Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Genesis

Genesis 1

Genesis 1:1-2

Hapo mwanzo Mungu aliumba nini?

Mungu aliziumba mbingu na nchi.

Roho wa Mungu alikuwa akifanya nini hapo mwanzo?

Roho wa Mungu alikuwa akitembea juu ya vilindi juu ya maji.

Genesis 1:3-5

Mungu aliumbaje nuru?

Mungu alisema, "na kuwe na nuru"

Genesis 1:6-8

Mungu alitengeneza nini katika siku ya pili?

Mungu alitengeneza anga katikati ya maji yaliyo kuwa chini ya anga na maji ambayo yalikuwa juu ya anga

Genesis 1:9-10

Mungu aliitaje ardhi kavu na maji yaliyokusanyika?

Mungu aliita ardhi kavu "nchi" na maji yaliyokusanyika "bahari"

Genesis 1:11-13

Ni viumbe gani hai Mungu aliviumba siku ya tatu?

Mungu aliumba mimea, miti ya matunda, na miche.

Genesis 1:14-15

Kusudi la mianga angani ni lipi?

Ni kwa ajili ya kutenganisha mchana na usiku, na kama ishara kwa majira, kwa siku na miaka.

Genesis 1:16-19

Mungu aliumba nini katika siku ya nne?

Mungu aliumba mianga mikuu miwili na nyota.

Genesis 1:20-21

Mungu aliumba nini katika siku ya tano?

Mungu aliumba viumbe hai vya baharini, na ndege.

Genesis 1:22-25

Mungu alitoa amri gani kwa viumbe wa baharini na ndege?

Zaeni na muongezeke.

Genesis 1:26-27

Mungu aliumba nini katika mfano wake?

Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake.

Mtu alipewa mamlaka juu ya vitu gani?

Mungu alimpatia mtu mamlaka juu ya samaki wa baharini, juu ya ndege wa angani, juu ya wanyama wa kufuga, na juu ya kila kitambaacho kinacho tambaa juu ya nchi.

Kitu gani kilikuwa tofauti juu ya jinsi Mungu alivyoumba mtu?

Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake.

Genesis 1:28-29

Mungu alimpatia mtu amri gani?

Zaeni na kuongezeka, jazeni nchi na muitawale.

Mungu alimpatia mtu ale nini?

Mungu aliwapatia wao kila mmea uzaao mbegu na kila mti wenye tunda.

Genesis 1:30-31

Mungu alipoona kila kitu alichokiumba, alifikiri nini juu yake?

Mungu alifikiri ya kwamba kilikuwa chema sana.

Genesis 2

Genesis 2:1-3

Mungu alifanya nini katika siku ya saba?

Alipumzika kutoka kwa kazi yake yote, na kuibariki na kuitakasa siku hiyo.

Genesis 2:4-6

Kabla Yahwe hajasababisha mvua kunyesha, nchi ilikuwa inapataje maji?

Ukungu uliinuka juu kutoka kwenye nchi.

Genesis 2:7-8

Yahwe alimuumbaje mtu?

Yahwe alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi na kupuliza pumzi ya uhai kwake.

Yahwe alimweka wapi mtu wa kwanza?

Katika shamba la Edeni.

Genesis 2:9-14

Miti gani miwili ilikuwa miongoni mwa bustani?

Mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

Genesis 2:15-17

Mtu alipaswa kufanya nini bustanini?

Alipaswa kulima na kutunza bustani.

Yahwe alimpa mtu amri gani kuhusu kile alichopaswa kula?

Unaweza kula katika kila mti bustanini, isipokuwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

Yahwe alisema nini kingetokea iwapo mtu angevunja amri hii?

Katika siku ambayo mtu atavunja amri hii, hakika atakufa.

Genesis 2:18-20

Yahwe alisema nini hakikuwa kizuri?

Alisema haikuwa vizuri ya kwamba mtu alikuwa peke yake.

Yahwe alimfanya mtu kutenda nini na kila kiumbe hai?

Mtu aliwapatia kila kiumbe hai jina.

Ni nini hakikupatikana miongoni mwa viumbe hai?

Msaidizi wa mtu atakayemfaa yeye.

Genesis 2:21-23

Yahwe alimuumbaje mwanamke?

Yahwe alimsababisha mwanamume kulala na kuchukua mbavu za mwanamume, na kumuumba mwanamke kutoka kwa ubavu ule.

Kwa nini mwanamume alimuita "mwanamke"?

Kwa sababu alichukuliwa kutoka kwa mwanamume.

Genesis 2:24-25

Mwanamume na mwanamke wanakuaje mwili mmoja?

Mwanamume anaungana na mwanamke kama mke wake.

Je mwanamume na mke wake walikuwa na aibu kuwa uchi?

Hapana.

Genesis 3

Genesis 3:1-3

Nyoka aliuliza swali gani la kwanza kwa mwanamke?

Nyoka alimuuliza mwanamke, "Je ni kweli Mungu amesema, 'Msile matunda kutoka kwenye mti wowote bustanini'?"

Genesis 3:4-6

Mwanamke aliposema Mungu aliwaambia ya kuwa watakufa iwapo watakula kutoka kwenye mti katikati ya bustani, nyoka alisema nini?

Nyoka alisema, "hakika hamtakufa"

Nyoka alisema nini kingetokea kwa mwanamume na mwanamke iwapo watakula tunda lile?

Nyoka aliwaambia ya kuwa watakuwa kama Mungu, kujua mema na mabaya.

Nini kilimvutia mwanamke kwa tunda la mti?

Aliona kuwa tunda ni zuri kwa chakula, na kuwa linapendeza macho, na kwamba linatamanisha kumfanya mtu awe na hekima.

Ni nani alikula tunda lile?

Mwanamke alikula , na kumpatia sehemu kwa mumewe ambaye alikula pia.

Genesis 3:7-8

Nini kilitokea kwao walipokula lile tunda?

Walipokula, macho yao yalifumbuliwa na wakajua ya kwamba wapo uchi.

Mwanamume na mwanamke walifanya nini Mungu alipokuja bustanini?

Walijificha kutoka kwa Mungu.

Genesis 3:9-11

Kwa nini mwanamume alijificha kutoka kwa Mungu alipokuja bustanini?

Mwanamume alijificha kutoka kwa Mungu kwa sana alikuwa uchi na hivyo kuogopa.

Genesis 3:12-13

Mwanamume alisema ni nani alihusika kumpatia tunda lile?

Mwanamume alisema mwanamke ndiye aliyehusika.

Mwanamke alisema ni nani alihusika kumpatia tunda lile?

Mwanamke alisema ya kwamba nyoka alihusika.

Genesis 3:14-15

Mungu alisema ni aina gani ya mahusiano yangekuwa kati ya nyoka na mwanamke?

Mungu alisema angesababisha wao kuchukiana.

Genesis 3:16

Ni laana gani Mungu alimpatia mwanamke kuhusu kuzaa watoto?

Mungu alizidisha uchungu wa mwanamke maradufu wakati wa kuzaa watoto.

Genesis 3:17-19

Mungu alimpatia laana gani mwanamume kuhusu kazi yake?

Mungu alilaani ardhi ili kwamba iwe kwa kazi ya maumivu ndipo mwanamume atakula kutoka pale.

Genesis 3:20-21

Mwanamume alimpatia jina gani mwanamke, na kwa nini?

Mwanamume alimpatia mwanamke jina la Hawa, kwa sababu alikuwa mama wa viumbe wote hai.

Mungu alitengeneza nini kwa ajili ya Adamu na Hawa, na kwa nini?

Mungu alitengeneza mavazi ya ngozi ili kuwavisha.

Genesis 3:22-24

Kwa nini Mungu alisema ya kwamba sasa Adamu hapaswi kula katika mti wa uzima wa milele?

Mungu alisema ya kwamba kwa kuwa Adamu sasa anajua mema na mabaya hapaswi kula katika mti wa uzima, kwa sababu ataweza kuishi milele.

Mungu alifanya nini kumzuia Adamu kula kutoka katika mti wa uzima?

Mungu alimfukuza mtu kutoka katika bustani na kuweka upanga wa moto pale kulinda njia ya kuelekea mti wa uzima.

Genesis 4

Genesis 4:1-2

Kaini na Habili walifanya kazi gani?

Kaini alilima udongo, na Habili alikuwa mchungaji.

Genesis 4:3-5

Kaini alileta sadaka gani kwa Yahwe?

Kaini alileta baadhi ya matunda ya ardhi.

Habili alileta sadaka gani kwa Yahwe?

Habili alileta baadhi ya wazawa wa kwanza wa mifugo yake na sehemu ya wanyama walionona.

Mungu aliitikiaje sadaka ya Kaini na Habili?

Yahwe alipokea sadaka ya Habili, lakini hakupokea sadaka ya Kaini.

Kaini alionyesha hisia gani?

Kaini alikasirika sana, na uso wake ukahuzunika.

Genesis 4:6-7

Yahwe alimwambia Kaini alitakiwa kufanya nini ili akubalike?

Yahwe alimwambia Kaini kufanya lililo jema na atakubalika.

Genesis 4:8-9

Baadae, nini kilitokea kwa Kaini na Habili shambani?

Kaini aliinuka juu na kumuua Habili.

Yahwe alipomuuliza Kaini ndugu yake alikuwa wapi, Kaini alisema nini?

Kaini alisema, "mimi sijui. Je mimi ni mlinzi wa ndugu yangu"?

Genesis 4:10-12

Laana ya Mungu juu ya Kaini ilikuwa ipi?

Laana ya Kaini ilikuwa kwamba nchi haitazaa nguvu yake kwake na angekuwa kimbizi na mzururaji.

Genesis 4:13-15

Yahwe alifanya nini kuhakikisha hakuna mtu wa kumuua Kaini?

Yahwe aliweka alama juu ya Kaini.

Genesis 4:16-17

Kaini alikwenda kuishi wapi?

Kaini aliishi katika nchi ya Nodi, mashariki mwa Edeni.

Genesis 4:18-22

Mzawa wa Kaini Lameki alikuwa na wake wangapi?

Lameki alikuwa na wake wawili.

Genesis 4:23-24

Lameki aliwaambia wake zake amefanya kitu gani?

Lameki aliwaambia wake zake ya kwamba amemuua mtu.

Genesis 4:25-26

Mwana mwingine aliyezaliwa kwa Adamu na Hawa alikuwa anaitwa nani?

Mwana mwingine wa Adamu na Hawa alikuwa anaitwa Sethi.

Watu walianza kufanya nini katika siku za mwana wa Sethi Enoshi?

Watu walianza kuliita jina la Yahwe.

Genesis 5

Genesis 5:1-2

Sura ya tano ya Mwanzo ni kumbukumbu ya nini?

Sura ya tano ya Mwanzo ni kumbukumbu ya vizazi vya Adamu.

Binadamu aliumbwa katika mfano wa nani?

Binadamu aliumbwa katika mfano wa Mungu.

Mungu aliumba binadamu wa jinsia gani?

Mungu aliumba binadamu wa kiume na kike.

Genesis 5:3-5

Adamu aliishi muda gani?

Adamu aliishi miaka 930.

Genesis 5:6-11

Sethi aliishi muda gani?

Sethi aliishi miaka 912.

Genesis 5:12-17

Kenani aliishi muda gani?

Kenani aliishi miaka 910.

Genesis 5:18-20

Yaredi aliishi muda gani?

Yaredi aliishi miaka 962.

Genesis 5:21-27

Mahusiano ya Henoko na Mungu yalikuwaje, na nini kilitokea kwake?

Henoko alitembea na Mungu, na Mungu akamtwaa.

Genesis 5:28-31

Lameki alisema nini kuhusu mwanawe Nuhu?

Lameki alisema ya kwamba Nuhu atawapa wanadamu pumziko kutoka kwa kazi na taabu iliyosababishwa na ardhi ambayo Mungu aliilaani.

Genesis 5:32

Wana wa Nuhu walikuwa kina nani?

Wana wa Nuhu walikuwa Shemu, Hamu, na Yafethi.

Genesis 6

Genesis 6:1-3

Binadamu alipoongezeka juu ya nchi, wana wa Mungu walifanya nini?

Wana wa Mungu walijitwalia kwa ajili yao wake katika binti za binadamu.

Mungu alisema nini juu ya urefu wa maisha ya mwanadamu?

Mungu alisema ya kwamba mwanadamu ataishi miaka 120.

Genesis 6:4

Watu hodari wa zamani, watu wenye sifa walikuwa kina nani?

Watu hodari wa zamani walikuwa majitu makubwa waliozaliwa kutokana na ndoa ya wana wa Mungu na binti za watu.

Genesis 6:5-6

Yahwe aliona kitu gani ndani ya mioyo ya wanadamu katika siku hizo?

Yahwe aliona ya kwamba uovu wa wanadamu ulikuwa mkubwa, na kwamba kila wazo lao lilikuwa ovu.

Genesis 6:7-8

Yahwe aliamua kufanya nini na mwanadamu?

Yahwe aliamua kuwafutilia wanadamu katika uso wa nchi.

Lakini ni nani aliyepata kibali na Yahwe?

Nuhu alipata kibali na Yahwe.

Genesis 6:9-12

Nuhu alikuwa mtu wa aina gani?

Nuhu alikuwa mtu mtakatifu, asiye na lawama, na mtu aliyetembea pamoja na Mungu.

Genesis 6:13-15

Mungu alimwambia nini Nuhu kufanya kabla Mungu hajaangamiza wanadamu?

Mungu alimwambia Nuhu kujenga safina.

Genesis 6:16-17

Mungu alisema ataangamiza wenye mwili wote wenye pumzi ya uhai ndani mwao kwa jinsi gani?

Mungu alisema ya kwamba alikwenda kuleta gharika la maji juu ya nchi.

Genesis 6:18-19

Lakini Mungu alithibitisha agano lake na nani?

Mungu alithibitisha agano lake na Nuhu.

Mungu alimwambia Nuhu amlete nani ndani ya safina?

Mungu alimwambia Nuhu kumleta mke wake, wanawe watatu wa kiume, na wake za wanawe.

Ni wanyama gani waliotakiwa kuletwa ndani ya safina kuwekwa hai?

Wawili wa kila aina ya kiumbe hai, wa kiume na kike, walitakiwa kuletwa ndani ya safina.

Genesis 6:20-22

Nuhu aliitikiaje amri ya Mungu?

Nuhu alifanya yote aliyoamriwa na Mungu.

Genesis 7

Genesis 7:1-3

Dume na jike saba wa aina gani ya wanyama walipaswa kuingia ndani ya safina?

Dume na jike saba wa kila mnyama safi na ndege walipaswa kuingia ndani ya safina.

Genesis 7:4-5

Mungu alisema mvua itaendelea juu ya nchi kwa muda gani?

Mungu alisema ya kwamba mvua itaendelea kwa siku arobaini za mchana na siku arobaini za usiku.

Genesis 7:6-7

Nuhu alikuwa na umri gani gharika lilipokuja juu ya nchi?

Nuhu alikuwa na umri wa miaka mia sita pale ambapo gharika lilikuja juu ya nchi.

Genesis 7:8-10

Nuhu aliwaletaje wanyama ndani ya safina?

Wanyama walikuja kwa Nuhu na kuingia ndani ya safina.

Genesis 7:11-14

Maji ya gharika yalitoka katika vyanzo gani viwili?

Maji yalitoka katika chemichemi zote za vilindi , na kutoka angani.

Genesis 7:15-18

Pale watu na wanyama walipokwisha ingia ndani ya safina, nani aliufunga mlango?

Yahwe aliufunga mlango nyuma yao.

Genesis 7:19-20

Maji yalipanda kimo gani juu ya nchi?

Maji yalipanda urefu wa dhiraa kumi na tano juu ya vilele vya milima.

Genesis 7:21-22

Nini kilikufa juu ya nchi kwa sababu ya gharika?

Viumbe wote waliotembea juu ya nchi, na wanadamu wote walikufa.

Genesis 7:23-24

Watu gani pekee ndio waliosalia juu ya nchi?

Nuhu pekee na wale waliokuwa naye ndani ya safina walibaki hai.

Genesis 8

Genesis 8:1-3

Mungu alifanyaje maji kupungua?

Mungu alifanya upepo kuvuma, chemichemi za vilindi kufungwa, na mvua kusimama.

Genesis 8:4-7

Safina lilikuja kutulia wapi juu ya nchi?

Safina lilikuja kutulia juu ya milima ya Ararati.

Genesis 8:8-9

Nini kilitokea mara ya kwanza Nuhu alipomtuma njiwa kutoka kwenye safina?

Mara ya kwanza, njiwa hakupata sehemu ya kutua nyayo zake, na akarudi kwa Nuhu katika safina.

Genesis 8:10-12

Nini kilitokea mara ya pili Nuhu alipomtuma njiwa kutoka katika safina?

Mara ya pili, njiwa alirudi na jani bichi la mzeituni lililochumwa.

Nini kilitokea mara ya tatu Nuhu alipomtuma njiwa kutoka katika safina?

Mara ya tatu, njiwa hakurudi kwa Nuhu.

Genesis 8:13-14

Nuhu aliona nini alipotoa kifuniko cha safina na kutazama nje?

