Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Amos

Amos 1

Amos 1:1-2

Je! Amosi alipokeaje mambo aliyoyaongea kuhusu Israeli?

Amosi aliyapokea mambo aliyaongea kuhusu Israeli katika maono.

Je! Amosi alikuwa anafanya kazi gani?

Amosi alikuwa mchungaji.

Amos 1:3-5

Kwa nini Yahwe anatangaza adhabu juu ya Damaski?

Yahwe anatangaza adhabu juu ya Damaski kwa sababu wameipura Gileadi pamoja na vyombo vya chuma.

Amos 1:6-8

Kwa nini Yahwe anatangaza ghadhabu juu ya Gaza?

Yahwe anatangaza ghadhabu juu ya Gaza kwa sababu wmateka watu wote kuwashika juu ya Edomu.

Je! Yahwe alitangaza nini angefanya kwenye boma ya Ben Hadadi, Gaza, na Tire?

Yahwe ametangaza angeiteketeteza boma ya Ben Hadadi, Gaza, na Tire.

Amos 1:9-10

Kwa nini Yahwe alitangaza ghadhabu juu ya Tire?

Yahwe alitangaza ghadhabu juu ya Tire kwa sababu waliwachukua makundi ya watu wote na kuuvunja mkataba wao wa undugu.

Amos 1:11-12

Kwa nini Yahwe anatangaza ghadhabu juu ya Edomu?

Yahwe alitangaza ghadhabu juu ya Edomu kwa sababu alimfuata ndugu yake kwa upanga.

Amos 1:13

Kwa nini Yahwe anatangaza ghadhabu juu ya Amoni?

Yahwe alitangaza ghadhabu juu ya Amoni kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba.

Amos 1:14-15

Je! Yahwe alitangaza nini angefanya kwenye maeneo ya Raba?

Yahwe alitangaza angeyateketeza maeneo ya Raba.

Je! Yahwe alitangaza nini kingetokea kwa mfalme wa Amoni?

Yahwe alimtangazia mfalme wa Amoni kwenda kwenye uhamisho.

Amos 2

Amos 2:1-3

Kwa nini Yahwe anatangaza ghadhabu juu ya Moabu?

Yahwe anatangaza ghadhabu juu ya Moabu kwa sababu Moabu ameichoma mifupa ya mfalme wa Edomu.

Amos 2:4-6

Kwa nini Yahwe altangaza ghadhabu juu ya yuda?

Yahwe alitangaza ghadhabu juu ya Yuda kwa sababu Yuda alikataa sheria ya Yahwe.

Je! Yahwe alitangaza nini angefanya kwenye boma ya Moabu na Yuda?

Yahwe alitangaza angeziteketeza boma za Moabu na Yuda.

Amos 2:7-8

Kwa nini Yahwe anatangaza ghadhabu juu ya Israeli?

Yahwe alitangaza ghadhabu juu ya Israeli kwa sababu Israeli imevikanyaga vichwa vya maskini.

Amos 2:9-10

Je! Ni urefu wa nani ulikuwa kama urefu wa mti wa mkangazi; alikuwa hodari kama mwaloni?

"waliokuwa warefu kuliko miti yote uliyo ijua na hodari kama mbao uijuayo"

Amos 2:11-12

Je! Waisraeli walifanya pamoja na manabii Yahwe aliokuwa amewafufua miongoni mwao?

Waisraeli waliwaamuru manabii wasitabiri.

Je! Waisraeli walifanya nini pamoja na Wabazareti Yahwe alipowafufua miongoni mwao?

Waisraeli waliwashawishi Wanazareti kunywa mvinyo.

Amos 2:13-14

Je! mtu akimbiaye na mtu hodari hawataweza kufanya?

Mtu akimbiaye hataona pakumbilia na mtu hodari hatajiongeza nguvu zake mwenyewe.

Amos 2:15-16

Je! Yahwe alitangaza nini kuhusiana na mpinda upinde, mkimbia haraka, mwendesha farasi, na mpiganaji shujaa?

Yahwe alimtangazia mpinda upinde hatasimama, mkimbia haraka hatakimbia, mwendesha farasi hatajiokoa mwenyewe, na hata mpiganaji shujaa atakimbia uchi katika hiyo siku.

Amos 3

Amos 3:1-2

Je! Neno la Yahwe li juu ya nani?

Neno la Yahwe li juu ya watu wa Israeli, familia yote Yahwe aliyoitoa Misri.

Je! Yahwe alimchagua nani kutoka familia zote za dunia?

Yahwe alimchagua Israeli kutoka familia zote za dunia.

Amos 3:3-4

Je! watu wawili wafanye nini ili kutembea pamoja?

Watu wawili lazima wakubaliane ili kutembea pamoja.

