Ruth
Ruth 1
Ruth 1:1-2
Kipindi gani katika historia ya Kiyahudi stori ya Ruthi ilitokea?
Ilitokea kipindi cha waamuzi
Kwanini Elimeleki aliamia Moabu na familia yake?
Alihamia kwasababu kuna ukame Yuda.
Ruth 1:3-5
Nini kilitokea familia ya Naomi Moabu?
Bwana wake na wana wake wa kiume wakafa, na kuacha nyuma mabinti wawili wakwe
Ruth 1:6-7
Kwanini Naomi aliamua kurudi Yuda?
Alisika kwamba Yahweh aliwapa watu wa Yuda chakula.
Ruth 1:8-10
Nini Naomi alitaka mabinti zake wakwe kufanya?
Warudi nyumbani kwa mama zao au kupata mabwana wengine
Ruth 1:11-15
Nani Naomi aliamini ni chanzo cha shida zake?
Yahweh ndiye chanzo cha shida zake
Ruth 1:16-18
Ruthi alimpa Noami ahadi gani alipo ishi naye?
Alisema "Utakapo enda, nitaenda; na utakapo ishi, nitaishi; watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu; utakapo kufa nitakufa."
Ruth 1:19-21
Naomi alirudi mji gani?
Bethilehemu
Ruth 1:22
Wakati gani wa mwaka Naomi na Ruthi walifika Bethilehemu?
Kipindi cha mavuno ya nafaka
Ruth 2
Ruth 2:1-2
Kulikuwa na mahisiano gani kati ya mume aliye kufa wa Ruthi na Boazi
Walikuwa ndugu
Ruth 2:3-4
Salamu gani Boazi aliwapa wafanya kazi wake?
Alisema, "Yahweh awe nawe"
Ruth 2:5-7
Nini Boazi alitaka kujua kuhusu Ruthi?
Alitaka kujua alikuwa wa mwanaume gani?
Ruth 2:8-9
Maelekezo gani Boazi alimpa Ruthi kuhusu kazi yake?
Alisema "Baki na ufanye kazi shambani na wafanya kazi wangu wa kike"
Ruth 2:10-18
Baada ya kupokea maelekezo mazuri, swali gani Ruthi alimuuliza Boazi?
Alimuuliza, "kwanini nimepata kibali machoni pako"
Ruth 2:19-20
Naomi alipo ona kiasi kikubwa cha nafaka Ruthi alicho nunua, swali gani alimuuliza Ruthi?
Alimuuliza, "Wapi umefanya kazi leo?"
Kwanini Naomi alimtakia Boazi alipo sikia kuwa Boazi amemsaidia Ruthi?
Alisema "Abarikiwe na Yahweh"
Ruth 2:21-22
Kwanini Naomi alifikiri ni vizuri Ruthi kufanya kazi na wafanya kazi wa kike wa Boazi?
Kwa kufanya hivyo, Ruthi hatakuja kudhuru shamba lingine
Ruth 2:23
Nini Ruthi alifanya kwa kipindi chote cha mavuno ya nafaka?
Alifanya kazi na wafanya kazi wa Boazi na kuishi na Naomi
Ruth 3
Ruth 3:1-2
Nini Naomi alisema ni matamanio yake kwa Ruthi?
Alitamani kwamba Ruthi awe na sehemu ya kupumzika, na maombo yatamuendea vizuri.
Ruth 3:3-7
Nini Naomi alimwambia Ruthi afanye kabla ya kwenda chini kupepeta?
Alimwambia ajisafishe, pake marashi, na kubadilisha nguo
Ruth 3:8-9
Wakati wa usiku, Boazi alishanga kuona nini?
Alishanga kuona mwanamke amelala miguuni mwake
Ruth 3:10-11
Kwanini Boazi aliomba baraka kwa Yahweh kwa ajili ya Ruthi?
Kwasababu Ruthi alimtaka Boazi na sio vijana
Nini Boazi alisema ata fanya kwa ajili ya ombi la Ruthi?
Alisema kwamba ata fanya yote aliyo muomba
Ruth 3:12-13
Kizuizi gani kilimzuia Boazi kutofanya sehemu ya ndugu kwa Ruthi?
Kulikuwa na ndugu mwingine wa karibu zaidi kuliko Boazi
Ruth 3:14-15
Kwanini Ruthi aliondoka eneo la kupeta kabla ya mtu kumtambua?
Maana Boazi alisema isijulikana kuwa amekuja eneo la kupeta
Ruth 3:16-18
Naomi alikuwa na uhakika kuwa Boazi ata suluhisha jambo kwa muda gani?
Ata suluhisha siku hiyo hiyo
Ruth 4
Ruth 4:1-2
Wapi Boazi alienda kusuluhisha jambo nani atakaye kuwa ndugu kwa Ruthi?
Alienda mjini.
Ruth 4:3-4
Nini Boazi aliwauliza ndugu mwingine kukuomboa kama akitaka?
Alimuza kukuomba eneo la ardhi lilo milikiwa na Elimeleki.
Nini lilikuwa jibu la ndugu huyo mwingine?
Alisema, "Nitakomboa."
Ruth 4:5-6
Maombi gani ya ziada Boazi alitaka kwa ndugu huyo mwingine afanye?
Alimwambia pia ata bidi amchukuwe Ruthi ili kuweza kuendeleza jina la Elimeleki
Ruth 4:7-8
Nini ndugu mwingine alifanya kuonyesha kuwa alikubaliana na Boazi kuwa mkombozi?
Alivua kiatu chake na kumpa Boazi.
Ruth 4:9-10
Boazi aliwakumbusha wazee kuwa wameshuhudia makubaliano gani mawili?
Wameshuhudia kwamba Boazi amenunua yote yaliyo kuwa ya Elimeleki, na pia amemchukuwa Ruthi kama mke wake.
Ruth 4:11-12
Baraka gani watu walitamani kwa Boazi?
Walitamani wazao kupitia Ruthi
Ruth 4:13-15
Kwanini wanawake walisema kwamba Ruthi alikuwa bora kuliko Naomi watoto saba wa kiume?
Kwasababu ya upendo wa Ruthi kwa Naomi, na kwasababu Ruthi alimzaa mjukuu kwa Naomi
Ruth 4:16-22
Nini ni mahusiano ya Naomi na mwana wa Ruthi?
Naomi alikuwa mlezi wake.