Nuhu aliona ya kwamba uso wa nchi ulikuwa umekauka.

Genesis 8:15-19

Mungu alitaka viumbe wote katika safina kwenda kufanya nini walipotoka katika safina?

Mungu alitaka viumbe wote hai kuzaana na kuongezeka juu ya nchi.

Genesis 8:20-22

Nuhu alifanya nini alipoondoka katika safina?

Nuhu alijenga madhabahu kwa ajili ya Yahwe na sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.

Ahadi gani mbili Mungu alizifanya kwa wanadamu katika kipindi hiki?

Mungu aliahidi kutolaani tena ardhi, na kutoangamiza kila kiumbe hai tena.

Mungu alisema mwanadamu ana nia gani tangu utoto wake?

Mungu alisema ya kwamba nia ya mwanadamu kutoka utotoni ilikuwa ni ya uovu.

Genesis 9

Genesis 9:1-2

Mungu alimwambia nini Nuhu na wanawe kufanya baada ya kutoka katika safina?

Mungu alimwambia Nuhu na wanawe kuzaana, kuongezeka na kujaza nchi.

Genesis 9:3-4

Mungu alimpatia nini Nuhu na wanawe sasa kama chakula?

Mungu alimpatia Nuhu na wanawe wote mimea ya kijani na kila kitu chenye uhai kama chakula.

Mungu aliamuruje ile nyama iweze kuliwa kwa namna gani?

Mungu aliamuru ya kwamba nyama isiliwe na damu ndani mwake.

Mungu alisema ni nini kimo ndani ya damu?

Mungu alisema ya kwamba kulikuwa na uhai ndani ya damu.

Genesis 9:5-10

Mungu alitamka ni adhabu gani kwa kumwaga damu ya binadamu?

Mungu alitamka ya kwamba yule atakayemwaga damu ya mtu atalazimika kumwaga damu yake.

Mungu alimfanya mwanadamu kwa mfano wa nani?

Mungu alimfanya mwanamume katika mfano wa Mungu.

Genesis 9:11-13

Mungu alitoa ishara gani kama agano alilofanya pamoja na nchi?

Mungu aliweka upinde wa mvua katika mawingu kama ishara ya agano alilofanya pamoja na nchi.

Genesis 9:14-17

Mungu alifanya ahadi gani ya agano na kila kitu kilichokuwa kikiishi juu ya nchi?

Mungu alifanya agano la ahadi ya kwamba kila chenye mwili hatakiangamiza kwa gharika tena.

Genesis 9:18-19

Majina ya wana wa Nuhu yalikuwa ni yapi?

Majina ya wana watatu wa Nuhu yalikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi.

Genesis 9:20-21

Nini kilitokea kwa Nuhu baada ya kupanda mizabibu?

Baada ya kupanda mizabibu, Nuhu alikunywa sehemu ya divai na akalewa.

Genesis 9:22-23

Shemu na Yafethi walifunikaje uchi wa baba yao?

Shemu na Yafethi walitembea kinyumenyume na kanzu, huku wakiwa wametazama upande mwingine, ili kufunika uchi wa baba yao.

Genesis 9:24-25

Nuhu aliweka laana gani juu ya Hamu?

Nuhu alimlaani Hamu na kusema, "Alaaniwe Kanaani. Na awe mtumishi kwa watumishi wa ndugu zake"

Genesis 9:26-29

Nuhu alimbariki nani?

Nuhu aliwabariki wote Shemu na Yafethi.

Genesis 10

Genesis 10:2-7

Baada ya gharika, hatimaye vizazi vya Nuhu vilisambaa kwenye nchi katika koo, na waliposambaa, kila koo ilikuwa na kitu gani chake?

Hatimaye kila koo ziliposambaa, kila koo ikawa na lugha yake.

Genesis 10:8-10

Nimrodi, uzao wa hamu, alijulikana kwa lipi?

Nimrodi alijulikana kama mwindaji hodari mbele ya Yahwe.

Miji ya msingi ya kwanza ya Nimrodi katika nchi ya Shinari ilikuwa ipi?

Miji ya msingi ya Nimrodi ya kwanza ilikuwa Babeli.

Genesis 10:11-14

Juu ya ardhi ya Shinari, sehemu gani nyingine Nimrodi alijenga miji?

Nimrodi alijenga miji katika Assiria.

Genesis 10:15-18

Kaanani alikuwa uzao wa mwana wa nani wa Nuhu?

Kaanani alikuwa uzao wa Hamu.

Genesis 10:19-23

Baada ya gharika, hatimaye vizazi vya Nuhu vilisambaa kwenye nchi katika koo, na waliposambaa, kila koo ilikuwa na kitu gani chake?

Hatimaye kila koo ziliposambaa, kila koo ikawa na lugha yake.

Genesis 10:24-29

Nini kilitokea katika siku za Pelegi, uzao wa Shemu.

Katika siku za Pelegi, nchi ilikuwa imegawanyika.

Genesis 10:30-31

Baada ya gharika, hatimaye vizazi vya Nuhu vilisambaa kwenye nchi katika koo, na waliposambaa, kila koo ilikuwa na kitu gani chake?

Hatimaye kila koo ziliposambaa, kila koo ikawa na lugha yake.

Genesis 10:32

Mataifa yaliyosambaa juu ya uso wa nchi yalitoka wapi baada ta gharika?

Mataifa yalitoka katika koo za wana wa Nuhu.

Genesis 11

Genesis 11:1-2

Mara baada ya gharika, kulikuwa na lugha ngapi juu ya uso wa nchi yote?

Mara baada ya gharika, kulikuwa na lugha moja juu ya nchi yote.

Kwa nini watu walijenga mji na mnara wao?

Watu walijenga mji wao na mnara katika nchi ya Shinari.

Genesis 11:3-4

Watu waliamua kufanya nini badala ya kusambaa juu ya nchi yote kama vile Mungu alivyowaamuru?

Badala ya kusambaa juu ya nchi yote kama vile Mungu alivyoamuru, watu waliamua kujenga mji na mnara.

Watu walitaka kutengeneza nini kwa ajili yao wenyewe?

Watu walitaka kujitengenezea jina kwa ajili yao.

Genesis 11:5-7

Yahwe alishuka chini kufanya nini kwa watu?

Yahwe alishuka chini na kuchanganya lugha ya watu.

Kwa nini Mungu alifanya hivi?

Mungu alichanganya lugha zao ili wasiweze kuelewana wao kwa wao.

Genesis 11:8-9

Mungu alisababisha nini kwa watu kufanya?

Mungu alisababisha watu kusambaa juu ya uso wa nchi yote, kama alivyokuwa ameamuru.

Jina la mji ambao watu walijaribu kujenga ulikuwa unaitwaje?

Jina la mji ulikuwa Babeli.

Genesis 11:10-23

Ni vizazi wa mwana yupi wa Nuhu wanapewa katika sura hii?

Vizazi vya Shemu, mwana wa Nuhu, wanapewa katika sura hii.

Genesis 11:24-26

Nani alikuwa baba wa Abramu?

Baba wa Abramu alikuwa Tera.

Genesis 11:27-28

Mwana wa Tera Harani alikuwa na mwana mwenye jina gani?

Mwana wa Tera Harani alikuwa na mwana aliyeitwa Lutu.

Tera alikuwa akiishi wapi?

Tera aliishi Uru miongoni mwa Wakaldayo.

Genesis 11:29-30

Jina la mke wa Abramu lilikuwa nani?

Mke wa Abramu alikuwa akiitwa Sarai.

Mke wa Abramu alikuwa na tatizo gani?

Mke wa Abramu Sarai alikuwa tasa na hakuwa na watoto.

Genesis 11:31-32

Tera alihama pamoja na Abramu, Sarai na Lutu kwenda wapi?

Tera alihama katika nchi ya Kaanani pamoja na Abramu, Sarai na Lutu.

Genesis 12

Genesis 12:1-3

Abramu alipokuwa akiishi Harani, Yahwe alimwambia Abramu afanye nini?

Yahwe alimwambia Abramu kuacha nyumba ya baba yake na kwenda katika nchi ambayo angemuonyesha Abramu.

Ahadi gani aliyoifanya Yahwe kwa Abramu?

Yahwe aliahidi ya kwamba angembariki Abramu, kumfanya kuwa taifa kubwa, na kubariki familia zote za duniani kupitia kwake.

Genesis 12:4-5

Nani alisafiri pamoja na Abramu?

Abramu alisafiri pamoja na Sarai, mke wake, na Lutu, mwana wa ndugu yake.

Abramu alisafiri katika nchi gani?

Abramu alisafiri katika nchi ya Kaanani.

Genesis 12:6-7

Yahwe alipomtokea Abramu, alitoa ahadi gani kwake?

Yahwe aliahidi ya kwamba uzao wa Abramu utaishi Kaanani.

Genesis 12:8-9

Abramu alimuabuduje Yahwe?

Abramu alijenga madhabahu kwa ajili ya Yahwe na kuliita jina la Yahwe.

Genesis 12:10-13

Abramu alisafiri kwenda wapi, alipoondoka Kaanani?

Abrahamu alisafiri kwenda Misri, alipoondoka Kaanani.

Alipoingia Misri, Abramu alihangaishwa na nini?

Abramu alihangaishwa na Wamisri kumuua na kuchukua mke wake Sarai kwa sababu alikuwa mzuri.

Abramu alimwambia Sarai awaambie nini Wamisri wote juu yake?

Abramu alimuomba Sarai kuwaambia Wamisri ya kwamba yeye alikuwa dada wa Abramu.

Genesis 12:14-16

Nini kilitokea kwa Sarai alipoingia Misri?

Farao alimchukua Sarai katika nyumba yake.

Genesis 12:17-20

Nini kilitokea kwa Farao katika kipindi hiki?

Yahwe akampiga Farao na nyumba yake na mapigo makuu.

Farao alimuuliza Abramu swali gani?

Farao alimuuliza Abramu kwa nini alimwambia ya kwamba Sarai alikuwa dada yake badala ya mke wake.

Farao alifanya nini na Abramu na Sarai?

Farao aliwaondoa Abramu na Sarai.

Genesis 13

Genesis 13:1-4

Baada ya kuondoka Misri, Abramu alisafiri kwenda wapi?

Abramu alisafiri kwenda Negebu.

Abramu alibeba nini pamoja naye?

Abramu alibeba wanyama wengi, na fedha na dhahabu nyingi.

Genesis 13:5-7

Kwa nini kulikuwa na ugomvi kati ya wachungaji wa Abramu na wa Lutu?

Kulikuwa na ugomvi kwa sababu nchi haikuweza kuwatunza Abramu na Lutu walipoishi karibu pamoja na mali zao zote.

Genesis 13:8-9

Abramu alitoa ahadi gani kwa Lutu

Abramu alimwambia Lutu kuchagua wapi pa kuishi, na kisha Abramu angetafuta mahali pake pa kuishi tofauti na Lutu.

Genesis 13:10-11

Lutu alichagua kusihi wapi na kwa nini?

Lutu alichagua kuhama mashariki na kuishi katika nchi tambarare za Yordani kwa sababu zilikuwa na maji kila mahali.

Genesis 13:12-13

Abramu alikuwa akiishi wapi?

Abramu aliishi katika nchi ya Kaanani.

Aina gani ya watu walikuwa wakiishi Sodoma?

Watu wa Sodoma walikuwa wenye dhambi waovu dhidi ya Yawhe.

Genesis 13:14-15

Katika kipindi hiki, Yahwe alisema angempatia nini Abramu?

Yahwe aliahidi ya kwamba nchi yote ambayo Abramu aliweza kuiona pale alipokuwa amesimama ingepewa kwake.

Genesis 13:16-18

Yahwe alimwambia Abramu atakuwa na vizazi vingapi?

Yahwe alimwambia Abramu ya kuwa angekuwa na vizazi zaidi ya uwezo wa kuhesabu, "wengi kama mavumbi ya nchi"

Abramu alikwenda karibu na mji upi?

Abramu alikwenda karibu na mji wa Hebroni.

Genesis 14

Genesis 14:10-12

Nini kilitokea kwa Sodoma kama matokeo ya vita ya wafalme katika bonde la Sidimu?

Mali zote za Sodoma zilichukuliwa, na Lutu pamoja na mali zake zilichukuliwa pia.

Genesis 14:13-14

Abramu alifanya nini alipoambiwa ya kwamba Lutu alichukuliwa?

Abramu alikusanya wanamume wake waliofunzwa 318 kuwafuata.

Genesis 14:15-16

Abramu alipigana karibu na mji gani mkubwa, na nini kilikuwa matokeo ya vita hii?

Abramu alipigana wafalme wa kaskazini mwa Dameski, na alirudisha mali, Lutu, na watu wengine.

Genesis 14:17-18

Wafalme gani wawili walikutana na Abramu aliporudi?

Mfalme wa Sodoma na Melkizedeki, mfalme wa Salemu, alikutana na Abramu aliporudi.

Mahusiano ya Melkizedeki na Mungu yalikuwaje?

Melkizedeki alikuwa kuhani wa Mungu wa Juu Sana.

Melkizedeki alileta nini pamoja naye alipokutana na Abramu?

Melkizedeki alileta mkate na divai pamoja naye alipokutana na Abramu.

Genesis 14:19-20

Melkizedeki alimwambia nini Abramu?

Melkizedeki alimbariki Abramu, na kumbariki Mungu Aliye Juu Sana.

Abramu alifanya nini baada ya Melkizedeki kuzungumza naye?

Abramu alimpatia Melkizedeki moja ya kumi ya kila kitu.

Genesis 14:21-24

Mfalme wa Sodoma alitoa ahadi gani kwa Abramu?

Mfalme wa Sodoma aliahidi kumruhusu Abramu kukaa na mali zote, kama Abramu atawapa watu kwa mfalme.

Kwa nini Abramu hakutaka mali yoyote ile?

Abramu alikuwa ameinua mkono wake kwa Yahwe, Mungu aliye Juu Sana, na hakutaka mfalme wa Sodoma kuweza kusema ya kwamba amemfanya Abramu kuwa tajiri.

Abramu aliitikiaje kwa ahadi ya mfalme wa Sodoma?

Abramu alisema ya kwamba hakutaka mali yoyote ile, isipokuwa kile walichokula vijana na sehemu kwa ajili ya wanamume waliokwenda naye.

Genesis 15

Genesis 15:1-3

Yahwe alipojitokeza kwa Abramu, alimpatia Abramu tumaini gani?

Yahwe alimwambia Abramu kutokuwa na hofu, na kwamba alikuwa ngao ya Abramu na dhawabu yake kubwa sana.

Abramu alikuwa na wasiwasi juu ya nini?

Abramu alikuwa na wasiwasi kwa sababu alikuwa bado hana mtoto, na mtumishi wa nyumba yake alikuwa ndiye mrithi wake.

Genesis 15:4-5

Yahwe alisema ni nani angekuwa mrithi wa Abramu?

Yahwe alisema ya kwamba mmoja atokaye kutoka kwa mwili wa Abramu atakuwa mrithi wake.

Yahwe alisema Abramu atakuwa na vizazi vingapi?

Yahwe alisema ya kwamba Abramu angekuwa na vizazi vingi kama wingi wa nyota.

Genesis 15:6-8

Abramu aliitikiaje ahadi ya Yahwe, na kisha Yahwe alifanya nini?

Abramu alimuamini Yahwe, na Yahwe alimhesabia Abramu kuwa mwenye haki.

Abramu alimuuliza Yahwe swali gani kuhusu nchi?

Abramu alimuuliza Yahwe, "nitajuaje kuwa nitairithi?"

Genesis 15:9-11

Abramu alifanya nini na wanyama alioambiwa kuwaleta?

Abramu aliwakata wanyama mara mbili na kuwaweka kila nyama mkabala na nyenzake.

Genesis 15:12-13

Nini kilitokea kwa Abramu jua lilipokuwa linazama?

Jua lilipokuwa likizama chini, Abramu alilala usingizi mzito na giza kuu ya kutisha ikamfunika.

Yahwe alisema vizazi vya Abramu vitatumikishwa na kuteswa kwa muda gani?

Yahwe alimwambia Abramu vizazi vyake vitatumikishwa na kuteswa kwa miaka mia nne.

Genesis 15:14-16

Yahwe alisema nini kitatokea kwa taifa ambalo litatumikisha vizazi vya Abramu?

Yahwe alisema ya kwamba atahukumu taifa hilo.

Yahwe alisema maisha ya Abramu yatamalizikaje?

Yahwe alisema ya kwamba Abramu atakufa kwa amani katika uzee mwema.

Nini kitafikia kikomo kabla vizazi vya Abramu havijarudi katika nchi iliyoahidiwa kwao?

Dhambi ya Waamori itafikia kikomo kabla ya vizazi vya Abramu kurudi.

Genesis 15:17-21

Kitu gani kilitokea miongoni mwa vipande vya wanyama alioandaa Abramu usiku huo?

Chungu cha moshi wenye moto na miali ya mwanga ilipita kati ya vile vipande vya wanyama.

Yahwe alifanya agano gani na Abramu siku hiyo?

Yahwe alifanya agano na Abramu ya kwamba angempatia nchi hii uzao wa Abramu.

