Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

32-01

Siku moja

Aya hii inatambulisha Tukio ambalo lilitokea wakati wa Nyuma, Lakini haisemi wakati maalumu. Lugha nyingi zina namna moja ya kuanza kusimulia habari ya kweli.

Watu wa Gerasi

Wagerasi waliishi eneo la pwani upande wa mashariki mwa Bahari ya Galilaya. Walikuwa ni ukoo wa kiyahudi, Lakini tunajua habari chache tu kuwahusu wao.

32-02

Mtu mwenye mapepo

Hii ni, "Mtu aliyekuwa na mapepo ndani yake" au, Mtu aliyeongozwa na roho chafu."

Akaja anakimbilia kwa

Hii ni kuwa, "Kimbilia kwa" au "Kimbilia na kusimama mbele ya"

32-03

Alifungwa miguu na mikono yake

Hii ni kwamba, "Kuzuia" au, "Kufungwa"

Aliendelea kuzikata.

Lugha zingine zinaweza kusema, "Aliendelea kuvunja minyororo"

32-04

Katakati ya Makaburi

Hii ni, "Karibu na makaburi" au, Kuzunguka makaburi"

32-05

akapiga magoti.

Hii ni, "Haraka alipiga magoti chini kwenye ardhi"

32-06

Alilia

Hii ni, "Kupiga kelele" au, "toa sauti"

Unataka nini kwangu

Hii tafsiri ina maanisha, "Unaenda kufanya nini kwangu? au, "Unataka kunifanya nini?"

Mungu aliye juu.

Hii ni, "Mungu mkuu" au, "Mungu mwenye Enzi" Maana ya "Juu" hapa linahusika na ukuu wa Mungu. haimaanishi urefu au kuwa mrefu.

kundi

Hili lilikuwa ni jina la kikundi cha mapepo, Lakini pia imetafsiriwa kwamba roho chafu walikuwa wanatofautiana. Tumia jina hili kwa kuzingatia ili kwamba lilete maana iliyo wazi kwa lugha yako. kama sivyo unahitaji kutafsiri neno kama, "Jeshi" au, "Umati wa watu" au, Maelfu

Tuko wengi

Tuko wengi- Hii ni, "Wako wengi kati" Tuko mapepo wengi"

32-07

usitufukuze

Hii ni, "Usitufanye tuondoke." au, "Usituondoe"

tafadhali tuamuru

hii ni, "Tafadhali Turuhusu twende"

Badala yake.

Hii ni, "Badala ya kutuacha twende mbali"

Nenda!

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "nendeni mkaingie kwa Nguruwe!" au, "mnaweza kwenda kwa wale Nguruwe"

32-08

Kundi

Hii ni, "Kundi la nguruwe" au, "Au kikundi cha nguruwe" Lugha nyingi zina majina maalumu kwa makundi ya wanyama, "Kundi la kundoo" "Kundi la mifugo" "kundi la Mbwa" na "Kundi la samaki." Tumia neno ambalo linaweza kuwa sahihi linaloweza kutumika katika kundi la nguruwe.

32-09

Nini Kimetokea

Hii ni, "Jinsi Yesu alivyowatoa pepo nje ya huyo mtu na akwaagiza kwenda kuingia kwa nguruwe."

Aliyekuwa na mapepo

Hii ni, "Ambaye mapepo yalikaa ndani yake" au, "Aliyekuwa akiongozwa na roho chafu"

32-10

Watu

Lugha zingine zingependekeza kusema, Watu kutoka katika mkoa ule" au, "Watu wa Gerasini"

Ogopa

Itakuwa vizuri kusema, "Ogopa kwa sababu ya kile Yesu alifanya"

Andaliwa

Hii ni, "Alikuwa anajitayarisha"

Alisihi kwenda pamoja na Yesu

Hii ni, "alimsihi Yesu kwenda pamoja naye" au, "alimuuliza Yesu kwa Bidii kama anaweza kwenda naye"

32-11

alivyokuwa na huruma juu yako

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Namna alivyoonyesha huruma kwako" au, "Hivyo ndivyo alivyokuwa na huruma kwako"

32-12

aliyesikia habari yake

hii ni, "Kusikia mtu anasema kilichotokea kwake"

alistaajabishwa na kushangazwa

Maneno "Mshangao" na "Ajabu" yana maana sawa. Walikuwa wakiyatumia pamoja ili kusisitiza namna watu wa walivyokuwa wakifanyiwa. Hii inaweza kutasriwa kama, "Kushangazwa kabisa kuhusiana na kile alichowaambia"

32-13

Kumsonga sana

Hii ni, "kumkandamiza zaidi" au, "Makutano walimbana wakimzunguka"

Hali iliendelea kuwa mbaya

Hii ni, "Hali yake iliendelea kuwa mbaya," au, "Afya yake ilikuwa mbaya badala ya kuwa nzuri" au, "Badala yake alizidi kuwa Mgonjwa."

32-15

Nguvu zimemtoka

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Nguvu ya uponyaji imehama kutoka kwake kwenda kwa mtu mwingine" au, "Nguvu yake imemponya mtu fulani." Yesu hakupoteza nguvu yeyote kwa sababu ya hili

kwa nini uliuliza, nani amenigusa?'

kwa lugha nyingine ni nzuri kutumia nukuu isiyo ya moja kwa moja hapa kama, "Kwa nini uliuliza nani alikuwa anakugusa?" au, "Kwa nini unashangaa aliyekugusa?"

32-16

alipiga magoti

Hii ni, "Akapiga magoti haraka"

kumwelekea Yesu

Hii ni, "mbele zaYesu."

akitetemeka na uoga mwingi

Hii ni, "Kutetemeka kwa hofu" au,"alitetemeka kwa sababu alikuwa ameogopa"

Imani yako imekuponya

hii ingeweza kutafsriwa kama, "Umeponywa kwa sababu ya Imani yako."

Enenda kwa amani.

Watu husema kama baraka za kimila pale wanapoachana kila mtu. Lugha zingine zingesema mambo ya kufanana kama," Nenda vizuri" "Enenda na Mungu" au "amani." Njia nyingine ya kutafsiri hii ingekuwa, Uwe na amani unapoenda" au, "Nenda ukijua kuwa kila kitu kiko sawa kati yetu."