Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

2 Corinthians

2 Corinthians 1

2 Corinthians 1:1-2

Ni nani aliyeandika barua hii?

Paulo na Timotheo waliandika barua.

Barua illiandikwa kwa nani?

Iliandikwa kwa kanisa la Mungu lililoko Koritho na kwa watakatifu wote katika kanda nzima ya Akaya.

2 Corinthians 1:3-7

Paulo anamuelezeaje Mungu?

Paulo anamuelezea Mungu kama Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, baba wa huruma na Mungu wa faraja.

Kwa nini Mungu hutufariji katika dhiki yetu?

Anatufariji ili tuweze kuwafariji wale walio katika shida, kwa faraja sawa ambayo sisi wenyewe tunafarijiwa na Mungu.

2 Corinthians 1:8-10

Paulo na rafiki zake walipata shida gani huko Asia?

Walionewa zaidi ya vile wawezavyo kustahimili. Walikuwa na hukumu ya kifo juu yao.

Paulo na rafiki zake walipata shida gani huko Asia?

Walionewa zaidi ya vile wawezavyo kustahimili. Walikuwa na hukumu ya kifo juu yao.

Kwa sababu gani ilipangwa hukumu ya kifo kwa Paulo na wenzake?

Hukumu ya kifo iliwafanya wasiweke imani yao, badala yake wamwamini Mungu

2 Corinthians 1:11

Paulo alisema kwamba kanisa la Korintho lingewasaidiaje?

Paulo alisema kanisa la Koritho lingewasaidia kwa maombi yao.

2 Corinthians 1:12-14

Paulo alisema juu ya nini kwamba yeye na rafiki zake walijivunia?

Walijivunia ushuhuda wa dhamiri zao, ambayo ni kwamba wamekuwa na mwenendo wao wenyewe katika dunia na hasa katika kushughulika na kanisa la Koritho - pamoja na utakatifu na usafi ambao unatoka kwa Mungu, sio katika hekima ya uliwengu lakini kwa neema ya Mungu.

Paulo alikuwa na uhakika nini kitatoke katika siku ya Bwana wetu Yesu?

Alikuwa na hakika kwamba siku hiyo Paulo na wenzake watakuwa sababu ya kiburi cha watakatifu wa Korintho.

2 Corinthians 1:15-20

Paulo alikuwa anapanga mara ngapi kuwatembelea watakatifu wa Koritho?

Alikuwa anapanga kuwatembelea mara mbili.

2 Corinthians 1:21-22

Ni sababu gani mojawapo iliyomfanya Kristo kutupatia Roho Mtakatifu kwenye mioyo yetu?

Ametupa Roho kama uthibitisho wa kile atakachotupa sisi baadaye.

2 Corinthians 1:23-24

Kwa nini Paulo hakuja Koritho?

Hakuja Koritho ili kwamba asiwalemee wao

Paulo alisema nini yeye na Timotheo nini hawakufanya kwa kanisa la Korintho?

Paulo alisema hawajaribu kudhibiti kile imani yao inapaswa kuwa, lakini walikuwa wakifanya kazi na kanisa la Korintho kwa furaha yao.

2 Corinthians 2

2 Corinthians 2:1-2

Paulo alikuwa anajaribu kuepuka hali gani kwa kutokuja kanisa la Koritho?

Paulo alikuwa anakwepa kuja kanisa la Koritho katika hali ya maumivu.

2 Corinthians 2:3-4

Kwa nini Paulo anaandika kama alivyofanya katika barua yake iliyopita kwa kanisa la Korintho?

Aliandika kama alivyofanya ili kwamba atakapokuja kwao asiweze kuumizwa na wale ambao wangemfanya yeye afurahi.

Ni wakati gani Paulo aliwaandikia Wakorintho kabla ya kuwa na mawzo mengi?

Alikuwa katika taabu kubwa na maumivu ya moyo.

Kwa nini Paulo aliwaandikia barua kanisa la Korintho

He wrote to them so that they would know the depth of the love that he had for them.

2 Corinthians 2:5-7

Paulo alisema nini watakatifu wa Korintho wanapaswa sasa kufanya kwa wale waliowaadhibu?

Paulo alisema wanapaswa kumsamehe na kumfariji mtu huyo.

Paulo alisema nini watakatifu wa Korintho wanapaswa sasa kufanya kwa wale waliowaadhibu?

Paulo alisema wanapaswa kumsamehe na kumfariji mtu huyo.

Paulo alisema nini watakatifu wa Korintho wanapaswa sasa kufanya kwa wale waliowaadhibu?

Paulo alisema wanapaswa kumsamehe na kumfariji mtu huyo.

2 Corinthians 2:8-9

Nini sababu nyingine Paulo aliyoandikia kanisa la Korintho?

Paulo aliwaandikia kuwajaribu na kujua kama walikuwa wakitii katika kila kitu.

