazi la kifalme
Hii ni, "vazi linalofanana na vazi la mfalme." Vazi hili lilikuwa na rangi ya kung'aa, hivyo lilionekana ni sawa na lile alilovaa mfalme.
Taji lililotengenezwa kwa miiba
Hii inamaana kwamba walifunga matawi kwa duara ionekane kama taji. Taji ni mapambo ambayo mfalme huvaa kichwani kuonesha mamlaka. Lakini taji walilomvisha Yesu lilichoma, likiwa na miiba mikali.
Tazama
Hii ni, "Tazama" au "Hapa ni"
Mfalme wa Wayahudi
Kwa kuwa askari walimdhihaki Yesu, hii inaweza kutafsiriwa kama, "anayeitwa Mfalme wa Wayahudi"