Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

30-01

Faragha

Hii inamaanisha mahali palipo na watu wachache ambapo wangelikuwa wao pekeyao.

30-02

Walipowasili

Hii ni kwamba, "walifika ng'ambo ya pili ya ziwa" au, "walifika pale."

30-03

bila kuhesabu wanawake na watoto

Hii ni kwamba, "bila kuhesabu wanawake na watoto waliokuwa nao" au " na pia walikuwepo wanawake na watoto zaidi kama ongezeko la idadi ya wanaume." Njia nyingine ya kutafsiri hii inaweza pia kuwa, zaidi ya wanaume, kulikuwa na wanawake na watoto."

Kwa Yesu

Hii ni kwamba, "Yesu alifahamu kwamba" au, Yesu alijua kwamba."

Kama kondoo wasio na mchungaji

Hii inaweza kutafsiriwa kuwa, "waliohatarini na waliopotea, kama vile kondoo wanavyokuwa wanapokuwa hawana mchungaji wa kuwaangalia."

30-04

Baadaye mchana

Hiiinaweza pia kutafsiliwa kama, "Wakati ilipokuwa karibu na jioni."

Watume watu waende zao

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Tafadhali waambie watu waende mjini" au kwa nini usiwambie watu kwenda mahali fulani?" au "Waache watu waende mjini." Hakikisha kwamba itasikika kama ombi la kumsihi mtu, si amri.

30-05

Ni jinsi gani tunaweza kufanya hivyo?

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Hatuwezi kufanya hivyo!" au "Haiwezekani kufanya hivyo!" Wanafunzi hawakuwa wanauliza swali halisi. Isipokuwa, walikuwa wanaeleza kwamba hawakudhani hili kuwa linawezekana.

30-08

Vunja mkate na samaki

Hiyo ni, "kuvunja mkate na samaki."

Haikumalizika

Njia nyingine ya kusema hii ingelikuwa, kulikuwa daima na ziada iliyosalia."

Alitosheka

Hii ni kwamba, "Hawakuwa na njaa tena" au, "hawakuwa na njaa kabisa,"