Amos 3:5-6

Wakaji janga lijapo juu ya mji, je! ni nani aliyelileta?

Wakati janga lijapo kwenye mji, Yahwe ndiye aliyelileta.

Amos 3:7-8

Je! Yahwe hufanya nini kabla ya kuchukua uamuzi?

Yahwe hufunua mpango wake kwa manabii wake kabla ya kuchukua uamuzi.

Amos 3:9-10

Je! Misri ingeona nini kama wangeona kile kilichokuwa kikitokea katika Samaria?

Misri wangeona ghasia kubwa na dhuluma katika Samaria.

Je! Israeli iliweka nini katika ngome zao?

Israeli iliweka nguvu na uharibifu katika ngome zao.

Amos 3:11-12

Je! Ni adhabahu gani ambayo Yahwe aliitangaza juu ya Israeli?

Yahwe alitangaza kwamba adui ataziteka nyara ngome za Israeli.

Je! Ni nani atakayeikimbia ghadhabu ya Yahwe?

Wachache wataikimbia ghadhabu ya Yahwe.

Amos 3:13-15

Katika siku Yahwe atakayo adhibu makosa ya Israeli, nani mwingine ataadhibiwa?

Yahwe ataziadhibu madhabahu za Betheli pia, kwa nyumba ya Yakobo.

Amos 4

Amos 4:1-3

Ni jina gani ambalo Yahwe aliwapatia wake wa tajiri waliokuwa wakiishi Samaraia?

Yawhe aliwaita wake za tajiri, "ngombe wa Bashani".

Je! Wake wa tajiri wanafanya nini katika Samaria kwa maskini?

Wake wa tajiri wanawadhulumu maskini na kuwaponda wahitaji.

Je! Yahwe anasema nini kitatokea kwa wake wa tajiri katika Samaria?

Yahwe anasema wake watachukuliwa mbali kwa ndoana na kutolewa katika mji.

Amos 4:4-5

Je! Ni nini kiwapendezacho watu wa Israeli?

Watu wa Israeli wamependezwa na dhambi katika Betheli na kuongeza dhambi katika Gilgali, kuleta dhabihu na zaka, kutoa sadaka ya shukrani, na kutangaza sadaka za hiari.

Amos 4:6-7

Je! Yahwe alifanya nini kwenye mvua ili watu wa Israeli wamrudie yeye?

Yahwe alizuia mvua kutoka Israeli ili watu wa Israeli wamrudie.

Amos 4:8-9

Je! Yahwe alifanya nini kwenye bustani, shamba la mizabibu, na miti ili watu wa Israeli wamrudie?

Yahwe alizipiga bustani, mashamba ya mizabibu, na miti kwa maradhi yanayosababisha kuvu, na kuwateketeza kwa nzige.

Amos 4:10-13

Je! Yahwe alifanya nini kwa watoto wa kiume ili watu wa Israeli wamrudie?

Yahwe aliwaua watoto wa kiume kwa upanga ili watu wa Israeli wamrudie.

Je! Yahwe alifanya nini kwa miji ili watu wa Israeli wamrudie?

Yahwe aliiangamiza miji ili watu wa Israeli wamrudie.

Je! Watu wa israeli walijibu vipi kwa majaribu ya Yahwe kuwasababisha kurudi?

Watu wa Israeli hawakumrudia Yahwe.

Amos 5

Amos 5:1-3

Je! Ni nani alianguka katika haya maombolezo?

Bikira wa Israeli alianguka katika haya maombolezo.

Amos 5:4-7

Je! Yahwe anaiambia kufanya nini nyumba ya Israeli?

Yahwe anaiambia nyumba ya Israeli kumtafuta na kuishi.

Amos 5:8-9

Je! Yahwe analeta nini juu ya hodari?

Yahwe huleta uharibifu wa ghafla juu ya hodari.

Amos 5:10-11

Nani amefanya chukizo thabiti na chuki?

Hodari huwachukia wale wanaowakosoa, na kumchukia kila mtu asemaye ukweli.

Je! Hodari amefanya nini, kwa kile ambacho Yahwe atakacho waadhibu?

Hodari amemkanyaga chini maskini, ndicho ambacho Yahwe atawaadhibu.

Amos 5:12-13

Je! Mtu mwenye busara hufanya nini katika wakati wa uovu kama huo?

Mtu mwenye busara yuko kimya katika wakati wa uovu kama huo.

Amos 5:14-15

Je! Watu wangefanya nini ili kwamba Yahwe awe nao kweli?

Watu wangetafuta uzuri na sio uovu, ili kwamba Yahwe awe nao kweli.

Amos 5:16-17

Je! Nini kitasikika katika mitaa wakati Yahwe apitapo kati ya watu?

