Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Romans

Romans 1

Romans 1:1-3

Kwa jinsi gani Mungu alikua ameahidi injili kabla ya wakati Paulo?

Mungu aliahidi injili zamani kwa manabii wake katika maandiko matakatifu.

Mwana wa Mungu alizaliwa katika ukoo gani kwa jinsi ya mwili?

Mwana wa Mungu alizaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili.

Romans 1:4-7

Kwa tukio gani Yesu Kristo alitangazwa kuwa Mwana wa Mungu?

Yesu Kristo alitangazwa kuwa Mwana wa Mungu kwa ufufuo kutoka kwa wafu.

Paulo alipokea neema na utume kutoka kwa Kristo kwa lengo gani?

Paulo alipokea neema na utume kutokana na utii wa imani kati ya mataifa yote.

Romans 1:8-10

Paulo anamshukuru Mungu, kwa habari ya waumini walioko Rumi kwa sababu zipi?

Paulo anamshukuru Mungu kwa sababu ya imani yao inayohubiriwa katika dunia nzima.

Romans 1:11-12

Kwa nini Paulo anahamu ya kuwaona waumini walioko Rumi?

Paul anatamani kuwaona ili awape baadhi ya vipawa vya kiroho ili waimarishwe.

Romans 1:13-15

Kwa nini Paulo alikuwa ameshindwa kuwatembelea waumini walioko Rumi mpaka sasa?

Paulo alikuwa hajaweza kuwatembelea kwa sababu alikuwa amezuiliwa.

Romans 1:16-17

Paulo anasema injili ni nini?

Paulo anasema injili ni nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu kwa kila mtu aaminie.

Romans 1:18-19

Kitu gani waovu na wasio waadilifu hufanya ingawa yote yanayojulikana juu ya Mungu yako wazi kwao?

waovu na wasio waadilifu hukataa ukweli ingawa yote yanayojulikana juu ya Mungu yako wazi kwao.

Romans 1:20-23

Jinsi gani mambo yasiyoonekana kuhusu Mungu yanaonekana wazi?

Mambo yasiyoonekana kuhusu Mungu yanaonekana wazi kupitia uumbwaji wa vitu.

Ni tabia gani za Mungu zinaonekana wazi?

uwezo wa milele wa Mungu na asili ya Mungu vipo wazi.

Romans 1:24-25

Mungu huwafanya nini kwa wale ambao hubadilisha utukufu wake kwa sanamu za wanaume na wanyama waharibikao?

Mungu huwaacha wafuate tamaa za mioyo yao kwa uchafu, kwa miili yao kufedheheshwa baina yao.

Romans 1:26-27

Ni kwa tamaa zipi mbaya wanawake na wanaume huchoma katika hamu zao?

wanawake huona tamaa juu yao kwa wao, na wanaume huona tamaa juu yao wenyewe.

Romans 1:28

Mungu huwafanya nini wale ambao hawakubali kuwa nae katika ufahamu wao?

Mungu anawapa nia zao za upotovu, kufanya mambo yale ambayo si sahihi.

Romans 1:29-31

Je, wale ambao wanania ya upotovu wana tabia gani?

Wale ambao wana nia zao za upotovu wamejawa na wivu, uuaji, ugomvi, udanganyifu, na nia mbaya.

Romans 1:32

Je, wale walio na nia za upotovu huelewa nini kuhusu matakwa ya Mungu?

Wale walio na nia za upotovu huelewa kwamba wale wanaotenda mambo hayo wamestahili mauti.

Japokuwa wale walio na nia za upotovu huelewa matakwa ya Mungu, bali huwa wanafanya nini?

Wao hufanya mambo yao wasio haki , na huwapongeza wale wanayoyatenda.

Romans 2

Romans 2:1-2

Kwa nini baadhi ya watu wasiwe na udhuru katika hukumu zao?

Baadhi ya watu wasiwe na udhuru katika hukumu zao kwa sababu hayo wanayo yahukumu kwa wengine waopia wanayafanya.

Ni kwa jinsi gani Mungu huwahukumu wale wafanyao matendo yasiyo haki?

Mungu anahukumu kulingana na kweli

Romans 2:3-4

Subira na wema wa Mungu vina manufaa gani?

vinapaswa kuwaongoza watu katika toba.

Romans 2:5-7

Je, wale wenye mioyo migumu na isiyotubu kwa Mungu wanajiwekea akiba gani ya wenyewe?

Wale walio mioyo migumu na isiyotubu hujihifadhia wenyewe ghadhabu kwa siku ile ya hukumu ya uadilifu ya Mungu.

Romans 2:8-9

Je wale wanaotii isiyo haki hupata nini?

hupokea ghadhabu, hasira kali, na dhiki.

Romans 2:10-12

Ni kwa jinsi gani Mungu haoneshi upendeleo kati ya Myahudi na Myunani katika hukumu yake?

Mungu hana upendeleo kwa sababu wote watendao dhambi wataangamia, Myahudi kwa Myunani.

Romans 2:13-20

Nani anahaki mbele za Mungu?

watendaji wa sheria ndo wana haki mbele ya Mungu.

Ni jinsi gani watu wa mataifa huonesha ya kuwa wanayo sheria juu yao?

hufanya hivyo kwa wafanyapo kwa asili matendo ya sheria.

Romans 2:21-22

Paulo anawapa changamoto gani Wayahudi ambao wanakaa katika sheria na kuwafundisha wengine?

