Jude
Jude 1
Jude 1:1-2
Yuda alikuwa mtumishi wa nani?
Yuda alikuwa mtumishi wa Yesu Kristo
Ni nani aliyekuwa kaka yake na Yuda?
Yuda alikuwa kaka wa Yakobo
Yuda aliwaandikia akina nani?
aliandika kwa wale waliokuwa wameitwa, wapendwao katika Mungu Baba, na kutunzwa kwa ajili a Kristo.
Yuda alitaka ao aliowandikia waongezewe nini?
Yuda alitaka rehema, amani, na upendo uzidishwe.
Jude 1:3-4
Yuda alitaka kuandika kuhusu nini kwanza?
Yuda alitaka kuandika kwanza kuhusu wokovu wao wa kawaida.
Kweli Yuda aliandika kuhusu nini?
Kweli Yuda aliandika kuhusu uhitaji wa kupambana kwa ajili ya imani ya watakatifu.
Watu walio hukumiwa na wasio wa utaua walikujaje?
Walibadili neema ya Mungu kuwa ufisadi na kumkana Yesu Kristo.
Jude 1:5-6
Kutoka wapi Bwana aliwaokoa watu mara moja?
Bwana aliwaokoa kutoka nchi ya Misri.
Bwana alifanya nini kwa wale watu ambao hawakuamini?
Bwana aliwaangamiza wale watu ambao hawakuamini.
Bwana aliwafanya nini wale malaika walio acha makao yao maalum?
Bwana aliwaweka katika minyororo ndani ya giza kwa ajili ya hukumu.
Jude 1:7-8
Sodoma, Gomora na miji inayozunguka walifanya nini?
walifanya uasherati na kuchochea tamaa zisizo za asili.
Kama Sodoma, Gomora, na miji iliyowazunguka, watu walio hukumiwa na waasi wanafanya nini?
Wanachafua miili yao, na hukataa mamlaka, na wananena uongo.
Jude 1:9-11
Malaika mkuu Mikaeli alisema nini kwa Shetani
Malaika mkuu Mikaeli alisema, "Bwana na akukemee."
Jude 1:12-13
Ni kwa nani watu waliohukumiwa adhabu na wasio na mungu hujali pasipo aibu?
Hujijali wenyewe pasipo aibu.
Jude 1:14-16
Enoka alikuwa nafasi gani katika ukoo wa Adamu?
Enoka alikuwa wa saba katika ukoo wa Adamu.
Bwana atafanya hukumu kwa nani?
Bwana atafanya hukumu kwa watu wote.
Waasi gani ambao watahukumiwa?
Wanung'unikao, walalamikao ambao hufauata tamaa zao za uovu, wajivunao mno, ambao kwa faida yao hudanganya wengine.
Jude 1:17-19
Nani aliongea maneno hapo zamani kuhusu wenye dharau?
Mitume wa Bwana Yesu Kristo waliongea maneno hapo zamani kuhusu wenye dharau.
Nini ni cha kweli kuhusu wadhihaki wanao fuata tamaa zao, wasababisha utengano na utawaliwa na tamaa za asili?
Hawana Roho Mtakatifu.
Jude 1:20-21
Ni jinsi gani wapendwa walikuwa wakijijenga wenyewe na kuomba?
Wapendwa walikuwa wakijijenga wenyewe zaidi katika imani yao takatifu, na kuomba katika Roho Mtakatifu.
Wapenzi walitakiwa kujitunza katika nini nakutazamia nini?
Wapenzi walipaswa kujihifadhi na kuutazama upendo wa Mungu, na rehema za Bwana wetu Yesu Kristo.
Jude 1:22-23
Ni akina nani ambao wapendwa walipaswa kuwa na huruma juu yao na kuwaokoa?
Wapendwa walipaswa kuwa na huruma juu yao na kuwaokoa wale waliokuwa katika mashaka au wenye vazi lililo kwenye mwili, na wote walio kwenye moto.
Jude 1:24-25
Mungu Baba Mwokozi wao, kupitia Yesu Kristo aliweza kuwafanyia nini?
Mungu aliweza kuwalinda wasijikwae na kuwasababisha wasimame mbele ya utufu wake bila mawaa.
Mungu alikuwa lini na utufu?
Mungu alikuwa na utukufu kabla ya nyakati zote, sasa, na hata milele.