Maomboleza na vilio vitasikia katika mitaa wakati Yahwe apitapo kati ya watu.

Amos 5:18-20

Je! Siku ya Yahwe itakuwaje?

Siku ya Yahwe itakuwa giza na nuru.

Amos 5:21-22

Je! Yahwe anafikiria nini kuhusu mikutano ya dini ya watu?

Yahwe huchukia mikutano ya dini ya watu.

Amos 5:23-24

Je! Yahwe anataka kuona nini kikitiririka kutoka kwa watu?

Yahwe anataka kuona haki na usawa vikitoka kwa watu.

Amos 5:25-26

Je! Watu walitengeneza nini kwa ajili yao?

Watu walitengeneza sanamu kwa ajili yao.

Amos 5:27

Je! Yahwe atawapeleka wapi watu?

Yahwe atawahamisha watu nyuma ya Damaskasi.

Amos 6

Amos 6:1-4

Je! Ni juu ya nani Yahwe anatangaza ole?

Yahwe anatangaza ole juu ya wale wanaostarehe katika Sayuni, na wale waliookoka katika Samaria.

Amos 6:5-6

Je! Hao wanaopokea ole wa Yahwe wanafanya nini na mda wao?

Wale wanaopokea ole wa Yahwe wanatumia mda wao kupumzika, kusherekea, kuimba nyimbo, na kunywa.

Je! Wale wanaopokea ole wa Yahwe hatafanya nini na mda wao?

Wale wanaopokea ole wa Yahwe hawatumii mda wao kuhuzunika juu ya mateso ya Yusufu.

Amos 6:7-10

Je! Wale wanaopokea ole wa Yahwe wanaenda wapi sasa?

Wale wanaopokea ole wa Yahwe sasa wanenda kwenye uhamisho.

Je! Yahwe anachuki ninia kuhusu hawa watu wa Yakobo?

Yahwe huchukia majivuno na ngome za hawa watu wa Yakobo.

Amos 6:11

Je! Nini kitatokea kwa nyumba za hawa watu wa Yakobo?

Nyumba zao zitapigwa nyufa

Amos 6:12-13

Je! hawa watu wa Yakobo wamefanya sahihi na haki?

Hawa watu wa Yakobo wamegeuza usawa kuwa sumu na haki kuwa uchungu.

Amos 6:14

Je! Yahwe ametangaza atafanya nini juu ya nyumba ya Israeli?

Yahwe ametangaza ataliinua taifa juu ya nyumba ya Israeli.

Je! hili taifa litafanya nini juu ya nyumba ya Israeli?

Hili taifa litawatesa nyumba ya Israeli.

Amos 7

Amos 7:1-3

Katika maono yake, je! Amosi aliona nini Yahwe akiumba katika kuchepuka?

Amosi aliona Yahwe akiumba kundi kubwa la nzige katika kuchepua kula mboga mboga za nchi.

Wakati Amosi alipomuuliza Yahwe kumsamehe Yakobo na sio kuleta hili janga juu yao, je! Yahwe alijibu nini?

Yahwe alijibu kwamba hili janga lisingeweza kutokea.

Amos 7:4-6

Katika maono yake, ni kwa namna gani Amosi alimuona Yahwe akiita?

Amosi alimuona Yahwe akiita juu ya moto kuhukumu.

Wakati Amosi alimuuliza Yahwe kumsamehe Yakobo na asilete hili janga juu yao, Je! Yahwe aliji nini?

Yahwe alijibu kwamba hili janga halitatokea tena.

Amos 7:7-8

Katika maono yake, Je! Amosi aliona nini Bwana akituma na kufanya?

Amosi alimuona Bwana amesimama karibu na ukuta pamoja na uzi wa timazi katika mkono wake.

Je! Yahwe alisema nini ilikuwa maana ya uzi wa timazi?

Bwana alisema uzi wa timazi ulimaanisha Israeli haitaharibiwa tena.

Amos 7:9

Je! Yahwe alitangaza nini angefanya kwa Israeli?

Yahwe alisema angepaharibu mahali patakatifu na patakatifu pa Israeli.

Amos 7:10-11

kwa ajili ya nini Amosi alishtakiwa kwa Amazia, kuhani wa Betheli?

Amosi alishtakiwa kufanya njama juu ya Yeroboamu, mfalme wa Israeli.

Je! Amosi alitabiri nini kuhusu Yeroboamu?

Amosi alitabiri kwamba Yeroboamu angekufa kwa upanga.

Amos 7:12-13

Kwenda wapi Amosi aliambiwa kurudi na kutabiri?

Amosi aliambiwa arudi kwenye nchi ya Yuda na kutabiri hapo.