2 Corinthians 2:10-11

Kwa nini ilikuwa muhimu kwa kanisa la Korintho kujua kwamba yeyote ambaye wamesamehewa pia alisamehewa na Paulo na mbele ya Kristo?

Ilikuwa hivyo kwamba Shetani asiwadanganye.

2 Corinthians 2:12-13

Kwa nini Paulo hakuwa na amani ya moyo alipoenda mji wa Troasi?

Alikuwa na amani ya moyo kwa sababu hakuweza kumwona ndugu yake Tito huko Troas.

2 Corinthians 2:14-15

Mungu alifanya nini kupitia Paulo na wenzake?

Kupitia Paulo na wenzake Mungu alisambaza harufu tamu ya maarifa ya Kristo kila mahali.

Mungu alifanya nini kupitia Paulo na wenzake?

Kupitia Paulo na wenzake Mungu alisambaza harufu tamu ya maarifa ya Kristo kila mahali.

2 Corinthians 2:16-17

Paulo alisemaje kwamba yeye na wenzake walikuwa tofauti na watu wengi ambao walinunua neno la Mungu kwa faida?

Paulo na wenzake walikuwa tofauti kwa kuwa walizungumza kwa usafi wa nia, kama waliotumwa kutoka kwa Mungu, mbele ya Mungu, wakiongea katika Kristo.

2 Corinthians 3

2 Corinthians 3:1-3

Ni barua gani ya mapendekezo ambayo Paulo na wenzake walikuwa nayo?

Watakatifu wa Korintho walikuwa walikua nabarua ya mapendekezo, inayojulikana na kusomwa na watu wote.

2 Corinthians 3:4-6

Ni ujasiri gani ambao Paulo na wenzake walikuwa nao katika Mungu kupitia Kristo?

Ujasiri wao haukuwa katika wao wenyewe bali ni utoshelevu ambao Mungu aliwapa.

Ni ujasiri gani ambao Paulo na wenzake walikuwa nao katika Mungu kupitia Kristo?

Ujasiri wao haukuwa katika wao wenyewe bali ni utoshelevu ambao Mungu aliwapa.

Ilikuwa msingi gani wa agano jipya ambalo Mungu alikuwa amewastahili Paulo na wenzake kuwa watumishi?

Agano jipya lilitokana na roho ambaye hutoa uzima, sio barua inayoua.

2 Corinthians 3:7-8

Kwa nini watu wa Israeli hawakuuangalia moja kwa moja uso wa Musa?

Hawakuangalia moja kwa moja kwenye uso wake kwa sababu ya utukufu wa uso wake, utukufu ambao ulikuwa unaishiria.

2 Corinthians 3:9-13

Nini kitakuwa na utukufu zaidi, utumishi ya hukumu au utumishi ya haki?

Utumishi wa haki huzidi zaidi katika utukufu.

2 Corinthians 3:14-16

Jinsi gani ufahamu wa waisraleli ulifunguliwa na utaji kuondolewa katika mioyo yao?

Pale tu waisraeli wanapomrudia Krito Bwana ufahamu wao unafunguliwa na utaji kuondolewa.

Tatizo gani lipo hata leo kwa watu wa Israeli wakati agano la kale la Musa linasoma?

Tatizo lao ni akili zao zimefungwa na kufunika uongo juu ya mioyo yao.

Nini Waisraeli wanaweza kufunguliwa na pazia limeondolewa miyoyoni mwao?

Wakati tu Waisraeli watakapo mrudia Bwana Kristo mawazo yao yaliyofunguliwa na pazia limeondolewa.

2 Corinthians 3:17-18

Nini kinapatikana palipo na Roho wa Bwana?

Pale alipo Roho wa Bwana, kuna uhuru.

Kwa nini wote wanaouona utukufu wa Bwana wanapaswa kubadilishwa?

Wanapaswa wanabadilishwa kuwa sawa mfano wa utukufu kutoka kiwango fulani cha utukufu hadi kingine.

2 Corinthians 4

2 Corinthians 4:1-2

Kwa nini Paulo na wenzake hawakukata tamaa?

Hawakukata tamaa kwa sababu ndani yao walikuwa wakifanywa upya siku hadi siku. Pia, wakati wao, mwanga wa mateso ulikuwa ukiwandaa kwa ajili ya uzito wa utukufu ambao unazidi vipimo vyote. Mwisho, walikuwa wanatazamia vitu vya milele.

Ni njia gani ambazo Paulo na wenzake waliziacha?

Walikuwa wamekataa njia ambazo ni aibu na za siri. Hawakuishi kwa udanganyifu na hawakutumia vibaya neno la Mungu.

Paulo na wengine walijishughulishaje wenyewe kwa dhamiri ya kila mtu mbele ya Mungu?

Walifanya hivyo kwa kuwasilisha ukweli.