Paulo anawapa changamoto kwamba kama wakiwafundisha wengine sheria, wanapaswa wajifundishe wenyewe pia.

Paulo anataja dhambi gani walimu wa sheria za Kiyahudi wanapaswa kuacha kufanya?

Paulo anataja dhambi za wizi, uzinzi, na wizi wa mahekalu.

Romans 2:23-24

Kwa nini jina la Mungu hufedheheshwa kati ya watu wa mataifa kwa sababu ya walimu Wayahudi wa Sheria?

jina la Mungu linafedheheshwa kwa sababu walimu wa sheria za Kiyahudi wanazivunja sheria.

Romans 2:25-27

Paulo asema nini mtu wa kiyahudi alietairiwa anaweza kuwa hajatairiwa?

Paulo anasema kwamba mtu wa Kiyahudi alietairiwa anaweza awe hajatairiwa kama mtu huyo ni mkiukaji wa sheria.

Romans 2:28-29

Nani Paulo anasema ni Myahudi wa kweli?

Paulo anasema kwamba Myahudi wa kweli ni Myahudi wa ndani, mwenye tohara ya moyo.

Romans 3

Romans 3:1-2

Faida ya kwanza ya Myahudi ni ipi?

Faida ya kwanza ya Wayahudi ni kwamba walikabidhiwa ufunuo kutoka kwa Mungu.

Romans 3:3-4

Japokuwa kila mtu ni mwongo, Mungu yeye yukoje?

Mungu yeye anabaki kuwa mkweli

Romans 3:5-6

Kwa sababu Mungu ni mwenye haki, yeye anaweza kufanya nini?

Kwa sababu Mungu ni mwenye haki, yeye ni mwenye uwezo wa kuhukumu ulimwengu.

Romans 3:7-8

Ni kitu gani huwapata wale ambao husema, "Acha tufanye maovu, ili uzuri uje?

Hukumu huja juu ya wote wasemao hivyo.

Romans 3:9-10

Imeandikwa nini katika maandiko kuhusu haki ya wote, Wayahudi kwa Wayunani?

Imeandikwa kwamba hakuna mwenye haki hata mmoja.

Romans 3:11-18

Kwa mujibu wa yale yaliyoandikwa, ni nani anaelewa na kumtafuta Mungu?

Kwa mujibu wa yale yaliyoandikwa, hakuna anayelewa na hakuna anayemtafuta Mungu.

Romans 3:19-20

Ni nani atakayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria?

Hakuna atakayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria.

Ni kitu gani huja kwa njia ya sheria?

Ujuzi wa dhambi unakuja kwa njia ya sheria

Romans 3:21-22

Ni kwa ushahidi gani haki pasipo sheria sasa imewekwa wazi?

Kwa ushahidi wa Sheria na Manabii haki pasipo sheria imefunuliwa.

Romans 3:23-24

Ni jinsi gani mtu huhesabiwa haki mbele za Mungu?

Mtu huhesabiwa haki mbele za Mungu bure kwa neema kupitia ukombozi ulio katika Kristo Yesu.

Romans 3:25-26

Kwa kusudi gani Mungu alimtoa Kristo Yesu?

Mungu alimtoa Kristo Yesu kuwa patanisho kwa imani katika damu yake.

Mungu alionesha nini kupitia yote yaliyotokea kupitia Yesu Kristo?

Mungu alionesha kuwa ni yeye peke yake anayemhesabia mtu haki kwa njia ya imani katika Yesu.

Romans 3:27-28

Matendo ya sheria yana nafasi gani katika kuhesabiwa haki?

Mtu anahesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.

Romans 3:29-30

Ni kwa jinsi gani Mungu humhesabia haki Myahudi aliyetahiriwa na mtu wa Mataifa asiyetahiriwa?

Mungu huwahesabia haki wote kwa njia ya imani.

Romans 3:31

Tufanye nini juu ya sheria tukiwa na imani?

Tutimize sheria kwa imani.

Romans 4

Romans 4:1-3

Ni kitu gani kingemfanya Abrahamu ajivune?

Abrahamu angekuwa na sababu ya kujivuna kama angehesabiwa haki kwa sababu ya matendo yake.

Romans 4:4-5

Ni aina gani ya watu ambao Mungu huwahesabia haki?

Mungu huwahesabia haki watu waovu

Romans 4:6-8

Kwa mujibu wa Daudi, ni kwa njia gani mtu hubarikiwa na Mungu?

Kwa mujibu wa Daudi, heri ni mtu ambaye dhambi zake zimesamehewa na ambaye dhambi zake hazikuhesabiwa na Bwana.

Romans 4:9-10

Ilikuwa imani ya Ibrahimu kuhesabiwa kuwa ni haki kabla au baada ya kutahiriwa?

Imani ya Ibrahimu ilihesabiwa kuwa ni haki kabla ya kutahiriwa.

Romans 4:11-12

Ibrahimu ni baba wa makundi gani ya watu?

Ibrahimu ni baba wa wote wanaoamini, wote wasiotahiriwa na waliotahiriwa.

Romans 4:13-15

Ni ahadi gani ilitolewa kwa Abrahamu na kizazi chake kupitia haki ya imani?

Abrahamu na kizazi chake waliahidiwa kwamba wangekuwa warithi wa dunia.