Amos 7:14-15

Je! Kazi ya Amosi ilikuwa ipi kabla Yahwe hajamchukua kuwa nabii wake?

Amosi alikuwa mchungaji wa mifugo na mtunza mikuyu.

Amos 7:16-17

Je! Yahwe alitangaza nini juu ya Amzia, kuhani wa Betheli?

Yahwe alitangaza kwamba Amazia angekufa katika nchi najisi, mke wake atakuwa kahaba, wana wake waume na binti wataanguka, na nchi yake itagawanywa.

Je! Yahwe alitangaza nini angefanya na Israeli?

Yahwe alitangaza angewahamisha Israeli kutoka katika nchi yake.

Amos 8

Amos 8:1-3

Je! Yahwe alimuonyesha nini Amosi?

Yahwe alimuonyesha Amosi kikapu cha matunda ya hai.

Je! Yahwe alisema nini kingekuja kwa ajili ya watu wa Israeli?

Yahwe alisema mwisho umefika kwa watu wake Israeli.

Amos 8:4-6

Je! Ni dhambi zipi watu wa Israeli walizifanya?

Watu wa Israeli waliwakanyaga na kuwaondoa maskini wa nchi.

Kwa nini watu walikuwa na wasiwasi kwa ajili ya mwezi mpya na sabato kuisha?

Watu walikuwa na wasi wasi kwa sababu walitaka kuuza mazao na kudanganya maskini.

Amos 8:7-8

Je! Yahwe alisema hatafanya nini kwa matendo ya mtu yeyote?

Yahwe anasema hatasahau kamwe matendo yoyote ya watu.

Amos 8:9-10

Katika hiyo siku, Yahwe alisema nini angefanya kwenye jua?

Katika siku hiyo, Yahwe anasema angelifanya jua litue mchana.

Je! Watu watavaa nini siku hiyo?

Watu watavaa nguo za gunia siku hiyo.

Amos 8:11-12

Je! Ni njaa gani ambayo Yahwe amesema angeipeleka katika nchi?

Yahwe anasema angepeleka njaa katika nchi kwa kusikia maneno ya Yahwe.

Amos 8:13-14

Katika siku hiyo, ni nani watakaozimia kutokana na kiu?

Katika siku hiyo, wanawali wazuri na wavulana watazimia kutokana na njaa.

Je! Ni nani ambaye Yahwe amesema hatainuka tena?

Wale waapao kwa dhambi ya Samaria hawatainuka tena.

Amos 9

Amos 9:1-2

Je! Nani ataikimbia hukumu ya Bwana wa Israeli?

Hakuna hata mmoja wao atakayeikimbia hukumu ya Bwana.

Amos 9:3-4

Je! Bwana atafanya nini kwa wale ambao watajificha kwenye vilindi vya bahari?

Bwana atamwagiza nyoka kuwang'ata.

Kwa sababu ipi Bwana ataweka mcho yake juu ya Israeli?

Bwana ataweka macho yake juu ya israeli kwa ubaya.

Amos 9:5-6

Je! Watu hufanya nini wakati Yahwe agusapo nchi kuiyeyusha?

Watu waliomboleza wakati Yahwe alipogusa nchi kuiyeyusha.

Amos 9:7-8

Je! Yahwe aliwapandisha Israeli kutoka wapi?

Yahwe aliwapandisha Israeli kutoka nchi ya Misri.

Je! Yahwe aliwapandisha Wafilisti kutoka wapi?

Yahwe aliwaleta Wafilisti kutoka Krete.

Je! Yahwe anasema atawaharibu kabisa watu wa israeli?

Hapana, Yahwe anasema hatawaharibu kabisa watu wa Israeli.

Amos 9:9-10

Je! Watenda dhambi katika Israeli walikuwa wanasema nini, wale ambao Yahwe atawaua?

Watenda dhambi walikuwa wakisema kwamba janga halitawapita.

Amos 9:11-12

Katika siku hiyo, Je! Yahwe anasema atainua nini?

Katika siku hiyo, Yahwe anasema kwamba atainua hema ya Daudi ambayo ilikuwa imeanguka.

Amos 9:13

Je! Pamoja na nini Yahwe anasema milima itadondoka na vilima vitabubujika katika siku zaijazo?

Katika siku zijazo, milima itadondoka na vilima vitabubujika divai tamu.

Amos 9:14-15

Je! Kutoka wapi Yahwe ameahidi kuwarudisha Israeli?

Yahwe ameahidi kuwaleta Israeli kutoka utumwani.

Baada ya Yahwe kuwarudisha Israeli, je! Ni mda gani Israeli watabaki kwa muda gani kwenye nchi?

Baada ya Yahwe kuwarudisha Israeli, Israeli itabaki kwenye nchi milele.