2 Corinthians 4:3-4

Kwa nani Injili imefichika ?

Imefichika kwa wale ambao wanaangamia.

Kwa nini injili imefunikwa kwa wale ambao wanaangamia?

Imefunikwa kwa sababu mungu wa ulimwengu huu amewapofusha akili zao zisizoamini ili wasiweze kuona mwanga wa injili.

2 Corinthians 4:5-6

Paulo na wenzake walitangaza nini kuhusu Yesu na kuhusu wao wenyewe?

Walimtangaza Kristo Yesu kama Bwana na wao wenyewe kama watumishi wa kanisa la Koritho kwa ajili ya Yesu.

2 Corinthians 4:7-12

Kwa nini Paulo na wenzake wana hii hazina kwenye vyombo vya udongo?

Walikuwa na hii hazina kwenye vyombo vya udongo ili kwamba ieleweke kuwa ile nguvu kubwa inayozidi ni ya Mungu na sio ya kwao.

Kwa nini Paulo na wenzake walibeba katika miili yao kifo cha Yesu?

Walibeba kifo cha Yesu katika miili yao ili uhai wa Yesu uweze pia kuonyeshwa katika miili yao.

2 Corinthians 4:13-15

Ni nani atakayefufuliwa na kuletwa mbele ya yeye aliyemfufua Bwana Yesu?

Paulo na wenzake pamoja na watakatifu wa Korintho wataletwa mbele ya yeye aliyemfufua Bwana Yesu.

Nini kitatokea kama matokeo ya neema inayoenea kwa watu wengi?

Kama neema imeenea kwa watu wengi, shukrani itaongezeka kwa utukufu wa Mungu.

2 Corinthians 4:16-18

Kwa nini Paulo na wenzake wana sababu ya kukata tamaa?

Walikuwa na sababu ya kukata tamaa kwa sababu kwa nje walikuwa wanachakaa.

Kwa nini Paulo na wenzake hawakukata tamaa?

Hawakukata tamaa kwa sababu ndani yao walikuwa wanafanywa upya siku hadi siku. Pia, kwa kipindi hiki kifupi, mateso madogo yalikuwa yanawaandaa wao kwa uzito wa utukufu ambao unazidi vipimo vyote. Mwisho, walikuwa wanatazama kwa ajili ya vitu vya milele visivyo onekana.

Kwa nini Paulo na wenzake hawakukata tamaa?

Hawakukata tamaa kwa sababu ndani yao walikuwa wanafanywa upya siku hadi siku. Pia, kwa kipindi hiki kifupi, mateso madogo yalikuwa yanawaandaa wao kwa uzito wa utukufu ambao unazidi vipimo vyote. Mwisho, walikuwa wanatazama kwa ajili ya vitu vya milele visivyo onekana.

2 Corinthians 5

2 Corinthians 5:1-3

Kwa nini Paulo alisema bado tunayo kama masikani ya duniani imeharibiwa?

Paulo alisema tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba isiyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu, bali nyumba ya milele, katika mbingu.

2 Corinthians 5:4-5

Kwa nini Paulo alisema kwamba wakati tuko katika hema hii, tunaugua?

Paulo alisema hivi kwa sababu wakati tuko katika hema hii, tunalemewa na tunataka kuvishwa, il kwamba kile kinacho kufa kiweze kumezwa na uzima.

Mungu alitupatia nini kama ahadi ya kile kinachokuja?

Mungu alitupatia Roho kama ahadi ya kile kitakachokuja.

2 Corinthians 5:6-8

Je! Paulo angeweza kuwa katika mwili, au nyumbani na Bwana?

Paulo alisema, "tungependa kuwa mbali na mwili na nyumbani pamoja na Bwana.

2 Corinthians 5:9-10

Lengo la Paulo lilikwa ni nini?

Paulo alilifanya lengo lake kumpendeza Bwana.

Kwa nini Paulo alifanya kuwa lengo lake kumpendeza Bwana?

Paulo alifanya lengo hili kwa sababu sisi sote tupaswa kuonekana mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo kupokea kile kinachofaa kwa mambo yaliyofanyika katika mwili, iwe kwa mema au mabaya.

2 Corinthians 5:11-12

Kwa nini Paulo na wenzake walishawishi watu?

Waliwashawishi watu kwa sababu waliijua hofu ya Bwana.

Paulo alisema hawakujipendekeza wenyewe kwa watakatifu wa Korintho. Walifanya nini?

Walikuwa wakiwapa watakatifu wa Korintho sababu ya kujivunia wao, ili watakatifu wa Korintho wawe na jibu kwa wale ambao walijisifu juu ya maonyesho lakini si kuhusu yaliyo ndani ya moyo.

2 Corinthians 5:13-15

Kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya wote, wanaoishi wanapaswa kufanya nini?