Romans 4:16-17

Kwa sababu gani ahadi ilitolewa kwa imani?

Ahadi imetolewa kwa imani ili kwamba iwe ni kwa neema, na hivyo kuwa ni uhakika.

Romans 4:18-19

Ni mazingira gani ya nje yalifanya iwe vigumu kwa Abrahamu kuamini ahadi ya Mungu kwamba atakuwa baba wa mataifa mengi?

Mungu alipompa Abrahamu ahadi, Abrahamu alikuwa na umri karibu miaka mia moja na tumbo la Sara lilikuwa haliwezi kuzaa tena.

Jinsi gani Abrahamu alipokea ahadi ya Mungu hata kwa mazingira haya ya nje?

Abrahamu kwa ujasiri alimwamini Mungu na hakusita katika kutoamini.

Romans 4:20-22

Jinsi gani Abrahamu alipokea ahadi ya Mungu hata pamoja na mazingira haya ya nje?

Abrahamu kwa ujasiri alimwamini Mungu na hakusita kuamini.

Romans 4:23-25

Habari za Abrahamu ziliandikwa kwa ajili ya nani?

Habari za Abrahamu ziliandikwa kwa manufaa yake, na kwa faida yetu.

Tunaamini kwamba amefanya nini kwa ajili yetu?

Tunaamini kuwa Mungu alimfufua Yesu kutoka katika wafu, ambaye aliinuliwa kwa sababu ya dhambi zetu na upatanisho wetu.

Romans 5

Romans 5:1-2

Je waamini wana nini kutokana na kuhesabiwa haki kwa imani?

Kwa sababau wamehesabiwa haki, waamini wana amani na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.

Romans 5:3-7

Je ni mambo gani matatu ambayo yanaletwa na mateso?

Mateso huleta uvumilivu, kukubalika, na ujasiri.

Romans 5:8-9

Je ni jinsi gani Mungu hutuhakikishia upendo kwetu?

Mungu hutuhakikishia upendo kwetu, kwa sababu wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.

Romans 5:10-11

Je ni uhusiano wa namna gani wasio amini wanao pamoja na Mungu kabla hawajapatanishwa na Mungu kwa njia ya Yesu?

Wasio amini ni maadui wa Mungu kabla hawaja patanishwa na Mungu kwa njia ya Yesu.

Romans 5:12-13

Je nini kilitokea kwa sababu ya dhambi ya mtu mmoja?

Kwa sababu ya dhambi ya mtu mmoja, dhambi iliingia duniani,kifo kiliingia kwa sababu ya dhambi, na kifo kikasambaa kwa watu wote.

Romans 5:14-15

Je ni mtu gani ambaye kupitia yeye dhambi iliingia duniani.

Adam alikuwa ni mtu ambaye kupitia yeye dhambi iliingia duniani.

Romans 5:16-17

Nini kilitokea kwa sababu ya dhambi ya Adamu na nini kilitokea kutoka kwa zawadi ya bure ya Mungu?

Hukumu ya hukumu ilitokana na dhambi ya Adam, lakini haki ilipatikana kutoka kwa zawadi ya bure ya Mungu.

Romans 5:18-19

Ni kitu gani waatu wengi walifanyiwa kupitia uasi wa Adam, na ni kitu gani watu wengi watafanyiwa kupitia utii wa Kristo?

Wengi walifanywa kuwa wenye dhambi kupitia uasi wa Adam, na wengi watafanywa kuwa wenye haki kupitia utii wa Kristo.

Romans 5:20-21

Kwa nini sheria iliingia?

Sheria iliingia ili kwamba makosa liongezeke.

Nini kilizidi zaidi kuliko makosa?

Neema ya Mungu ilizidi zaidi kuliko makosa.

Romans 6

Romans 6:1-3

Je waamini wanapaswa kuendelea kufanya dhambi ili kwamba neema izidi?

La hasha! isifanyike hivyo.

Watu waliobatizwa ndani ya Kristo walibatizwa katika nini?

Walibatizwa katika mauti ya Kristo

Romans 6:4-5

Je waamini wafanye nini ikiwa Kristo alifufuliwa kutoka wafu?

Waamini wanapswa kutembea katika upya wa maisha.

Ni kwa njia zipi mbili waamini wameunganishwa na Kristo kupitia ubatizo?

Waumini wameunganishwa na Kristo katika mauti na ufufuo.

Romans 6:6-7

Je nini kilifanyika kwetu ili kwamba tusiwe tena watumwa wa dhambi?

Utu wetu wa zamani ulisulibiwa pamoja na kristo, ili kwamba tusiwe tena watumwa wa dhambi.

Romans 6:8-9

Tunajuaje kwamba mauti haimtawali Kristo tena?

Tunajua hivyo kwa sababu Kristo alifufuliwa kutoka katika wafu.

Romans 6:10-11

Je ni mara ngapi Kristo alikufa kwa dhambi na alikufa kwa ajili ya watu wangapi?

Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi mara moja kwa ajili ya wote.

Ni namna gani mwamini anapaswa kufikiri juu yake mwenyewe kuhusiana na dhambi?

Mwamini anapaswa kutambua mwenyewe kwamba ni mfu kwa dhambi.

Je ni kwa ajili ya nani mwamini huishi maisha yake?

Mwamini huishi maisha yake kwa ajili ya Mungu.

