Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

33-01

Siku moja

hii aya, inatambulisha tukio lililotokea wakati wa nyuma, lakini haioneshi wakati maalumu. Lugha nyingi zina namna moja ya kusimulia habari ya kweli.

33-02

Kumwaga mbegu kwa mkono

Hii ni, "Kutupa mbegu kwenye udongo" au, "kufunika mbegu zake zote kwa udongo." Hii ndiyo njia kwa wakulima wa kale Mashariki ya kati walivyopanda nafaka zao kuzalisha mazao.

33-03

ardhi yenye mawe

hii ni, "ardhi ambayo imejaa miamba."

33-04

Miiba

Hii ni, "Miti ya miiba" au, "Kichaka cha miiba."

ikaisonga

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "ikazifunikana na kivuli" au, "Kuibana."

Ardhi ya miiba

hii ni, "Ardhi ambayo imefunikwa na kichaka la miiba."

33-05

udongo mzuri

Hii ni, "udongo wenye rutuba" au, "udongo ambao ni mzuri kuotesha mmea."

mwenye masikio, na asikie!

msemo huu unamaanisha, "Kila mmoja anayesikia ninachosema anapaswa kunisikiliza kwa makini" au, "kama kila mmoja amesikia nilichosema anapaswa kuwa makini kwa kile nilichomaanisha." hii pia inaweza kutafsiriwa kama amri. "Ikiwa una masikio ya kusikia, sikiliza kwa makini kwa kile ninachomanisha."

33-06

Habari hii iliwachanganya wale wanafunzi.

Hii ni, "wanafunzi hawakuelewa habari hii."

Ni mtu

Huu mlinganisho unaweza kutafsiriwa kama, "ni kama mtu" au, "Inawakilisha mtu" au, "Inahusiana na mtu" au "anaongelea kuhusu mtu."

hulichua neno kutoka kwake

Hii inaweza kutafsiriwa kama, Huchukua neno la Mungu, anasababisha kulisahau" au, "huiba neno kutoka moyoni mwake ili kwamba hawezi kuliamini neno na kuokolewa." unaweza kuongeza pia haya yafuatayo: ndege walikula mbegu zilizoanguka kwenye njia."

33-07

ardhi yenye miamba

Onyesha ni jinsi gani unaweza kutafsili

ni mtu

Angalia jinsi unaweza kutafsili maelezo haya

analipokea kwa furaha

Hiyo ni, "Wanaamini kwa furaha" au Kukubali kwa furaha kuwa ni kweli."

huangukia mbali

Hiyo ni, "Hamfuati Mungu au kumtii yeye" au, "Kuacha kumfuata au kumtii Mungu"

33-08

ardhi ya miiba

Angalia jinsi unaweza kutafsili hii

ni mtu

Ona jinsi gani unaweza kutafsili hii

kujali

hiyo ni, "Wasiwasi" au "Mahitaji" au Matatizo."

utajiri

hiyo ni, "Tamaa ya utajiri."

Anasa za maisha

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama "Kufanya vitu flani ili kupata anasa" au "Kushughulika na vitu ambavyo zitakupa anasa."

hulisonga

hii ni, "Vuruga" au, "Haribu" au kushinda." haya maneno yanaweza pia kutafsiriwa kama, "Humsababisha kuacha kumpenda Mungu."

haikuweza kuzaa matunda

Hii ni, "Hawezi kuzaa matunda ya kiroho" au, "haonyeshi hali ya Roho wa Mungu ambaye anafanya kazi ndani yake."

33-09

udongo mzuri

Angalia jinsi unaweza kutafsili hii

ni mtu

Angalia jinsi unaweza kutafsili maelezo haya

zaa matunda

...Angalia jinsi unaweza kutafsili kipengele hiki