Hawapaswi kuishi si kwaajiri yao wenyewe, bali kwa ajili ya yeye aliyekufa na aliyefufuliwa.

2 Corinthians 5:16-17

Kwa nini Paulo alisema hatuta muhukumu yeyote kulingana na viwango vya wanadamu?

Hii ni kwa sababu Kristo alikufa kwa ajili ya wote, na hatuishi tena kwa ajili yetu, bali kwa ajili ya Kristo.

Ni nini kinachotokea kwa mtu yeyote aliye ndani ya Kristo?

Yeye ni kiumbe kipya. Mambo ya kale yamepita. Tazama, yamekuwa mapya.

2 Corinthians 5:18-19

Wakati Mungu kupitia Kristo huwaunganisha watu yeye mwenyewe Mungu anawatendea nini?

Mungu hawahesabu makosa yao ya dhambi dhidi yao na anawapa ujumbe wa kuunganishwa.

2 Corinthians 5:20-21

Kama tulio chaguliwa wawakilishi wa Kristo, nini maombi ya Paulo na wenzake na huruma yake kwa Wakoritho?

Maombi yao kwa Wakoritho ni kupatanishwe kwa Mungu kwa ajili ya Kristo!.

Kwa nini Mungu alimfanya Kristo awe dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu?

Mungu alifanya hivyo ili kwa Kristo tupate kuwa haki kwa Mungu.

2 Corinthians 6

2 Corinthians 6:1-3

Paulo na wenzake waliwasihi Wakoritho wasifanye nini?

Waliwasihi Wakoritho wasiipokee neema ya Mungu pasipo faida.

Ni wakati gani mzuri? Siku ya wokovu ni lini?

Sasa ni wakati mzuri. Sasa ni siku ya wokovu.

Kwa nini Paulo na wenzake hawakuweka kizuizi mbele ya mtu yeyote?

Hawakuweka kizuizi mbele ya mtu yeyote, kwa sababu hakutaka huduma yao iletwe kinyume.

2 Corinthians 6:4-7

Tendo gani la Pauo na wenzake lilithibitisha?

Matendo yao yalithibitisha walikuwa watumishi wa Mungu.

Ni baadhi ya mambo gani ambayo Paulo na wenzake waliyapitia?

Walipitia mateso, dhiki, ugumu wa maisha, kupigwa, vifungo, ghasia, kazi kwa bidii, kukosa usingizi usiku, na njaa.

Ni baadhi ya mambo gani ambayo Paulo na wenzake waliyapitia?

Walipitia mateso, dhiki, ugumu wa maisha, kupigwa, vifungo, ghasia, kazi kwa bidii, kukosa usingizi usiku, na njaa.

2 Corinthians 6:8-10

Japokuwa Paulo na wenzake walikuwa wakweli, walituhumiwa kwa ajili gani?

Walituhumiwa kwa kuwa wadanganyifu.

2 Corinthians 6:11-13

Badiliko gani Paulo anatamani kulifanya na kanisa la Koritho?

Paulo anasema mioyo yao ilikuwa imefunguliwa kwa upana kwa Wakoritho na katika mabadiliko ya haki Paulo alitaka watakatifu wa Koritho kufungua mioyo yao kwa upana, kwa Paulo na wenzake.

2 Corinthians 6:14-16

Sababu gani Paulo anazitoa kama kwa nini watakatifu wa Koritho wanapaswa kutokufungamana pamoja na wasioamini?

Paulo anatoa sababu zifuatazo: kuna ushirika gani kati ya haki na uasi? Nuru inaushirika na Giza? Kristo anakubaliana na Beliari? Aaminiye anasehemu gani pamoja na asiyeamini? Kunaweza kuwa na makubaliano kati ya hekaru na sanamu?.

2 Corinthians 6:17-18

Mungu anasema nini kwamba atafanya kwa ajili ya wale ambao wata, "toka kati yao na kutengwa nao, na msiguse kilicho kichafu...?

Bwana anasema atawakaribisha wao. Atakuwa baba kwao nao watakuwa watoto wake wa kike na wakiume.

2 Corinthians 7

2 Corinthians 7:1

Ni nini Paulo anasema tunapaswa kujitakasa wenyewe?

Tunapaswa kujitakasa wenyewe kwa kila kitu kinachofanya sisi kuwa najisi katika mwili na roho.

2 Corinthians 7:2-4

Paulo alitaka watakatifu wa Korintho kufanya nini kwaajiri yake mwenyewe na wenzake?

Paulo alitaka wao, "kuweka nafasi kwaajiri yao!"

Maneno gani ya kuhimiza aliyonayo Paulo kwa watakatifu wa Korintho?

Paulo aliwaambia watakatifu wa Korintho walikuwa ndani ya mioyo yao, kufa pamoja na kuishi pamoja. Paulo pia aliwaambia kuwa alikuwa na ujasiri mkubwa ndani yao na alikuwa na ninajivuna kwa ajili yao.