Romans 6:12-14

Mwamini anapaswa kuvitoa viungo vyake vya mwili kwa nani, na kwa lengo lipi?

Anapaswa kuvitoa viungo vyake kwa Mungu kama vyombo vya haki.

Aliye amini anaishi chini ya nini ambacho pia humwezesha kuitawala dhambi?

Aliye amini anaishi chini ya neema ambayo humwezesha kuitawaa dhambi.

Romans 6:15-18

Mwisho wa mtu anayeitumikia dhambi ni nini?

Mwisho wake ni mauti.

Romans 6:19-21

Mwisho wa mtu anayeitumikia dhambi ni nini?

Mwisho wake ni mauti.

Romans 6:22-23

Watumwa wa Mungu wana dhawabu yao kwa ajili gani?

Watumwa wa Mungu wana dhawabu yao kwa ajili ya utakaso.

Mshahara wa dhambi ni nini?

Mshahara wa dhambi ni mauti

Zawadi ya bure ya Mungu ni nini?

Ni uzima wa milele.

Romans 7

Romans 7:1

Ni kwa muda gani sheria humtawala mtu?

Sheria humtawala mtu kwa kipindi chote anachoishi.

Romans 7:2-3

Ni kwa muda gani mwanamke aliyeolewa hufungwa katika sheria ya ndoa?

Mwanamke aliyeolewa amefungwa na sheria ya mpaka mme wake akifariki.

Mwanamke anaweza kufanya nini akisha kuwa huru dhidi ya kifungo cha ndoa?

Anaweza kuolewa na mwanamme mwingine.

Romans 7:4-6

Ni kwa jinsi gani walioamini wamefanywa kuwa wafu kwa sheria?

Walioamini wamefanywa kuwa wafu kwa sheria kwa njia ya mwili wa Kristo.

Baada ya kufanywa kuwa wafu kwa sheria, walioamini wanaweza kufanya nini?

Baada ya kufanywa wafu kwa sheria, Walioamini wanaweza kuunganishwa na Kristo.

Romans 7:7-10

Ni jambo gani ambalo sheria hufanya?

Sheria hufanya dhambi ijulikane.

Je sheria ni dhambi au takatifu?

Sheria ni takatifu, na amri ni takatifu, ya haki, na njema.

Romans 7:11-12

Je sheria ni takatifu?

Ndiyo, sheria ni takatifu, na amri ni takatifu, ya haki na nzuri.

Romans 7:13-14

Paulo anasema dhambi inafanya nini kwake?

Paulo anasema kwamba, dhambi kupitia sheria, inaleta mauti kwake.

Romans 7:15-16

Nini kinamfanya Paulo asikubaliane na sheria ya kwamba ni njema?

Ni pale Paulo anafanya kile ambacho hataki kukifanya, ndipo hukubaliana ya kwamba sheria ni njema.

Romans 7:17-18

Ni nani afanyae mambo ambayo Paulo anafanya, lakini hapendi kuyafanya?

Dhambi iishiyo ndani ya Paulo hufanya mambo ambayo hapendi kuyafanya.

Ni kitu gani kinaishi ndani ya mwili wa Paulo?

Hakuna kilicho chema kinaishi ndani ya mwili wa Paulo.

Romans 7:19-21

Ni kanuni ipi ambayo Paulo anaona inatenda kazi ndani yake?

Paulo anaona ya kwamba anatamani kufanya mema, lakini uovu upo ndani yake.

Romans 7:22-23

Utu wa ndani wa Paulo una mtazamo gani juu ya sheria ya Mungu?

Utu wa ndani wa Paulo unafurahia katika sheria ya Mungu.

Ni kanuni gani Paulo anaiona katika viungo vyake vya mwili?

Paulo anaona katika viungo vyake vya mwili kuwa kanuni ya dhambi inamlemea.

Romans 7:24-25

Ni nani atakayemwokoa Paulo kutoka katika mwili wake wa mauti?

Paulo anamshukuru Mungu kwa ajili ukombozi wake kupitia Yesu Kristo.

Romans 8

Romans 8:1-2

Ni kitu gani kimemweka Paulo kuwa huru dhidi ya dhambi na mauti?

Roho wa uzima aliye katika Kristo yesu ndiye alimweka Paulo kuwa huru dhidi ya dhambi na mauti.

Romans 8:3-5

Kwanini sheria haikuwa na uwezo wa kuwaweka watu huru kutokana na kanuni ya dhambi na kifo?

Sheria haiukuwa na uwezo kwa sababu ilikuwa dhaifu katika mwili.

Wote wanaoenenda kulingana na Roho hufuata nini?

Huwa makini na kufuata mambo ya Roho.

Romans 8:6-8

Uhusiano wa mwili na Mungu na sheria ni nini?

Mwili hukaidi mambo ya Mungu na hautii sheria.

Romans 8:9-10

Ni kitu gani watu ambao sio wa Mungu wanakikosa?

Watu ambao sio wa Mungu hawana Roho wa Kristo

Romans 8:11-13

Ni kwa jinsi gani Mungu huupa uhai mwili wa mauti wa aliyeamini?

Mungu huupa uhai mwili wa mauti wa aliyeamini kwa njia ya Roho, anayeishi ndani ya muumini.

Romans 8:14-15

Ni jinsi gani wana wa Mungu wanaongozwa kuishi?

Wana wa Mungu wanaongozwa na Roho wa Mungu.

