2 Thessalonians
2 Thessalonians 1
2 Thessalonians 1:3-5
Ni kwa mambo gani mawili ambayo Paulo anamshukuru Mungu kwayo katika kanisa la Thesalonike?
Paulo anamshukuru Mungu kwa ajili kukua kwa imani yao na kwa upendo wao kati yao.
Ni hali gani ambayo waumini wa Thesalonike wanavumilia?
Waumini wanavumilia mateso na dhiki.
Ni matokeo gani chanya/mazuri ambayo waumini watapata kutokana na kuvumilia kwao?
Waumini watahesabiwa kuwa wanasitahili kwa ufalme wa Mungu.
2 Thessalonians 1:6-8
Mungu atawafanya nini wale wanaowatesa walioamini?
Mungu atawaadhibu wale wote wanaowatesa walioamini, atawaadhibu kwa mwali wa moto.
Je waumini watapumzishwa katika dhiki zao?
Waumini watafarijiwa wakati Yesu atakapofunuliwa kutoka mbinguni.
Mungu atawafanya nini wale ambao wanawatesa waumini?
Mungu atawatesa wale wanaowatesa waumini, kuwaadhibu katika mwali moto.
2 Thessalonians 1:9-10
Adhabu wale wote wasiomjua Mungu itakuwa ya muda gani?
Adhabu kwa wale wote wasiomjua Mungu itakuwa ya milele.
Wale wote wasiomjua Mungu wametengwa na nini kama sehemu ya adhabu yao?
Wale wote wasiomjua Mungu wametegwa na uwepo wa Bwana kama sehemu ya adhabu yao.
Waumin watafanya nini wakati watakapomwona Kristo akija siku yake?
Waumini watamshangaa Yesu atakapokuja katika siku ya ujio wake.
2 Thessalonians 1:11-12
Nini matokeo ya kazi nzuri ya imani ya waumini iliyofanywa kwa nguvu ya Mungu?
Matokeo ya kazi zao nzuri ni kwamba jina la Bwana Yesu Kristo linatukuzwa.
2 Thessalonians 2
2 Thessalonians 2:1-2
Ni kuhusu tukio gani Paulo anasema sasa anaenda kuandika?
Paulo anasema sasa anaenda kuandika kuhusu ujio wa Bwana Yesu Kristo.
Paulo anawambia wasiamini nini?
Paulo anawambia kwamba wasiamini kwamba siku ya Bwana imekwisha kuja.
2 Thessalonians 2:3-4
Paulo anasema nini lazima kije kabla ya siku ya Bwana?
anguko na kufunuliwa kwa yule mtu wa kuasi lazima vitokee kabla ya siku ya Bwana.
Yule mtu wa kuasi anafanya nini?
Yule mtu wa kuasi anampinga na anajiinua kiyume na Mungu, akikaa ndani ya hekalu na yeye mwenyewe kujifanya kuwa Mungu
2 Thessalonians 2:5-7
Hamukumbuki...haya mambo?
Paulo anatumia swali lisilo hitaji kujibiwa kuwa kumbusha fundisho alilowafundisha alipokuwa nao. AT: " Nina hakika mnakumbuka mambo haya."
atafunuliwa katika wakati mwafaka
Hili linaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: "Mungu atamfunua mtu wa kuasi wakati utakapotimilika"
siri ya uasi/ kuasi
Hii ina maanisha siri ya kiungu ambayo Mungu pekee ndiye aliye nayo.
Anayemzuia
kumzuia mtu ni kumshika nyuma au kuwafanya wasifanye kile wanachotaka kufanya.
2 Thessalonians 2:8-10
Yesu atakapofunuliwa atafanya nini kwa yule mtu wa kuasi?
Yesu atakapofunuliwa atamuua yule mtu wakuasi.
Ni nani anayefanya kazi na kumpa nguvu, ishara, na maajabu ya uongo?
Shetani anafanya kazi na mtu wa kuasi akimpa nguvu,, ishara na maajabu ya uongo
Ni kwa nini wengine wamedanganywa na mtu wa kuasi na wanaangamia?
wengine wanadanganywa kwa sababu hawakupokea upendo wa kweli ili kwamba waweze kuokolewa.
2 Thessalonians 2:11-12
Wale wanaodanganywa na kuangamia wabajifurahisha katika kitu gani?
Wale ambao wamedanganywa na wanaangamia wanajifurahisha katika udhalimu.
2 Thessalonians 2:13-15
Mungu aliwachangua Wathesalonike wapate nini kupitia injili?
Mungu alichagua Wathesalonike wapate utukufu wa Bwana Yesu Kristo kupitia injili.
Paulo anawataka Wathesalonike wafanye nini sasa kuwa wamekwisha kuipokea injili?
Paulo anawtaka Wathesalonike wasimame imara na kuendelea katika desturi waliyofundishwa.
2 Thessalonians 2:16-17
Paulo anatamani Wathesalonike wafanyiwe nini katika mioyo yao?
Paulo anatamani kwamba Wathesalonike waweze kuimalika kwa kila nzuri na neno.
2 Thessalonians 3
2 Thessalonians 3:1-3
Paulo anawataka Wathesalonike waombe nini kuhusu neno la Bwana?
Paulo anahitaji Wathesalonike waombe ili kwamba neno la Mungu liweze kusambaa kwa haraka na kutukuzwa.
Pauo anahamu kuokolewa kutoka kwa nani?
Paulo anatamani kuokolewa kutoka kwa watu waovu na wandeao dhambi ambao hawana imani.
2 Thessalonians 3:4-5
Paulo anawambia Wathesalonike waendelee kufanya nini?
Paulo anawambia Wathesalonike waendelee kufanya vitu alivyoawaagiza.
2 Thessalonians 3:6-9
Waumini waishije na kila ndugu aishie pasipo utaratibu?
Waumini wanapaswa kutochangamana na kila ngudu aishie pasipo utaratibu.
Ni mfano gani Paulo aliuweka kwa Wathesalonike juu ya kazi yake na kujitegemeza?
Paulo alifanya kazi mchana na usiku, akijilipia chakula chake na kutokuwa mzigo kwa mtu yeyote.
2 Thessalonians 3:10-12
Paulo aliamuru nini kwa kuhusu yeyote asiyetaka kufanya kazi?
Paulo aliamuru kuwa mtu yeyote asiyetaka kufanya kazi na asile.
Badala ya kuwa wavivu Paulo anawaamuru watu wa jinsi hiyo kufanya nini?
Paulo anawaamuru wavivu kufanya kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.
2 Thessalonians 3:13-15
ndugu wanapaswa wafanye nini na mtu yeyote ambaye hatii maelekezo ya Paulo katika barua hii?
Ndugu wanapaswa kujitenga na mtu yeyote ambaye hatii maelekezo ya Paulo katika barua hii.
2 Thessalonians 3:16-18
Paulo anatamani Bwana awape nini Wathesalonike
Paulo anatamani kuwa Bwana angewapa Wathesalonike amani muda wote na kwa njia zote.
Paulo anaonyeshaje kuwa yeye ni mwandishi wa barua hii?
Paulo aliandika salamu kwa mikono yake mwenyewe na akasaini kuwa yeye ndiye mwandishi.