Kiswahili: Open Bible Stories Translation Notes

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

34-01

Habari

Yesu alitumia habari hizi kufundisha ukweli wa ufalme wa Mungu. haiko wazi kama tukio lilitukia au hakuna. Kama lugha yako ina neno linalounganisha vyote habari za kutunga na za kweli, unaweza kuitumia hapa.

punje ya haradali

Hii pengine inatoakana na mbegu ya haradali Nyeusi, ambayo ina vimbegu vidogo ambavyo vinakua haraka na kuwa mti mkubwa . kama kuna neno katika mti huu kwa Lugha yako, unaweza kutumia. kama hakuna unahitaji mbala wa jina la mti huo wenye sifa zinazofanana.

mbegu ndogo kuliko zote

Hiyo ni, ni mbegu ndogo kuliko zote ambazo watu wanapanda."

34-02

Punje ya haradali

Angalia jinsi unaweza kutafsili hii

kukua

Unaweza kuongeza, "mmea uliokua."

Mimea ya Bustanini

Hii pia inaweza kuytafsiriwa kama, "mmea unaopandwa kwenye bustani."

Kupumzika ndani yako

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "Kukaa juu, "Kutua juu yake."

34-03

Habari

Angalia jinsi unaweza kutafsili hii

hamira

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "chachu" au, "chachu kidogo" inawekwa kwenye unga wa mkate ili kutengeza Donge. mara chache hamira inaweza kuchanganywa na unga mwingi na kuufanya unga wote kuumka.

34-04

Hazina

hiyo ni, "Ni kitu ambacho ni cha thamani."

kuizika tena

Inawezekana pia kuongeza, Ili kwamba hakuna mwingine anaweza kuipata."

akijawa na furaha

Njia nyingine ya kusema hii ni kwamba, "Furaha kuu" au, "Msisimko"

nunua shamba lile

watu wengine wanaweza kuongeza. "Ili kwamba hazina iwe yake."

34-05

Lulu Kamili

Hii ni, "lulu isiyokuwa na kasoro."

Lulu

Kama lulu haijulikani, hii inaweza kutafsiriwa kama, "Jiwe zuri" au, "kama aina fulani ya jiwe."

yenye thamani kubwa

Hii ni, "hiyo ni ya thamani kubwa" au, "hii ilikuwa thamni ya pesa nyingi."

Mfanya Biashara wa Lulu

Hii ni, "Muuzaji wa lulu" au, "Mchuuzi wa lulu."Hii inatokana na mtu ambaye biashara yake ni kununua na kuuza.

34-06

habari

Angalia jinsi unaweza kutafsili hii

wanatumaini matendo yao mema.

Hii ni, "waliamini kuwa matendo yao mema yanawafanya kuwa wenye haki" au, "walijivunia kuwa wakamilifu kwa kushika sheria" au, "Waliamini kuwa matendo yao mema yanamfanya Mungu awafurahi kikamilifu."

Dharau watu wengine

Hii ni "inahusisha watu wengine ambao wana waudhi " au " kuonekana chini kwa watu wengine"

34-07

Viongozi wa dini waliomba hivi

Njia nyingine ya kusema hii ingekuwa, "Hivi ndivyo viongozi wa dini waliomba" au, "viongozi wa dini waliomba kwa njia hii."

mimi simenye dhambi kama

Hii ni, "Mimi si mwenye dhambi kama" au, "mimi ni mwenye haki , si kama."

wasio haki

hiyo ni, "watu wasio haki " au, "Watu wanaofanya mambo maovu" au, "Wajunja sheria'"

34-08

Ninafunga

watawala wa kidini waliamini kuwa kwa kufanya hivi kunaweza kupata Neema kwa Mungu.

Asilimia kumi

Hii ni, "Moja ya Kumi." au "zaka."

34-09

simama mbali

Hii inaweza pia kutafsiriwa kama, "Simama kwa umbali" au, "Kukaa umejitenga."

Hakutazama hata juu mbinguni

Neno "hata" linaashiria kuwa watu kawaida huangalia juu wanapokuwa wanaomba kwa Mungu, lakini huyu mtu hakufanya hivyo kwa sababu alikuwa anaona aibu kwa ajili ya dhambi zake.

alijipigapiga juu ya kifua chake kwa ngumi

Hii inaweza kutafsiriwa kama, "Kwa sababu ya huzuni, alipigapiga kifua chake kwa ngumi" au, "alipigapiga kifua kwa huzuni" kama watu watagundua kuwa hii kuwa ni ngumu kuelewa kwa sababu huwanapiga vifua vyao kwa sababu nyingine, unaweza kutafsiri hii kama, "Alionyesha kukata tamaa."

34-10

kumtangaza kuwa mwenye haki

hii ni, "kumfikiria kuwa ni mwenye haki." hata hivyo watoza ushuru walikuwa wenye dhambi, Mungu alikuwa mwaminifu kwake kwa sababu ya utu wake na toba yake.

kunyenyekea

Hii pia inaweza kutafsiriwa kama, "alijishusha" au, "itakufanya kutokuwa wa muhimu." inaweza kutafsiriwa pia lugha ya mafumbo, "atakushusha"

atakuinua

hiyo ni, "atakupa nafasi ya juu" au, "atakuheshimu."

kujishusha mwenyewe

Hii ni, "Kuchagua kuishi kwa kujishusha" au, "ana tabia za kujishusha yeye mwenyewe."