Romans 8:16-17

Kama watoto wa Mungu, ni faida gani nyingine ambazo walioamini hupokea katika familia ya Mungu?

Katika familia ya Mungu, walio amini pia ni warithi pamoja na Kristo.

Romans 8:18-19

Kwanini walio amini wakati huu wavumilie mateso ya wakati huu?

Ili kwamba walio amini watukuzwe pamoja na Kristo wakati wana wa Mungu watakapodhihiriswa.

Romans 8:20-22

Kwa kipindi hiki, uumbaji upo chini ya utumwa wa namna gani?

Uumbaji upo katika utumwa wa uharibifu

Uumbaji utaokolewa katika nini?

Uumbaji utaokolewa katika uhuru wa utukufu wa wana wa Mungu.

Romans 8:23-25

Jinsi gani walioamini watangoja ukombozi wa mwili?

Walioamini wanapaswa kuongoja ukombozi wa mwili kwa kutumaini.

Romans 8:26-27

Ni nini Roho mwenyewe hufanya kuwasaidia watakatifu udhaifu wao?

Roho mwenyewe huomba kwa kuugua kwa niaba ya watakatifu kulingana na mapenzi ya Mungu.

Romans 8:28-30

Ni jinsi gani Mungu hufanya mambo yote pamoja na wale wampendao Mungu na walioitwa kulingana na kusudi lake?

Mungu hufanya mambo yote pamoja kwa wema kwa ajili ya wote wampendao Mungu na walioitwa kulingana na kusudi lake.

Romans 8:31-32

Wali amini wanajuaje kuwa Mungu atawapa vitu vyote bure?

Kwa sababu Mungu alimtoa bure mwana wake wa pekee kwa niaba ya wote walio amini.

Romans 8:33-36

Yesu Kristo anafanya nini katika mkono wa kuume wa Mungu?

Kristo Yesu anawaombea watakatifu katika mkono wa kuume wa Mungu.

Romans 8:37-39

Jinsi gani walioamini ni zaidi ya washindi juu ya dhiki, mateso, au hata kifo?

Walioamini ni zaidi ya washindi kupitia yeye aliyewapenda.

Romans 9

Romans 9:1-2

Kwanini Paulo alikuwa na masikitiko makubwa pamoja na maumivu yasiyo koma katika moyo wake?

Paulo alikuwa na masikitiko pamoja na maumivu kwa ajili ya ndugu zake kwa mujibu wa mwili, waisrael.

Romans 9:3-5

Waisraeli wana kitu gani katika historia yao?

Waisraeli wameasiliwa, wana utukufu, wana agano, wana sheria, wana ibada ya Mungu, na ahadi.

Romans 9:6-7

Ni kitu gani Paulo anasema si cha kweli kuhusu kila mmoja katika Israel, na wote ambao ni uzao wa Abrahamu?

Paulo anasema siyo kila mtu katika Israeli ni Muisraeli halisi na siyo uzao wote wa Abrahamu ni watoto wake halisi.

Romans 9:8-9

Je ni watu gani wasiohesabika kama wana wa Mungu?

Wana wa mwili hawahesabiki kama watoto wa Mungu.

Nii akina nani wanahesabika kama watoto wa Mungu?

Wana wa ahadi wanahesabika kama watoto wa Mungu.

Romans 9:10-13

Ni sababu gani iliyo nyuma ya kauli iliyotolewa kwa Rebeka, "Mkubwa atamtumikia mdogo," kabla ya watoto wake hawajazaliwa?

Kusudi la Mungu kuli ngana na uchaguzi ilikuwa ni sababu ya kauli iliyotolewa kwa Rebeca.

Romans 9:14-18

Nini ilikuwa sababu ya zawadi za Mungu za rehema na huruma?

Sababu iliyokuwa nyuma ya zawadi za Mungu ambazo ni rehema na huruma ilikuwa ni uchaguzi wa Mungu.

Romans 9:19-21

Majibu ya Paulo ni yapi dhidi ya wote ambao wangehoji haki ya mungu kwa sababu anaona makosa kwa wanadamu?

Paulo alisema, "Ninyi ni akina nani mpaka mumhoji Mungu?"

Romans 9:22-26

Je Mungu alifanya nini kwa wale walioandaliwa kwa ajili ya uharibifu?

Mungu aliwavumilia kwa subira kuu wale walioandaliwa kwa ajili ya uharibifu.

Romans 9:27-29

Je ni wangapi wataokolewa kutoka kwa wana wote wa Israeli?

Kutoka kwa wana wote wa Israeli, aliyesalia ataokolewa.

Romans 9:30-31

Ni kwa jinsi gani watu wa mataifa ambao walikuwa hawatafuti haki, waliipata?

Watu wa mataifa waliipata haki kutokana na imani

Romans 9:32-33

Kwa nini Israeli ingawa walitafuta sheria ya haki, hawakuifikia?

Israeli hawakuifikia haki kwa sababu waliitafuta kwa njia ya matendo, na si kwa imani

Je Waisrael walijikwaa kwa kitu gani?

Waisrael walijikwaa katika jiwe la kujikwaa na katika mwamba wa makosa.

Romans 10

Romans 10:1-3

Je haja ya Paulo kwa ndugu zake Waisrael ni nini?

Haja ya Paulo kwa Waisraeli ni wokovu.

Waisraeli wanalenga kujijengea nini?

Waisraeli wanataka kujijengea haki yao wenyewe.

Romans 10:4-7

Je Kristo amefanya nini kwa habari ya sheria?

Kristo ni utimilifu wa sheria kwa ajili ya haki kwa kila mtu aaminiye.

Romans 10:8-10

Je neno la imani ambalo Paulo anahubiri liko wapi?

Neno la imani liko karibu, katika kinywa na katika moyo.

Romans 10:11-13

Kila mtu afanyae nini ataokolewa?

Kila mtu aliitiaye jina la Bwana ataokolewa.

Romans 10:14-15

Je Paulo anasema ni nini mfululizo wa hatua ambazo zinaleta habari njema kwa mtu, ili aweze kuliitia jina la Bwana?

Paulo anasema kuwa, kwanza muhubiri anapelekwa, na habari njema zinasikika na kuaminiwa, ili kwamba mtu aweze kuliitia jina la Bwana.

Romans 10:16-17

Ni kitu gani ambacho kwa kukisikia huleta imani?

Neno la Kristo huleta imani

Romans 10:18

Je Israeli alisikia injili?

Ndiyo, Israeli alisikia injili.

Romans 10:19

Ni kwa namna gani Mungu alisema atachochea wivu kwa Israeli?

Mungu alisema angeweza kuchochea wivu kwa Israeli kwa kupatikana kwa wale ambao hawakumuomba.

Romans 10:20-21

Mungu alipata nini alipowaita Israeli?

Mungu alipomwita Isaraeli, alikutana na watu wasiotii.

Romans 11

Romans 11:1-3

Je Mungu aliwakataa Waisraeli?

Hapana

Romans 11:4-5

Je Paulo anasema kuna waaminifu katika Waisraeli wamebaki, na kama wapo, ni kwa jinsi gani wamesalia?

Paulo anasema kuna masalia waliobakizwa kwa uchaguzi wa neema.

Romans 11:6-10

Ni akina nani katika Israeli walipata wokovu, na nini kilitokea kwa wengine?

Waliochaguliwa katika Israeli walipata wokovu, na wengine walipewa ugumu wa moyo.

Romans 11:11-12

Ni jambo gani jema litatokea ikiwa Waisraeli wakikataa kuipokea injili?

Wokovu utakuja juu ya Mataifa.

Ni madhara gani yatatokea baada ya Mataifa kupata wokovu wa Waisraeli?

Wokovu wa Mataifa utawafanya Waisraeli wawe na wivi.

Romans 11:13-16

Kwenye maelezo ya Paulo juu ya mti wa mzeituni na matawi ya porini, nani ni mzizi na nani ni matawi ya porini?

Mzizi ni Israeli, na matawi ya porini ni Mataifa.

Romans 11:17-18

Kwenye maelezo ya Paulo juu ya mti wa mzeituni na matawi ya porini, nani ni mzizi na nani ni matawi ya porini?

Mzizi ni Israeli, na matawi ya porini ni Mataifa.

Romans 11:19-21

Ni onyo gani Paulo anayapa matawi yasiyo ya asili?

Paulo anaonya kwamba kama Mungu hakuyabakiza matawi ya asili, vivyo hivyo hatayaacha matawi yasiyo ya asili.

Romans 11:22

Ni onyo gani Paulo anawapa matawi ya porini.

Paulo anayaonya matawi ya porini kuwa kama Mungu hakuwaonea huruma matawi ya asili pia hatawaacha matawi ya porini ikiwa hawataamini.

Romans 11:23-24

Mungu atafanya nini kwa matawi ya asili kama yasipoendelea katika kutokuamini kwao?

Mungu atawapandikizia kwenye mti wa mzeitumi wenye matawi ya asili ikiwa hawataendelea katika kutokuamini kwao.

Romans 11:25-27

Ni kwa mda gani ubaguzi mgumu wa Israeli utadumu?

Ubaguzi mgumu wa Israeli utaendelea mpaka ukamilifu wa Mataifa utakapokuja.

Romans 11:28-29

Pamoja na kuasi kwao, kwa nini Waisraeli waliendelea kupendwa na Mungu?

Waisraeli waliendelea kupendwa na Mungu kwa sababu ya mababu, na kwa sababu wito wa Mungu haubadiliki.

Romans 11:30-32

Ni nini ambacho wote Wayahudi na Mataifa walionyeshwa wafanye na Mungu?

Wote Wayahudi na Mataifa walionyeshwa

Ni nini Mungu aliwaonyesha wale wasiomtii?

Mungu aliwaonyesha rehema kwa sasiomtii, wote wWayahudi na Mataifa.

Romans 11:33-34

Ni nani anaweza kutafuta hukumu ya Mungu na kumpa ushauri?

Hamna mtu anayeweza kutafuta hukumu ya Mungu na kumpa ushauri.

Romans 11:35-36

Kwa njia zipi tatu kwamba vitu vyote vina ushirika na Mungu?

Vitu vyote hutoka kwa Mungu, katika Mungu, na kwa ajili ya Mungu.

Romans 12

Romans 12:1-2

Ipi ni huduma ya kiroho ya Mungu kwa mwamini?

Huduma ya kiroho ya mwamini ni kujitia mwenyewe kuwa dhabihu iliyohai kwa Mungu.

Akili iliyogeuzwa inamsaidia aliye amini kufanya nini?