Genesis 16

Genesis 16:1-4

Sarai alikuwa na wazo gani kwa ajili ya kumpatia Abramu uzao?

Sarai alimwambia Abramu kulala na mtumishi wake Hajiri, ili kwamba apate watoto kupitia kwake.

Nini kilitokea kati ya Hajiri na Sarai pale Hajiri alipobeba mimba ya mtoto wa Abramu?

Baada ya Hajiri kushika mimba, Hajiri alimdharau Sarai.

Genesis 16:5-8

Sarai alitoa malalamiko gani kwa Abramu, na Abramu aliitikiaje?

Sarai alilalamika ya kwamba lilikuwa kosa la Abramu kwa Hajiri kumdharau, na Abramu akamwambia Sarai kufanya alichofikiri ni sahihi kwa Hajiri.

Sarai alimtendeaje Hajiri baada ya Hajiri kupata mimba, na Hajiri alifanyaje?

Sarai alimtendea ukatili Hajiri, na Hajiri alitoroka.

Genesis 16:9-10

Malaika wa Yahwe alimwambia Hajiri kufanya nini katika jangwa?

Malaika wa Yahwe alimwambia Hajiri kurudi kwa Sarai na kujishusha chini ya mamlaka yake.

Malaika wa Yahwe alitoa ahadi gani kwa Hajiri?

Malaika wa Yahwe alimuahidi Hajiri ya kwamba vizazi wake watakuwa wengi wasioweza kuhesabika.

Genesis 16:11-12

Kwa nini Hajiri aliambiwa kumuita mwanawe Ishmaeli?

Hajiri aliambiwa kumuita mwanawe Ishmaeli kwa sababu Yahwe amesikia mateso yake.

Ishmaeli atawatendeaje watu wengine?

Ishmaeli atakuwa na uhasama dhidi ya kila mtu, na ataishi kando na ndugu zake wote.

Genesis 16:13-14

Hajiri alimpatia jina gani Yahwe?

Hajiri alimpatia Yahwe jina la, "Mungu anayeniona"

Genesis 16:15-16

Abramu alikuwa na umri gani Ishmaeli alipozaliwa?

Abramu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita Ishmaeli alipozaliwa.

Genesis 17

Genesis 17:1-2

Abramu alikuwa na umri gani Yahwe alipomtokea tena kuthibitisha agano lake pamoja naye?

Abramu alikuwa na miaka tisini na tisa Yahwe alipomtokea tane Abramu.

Yawhe alimpatia Abramu amri gani kuhusu njia ya maisha ya Abramu?

Yahwe alimuamuru Abramu kuenenda mbele yake kikamilifu.

Genesis 17:3-6

Yahwe alibadili jina la Abramu kuwa nani, na jina lina maana gani?

Yahwe alibadili jina la Abramu kuwa Abrahamu ambayo ina maana ya "baba wa mataifa mengi"

Genesis 17:7-8

Yahwe alitoa nini kwa vizazi vya Abrahamu kama sehemu ya agano?

Yahwe aliwapa vizazi vya Abrahamu nchi yote ya Kaanani kama sehemu ya agano.

Yahwe alisema mahusiano kati ya vizazi vya Abrahamu na Yahwe yangekuwaje?

Yahwe alisema ya kwamba angekuwa Mungu kwa vizazi vya Abrahamu.

Genesis 17:9-11

Yahwe aliamuru nini kifanyike kama ishara ya agano kati ya Abrahamu na Yahwe?

Yahwe aliamuru ya kwamba kila mwanamume altahiriwe kama ishara ya agano kati ya Abrahamu na Yahwe.

Genesis 17:12-14

Mtoto alitahiriwa katika umri gani?

Mtoto alipaswa kutahiriwa baadaya siku nane.

Mgeni aliyejiunga na familia ambayo ilikuwa na agano na Yahwe ilipaswa kufanywa nini?

Wageni waliojiunga na nyumba iliyokuwa ndani ya agano na Yahwe pia walipaswa kutahiriwa.

Nini kilitokea kwa mwanamume yeyote ambaye hakutahiriwa?

Mwanamume yeyote ambaye hakutahiriwa alitengwa na watu wake kwa sababu alivunja agano.

Genesis 17:15-16

Yahwe alibadili jina la Sarai kuwa nani?

Yahwe alibadili jina la Sarai kuwa Sara.

Yahwe aliahidi kungekuja nini kwa Sara?

Yahwe aliahidi ya kwamba mwana wa Abrahamu angekuja kwa Sara.

Genesis 17:17-18

Ni kwa namna gani Abrahamu alichukulia ahadi ya Yahwe kuhusu Sara?

Abrahamu alicheka na kuuliza ni namna gani mtoto anaweza kuzaliwa kwa mwanamume na mwanamke ambao ni wazee sana.

Genesis 17:19-23

Mungu alisema Abrahamu alipaswa kumpatia jina lipi mwanawe ambaye angekuja kwa Sara?

Mungu alisema ya kwamba Abrahamu anapaswa kumtaja mwanawe Isaka.

Mungu alisema angethibitisha nini na Isaka?

Mungu alisema ya kwamba angethibitisha agano lake na Isaka.

Mungu alitoa ahadi gani kuhusu Ishmaeli?

Mungu aliahidi kumbariki Ishmaeli, kumzidishia, na kumfanya kuwa taifa kubwa.

Genesis 17:24-27

Abrahamu alifanya nini katika siku hiyo, baada ya Mungu kumuacha Abrahamu?

Katika siku hiyo, Abrahamu alitahiri wanamume wote wa nyumba yake.

Ishmaeli alikuwa na umri wa miaka mingapi alipotahiriwa?

Ishmaeli alikuwa na umri wa miaka kumi na tatu alipotahiriwa.

Genesis 18

Genesis 18:1-2

Abrahamu alipokuwa ameketi mlangoni mwa hema lake, aliona nini alipotazama juu?

Abrahamu aliona wanamume watatu wamesimama mbele yake.

Genesis 18:3-8

Abrahamu aliwapatia nini wanamume hawa?

Abrahamu aliwapatia wanamume hawa maji ya kunawa, na chakula kidogo.

Genesis 18:9-10

Sara alikuwa wapi mgeni alipotoa utabiri wake?

Sara alikuwa ndani ya tenti.

Mgeni mmoja alitoa utabiri gani kuhusu Sara?

Mgeni mmoja alisema ya kwamba atakaporudi, Sara angekuwa na mtoto wa kiume.

Genesis 18:11-12

Sara alichukuliaje utabiri wa mgeni?

Sara alicheka mwenyewe aliposikia utabiri wa mgeni.

Genesis 18:13-15

Yahwe, mgeni, alisema kitu gani kuhusu mwitikio wa Sara?

Yahwe alimuuliza Sara kwa nini alicheka, kwa kusema, "Je kuna jambo lolote gumu sana kwa Yahwe?"

Genesis 18:16-19

Wanamume walipoondoka katika nyumba ya Abrahamu, walielekea upande gani?

Wanamume waliondoka nyumbani mwa Abrahamu na kuelekea upande wa Sodoma.

Yahwe aliuliza swali gani walipokuwa wakitembea?

Yahwe alisema, "Je nimfiche Abrahamu kile ninachokusudia kufanya"?

Yahwe alisema Abrahamu anapaswa kufanya nini ili kwamba Yahwe aweze kutimiza ahadi iliyopewa kwa Abrahamu?

Yahwe alisema ya kwamba Abrahamu anapaswa kuwaongoza watoto wake na nyumba yake kutenda utakatifu na haki.

Genesis 18:20-21

Kwa nini wanamume walikuwa wakielekea upande wa Sodoma?

Wanamume walikuwa wakielekea upande wa Sodoma kwa sababu vilio dhidi ya Sodoma na Gomora vilikuwa vikubwa, na walitaka kuona kama miji ilikuwa na uovu kama vilio vilivyoashiria.

Genesis 18:22-23

Abrahamu aliposimama na Yahwe, alimuuliza swali gani Yahwe?

Abrahamu aliuliza, "Je utawafutilia mbali watakatifu pamoja na waovu?"

Genesis 18:24-26

Yahwe alisema angefanya nini iwapo kungekuwa na watakatifu hamsini ndani ya mji?

Yahwe alisema angeacha kuangamiza sehemu ile yote kwa niaba yao.

Genesis 18:27-28

Yahwe alisema angefanya nini iwapo kungekuwa na watakatifu arobaini na tano ndani ya mji?

Yahwe alisema angeacha kuangamiza sehemu ile yote kwa niaba yao.

Genesis 18:29-31

Yahwe alisema angefanya nini iwapo kungekuwa na watakatifu arobaini ndani ya mji?

Yahwe alisema angeacha kuangamiza sehemu ile yote kwa niaba yao.

Yahwe alisema angefanya nini iwapo kungekuwa na watakatifu thelathini ndani ya mji?

Yahwe alisema angeacha kuangamiza sehemu ile yote kwa niaba yao.

Yahwe alisema angefanya nini iwapo kungekuwa na watakatifu ishirini ndani ya mji?

Yahwe alisema angeacha kuangamiza sehemu ile yote kwa niaba yao.

Genesis 18:32-33

Yahwe alisema angefanya nini iwapo kungekuwa na watakatifu kumi ndani ya mji?

Yahwe alisema angeacha kuangamiza sehemu ile yote kwa niaba yao.

Genesis 19

Genesis 19:1-3

Lutu alipowaona wale malaika wawili wakija Sodoma, alitaka kuwapa nini?

Lutu aliwaomba ya kwamba wakae katika nyumba yake kwa usiku, na kisha kuondoka asubuhi.

Mwitikio wa malaika kwa Lutu ulikuaje?

Malaika walisema ya kwamba wangekaa usiku katika uwanja wa mjini.

Kwa msisitizo wa Lutu, hatimaye malaika waliamua kukaa wapi usiku huo?

Hatimaye, malaika walienda pamoja na Lutu katika nyumba yake kwa usiku huo.

Genesis 19:4-5

Wanamume wa mji waliozunguka nyumba ya Lutu walimtaka Lutu kufanya nini?

Wanamume walimtaka Lutu kuwatoa nje wanamume wale wawili waliomtembelea, ili waweze kulala nao.

Genesis 19:6-8

Lutu aliwapa nini wanamume wa mji kama mbadala?

Lutu aliwapa wanamume wa mji binti zake wawili badala ya wageni wawili.

Genesis 19:9

Wanamume waliitikiaje kwa ahadi ya Lutu?

Wanamume walimwambia Lutu kusimama nyuma na karibu wavunje mlango.

Genesis 19:10-11

Malaika walifanya nini punde?

Malaika walimvuta Lutu nyuma ndani ya nyumba na kuwapiga wanamume nje kwa upofu.

Genesis 19:12-13

Malaika walisema walitumwa kufanya nini na Yahwe?

Malaika walisema walitumwa kuangamiza huo mji.

Genesis 19:14-15

Wakwe za Lutu walipokeaje pale Lutu alipowaambia kuharakisha na kuondoka Sodoma kwa sababi ilikuwa inakaribia kuangamizwa?

Wakwe za Lutu walifikiri Lutu alikuwa akitania.

Asubuhi palipokucha, malaika walimwambia Lutu kufanya nini?

Malaika walimwambia Lutu kumchukua mke wake na binti zake na kuondoka nje ya mji.

Genesis 19:16-20

Kwa nini malaika waliwaleta Lutu na familia yake kwa kuwashika mikono yao nje ya mji licha ya Lutu kukawia-kawia?

Malaika waliwaweka nje ya mji kwa sababu Yahwe alikuwa amewahurumia.

Malaika walitoa maelekezo gani kwa Lutu walipokuwa nje ya mji?

Malaika walimwambia Lutu na familia yake kutoroka ili waokoe nafsi zao na kutotazama nyuma.

Genesis 19:21-22

Malaika aliwaruhusu Lutu na familia yake kutorokea wapi?

Lutu na familia yake waliruhusiwa kutorokea katika mji mdogo unaoitwa Soari.

Genesis 19:23-25

Yahwe alifanya nini Lutu alipofika Soari?

Yahwe alinyeshea chini salfa na moto kutoka mbinguni juu ya Sodoma na Gomora.

Genesis 19:26-29

Mke wa Lutu alifanya nini na nini kilitokea kwake?

Mke wa Lutu alitazama nyuma, naye akawa nguzo ya chumvi.

Abrahamu aliona nini mapema ya asubuhi alipotazama katika nchi yote ya bondeni?

Abrahamu aliona moshi ukipanda kutoka katika nchi kama moshi wa tanuru.

Genesis 19:30

Lutu alihamia wapi na kwa nini?

Kisha Lutu akahamia katika milima kwa sababu alikuwa na hofu ya kuishi Soari.

Genesis 19:31-35

Mabinti wa Lutu walikuwa na mpango gani iliyomhusisha baba yao.

Mabinti za Lutu walipanga kumlewesha baba yao, kisha kulala naye ili kwamba waweze kupata watoto.

Genesis 19:36-38

Makundi gani mawili yalitokana na binti wa Lutu?

Kundi la watu wa Wamoabi na Waamoni walitokana na mabinti wa Lutu.

Genesis 20

Genesis 20:1-3

Abrahamu alisema nini kuhusu Sara walipokuwa wakiishi Gerari?

Abrahamu alisema ya kwamba Sara alikuwa dada yake.

Mungu alisema nini kwa Abimeleki baada ya kumchukua Sara?

Mungu alikuja kwa Abimeleki katika ndoto na kumwambia ya kwamba alikuwa mtu mfu kwa sababu alichukua mke wa mtu.

Genesis 20:4-5

Abimeleki alisema nini kwa Mungu ya kuwa aliambiwa na Abrahamu na Sara?

Abimeleki alisema kwa Mungu ya kwamba Abrahamu alimwambia Sara alikuwa dad yake, na Sara alimwambia Abrahamu alikuwa kaka yake.

Genesis 20:6-7

Mungu alimwambia Abimeleki afanye nini, na Mungu alisema nini kingetokea iwapo hatafanya hivyo?

Mungu alimwambia Abimeleki kumrudisha Sara kwa Abrahamu; la sivyo, yeye na watu wake wote wangekufa.

Genesis 20:8-9

Watu wa Abimeleki waliitikiaje waliposikia kile ambacho Mungu alimwambia Abimeleki?

Watu wa Abimeleki waliogopa sana waliposikia kile ambacho Mungu alimwambia.

Genesis 20:10-14

Kwa nini Abrahamu alisema ya kuwa alimwambia Abimeleki ya kwamba Sara alikuwa ni dada yake?

Abrahamu alisema ya kwamba aliogopa Abimeleki angemuua kwa sababu ya Sara.

Kwa njia gani haswa Sara alikuwa dada yake Abrahamu?

Sara alikuwa binti wa baba wa Abrahamu lakini sio wa mama yake.

Genesis 20:15-16

Abimeleki alimpatia Abrahamu wanyama na watu gani?

Abimeleki alimpatia Abrahamu kondoo, maksai, watumwa wa kiume na kike.

Ni sababu ipi ambayo Abimeleki alimpatia Sara ni kwa nini alimpa kaka yake vipande elfu vya fedha?

Abimeleki alimwambia Sara ya kuwa amempatia vipande vya fedha kwa kaka yake kufunika kosa lolote dhidi ya Sara machoni pa wote waliokuwa na Sara, na mbele ya kila mtu.

Genesis 20:17-18

Abrahamu alipoomba kwa Mungu kwa ajili ya Abimeleki na watu wake nini kilitokea?

Mungu alimponya Abimeleki, mke wake, na watumwa wake wa kike ili waweze kupata watoto.

Genesis 21

Genesis 21:1-4

Yahwe alifanya nini kwa ajili ya Sara?

Yahwe alimtembelea Sara naye akazaa mtoto kwa Abrahamu katika muda alioahidi.

Isaka alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu alifanya nini?

Isaka alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu alimtahiri.

Genesis 21:5-7

Sara alisema Mungu amemfanya atende nini?

Sara alisema ya kwamba Mungu alimfanya acheke.

Genesis 21:8-9

Katika siku Isaka alipoachishwa kunyonya, Sara aliona nini?

Sara alimuona mtoto wa Hajiri akimdhihaki.

Genesis 21:10-11

Sara alimwambia Abrahamu afanye nini na Hajiri na mwanawe, na kwa nini?

Sara alimwambia Abrahamu kuwafukuza hajiri na mwanawe, kwa sababu mtoto wa hajiri asingeweza kuwa mrithi pamoja na Isaka.

Mwitikio wa Abrahamu kwa dai la Sara ulikuaje?

Abrahamu alihuzunishwa kwa dai la Sara.

Genesis 21:12-13

Mungu alimwambia Abrahamu afanye nini?

Mungu alimwambia Abrahamu kumsikiliza Sara.

Genesis 21:14-16

Hajiri na mwanawe walikwenda wapi baada ya Abrahamu kuwafukuza?

Hajiri na mwanawe walikwenda katika jangwa.

Genesis 21:17-18

Mungu alimwambi Hajiri angemfanyia nini mtoto wake?

Mungu alisema angemfanya mwanawe Hajiri kuwa taifa kubwa.

