Joel
Joel 1
Joel 1:1-3
Maneno ya nani yalikuja kwa Yoeli?
Maneno ya Bwana yalikuja kwa Yoeli.
Wazee walitakiwa wawaambie akina nani maneno ya Bwana?
Walitakiwa wawaambie watoto wao na watoto wao wawaambie watoto wao.
Joel 1:4
Nini kilitokea kwa kile kilichoachwa na nzige?
Panzi walikula kile kilichoachwa na nzige.
Joel 1:5-7
Kwa nini walevi wataomboleza?
Wataomboleza kwa sababu divai tamu itaondolewa kwao.
Adui alitengeneza mizabibu kwenye nini?
Alitengeneza mizabibu mahali pa kutisha.
Joel 1:8-12
Kwa sababu gani bikira aliomboleza?
Aliomboleza kwa sababu ya kifo cha mume wake kijana.
Nini kilitokea kwenye nafaka?
Nafaka ziliharibiwa.
Joel 1:13-14
Nini kilikuwepo kutoka kwenye nyumba ya Bwana?
Dhabihu za nafaka na vinywaji vilikuwepo toka kwenye nyumba ya Bwana.
Joel 1:15-17
Siku ya Bwana itakuwa lini?
Siku ya Bwana imekaribia.
Nini kimevunjwa?
Ghala zimevunjwa.
Joel 1:18-20
Kwa nini makundi ya wanyama yanateseka?
Makundi ya wanyama yanateseka kwa sababu hakuna malisho.
Yoeli alimuita nani?
Yoeli alimuita Bwana.
Wanyama walitweta kwa nani?
Wanyama walitweta kwa Bwana.
Joel 2
Joel 2:1-2
Kwa nini wenyeji wa nchi walitetemeka kwa woga?
Walitetemeka kwa woga kwa sababu siku ya Bwana inakuja.
Ni wakati gani lilikuwepo jeshi kama hili?
Hakujawahi kuwa na jeshi kama hili na haitatokea tena.
Joel 2:3
Nchi ipo kama nini nyuma ya jeshi?
Nyuma ya jeshi nchi ipo kama jangwa lililoharibiwa.
Joel 2:4-7
Jeshi linafanana na nini na linafanya nini?
Jeshi linafanana na farasi na kuendesha kama mpanda farasi.
Joel 2:8-9
Ni kwa namna gani jeshi liliingia kwenye jiji?
Waliukimbilia mji, walikimbia juu ya ukuta, walipanda kwenye nyumba na kupitia madirishani kama wezi.
Joel 2:10-11
Hili ni jeshi lanani?
Hili ni jeshi la Bwana.
Joel 2:12-14
Vitu gani viwili watu wanatakiwa wavirarue?
Wararue mioyo yao na mavazi yao.
Kwa nini watu wamrudie Bwana?
Ni wa rehema na neema, si mwepesi wa hasira, ana upendo mkuu na anatamani asitoe adhabu.
Joel 2:15-17
Kwa nini watu wapige tarumbeta huko Sayuni?
Wapige terumbeta ili kuweka wakfu mfungo na kuita kusanyiko takatifu.
Joel 2:18-20
Watu wa Bwana walikuwaje kati ya mataifa?
Watu wa Bwana walikuwa wakulaumiwa kati ya mataifa.
Joel 2:21-23
Kwa nini nchi isiogope?
Nchi isiogope kwa sababu Bwana ametenda mambo makuu.
Joel 2:24-25
Nani alituma jeshi lenye nguvu?
Bwana alituma jeshi lenye nguvu.
Joel 2:26-27
Je Bwana ataleta tena aibu kwa watu wake?
Hapana Bwana hataleta tena aibu kwa watu wake.
Je Bwana ataleta tena aibu kwa watu wake?
Hapana Bwana hataleta tena aibu kwa watu wake.
Joel 2:28-29
Nini kitatokea Bwana akimimina roho yake?
Wana na binti zao watafanikiwa, wazee wao wataota ndoto na vijana wao wataona maono.
Nini kitatokea Bwana akimimina roho yake?
Wana na binti zao watafanikiwa, wazee wao wataota ndoto na vijana wao wataona maono.
Joel 2:30-31
Bwana ataonesha nini mbinguni na duniani?
Bwana ataonesha maajabu mbinguni na duniani.
Jua litageuka kuwa nini?
Jua litageuka giza.
Joel 2:32
Nani ataokoka wakati huo?
Kila mtu aliitie jina la Bwana ataokoka.
Joel 3
Joel 3:1-3
Bwana atamleta nani katika bonde la Yehoshafau?
Bwana atayaleta mataifa katika bonde la Yehoshafau.
Mataifa yatawatawanyisha akina nani?
Mataifa yaliwatawanyisha watu wa Bwana.
Joel 3:4-6
Tiro, Sidoni na miji yote ya Filisti walimkasirikia nani?
Tiro, Sidoni na miji yote ya Filisti walimkasirikia Bwana.
Tiro, Sidoni na Filisti waliifanya nini hazina ya Bwana?
Waliileta hazina ya Bwana kwenye mahekalu yao.
Tiro, Sidoni na Filisti waliwafanya nini watu wa Yuda na Yeresalemu?
Waliwauza kwa Wayunani ili kuwaondoa kwenye milki yao.
Joel 3:7-8
Bwana atawafanya nini wana na binti za Tiro, Sidoni na Filisti?
Bwana atawauza wana na binti zao kwa Sheba kupitia mikono ya watu wa Yuda.
Joel 3:9-11
Mataifa yatapiga kwenye nini majembe yao?
Watapiga majembe yao kwenye upanga.
Joel 3:12-13
Bwana atayafanya nini mataifa yanayowazunguka?
Ataketi na kuhukumu mataifa yanayowazunguka.
Joel 3:14-15
Nini kitatokea kwa jua, mwezi na nyota?
Jua na mwezi vitakuwa giza na nyota hazitatoa mwanga wake.
Joel 3:16-17
Bwana atakuwa nani kwa watu wake?
Bwana atakuwa mchungaji na ngome kwa watu wake.
Joel 3:18-21
Vilima vitatiririsha nini?
Vilima vitatiririsha maziwa
Ni nani atakayeachwa kwa sababu ya vurugu waliyowafanyia watu wa Yuda?
Misri na Edomu zitaachwa.