Akili iliyogeuzwa inamsaidia aliye amini kujua kilicho chema, kinachokubalika, na mapenzi ya Mungu yaliyo kamili.

Romans 12:3

Kwa jinsi gani mwamini hapaswi kufikiri juu yake mwenyewe?

Mwamini hapaswi kufikiri zaidi sana kuliko anavyopaswa kufikiri.

Romans 12:4-5

Ni kwa jinsi gani waamini wengi wanahusiana wenyewe kwa wenyewe ndani ya Kristo.

Waamini wengi ni mwili mmoja ndani ya Kristo na mmoja mmoja kwa kila mmoja.

Romans 12:6-8

Ni kitu gani ambacho kila mwamini anatakiwa kufanya kutokana na kipawa alichopewa na Mungu?

Kila mwamini anapaswa kufanyia kazi kipawa alichopewa kwa kadri ya kiwango cha imani yake.

Romans 12:9-10

Ni jinsi gani walio amini wanapaswa kuchukuliana?

Walio amini wanapaswa kupendana na kuheshimiana.

Romans 12:11-13

Ni jinsi gani walio amini wanapaswa kuhusika katika mahitaji ya watakatifu?

walio amini wanapaswa kushiriki katika mahitaji ya watakatifu.

Romans 12:14-16

Ni kwa jinsi gani waamini wanapaswa kufanya juu ya wale wanaowatesa?

Waamini wanatakiwa kuwabariki na sio kuwalaani wale wanaowatesa.

Romans 12:17-18

Walio amini wanapaswa kutafuta nini kwa hali na mali na watu wote?

Walio amini wanapaswa kutafuta amani na watu wote.

Romans 12:19-21

Kwa nini waamini waliambiwa wasijilipize kisasi wenyewe?

Waamini hawatakiwi kujilipiza wenyewe maana kisasi ni cha Bwana.

Ni kwa jinsi gani walio amini wanapaswa kuushinda uovu?

Wanapaswa kuushinda uovu kwa wema.

Romans 13

Romans 13:1-2

Je ni kutoka wapi wenye mamlaka ya duniani hupata mamlaka?

Mamlaka ya duniani yanatolewa na Mungu, na wanapata mamlaka kutoka kwa Mungu.

Romans 13:3-5

Je Paulo anawambia nini waamini wafanye ili wasiweze kuogopa mamlaka inayotawala?

Paulo anawambia waamini wafanye mema ili wasiogope mamlaka itawalayo.

Romans 13:6-7

Je ni mamlaka gani ambayo Mungu ameitoa kwa watawala kuhusiana na fedha?

Mungu amewapatia watawala mamlaka kuhitaji malipo ya kodi.

Romans 13:8-10

Je ni jambo gani moja ambalo Paulo anasema lazima wadaiwe na wengine?

Paulo anasema waamini lazima wadaiwe upendo na waamini wengine.

Je ni kwa namna gani waamini wanatimiliza sheria?

Mwamini hutimiza sheria kwa kumpenda jirani yake.

Romans 13:11-12

Ni kitu ambacho Paulo anasema walio amini wanapaswa kukiweka kando, na kuvaa kitu gani?

Waweke kando matendo ya giza, na kuvaa silaha za nuruni

Romans 13:13-14

Je ni katika shuguli gani waamini hawapaswi kutembea?

Waamini hawapaswi kutembea katika sherehe za kidunia, ulevi, zinaa, Tamaa izidiyo, ugomvi, au wivu.

Romans 14

Romans 14:1-2

Ni chakula cha aina gani ambacho wenye imani imara hula, na mtu mwenye imani haba hula?

Mtu aliye imara katika imani anakula kila kitu, lakini mtu asiye na imani imara anakula mboga za majani tu.

Romans 14:3-4

Je ni mtazamo gani ambao waamini wanapaswa kuwa nao juu ya wale wanaotofautiana katika kile wanachokula?

Waamini wanaotofautioana juu ya kile wanachokula hawapaswi kudharau au kuhukumiana.

Je ni nani amempokea yule alaye chochote na yule ambaye anakula mboga za majani tu?

Mungu amewapokea wote yule anayekula chochotr na yule anayekula mboga za majani pekeyake.

Romans 14:5-6

Je ni mambo gani mengine ambayo Paulo anayataja kama mambo ambayo ni ya binafsi?

Paulo anataja mambo kama vile siku moja kuwa ni bora kuliko siku zingine au anasema siku zote zina uthamani ulio sawa

Romans 14:7-9

Je ni kwa ajili gani waamini wanaisha na kufa?

Waamini wanaishi na kufa kwa ajili ya Bwana.

Romans 14:10-11

Je ni mahali gani ambapo waamini wote mwishowe watasimama?

Waamini wote mwishowe watasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu, wakitoa hesabu yao wenyewe kwa Mungu.

Romans 14:12-13

Je ni mahali gani ambapo mwishowe waamini wote watasimama, na watakuwa wanafanya nini pale?

Waamini wote mwishowe watasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu, wakitoa hesabu yao wenyewe kwa Mungu.

Romans 14:14-15

Paulo ameshawishika katika Bwana Yesu ya kuwa ni chakula gani ambacho si safi?

Paulo ameshawishika kuwa hakuna chakula ambacho si safi.

Romans 14:16-19

Ufalme wa mbinguni ni kwa ajili ya nini?

Ufalme wa mbinguni ni kwa ajili ya haki, amani, na furaha katika Roho Mtakatifu.