Genesis 21:19-21

Hajiri na mwanawe waliponaje?

Mungu alifungua macho ya Hajiri naye akaona kisima cha maji.

Nini kilitokea kwa mtoto wa Hajiri alipokuwa akikua?

Mtoto wa Hajiri akawa mwindaji na mama yake akampatia mke kwa ajili yake kutoka Misri.

Genesis 21:22-24

Abimeleki alimtaka Abrahamu kuapa kufanya nini kwake?

Abimeleki alimtaka Abrahamu kuapa ya kwamba hatamfanyia baya Abimeleki, au watoto wake, au uzao wake. Abimeleki alimuomba Abrahamu kuonyesha kwake agano lile lile la uaminifu ambalo Abimeleki alikwisha muonesha Abrahamu.

Genesis 21:25-27

Abrahamu alilalamika juu ya nini kwa Abimeleki?

Abrahamu alilalamika kwa Abimeleki juu ya kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikichukua kutoka kwake.

Genesis 21:28-30

Kwa nini Abrahamu alituma kondoo wa kike saba kwa Abimeleki?

Abrahamu alituma kondoo saba wa kike kwa Abimeleki kama ushahidi ya kwamba alichimba kisima chenye malumbano.

Genesis 21:31-32

Abimeleki alirudi katika nchi gani?

Abimeleki alirudi katika nchi ya Wafilisti.

Genesis 21:33-34

Abrahamu alifanya nini katika mti wa mkwaju katika Beerisheba?

Abrahamu alimwabudu tahwe, Mungu wa milele.

Abrahamu aliishi wapi kwa siku nyingi?

Abrahamu aliishi katika nchi ya Wafilisti kwa siku nyingi.

Genesis 22

Genesis 22:1-3

Ni mtihani upi Mungu alimpatia Abrahamu?

Mungu alimwambia Abrahamu kwenda katika nchi ya Moria na kumtoa Isaka kama sadaka ya kuteketezwa.

Abrahamu aliitikiaje kwa amri ya Mungu

Abrahamu aliamka asubuhi na mapema na kuanza safari yake katika mahali Mungu alipomwambia.

Genesis 22:4-6

Abrahamu aliwaambia nini vijana wake wawili ya kuwa yeye na Isaka walikwenda kufanya nini?

Abrahamu aliwaambia vijana wake wawili ya kwamba yeye na Isaka walikwenda kuabudu na kisha wangerudi.

Genesis 22:7-8

Isaka alimuuliza swali gani Abrahamu walipokuwa wakitembea pamoja?

Isaka alimuuliza Abrahamu, "Yuko wapi mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?"

Abrahamu alijibuje swali la Isaka?

Abrahamu alisema ya kwamba Mungu mwenyewe angetoa mwanakondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketeza.

Genesis 22:9-10

Walipofika mahali pale, Abrahamu aliaanda nii kama sadaka ya kuteketezwa na alifanyaje?

Abrahamu alimuandaa Isaka kama sadaka wa kuteketezwa kwa kumfunga na kumlaza juu ya madhabahu.

Genesis 22:11-12

Abrahamu alipochukua kisu mkononi mwake, malaika wa Yahwe alimwambia nini Abrahamu?

Malaika wa Yahwe alimwambia Abrahamu kutomdhuru Isaka.

Malaika alisema alijua nini kuhusu Abrahamu?

Malaika alisema ya kwamba alijua ya kuwa Abrahamu alimcha Mungu.

Genesis 22:13-14

Mungu alitoaje sadaka wa kuteketezwa kwa ajili ya Abrahamu?

Kulikuwa na kondoo dume amenaswa katika vichaka nyuma ya Abrahamu, ambaye Abrahamu alimtumia kama sadaka wa kuteketezwa.

Abrahamu alipaitaje mahali pale pa sadaka ya kuteketezwa?

Abrahamu alipaita mahali pale, "Yahwe atatoa"

Genesis 22:15-17

Malaika alitoa sababu gani ya kumbariki Abrahamu?

Malaika wa Yahwe alimwambia angembariki Abrahamu kwa sababu Abrahamu hakujizuia mwanawe wa pekee.

Genesis 22:18-24

Ni kupitia kwa nani na kwa nini mataifa yote ya dunia yatabarikiwa?

Kupitia uzao wa Abrahamu mataifa yote ya dunia yatabarikiwa, kwa sababu Abrahamu alimtii malaika wa sauti ya Yahwe.

Genesis 23

Genesis 23:1-2

Abrahamu alifanya nini kwanza Sara alipokufa?

Sara alipokufa, Abrahamu aliomboleza kwanza kwa ajili yake na akamlilia.

Genesis 23:3-4

Abrahamu alitoa ombi gani kwa wana wa Hethi?

Abrahamu aliomba mali ya kutumia kama sehemu ya kuzikia.

Genesis 23:5-9

Wana wa Hethi walijibuje ombi la Abrahamu?

Wana wa Hethi walimpatia Abrahamu makaburi bora ya kwao.

Genesis 23:10-11

Abrahamu alipoomba pango la Efroni Mhiti, Efroni aliitikiaje?

Efroni alijitolea kumpatia Abrahamu pango na shamba kando yake.

Genesis 23:12-13

Abrahamu aliitikiaje kuhusu ahadi ya Efroni?

Abrahamu alijitolea kulipia shamba pamoja na pango.

Genesis 23:14-16

Abrahamu aliitikiaje kuhusu ahadi ya Efroni?

Efroni aliomba shekeli mia nne za fedha kwa ajili ya shamba na pango.

Mazungumzo kati ya Abrahamu na Efroni yalimalizikaje?

Abrahamu alilipa shekeli mia nne za fedha kwa Efroni kwa ajili ya sehemu ile ya shamba.

Genesis 23:17-18

Nini kilikuwa ndani ya manunuzi wa shamba la Efroni ambalo lilikuwa Makpela?

Shamba, pango lililokuwa ndani mwake, na miti yote iliyokuwa katika shamba na mpakani ilijumuishwa katika manunuzi ya Abrahamu wa shamba la Efroni.

Genesis 23:19-20

Abrahamu baadae alifanya nini na pango?

Abrahamu baadae alimzika Sara katika pango.

Genesis 24

Genesis 24:1-4

Abrahamu alimfanya mtumishi wake mkubwa kuapa jambo gani?

Abrahamu alimfanya mtumishi wake mkubwa kuapa ya kwamba angemtafutia mke kwa ajili ya Isaka kutoka kwa jamaa za Abrahamu.

Genesis 24:5-11

Abrahamu alisistiza ya kwamba mtumishi asifanye nini na Isaka?

Abrahamu alisisitiza ya kwamba mtumishi asimpeleke Isaka katika nchi ambayo Abrahamu alitoka.

Genesis 24:12-14

Mtumishi wa Abrahamu alimuomba Mungu afanye nini ili kumuonyesha ni mwanamke yupi Mungu amemchagua kwa ajili ya Isaka?

Mtumishi alimuuliza ya kwamba mwanamke ambaye atamuuliza kutua mtungi wake kupata maji na kufanya vile na kutoa maji kwa ngamia wake pia.

Genesis 24:15-16

Rebeka alikuwa na uhusiano gani kwa Abrahamu?

Rebeka alikuwa mjukuu wa Nahori, kaka yake Abrahamu.

Genesis 24:17-18

Rebeka alifanya nini pale mtumishi wa Abrahamu alipomuomba maji ya kunywa?

Rebeka alimpatia mtumishi maji.

Genesis 24:19-25

Rebeka alisema nini baada ya kumpatia mtumishi maji?

Baada ya Rebeka kumaliza kumpatia mtumishi maji alisema, "Nitachota maji kwa ajili ya ngamia wako pia, mpaka watakapomaliza kunywa".

Genesis 24:26-30

Mtumishi alifanya nini aliposikia ya kwamba Rebeka alikuwa na uhusiano kwa Abrahamu na kwamba angeweza kukaa usiku huo na familia yake?

Mtumishi alimuabudu Yahwe na kumbariki.

Genesis 24:31-32

Labani alifanya nini alipokutana na mtumishi wa Abrahamu?

Labani alimkaribisha mtumishi wa Abrahamu kukaa katika nyumba yake.

Genesis 24:33-38

Mtumishi wa Abrahamu alisisitiza kufanya nini kabla ya kula?

Mtumishi wa Abrahamu alisisitiza kusema kwa nini alikuja kabla hajala.

Genesis 24:39-46

Abrahamu alisemaje ya kwamba Yahwe angebariki njia ya mtumishi?

Abrahamu alisema ya kwamba Yahwe angetuma malaika wake pamoja na mtumishi kufanikisha njia yake.

Genesis 24:47-49

Mtumishi alimpatia nini Rebeka aliposikia alikuwa na uhusiano kwa Abrahamu.

Mtumishi wa Abrahamu alimpatia Rebeka pete ya dhahabu kwa ajili ya pua yake na bangili kwa ajili ya mikono yake.

Genesis 24:50-51

Labani na Bethueli walimjibuje mtumishi wa Abrahamu alipowauliza walitaka kufanya nini kuhusu Rebeka?

Labani na Bethueli walimjibu ya kwamba mtumishi amchukue Rebeka na kuondoka naye, ili kwamba Rebeka aweze kuwa mke wa mwana wa Abrahamu.

Genesis 24:52-53

Mtumishi wa Abrahamu alifanya nini aliposikia jibu kutoka kwa Labani na Bethueli?

Mtumishi aliinama chini kwa Yahwe na kutoa zawadi kwa Rebeka na kwa kaka na mama yake.

Genesis 24:54-55

Walipoamka asubuhi iliyofuata, kaka wa Rebeka na mama walimtaka mtumishi kufanya nini?

Walipoamka asunuhi iliyofuata, walimtaka mtumishi wa Abrahamu kubaki nao kwa angalau siku kumi zaidi.

Genesis 24:56-58

Mtumishi wa Abrahamu aliposema alitaka kwenda mara moja, Rebeka alisema alitaka kufanya nini?

Rebeka alisema ya kwamba anataka kuondoka pamoja na mtumishi.

Genesis 24:59-62

Familia ya Rebeka ilitoa baraka gani kwake alipoondoka na mtumishi wa Abrahamu?

Familia ya Rebeka ilimbariki ya kwamba aweze kuwa mama wa maelfu na makumi elfu na kwamba uzao wake waweze kumiliki lango la wale wanao wachukia.

Genesis 24:63-65

Isaka alikuwa akifanya nini Rebeka alipofika katika nyumba yake?

Isaka alikuwa nje shambani akitafakari.

Rebeka alifanya nini alipomwona Isaka?

Alipomwona Isaka, Rebeka aliruka chini kutoka kwenye ngamia na kujifunika kwa shela.

Genesis 24:66-67

Isaka alifanya nini baada ya mtumishi wa Abrahamu kurejea mambo yote aliyoyafanya?

Isaka alimchukua Rebeka katika hema la mama yake Sara na kumfanya kuwa mke wake.

Genesis 25

Genesis 25:1-4

Abrahamu alifanya nini baada ya mke wake Sara kufariki?

Abrahamu alichukua mke mwingine aliyeitwa Ketura.

Genesis 25:5-6

Abrahamu aligawanishaje utajiri wake?

Abrahamu alitoa zawadi kwa wana wa masuria wake, na kutoa kila alichokuwa nacho kwa mwanawe Isaka.

Genesis 25:7-8

Abrahamu aliishi miaka mingapi?

Abrahamu aliishi miaka mia moja na sabini na tano?

Genesis 25:9-16

Nani alimzika Abrahamu?

Wote Isaka na Ishmaeli walimzika Abrahamu.

Genesis 25:17-20

Wana kumi na mbili wa Ishmaeli waliishije kati yao?

Wana kumi na wawili wa Ishmaeli waliishi kwa uadui kati yao.

Genesis 25:21-22

Isaka alifanya nini kwa sababu Rebeka kuwa tasa?

Isaka aliomba kwa Yahwe kwa ajili ya mke wake, na Yahwe alijibu maombi yake, na Rebeka akabeba mimba.

Genesis 25:23

Yahwe alisema nini kuhusu wale watoto wawili waliopambana tumboni mwa Rebeka?

Yahwe alisema ya kwamba kutakuwa na mataifa mawili tumboni mwake, mtu mmoja mwenye nguvu zaidi ya mwenzake, na mkubwa atamtumikia mdogo.

Genesis 25:24-26

Nani alizaliwa kwanza, na alionekanaje?

Esau alizaliwa kwanza, naye alikuwa mwekundu kote kama vazi la nywele.

Nani alizaliwa wa pili, na alikuwa akifanya nini alipozaliwa?

Yakobo alizaliwa wa pili, naye alikuwa akikamata kisigino cha Esau alipozaliwa.

Genesis 25:27-28

Esau alikuwa mtu wa namna gani?

Esau alikuwa mwindaji hodari na mtu wa nyikani.

Yakobo alikuwa mtu wa namna gani?

Yakobo alikuwa mtu mkimya aliyetumia muda wake katika mahema.

Isaka alipenda nini, na Rebeka alimpenda nani?

Isaka alimpenda Esau, na Rebeka alimpenda Yakobo.

Genesis 25:29-30

Jina lingine la Esau lilikuwa ni lipi?

Edomu lilikuwa ni jina lingine la Esau.

Genesis 25:31-34

Yakobo aliomba nini kwa ajili ya mchuzi wa dengu ambao Esau alitaka kula kwa sababu alikuwa na njaa kali?

Yakobo alimuomba Esau haki yake ya kuzaliwa kwa ajili ya mchuzi wa dengu.

Jibu la Esau lilikuwa ni lipi kwa ahadi ya Yakobo?

Esau aliapa kiapo na kuuza haki yake ya kuzaliwa kwa Yakobo.

Esau alikuwa akitendeaje haki yake ya kuzaliwa alipokuwa akitoa jibu kwa njia kwa ahadi ya Yakobo?

Esau alikuwa akidharau haki yake ya kuzaliwa alipokuwa akijibu ahadi ya Yakobo kwa namna hii.

Genesis 26

Genesis 26:1

Kwa nini Isaka alikwenda katika mji wa Gerari ambako Abimeleki alikuwa mfalme wa Wafilisti?

Isaka alikwenda Gerari kwa sababu kulikuwa na njaa katika nchi.

Genesis 26:2-3

Yahwe alikuwa amemwambia nini Isaka kabla ya Isaka kwenda Gerari?

Yahwe alimwambia Isaka kutokwenda Misri na kukaa katika nchi ambayo alikwenda kumwambia Isaka.

Yahwe alimwambia nini Isaka kuhusu kiapo alichoapa Yahwe kwa baba yake Abrahamu?

Yahwe alimwambia Isaka ya kwamba atatimiza kiapo ambacho Yahwe aliapa kwa Abrahamu.

Genesis 26:4-5

Yahwe alisema alikwenda kufanya nini?

Yahwe alisema alikwenda kufanya hivyo kwa sababu Abrahamu alitii sauti yake na kushika maelekezo, amri, maagizo na sheria zake.

Genesis 26:6-8

Isaka alisema nini kwa wanamume wa Gerari kuhusu Rebeka, mke wake?

Isaka aliwaambiwa wanamume wa Gerari ya kwamba Rebeka alikuwa dada yake.

Genesis 26:9-14

Kulingana na Abimeleki, ni jambo gani lingeleta hatia juu ya watu kwa sababu ya uongo wa Isaka?

Kwa sababu ya uongo wa Isaka, mtu angeweza kulala na Rebeka na kuleta hatia juu ya watu.

Abimeleki alitoa amri gani kuhusu Rebeka?

Abimeleki aliamuru ya kwamba yeyote atakayemgusa Rebeka atauawa.

Genesis 26:15-17

Abimeleki alitoa sababu gani kwa kumuuliza Isaka kuondoka kwa Wafilisti?

Abimeleki alimwambia Isaka kuondoka kwa Wafilisti kwa sababu alisema, "... kwa kuwa wewe una nguvu kuliko sisi"

Genesis 26:18-20

Kwa nini Isaka ilimbidi kuchimbua visima vya maji ambavyo vilichimbwa katika siku za Abrahamu?

Ilimpasa Isaka kuchimbua visima vya maji ambavyo vilichimbwa katika siku za Abrahamu kwa sababu Wafilisti walivizuia baada ya kifo cha Abrahamu.

Genesis 26:21-22

Isaka alitajaje kisima ambacho wachungaji wa Gerari hawakukigombania na yeye?

Isaka alikiita kisima, ambacho wachungaji wa Gerari hawakukigombania naye, Rehobothi.

Genesis 26:23-27

Yahwe alimhakikishia nini Isaka alipomtokea Beersheba?

Yahwe alimhakikishia ya kwamba angembariki Isaka na kuvizidisha vizazi vyake.

Genesis 26:28-29

Abimeleki alitaka kufanya agano gani na Isaka, na kwa nini?

Abimeleki alitaka kufanya agano ambalo pande zote hazitamdhuru mwenzake, kwa sababu aliona ya kuwa Yahwe alikuwa pamoja na Isaka.

Genesis 26:30-33

Isaka alipokeaje ombi la Abimeleki kwa agano kati yao?

Isaka alifanya sherehe, na wakaapa kiapo kati yao.