2 Corinthians 7:5-7

Ni faraja gani ambayo Mungu alimpa Paulo na wenzake wakati walifika Makedonia na walikuwa na wasiwasi kwa kila njia - migogoro ya nje na hofu ndani?

Mungu aliwafariji kwa kuwasili kwa Tito, kwa ripoti ya faraja ambayo Tito alikuwa amepokea kutoka kwa watakatifu wa Korintho, na kwa upendo mkubwa wa Wakorintho, huzuni zao na wasiwasi mkubwa kwa Paulo.

2 Corinthians 7:8-10

Barua ya Paulo ya awali ili toa nini kwa watakatifu wa Korintho?

Watakatifu wa Korintho walipata huzuni, huzuni ya Mungu kwa kukabiliana na barua ya Paulo ya awali.

Barua ya Paulo ya awali ili toa nini kwa watakatifu wa Korintho?

Watakatifu wa Korintho walipata huzuni, huzuni ya Mungu kwa kukabiliana na barua ya Paulo ya awali.

Uvumilivu wa Mungu ulizalisha nini kwa watakatifu wa Korintho?

Huzuni ilileta toba ndani yao.

2 Corinthians 7:11-12

Huzuni ya Mungu ilizaa nini katika watakatifu wa Korintho?

Huzuni ya Mungu iliwaletea toba ndani yao na uamuzi mkubwa wa kuthibitisha kwamba hawakuwa na hatia.

2 Corinthians 7:13-14

Kwa nini Tito alikuwa na furaha?

Alifurahi kwa sababu roho yake ilifarijiwa na watakatifu wote wa Korintho.

2 Corinthians 7:15-16

Kwa nini upendo wa Tito kwa watakatifu wa Korintho ulikua hata zaidi?

Upendo wa Tito kwa watakatifu wa Korintho ulikua zaidi kama alikumbuka utii wa watakatifu wote wa Korintho kama walivyompokea kwa hofu na kutetemeka.

2 Corinthians 8

2 Corinthians 8:1-5

Paulo alitaka kaka na dada wa Korintho kujua nini?

Paulo alitaka wajue kuhusu neema ya Mungu iliyotolewa kwa makanisa ya Makedonia.

Makanisa ya Makedonia yalifanya nini wakati wa jaribio kubwa la taabu, na ingawa walikuwa maskini sana?

Walizalisha utajiri mkubwa wa ukarimu.

2 Corinthians 8:6-9

Paulo alimuomba Tito kufanya nini?

Paulo alimwomba Tito kuleta kukamilisha tendo hili la neema kwa upande wa watakatifu wa Korintho.

Kwa nini kingine waumini wa Korintho waliongeza?

Waliongezeka katika imani, kwa mazungumzo, kwa ujuzi, kwa bidii yote, na kwa upendo wao kwa Paulo

2 Corinthians 8:10-12

Paulo anasema nini ni zuri na linalokubalika?

Paulo anasema ni jambo nzuri na linalokubalika kwa watakatifu wa Korintho kuwa na hamu ya kufanya kazi hiyo.

2 Corinthians 8:13-15

Je! Paulo anataka kazi hii ifanyike ili wengine waweze kuokolewa na watakatifu wa Korintho wanaweza kulemewa?

Hapana. Paulo alisema wingi Wakorintho wakati huo wa sasa ungewapa kile ambacho wao (watakatifu wengine) walihitaji. Pia ili wingi wao pia utumie mahitaji ya mtakatifu wa Korintho, na ili uweze kuwa na haki.

Je! Paulo anataka kazi hii ifanyike ili wengine waweze kuokolewa na watakatifu wa Korintho wanaweza kulemewa?

Hapana. Paulo alisema wingi Wakorintho wakati huo wa sasa ungewapa kile ambacho wao (watakatifu wengine) walihitaji. Pia ili wingi wao pia utumie mahitaji ya mtakatifu wa Korintho, na ili uweze kuwa na haki.

2 Corinthians 8:16-19

Tito alifanya nini baada ya Mungu kuweka ndani ya moyo yao uangalifu huo ambao Paulo alikuwa nao kwa watakatifu wa Korintho?

Tito alikubali rufaa ya Paulo, na akiwa na bidii sana juu yake, alikuja kwa watakatifu wa Korintho kwa mapenzi yake mwenyewe.

2 Corinthians 8:20-21

Paulo alikuwa makini kuepuka nini katika vitendo vyake kuhusu tendo hili la ukarimu?

Paulo alikuwa makini kuepuka kutoa mtu yeyote sababu ya kulalamika kuhusu matendo yake.

2 Corinthians 8:22-24

Paulo aliwaambia watakatifu wa Korintho kufanya nini kuhusu ndugu waliotumwa kwao na makanisa mengine?