Romans 14:20-21

Paulo anasema mtu afanye nini mbele ya mwenzake asiyekula nyama au kunywa mvinyo?

Paulo anasema ni vyema ndugu huyo asile nyama wala kunywa mvinyo mbele ya ndugu huyo.

Romans 14:22-23

Nini matokeo ya mtu afanyae mambo pasipo imani?

Matendo yote yasiyotokana na imani ni dhambi.

Romans 15

Romans 15:1-2

Ni mwenendo upi ambao waumini wenye imani imara wauonyeshe mbele ya waumini wenye imani dhaifu?

Waumini wenye imani imara wanaweza kuchukuliana na wenye imani dhaifu ili kujengana wao kwa wao.

Romans 15:3-4

Paulo anatumia mfano wa nani ambaye hakuishi kwa kujipendeza mwenyewe, bali alitumikia wengine?

Kristo hakuishi maisha ya kujipendeza mwenyewe , bali aliwatumikia wengine.

Romans 15:5-9

Paulo anatamani kuona nini kwa waumini kupitia uvumilivu wao na kutiana moyo kwa kila mmoja wao?

Paulo anatamani kwamba waumini wawe na nia moja kwa kila mmoja.

Romans 15:10-12

Maandiko yanasema nini kuhusu mataifa watakachofanya kwasababu ya rehema ya Mungu kwao?

Maandiko yanasema mataifa watafurahi na kusifu kwa Bwana, wakiwa na tumaini kwake.

Romans 15:13-14

Paulo anasema nini kwa waumini watakachofanya kwa nguvu za Roho Mtakatifu?

Waumini watajazwa na furaha na amani, na watabaki katika tumaini.

Romans 15:15-16

Mungu alimpa Paulo kipawa gani, ambacho pia ndio utumishi wake?

Utumishi wa Paulo ni kuwa mtumishi wa Kristo Yesu aliyetumwa kwa watu wa Mataifa.

Romans 15:17-19

Ni kwa njia zipi Kristo amemtumia Paulo kuleta utii kwa watu wa Mataifa?

Kristo amemtumia Paulo kwa Neno na matendo, kwa nguvu ya ishara na miujiza, na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Romans 15:20-23

Mahali gani Paulo anatamani kuitangaza injili?

Paulo anatamani kuitangaza injili mahali Kristo hajajulikana jina lake.

Romans 15:24-25

Paulo anatazamia kwenda wapi ambapo pia itamruhusu kwenda Rumi?

Paulo anataraji kwenda Hispania ambako pia patamfanya kwenda Rumi.

Kwa nini Paulo anaenda Yerusalemu?

Paulo anaenda Yerusalemu kuwatumikia walio amini huko.

Romans 15:26-29

Kwa nini Paulo anasema ya kuwa waumini wa Mataifa wanawadai vitu waumini wa Kiyahudi?

Kwa sababu waumini wa Mataifa wameshiriki katika vitu vya rohoni vya waumini wa Kiyahudi.

Romans 15:30-33

Paulo anatarajia kupelekwa kwa nani?

Paulo anatamani kupelekwa kwa waasi wote wasiotii kule Yudea.

Romans 16

Romans 16:1-2

Dada Fibi alifanyika nini kwa Paulo?

Dada Fibi alikuwa mhudumu wa Paulo na kwa wengine wengi?

Romans 16:3-5

Priska na Akila walimfanyia nini Paulo hapo awali?

Walihatarisha maisha yao kwa ajili ya Paulo

Ni sehemu gani walio amini kule Rumi wanakutana?

Wanakutana nyumbani mwa Priska na Akila.

Romans 16:6-14

Ni hali gani ambayo Androniko na Yunia walishiriki pamoja na Paulo hapo zamani?

Walikuwa wafungwa pamoja na Paulo

Romans 16:15-16

Walio amini wanasalimianaje?

Kwa busu takatifu

Romans 16:17-18

Baadhi yao wanafanya nini ambacho husababisha mgawanyiko na vipingamizi?

Wengine wanaenenda kinyume na mafundisho ya waliyojifunza, wakidanganya mioyo ya wasio na hatia.

Paulo anawaambia nini cha kufanya kwa wale wanaosababisha mgawangiko na vipingamizi?

Paulo anawaambia waumini kugeuka kutoka kwao wanaosababisha mgawanyiko na vipingamizi.

Romans 16:19-20

Paulo anawataka waumini wawe na mtazamo gani juu ya mema na maovu?

Paulo anawataka waumini wawe na hekima kwa mema na kutokuwa na hatia kwa uovu.

Je Mungu wa amani anaenda kufanya nini hivi karibuni?

Mungu wa amani atamkanyaga Shetani chini ya miguu ya walio amini.

Romans 16:21-22

Ni nani kweli aliyeandika waraka huu?

Tertio ndiye aliyeandika waraka huu.

Romans 16:23-24

Kazi ya muumini Erasto ilikuwa nini?

Erasto alikuwa mtunza hazina wa Mji.

Romans 16:25-27

Ufunuo upi wa siri iliyokuwa imefichwa muda mrefu ambayo Paulo anaihubiri?

Paulo sasa anaihubiri siri ya ufunuo wa injili wa Yesu Kristo.

Paulo anahubiri kwa lengo gani?

Paulo anahubiri ili kuleta utii kati ya watu wa Mataifa.