Genesis 26:34-35

Wake wa Esau walitokana na makundi yapi mawili?

Wake wawili wa Esau walitoka kwa Wahiti.

Uhusiano kati ya wake wa Esau na Isaka na Rebeka ulikuaje?

Wake wa Esau walileta huzuni kwa Isaka na Rebeka.

Genesis 27

Genesis 27:1-2

Isaka alishindwa kufanya nini tena alipozeeka?

Isaka alipozeeka, hakuweza kuona tena.

Genesis 27:3-7

Isaka alimwomba Esau kufanya nini na kwa nini?

Isaka alimuomba Esau kwenda kuwinda na kumtengenezea aina ya chakula ambayo anaipenda, ili kwamba aweze kula na kumbariki Esau.

Genesis 27:8-10

Mpango wa Rebeka wa kuandaa chakula kwa ajili ya Isaka ulikuwa upi, na kwa nini?

Rebeka alimwambia Yakobo kuchukua mbuzi wawili na angetengeneza chakula ambacho Isaka alikipenda, ili kwamba Yakobo ampelekee Isaka na kupokea ile baraka.

Genesis 27:11-14

Yakobo alijishughulisha na nini katika kuleta chakula kwa Isaka?

Yakobo alijishughulisha ya kwamba Esau alikuwa mtu mwenye nywele na yeye alikuwa mtu laini, na kwamba Isaka angemgusa na kugundua ya kuwa Yakobo alikuwa mdanganyifu na angemlaani.

Genesis 27:15-19

Rebeka alitatuaje tatizo la Esau kuwa mtu wa nywele nyingi, na Yakobo kuwa mtu laini?

Rebeka alimpatia Yakobo nguo za Esau na kumvisha ngozi ya mbuzi juu ya mikono na shingo yake.

Genesis 27:20-21

Isaka alipouliza, Yakobo alisemaje ya kwamba amepata windo kwa haraka hivyo?

Yakobo alisema ya kwamba Yahwe, Mungu wa Isaka, alileta windo kwake.

Genesis 27:22-23

Kwa sababu hakuwa na uhakika, Isaka alijaribuje kuthibitisha ni nani aliyekuwa akimpatia chakula?

Isaka alimgusa Yakobo mkononi na kuhisi manyoya ya ngozi ya mbuzi.

Genesis 27:24-25

Yakobo alisema nini Isaka aliposema, "Wewe kweli ni mwanangu Esau?"

Yakobo alisema, "Ni mimi"

Genesis 27:26-28

Jambo gani mwishowe lilimshawishi Isaka ya kwamba mtu anayeleta chakula alikuwa Esau?

Yakobo alipomkaribia Isaka kumbusu, Isaka alinusa nguo za Esau.

Genesis 27:29

Isaka alisema ni nani angeinama chini kwa Yakobo?

Isaka alisema mataifa yangeinama chini kwa Yakobo na kwamba mwana wa mama wa Yakobo atainama chini kwake.

Genesis 27:30-33

Esau alifanya nini baada ya Yakobo kuondoka katika hema la Isaka?

Esau alirudi kutoka mawindoni, akaandaa chakula, na kukileta kwa Isaka.

Genesis 27:34-35

Isaka alisema nini Esau alipomuomba Isaka baraka yake?

Isaka alisema ya kwamba Yakobo amechukua baraka ya Esau kwa udanganyifu.

Genesis 27:36-38

Ni kwa njia gani mbili Esau alisema Yakobo amemdanganya?

Esau alisema ya kwamba Yakobo alimdanganya kwa haki yake ya kuzaliwa na baraka yake.

Genesis 27:39-40

Ni "baraka" gani ambayo Isaka alimpatia Esau?

Isaka alisema ya kwamba Esau ataishi mbali na utajiri wa nchi, ya kuwa atamtumikia ndugu yake, lakini hatimaye atapambana naye na kuondoa nira ya Yakobo juu yake.

Genesis 27:41-42

Esau aliamua kufanya nini baada ya kifo cha Isaka?

Esau aliamua kumuua Yakobo baada ya kifo cha Isaka.

Genesis 27:43-46

Rebeka alifanya nini baada ya kusikia mipango ya Esau?

Rebeka alimtuma Yakobo kwa Labani, kaka yake, Harani.

Genesis 28

Genesis 28:1-2

Isaka alitoa amri gani kwa Yakobo kabla hajaondoka?

Isaka alimuamuru Yakobo kutochukua mke wa Kaanani.

Isaka alimwambia Yakobo kuchukua mke mahali gani?

Isaka alimwambia kuchukua mke kutoka kwa mabinti wa Labani, kaka wa Rebeka.

Genesis 28:3-7

Ni baraka ya nani ambayo Isaka alimuomba Mungu ampatie Yakobo?

Isaka alimwomba Mungu ampatie Yakobo baraka ya Abrahamu.

Genesis 28:8-11

Esau alipata mmoja wa wake zake kutoka wapi alipogundua ya kwamba wanawake wa Kaanani hawakumpendeza Isaka?

Esau alichukua mke kutoka kwa binti wa Ishmaeli, mwana wa Abrahamu.

Genesis 28:12-15

Yakobo aliona nini katika ndoto alipokuwa njiana kwenda Harani?

Yakobo aliona ngazi kutoka kwenye nchi kwenda mbinguni na malaika wakipanda na kushuka juu yake, na Yahwe akisimama juu yake.

Yahwe alisema nini kuhusu nchi ambayo Yakobo aliyokuwa amelala juu yake?

Yahwe alisema ya kwamba nchi ambayo Yakobo amelala juu yake itapewa kwake na kwa uzao wake.

Ni baraka ya nani Yahwe alimpatia Yakobo?

Yahwe alimpatia Yakobo baraka ya Abrahamu.

Genesis 28:16-17

Yakobo alisema nini kuhusu mahali ambapo alipata ndoto ile?

Yakobo alisema mahali pale palikuwa nyumba ya Mungu na lango la mbinguni.

Genesis 28:18-19

Ni jina gani alilolipa Yakobo mahali pale ambapo alipata ile ndoto?

Yakobo alipaita mahali pale Betheli.

Genesis 28:20-22

Yakobo alisema Yahwe anapaswa kufanya nini ili kwamba Yahwe aweze kuwa Mungu wake?

Yakobo alisema ya kwamba Yahwe anapaswa kuwa pamoja naye na kumlinda katika safari yake ili kwamba arudi salama kwa nyumba ya baba yake.

Yakobo aliahidi kumpataia nini Yahwe iwapo Yahwe angefanya mambo haya kwake?

Yakobo aliahidi kumrudishia Yahwe moja ya kumi ya kila kitu Yahwe alichompatia Yakobo.

Genesis 29

Genesis 29:4-8

Wanamume ambao Yakobo alizungumza nao walitoka wapi?

Wanamume walitoka Harani.

Ni nani pia aliyekuja na kundi la kondoo kisimani?

Raheli, binti wa Labani, pia alikuja kisimani pamoja na kundi la kondoo.

Genesis 29:9-10

Yakobo alifanya nini na kondoo wa Labani?

Yakobo aliviringisha jiwe kutoka mdomoni mwa kisima na kuwanywesha kondoo.

Genesis 29:11-12

Yakobo alimwambia nini Raheli, na kisha Raheli alifanya nini?

Yakobo alimwambia Raheli ya kwamba alikuwa ndugu wa baba yake, na kisha Raheli alikimbia na kumwambia baba yake.

Genesis 29:13-14

Labani aliitikiaje aliposikia kuhusu ujio wa Yakobo?

Labani alikimbia kukutana na Yakobo, akamkumbatia, akambusu, na kumleta katika nyumba yake.

Genesis 29:15-18

Waelezee mabinti wawili wa Labani.

Lea alikuwa binti mkubwa naye alikuwa na macho dhaifu, wakati Raheli alikuwa mdogo naye alikuwa mzuri wa umbo na muonekano.

Labani na Yakobo walifanya utaratibu gani kuhusu kazi ya Yakobo?

Walikubaliana ya kwamba Yakobo atamtumikia Labani kwa miaka saba kwa ajili ya Raheli.

Genesis 29:19-22

Kwa nini miaka saba ya kazi ilionekana kama sikuchache tu kwa Yakobo?

Miaka saba ya kazi ilionekana kama siku chache tu kwa sababu ya upendo Yakobo aliokuwa nao kwa Raheli.

Genesis 29:23-25

Labani alimdanganyaje Yakobo?

Labani alimpatia Lea kwa Yakobo, badala ya Raheli, usiku kabla ya harusi.

Labani alimpatia nani kwa Lea, awe mtumishi wake?

Labani alimpatia mtumishi wake wa kike Zilpa kwa binti yake Lea, awe mtumishi wake.

Genesis 29:26-27

Kwa nini Labani alisema amemdanganya Yakobo?

Labani alisema ya kuwa haikuwa utamaduni wao kumtoa binti mdogo katika ndoa kabla ya mzaliwa wa kwanza.

Labani na Yakobo walifanya utaratibu gani kuhusu kazi ya Yakobo?

Walikubaliana ya kwamba Yakobo atamtumikia Labani kwa miaka saba zaidi kwa ajili ya Raheli.

Genesis 29:28-30

Labani alimpatia nani Raheli, awe mtumishi wake?

Labani alimpatia Bilha kwa binti yake Raheli, awe mtumishi wake.

Genesis 29:31-34

Yahwe alifanya nini alipogundua ya kwamba Yakobo hakumpenda Lea?

Yahwe alimsababisha Lea kupata mimba, lakini Raheli akawa tasa.

Lea alikuwa akitumaini nini iwapo atamzalia wana Yakobo?

Lea alitumaini ya kwamba Yakobo angempenda iwapo atamzalia wana kwa ajili yake?

Jina la mwana wa kwanza wa Lea ni nani?

Jina la mtoto wa kwanza wa Lea alikuwa Rubeni.

Genesis 29:35

Lea alisema nini baada ya kumzaa Yuda?

Baada ya kumzaa Yuda Lea alisema, "Wakati huu nitamsifu Yahwe"

Genesis 30

Genesis 30:1-2

Kulingana na Yakobo, kwa nini Raheli hakuwa na watoto?

Kulingana na Yakobo, Mungu alimzuia Raheli kupata watoto.

Genesis 30:3-6

Raheli alifanya nini ili apate watoto?

Raheli alimpatia Bilha kwa Yakobo mtumishi wake ili aweze kupata watoto kwa niaba ya Raheli.

Genesis 30:7-8

Kwa nini Raheli alisema alishinda dhidi ya dada yake Lea?

Raheli alisema ya kwamba alishinda kwa sababu Bilha mtumishi wake alimzalia watoto wawili kwa Yakobo.

Genesis 30:9-13

Lea alifanya nini alipoona ya kwamba ameshindwa kupata watoto?

Lea alimpatia Yakobo mtumishi wake Zilpa ili aweze kupata watoto kwa niaba ya Lea.

Nini kilisababisha Lea kusema, "Hii ni bahati njema!"

Lea alisema, "Hii ni bahati njema" kwa sababu Zilpa mtumishi wake alimzalia Yakobo mtoto wa kiume.

Genesis 30:14-18

Raheli alitoa nini kwa Lea ili kubalishana kwa tunguja za mwanawe?

Kwa kubadilishana na tunguja za Rubeni, Raheli alitoa kumruhusu Lea alale na Yakobo usiku huo.

Genesis 30:19-21

Lea alimzalia Yakobo wana wa kiume wangapi?

Lea alizaa wana wa kiume sita kwa Yakobo.

Genesis 30:22-24

Nini kilisababisha Raheli kusema ya kwamba aibu yake imetoweka?

Raheli alipomzaa mwana kwa Yakobo, alisema ya kwamba aibu yake imeondoka.

Genesis 30:25-26

Yakobo alitoa ombi gani kwa Labani baada ya Yusufu kuzaliwa?

Yakobo aliomba ya kwamba Labani amruhusu Yakobo aondoke na familia yake na kurudi kwa nyumba na nchi yake.

Genesis 30:27-30

Kwa nini Labani hakutaka Yakobo aondoke?

Labani aligundua ya kwamba Mungu alimbariki yeye kwa niaba ya Yakobo.

Genesis 30:31-34

Yakobo alipokea ujira upi kwa kazi kwa ajili ya Labani?

Yakobo alichukua kondoo wenye milia, mabaka na weusi na mbuzi wenye milia na mabaka kutoka kwa kundi la Labani aliowachunga.

Genesis 30:35-36

Labani alimdanganyaje Yakobo kuhusu ujira wa Yakobo?

Labani aliwatoa kwanza wanayma ambao Yakobo angewachukua, kabla hajawapa kwa Yakobo kuwachunga.

Genesis 30:37-38

Yakobo alitoa maganda ya matawi gani yenye mchirizi myeupe?

Yakobo alitoa maganda yenye michirizi myeupe katika matawi ya mipopla, mlozi na mwaroni mbichi.

Yakobo alifanya nini na fito alizokuwa amezibambua?

Yakobo akaziweka fito alizokuwa amezibambua mbele ya makundi ya kondoo, mbele ya mabirika yakunyweshea walipokuja kunywa maji.

Genesis 30:39-40

Nini kilitokea wanyama walipopanda mbele ya fito?

Wanyama wakapandana mbele ya fito; nao wakazaa watoto wenye milia, mabaka na wenye madoa

Genesis 30:41-43

Nini ilikuwa matokeo ya upandaji wa Yakobo wa wanyama?

Matokeo yake yakawa kwamba wanyama wa Labani wakawa dhaifu, na wanyama wa Yakobo wakawa wenye nguvu.

Genesis 31

Genesis 31:1-6

Labani na wanawe waliamini Yakobo alipata wapi utajiri wake wote?

Labani na wanawe waliamini ya kwamba Yakobo alipata utajiri wake kutoka kwa mali za Labani.

Yahwe alitoa maelekezo yapi kwa Yakobo?

Yahwe alimuelekeza Yakobo kurudi katika nchi ya baba zake na ndugu zake.

Genesis 31:7-13

Mungu alichukuaje mifugo wa Labani na kumpatia Yakobo?

Mungu alisababisha wanyama kuwa na mabaka, na watoto wao kuwa na milia ambayo ilikuwa ujira wa Yakobo.

Genesis 31:14-18

Raheli na Lea walikuwa na mtazamo gani dhidi ya baba yao Labani?

Raheli na Lea walisema ya kwamba Labani aliwatendea kama wageni na alitapanya pesa yao.

Genesis 31:19-21

Raheli alifanya nini kabla ya kuondoka na Yakobo?

Raheli aliiba miungu nyumbani mwa baba yake.

Yakobo alimdanganyaje Labani katika kipindi hiki?

Yakobo alimdanganya Labani kwa kutomuambia ya kuwa alikuwa akiondoka.

Genesis 31:22-23

Labani alifanya nini alipoambiwa ya kuwa Yakobo ametoroka?

Labani alichukua ndugu zake pamoja naye na kumfuata Yakobo, na kumpita baada ya siku saba.

Genesis 31:24-30

Mungu alimwambia nini Labani katika ndoto?

Mungu alimwambia Labani kutozungumza jambo jema au baya kwa Yakobo.

Genesis 31:31-33

Yakobo alisema ni kwa nini alimtokoka Labani kwa siri?

Yakobo alisema ametoroka kwa siri kwa sababu aliogopa ya kwamba Labani angewachukua binti zake kutoka kwake kwa nguvu.

Yakobo alisema nini pale Labani alipomtuhumu kuiba miungu ya nyumba yake?

Yakobo alisema ya kwamba yeyote aliyeiba miungu ya nyumba ya Labani hataendelea kuishi.

Genesis 31:34-40

Kwa nini Labani hakuipata miungu ya nyumba yake miongoni mwa mali za Yakobo?

Labani hakuipata miungu ya nyumba yake kwa sababu Raheli alikuwa amekalia na kisha akasema ya kwamba hakuweza kusimama kwa kuwa alikuwa katika kipindi cha hedhi.

Genesis 31:41-42

Yakobo alifanya kazi miaka mingapi kwa Labani, na mara ngapi Labani alibadili ujira wake?

Yakobo alifanya kazi kwa Labani miaka ishirini, na Labani alibadili ujira wake mara kumi.

Genesis 31:43-44

Labani alionyeshaje ya kuwa alidhania utajiri wa Yakobo bado ni wa kwake?

Labani alisema ya kwamba kila alikiona ni mali ya Yakobo kilikuwa chake.

Genesis 31:45-47

Yakobo na Labani waliweka alama gani katika nafasi ya agano lao?

Yakobo na Labani waliweka alama mahali pale pa agano kwa kupanga rundo la mawe.

Genesis 31:48-50

Ni nani alitajwa kuwa shahidi kati ya Yakobo na Labani kuhakikisha agano litatunzwa?

Mungu alitajwa kuwa shahidi kati ya Yakobo na Labani kuhakikisha agano litatunzwa.

Genesis 31:51-53

Rundo na nguzo zilikuwa kwa ajili ya nini?

Rundo na nguzo zote zilikuwa mashahidi kwa ajili ya agano ambalo lilisema ya kuwa Labani wala Yakobo hawatapita rundo au nguzo ile kwa kumdhuru mwenzake.

Ni agano gani Yakobo na Labani walifanya?

Yakobo na Labani kila mmoja alikubaliana kutopita ng'ambo ya pili ya rundo na mawe kumdhuru mwenzake.

Yakobo alifanya nini kuonyesha alikubaliana na agano jilo?

Kuonyesha ya kuwa alikubaliana na Labani juu ya agano Yakobo aliapa kwa Mungu, ambaye baba yake Isaka alimcha.

Genesis 31:54-55

Labani alifanya nini asubuhi iliyofuata?

Labani aliamka, akawabusu wajukuu na mabinti zake, akawabariki, na kurudu nyumbani.

Genesis 32

Genesis 32:3-5

Yakobo alituma ujumbe kwa nani alipokuwa njiani kuelekea Kaanani?

Yakobo alituma ujumbe kwa kaka yake Esau katika njia ya kuelekwa Kaanani.

Kwa sababu ipi Yakobo alituma ujumbe huu

Yakobo alitamani kupata kibali machoni pa Esau.

Genesis 32:6-10

Mwitikio wa Yakobo aliposikia Esau alikuwa akija na watu mia nne ulikuaje, na alifanya nini?

Yakobo aliogopa, kwa hiyo aligawanyisha watu wake katika makundi mawili ili kwamba kama Esau atashambulia kundi moja, kundi lingine liweze kutoroka.

Genesis 32:11-18

Ombi la Yakobo kwa Yahwe lilikuwa lipi?

Yakobo alimuuliza Yahwe kumuokoa kutoka mkono wa Esau.

Juu ya ahadi gani Yakobo alimkumbusha Yahwe?

Yakobo alimkumbusha Yahwe ya kuwa aliahidi kumfanikisha Yakobo, na kufanya uzao wake kama mchanga wa bahari.

Genesis 32:19-21

Yakobo alifikiri angefanikisha nini kwa kutuma zawadi kwa ndugu yake Esau?

Yakobo alifikiri ya kwamba labda angeweza kumtuliza Esau kwa zawadi ambazo alituma kwa Esau ili kwamba baadae, Yakobo atakapomuona, Esau aweze kumpokea.

Genesis 32:22-23

Yakobo aliishiaje kuwa peke yake usiku huo?

Alichukua wake zake, watumishi wake wa kike, na watoto wake katika kijito cha Yaboki.

Genesis 32:24-26

Yakobo alifanya nini usiku huo mpaka alfajiri?

Yakobo alishindana na mtu mpaka alfajiri.

mtu alifanya nini alipoona hakuweza kumshinda Yakobo?

Mtu alipiga nyinga ya Yakobo na kuitengua.

Yakobo alidai nini kabla ya kumruhu mtu kuondoka?

Yakobo alidai ya kwamba mtu ambariki.

Genesis 32:27-28

Mtu alisema jina la Yakobo lingekuwa lipi?

Mtu alisema ya kwamba jina la Yakobo sasa lingekuwa Israeli.

Genesis 32:29-30

Yakobo alisema amemuona nani uso kwa uso usiku huo?

Yakobo alisema amemuona Mungu uso kwa uso usiku huo.

Genesis 32:31-32

Yakobo alipata tatizo gani la kimwili baada ya usiku huo?

Yakobo alichechemea kwa sababu ya nyonga yake baada ya usiku huo.

Genesis 33

Genesis 33:1-3

Esau alipokuwa akija kwa Yakobo, Yakobo aliwaweka wake zake kwa mpangilio upi nyuma yake?

Yakobo aliwaweka watumishi wake wa kike kwanza, kisha Lea na baadae Raheli.

Yakobo alifanya nini alipokuja karibu na kaka yake?

Yakobo aliinama kuelekea ardhini mara saba alipokuja karibu na kaka yake.

Genesis 33:4-8

Esau alifanya nini alipokuja kwa ndugu yake?

Esau alikimbia kukutana na Yakobo, akamkumbatia, akakumbatia shingo yake, na kumbusu.

Genesis 33:9-11

Esau alimwambia nini Yakobo kufanya na zawadi alizozituma mapema kwa Esau?

Esau alimwambia Yakobo kubaki nazo mwenyewe, kwa kuwa alikuwa na za kutosha.

Ni sababu gani mbili Yakobo alimpa Esau apokee zawadi zake?

Yakobo alisema ya kwamba kwa sababu Mungu amemtendea mema kwake, na kwa sababu alikuwa na vya kutosha, Esau alipaswa kupokea zawadi zake.

Genesis 33:12-14

Kwa nini Yakobo alisema anataka Esau aende kabla yake, wakati yeye akisafiri taratibu zaidi?

Yakobo alisema alitaka Esau aende kabla yake kwa sababu wanyama wake wangekufa kama wangepelekeshwa kwa haraka sana.

Yakobo alisema angekwenda kuwaleta familia yake na wanyama wake wapi?

Yakobo alisema alikwenda kuwaleta familia yake na wanyama kwa Esau huko Seiri.

Genesis 33:15-17

Yakobo alisafiri kwenda wapi, ambapo alijijengea nyumba?

Yakobo alisafiri kwenda Sukothi, ambapo alijijengea nyumba.

Genesis 33:18-20

Yakobo alisafiri kwenda wapi, ambapo alijinunulia kipande cha ardhi?

Yakobo alisafiri kwenda Shekemu, ambapo alinunua kipande cha ardhi.

Genesis 34

Genesis 34:1-3

Shekemu, mwana wa Hamori, alifanya nini alipomuona Dina, binti wa Lea?

Shekemu alimkamata Dina, akamshambulia, na kumbaka.

Genesis 34:4-5

Yakobo alifanya nini awali aliposikia kuhusu kilichotokea kwa Dina?

Yakobo alijizuia kwanza hadi pale wanawe waliporudi kutoka shambani.

Genesis 34:6-7

Wana wa Yakobo waliitikiaje waliposikia kile alichofanya Shekemu kwa Dina?

Wana wa Yakobo walipatwa na hasira sana.

Genesis 34:8-10

Hamori, baba wa Shekemu, alimtaka Yakobo kufanya nini?

Hamori alimtaka Yakobo kumpatia Dina kuwa mke wa Shekemu, na kuruhusu familia ya Yakobo kuoana na familia ya Hamori.

Genesis 34:11-13

Shekemu alisema yupo tayari kufanya nini ili awe na Dina kama mke wake?

Shekemu alisema angelipa mahari kubwa ambayo Yakobo angetaja.

Ni kwa namna gani wana wa Yakobo walimjibu Shekemu, na kwa nini?

Wana wa Yakobo walimjibu Shekemu kwa udanganyifu, kwa sababu Shekemu alimnajisi Dina.

Genesis 34:14-21

Wana wa Yakobo walitaja mahitaji gani kwa Hamori kabla ya kukubali kuoana na familia ya Hamori?

Wana wa Yakobo walihitaji ya kwamba wanamume wote wa familia ya Hamori watahiriwe.

Genesis 34:22-23

Hamori na Shekemu walisema nini kingekuwa chao iwapo wataoana na familia ya Yakobo, walipokuwa wakizungumza na wanamume wa mji wao?

Walisema ya kwamba mifugo, mali, na wanyama wote wa Yakobo vitakuwa vyao iwapo wataoana na familia ya Yakobo.

Genesis 34:24-26

Wanamume wa mji wa Hamori walijibuje walipoulizwa kama walikuwa tayari kutahiriwa?

Wanamume wa mji wa Hamori walimsikiliza hamori na Shekemu na kila mwanamume alitahiriwa.

Simoni na Lawi walifanya nini katika siku ya tatu baada ya wanamume wa familia ya Hamori kuwa wametahiriwa?

Simoni na Lawi waliwaua wanamume wote katika mji wa Hamori.

Genesis 34:27-29

Wana wote wa Yakobo walifanya nini?

Wana wote wa Yakobo walipora mji, wakachukua utajiri wote, na kukamata watoto na wake.

Genesis 34:30-31

Yakobo aliitikiaje alipojua kuhusu kile walichofanya Simoni na Lawi?

Yakobo alisema ya kwamba Simoni na Lawi wameleta shida juu yake kwa sababu wakazi wa nchi ile wanaweza kumuangamiza yeye na nyumba yake.

Kwa nini Simoni na Lawi walisema walifanya vile?

Simoni na Lawi walisema walifanya vile kwa sababu Shekemu alimtendea dada yao Dina kama kahaba.

Genesis 35

Genesis 35:1-3

Mungu alimwambia Yakobo kwenda wapi na kufanya nini?

Mungu alimwambia yakobo kwenda Betheli na kujenga madhabahu kwa Mungu.

Yakobo kisha aliwaambia watu wa nyumba yake kufanya nini?

Yakobo aliwaambia kuweka mbali miungu yao ya kigeni, na kujitakasa wenyewe, na kubadili mavazi yao.

Genesis 35:4-5

Kwa nini watu wa miji iliyozumzunguka Yakobo na nyumba yake hawakumfuata walipokuwa wakisafiri?

Watu wa miji iliyomzunguka hawakumfuata kwa sababu walimuogopa Mungu.

Genesis 35:6-8

Kwa nini Yakobo alipaita mahali walipofikia "El Betheli"?

Yakobo alipaita "El Betheli" kwa sababu ilikuwa mahali Mungu alijifunua kwa Yakobo pale Yakobo alipokuwa akimtoroka Esau.

Genesis 35:9-10

Mungu alimpatia Yakobo jina gani jipya?

Mungu alimpatia Yakobo jina jipya la Israeli.

Genesis 35:11-15

Mungu alithibitisha ahadi gani kwa Yakobo?

Mungu alithibitisha ahadi ya kwamba Yakobo atakuwa kundi la mataifa lenye wafalme miongoni mwa uzao wake, na kwamba nchi ambayo Mungu alimuahidi Abrahamu na Isaka itapewa kwake na uzao wake.

Genesis 35:16-20

Nini kilitokea kwa Raheli wakati wa uchungu wake kwa Benyamini?

Raheli alikufa wakati wa uchungu kwa Benyamini.

Genesis 35:21-22

Israeli alisikia kuhusu jambo gani ambalo Rubeni alifanya?

Israeli alisikia ya kwamba Rubeni alilala na Bilha, suria wa Israeli.

Yakobo alikuwa na wana wangapi wa kiume?

Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili.

Genesis 35:23-27

Watoto gani wa Yakobo walizaliwa kutoka kwa Raheli

Yusufu na Benyamini walizaliwa kutoka kwa Raheli.

Genesis 35:28-29

Isaka aliishi miaka mingapi?

Isaka aliishi miaka mia moja na themanini.

Nani alimzika Isaka?

Esau na Yakobo walimzika Isaka.

Genesis 36

Genesis 36:1-5

Vizazi vya Esau vinaitwa kwa jina gani lingine?

Vizazi vya Esau pia vinaitwa Edomu.

Esau alipata wake zake kutoka wapi?

Esau alipata wake zake kutoka kwa Wakaanani.

Genesis 36:6-8

Kwa nini Esau aliondoka kutoka kwa ndugu yake Yakobo?

Esau aliondoka kutoka kwa ndugu yake Yakobo kwa sababu nchi haikuweza kuwatunza wote wawili kwa kuwa mali zao zilikuwa nyingi sana.

Esau alikaa wapi?

Esau alikaa katika kilima cha nchi ya Seiri.

Genesis 36:9-19

Jina la mwana wa kiume aliyezaliwa na Timna, suria wa mwana wa kwanza wa Esau Elipfazi lilikuwa nani?

Jina la mwana aliyezaliwa na Timna alikuwa Amaleki.

Genesis 36:20-30

Ni nani alikuwa baba wa wakazi wa nchi ambayo Edomu aliishi?

Seiri Mhori alikuwa baba wa wakazi wa nchi ambayo Edomu aliishi.

Genesis 36:31-39

Watu wa Edomu walikuwa na nini kabla Israeli kuwa nao?

Watu wa Edomu walikuwa na wafalme kabla mfalme yeyote hajatawala juu ya Waisraeli.

Genesis 36:40-43

Ni nani alikuwa baba wa Waedomu?

Esau alikuwa baba wa Waedomu.

Genesis 37

Genesis 37:1-2

Yakobo alikaa na kuishi wapi?

Yakobo aliishi katika nchi ya Kaanani.

Yusufu alileta nini kwa baba yake Yakobo alipochunga mifugo na ndugu zake?

Yakobo alileta taarifa mbaya kuhusu ndugu zake kwa baba yake.

Genesis 37:3-6

Israeli alionyeshaje ya kwamba anampenda Yusufu kuliko wanawe wengine?

Israeli alimshonea Yusufu vazi zuri.

Ndugu zake Yusufu walifikiri nini kuhusu Yusufu?

Ndugu zake Yusufu walimchukia na hawakuweza kuongea naye vyema.

Genesis 37:7-8

Yusufu aliona nini katika ndoto yake ya kwanza?

Yusufu aliona mganda umesimama wima wakati za ndugu zake zimeinama kwa mganda wake.

Ndugu zake na Yusufu walifikiri nini kuhusu Yusufu baada ya kuwaambia juu ya ndoto yake ya kwanza?

Ndugu zake Yusufu walimchukia tena zaidi.

Genesis 37:9-11

Yusufu aliona nini katika ndoto yake ya pili?

Yusufu aliona jua, mwezi, na nyota kumi na moja zikiinama chini kwake.

Katika ndoto ya pili ya Yusufu, jua, mwezi na nyota ziliwakilisha nini?

Jua, mwezi, na nyota ziliwakilisha baba, mama na kaka zake Yusufu

Genesis 37:12-17

Yakobo alimtuma Yusufu katika bonde la Hebroni kufanya nini?

Yakobo alimtuma Yusufu katika bonde la Hebroni kuona kama ndugu zake wako salama, na kuleta taarifa kwa Yakobo.

Genesis 37:18-20

Ndugu zake Yusufu walipanga kufanya nini walipomuona Yusufu akija?

Ndugu zake Yusufu walipanga kumuua Yusufu na kumtupa katika moja ya mashimo.

Genesis 37:21-26

Rubeni alitoa ushauri gani kwa ndugu zake, na kwa nini?

Rubeni alishauri ya kwamba ndugu wamtupe tu Yusufu katika shimo, ili kwamba aweze kumuokoa Yusufu baadae.

Genesis 37:27-30

Ndugu zake Yusufu walimuuza kwa nani na kwa kiasi gani?

Ndugu zake Yusufu walimuuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande ishiri vya fedha.

Yusufu alipelekwa wapi?

Yusufu alipelekwa Misri.

Genesis 37:31-33

Ndugu zake Yusufu walifanyaje ili ionekane kuwa Yusufu alikufa?

Ndugu zake Yusufu waliua mbuzi na kuchovya vazi la Yusufu ndani ya damu, na kumpatia Yakobo vazi hilo.

Genesis 37:34-36

Yakobo alifanya nini aliporidhia Yusufu alikufa?

Yakobo alirarua mavazi yake, akavaa mavazi ya magunia, na kuomboleza kwa ajili ya mwanawe kwa siku nyingi.

Yusufu aliuzwa kwa nani Misri?

Yusufu aliuzwa kwa Potifa, afisa wa Farao, huko Misri.

Genesis 38

Genesis 38:1-5

YUda alichukua mke kutoka kwa nani?

YUda alichukua mke kutoka mtu wa Kaanani.

Genesis 38:6-7

Yahwe alifanya nini na mwana wa kwanza wa Yuda, na kwa nini?

Yahwe alimuua Eri kwa sababu alikuwa muovu.

Genesis 38:8-10

Ni kwa namna gani mwana wa Onani wa pili hakutimiza wajibu wa shemeji wa kumpatia mtoto Eri?

Onani alimwaga mbegu zake juu ya ardhi alipolala na Tamari.

Yahwe alifanya nini na mwana wa Yuda wa pili Onani, na kwa nini?

Yahwe alimuua Onani kwa sababu alichofanya kilikuwa kiovu.

Genesis 38:11

Yuda kisha alitoa ahadi gani kwa Tamari?

Yuda alimuahidi Tamari mwanawe wa tatu Shela kuwa mumewe pale Shela atakapokua.

Genesis 38:12-16

Baada ya muda mrefu, kwa nini Yuda alitakiwa kufarijiwa?

Yuda alifarijiwa kwa sababu mke wake alifariki.

Tamari alifanya nini aliposikia ya kwamba Yuda alikuwa akielekea Timna?

Tamari alivua nguo zake za kijane, na kuvaa shela na kujifunika, na kukaa njiani kwenda Timna.

Kwa nini Tamari alifanya hivi?

Tamari alifanya hivi kwa sababu mwana wa Yuda wa tatu Shela alikua, lakini hakupewa kwake kama mke.

Genesis 38:17-20

Tamari alichukua nini kama rehani kwa malipo kabla Yuda hajalala naye?

Yuda alimpatia Tamari mhuri wake, mshipi, na fimbo kama rehani ya malipo.

Genesis 38:21-23

Yuda alipojaribu kurejesha rehani yake kwa kumlipa kahaba kwa mbuzi mdogo, alijifunza nini?

Yuda alijifunza ya kwamba hapakuwa na kahaba wa hekalu katika eneo lile.

Genesis 38:24-26

Yuda alitaka kufanya nini aligundua ya kwamba Tamari alikuwa mimba?

Yuda alitaka kumchoma Tamari kwa sababu alipata mimba kwa njia ya ukahaba.

Tamari alifanya nini alipoletwa nje kwa Yuda?

Alisema ya kwamba alipata mimba kwa mwanamume aliyemiliki mhuri, mshipi na fimbo alizokuwa nazo.

Yuda alijibuje alipoona mhuri, mshipi na fimbo yake?

Yuda alisema ya kwamba Tamari alikuwa mwenye haki kuliko yeye, kwa sababu hakumpatia Tamari kwa Shela awe mke wake.

Genesis 38:27-30

Tamari alizaa watoto wangapi?

Tamari alipata mapacha.

Mkunga alifanya nini pale mmoja wa mapacha wa Tamari alipotoa mkono wake nje mwa tumbo la Tamari?

Pale ambapo mmoja wa mapacha wa Tamari alipotoa mkono wake nje ya tumbo la Tamari, mkunga alichukua kamba ya rangi ya zambarau na kufunga mkononi mwake na kusema, "Huyu ametoka wa kwanza".

Genesis 39

Genesis 39:1-2

Ni nani alimnunua Yusufu Misri?

Potifa, afisa wa Farao, alimnunua Yusufu Misri.

Genesis 39:3-4

Kwa nini Yusufu alifanikiwa Misri?

Yusufu alikuwa na mafanikio kwa sababu Yahwe alikuwa pamoja naye.

Genesis 39:5-6

Potifa aliweka nini chini ya usimamizi wa Yusufu?

Potifa aliweka kila kitu alichokuwa nacho chini ya usimamizi wa Yusufu.

Genesis 39:7-9

Mke wa Potifa alimwambia Yusufu kufanya nini?

Mke wa Potifa alimwambia Yusufu kulala naye.

Yusufu alijibuje kwa ombi la mke wa Potifa?

Yusufu alikataa na kusema hawezi kufanya uovu mkubwa namna hii na kutenda dhambi dhidi ya Mungu.

Genesis 39:10-12

Yusufu alifanya nini pale mke wa Potifa alipomkamata nguo zake?

Yusufu aliacha nguo zake mikononi mwake na kukimbia nje.

Genesis 39:13-18

Mke wa Potifa alitoa mashataka gani dhidi ya Yusufu?

Alimshtaki kwa kujaribu kulala naye kinyume na ridhaa yake.

Genesis 39:19-20

Potifa alifanya nini aliposikia mashtaka dhidi ya Yusufu?

Potifa alipata hasira sana na kumweka Yusufu gerezani.

Genesis 39:21-23

Kwa kipindi hiki, Yahwe alionyesha nini kwa Yusufu?

Yahwe alionyesha agano lake la uaminifu kwa Yusufu katika kipindi hiki.

Mlinzi wa gereza aliweka nini chini ya usimamizi wa Yusufu?

Mlinzi wa gereza aliwaweka wafungwa wote chini ya usimamizi wa Yusufu.

Matokeo ya kila jambo aliyofanya Yusufu yalikuwa ni nini, na kwa nini?

Yahwe alifanikisha kila kitu alichofanya Yusufu.

Genesis 40

Genesis 40:1-3

Kwa nini mfalme aliwaweka mnyweshaji na mwokaji wake gerezani?

Aliwaweka gerezani kwa sababu walimkasirisha.

Genesis 40:4-5

Nini kilitokea kwa mnyweshaji na mwokaji usiku huo huo?

Mnyweshaji na mwokaji kila mmoja aliota ndoto usiku huo huo.

Genesis 40:6-11

Kwa nini mnyweshaji na mwokaji wote wawili walikuwa na huzuni asubuhi iliyofuata?

Wote wawili walikuwa na huzuni kwa sababu hakuna aliyeweza kutafsiri ndoto zao.

Yusufu alisema ni nani aliyeweza kutoa tafsiri ya ndoto zile?

Yusufu alisema ya kwamba Mungu angeweza kutoa tafsiri ya ndoto zile.

Genesis 40:12-13

Yusufu alisema tafsiri ya mnyweshaji ilikuwa ni nini?

Yusufu alisema ya kwamba ndoto ilimaanisha kuwa ndani ya siku tatu Farao atarejesha mnyweshaji katika shughuli yake.

Genesis 40:14-17

Yusufu alitoa ombi gani kwa mnyweshaji baada ya kutoa tafsiri ya ndoto yake?

Yusufu aliomba ya kwamba mnyweshaji amkumbuke, na kumtaja kwa Farao, na kumtoa nje ya gereza.

Genesis 40:18-19

Yusufu alisema tafsiri ya mwokaji ilikuwa ni nini?

Yusufu alisema ya kwamba ndoto ilimaanisha katika siku tatu Farao atamtundika mwokaji juu ya mti.

Genesis 40:20-23

Tukio gani muhimu lilitokea siku tatu baadae?

Siku ya kuzaliwa ya Farao ilikuwa siku tatu baadae.

Farao alifanya nini kwa mnyweshaji na mwokaji katika siku hiyo?

Farao alimrejesha mnyweshaji, lakini alimtundika mwokaji, kama Yusufu alivyotafsiri kwao.

Je mnyweshaji alikumbuka ombi la Yusufu kwake?

Hapana, mnyweshaji hakukumbuka kumsaidia Yusufu, lakini alimsahau.

Genesis 41

Genesis 41:4-6

Katika ndoto ya kwanza ya Farao, ng'ombe saba wembamba na ng'ombe saba wanene walifanya nini?

Ng'ombe saba wembamba waliwala wale ng'ombe saba wanene.

Genesis 41:7-11

Katika ndoto ya pili ya Farao, masuke saba membamba yalifanya nini kwa masuke saba mema?

Masuke saba membamba yalimeza yale masuke saba mema.

Waganga na wenye hekima wa Farao walitafsirije ndoto zake?

Waganga na wenye hekima wa Farao hawakuweza kutafsiri ndoto za Farao.

Genesis 41:12-13

Mkuu wa wanyweshaji alimwambia nini Farao kuhusu Yusufu?

Mkuu wa wanyweshaji alimwambia Farao ya kwamba kijana wa Kiebrania alitafsiri kwa usahihi na ndoto ya mwenzake walipokuwa kifungoni.

Genesis 41:14-24

Yusufu alisema ni nani angetafsiri ndoto ya Farao?

Yusufu alisema ya kwamba Mungu angejibu ndoto ya Farao na upendeleo.

Genesis 41:25-26

Yusufu alisema ya kuwa Mungu alikuwa akitamka nini kwa Farao?

Yusufu alisema ya kwamba Mungu alikuwa akitamka kwa Farao kile Mungu alichotaka kufanya.

Wale ng'ombe saba wema na masuke saba mema yaliwakilisha nini ndani ya ndoto?

Wale ng'ombe saba wema na masuke saba mema yaliwakilisha miaka saba ya mema.

Genesis 41:27-29

Wale ng'ombe saba nyembamba na masuke saba membamba yaliwakilisha nini ndani ya ndoto?

Wale ng'ombe saba wembamba na masuke saba membamba yaliwakilisha miaka saba ya njaa.

Genesis 41:30-32

Kulingana na Yusufu, kwa nini Farao alipewa ndoto mbili?

Farao alipewa ndoto mbili kwa sababu suala lilikuwa limethibitishwa na Mungu, na Mungu angetekeleza hivi karibuni.

Genesis 41:33-36

Yusufu alimshauri Farao kuchukua katika miaka saba ya mema sehemu ipi ya mazao ya Misri?

Yusufu alimshauri Farao kuchagua mtu kukusanya moja ya tano ya mazao katika miaka saba ya mema.

Genesis 41:37-38

Farao alisema nini imo ndani ya Yusufu?

Farao alisema ya kwamba Roho ya Mungu ilikuwa ndani ya Yusufu.

Genesis 41:39-47

Farao alimpatia Yusufu nafasi gani ya mamlaka?

Farao alimpatia Yusufu mamlaka juu ya nyumba ya Farao na juu ya nchi yote ya Misri, wa pili tu kwa Farao.

Genesis 41:48-49

Yusufu alitunza kiasi gani cha mazao katika miaka saba ya mema?

Yusufu alitunza mazao kama mchanga wa bahari, kiasi kisichohesabika.

Genesis 41:50-52

Wana wawili wa Yusufu waliozaliwa kabla ya njaa walikuwa kina nani?

Wana wa Yusufu walikuwa Manase na Efraimu.

Genesis 41:53-54

Miaka saba ya njaa ilisambaa kiasi gani?

Miaka saba ya njaa ilikuwa katika nchi yote.

Genesis 41:55-57

Yusufu alifanya nini watu wa Misri walipomlilia Farao kwa ajili ya chakula?

Yusufu alifungua maghala yote na kuuza chakula kwa Wamisri wote.

Ni nani alikuja Misri kununua mazao kwa Yusufu?

Dunia yote ilikuja Misri kununua mazao kutoka kwa Yusufu.

Genesis 42

Genesis 42:1-4

Yakobo alimtuma nani Misri kununua mazao?

Ndugu kumi wa Yusufu, bila Benyamini, walikwenda Misri kununua mazao.

Genesis 42:5-6

Ndugu wa Yusufu walifanya nini walipokuja kwa Yusufu kununua mazao?

Ndugu wa Yusufu waliinama chini kwake nyuso zao kuelekea ardhini.

Genesis 42:7-8

Yusufu alifanya nini alipowagundua ndugu zake.

Yusufu alijibadili na kuongea kwa ukali na ndugu zake.

Genesis 42:9-11

Yusufu alitoa mashtaka gani dhidi ya ndugu zake?

Yusufu aliwashtaki ndugu zake kuwa wapelelezi.

Genesis 42:12-13

Ndugu zake Yusufu walisema ndugu wao mdogo yupo wapi?

Ndugu zake Yusufu walisema ndugu yao mdogo alikuwa na baba yao katika nchi ya Kaanani.

Ndugu zake Yusufu walisema ndugu yao aliyepotea yupo wapi?

Ndugu zake Yusufu walisema ndugu yao aliyepotea hakuwa hai tena.

Genesis 42:14-17

Yusufu aliwapa ndugu zake mtihani gani kudhihirisha hawakuwa wapelelezi?

Yusufu alisema ndugu zake hawataondoka Misri, hadi pale ndugu yao mdogo aje Misri.

Yusufu aliwaweka ndugu zake wapi na kwa muda gani?

Yusufu aliwaweka ndugu zake kifungoni kwa siku tatu.

Genesis 42:18-20

Yusufu aliwaambia ndugu kufanya nini ili waweze kuishi?

Yusufu aliwaambia kuruhusu mmoja wa ndugu kuwekwa gerezani, wakati wengine wakichukua mazao hadi Kaanani na kumleta ndugu yao mdogo.

Genesis 42:21-22

Kwa nini ndugu zake Yusufu waliamini matatizo haya yalikuja juu yao?

Waliamini ya kwamba damu ya Yusufu ilidaiwa kwao kwa kile walichofanya kwa Yusufu.

Genesis 42:23-25

Yusufu alifanya nini aliposikia ndugu zake wakizungumza kuhusu kile walichofanya kwake?

Yusufu aliposikia ndugu zake wakizungumza kuhusu kile walichofanya kwake, Yusufu akatoka kwao na kulia.

Yusufu alirudisha nini ndani ya magunia ya kila ndugu?

Yusufu alirudihsa pesa ya kila ndugu ndani ya gunia lake.

Genesis 42:26-34

Ndugu walichukuliaje walipogundua ya kuwa kila gunia la ndugu lilikuwa na pesa ndani mwake?

Mioyo yao ilizimia na wakasemeshana kati yao wakitetemeka.

Ndugu walimlaumu nani kwa matatizo yao ya muda huo?

Ndugu walimlaumu Mungu, wakiuliza kwa nini Mungu alifanya hivi kwao.

Genesis 42:35-36

Ndugu na Yakobo waligundua nini walipotoa kila kitu ndani ya magunia?

Waligundua ya kwamba pesa ya kila mtu ilikuwa ndani ya gunia lake.

Yakobo aliogopa kitu gani kutokea kwa sababu ya suala lao?

Yakobo aliogopa ya kwamba Simoni na Benyamini watachukuliwa kutoka kwake.

Genesis 42:37-38

Rubeni alitoa kiapo gani kwa Yakobo?

Rubeni aliapa kumrudisha benyamini kwa Yakobo kutoka Misri; la sivyo watoto wawili wa Rubeni wanaweza kuuwawa.

Je Yakobo alimruhusu Rubeni kumpeleka Benyamni Misri?

Hapana, Yakobo hakumruhusu Rubeni kumpeleka Benyamini Misri.

Yakobo alisema nini kingetokea kwake kama Benyamni angekufa?

Yakobo alisema ya kuwa angeshuka na majonzi kaburini kama Benyamini angekufa.

Genesis 43

Genesis 43:1-2

Kwa nini Israeli aliwaambia wanawe kurudi tena na kununua chakula Misri?

Njaa ilikuwa kali sana na walikuwa wamekula nafaka waliokuwa wamenunua kutoka Misri katika safari ya kwanza.

Genesis 43:3-7

Yuda alisema ni lazima wawe na nini ili kwenda Misri tena?

Yuda alisema ni lazima wawe na ndugu yao Benyamini ili kushuka Misri.

Genesis 43:8-10

Ni kiapo gani alichofanya Yuda kwa baba yake Israeli?

Yuda alisema ya kwamba asipomrudisha Benyamini, angebeba lawama milele.

Genesis 43:11-12

Israeli aliwaambia nini ndugu kubeba nacho kwenda Misri?

Israeli aliwaambia ndugu kuchukua baadhi ya bidhaa za ardhi, na kubeba mara mbili ya pesa.

Genesis 43:13-17

Israeli alimwomba Mungu juu ya nini kuhusu safari hii?

Israeli alimwomba Mungu kuwapa ndugu neema kule Misri, ili kwamba ndugu wote waweze kuachiwa.

Genesis 43:18-20

Ndugu walichukuliaje walipochukuliwa katika nyumba ya Yusufu, na kwa nini?

Ndugu waliogopa wangekamatwa na kuchukuliwa kama watumwa kwa sababu ya pesa ndani ya magunia yao katika safari ya kwanza.

Genesis 43:21-25

Ndugu walimwambia nini mtunzaji wa nyumba wa nyumba ya Yusufu?

Ndugu walimwambia mtunzaji wa nyumba kuwa wameleta pesa iliyoachwa katika magunia yao, na pesa kwa ajili ya kununua chakula.

Mtunzaji wa nyumba alisema pesa iliyoachwa katika magunia yao ilitoka wapi?

Mtunzaji wa nyumba alisema pesa iliyoachwa katika magunia yao ilitoka kwa Mungu wao.

Genesis 43:26-29

Ndugu walifanya nini Yusufu alipokuja nyumbani?

Ndugu walileta zawadi katika nyumba, na kuinama chini mbele ya Yusufu hata chini.

Yusufu aliwauliza ndugu kuhusu nani?

Yusufu aliwauliza ndugu kuhusu hali ya baba yao.

Genesis 43:30-31

Kwa nini Yusufu aliharakisha kutoka chumbani, na alifanya nini baada ya kuondoka?

Yusufu aliharakisha kutoka chumbani kwa sababu aliguswa sana kuhusu Benyamini, na alikwenda chumbani kwake kulia.

Genesis 43:32-34

Kwa nini Wamisri na Waebrania walikula mahali tofauti?

Ilikuwa chukizo kwa Wamisri kula na Waebrania.

Ndugu walipangwa kwa namna gani katika meza?

Ndugu walipangwa katika meza kulingana na haki yao ya kuzaliwa na umri.

Kipi hakikuwa kawaida kuhusu kiasi cha chakula ndugu walichopewa?

Sehemu ya Benyamini ilikuwa mara tano zaidi ya yeyote wa ndugu zake.

Genesis 44

Genesis 44:1-2

Yusufu alimwambia mtunzaji wake wa nyumba kufanya nini na magunia ya ndugu zake kabla hawajaondoka?

Yusufu alimwambia mtunzaji wake wa nyumba kujaza magunia ya ndugu zake na chakula, na kuweka pesa yao ndani ya magunia, na kuweka kikombe chake cha fedha katika gunia la mdogo.

Genesis 44:3-7

Kwa hali ya kawaida Yusufu alimwambia mtunzanji wa nyumba kusema nini kwa ndugu alipowapita nje ya mji?

Yusufu alimwambia mtunzaji wa nyumba kuwauliza kwa nini walirudisha uovu kwa wema na kuwashtaki kuiba kikombe cha Yusufu.

Genesis 44:8-10

Ndugu waliapa wangefanya nini iwapo mmoja wao aliiba kikombe cha Yusufu?

Ndugu walisema mtu atakayekutwa na kikombe afe, na wengine wawe watumwa.

Adhabu gani mtunzaji wa nyumba alisema ilikuwa iwapo kikombe kiliibiwa?

mtunzaji wa nyumba alisema ya kwamba yule ambaye kikombe kitakutwa naye atakuwa mtumwa wake, na wengine watakuwa hawana hatia.