Paulo aliwaambia kanisa la Wakorintho kuwaonyesha upendo wao, na kuwaonyesha kwa nini Paulo alijisifu juu ya kanisa la Korintho miongoni mwa makanisa mengine.

2 Corinthians 9

2 Corinthians 9:1-2

Kuhusu nini Paulo anasema si lazima kuwandikia Wtakatifu wa Korintho?

Paulo anasema si lazima kuandikia kuhusu huduma kwa watakatifu.

2 Corinthians 9:3-5

Kwa nini Paulo aliwatuma ndugu huko Korintho?

Aliwatuma ndugu ili kujivunia kwake juu ya watakatifu wa Korintho isiwe bure, na hivyo kwamba watakatifu wa Korintho watakuwa tayari, kama Paulo alivyosema watakuwa.

Kwa nini Paulo alidhani ni muhimu kuwahimiza ndugu kwenda kwa watakatifu Wakorintho na kufanya mipango mapema kwa ajili ya zawadi Wakorintho walikuwa wameahidi?

Paulo alidhani ni muhimu ili Paulo na wenzake wasiwe na aibu ikiwa watu wa Makedonia walikuja na Paulo na wakaona Wakorintho wasio tayari. Paulo alitaka Wakorintho kuwa tayari na zawadi moja kwa uhuru inayotolewa na si kwa sababu Wakorintho walilazimika kutoa.

Kwa nini Paulo alidhani ni muhimu kuwahimiza ndugu kwenda kwa watakatifu Wakorintho na kufanya mipango mapema kwa ajili ya zawadi Wakorintho walikuwa wameahidi?

Paulo alidhani ni muhimu ili Paulo na wenzake wasiwe na aibu ikiwa watu wa Makedonia walikuja na Paulo na wakaona Wakorintho wasio tayari. Paulo alitaka Wakorintho kuwa tayari na zawadi moja kwa uhuru inayotolewa na si kwa sababu Wakorintho walilazimika kutoa.

2 Corinthians 9:6-9

Paulo anasema ni nini cha kutoa kwao?

Paulo anasema jambo hili ni "Mtu anayepanda kidogo atavuna kidogo, na yule anayepanda kwa manufaa atavuna manufaa."

Je! Kila mmoja anaweza kutoa nini?

Kila mmoja atoe kama alivyopanga moyoni mwake-si kwa wajibu wa kulazimisha au kuwa na huzuni wakati anatoa.

2 Corinthians 9:10-11

Ni nani ambaye hutoa mbegu kwa mkulima na mkate kwa ajili ya chakula cha kufanya kwa watakatifu wa Korintho?

Kwamba huyo angeenda kutoa na kuzidisha mbegu zao kwa kupanda na kuongeza mavuno ya haki yao. Walikuwa wakitengenezwa kwa kila njia ili waweze kuwa wenye ukarimu.

Ni nani ambaye hutoa mbegu kwa mkulima na mkate kwa ajili ya chakula cha kufanya kwa watakatifu wa Korintho?

Kwamba huyo angeenda kutoa na kuzidisha mbegu zao kwa kupanda na kuongeza mavuno ya haki yao. Walikuwa wakitengenezwa kwa kila njia ili waweze kuwa wenye ukarimu.

2 Corinthians 9:12-15

Ni jinsi gani Watakatifu wa Korintho walimtukuza Mungu?

Wakamtukuza Mungu kwa utiifu wa kukiri kwao ya injili ya Kristo, na ukarimu wa zawadi zao.

Kwa nini watakatifu waliwatamani watakatifu Wakorintho kama waliwaombea?

Walitamani kwa sababu ya neema kubwa sana ya Mungu iliyokuwa juu ya Wakorintho.

2 Corinthians 10

2 Corinthians 10:1-2

Paulo aliomba nini kwa watakatifu wa Korintho:

Paulo aliwaombea kwamba wakati alipokuwapo pamoja nao, hakuwa na ujasiri na kujiamini.

Kwa nini Paulo alifikiri angehitaji kuwa na ujasiri na kujiamini?

Paulo alidhani atakuwa na ujasiri na kujiamini wakati aliwapinga wale ambao walidhani kwamba Paulo na wenzake walikuwa wanaishi kulingana na mwili.

2 Corinthians 10:3-6

Wakati Paulo na wenzake walipigana vita, hawakutumia na silaha za aina gani?

Paulo na wenzake hawakutumia silaha za mwili wakati wakupigana vita.

Silaha ambazo Paulo alitumia zina uwezo wa kufanya nini?

Silaha ambazo Paulo alitumia zilikuwa na uwezo wa Mungu wa kuharibu ngome

2 Corinthians 10:7-8

Kwa sababu gani Bwana alimpa Paulo na wenzake mamlaka?