Genesis 44:11-13

mtunzaji wa nyumba alipata nini, na ndugu walichukuliaje?

mtunzaji wa nyumba alikuta kikombe katika gunia la Benyamini na ndugu zake wakararua nguo zao.

Genesis 44:14-15

Ndugu walifanya nini waliporudi katika nyumba ya Yusufu?

Ndugu waliinama chini mbele ya Yusufu hadi chini.

Genesis 44:16-19

Yuda alisema ni nani amegundua dhambi ya ndugu?

Yuda alisema ya kwamba Mungu aligundua dhambi yao.

Yuda alisema ndugu sasa watakuwa kina nani?

Yuda alisema ndugu wote sasa watakuwa watumwa wa Yusufu.

Yusufu alisema atahitaji adhabu gani kutoka kwa ndugu?

Yusufu alisema ya kwamba mtu ambaye mkono ulikuwa na kikombe atakuwa mtumwa wake, na wengine wangeondoka kwa amani.

Genesis 44:20-22

Yuda alitoa sababu zipi kwa nini baba yake alimpenda ndugu yao mdogo?

Yuda alisema ya kwamba ndugu yao mdogo alikuwa mtoto wa baba yake wa uzeeni, na mtoto pekee aliyebaki kwa mama yake.

Ndugu walikuwa na wasiwasi nini kingetokea kwa baba yao iwapo mdogo wao angemuacha?

Ndugu walikuwa na mashaka baba yao angekufa kama mdogo wao angemuacha.

Genesis 44:23-26

Yuda alisema ni kwa nini walilazimika kumleta Benyamini pamoja nao Misri?

Yuda alisema walilazimika kumleta Benyamini kwa sababu Yusufu alisema hadi pale ndugu yao mdogo aje, wasingeuona uso wa Yusufu.

Genesis 44:27-29

Israeli alidhani ni nini kilitokea kwa Yusufu?

Israeli alidhani ya kuwa hakika Yusufu aliraruliwa katika vipande.

Israeli alisema nini kingetokea kwake iwapo Benyamini angechukuliwa kutoka kwake?

Israeli alisema ya kwa ndugu wangeletea mvi kwa majonzi hadi kaburini.

Genesis 44:30-32

Yuda alisema nini kingetokea kwa baba yake iwapo watarudi bila Benyamini?

Yuda alisema ya kwamba baba yake angekufa.

Yuda alisema amekuwa uhakika gani kwa Benyamini?

Yuda alisema ya kwamba kama hatamrudisha Benyamini kwa baba yake, atabeba hatia milele.

Genesis 44:33-34

Yuda alimuuliza nini Yusufu kufanya ili kwamba Benyamini arudi kwa baba yake?

Yuda alimwomba Yusufu kumfanya awe mtumwa wa Yusufu, ili kwamba Benyamini aweze kurudi kwa baba yake.

Genesis 45

Genesis 45:1-6

Yusufu alifanya nini alipojidhihirisha kwa ndugu zake, ambacho Wamisri walisikia?

Yusufu alilia kwa sauti alipojidhihirisha kwa ndugu zake.

Ndugu waliitikiaje pale Yusufu alipojidhihirisha kwao?

Ndugu hawakuweza kumjibu Yusufu kwa maana walikuwa wameshtushwa.

Genesis 45:7-8

Kulingana na Yusufu, kwa nini Mungu alimtuma Yusufu Misri?

Mungu alimtuma Yusufu Misri kuhifadhi uhai, na kutunza familia yake kama msalia wa duniani.

Mungu alimfanya Yusufu nini katika nchi ya Misri?

Mungu alimfanya Yusufu baba kwa Farao, bwana wa nyumba yote ya Farao, na mtawala juu ya nchi yote ya Misri.

Genesis 45:9-11

Yusufu alipangaje kuitunza familia yake?

Yusufu aliambia familia yake kuja na kuishi katika nchi ya Gosheni ambapo angewapa mahitaji.

Genesis 45:12-15

Yusufu aliwaambia ndugu zake kuharakisha kufanya nini?

Yusufu aliwaambia ndugu zake kuharakisha na kumleta baba yake Misri.

Genesis 45:16-20

Farao aliitikiaje aliposikia ya kwamba ndugu zake Yusufu wamekuja Misri?

Farao alipendezwa sana, na akamwambia Yusufu kuwaambia ndugu zake kumleta baba yao na nyumba zao kuishi katika nchi nzuri ya Misri.

Genesis 45:21-23

Ni nani alipokea zawadi za ziada na mgawanyo kwa ajili ya safari?

Benyamini alipokea vipande mia tatu vya fedha na mavazi matano ya kubadilisha, na Israeli alipokea punda ishirini ya punda waliobeba bidhaa.

Genesis 45:24-26

Israeli aliitikiaje aliposikia ya kuwa Yusufu alikuwa hai na mtawala wa nchi yote ya Misri?

Moyo wa Israeli ulishikwa na mshangao, kwa maana hakuamini ndugu walipomwambia.

Genesis 45:27-28

Israeli alisema alitaka kufanya nini kabla hajafa?

Israeli alisema alitaka kumuona Yusufu kabla hajafa.

Genesis 46

Genesis 46:1-4

Israeli alifanya nini Beersheba?

Israeli alitoa sadaza kwa Mungu wa baba yake Isaka.

Mungu alitoa ahadi gani kwa Israeli kule Beersheba?

Mungu aliahidi kumfanya Israeli kuwa taifa kubwa, na kwenda na Israeli Misri, na kumleta tena Israeli kutoka Misri, na kumfanya Yusufu afunike macho yake.

Genesis 46:5-11

Ni nani alikwenda Misri na Israeli?

Israeli na vizazi vyake vyote walikwenda Misri.

Genesis 46:12-25

Wana gani wa Yuda walikufa katika nchi ya Kaanani?

Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kaanani.

Genesis 46:26-27

Watu wangapi wa nyumba ya Yakobo walikuja Misri?

Watu sabini wa nyumba ya Yakobo walikuja Misri.

Genesis 46:28-32

Yusufu alifanya nini kukutana na baba yake?

Yusufu alikwenda na kibandawazi chake na kukutana na baba yake Israeli Gosheni.

Yusufu alifanya nini alipomwona baba yake?

Yusufu alimkumbatia shingo ya baba yake na kulia kwa muda mrefu.

Genesis 46:33-34

Yusufu aliwaambia nini ndugu zake kusema kwa Farao kuhusu kazi yao?

Ndugu walitakiwa kumwambia Farao ya kuwa walikuwa wafugaji wa mifugo tangu ujana wao.

Genesis 47

Genesis 47:3-4

Ndugu watano wa Yusufu walimwambia Farao kazi yao ilikuwa ipi?

Ndugu watano walimwambia Farao kazi yao ilikuwa ufugaji.

Ndugu walisema wao walikuwa wakazi wa aina gani katika nchi ya Misri?

Ndugu walisema walikuwa wakazi wa muda katika nchi ya Misri.

Genesis 47:5-6

Farao alimwambia nini Yusufu kufanya na familia ya Yusufu?

Farao alimwambia Yusufu kuwaweka familia ya Yusufu katika sehemu nzuri, nchi ya Gosheni.

Genesis 47:7-12

Yakobo alifanya nini kwa Farao alipokutana naye na alipotoka katika uwepo wake?

Yakobo alimbariki Farao alipokutana naye na alipotoka katika uwepo wake.

Yakobo alikuwa ameishi muda gani alipokutana na Farao?

Yakobo aliishi miaka mia moja na thelathini.

Yakobo alisema maisha yake yalikuaje kulinganisha na baba zake?

Yakobo alisema maisha yake hayakuwa marefu kama maisha ya baba zake.

Genesis 47:13-14

Yusufu aliweza kufanya nini kwa kuuza nafaka?

Yusufu aliweza kukusanya pesa yote katika nchi ya Misri na katika nchi ya Kaanani.

Genesis 47:15-17

Yusufu kisha aliweza kufanya nini kwa kubadilishana chakula na Wamisri?

Yusufu aliweza kubadili chakula kwa wanyama wote wa Wamisri.

Genesis 47:18-22

Baada ya pesa na wanyama kuwa wametolewa kwa Farao kwa kubadilisha na chakula watu wa Misri walitoa nini kama kubadilisha kwa chakula zaidi?

Watu wa Misri walitoa ardhi zao na wao wenyewe kama watumishi wa Farao kwa kubadilishana kwa chakula zaidi.

Genesis 47:23-26

Yusufu alihitaji sehemu gani ya mavuno yote kupewa kwa Farao?

Yusufu alihitaji moja ya tano ya mavuno iweze kupatiwa Farao.

Genesis 47:27-28

Kwa njia zipi watu wa Israeli walifanikiwa katika nchi ya Misri?

Watu wa Israeli walipata mali katika nchi ya Misri, na waliongezeka na kuzaana kwa wingi.

Yakobo alikufa katika umri gani?

Yakobo alifariki katika umri wa miaka mia moja na arobaini na saba.

Genesis 47:29-31

Israeli alimwomba Yusufu aape kufanya nini?

Israeli alimwomba Yusufu kuapa ya kuwa atabeba mifupa ya Israeli katika eneo la baba zake.

Genesis 48

Genesis 48:1-2

Yusufu aliskia ujumbe gani kuhusu baba yake, na kisha alifanya nini?

Yusufu alisikia ya kuwa baba yake alikuwa mgonjwa, kwa hiyo akachukua wanawe wawili.

Genesis 48:3-4

Yakobo alimkumbusha Yusufu ahadi gani kutoka kwa Mungu?

Yakobo alimkumbusha ya kwamba Mungu alimuahidi kuongezeka na kuzaana, atakuwa kusanyiko la mataifa, na nchi ya Kaanani itakuwa milki ya milele kwa uzao wake.

Genesis 48:5-7

Yakobo alisema angewafikiriaje wana wawili wa Yusufu katika urithi?

Yakobo alisema angewafikiria wana wawili wa Yusufu kama wanawe.

Genesis 48:8-13

Kwa nini Israeli hakutambua wana wa Yusufu?

Israeli hakuwatambua wana wa Yusufu kwa sababu macho yake yalikuwa yanashindwa kwa sababu ya umri wake.

Genesis 48:14-16

Nani alikuwa mwana wa kwanza wa Yusufu?

Manase alikuwa mwana wa kwanza wa wana wa Yusufu.

Israeli aliweka mkono wake wa kulia juu ya nani, na wa kushoto kwa nani?

Israeli aliweka mkono wake wa kulia juu ya Efraimu, na wa kushoto kwa Manase.

Genesis 48:17-18

Kwa nini Yusufu alijaribu kubadili nafasi ya mikono ya Israeli?

Yusufu alitegemea mkono wa kulia wa Israeli kuwa juu ya Manase kwa sababu alikuwa mzaliwa wa kwanza.

Genesis 48:19-20

Kwa nini Israeli alikataa kubadili nafasi ya mikono yake juu ya wana wawili wa Yusufu?

Israeli alikataa kwa sababu ndugu mdogo angekuwa mkubwa kuliko mzaliwa wa kwanza.

Israeli alisema watu wa Israeli watatamka baraka gani?

Israeli alisema watu wa Israeli watatamka baraka ya, "Mungu na akufanye kama Efrahimu na kama Manase"

Genesis 48:21-22

Israeli alisema nini kingetokea kwa Yusufu?

Israeli alisema ya kwamba Yusufu atarudishwa katika nchi ya baba zake.

Genesis 49

Genesis 49:1-2

Kwa nini Yakobo alikusanya wanawe pamoja?

Yakobo alikusanya wanawe pamoja kuwaambia nini kingetokea kwao na vizazi vya vya baadae.

Genesis 49:3-6

Rubeni alikuwa ni sifa gani nzuri?

Rubeni alikuwa aliyesalia mwenye heshima na nguvu.

Kwa nini Rubeni hangekuwa na umaarufu ingawa alikuwa mzawa wa kwanza?

Rubeni hangekuwa na umaarufu kwa sababu alinajisi kitanda cha baba yake.

Genesis 49:7

Yakobo alilaani nini juu ya Simoni na Lawi?

Yakobo alilaani ukali na hasira ya ukatili ya Simoni na Lawi.

Genesis 49:8-9

Yakobo alisema wanawe wengine watafanya nini mbele ya Yuda?

Yakobo alisema wanawe wengine watainama chini mbele ya Yuda.

Genesis 49:10-12

Ahadi gani kuhusu miaka ya baadae ilifanya kwa Yuda?

Yuda aliahidiwa ya kwamba fimbo ya utawala haitatoka kutoka kwake hadi Shilo atakapokuja, na kwamba mataifa watamtii yeye.

Genesis 49:13-15

Yakobo alisema vizazi vya Zebuloni vitaishi wapi?

Yakobo alisema vizazi vya Zebulono vitaishi katika fukwe ya bahari.

Genesis 49:16-18

Yakobo alisema Dani atakuwa kama mnyama gani?

Yakobo alisema Dani angekuwa kama nyoka mwenye sumu.

Genesis 49:19-21

Yakobo alisema Asheri atajulikana kwa jambo gani?

Yakobo alisema Asheri atajulikana kwa kutoa vyakula vya kifalme.

Genesis 49:22-23

Yakobo alisema Yusufu angekuwa kama aina gani la mmea?

Yakobo alisema Yusufu angekuwa kama tawi lizaalo ambaye matawi yake hupanda juu ya ukuta.

Genesis 49:24-30

Yakobo alisema ni nani angetunza upinde wa Yusufu imara na mikono yake hodari?

Yakobo alisema mikono ya mwenye nguvu wa Yakobo, Mwamba wa Israeli atatunza upinde wa Yusufu imara na mikono yake hodari.

Genesis 49:31-33

Ni nani aliyekuwa amezekwa katika sehemu ambayo Yakobo alitamani kuzikwa?

Abrahamu, Sara, Isaka, Rebeka, na Lea walikuwa wamezikwa kule.

Yakobo alifanya nini baada ya kutoa baraka zake na maelekezo kwa wanawe?

Yakobo alipumua pumzi yake ya mwisho na kwenda kwa watu wake.

Genesis 50

Genesis 50:1-3

Yusufu alifanya nini na mwili wa Israeli baada ya Israeli kufariki?

Yusufu alitia dawa mwili wa Israeli.

Genesis 50:4-6

Yusufu alitoa ombi gani kwa Farao kuhusu mazishi ya baba yake, na kwa nini alifanya ombi hili?

Yusufu aliomba aweze kwenda katika nchi ya Kaanani kumzika baba yake, kwa maana baba yake alimfanya aape.

Genesis 50:7-9

Nani aliondoka pamoja na Yusufu kumzika Israeli?

Maafisa wote wa Farao, washauri wa nyumba yake, maafisa waandamizi wa Misri, nyumba ya Yusufu, ndugu wa Yusufu, nyumba ya baba yake, na vibandawazi na wapanda farasi wote walikwenda na Yusufu.

Genesis 50:10-11

Wakaanani walisema nini walipomwona Yusufu pamoja na wale aliokuwa nao?

Wakaanani walisema ya kwamba hili lilikuwa tukio la huzuni sana kwa Wamisri.

Genesis 50:12-14

Yusufu na ndugu zake walikwenda wapi baadaya kumzika baba yao?

Yusufu na ndugu zake walirudi Misri.

Genesis 50:15-17

Ndugu wa Yusufu walikuwa na mashaka juu ya nini baada ya Israeli kufariki?

Ndugu zake Yusufu walikuwa na mashaka ya kwamba Yusufu angelipiza kisasi kwa maovu yote ndugu waliyofanya kwake.

Ndugu walimwomba Yusufu kufanya nini kuhusu makosa waliyoyafanya dhidi ya Yusufu?

Ndugu walimwomba Yusufu kuwasamehe kwa makosa waliyoyatenda dhidi ya Yusufu.

Genesis 50:18-21

Ndugu wa Yusufu walifanya nini walipokuja kwa Yusufu?

Walipokuja kwa Yusufu, ndugu zake Yusufu walianguka chini mbele zake.

Yusufu alisema ni wema gani ambao Mungu alifanya kupitia matendo maovu ya ndugu zake?

Yusufu alisema Mungu alifanya mema ya kuhifadhi maisha ya watu wengi.

Genesis 50:22-23

Yusufu aliishi muda gani?

Yusufu aliishi miaka mia moja na kumi.

Genesis 50:24-26

Yusufu alisema nini kinakaribia kutokea kwake?

Yusufu alisema ya kwamba alikaribia kufa.

Yusufu alisema ni ahadi gani ambayo Mungu angetimiza kwa uzao wa Israeli?

Yusufu alisema Mungu angekuja kwa watu na kuwaongoza katika nchi ambayo Mungu aliwaahidi kwa Abrahamu, Isaka na Yakobo.

Yusufu aliwafanya watu wa Israeli kuapa kuwa wangefanya?

Yusufu aliwafanya waape ya kuwa watabeba mifupa ya Yusufu kutoka Misri watakaondoka Misri.

Nini kilitokea kwa mwili wa Yusufu alipokufa?

Mwili wa Yusufu ulitiwa dawa na kuwekwa katika jeneza huko Misri.