Bwana alimpa Paulo na wenzake mamlaka ili waweze kuwajenga watakatifu wa Korintho na kuwaangamiza.

2 Corinthians 10:9-10

Watu wengine walikuwa wanasema nini kuhusu Paulo na Nyaraka zake?

Wengine walisemaNyaraka za Paulo zilikuwa zenye nguvu na zenye nguvu, lakini kimwili alikuwa dhaifu na hotuba yake haikuwa ya thamani ya kusikiliza.

2 Corinthians 10:11-12

Paulo aliwaambia nini wale waliodhani kwamba alikuwa tofauti sana na mtu kuliko Nyaraka zake zilizothibitishwa?

Paulo alisema kwamba aliyosema kwa barua wakati alipokuwa mbali kingekuwa sawa na atakavyofanya wakati alipokuwapo na watakatifu wa Wakorintho

2 Corinthians 10:13-14

Ni wapi mipaka ya kujivunia kwa Paulo?

Paulo alisema kujivunia kwao kungekuwa katika eneo ambalo Mungu alikuwa amewapa, hata kufikia mbali na Wakorintho. Paulo alisema hawatajivunia juu ya kazi ya wengine, kuhusu kazi inayofanyika katika eneo lingine.

2 Corinthians 10:15-16

Ni wapi mipaka ya kujivunia kwa Paulo?

Paulo alisema kujivunia kwao kungekuwa katika eneo ambalo Mungu alikuwa amewapa, hata kufikia mbali na Wakorintho. Paulo alisema hawatajivunia juu ya kazi ya wengine, kuhusu kazi inayofanyika katika eneo lingine.

2 Corinthians 10:17-18

Yeye aliyethibitishwa ni nani?

Yeye aliyethibitishwa ni yule ambaye Bwana amemkubali.

2 Corinthians 11

2 Corinthians 11:1-2

Kwanini Paulo alikuwa na wivu wa Kimungu juu ya watakatifu wa Korintho?

Alikuwa na wivu kwa sababu aliwaahidi kuwa ndoa ya mme mmoja, na kuwahifadhi kama mabinti bikira kwa ajili ya Kristo.

2 Corinthians 11:3-6

Paulo aliogopa nini kuhusu watakatifu wa Korintho?

Paulo alikuwa na hofu mawazo yao yanaweza kuongozwa kutoka kwa kujitolea kwa kweli na safi kwa Kristo.

2 Corinthians 11:7-13

Paulo alihubirije Injili kwa Wakorintho?

Paulo alihubiri injili kwa uhuru kwa Wakorintho.

2 Corinthians 11:14-15

Shetani hujigeuzaje mwenyewe?

Hujigeuza mwenyewe kama malaika wa nuru.

2 Corinthians 11:16-18

Kwa nini Paulo aliwauliza watakatifu wa Korintho kumpokea kama mpumbavu?

Paulo aliwaomba wapate kumpokea kama mpumbavu ili aweze kujivunia kidogo.

2 Corinthians 11:19-21

Ni mtu gani ambaye Paulo anamtaja kuwa watakatifu wa Korintho walielewana nae kwa furaha.

Paulo alisema wamesimama kwa furaha na wajinga, na mtu aliyewafanya watumwa, na mtu aliyesababisha mgawanyiko miongoni mwao, na mtu ambaye alitumia faida yao, pamoja na mtu aliyevaa hewa, au mtu aliyewapiga makofi.

2 Corinthians 11:22-23

Paulo anajivunia nini akijilinganisha na wale ambao wanataka kupatikana kuwa sawa na Paulo katika yale waliyojisifia?

Paulo alijisifu kwamba alikuwa Mhebrania, Muisraeli na uzao wa Ibrahimu kama vile wale waliodai kuwa sawa na Paulo. Paulo alisema alikuwa mtumishi zaidi wa Kristo kuliko walivyokuwa-katika kazi ngumu zaidi, katika magereza mengi zaidi, katika kupigwa zaidi kuliko kipimo, katika kukabiliwa na hatari nyingi za kifo.

2 Corinthians 11:24-26

Ni baadhi ya hatari gani ambazo Paulo alivumilia?

Paulo alipokea mara tano "mapigo arobaini toa moja" kutoka kwa Wayahudi. Mara tatu alipigwa kwa fimbo. Mara alipigwa mawe. Mara tatu alivunjika meli. Alikaa usiku na mchana katika bahari ya wazi. Alikuwa katika hatari kutoka mito, kutoka kwa wezi, kutoka kwa watu wake mwenyewe, kutoka kwa Mataifa. Alikuwa katika hatari katika mji, jangwani, baharini na katika hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. Paulo pia alikuwa katika hatari kutoka kwa gavana wa Dameski.

2 Corinthians 11:27-29

Kwa mujibu wa Paulo, nini kilimfanya aumie ndani?

Watu kuwasababisha wenzao kutenda dhambi kilimfanya Paulo aumie ndani.

2 Corinthians 11:30-31

Paulo alisema nini angejivunia, ikiwa alikuwa na kujivunia?

Paulo alisema angejivunia juu ya kile kilichoonyesha udhaifu wake.

2 Corinthians 11:32-33

Ni baadhi ya hatari gani ambazo Paulo alivumilia?

Paulo alipokea mara tano "mapigo arobaini toa moja" kutoka kwa Wayahudi. Mara tatu alipigwa kwa fimbo. Mara alipigwa mawe. Mara tatu alivunjika meli. Alikaa usiku na mchana katika bahari ya wazi. Alikuwa katika hatari kutoka mito, kutoka kwa wezi, kutoka kwa watu wake mwenyewe, kutoka kwa Mataifa. Alikuwa katika hatari katika mji, jangwani, baharini na katika hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. Paulo pia alikuwa katika hatari kutoka kwa gavana wa Dameski.

2 Corinthians 12

2 Corinthians 12:1-5

Kuhusu nini Paulo alisema angeweza kujivunia sasa ?

Paulo alisema angeendelea kujisifu kuhusu maono na mafunuo kutoka kwa Bwana.

2 Corinthians 12:6-7

Kwa nini Paulo anasema haiwezi kuwa upumbavu ikiwa alijisifu?

Paulo alisema haitakuwa upumbavu kwa ajili ya kujivunia kwa sababu angekuwa anasema kweli.

2 Corinthians 12:8-10

Bwana alimwambia nini Paulo baada ya Paulo kumwomba amuondolee mwiba uliokuwa mwilini mwake?

Bwana alimwambia Paulo, "Neema yangu yakutosha, kwa kuwa nguvu inakamilishwa katika udhaifu."

2 Corinthians 12:11-13

Ni jambo gani lilifanyika kwa uvumilivu wote miongoni mwa Wakorintho?

Ishara, miujiiza na matendo makuu, ishara sahihi ya mtume vilifanyika kati yao kwa uvumilivu wote.

2 Corinthians 12:14-18

Kwa nini Paulo aliwaambia Wakorintho kuwa hatakuwa mzigo kwao?

Paulo aliwaambia hivi kuwaonyesha kwamba hakutaka vilivyo yao. Aliwataka wao.

2 Corinthians 12:19

Paulo alikuwa na kusudi gani kuwaambia watakatifu wa Korintho mambo haya yote?

Paulo alisema mambo yote haya ili kuwajenga watakatifu wa Korintho.

2 Corinthians 12:20-21

Paulo alikuwa na hofu gani anaweza kupata wakati aliporudi kwa watakatifu wa Korintho?

Paulo alihofia kwamba kunaweza kuwa na majadiliano, wivu, milipuko ya hasira, tamaa ya ubinafsi, umbeya, kiburi, na ugomvi.

2 Corinthians 13

2 Corinthians 13:1-2

Paulo alikuwa amefika mara ngapi kwa watakatifu wa Korintho mpaka kufikia 2 Wakorintho waliandikwa?

Paulo alikuwa amewajia kufikia 2 Wakorintho waliandikwa.

2 Corinthians 13:3-4

Kwa nini Paulo aliwaambia watakatifu Wakorintho ambao walikuwa wametenda dhambi na wengine wote kwamba ikiwa angekuja tena asingewazuia?

Paulo aliwaambia jambo hili kwa sababu watakatifu wa Korintho walitaka ushahidi kwamba Kristo alikuwa akizungumza kupitia Paulo.

2 Corinthians 13:5-6

Kwa nini Paulo aliwaambia watakatifu wa Korintho kuchunguza na kujijaribu wenyewe?

Paulo aliwaambia wafanye uchunguzi na kujijaribu wenyewe ili kuona kama walikuwa katika imani.

2 Corinthians 13:7-8

Ni kitu gani ambacho Paulo alisema kuwa yeye na wenzake hawakuwa na uwezo wa kufanya?

Paulo alisema kuwa hawakuwa na uwezo wa kufanya chochote kilicho kinyume na kweli.

2 Corinthians 13:9-10

Kwa nini Paulo aliwaandikia watakatifu wa Korintho mambo haya wakati alikuwa mbali nao?

Paulo alifanya hivi ili kwamba atakapokuwa nao, asionekane mwenye hasira kwao.

2 Corinthians 13:11-12

Kwa kumalizia, Paulo aliwataka Wakorintho kufanya nini?

Paulo alitaka waweze kufurahi, kufanya kazi kwa ajili ya kurejeshwa, kukubaliana, kuishi kwa amani, na kusalimiana kila mmoja kwa busu takatifu.

2 Corinthians 13:13-14

Ni kitu gani ambacho Paulo alitaka kila mtakatifu wa Korintho awe nacho?

Paulo alitaka wote wawe na neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu.