Ezekiel
Ezekiel 1
Ezekiel 1:1-3
Miongoni mwa nani Ezekieli alikuwa akiishi wakati alipokuwa na maono ya Mungu?
Ezekieli alikuwa akiishi miongoni mwa mateka katika nchi ya Wakaldayo wakati alipokuwa na maono ya Mungu.
Ezekiel 1:4-6
Nini kilikuwa katikati ya wingu kubwa alilokuwa ameliona likija kutoka kaskazini?
Katikati ya wingu kulikuwa na mfanano wa viumbe hai wanne, kila mmoja alikuwa na nyuso nne na mabawa manne.
Ezekiel 1:7-9
Je! viumbe
Viumbe hawakugeuka walipokuwa wakienda lakini kila kimoja kilienda mbele.
Ezekiel 1:10-12
Wale viumbe hai walikuwa na muonekano gani kwenye nyuso zao?
Nyuso zao zilikuwa na mwonekano wa mtu, simba, ng'ome, na tai.
Mwelekeo na kwenda kwa hao viumbe hai wanne kulikuwaje?
Roho alikuwa akiwaelekeza kwenda kwa hao viumbe hai wanne.
Ezekiel 1:13-16
Wakati wale viumbe hai wanne walipokuwa wakienda mbele na nyuma, walionekana kama nini?
Walipokuwa wakienda, wale viumbe hai wanne walionekana kama radi.
Ezekiel 1:17-18
Hayo magurudumu manne yalikuwa nini karibu na viumbe wanne kuweza kufanya?
Yale magurudumu manne yaliweza kwenda sehemu yoyote bila kugeuka.
Ezekiel 1:19-21
Kwa nini magurudumu yalienda popote viumbe hai vilipoenda?
Magurudumu yaliwafuata wale viumbe hai kwa sababu roho wa wale viumbe hai alikuwa katika yale magurudumu.
Ezekiel 1:22-23
Nini kilikuwa juu ya vichwa vya wale viumbe hai?
kulikuwa na kipara chenye kutanuka juu ya vichwa vya wale viumbe hai.
Hao viumbe hai walifanya nini na mabawa yao?
Kila mabawa ya kila kiumbe yalinyooka mbele na kugusa mabawa ya kiumbe kingine na kila kiumbe hai kilikuwa na jozi moja kwa ajili ya kujifunika mwili wake mwenyewe.
Ezekiel 1:24-25
Ezekieli alisema mabawa ya wale viumbe ulikuwa unaliaje?
Mlio wa mabawa ya wale viumbe ulikuwa kama maji yanayotimua, kama sauti ya Mwenye enzi, kama dhoruba ya mvua, na kama jeshi.
Ezekiel 1:26
Nini kilikuwa juu ya anga, ambacho kilikuwa juu ya vichwa vya viumbe?
Juu ya anga kulikuwa na kiti cha enzi, na juu ya kiti cha enzi kulikuwa na muonekano wa mmoja aliyeonekana kama mtu.
Ezekiel 1:27-28
kama mng'ao wa umbo la namna gani lilimtokea Ezekieli?
Umbo la mwanga ulionekana kama utukufu wa Yahwe.
Ezekieli alifanya nini alipoona umbo la mng'ao?
Wakati alipoona umbo la mng'ao, Ezekieli alisikia kwenye uso wake.
Ezekiel 2
Ezekiel 2:1-3
Roho alifanya nini kwa Ezekieli kama Roho alivonena kwa Ezekieli?
Roho alimsimamisha Ezekieli juu ya miguu yake alikuwa akinena na Ezekieli.
Roho alimtuma Ezekieli kwa nani?
ROho alimtuma Ezekieli kwa watu wa Israeli.
Ezekiel 2:4-5
Kutokana na Roho, ni watu wa aina gani waliokuwa uzao wa Israei?
Uzao walikuwa wakaidi, wenye mioyo migumu na watu waasi.
Ezekieli alikuwa aseme nini kwa watu wa Israeli?
Ezekieli alikuwa aseme, "Hivi ndivyo Yahwe asemavyo," kwa watu wa Israeli.
Watu wa Israeli walipaswa kufahamu nini kwa sababu ya Ezekieli kunena nao?
Watu wa Israeli wangejua kwamba nabii alikuwa miongoni mwao.
Ezekiel 2:6
Roho alimwambia Ezekieli asifanye sisi alipokuwa akinena na watu wa Israeli?
Roho alimwambia Ezekieli asiwaogope watu wa Israeli anapokuwa ananena nao.
Ezekiel 2:7-8
Je Ezekia alitakiwa kuwa tofauti vipi kuliko watu wa Israeli?
Ezekieli hakutakiwa kuwa muasi kama watu wa Israeli.
Ezekiel 2:9-10
Nini kilikunjuliwa mbele ya Ezekieli?
Hati ya kukunja iliyoandikwa ilikunjuliwa mbele ya Ezekia.
Nini kiliandikwa juu ya haiyo hati ya kukunja?
Juu ya hiyo hati kulikuwa kumeandikwa maombolezo, majonzi, na matatizo.
Ezekiel 3
Ezekiel 3:1-3
Roho alimpatia nini Ezekieli na Ezekieli alifanya nini pamoja nayo?
Roho alimpatia Ezekieli hati ya kukunja na Ezikieli akaila.
Ezekiel 3:4-7
Roho alimwambia Ezekieli aende wapi na kufanya nini?
Roho alimwambia Ezekieli na kunena maneno ya Roho kwenye nyumba ya Israeli.
Kutokana na Roho, kama Ezekieli angepelekwa kwa watu wageni, je wangejibu nini kwa maneno ya Ezekieli?
Kama Ezekieli nagepelekwa kwa watu wageni, wangesikiliza maneno ya Ezekieli.
Kutokana na Roho, je nyumba ya Israeli ingejibu nini kwa maneno ya Ezekieli?
Nyumba ya Israeli isingekuwa tayari kusikiliza maneno ya Ezekieli.
Ezekiel 3:8-11
Je Roho alimfanya nini Ezekieli ili asiwe na hofu wala kufadhaika?
Roho alimfanya Ezekieli mkaidi, na paji lake kama almasi.
Ezekiel 3:12-13
Sauti kubwa iliyokuwa nyuma ya Ezekieli ilisema nini?
Sauti kubwa ilisema, "Ubarikiwe utukufu wa Yahwe kutoka mahali pake!"
Ezekiel 3:14-15
Ezekieli alifanya baada ya siku saba, na hali yake ilikuwaje?
Ezekieli aliketi pamoja na mateka kwa mda wa siku saba, alishinda katika mshangao.
Ezekiel 3:16-19
Yahwe alisema alimfanya nini Ezekieli kwa ajili ya nyumba ya Israeli?
Yahwe alisema alimfanya Ezekieli mlinzi wa nyumba ya Israeli.
Yahwe alima nini kingetokea kwa Ezekieli kama angewaonya waovu kuhusu matendo yao maovu?
Kama Ezekieli angewaonya waovu, kisha Ezekieli angejiokoa mwenyewe.
Ezekiel 3:20-21
Yahwe alisema nini kingetokea kwa Ezekieli kama asingewaonye waovu kuhusu matendo yao maovu?
Kama Ezekieli asingewaonya waovu, Yahwe angaitaka damu yao kutoka kwenye mkono wa Ezekieli.
Yahwe alisema nini kingetokea kwa Ezekieli kama asingemuonya mtu mwenye haki ambaye ageukaye na kutendo yasiyo haki?
Kama Ezekieli asingemuonya mtu mwenye haki ambaye ageukaye Yahwe angeitaka damu yake kuto mkono wa Ezekieli.
Yahwe alisema nini kingetokea kwa mtu mwenye haki ambaye ageukaye na kutendo yasiyo haki?
Yahwe amesema mtu mwenye haki ambaye ageukaye na matendo yasiyo haku angekufa katika dhambi yake.
Yahwe alisema nini kingetokea kwa Ezekieli kama angemuonya mtu mwenye haki ambaye ageukaye na kutenda yasiyo haki?
Kama Ezekieli angemuonya mtu mwenye haki ambaye ageukaye, kisha Ezekieli angejiokoa mwenyewe.
Ezekiel 3:22-23
Ezekieli alifanya nini wakati alipoona utukufu wa Yahwe katika uwanda?
Wakati Ezekieli alipoona utukufu wa Yahwe, akaanguka kifudi fudi.
Ezekiel 3:24-25
Roho alimwambia Ezekieli kufanya nini?
Roho alimwambia ezekieli kwenda na kujifungia katika nyumba yake.
Ezekiel 3:26-27
Roho alisema Ezekieli asingeweza kufanya nini kwa maneno yake mwenyewe?
Roho alisema Ezekieli asingeweza kuionya nyumba ya Israeli kwa maneno yake mwenyewe.
Roho alisema Ezekieli angeweza kufanya nini wakati Roho atakapo nena naye?
Roho alisema Ezekieli angeweza kufungua kinywa chake na kusema, "Ndivyo Bwana Yahwe asemavyo," wakati Roho aliponena nay.
Ezekiel 4
Ezekiel 4:1-3
Yahwe alimwambia Ezekieli afanye nini na tofali?
Yahwe alimwambia Ezekieli kuuchonga mji wa Yerusalemu juu ya tofali na kisha kuilaza ngome juu yake.
Kwa nini Yahwe anamwambia Ezekieli kufanya hivi na tofali?
Yahwe alimwambia Ezekieli kufanya hivi kama ishara kwa nyumba ya Israeli.
Ezekiel 4:4-5
Kwa nini Yahwe anamwambia Ezekieli kulala upande wa kushoto kwake?
Yahwe alimwambia Ezekieli kulalia upande wa kushoto kwake kubeba dhambi ya nyumba ya Israeli.
Kwa nini Ezekieli alilalia upande wa kushoto kwa siku 390?
Ezekieli alikuwa alalie upande wake wa kushoto kwa siku 390 kuwakilisha miaka 390 ya kuiangamiza nyumba ya Israeli.
Ezekiel 4:6-8
Kwa nini Ezekieli alitakiwa kulalia upande wake wa kushoto?
Ezekieli alitakuwa kulalia upande wake wa kushoto ili kubeba dhambi ya nyumba ya Israeli.
Kwa nini Ezekieli alilalia upande wake wa kulia kwa siku 40?
Ezekieli alitakiwa kulalia upande wake wa kulia kwa siku 40 kuwakilisha miaka 40 ya adhabu kwa ajili ya nyumba ya Israeli.
Ezekiel 4:9-11
Yahwe alimwambia Ezekieli kula na kunywa nini wakati alipolalia upande wake?
Yahwe alimwambia Ezekieli kula shayiri na kunywa maji.
Ezekiel 4:12-13
Yahwe alimwambia Ezekieli kula na kunywa nini wakati anapolalia upande wake?
Yahwe alimwambia Ezekieli kula keki za sheyiri na kunywa maji.
Kwa nini Yahwe alimwambia Ezekieli kuoka kutumia kinyesi cha binadamu ndani ya uso wa nyumba ya Israeli?
Ezekieli alioka kutumuia kinyesi cha binadamu kama ishara kwamba chakula watu wa israeli watakachukula miongoni mwa mataifa wangekuwa najisi.
Ezekiel 4:14-15
Kwa nini Yahwe anamruhusu Ezekieli kutumia kinyesi cha ng'ombe badala ya kinyesi cha binadamu kuoka?
Yahwe aliruhusu kinyesi cha ng'ombe kwa sababu Ezekieli hajawahi kula chochote kinajisi katika maisha yake.
Ezekiel 4:16-17
Yahwe alisema nini kingetokea katika Yerusalemu kuhusu chakula na kinywaji?
Yahwe alisema huo mkate na maji vingegawiwa.
Yahwe alisema nini kingetokea kwa watu wa Yerusalimu katika kipindi hiki?
Yahwe aliwaambia watu wa Yerusalemu wangefadhaishwa na kumalizika.
Ezekiel 5
Ezekiel 5:1-4
Ezekieli alifanya nini kwa kila robo tatu ya nywele zake?
Ezekieli aliteketeza robo tatu katika mji, kupiga robo tatu kwa upanga kuzunguka mji, na kutawanya robo tatu kwenye upepo.
Yahwe alisema nini angefanya baada ya Ezekieli kumaliza?
Yahwe alisema angeusogeza upanga kuwafukuza watu.
Ezekiel 5:5-6
Kulingana na Yahwe, Yerusalemu iko wapi?
Yerusalemu iko kati ya mataifa.
Kwa nini Yahwe anasema ameizunguka Yerusalemu pamoja na nchi nyingine?
Yerusalemu ilikataa maagizo ya Yahwe na na kutotembea katika sheria zake (sheria).
Ezekiel 5:7-8
Yahwe anasema atafanya nini kwa sababu ya ya tabia ya Israeli?
Yahwe asema atatenda juu ya taifa la israeli na kutimiza hukumu kati yake.
Ezekiel 5:9-10
Ni mambo gani ya kuogofya watu wa Israeli wanafanya kwa sababu ya hukumu ya Yahwe juu yao?
Mababa watawala watoto wao, na wana watawala mababa zao.
Ezekiel 5:11-12
Kwa nini Yahwe anasema haendi kuwaangamiza watu wa Israeli?
Yahwe hatawaangamiza kwa sababu wameinajisi mahali patakatifu pa Yahwe.
Yahwe atafanya nini pamoja na kila robo tatu ya watu?
Robo tatu itakufa kwa tauni, robo tatu itaanguka kwa upanga, na robo tatu itatawanywa.
Yahwe anasema angefanya nini baada ya robo tatu ya watu waliokuwa wamehukumiwa?
Yahwe anasema angeusogeza upanga kuwafukuza watu.
Ezekiel 5:13-14
Yahwe anasema atafanya nini na hasira yake baada ya hukumu yake?
Yahwe asema hasira yake itakamilishwa baada ya hii hukumu yake.
Ezekiel 5:15-17
Watu wengine watasema nini kuhusu Yerusalemu baada ya hukumu ya Yahwe?
Watu wengine wataishutumu na kuidhihaki Yerusalemu baada ya hukumu za yahwe.
Ezekiel 6
Ezekiel 6:1-3
Ezekieli alitabiri nini juu ya mahali pa juu pa Israeli?
Ezekieli alitabiri Bwana Yahwe atapaangamiza mahali pa juu pa Israeli kwa upanga.
Ezekiel 6:4-5
Nini kitatokea mbele ya madhabahu za sanamu ya Israeli?
Bwana Yahwe ataziangusha maiti za watu wa israeli mbele ya madhabahu.
Ezekiel 6:6-7
Nini kitatokea kwenye miji ya Israeli?
Miji ya Israeli itaangushwa ovyo ovyo.
Kama matokeo yote ya uharibifu, watu wa Israeli watajua nini?
Watu wa Israeli watajua kwamba Bwana ni Yahwe.
Ezekiel 6:8-10
Masalia waliokimbia watafanya nini baada ya kutawanyika?
Masalia watamkumbuka Yahwe na kumuonyesha chuki juu ya nyuso zao kwa ajili ya udhaifu wao.
Ezekiel 6:11-12
Kwa nini Yahwe analeta upanga, njaa, na tauni kwenye nyumba ya Israeli?
Kwa sababu ya uovu wa ufisadi wa nyumba ya Israeli, Yahwe analeta upanga, njaa, na tauni.
Ezekiel 6:13-14
Watu wa Israeli walikuwa wakifanya nini juu ya vilele vya mlima na chini ya miti?
Watu wa Israeli walikuwa wakitoa kitu chenye harufu nzuri kwa sanamu zao zote.
Nini kitatokea kwenye nchi wakati Yahwe atakapo jinyoosha?
Nchi itakuwa ukiwa na isiyofaa wakati yahwe ajinyooshapo.
Ezekiel 7
Ezekiel 7:1-2
Kutokana na neno la Yahwe, nini kilikuwa kinakuja kwenye nchi ya Israeli?
Kutokana na neno la Yahwe, mwisho ulikuwa ukija kwenye nchi ya Israeli.
Ezekiel 7:3-4
Yahwe ataihukumu Israeli kutokana na nini?
Yahwe ataihuku Israeli kutokana na njia zao.
Ezekiel 7:5-7
Ni mda wa nini unakuja kwa ajili ya Israeli?
Mda wa maangamizi ya Israeli na uharibifu umekuja.
Ezekiel 7:8-9
Yahwe anamwaga nini na kujaza nini juu ya Israeli?
Yahwe anamwaga ghadhabu yake na kujaza na kujaza hasira yake juu ya Israeli.
Ezekiel 7:10-11
Ni kitu gani hakitabaki katika Israeli?
Hakuna kati ya kundi, hakuna katika utajiri wao, na hakuna katika vitu vya muhimu vitabakia.
Ezekiel 7:12-13
Kwa nini wanunuzi hawafurahii na wauzaji hawaombolezi katika Israeli?
Wanunuzi hawatafurahia na wauzaji hawatahuzunika kwa sababu hasira ya Yahwe i juu ya kundi zima.
Ezekiel 7:14-16
Je! Wale watu walio katika mji watakufaje?
Wale walio katika mji watakufa kwa njaa na tauni.
Watakao okoka watakimbilia wapi?
Watakao okoka watakimbilia milimani.
Ezekiel 7:17-19
Nini hakitaweza kupelekwa kwa watu wa Israeli?
Fedha zao na dhahabu hazitaweza kupelekwa kwa watu wa Israeli.
Ezekiel 7:20-22
Nini kitatokea kwa vitu vyote vya thamani vya mapambo za watu wa Israeli?
Mapambo yatatolewa kwenye mikono ya wageni na waovu kama mateka.
Nini kitatokea mahali pote pa Yahwe pa siri?
Maharamia wataingia mahali pa Yahwe pa siri na kupanajisi.
Ezekiel 7:23-25
Watu wa Israeli watatafuta nini, lakini hawatakipata?
Watu wa Israeli watatitafuta amani, lakini haitakuwepo.
Ezekiel 7:26-27
Nini kitatokea wakati watu watakapotafuta ono kutoka kwa nabii?
Wakati watu watakapotafuta ono, sheria na ushauri utawaangamiza.
Je! Mfalme na watu watajali vipi wakati hukumu ya Yahwe ijapo?
Wakati hukumu ijapo, mfalme ataomboleza na watu watatetemeka kwa hofu.
Ezekiel 8
Ezekiel 8:1-2
Ezekieli alikuwa wapi wakati mkono wa Bwana Yahwe ulipo gusa juu yake?
Ezekieli alikuwa ameketi katika nyumba yake, pamoja na wazee wa Yuda wameketi mbele yake.
Ezekiel 8:3-4
Roho alimchukua wapi Ezekieli, na nini aliona huko?
Roho alimchukua Ezekieli kwenye lango la ndani la Kaskazini katika Yerusalemu, ambapo aliona sanamu ambayo ichocheayo wivu.
Ezekiel 8:5-6
Roho alisema alilazimishwa kufanya nini kwa sababu ya chuki kubwa (uovu) wa nyumba ya Israeli?
Roho alisema alilazimishwa kwenda mbali na patakatifu pake mwenyewe.
Ezekiel 8:7-11
Baada ya Ezekieli kuchimba kwenye ukuta na kuona dirisha, Roho alimwambia Ezekieli nini cha kufanya?
Roho alimwambia Ezekieli, "Kwenda na kuona machukizo makubwa ya uovu ambayo wanaendelea vema huko."
Ezekiel 8:12-13
Wazee walikuwa wakisema nini kuhusu Yahwe walipokuwa wakiabudu sanamu?
Wazee walikuwa wakisema kwamba Yahwe hawaoni na kwamba Yahwe ameitelekeza nchi.
Ezekiel 8:14-15
Ezekieli aliona wanawake wakifanya nini kwenye lango upande wa kaskazini mwa nyumba ya Yahwe?
Wanawake walikuwa wameketi huko wakiomboleza kwa ajili ya Tamuzi.
Ezekiel 8:16
Ezekieli aliona nini katika ua wa ndani ya nyumba ya Yahwe?
Kulikuwa na watu ishirini na nne pamoja na nyuso zao kuelekea magharibi wakimwabudu Shameshi.
Ezekiel 8:17-18
Kwa sababu ya machukizo makubwa ya nyumba ya Israeli, Roho alisema nini alikuwa anaenda kufanya nini?
Roho alisema kwamba angetenda na kuwaharibu, bila huruma hata kama watalia kwa sauti kuu.
Ezekiel 9
Ezekiel 9:1-2
Roho alimuita nani kuja kwenye mji?
Roho aliwaita watu sita pamoja na silaha za uharibifu, na mtu mmoja na kifaa cha uandishi.
Ezekiel 9:3-4
Utukufu wa Mungu ulihama kutoka wapi, na ulienda wapi?
Utukufu wa Mungu wa Israeli ulihama kutoka kwenye kerubi ulipokuwa na kwenda kwenye kizingiti cha mlango wa nyumba.
Yahwe alimwambia mwandishe afanye nini?
Yahwe alimwambia mwandishi kufanya alama juu ya kizingiti cha mlango wa watu waliotambaa na kuona mbali kama machukizo kuwa yamefanywa katika mji.
Ezekiel 9:5-6
Yahwe aliwaambia nini cha kufanya wale watu sita pamoja na silaha za uharibifu?
Yahwe aliwaambia wale watu sita kuwaua watu wote isipokuwa wale wenye alama juu ya vichwa vyao.
Ezekiel 9:7-8
Ni swali gani Ezekieli alimuuliza yahwe alipowaona watu sita waliouharibu mji?
Ezekieli alimuuliza yahwe kama mabaki yote ya Israeli yangeangamizwa kwa hasira ya Yahwe.
Ezekiel 9:9-11
Jibu la Yahwe lilikuwaje kwa swali la Ezekieli?
Yahwe alijibu kwamba uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ulikuwa mkubwa, na kwamba asinge waharibu.
Taarifa ya mwandishi ilikuwaje?
Mwandishi alitoa taarifa kwamba aliyafanya yote Yahwe aliyokuwa amemwamuru.
Ezekiel 10
Ezekiel 10:1-2
Yahwe alimwambia nini cha kufanya yule mtu aliyekuwa amevalia katika utepe?
Yahwe alimwambia yule mtu aliyevalia katika utepe kuijaza mikono yake yote kwa mkaa wa mawe na kuwatawanya juu ya mji.
Ezekiel 10:3-5
Kisha utukufu wa Mungu ulifanya nini?
Kisha utukufu wa Mungu uliinuka na kusimama juu ya kizingiti cha mlango wa nyumba, kuijaza nyumba pamoja na wingu na ua na mng'ao.
Ezekiel 10:6-8
Je! yule mtu alivaaje katika utepe kupokea moto uliokuwa miongoni mwa kerubi?
Yule mtu aliyekuwa amevalia utepe aliingia ndani, na kerubi likasalia kwenye moto na kuliweka kwenye mikono ya yule mtu.
Ezekiel 10:9-11
Mfanano wa magurudumu ulikuwaje ambao ulikuwa karibu na kerubi?
Magurudumu ambayo yalikuwa karibu na kerubi yalikuwa kama gurudumu lililokingamana na kurudumu jingine.
Ezekiel 10:12-14
Nini kilifunika kerubi na magurudumu manne?
Macho yalifunika kerubi na yale magurudumu manne.
Yale magurudumu manne yalipewa majina gani?
Yale magurudumu manne yaliitwa "mzunguko"
Ezekiel 10:15-17
Magurudumu yalifanya nini kerubi lilipokuwa likizunguka?
Magurudumu yalienda karibu na kerubi wakati kerubi lilipokuwa likitembea.
Ezekiel 10:18-19
Utukufu wa yahwe, kerubi, na magurudumu vilielekea wapi?
Utukufu wa Yahwe, kerubi, na magurudumu vilielekea magharibi kuingia nyumba ya Yahwe.
Ezekiel 10:20-22
Ezekieli aliona viumbe hai wale wale kabla?
Ezekieli aliona viumbe hai wale wale mbele karibu na Kerubi kanali.
Ezekiel 11
Ezekiel 11:1
Ezekieli aliona nini wakati Roho alipomleta kwenda lango la magharibi mwa nyumba ya Yahwe?
Ezekieli aliona watu ishirini na nne, pamoja na viongozi wa watu miongoni mwao.
Ezekiel 11:2-4
Kwa nani Mungu alisema watu ishirini na tano walikuwa na hatia?
Mungu alisema wale watu ishirini na tano walikuwa na hatia ya kushauri udhalimu na kuamua mipango katika mji.
Ezekiel 11:5-7
Wale watu ishirini na tano waliijaza mitaa na nini?
Wale watu ishirini na tano waliijaza mitaa kwa watu waliokuwa wamewaua.
Ezekiel 11:8-10
Wale watu ishirini na tano waliogopa nini, na Yahwe alisema angeleta nini?
Wale watu ishirini na tano waliogopa upanga, na Yahwe kusema angeleta upanga juu yao.
Yahwe mikono ya nani Yahwe alikuwa anaenda kuwaweka wale watu ishirini na moja?
Yahwe alikuwa anaenda kuwaweka wale watu ishirini na tano kwenye mikono ya wageni.
Wale watu ishirini na tano walihukumiwa wapi na kwa sababu ya hukumu ya Yahwe juu yao, je wale ishirini na tano walijuaje?
Wale watu ishirini na tano walikuwa wahukumiwe ndani ya mipaka ya Israeli na kwa sababu ya hukumu ya Yahwe juu yao, wale watu wangejua kwamba Bwana ni yahwe.
Ezekiel 11:11-12
Ni amri zipi walizokuwa wamezibeba wale watu ishirini na tano?
Wale watu ishirini na tano walibeba amri za mataifa yaliyowazunguka.
Ezekiel 11:13-15
Ezekieli alikuwa akihofia nini kwamba Yahwe angelifanya kwa Israeli?
Ezekieli alihofiakwamba Yahwe angewaangamiza kabisa mabaki ya Israeli.
Ezekiel 11:16-18
Yahwe aliwapatia ahadi gani Israeli licha ya hukumu yao juu yao?
Yahwe aliahidi kuikusanya Israeli kutoka kwa watu, na kuwakusanya katika nchi ya Israeli.
Ezekiel 11:19-21
Yahwe aliahidi kuchukua nini kutoka kwa watu wa Israeli, na kuwapatia badala ya?
Yahwe aliahidi kuchukua moyo mgumu kutoka kwao, na kuwapatia moyo wa nyama.
Je! Watu wa Israeli walienendaje?
Watu wa israeli walienenda katika maagizo ya Yahwe na amri.
Yahwe alisema angefanya nini kwa ajili ya wale wanaoeneda kwa tabia ya kujifanya kuelekea mambo yao maovu?
Yahwe alisema angeleta mwenendo wao juu ya vichwa vyao wenyewe.
Ezekiel 11:22-23
Utukufu wa Yahwe ulitokea wapi kuondoka na utukufu wa Yahwe ulielekea wapi?
Utukufu wa Yahwe uliondoka kati ya mji na kusimama juu ya mlima magharibi mwa mji.
Ezekiel 11:24-25
Ezekieli alifanya nini wakati Roho alipomleta Kaldayo?
Ezekieli aliwatangazia wale mateka vitu vyote vya Yahwe alivyokuwa ameviona.
Ezekiel 12
Ezekiel 12:1-2
Yahwe anasema Ezekieli aliishi wapi?
Yahwe alisema Ezekieli aliishi katikati ya ya nyumba ya uasi.
Ezekiel 12:3
Ezekieli alitakiwa kufanya nini katika uso wa watu wa Israeli?
Ezekieli alitakiwa kujiandaa kwa ajili ya uhamisho, kutoka nje katika uso wao kwenda mahali pengine.
Ezekiel 12:4-7
Je! Yahwe alimwambiaje Ezekieli kutoka nje?
Yahwe alimwambia Ezekieli kuchimba shimo kupitia kwenye ukuta na kutoka nje kupitia humo.
Kulingana na Yahwe, sababu ya uhamisho wa Ezekieli ilikuwa nini?
Yahwe alisema kwamba uhamisho wa Ezekieli ilikuwa ishara kwenye nyumba ya Israeli.
Ezekiel 12:8-10
Ni swali gani nyumba ya Israeli ilimuuliza Ezekieli alipokuwa amekuja kutoka kwenye nyumba yake?
Nyumba ya Israeli ilikuwa ikiuliza, "Unafanya nini?"
Kitendo cha unabii cha Ezekieli kinamuhusu nani?
Kitendo cha Ezekieli cha kinabii kilimuhusu mwana wa mfalme katika Yerusalemu na na nyumba yote ya Israeli.
Ezekiel 12:11-13
Yahwe alisema nini kingemtokea mwana wa mfalme katika Yerusalemu?
Yahwe alismea kwamba mwana wa mfalme katika Yerusalemu atatoka nje kupitia ukuta, lakini atakamatwa na kuchukuliwa kwenda Babeli ambapo atakufa bila kuona.
Ezekiel 12:14-18
Yahwe alisema nini kingetokea kwa jeshi la mwana wa mfalme katika Yerusalemu?
Yahwe alisema jeshi litatawanyika, na angepeleka upanga kwao.
Ni sababu zipi mbili Yahwe alizitoa kwa ajili ya kuacha kuwaharibu watu?
Yahwe alisema angeacha kuwahahribu watu ili wasihifadhi machukizo ya Israeli, na hivyo wangejua kwamba Bwana ndiyr Yahwe.
Ezekiel 12:19-20
Je! Yahwe anasema watu wa nchi ya Israeli watakulaje na kunywa?
Yahwe alisema watu watakula mkate wao kwa kutetemeka na kunywa maji yao wakiwa wanatikisika.
Je! Yahwe anasema nini kingetokea kwa miji na nchi?
Yahwe alisema miji itahuzunika na nchi itakuwa takataka.
Ezekiel 12:21-23
Watu wa Israeli walifikiri nini kuhusu maono ya nabii?
Watu walifikiri kwamba kila ono la kinabii yalikuwa marefu na yametunzwa.
Ezekiel 12:24-25
Yahwe alisemaje hakutakuwa na nini tena kupitia nyumba ya Israeli?
Yahwe asema hakutakuwa na maono ya uongo tena au ubashiri wenye kufaa ndani ya nyumba ya Israeli.
Ezekiel 12:26-28
Ni lini nyumba ya Israeli ilidhani ono la kinabii wa Ezekieli ungekamilishwa?
Nyumba ya Israeli ilisema, 'Ono alilo liona ni kawa ajili ya siku nyingi kutoka sasa, na anatafsiri kwa nyakati za mbeli.'
Yahwe anasema nini kuhusu ukamilifu wa ono la Ezekia?
Yahwe alisema maneno yake hatachelewa tena lakini neno ambalo Yahwe alilinena litakamilishwa.
Ezekiel 13
Ezekiel 13:1-4
Kutoka wapi manabii wa uongo wa Israeli walikuwa wakipata unabii wao?
Manabii wa uongo katika Israeli walikuwa wakipata unabii wao kutoka kwenye akili zao wenyewe na roho.
Ezekiel 13:5-7
Manabii wa uongo walishindwa kufanya nini?
Manabii wa uongo walishindwa kutengeneza matofali katika ukuta kuzunguka nyumba ya Israeli.
Manabii wa uongo walikuwa wakisema nini, hata kama Yahwe hakuwatuma?
Manabii wa uongo walikuwa wakisema, "Hivi na hivi ndivyo Yahwe asemavyo," hata kama Yahwe hakuwatuma.
Ezekiel 13:8-12
Ni tangazo lipi Yahwe alilifanya juu ya manabii wa uongo wa Israeli?
Yahwe alitangaza kwamba mkono wake ulikuwa juu ya manabii wa uongo, na wasingeweza kujiandikisha katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli.
Ezekiel 13:13-14
Watu wangejua nini wakati Yahwe atakapowaharibu manabii wa uongo?
Watu watajua kwamba Bwana ni Yahwe.
Ezekiel 13:15-16
Yahwe alisema angefanya nini kwa ukuta na wale waupakao chokaa?
Yahwe alisema angeuangamiza ukuta na wale waupakao chokaa.
Manabii wa uongo walikuwa wakitabiri nini kwa watu kuhusiana na Yerusalemu?
Manabii wa uongo walikuwa wakitabiri amani kwa ajili ya Yerusalemu.
Ezekiel 13:17-19
"mwana wa mwanadamu" aliambiwa afanye nini kuhusu binti za watu wake ambao wanaotabiri kutokana na akili zao wenyewe?
"Mwana wa binadamu" aliambiwa kutabiri juu yao.
Irizi zilikuwaje na vitambaa vya shela vilitengenezwa vitumike kwa ajili ya nini?
Irizi na vitambaa vya shela vilivyokuwa vimetengenezwa na wanawake vilitumika kuwindia watu.
Ezekiel 13:20-21
Yahwe alisema angefanya nini kwa ajili ya watu wake ambao waliotengwa?
Yahwe alisema angewaacha watu wake waliotengwa kuwa huru.
Ezekiel 13:22-23
Manabii wa uongo walikuwa wakiwafanya nini wenye haki na watu waovu?
Manabii wa uongo walikuwa wakiwavunja moyo wenye haki na kuwatia moyo waovu.
Yahwe anasema manabii wa uongo hawatakuwa na nini?
Yahwe alisema manabii wa uongo hawatakuwa na maono au kuendelea kufanya utabiri wa uongo.
Ezekiel 14
Ezekiel 14:1-3
Nani alikuja kwa Ezekieli kumuulizia?
Wazee wa Israeli walikuja kwa Ezekieli kumuulizia.
Kwa nini Yahwe aliuliza kama kama angeuliziwa na hawa watu?
Yahwe aliuliza kwa sababu wazee walikuwa wamechukuliwa sanamu zao kwenye mioyo yao.
Ezekiel 14:4-5
Je! Yahwe alisema angewajibu vipi wale wachukuao sanamu kwenye mioyo yao?
Yahwe alisema angewajibu wale wachukuao sanamu kwenye mioyo yao kutokana na hesabu ya sanamu zao.
Ezekiel 14:6
Yahwe aliwaita nyumba ya Israeli kufanya nini?
Yahwe aliita nyumba ya Israeli kutubu na kugeuka kutoka sanamu zao.
Ezekiel 14:7-8
Yahwe angemfanya kila mtu aabuduye sanamu na kisha kutafuta kuuliza kutoka kwa nabii wa Yahwe?
Yahwe alisema angamfanya huyo mtu ishara na mithali kwa kumkatilia mbali kutoka kwa watu wa Israeli.
Ezekiel 14:9-11
Yahwe alisema angefanya nini kwa kila nabii atakayedanganya?
Yahwe alisema angemdanganya yule nabii na kumwangamiza.
Ni mahusiano gani Yahwe anasema aliyataka pamoja na watu wa Israeli?
Yahwe alisema aliwataka watu kuwa watu wake, na yeye kuwa Mungu wao.
Ezekiel 14:12-14
Wakati Yahwe atakapoleta hukumu, yote yatakuwa ambayo hata mwenye haki zaidi katika nchi atafanya nini?
Wakati Yahwe atakapoleta hukumu, hata mwenye haki zaidi ataweza kupeleka roho zao wenyewe.
Yahwe alimtumia nani kama mfano wa baadhi ya watu wenye haki zaidi katika historia?
Yahwe aliwatumia kama mifano ya watu wenye haki zaidi katika historia ni Nuhu, Danieli, na Ayubu.
Ezekiel 14:15-16
Yahwe aliwatumia akina nani kama mifano ya baadhi ya watu wenye haki zaidi katika historia?
Yahwe aliwatumia kama mifano baadhi ya watu wenye haki zaidi katika historia ni Nuhu, Danieli, na Ayubu.
Yahwe alileta lini hukumu, na mwenye haki zaidi katika hataweza kupelekwa?
Wakati Yahwe atakapoleta hukumu, mwenye haki zaidi katika nchi ataweza kupeleka wana au binti zake.
Ezekiel 14:17-18
Yahwe alimtumia nani kama mifano ya baadhi ya watu wenye haki zaidi katika historia?
Yahwe aliwatumia kama mifano ya baadhi ya watu wenye haki zaidi katika historia ya Nuhu, Danieli, na Ayubu.
Wakati Yahwe atakapoleta hukumu, nani atakuwa mwenye haki zaidi katika nchi haitaweza kupeleka?
Wakati Yahwe atakapoleta hukumu, mwenye haki zaidi katika nchi ataweza kupeleka wana na binti zake.
Ezekiel 14:19-20
Yahwe alimtumia nani kama mifano ya baadhi ya watu wenye haki zaidi katika historia?
Yahwe alitumia kama mifano ya baadi ya watu wenye haki zaidi katika historia ya Nuhu, Danieli, na Ayubu.
Yahwe analeta nini hukumu, nani angekuwa mwenye haki zaidi katika nchi sio kupelekwa?
Wakati Yahwe atakapoleta hukumu, wenye haki zaidi katika nchi wataweza kupleka wana wao au binti.
Ezekiel 14:21
Ni adhabu zipi nne ambazo Yahwe alisema angetuma kwa Yerusalemu?
Yahwe alisema angetuma adhabu nne ya njaa, wanyama pori, na tauni.
Ezekiel 14:22-23
Baada ya hukumu ya Yahwe, nani angeondoka?
Baada ya hukumu ya Yahwe, mabaki yatabaki ambayo watatoka pamoja na wana na binti.
Nini kilimfanya Ezekieli kutiw moyo?
Ezekieli aliona njia na matendo ya mabaki ya waliookoka, atiwa moyo.
Ezekiel 15
Ezekiel 15:1-4
Ni vitu gani viwili katika msitu ambavyo Yahwe anavilinganisha?
Yahwe analinganisha mzabibu na mti wowote wenye matunda.
Ezekiel 15:5-6
Bwana Yahwe alisema alitoa mzabibu kwa ajili ya nini?
Bwana Yahwe alisema alitoa mzabibu kama kuni kwa ajili ya moto.
Yahwe anaseje wenyeji wa Yerusalemu wako kama mzabibu?
Yahwe anasema wenyeji wa Yerusalemu wako kama mzabibu katika huo wote wamepatiwa ukuni kwa ajili ya moto.
Ezekiel 15:7-8
Wote watajua nini wakati Yahwe atakapo waangamiza wenyeji wa Yerusalemu kwa moto?
Wote watajua kwamba Bwana ni Yahwe.
Kwa nini Yahwe atafanya nchi kuwa ukiwa?
Yahwe ataifanya nchi kuwa ukiwa kwa sababu wenyeji wa Yerusalemu wamefanya dhambi.
Ezekiel 16
Ezekiel 16:1-3
Je! Yahwe alsema wapi mwazo na kuzaliwa kwake Yerusalemu?
Yahwe alisema Yerusalemu alikuwa na mwanzo wake na kuzaliwa katika nchi ya Kanaani.
Ezekiel 16:4-5
Nini kilifanyika Yerusalemu katika siku ilipozaliwa?
Yerusalemu alitupwa nje kwenye uwanda katika siku alipozaliwa.
Ezekiel 16:6-7
Yahwe alifanye nini kwa ajili ya Yerusalemu baada kuzaliwa kwake?
Yahwe aliifanya Yerusalemu kukua kama mmea katika shamba baada ya kuzaliwa kwake.
Ezekiel 16:8-12
Je! Yahwe alifanya nini kwa ajili ya Yerusalemu ilipofikisha umri wa kukomaa?
Yahwe alitandika joho lake juu ya Yerusalemu, na kuileta kwenye agano pamoja naye.
Ezekiel 16:13-14
Kwa nini umashuhuri wa Yerusalemu ulienda miongoni mwa mataifa?
Umaarufu wa Yerusalemu uleinda miongoni mwa mataifa kwa sababu ya uzuri wake.
Ezekiel 16:15-19
Je! Yerusalemu ilitendaje baada ya umaarufu wake kwenda miongoni mwa mataifa?
Yerusalemu alitenda kama kahaba baada ya umaarufu wake kwenda miongoni mwa mataifa.
Ezekiel 16:20-22
Je! Yerusalemu alifanya nnini na wana wake na binti waliozaliwa kwa ajili ya Yahwe?
Yerusalemu aliwatoa sadaka wana wake na binti kwa sanamu.
Ezekiel 16:23-26
Je! Yerusalimu alifanya nini katika kila sehemu penye watu wengi?
Yerusalemu alifanya madhabahu katika kila sehemu yenye watu wengi.
Ezekiel 16:27-31
Je! Yahwe alisema angekatilia mbali nini kwa sababu ya ukahaba wa Yerusalemu?
Yahwe alisema angekatilia mbali chakula chakula cha Yerusalemu kwa sababu ya ukahaba wake.
Ezekiel 16:32-34
Je! Yahwe alisemaje ni tofauti kati ya Yerusalemu na kila kahaba?
Yahwe alisema tofauti ni kwamba makahaba hulipwa kwa ajili ya matendo yao, lakini Yerusalemu huwalipa upendo wake na rushwa.
Ezekiel 16:35-39
Je! Yahwe alisema atamkusanya nani juu ya Yerusalemu?
Yahwe alisema atawakusanaya wote wanaompenda Yerusalemu juu yake katika kila upande.
Ezekiel 16:40-46
Je! mwonekano wa Yahwe ulikujwa mbele ya mabadiliko ya Yerusalemu baada ya kuadhibiwa kwake?
Baada ya Yerusalemu kuadhibiwa, Yahwe hatakuwa na hasira tena na Yerusalemu.
Ezekiel 16:47-48
Je! Nani alisema kwamba Yerusalemu alifanya uovu zaidi kuliko sehemu mbili nyingine zipi?
Yahwe alisema kwamba Yerusalemu alifanya uovu zaidi kuliko Sodoma na Samaria.
Ezekiel 16:49-55
Je! Sodoma alikataa kumsaidia nani?
sodoma alikataa kumsaidia maskini na mhitaji.
Ezekiel 16:56-58
Je! Watu waote waizungukayo Yerusalemu walifikiri nini kuhusu ule mji?
Watu wote wanayoizunguka Yerusalemu waliidharau na kuifanya kitu cha dharau.
Ezekiel 16:59
Yahwe alisema atamtendea Yerusalemu kama atakavyomtendea kila mmoja aliyefanya nini?
Yahwe alisema atamtendea Yerusalemu kama atakavyomtendea kila mmoja alidharau agano lao na kuvunja agano.
Ezekiel 16:60-61
Je! Yahwe angekumbuka nini na kuanzisha?
Yahwe alisema atakumbuka agano lake na Yerusalemu na kuanzisha agano la milele pamoja naye.
Ezekiel 16:62-63
Je! Jibu la Yerusalemu litakuwaje wakati Yahwe atakapoisamehe kwa ajili ya yote aliyoyafanya?
Yerusalemu ataaibika na hatanena tena kwa sababu ya aibu yake.
Ezekiel 17
Ezekiel 17:1-4
Yahwe alimwambia nini Ezekieli kuwasilisha na kunena kwenye ya Israeli?
Yahwe alimwambia Ezekieli kuwasilisha tega kitendawili na neno fumbo kwenye nyumba ya Israeli.
Katika fumbu, yule tai mkubwa alipanda wapi vionyo vya matawi ya mkangazi?
Yule tai mkubwa alipanda vionyo vya matawi ya mkangazi katika nchi ya Kanaani katika mji wa mabaharia.
Ezekiel 17:5-6
Katika fumbo, yule tai mkubwa alipanda wapi mbegu ya nchi, na ilimeaje?
Tai mkubwa alipanda mbegu kando kando ya maji mengi, na mzabibu aulitoa matawi na kuyatapanya.
Ezekiel 17:7-8
Katika fumbo, mzabibu ulifanya nini wakati tai mwingine mkubwa atakapokuja?
Mzabibu umegeuka kuwa mizizi kuelekea tai mwingine mkubwa.
Ezekiel 17:9-10
Yahwe alisema nini kitatokea kwenye mzabibu kwenye fumbo?
Yahwe alisema kwamba mzabibu utanyauka kabisa katika kiwanja chake.
Ezekiel 17:11-12
Mfalme wa Babeli alifanya nini na mfalme wa Yerusalemu?
Mfalme wa Babeli alimchukua mfalme wa Yerusalemu kwenda Babeli.
Ezekiel 17:13-14
Mfalme wa Babeli alifanya nini na uzao wa kifalme wa mfalme wa Yerusalemu?
Mfalme wa Babeli alfanya agano pamoja na uzao wa kifalme wa mfalme Yerusalemu.
Je! Yahwe anasema nchi ya Israeli itaokokaje?
Yahwe alisema nchi ya Yerusalemu itaokoka kwa mfalme wa Yerusalemu kutunza agano lake pamoja na mfalme wa Babeli.
Ezekiel 17:15-18
Je! Mfalme wa Yerusalemu alikiukaje agano alilolifanya pamoja na mfalme wa Babeli?
Mfalme wa Yerusalemu aliasi na kupeleka wajumba kwenda Misri kutaka farasi na jeshi.
Yahwe alisema nini kitatokea kwa mfalme wa yerusalemu?
Yahwe alisema mfalme wa Yerusalemu atakufa katikati ya Babeli.
Ezekiel 17:19-21
Kutokana na Yahwe, mfalme wa Yerusalemu alivunja agano la nani hasa?
Kutokana na Yahwe, mfalme wa Yerusalemu hasa alivunja agano lake pamoja na Yahwe.
Yahwe alitangaza nini kitatokea kwenye majeshi ya mfalme wa Yerusalemu?
Yahwe alitangaza majeshi ya mfalme wa Yerusalemu yataanguka kwa upanga.
Ezekiel 17:22-24
Yahwe anasema angefanya nini na matawi laini ya mti wa mkangazi?
Yahwe alisema angepanda matawi laini pamoja juu ya mlima mrefu.
Matawi laini ambayo Yahwe ayapandayo yatakuwaje?
Matawi laini Yahwe ayapandaye yatakuwa mkangazi wa fahari ambapo kila bawa la ndege litaishi.
Ezekiel 18
Ezekiel 18:3-6
Yahwe anasema nini kitatokea kwa kila mtu atendaye dhambi?
Yahwe anasema kwamba kila mtu atendaye dhambi atakufa.
Ezekiel 18:7-11
Mtu mwenye haki atamsaidia nani?
Mtu mwenye haki humpatia chakula mwenye njaa na kumfunika mtupu kwa mavazi.
Mwenye haki anaenenda nini na kutunza?
Mtu mwenye haki huenenda katika sheria za Yahwe na kutunza amri za Yahwe.
Yahwe anasema nini kitatokea kwa mtu mwenye haki?
Yahwe anasema mtu mwenye haki ataishi
Ezekiel 18:12-15
Kama mtu mwenye haki ana mtoto ambaye huwakandamiza maskini na wahitaji, Yahwe anasema nini kitatoke juu yake?
Yahwe anasema kwamba mwana asiye haki hataishi.
Ezekiel 18:16-18
Kama mwana hataenenda katika dhambi za babaye, je huyo mwana atakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake?
Kama mwana akizibeba amri za Yahwe na kuenenda kulingana na maagizo ya Yahwe, kisha hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake.
Ezekiel 18:19-20
Kwa nini mwana wa mwenye haki asibeubebe uovu wa baba yake?
Mwana wa mwenye haki hawezi kubeba uovu wa baba kwa sababu hubeba yaliyo halali na haki.
Ezekiel 18:21-23
Yahwe anatangaza nini kitatokea kwa mtu muovu ageukaye kutoka njia zake zote?
Yahwe anatangaza wamba mtu muovu ageukaye kutoka dhambi zake zote hakika ataishi.
Ezekiel 18:24-28
Yahwe alitangaza nini kitatokea kwa mtu mwenye haki ambaye ageukaye na kufanya dhambi na kutenda maovu?
Yahwe alitangaza kwamba mtu mwenye haki ageukaye na kufanya uovu atakufa katika dhambi alizozifanya.
Ezekiel 18:29-30
Je! Yahwe anasemaje atamuhukumu kila mtu?
Yahwe asema atamuhukumu kila mtu kulingana na njia zake.
Yahwe anawaita nyumba ya Israeli kufanya nini?
Yahwe anawaita nyumba ya Israeli kutubu na kugeuka kutoka dhambi zake zote.
Ezekiel 18:31-32
Yahwe aliwaita nyumba ya Israeli kufanya nini kwa ajili yao wenyewe?
Yahwe aliita nyumba ya Israeli kufanya moyo mpya na roho mpya kwa ajili yao wenyewe.
Ezekiel 19
Ezekiel 19:1-4
Ezekieli aliambiwa ainue nini?
Ezekieli aliambiwa ainue maombolezo juu ya viongozi wa Israeli.
Katika fumbo la simba, mmoja wa wtoto wa simba alijifunza kufanya nini?
Mmoja wa watoto wa simba alijifunza kuwinda na kuwameza watu.
Wakati mataifa waliposikia kuhusu mtoto wa simba, walifanya nini?
Mataifa walimtega mtoto wa simba na kumleta kwenye nchi ya Misri.
Ezekiel 19:5-7
Baada ya mtoto wa simba kwenda, yule mwana simba wa pili alijifunza kufanya nii?
Yule mwana simba alijifunza kuwararua kuwinda mawindo yake na kuwala watu.
Ezekiel 19:8-9
Mataifa yalifanya nini na mwana simba?
Mataifa yalimkamata mwana simba na kumleta kwa mfale wa Babeli
Ezekiel 19:10-11
Mama wa Israeli alikuwaje?
Mama wa Israeli alikuwa kama mzabibu uzaao matunda uliopandwa kando ya maji.
Matawi yake imara yalitumika kwa ajili ya nini?
Matawi yake imara yalitumika kwa ajili ya fimbo ya utawala
Ezekiel 19:12-13
Nini kilitokewa kwenye mzabibu?
Mzabibu uling'olewa, kwenda chini, na kukaushwa kwa upepo wa mashariki.
Mzabibu uko wapi?
Mzabibu upo katika jangwa.
Ezekiel 19:14
Mzabibu hauna nini tena?
Mzabibu hauna matawi imara wala fimbo ya utawala.
Ezekiel 20
Ezekiel 20:1
Je! Nani walikuja kwa Ezekieli na kwa nini walikuja?
Wazee wa Israeli walikuja kwa Ezekieli kumuuliza Yahwe.
Ezekiel 20:2-3
Je! Majibu ya Yahwe yalikuwaje kwa wale waliokuja kwa Ezekieli?
Yahwe alisema kwamba asiulizwe na wazee wa Israeli.
Ezekiel 20:4-6
Je! Yahwe aliapa atafanya nini kwa ajili ya Israeli wakati walipokuwa katika nchi ya Misri?
Yahwe aliapa kwamba atawaleta kwenye nchi inayotiririka maziwa na asali.
Ezekiel 20:7
Je! Ni amri gani Yahwe aliwapatia watu wa Israeli katika nchi ya Misri?
Yahwe aliwaamuru watu kutupa mbali sanamu zao za Misri.
Ezekiel 20:8-9
Je! Watu wa Israeli waliitikiaje amri ya Yahwe?
Watu waliasi juu ya Yahwe na hawakuwa tayari kusikiliza.
Kwa nini Yahwe alisema alitenda kuwaleta watu wa Israeli kutoka nchi ya Misri?
Yahwe alisema alitenda kwa ajili ya jina lake ili kwamba lisinajisiwe katika macho ya mataifa.
Ezekiel 20:10-12
Je! Yahwe aliwapatia nini watu wa Israeli katika jangwa?
Yahwe aliwapatia watu wa Israeli maagizo yake, sheria na Sabato.
Je! Yahwe aliwapatia nini watu kuweza kufanya kama wangetii sheria zake?
Yahwe aliwaambia watu wangeweza kuishi kama wangezitii sheria zake.
Ezekiel 20:13-14
Je! Watu wa Israeli waliitikiaje kwa kile Yahwe alichowapatia jangwani?
Watu waliasi juu ya Yahwe na kuyakataa maagizo yake.
Je! Yahwe aliwaambia nini watu wataweza kufanya kama wakitii maagizo yake?
Yahwe aliwaambia watu wataweza kuishi kama wangetii maagizo yake.
Ezekiel 20:15-20
Je! Yahwe aliapa hatafanya nini kwa ajili ya watu wa Israeli kwa sababu wameyakataa maagizo yake?
Kisha Yahwe aliapa hatawaleta kwenye nchi aliyokuwa anaenda kuwapatia.
Ezekiel 20:21-22
Je! wana na binti wa Israeli walijibu vipi wakati Yahwe alipowaamuru kuenenda katika maagizo yake?
Wana na binti wa Israeli waliasi juu ya Yahwe na kuacha kutunza maagizo yake.
Je! Yahwe aliwaambia nini watu wataweza kufanya kama wakitii maagizo yake?
Yahwe aliwaambia watu wataweza kuishi kama wakiyatii maagizo yake.
Ezekiel 20:23-26
Ywake aliapa kufanya nini kwa wana na binti za Isareli?
Yahwe aliapa kuwatawanya miongoni mwa mataifa.
Ezekiel 20:27-29
Je! mababa a Israeli walimkufuru vipi na kumsaliti Yahwe?
Mababa wa Israeli walimkufuru na kumsaliti Yahwe kwa kutoa sadaka kwa sanamu mahali pa juu.
Ezekiel 20:30-32
Je! Watu wa Israeli walikuwa wakifanya nini pamoja na wana wao?
Watu wa Israeli walikuwa wakisababisha wana wao kupitia kwenye moto.
Je! Ni wazo gani lilikuwa katika akili za watu wa Israeli?
Watu wa Israeli walikuwa wakifikiria wanataka kuwa kama mataifa mengine, kuabudu mti na jiwe.
Ezekiel 20:33-35
Je! Yawe alisema atafanya nini kwa watu wa Israeli ili kuwahukumu uso kwa uso?
Yahwe alisema atawakusanya watu wa Israeli kutoka nchi walizokuwa wametawanyika kwenye jangwa la watu.
Ezekiel 20:36-39
Je! Yahwe alisema atawasafisha kutoka nini miongoni mwa watu wa Israeli?
Yahwe alisema atawasafisha kutoka miongoni mwa watu wa Israeli
Ezekiel 20:40-41
Baada ya Yahwe kuikusanya nyumba ya Israeli katika mlima wake mtakatifu, je Israeli alimtendaje Yahwe?
Baada ya Yahwe kuikusanya nyumba ya Israeli katika mlima wake mtakatifu, Israeli atamtenda Yahwe kama mtakatifu katika uso wa mataifa.
Ezekiel 20:42-44
Je! Nyumba ya Israeli ilifikiri nini kuhusu wao wenyewe walipokumbuka nja zao mbaya za nyuma?
Nyumba ya Israeli watajichukia wenyewe kwa ajili ya matendo yao maovu waliyafanya.
Ezekiel 20:45-47
Je! Ni tangazo gani ambalo Yahwe alilifanya juu ya msitu wa Negebu?
Yahwe alitangaza kwamba atawasha mto ambao utauchoma kila uso kutoka kusini hata kaskazini.
Ezekiel 20:48-49
Je! Watu wa Israeli walikuwa wakisema nini kuhusu Ezekieli?
Watu wa Israeli walikuwa wakisema Ezekieli alikuwa akinena mafumbo matupu.
Ezekiel 21
Ezekiel 21:1-5
Yahwe alimwambia Ezekieli anene juu ya nani?
Yahwe alimwambia Ezekieli kunena juu ya patakatifu; juu ya nchi ya Israeli.
Yahwe anasema atamkatilia mbali nani kutoka nchi ya Israeli?
Yahwe alisema atawakatilia mbali wote mwenye haki haki na mtu muovu kutoka kwenye nchi ya Israeli.
Ezekiel 21:6-9
Yahwe alimwambia Ezekieli kufanya nini mbele ya macho ya watu?
Yahwe alimwambia Ezekieli kutambaa mbele ya macho ya wale watu.
Kwa nini Yahwe alimwambia Ezekieli kufanya hivi mbele ya macho ya watu?
Yahwe alimwambia Ezekieli kufanya hivi kuonyesha ambavyo itakavyokuwa kwa ajili yao wakato Yahwe atapoleta upanga juu yao.
Ezekiel 21:10-11
Nani alikuwa apatiwe upanga uliosuguliwa na kung'arishwa?
Ule upanga uliokuwa umesuguliwa na kung'ariwa ulikuwa apatiwe kwenye mkono wa muuaji.
Ezekiel 21:12-14
Huo upanga utakuja juu ya nani?
Huo upanga utakuja juu ya watu wa Yahwe na viongozi wa Israeli.
Ezekiel 21:15-17
Nini kitakuja kwa waliosalia baada ya machinjio makubwa?
Baada ya machinjio makubwa, ghadhabu ya Yahwe itakaposalia.
Ezekiel 21:18-20
Hatma ya zile barabara mbili kwa ajili ya mfalme wa Babeli ilikuwaje?
Hatma mbili zilikuwa Raba wa Amoni, na Yuda wa Yerusalemu.
Ezekiel 21:21-24
Je! Mfalme wa Babeli alibainishaje ni njia ipi ya kuenenda?
Mfalme wa Babeli alijipatia ujumbe wa nabii kutoka utabiri kubainisha njia ipi ya kuenenda.
Mfalme wa Babeli aliishtaki Israeli kwa ajili ya nini ili kuwashambulia?
Mfalme wa Israeli aliwashtaki Israeli kwa ajili kukiuka mkataba ili kwashambulia.
Ezekiel 21:25-27
Yahwe anamwambia kufanya nini mtawala muovu wa Israeli, na kwa nini?
Yahwe alimwambia mtawala muovu wa Israeli kuondoa kilemba chake na taji, kwa sababu taji haitaishi tena.
Yahwe alisema atairusha lini taji katika Israeli?
Yahwe alisema atairudisha taji katika Israeli wakati atakapokuja yule aliyekuwa na haki kwa hiyo.
Ezekiel 21:28-29
Manabii wa Amoni wamefanya nini kwa ajili ya watu wa Amoni?
Manabii wa Amoni wameona maono yasiyo na maana kwa ajili ya watu wa Amoni, wakati wafanyapo matambika ili kuja na waongo kwa ajili ya watu wa Amoni.
Ezekiel 21:30-32
Bwana Yahwe alikuwa anaenda kuwatoa watu wa Amoni kwa nani?
Bwana Yahwe alikuwa akienda kuwatoa Waamoni kwenye mkono wa watu wakaidi, mafundistadi wa uharibifu.
Ezekiel 22
Ezekiel 22:1-3
Ni jina gani ambalo Yahwe anaupa mji wa Yerusalemu ambao anauhukumu?
Yahwe anauita mji wa Yerusalemu mji wa damu.
Ezekiel 22:4-5
Ni dhambi gani mbili ambazo Yahwe amezitaja kwamba zimeufanya mji kuwa na hatia?
Mji una hatia ya damu iliyomwagwa, na umefanywa najisi na sanamu zilizofanywa.
Ni picha gani ambayo mji utakuwa nayo baada ya Yahwe kuihukumu?
Picha ijulikanayo kila mahali utakuwa kwamba mji wa machafuko.
Ezekiel 22:6-9
Ni makundi yapi matatu ya watu yamekuewa yakiwatenda vibaya na watawala wa Israeli?
Wababa na wamama wamekuwa hawana heshima, wageni walikuwa wakiwakandamiza, na yatima na wajane wamekuwa wakitendewa mabaya.
Ezekiel 22:10-12
Ni dhambi zipi tatu za kujamiiana zilizofanywa na watu katika mji?
Watu wanaofanya dhambi na mke wa jirani yake, wanawafanywa wakwe zao wa kike najisi, na kuwatusi dada zao.
Ezekiel 22:13-16
Yahwe anasema anaenda kuwafanya nini watu kwa sababu ya dhambi zao?
Yahwe anasema anaenda kuwatawanya watu miongoni mwa mataifa.
Watu watajua nini baada ya Yahwe kuwapiga?
Watu wajua kwamba Bwana ni Yahwe.
Ezekiel 22:17-19
Katika fumbo lake, Yahwe anaifananisha nyumba ya Israeli na nini?
Katika mfano wake, Yahwe anaifananisha na nyumba ya Israeli isiyofaa.
Yahwe anasema ataukusanya uchafu wapi?
Yahwe anasema ataukusanya uchafu kwenye katikati ya Yerusalemu.
Ezekiel 22:20-25
Yahwe atafanya nini kwenye uji wa chuma atakapokuwa akiimwaga ghadhabu yake?
Yahwe atamwaga uji wa chuma na kuuyeyusha chini atakapokuwa anamwaga ghadhabu yake.
Ezekiel 22:26-29
Makuhani wa nchi wanashindwa kutofautisha nini na kushindwa kufundisha?
Makuhani wanashindwa kutofautisha patakatifu na kunajisi vitu, na kushindwa kufundisha tofauti kati ya najisi na isiyonajisi.
Manabii wa nchi wanafanya nini?
Manabii wa nchi wanapaka kwa chokaa, kuona maono ya uongo na kufanya utabiri wa uongo.
Ezekiel 22:30-31
Yahwe alikuwa akitafuta nini na hakukiona?
Yahwe alikuwa akimtafuta mtu ambaye angejenga ukuta na kusimama mbele yake katika kuvunja mkataba kwa ajili ya nchi, lakini hakumkuta mtu.
Ezekiel 23
Ezekiel 23:1-4
Katika fumbo la Yahwe, je! wale binti wawili wanafanya nini Misri?
Wale binti wawili hutenda kama makahaba katika Misri.
Je! Yule binti mkubwa anawakilisha nini na yule binti mdogo anawakilisha nini?
Yule binti mkubwa huwakilisha Samaria na yule binti mdogo anawakilisha Yerusalemu.
Ezekiel 23:5-7
Je! Yule dada mkubwa alifanya nini ingawa alikuwa wa Yahwe?
Yule dada mkubwa alijitoa mwenyewe kama kahaba kwa watu wa Ashuru.
Ezekiel 23:8-10
Je! wale wapenzi wa yule binti mkubwa walifanya nini kwake wakati Yahwe alipompatia juu yao?
Wale wapenzi wa dada mkubwa waliufunua uchi wake, akawachukua wana na binti zake, na kumuua.
Ezekiel 23:11-17
Je! Yule binti mdogo alifanya nini wakati alipoona kilichotokea kwa yule binti mkubwa?
Yule binti mkubwa alitenda kama kahaba hata zaidi kuliko dada yake.
Ezekiel 23:18-21
Kwa sababu ya ukahaba wao, je mwonekano wa Yahwe ulibadilikaje mbele ya wale dada wawili?
Kwa sababu ya ukahaba wao, Yahwe aliurudisha moyo wake kutoka kwa wale dada wawili.
Ezekiel 23:22-23
Je! Yahwe alisema atafanya nini kwa yule dada mdogo kwa sababu ya ukahaba wake?
Yahwe alisema atawarudisha wapenzi wake juu yake.
Ezekiel 23:24-27
Je! Yahwe anasema nini kitatokea kwa yule dada mdogo na uzao wake?
Yule dada mdogo atakatwa na pua na maskio yake, na uzao wake utaliwa kwa moto.
Ezekiel 23:28-29
Je! Nini kitafunuliwa wakati dada mdogo anapotolewa kwenye mkono wa yule amchukiaye?
Aibu ya utupu wa ukahaba wa yule dada mdogo utafunuliwa.
Ezekiel 23:30-31
Kwa sababu ya ukahaba wao, je! Yahwe aliweka nini kwenye mikono ya dada mdogo na mkubwa?
Kwa sababu ya ukahaba wao, Yahwe ataweka kikombe cha adhabu kwenye mikono ya dada mdogo na mkubwa.
Ezekiel 23:32-35
Je! yule dada mdogo atakuwaje kwa wale waliomzunguka?
Yule dada mdogo atakuwa dhihaka na kutawaliwa na dharau kwa wale waliomzunguka.
Ezekiel 23:36-37
Je! Wale dada wawili walikuwa wakifanya nini pamoja na wana wao waliozaliwa kwa ajili ya Yahwe?
Wale dada wawili walikuwa walikuwa wakiwapitisha wana walizaliwa kwa ajili ya Yahwe kupitia moto kwa ajili uya kuliwa.
Ezekiel 23:38-42
Je! Wale dada wawili walifanya nini siku moja waliyochinja watoto wao?
Siku hiyo hiyo walipowachinja watoto wao, wale dada wawili walikuja patakatifu pa Yahwe kupanajisi.
Ezekiel 23:43-45
Je! Yahwe anasema watu wenye haki watawafanya nini makahaba?
Yahwe anasema watu wenye haki watawashutumu makahaba kwa adhabu kwa ajili ya uzinzi.
Ezekiel 23:46-47
Je! Kundi la watu litafanya nini kwamba Yahwe ainukapo juu ya makahaba?
Kundi la watu ambalo Yahwe atakaloliinua litawapiga mawe makahaba kwa mawe na kuwakatilia chini kwa panga zao.
Ezekiel 23:48-49
Je! makahaba watajua nini wakati watakapobeba hatia ya dhambi zao pamoja na sanamu zao?
Wakati watakapobeba hatia ya dhambi zao pamoja na sanamu zao, makahaba watajua kwamba Bwana ni Yahwe.
Ezekiel 24
Ezekiel 24:1-2
Yahwe anasema nini kilikuwa kikitokea juu ya siku sahihi aliponena Ezekieli?
Yahwe alisema kwamba mfalme wa Babeli alikuwa akiishambulia Yerusalemu katika siku hiyo sahihi.
Ezekiel 24:3-5
Katika fumbo wa Yahwe, Yahwe anawaambia nini wa Yerusalemu wafanye nini?
Yahwe anawaambia kumwaga maji kwenye chungu cha kuchemshia, kukijaza kwa mifupa bora, na ichemshe kikamifu.
Ezekiel 24:6
Kuna tatizo gani kuchemsha chungu cha Yerusalemu ambacho hakitatoka nje ya hicho?
Kuchemsha chungu cha Yerusalemu chenye kutu katika hicho hiyo haitatoka nje ya hicho.
Ezekiel 24:7-10
Yerusalemu imefanya nini kushurutisha kisasi kutoka kwa Yahwe?
Yurusalemu haijapona damu ambayo ipo katikati yake.
Ezekiel 24:11-13
Kwa nini kuweka chungu kitupu juu ya moto?
Chungu kitupu juu ya moto kwa ajili ya kuchemsha na kuchoma shaba, hivyo uchafu wake ndani yake utayeyushwa, kutu yake imekula!
Kitu gani hakikutolewa kutoka Yarusalemu kwa moto?
Kutu ya Yerusalemu haikuwa imetolewa kwa moto.
Ezekiel 24:14
Kutokana na Yahwe, ni kwa namna gani watu wa Yerusalemu watahukumiwa?
Watu wa Yerusalemu watahukumiwa kwa njia zao na shughuli zao.
Ezekiel 24:15-18
Yahwe alisema alikuwa akichukua nini kutoka kwa Ezekieli?
Yahwe alisema alikuwa akimchukua mke wa Ezekieli kutoka kwake.
Yahwe alimwambia Ezekieli asichukue nini?
Yahwe alimwambia Ezekieli asiomboleze wala kulia kwa kumpoteza mke wake.
Ezekiel 24:19-21
Yahwe alisema nini kilikuwa kama maana ya matukio ambayo yalitokea kwa Ezekieli?
Yahwe alisema kwamba tamaa ya macho ya watu yalipanajisi patakatifu, hivyo binti zao na wana wataanguka kwa upanga.
Ezekiel 24:22-24
Watu wa Yerusalemu watafanya nini wakati wakisumbuka kupotelewa kwao?
Watu watafanya hasa kama Ezekieli alivyofanya, na sio kuomboleza wala kulia.
Ezekieli aliwatumikia watu wa Yerusalemu kama nini?
Ezekieli aliwatumikia kama ishara kwa ajili ya watu wa Yerusalemu.
Ezekiel 24:25-27
Yahwe alisema nini kingetokea juu ya siku hekalu lilipochukuliwa?
Yahwe alisema juu ya siku hekalu lilipochukuliwa, wakimbizi watakuja kwa Ezekieli kumpatia habari.
Katika siku ambayo hekalu lilichukuliwa, watu wa Yerusalemu watajuaje?
Katika siku hekalu litakapochukuliwa, watu wa Yerusalemu watajua kwamba Yahwe ni Bwana.
Ezekiel 25
Ezekiel 25:1-2
Yahwe alimwambia Ezekieli atabiri juu ya nani?
Yahwe alimwambia Ezekieli kutabiri juu ya watu wa Amoni.
Ezekiel 25:3-5
Watu wa Amoni walifanya nini wakati patakatifu palipo najisiwa na nyumba ya Yuda kwenda utumwani?
Wakati patakatifu paliponajisiwa na nyumba ya Yuda kwenda utumwani, watu wa Amoni walisema, "Aha!"
Yahwe atafanya nini kwa watu wa Amoni kwa sababu ya kile walichokisema wakati nyumba ya Yuda ilipokwenda utumwani?
Yahwe atawatoa watu wa Amoni kwa watu katika magharibi.
Ezekiel 25:6-7
Yahwe atafanya nini kwa Amoni ambacho kitawasababisha kujua kwamba Yahwe ni Bwana?
Yahwe atamkatilia mbali Amoni kutoka watu wengine na kuwaangamiza.
Ezekiel 25:8-11
Moabu na Seiri walisema nini wakati nyumba ya Yuda ilipoenda utumwani?
Wakati nyumba ya Yuda ilipoenda utumwani, Moabu na Seiri walisema kwamba nyumba ya Yuda ilikuwa kama kila taifa jingine.
Nini hakitakumbukwa miongoni mwa mataifa?
Watu wa Amoni hawatakumbukwa tena miongoni mwa mataifa.
Ezekiel 25:12-14
Edomu alifanya nini juu ya nyumba ya Yuda?
Edomu alilipiza kisasi juu ya nyumba ya Yuda.
Yahwe atafanya nini kwa Edomu kwa sababu ya kile Edomu alichokifanya kwenye nyumba ya Yuda?
Yahwe atamwangamiza kila mtu na mnyama katika Edomu.
Ezekiel 25:15-17
Wafilist walifanya nini juu ya nyumba ya Yuda?
Wafilisi walilipa kisasi pamoja na dharau juu ya nyumba ya Yuda.
Yahwe atafanya nini kwa Wafilisti kwa sababu ya kile Wafilisti walichokifanya kwenye nyumba ya Yuda?
Yahwe atawaangamiza Wafilist.
Ezekiel 26
Ezekiel 26:1-2
Watu wa Tire walikuwa wakisema nini juu ya Yerusalemu?
Watu wa Tire walikuwa wakisema watajazwa kama Yerusalemi ilivyokuwa imeharibiwa.
Ezekiel 26:3-4
Yahwe anasema ataifanya nini Tire?
Yahwe alisema angeyafufua mataifa mengi juu ya Tire, ambayo yangeziangamiza kuta zake na minara.
Ezekiel 26:5-6
Yahwe anasema nini kitafanyika Tire itakapo simama?
Yahwe amesema kwamba nyavu zitakaushwa Tire isimamapo.
Ezekiel 26:7-8
Yahwe anasema atamleta nani Tire?
Yahwe alisema alikuwa akimleta Nebukadneza, mfalme wa Babeli, dhidi ya Tire.
Ezekiel 26:9-11
Yahwe anasema kuta za Tire zitaangushwaje chini?
Yahwe alisema zile kuta za Tire zitaangushwa chini na vitu vya kubomolea vya Nebukadneza.
Ezekiel 26:12-14
Yahwe anasema lile jiwe na kuni za nyumba ya Tire zitalazwa wapi?
Yahwe alisema lile jiwe na kuni za nyumba ya Tire zitalazwa katikati ya maji.
Ezekiel 26:15-16
Wakuu wa bahari watafanya nini wakati mauaji mabaya yatokeapo katika Tire?
Wakuu wa bahari watashuka chini kutoka kwenye kiti cha utawala, watalaza majoho yao, watavua nguo zao zenye rangi, na kuketi juu ya nchi wakitetemeka.
Ezekiel 26:17-18
Wakuu ya bahari wanaombolezea kwamba ule mji maarufu wa Tire uko wapi?
Wakuu wa bahari wanaomboleza kwamba ule mji maarufu wa Tire upo katika bahari sasa.
Ezekiel 26:19-21
Yahwe amesema atawaleta watu wa Tire kwenda wapi?
Yahwe amesema watu wa Tire wataletwa chini hata kwenye shimo.
Kutokana na Yahwe, Tire itaonekana lini tena?
Kutokana na Yahwe, Tire haitaonekana tena.
Ezekiel 27
Ezekiel 27:1-5
Je! Tiro ilikuwa maarufu kwa biashara gani?
Watu wa Tiro walikuwa maarufu kwa ajili ya bidhaa za watu kwa visiwa vingi.
Je! Tiro alisema nini kuhusu yeye mwenyewe?
Tiro alisema kuhusu yeye mwenyewe kwamba ilikuwa imekamilika kwa uzuri.
Ezekiel 27:6-7
Ilikuwa meli ya sitaha gani Tiro aliitengeneza?
Meli ya sitaha ya Tiro ilikuwa imetengezwa kwa mbao za kitimu zilizotengenezwa kwa pembe.
Ezekiel 27:8-11
Je! Nani walikuwa marubani wa meli ya Tiro?
Marubani wa meli walikuwa wenye busara wa Tiro
Je! Meli za Tiro zilikuwa zikibeba nini?
Meli za Tiro zilikuwa zikiwabeba bidhaa kwa ajili ya biashara.
Ezekiel 27:12-15
Kwa Tarshishi alikuwa mteja wa Tiro?
Tarshishi alikuwa mteja wa tiro kwa sababu ya mtazamo wa kila aina ya utajiri.
Ni katika njia gani Tiro alikuwa akishughulika na Yavani, Tubali, na Mesheki?
Tiro alikuwa akishugulika na maisha ya watu na vitu vyao vya shaba.
Ezekiel 27:16-21
Ni kwa vitu gani Yuda na nchi ya Israeli walifanya biashara na Tiro?
Yuda na nchi ya Israeli walifanya biashara kwa ngano, mtama, asali, mafuta, na lihamu.
Ezekiel 27:22-25
Ni kwa kitu gani Sheba alifanya biashara na Tiro?
Sheba alifanya biashara kwa viungo, vito vya thamani, na dhahabu.
Ezekiel 27:26-27
Yahwe anasema nini kitatokea kwa utajiri wa Tiro katika siku ya uharibifu wake?
Yahwe alisema utajiri wa Tiro utaanguka kwenyi vilindi vya bahari katika siku ya uharibifu wake.
Ezekiel 27:28-33
Je! Miji ya kwenye bahari itafanya nini wakati watakaposikia sauti za marubani wao wakilia?
Miji ya kwenye bahari itatetemeka kwa sauti ya marubani zao wakilia.
Ezekiel 27:34-36
Je! Wafalme wa pwani walifanya nini wakati walipouona uharibifu wa
Wafalme wa pwani watatetemeka katika kitisho na kutetemeka watakapoona uharibifu wa Tiro.
Yahwe alisema Tiro atatokea lini?
Yahwe alisema Tiro hataonekana tena.
Ezekiel 28
Ezekiel 28:1-3
Je! Mfalme kiongozi wa Tiro alisema nini kuhusu yeye?
Kiongozi wa Tiro alisema kuhusu yeye, "Mimi ni mungu!
Ezekiel 28:4-5
Kwa nini moyo wa kiongozi wa Tiro ulikuwa na kiburi?
Moyo wa kiongozi ulikuwa na kiburi kwa sababu ya utajiri wake.
Ezekiel 28:6-7
Yahwe angefanya nini kwa mtawala wa Tiro kwa sababu ya kiburi chake?
Yahwe alisema angelwaleta wageni dhidi ya kiongozi wa Tiro.
Ezekiel 28:8-10
Je! Yahwe alisema kiongozi wa Tiro angekufaje?
Kiongozi wa Tiro angekufa kifo cha asiyetahiriwa kwa mkono wa wageni.
Ezekiel 28:11-13
Je! Yahwe alisema mfalme wa Tiro alikuwaje?
Yahwe alisema mfalme wa Tire aliumbwa kwa ukamilifu, amejawa na hekima, na ukamilifu wa uzuri.
Kutokana na Yahwe, mfalme wa Tiro alikuwa wapi wakati alipoumbwa?
Mfalme wa Tiro alikuwa katika Edeni, bustani ya Mungu.
Ezekiel 28:14-15
Yahwe alimuweka wapi mfalme wa Tire, na mfalme wa Tire ana majukumu gani?
Mfalme wa Tire alikuwa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu kama kerubi aliyepakwa mafuta kumlinda mwanadamu.
Ni barua gani ilipatikana kwa mfalme wa Tire?
Udhali ilikuwa barua iliyokuwa imepatikana ndani ya mfalme wa Tire.
Ezekiel 28:16-17
Kwa sababu ya dhambi ya mfalme wa Tire, Yahwe alimfanyia nini?
Yahwe alimtupa mfalme wa Tire chini kama najisi kutoka kwenye mlima wa Mungu na kumwangamiza.
Ezekiel 28:18-22
Wale waliokuwa wanamfahamu mfalme wa Tire watafanya nini wakati watapouona uharibifu wake?
Wale waliomfahamu mfalme wa Tire watamtetemekea na kuogopa.
Ezekiel 28:23-24
Yahwe alisema alikuwa akipeleka nini Sidoni?
Yahwe alisema alikuwa akipeleka pigo na damu katika mitaa ya Sidoni.
Kutokana na Yahwe, watu waliokuwa wameizunguka Israeli walikuwa wanapenda kwa ajili ya nyumba ya Israeli?
Watu walioizunguka Israeli walikuwa kama wanchoma shayiri na maumivu ya miiba.
Ezekiel 28:25-26
Baada ya Yahwe kutekeleza haki juu ya yule anayeidharau Israeli, nini kitatokea kwa Israeli?
Israeli ataishi salama, atajenga nyumba, na kupanda mizabibu katika nchi Yahwe atakayompatia Yakobo mtumishi wake.
Ezekiel 29
Ezekiel 29:1-3
Yahwe alimwambia Ezekieli atabiri juu ya nani?
Yahwe alimwambia Ezekieli atabiri juu ya Farao, mfalme wa Misri.
Yahwe anasema anaifananisha Misri na mnyama gani?
Yahwe anasema mfalme wa Misri ni kama mnyama wa bahari kuu adanganyaye katikakati ya mto.
Ezekiel 29:4-5
Yahwe anasema anaenda kumtupia wapi mfalme wa Misri?
Yahwe asema anaenda kumtupa mfalme wa Misri chini kwenye jangwa.
Ezekiel 29:6-7
Yahwe anasema ni aina gani ya mmea ambao Misri ipo kama nyumba ya Israeli?
Yahwe anasema Misri ni kama mwanzi wa kutegemewa kwenye nyumba ya Israeli.
Yahwe alifanya nini wakati nyumba ya Israeli ilipoiegemea Misri?
Misri iliivunjavunja miguu ya Misri na tunda lao la waridi kutikisika wakati Israeli ilipojifunza juu ya Misri.
Ezekiel 29:8-10
Yahwe anasema nchi ya Misri itatolewa kwa nani?
Yahwe asema nchi ya Misri itatolewa kwenye huzuni na isiyofaa.
Ezekiel 29:11-12
Kwa mda gani Yahwe anasema nchi ya Misri haitakuwa urithi?
Yahwe asema Misri haitakuwa urithi kwa miaka arobaini.
Ezekiel 29:13-16
Yahwe anasema Misri itakujwa baada ya kurudi kutoka kutawanyika?
Yahwe asema Misri itakuwa utawala mdogo baada ya kurudi kutoka kutawanyika.
Ezekiel 29:17-18
Ni mshahara gani Nebukadneza mfalme wa Babeli alipokea kwa ajili ya kazi yote ngumu aliyoifanya juu ya Tire?
Nebukadneza alipokea mshahara kwa kazi yote ngumu aliyoifanya juu ya Tire.
Ezekiel 29:19-20
Yahwe atampatia nini Nebukadneza kurudisha kwa kazi yote ngumu aliyoifanya juu ya Tire?
Yahwe atampatia Nebukadneza nchi ya Misri kama mshahara kwa ajili ya kazi yote ngumu aliyoifanya juu ya Tire.
Ezekiel 29:21
Katika siku hiyo, Yahwe atamfanya Ezekieli kufanya nini?
Katika hiyo siku, Yahwe atamfanya Ezekieli kunena katikati ya nyumba ya Israeli.
Katika hiyo siku, nyumba ya Israeli itajua nini?
Katika hiyo siku, nyumba ya Israeli itajua kwamba Bwana ni Yahwe.
Ezekiel 30
Ezekiel 30:1-3
Kutokana na Yahwe, ni aina gani ya siku na mda unakuja wa siku ya Yahwe?
Siku inayokuja ya Yahwe ni siku ya mawingu, mda wa hukumu kwa ajili ya mataifa.
Ezekiel 30:4-7
Katika siku ya Yahwe, nini kitatokea kwa Misri, Kushi, Putu, Ludi, na watu wanaomiliki agano?
Katika siku ya Yahwe, wote wataanguka kwa upanga.
Ezekiel 30:8-9
Watu watajua nini wakati Misri na wasaidizi wake watakapo angamizwa?
Watu watajua kwamba Yahwe ni Bwana.
Ezekiel 30:10-12
Yahwe atatumia mkono wa nani kuangamiza nchi ya Misri?
Yahwe atatumia mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, kuharibu nchi ya Misri.
Ezekiel 30:13-16
Yahwe ataleta mwisho kwenye nini katika Nofu?
Yahwe ataiangamiza na kuuleta mwisho hata sanamu zisizofaa za Nofu.
Ezekiel 30:17-19
Nini kitatokea kwa masalia katika miji ya Misri wakati Yahwe aletapo uharibifu?
Masalia yataenda kwenye uhamisho wakati atakapoleta uharibifu.
Ezekiel 30:20-21
Yahwe anasema aliufanya nini mkono wa Farao, na Farao hawatweza kufanya nini sasa?
Yahwe alisema aliuvunja mkono wa Faro, hivyo haukuwa imara vya kutosha kushika upanga.
Ezekiel 30:22-24
Baada ya Misri kuwa imeangamizwa, Yahwe ataifanya nini Misri miongoni mwa mataifa?
Yahwe ataitawanya na kuitapanya Misri miongoni mwa mataifa.
Ezekiel 30:25-26
Yahwe ataunyoosha mikono wa nani?
Yahwe ataunyoosha mikono ya mfalme wa Babeli.
Nini kitatokea kwa mikono ya Yahwe?
Mikono ya Farao itaanguka.
Ezekiel 31
Ezekiel 31:1-2
Yahwe alimwambia Ezekieli atabiri kwa nani?
Yahwe alimwambia Ezeki atabiri kwa Farao, mfalme wa Misri.
Ezekiel 31:3-4
Ni aina gani ya mmea Yahwe aliipungza Ashuru?
Yahwe aliipunguza Ashuru kuwa mkangazi mkubwa katika Lebanoni.
Ezekiel 31:5-7
Katika mfano wa Yahwe wa Ashuru kama mti, nini kiliishi ndani na kuzunguka mkangazi mkubwa?
Kila ndege wa mbinguni alijenga kiote katika matawi ya mkangazi, na kila kiumbe hai kwenye shamba kilizaa chini ya jani.
Ezekiel 31:8-9
Nini kilikuwa kikubwa zaidi kuliko mkangazi wa Ashuru kuliko?
Mkangazi mkubwa wa Ashuru ulikuwa mkubwa zaidi kuliko miti yote katika bustani ya Mungu.
Ezekiel 31:10-12
Kwa nini Yahwe aliishika Ashuru na kuitupilia mbali?
Yahwe aliitupa Ashuru na kuitupilia mbali kwa sababu moyo wake ulikuwa umeinuliwa juu (kujiinua) na ulikuwa mdhaifu.
Ezekiel 31:13-14
Baada ya mkangazi wa Ashuru kuwa umetelekezwa, Yahwe alisema nini hakitatokea tena?
Yahwe alisema kwamba hakuna mti mwingine utakao mea tena huo urefu.
Ezekiel 31:15
Yahwe ataleta nini kwenye nchi katika siku wakati Ashuru atakaposhuka chini hata Sheole?
Katika siku Yahwe atakapoleta maombolezo kwenye nchi.
Ezekiel 31:16
Hadi wapi Yahwe alitupa mkangazi mkubwa wa Ashuru?
Yahwe aliutupa mkangazi mkubwa wa Ashuru chini hata Sheole
Ezekiel 31:17-18
Nini kilitokea kwa yale mataifa ambayo yaliishi katika kivuli cha mkangazi mkubwa wa Ashuru?
Yale mataifa yaliyoishi katika kivuli cha Ashuru vili vile yalishuka chini hata Sheole.
Yahwe alitangaza nani atashushwa chini hadi kwenye sehemu za nchi?
Yahwe alitangaza kwamba huyo Farai na watumishi wake watashushwa chini hadi sehemu za chini ya nchi.
Ezekiel 32
Ezekiel 32:1-2
Yahwe alimwambia nini Ezekieli kuinua kuhusiana na Farao?
Yahwe alimwambia Ezekieli kuinua maombolezo kuhusiana na Farao.
Ni wanyama gani wawili ambao Yahwe alisema Farao alikuwa anafanana nao?
Yahwe alisema Farao alikuwa kama mwana simba na kama joka katika bahari.
Ezekiel 32:3-6
Wakati Yahwe atakapo tupa jinamizi la bahari kwenye uwanda, nini kitatokea kwalo?
Wakati jinamizi la bahari litakapotupwa kwenye uwanda, ndege na wanyama watalila.
Ezekiel 32:7-8
Nini kitatoka katika mbingu wakati Yahwe atakapo weka taa ya Misri?
Nyota zitakuwa giza, mawingu yatafunika jua, na mwezi hautatoa nuru.
Ezekiel 32:9-10
Je watu wa nchi watapokeaje watakapoona Misri inavunjika?
Watu wa nchi wataogopa na kutetemeka kwa kitisho.
Ezekiel 32:11-12
Nani atakuja juu ya Misri na kuiteketeza?
Mfalme wa Babeli atakuja juu ya Misri na kuiteketeza.
Ezekiel 32:13-14
Yahwe anasema nini kitatokea kwa mtu na mnyama katika Misri?
Si mtu wala mnyama watayavuruga maji ya Misri.
Ezekiel 32:15-16
Watu wa Misri watajua nini wakati watakaposhambuliwa na kuangamizwa?
Watu wa Misri watajua kwamba Yahwe ni Bwana.
Ezekiel 32:17-18
Watumishi wa Misri na binti za wakuu wa nchi watatupwa wapi?
Watatupwa chini hata chini kabisa ya nchi pamoja na wale walioshuka chini hata kwenye shimo.
Ezekiel 32:19-23
Wapiganaji wa Sheoli walisema nini kuhusu Misri na rafiki zake?
Watasema kwamba Misri na rafiki zake wameshuka chini hapa na watadanganya pamoja na wasiotahiriwa waliouawa kwa upanga.
Ezekiel 32:24-29
Elamu alifanya nini kwenye nchi ya kuishi?
Elamu alileta wapiganaji kwenye nchi ya kuishi.
Ezekiel 32:30
Wana mfalme wa kaskazini na Wasidoni ambao walikuwa wameshuka chini na maiti walibeba nini?
Wamebeba aibu yao wenyewe.
Ezekiel 32:31-32
Nini kitamfariji Farao katika Sheoli?
Katika Sheoli, Farao atafarijika kuhusu watumishi wake wote waliokuwa wameuawa kwa upanga.
Ezekiel 33
Ezekiel 33:1-4
Mlinzi anafanya nini kwa ajili ya watu wa nchi?
Mlinzi anatafuta upanga unaokuja juu ya nchi, na kupiga tarumbeta kuwaonya watu.
Nini kitatokea kama watu wasipokuwa makini kwa mlinzi?
Kama watu wasipokuwa makini, upanga utawaua watu na damu ya kila mmoja i juu ya kichwa chake mwenyewe.
Ezekiel 33:5-6
Nini kimetokea kwa mlinzi kama asipowaonya watu?
Kama mlinzi hatawaonya watu, Yahwe ataihitaji damu yake.
Ezekiel 33:7-9
Yahwe alimuweka nani kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli?
Yahwe alimfanya Ezekieli mlinzi kwa ajili ya nyumba ya Israeli.
Ezekiel 33:10-11
Yahwe anasema hapendezwi na nini?
Yahwe anasema hapendezwi na kifo cha mwovu.
Yahwe anamwita mwovu kufanya nini?
Yahwe anamwita mwovu kutubu ili aishi.
Ezekiel 33:12-13
Yahwe anasema nini kitatokea kwa mtu mwenye haki ambaye afanyaye isiyohaki?
Yahwe anasema yule mtu mwenye haki afanyaye isiyohaki atakufa katika uovu ambao alioufanya.
Ezekiel 33:14-16
Yahwe anasema nini kitatokea kwa mtu mwovu atubuye na kufanya haki na kweli?
Yahwe anasema mtu mwovu atubuye na kufanya kilicho haki na kweli ataishi hakika.
Ezekiel 33:17-20
Kutokana na Yahwe, njia za nani haziko sawa?
Kutokana na Yahwe, njia za watu wa Israeli haziko sawa.
Je Yahwe anasema atahukumu vipi kila mtu wa nyumba ya Israeli?
Yahwe anasema atamuhukumu kila mtu kulingana na njia yake.
Ezekiel 33:21-22
Yule mkimbizi alileta ujumbe gani kwa Ezekieli?
Yule mkimbizi alileta ujumbe kwamba nchi ya Yerusalemu imetekwa.
Ezekiel 33:23-24
Watu wa Israeli walikuwa wakisema nini kuhusu nchi ambayo Abrahamu aliyoirithi?
Watu wa Israeli walikuwa wakisema nchi ambayo Abrahamu aliyoirithi ilikuwa milki yao.
Ezekiel 33:25-26
Kwa nini Yahwe anauliza kama watu wa Israeli kweli watamiliki nchi au hapana?
Yahwe anauliza swali kama watamiliki nchi kwa sababu walitegemea panga zao na walifanya mambo maovu.
Ezekiel 33:27-29
Yahwe anasema atafanya nini kwenye nchi kwa sababu ya mambo watu wa Israeli waliyoyafanya?
Yahwe anasema atairudisha nchi kuwa ukiwa chukizo kwa sababu ya mambo ambayo watu wa Israeli waliyoyafanya.
Ezekiel 33:30-31
Watu wa Israeli watafanya nini na maneno ya Ezekieli?
Watu wa Israeli watayasikiliza maneno ya Ezekieli, lakini hawatayatii.
Ezekiel 33:32-33
Watu wa Israeli watajua nini wakati kila kitu kitakapopita?
Watu wa Israeli watajua kwamba nabii alikuwa miongoni mwao wakati kila kitu kitakapopita.
Ezekiel 34
Ezekiel 34:1-3
Yahwe alifanya mashtaka gani juu ya wachungaji wa Israeli?
Yahwe aliwashtaki wachungaji wa Israeli kwa kuacha kuchunga wakati wote, lakini kwa kuchinja wanayama bora wa kundi.
Ezekiel 34:4-6
Je wachungaji wa Israeli waliongozaje kundi?
Wachungaji wa Israeli walioongoza kundi kwa nguvu na vurugu.
Nini kilitokea kwa kundi?
Kundi lilitawanyika na kuwa chakula kwa ajili wanyama katika mashamba.
Ezekiel 34:7-8
Ni nani walikuwa wachungaji halisi wa Israeli wakichunga?
Wachungaji wa Israeli walikuwa wakijichunga wenyewe.
Ezekiel 34:9-10
Yahwe anasema atafanya nini kwa wachungaji wa Israeli?
Yahwe anasema atawasitisha wachungaji wa Israeli na kuchukua kundi kutoka midomo yao.
Ezekiel 34:11-13
Yahwe anasema atakusanya kundi lake kutoka wapi?
Yahwe anasema atawaokoa kutoka sehemu zote walipotawanyika siku ya mawingu na giza. Kisha watawaleta kutoka miongoni mwa watu, atawakusanya kutoka nchi.
Ezekiel 34:14-16
Yahwe anasema atachungaje?
Yahwe anasema atachunga kwa haki.
Ezekiel 34:17-19
Yahwe anasema atahukumu miongoni mwa makundi matatu?
Yahwe anasema atahukumu miongoni mwa kondoo, kondoo dumu, na mbuzi.
Ezekiel 34:20-21
Nini kilifanyika kwa kondoo mdhaifu na aliyekonda?
Kondoo mdhaifu na aliyekonda walisukumwa na kutapakaa damu hadi watakapotawanyika.
Ezekiel 34:22-24
Yahwe anasema atamwinua nani kuchunga kondoo?
Yahwe anasema atamwinua mtumishi wake Daudi kuchunga kundi.
Ezekiel 34:25-27
Wakati Yahwe atakapo mwinua mchungaji wake, Yahwe atafanya nini ili kondoo aishi salama?
Yahwe atafanya agano la amani pamoja na kondoo na kuondoa uovu wanyama pori kutoka ile nchi.
Ezekiel 34:28-29
Mataifa hayataweza kufanya nini kwenye kondoo?
Mataifa hayataweza tena kuteka nyara kondoo au kuleta fedheha juu yao.
Ezekiel 34:30-31
Nyumba ya Israeli itajua nini?
Nyumba ya Israeli itajua kwamba Mungu wao yu pamoja nao.
Yahwe anatangaza kwenye kondoo, nyumba ya Israeli?
Yahwe anatangaza kwamba yeye ni Mungu wa Israeli, na kwamba wao ni watu wake.
Ezekiel 35
Ezekiel 35:1-3
Yahwe anamwambie Ezekieli atabiri dhidi ya?
Yahwe anamwambia Ezekieli atabari dhidi ya Mlima Seiri.
Yahwe anasema ataufanya nini Mlima Seiri?
Yahwe anasema ataufanya Mlima Seiri ukiwa na chukizo.
Ezekiel 35:4-6
Watu wa Mlima Seiri walifanya nini ambacho ni kuleta hukumu ya Yahwe juu yao?
Watu wa Mlima Seiri walikuwa maadui kwa watu wa Israeli, na kuwamwaga kwenye mikono ya upanga.
Kutokana na Yahwe, nini kitaandamana na watu wa Mlima Seiri, na kwa nini?
Damu kumwagwa itaandamana na watu wa Mlima Seiri kwa sababu hawakuchukia kumwagwa damu.
Ezekiel 35:7-9
Nini kitaijaza milima katika eneo la Milima Seiri?
Milima katika eneo la Mlima Seiri litajazwa na maiti zao.
Ni kwa mda gani majozi ya Mlima Seiri yatadumu?
Huzuni ya Mlima Seiri itabaki ukiwa daima.
Ezekiel 35:10-11
Watu wa Mlima Seiri walisema nini kuhusu mataifa mawili ya watu wa Yahwe Israeli?
Watu wa Mlima Seiri walisema kwamba haya mataifa mawili yatakuwa yao.
Ezekiel 35:12-13
Yahwe alisikia nini watu wa Mlima Seiri wakisema juu yake?
Yahwe alisikia watu wa Mlima Seiri wakijiinua juu ya Yahwe na kusema mambo mengi juu yake.
Ezekiel 35:14-15
Dunia nzima itafanya nini wakati watu wa Mlima Seiri wakiwa na majonzi?
Dunia nzima itafurahia wakati watu wa Mlima Seiri wakiwa na huzuni.
Watu wa Mlima Seiri walifanya nini wakati watu wa Israeli walipohuzunishwa?
Watu wa Mlima Seiri walifurahi wakati watu wa Israeli walipohuzunishwa.
Yahwe anasema kwamba eneo gani litakuwa na huzuni?
Yahwe asema kwamba Mlima Seiri na Edomu yote zitakuwa na huzuni.
Watu wa Mlima Seiri na Edomu watajua nini wakati Yahwe atakapowahukumu?
Watu wa Mlima Seiri na Edomu watajua kwamba Bwana ni Yahwe wakati Yahwe atakapowahukumu.
Ezekiel 36
Ezekiel 36:1-3
Yahwe alimwambia Ezekieli atabiri juu ya nini?
Yahwe alimwambia Ezekieli atabiri juu ya milima ya Israeli.
Adui alikuwa akisemaje kuhusu milima ya Israeli?
Adui alikuwa akisema kwamba mahali pa juu pa zamani pamekuwa milki yao.
Ezekiel 36:4-6
Yahwe alinena katika ghadhabu ya moto yake juu ya nani?
Yahwe alinena katika ghadhabu ya moto juu ya Edomu na wote walioichukua nchi ya Israeli.
Ezekiel 36:7
Yahwe aliapia nini kuhusiana na mataifa yaliyoizunguka Israeli?
Yahwe aliapa kwamba yale mataifa yaliyoizunguka Israeli yataibeba aibu yao wenyewe.
Ezekiel 36:8-9
Yahwe alisema nani atakuwa anarudi baada ya kitambo kwenye milima ya Israeli?
Yahwe alisema watu wa Israeli watakuwa wakirudi baada kitambo kwenye milima ya Israeli.
Ezekiel 36:10-15
Ni kitu gani kitaongezeka juu ya milima ya Israeli?
Mtu na wanyama wataongezeka juu ya milima ya Israeli.
Ezekiel 36:16-18
Kwa nini Yahwe aliimwaga ghadhabu yake juu ya Israeli?
Yahwe aliimwaga ghadhabu yake juu ya Israeli kwa sababu Israeli ameichafua nchi kwa sanamu.
Ezekiel 36:19-21
Watu wa Israeli walifanya nini wakati walipoenda kwa mataifa?
Wakati walipoenda kwa mataifa, watu wa Israeli walilinajisi jina takatifu la Yahwe.
Ezekiel 36:22-25
Kwa nini Yahwe anasema anaenda kuirudisha nyumba ya Israeli kwenye milima ya Israeli?
Yahwe anasema anaenda kuirudisha nyumba ya Israeli kwa ajili ya jina lake takatifu.
Ezekiel 36:26-28
Yahwe alisema atafanya kwenye nyumba ya Israeli kuwawezesha kuenenda katika amri zake na kuzitunza sheria zake?
Yahwe alisema atamuweka Roho wake kati yao na kuwawezesha kuenenda katika sheria zake na kutunza maagizo yake, hivyo watayafanya.
Ezekiel 36:29-31
Baada ya Yahwe kuiokoa nyumba ya Israeli, nyumba ya Israeli itafikiri nini juu ya njia zao mbaya za nyuma?
Nyumba ya Israeli itajichukia yenyewe kwa sababu ya njia zao za nyuma.
Ezekiel 36:32-34
Yahwe anasema nini kitatokea kwenye miji na sehemu zilizoharibika za Israeli?
Yahwe anasema miji itakuwa maskani na sehemu ziliharibiwa zitajengwa tena.
Ezekiel 36:35-36
Nchi ya Israeli itakuwa kama sehemu gani?
Nchi ya Israeli itakuwa kama bustani ya Edeni.
Mataifa mengine yatajua nini wakati watakapoona wenyeji wa mji na kujenga tena uharibifu wa Israeli?
Mataifa yatajua kwamba Bwana ndiye Yahwe, na kwamba Yahwe ameijenga tena Israeli.
Ezekiel 36:37-38
Yahwe alisema hesabu ya wana wa Israeli itakuwa kama nini?
Hesabu ya watu wa Israeli itakuwa kama kundi la mifugo katika Yerusalemu kwenye sikukuu zilizoteuliwa.
Ezekiel 37
Ezekiel 37:1-3
Roho wa Yahwe alimuweka Ezekieli wapi, na nini kilikuwa huko?
Roho wa Yahwe alimuweka Ezekieli chini katikati ya bonde lililojaa mifupa.
Yahwe alimuuliza Ezekieli swali gani?
Yahwe alimuuliza Ezekieli kama mifupa mikavu itaishi tena.
Ezekiel 37:4-6
Ezekieli alitabiri nini kingetokea kwa mofupa mikavu?
Ezekieli alitabiri kwamba ile mifupa mikavu itakuwa na nyama na kuishi tena.
Ezekiel 37:7-8
Nini kilitokea kwenye mifupa wakati Ezekieli alipotabiri kwao mara ya kwanza?
Wakati Ezekieli alipotabiri kwao mara ya kwanza, mifupa mikavu kuileta pamoja na nyama na ngozi iliwafunika.
Ezekiel 37:9-10
Nini kilitokea kwa mifupa wakati Ezekieli alipotabiri kwao mara ya pili?
Wakati Ezekieli alipotabiri kwa mifupa mara ya pili, Roho akaja kwao na wakaishi
Ezekiel 37:11-14
Kutokana na Yahwe, bonde la mifupa mikavu linawakilisha nini?
Kutokana na Yahwe, bonde la mifupa mikavu linwakilisha nyumba nzima ya Israeli.
Yahwe alisema atafanya nini kwa ajili ya Israeli, kipi kilikuwa kikiwakilishwa na mifupa mikavu kufufuliwa?
Yahwe alisema atawainua watu wa Israeli kutoka makaburi yao na kuwarudisha kwenye nchi ya Israeli
Ezekiel 37:15-17
Yahwe alimwambia Ezekieli kufanya nini na zile fimbo mbili?
Yahwe alimwambia Ezekieli kuandika jina juu ya kila fimbo, Yuda na Yusufu, na kisha kuzileta fimbo zote pamoja.
Ezekiel 37:18-20
Yahwe alisema fimbo mbili za Ezekieli zilikuwa na maana gani?
Yahwe alisema alikuwa akiunganisha matawi mawili ya Yusufu na Yuda ili wawi wamoja katika nchi yake.
Ezekiel 37:21-23
Yahwe alisema alitaka kufanya nini kwa ajili ya watu wa Israeli?
Yahwe alisema alitaka kuwakusanya watu wa Israeli juu ya milima ya Israeli kama taifa moja lenye mfalme mmoja.
Ezekiel 37:24-25
Yahwe alisema nani atakuwa mfalme juu ya muungano wa nchi ya Israeli?
Yahwe alisema kwamba mtumishi wake Daudi atakuwa mfalme juu muungano wa nchi ya Israeli.
Kulingana na Yahwe, mkuu wao atakuwa mfalme wa Israeli kwa mda gani?
Kulingana na Yahwe, mfalme wa Israeli atakuwa mkuu wao milele.
Ezekiel 37:26-28
Yahwe alisema ataimarisha nini pamoja na Israeli, na kwa mda gani?
Yahwe alisema angeimarisha agano la amani pamoja na Israeli daima.
Yahwe alisema ataishi wapi milele?
Yahwe alisema ataishi milele katikati ya watu wa Israeli.
Ezekiel 38
Ezekiel 38:1-3
Yahwe anamwambia Ezekieli atabiri juu ya nani?
Yahwe alimwambia Ezekieli atabiri juu ya Gogu kutoka nchi ya Magogu.
Ezekiel 38:4-6
Yahwe anasema atamfukuza Gogu kwa namna gani?
Yahwe anasema atamfukuza Gogu pamoja na jeshi lake lote, farasi, na waendesha farasi.
Ezekiel 38:7-9
Kamanda ya vikosi vya majeshi yote ni nani kutoka Perisia, Kushi, Puto, Goma, na Beth Togama?
Gogu ndiye kamanda wa hivi vikosi vyote vya jeshi vilivyokusanyika pamoja naye.
Gogu ataitwa kwenda nchi gani?
Gogu ataenda katika nchi ambayo iliyofunikwa na upanga na kwamba iliyokusanywa kutoka watu wengi hata milima ya Israeli.
Ezekiel 38:10-13
Ni njama gani mbaya ambayo Gogu ataitunga?
Gogu atatunga njama kuteka mateka na kuteka nyara kutoka watu wapole waishio katika usalama.
Ezekiel 38:14-16
Gogu na jeshi lake kubwa walitokea upande gani?
Gogu na jeshi lake walikuja kutoka mbali katika kaskazini.
Ezekiel 38:17-18
Yahwe alinena kupitia nani kwamba Gogu atakuja juu ya Israeli?
Yahwe alinena kupitia manabii wa Israeli kwamba Gogu atakuja juu ya Israeli.
Je! Yahwe ataitikia vipi wakati Gogu atakapoishambulia nchi ya Israeli?
Wakati Gogu atakapoishambulia nchi ya Israeli, Yahwe ataitikia kwa ghadhabu katika matundu ya pua zake.
Ezekiel 38:19-20
Ni tukio gani kubwa litatokea Yahwe anasema siku hiyo Gogu atakapoishambulia Israeli?
Yahwe anasema kwamba kutakuwa na tetemeko kubwa siku hiyo Gogu atakapoishambulia Israeli.
Ezekiel 38:21-23
Kwa namna gani Yahwe ataihukumu Gogu na vikosi vyake vya jeshi siku hiyo?
Yahwe ataihukumu Gogu na vikosi vyake siku hiyo kwa tauni, damu, mvua za mafuriko, mvua ya moto ya mawe, na mvua za kiberiti.
Katika siku hiyo, Yahwe ataonyesha nini katika macho ya mataifa mengi?
Katika siku hiyo, Yahwe ataonyesha ukuu wake na utakatifu katika macho ya mataifa mengi.
Ezekiel 39
Ezekiel 39:1-3
Yahwe anasema tamleta Gogu wapi, mkuu wa Mesheki na Tubali?
Yahwe anasema atamleta Gogu kwenye milima ya Israeli.
Ezekiel 39:4-6
Gogu ataanguka kufia wapi?
Gogu ataanguka kufa juu ya milima ya Israeli.
Yahwe atafanya nini kwa Magogu na wale wanaoishi katika usalama juu ya pwani?
Yahwe atapeleka moto kwenda Magogu na kwa wale wanaoishi katika usalama juu ya pwani.
Ezekiel 39:7-8
Yahwe anasema hataruhusu nini tena?
Yahwe anasema hataruhusu jina lake takatifu kunajisiwa.
Ezekiel 39:9-10
Kwa nini yule anayeishi katika mji wa Israeli hahitaji kukusanya kuni kwa siku saba?
Hawatahitaji kukusanya kuni kwa miaka saba kwa sababu watazichoma silaha za Gogu.
Ezekiel 39:11
Gogu na makundi yake wote watazikwa wapi?
Gogu na makundi yake yote watazikwa katika Bonde la Hamon Gogu.
Ezekiel 39:12-16
Nyumba ya Israeli itatakiwa kufanya nini ili kuitakasa nchi?
Nyumba ya Israeli itatakiwa kuizika Gogu na makundi yake yote kwa siku saba ili kuitakasa nchi.
Ezekiel 39:17-20
Yahwe anafanya dhabihu gani juu ya milima ya Israeli?
Yahwe anafanya dhabihu kubwa ya nyama ya mashujaa na damu ya wana wa makuhani wa dunia juu ya milima ya Israeli.
Ezekiel 39:21-22
Mataifa yote yataona nini wakati Yahwe afanyapo dhabihu yake kubwa juu ya milima ya Israeli?
Mataifa yote yataiona hukumu ya Yahwe na mkono wake.
Ezekiel 39:23-24
Kwa nini nyumba ya Israeli inaenda utumwani?
Nyumba ya Israeli ilienda utumwani kwa sababu ya dhambi zao.
Ezekiel 39:25-27
Yahwe atafanya nini kwa ajili ya nyumba ya Isralei wakati atakapoona wivu kwa ajili ya jina lake?
Yahwe atawarudisha wenyeje wa Yakobo na kuihurumia nyumba ya Israeli.
Nyumba ya Israeli itasahau nini wakati watakapopumzika katika nchi yao salama?
Nyumba ya Israeli itasahau nini aibu yao na uhaini ambapo walimsaliti Yahwe.
Ezekiel 39:28-29
Yahwe anatangaza atafanya nini wakati atakapo mmwaga Roho wake juu ya nyumba ya Israeli?
Yahwe anatangaza kwamba wakati atapommwaga Roho wake juu ya nyumba ya Israeli hataficha tena uso wake kutoka kwao.
Ezekiel 40
Ezekiel 40:1-2
Ni kwa miaka mingapi Ezekieli alikuwa mtumwa wa Babeli?
Ezekieli alikuwa mtumwa wa Wababeli kwa miaka ishirini na tano.
Je! Mji wa Yerusalemu ilikuwa imetekwa kwa miaka mingapi?
Mji wa Yerusalemu ulikuwa uemtekwa mika kumi na nne iliyopita.
Mungu alimleta Ezekieli wapi kwa maono?
Mungu alimleta Ezekieli kwenye nchi ya Israeli katika maono.
Ezekiel 40:3-4
Je! Ezekieli aliambiwa kutoa taarifa gani kwenye nyumba ya Israeli?
Ezekieli aliambiwa kutoa taarifa ya kila kitu alichokiona kwenye nyumba ya Israeli.
Ezekiel 40:5-10
Katika maono ya Ezekieli, je! nini kilikuwa kimezunguka sehemu ya hekalu?
Katika maono ya Ezekieli, ukuta ulizunguka sehemu ya hekalu.
Ezekiel 40:11-13
Je! Yule mtu aliyefanana na shaba alipima upana wa lango la kuingia kuwa kiasi gani?
Yule mtu aliyefanana na shaba aliyepima upana wa lango la kuingia kuwa dhiraa kumi.
Ezekiel 40:14-16
Je! Ezekieli aliona nini kimechongwa kwenye kuta?
Ezekieli aliona miti ya mnazi iliyochongwa juu ya kuta.
Ezekiel 40:17-21
Je! Yule mtu aliyeonekana kama shaba alimchukua wapi Ezekieli baada ya kupima katika eneo la lango?
Yule mtu alimchukua Ezekieli kwenda ua wa nje wa hekalu.
Ezekiel 40:22-27
Je! kupitia nini mtu alienda ili kuingia kwenye ua wa ndani?
Mtu alienda kupitia lango ili kuingia kwenye ua wa ndani.
Ezekiel 40:28-37
Je! Malango ya kwenda ua wa ndani yalilingana vipi katika kipimo?
Malango ya ua wa yote yalikuwa na kipimo kimoja.
Ezekiel 40:38-39
Kwa ajili ya nini vyumba vyenye milango kwa kila lango la njia ya ndani lilitumika?
Vyumba vyenye milango kwa kila lango la njia ya ndani vilitumika kusafisha sadaka ya kuteketeza.
Ezekiel 40:40-45
Je! Ni kwa ajili ya nini meza nne kwa pande zote za kila lango zilitumika?
Zile meza nne kwa kila upande wa kila lango zilitumika kwa ajili ya kuchinja wanyama.
Ezekiel 40:46-47
Je! Ni wana wa nani walikuwa wakitumika kama makuhani katika hekalu?
Wana wa Zadoki walikuwa wakitumika kama makuhani katika hekalu.
Je! Lango la ndani lilikuwa na ukubwa gani?
Lile lango la ndani lilikuwa na dhiraa mia moja urefu na upana katika mraba.
Ezekiel 40:48-49
Je! Nini kilisimama pande zote ya varanda za patakatifu?
Nguzo zilisimama pande zote za varanda ya patakatifu.
Ezekiel 41
Ezekiel 41:1-2
Yule mtu alimleta Ezekieli wapi?
Yule mtu alimleta Ezekieli mahali patakatifu pa hekalu.
Ezekiel 41:3-4
Yule mtu alienda wapi baada ya hapo?
Baada ya hapo yule mtu alienda mhali patakatifu sana.
Ezekiel 41:5-11
Je! Mtu alipataje kuwa sehemu ya juu ya nyumba?
Kupata kufika sehemu ya juu ya nyumba, kulikuwa na ngazi ambayo ilipanda juu kupitia sehemu ya kati.
Ezekiel 41:12-14
Kipimo cha patakatifu kilikuwaje na upana wa mbele ya ua mbele ya patakatifu?
Patakatifu na mbele ya ua kote kulikuwa dhiraa mia.
Ezekiel 41:15-17
Nini kilikuwa juu ya njia ya kuingia kuelekea patakatifu pa ndani?
Juu ya njia ya kuingia patakatifu pa ndani kulikuwa na pazia iliyopimwa.
Ezekiel 41:18-20
Ni sura gani mbili ambazo kila kerubi alikuwa nazo?
Kila kerubi lilikuwa na sura ya mtu na sura ya mwana simba.
Ezekiel 41:21-24
Yule mtu alisemaje kuhusu madhabahu ya mbao mbele ya mahali patakatifu?
Yule mtu alisema kwamba madhabahu ya mbao ilikuwa meza iliyokuwa imesimama mbele ya Yahwe.
Ezekiel 41:25-26
Nini kilikuwa kimefunika juu ya milango ya mahali patakatifu?
Kerubi na miti ya minazi vilikuwa vimeifunika milango ya mahali patakatifu.
Ezekiel 42
Ezekiel 42:1-12
Ni eneo lipi ambalo yule mtu alimtuma Ezekieli?
Yule mtu alimtuma Ezekieli kwenye ua wa nje upande wa kaskazini
Ezekiel 42:13-15
Yule mtu alisema vyumba vya magharibi na kusini mbele ya ua wa ndani vilitumika kwa ajili ya nini?
Katika hivyo vyumba makuhani walikuwa chakula kitakatifu zaidi, na kuweka vitu vitakatifu zaidi.
Ni vitu gani vilikuwa vitakatifu sana vya makuhani?
Vitu vitakatifu sana vya makuhani vilikuwa sadaka ya chakula, sadaka ya dhambi, na sadaka ya kutekeza.
Yule mtu alisema ni aina gani mahali ambako vyumba vya kaskazini na kusini vilikuwa?
Yule mtu alisema vyumba vya kaskazini na kusini vilikuwa mahali patakatifu.
Makuhani walifanya nini kabla ya kwenda karibu na watu?
Makuhani walivaa mavazi mengine kabla ya kwenda karibu na watu.
Ezekiel 42:16-19
Urefu wa kila upande ulikuwa kiasi gani; kaskazini, kusini mashariki na magharibi?
Kila upande ulikuwa na dhiraa mia tano urefu.
Ezekiel 42:20
Ni vitu gani viwili vilivyokuwa vimetenganisa kati ya lango la mashariki?
Lango la mashariki lilitenganisha patakatifu na ambako sio patakatifu.
Ezekiel 43
Ezekiel 43:1-2
Yule mtu alimleta wapi Ezekieli?
Yule mtu alimleta Ezekieli kwenye lango lililokuwa limefunguliwa kuelekea mashariki.
Ezekieli aliona nini na kutoka uelekea gani ulitokea?
Ezekieli aliona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka mashariki.
Ezekiel 43:3-5
Ezekieli iliingiaje kwenye ua wa ndani?
Roho alimbeba Ezekieli juu na kumleta kwenye ua wa ndani.
Ezekiel 43:6-9
Yahwe alisema nini angefanya katika ua wa ndani?
Yahwe alisema angekiweka kiti chake cha enzi huko na angeishi katikati ya watu wa Israeli huko daima.
Ni katika njia gani watu wa Israeli hawatalikufuru jina la Yahwe takatifu?
Watu wa Israeli wasingelikufuru tena jina la Yahwe kwa kuweka vizingiti kwenye kwenye madhabahu zao karibu na Yahwe.
Ezekiel 43:10-11
Yahwe alimwambia Ezekieli afanye nini kuhusu nyumba aliyokuwa ameiona katika ndoto?
Yahwe alimwambia Ezekieli kuiambia nyumba ya Israeli kuhusu nyumba aliyokuwa ameiona katika ndoto.
Waisrali walitakiwa kufanya nini ili kwa ajili ya Ezekieli kuwafunulia ubunifu wa nyumba?
Israeli walitakiwa kuwa na aibu ya dhambi zao ili kwa ajili ya Ezekieli kuwafunulia ubunifu wa nyumba ya Israeli.
Ezekiel 43:12-14
Ni jambo gani ambalo Yahwe alisema ni kanuni kwa ajili ya nyumba?
Yahwe alisema kanuni kwa ajili ya nyumba ilikuwa kwamba palikuwa mahali patakatifu sana.
Ezekiel 43:15-17
Meko ilikuwa ikitumika kwa ajili ya nini kwenye madhabahu?
Meko ilitumika kwenye madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezea sadaka.
Ni vitu gani vilivyokuwa kwenye meko?
Kulikuwa na pembe nne zilizo elekea kwenye meko.
Ezekiel 43:18-19
Yahwe alisema sadaka ya dhambi ingekuwa nini kwa ajili ya makuhani Walawi katika siku ya kwanza?
Yahwe alisema ng'ombe kutoka kwenye mifugo alikuwa kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya makuhani Walawi katika siku ya kwanza.
Ukoo wa nani ulitumika kama makuhani Walawi kwenye hii madhabahu?
Ukoo wa Zadoki walitumika kama makuhani Walawi kwenye hii madhabahu.
Ezekiel 43:20-21
damu ilihifadhiwa kwenye madhabahu kwa ajili ya kuifanyia nini?
Kuhifadhiwa damu kwenye madhabahu ingeisafisha na kufanya upanisho kwa hiyo.
Ezekiel 43:22-24
Yahwe alisema nini kitakuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya makuhani Walawi katika siku ya pili?
Yahwe alisema mbuzi mmoja dume asiye na dosari atakuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya makuhani Walawi katika siku ya pili.
Ezekiel 43:25-27
Makuhani walitakiwa kufanya nini kwa mda wa siku saba ili kulipia kusa kwa ajili ya madhabahu?
Makuhani walitakiwa kuandaa ng'ombe asiyekuwa na hatia na kondoo dume asiye na hatia kama sadaka ya kutekeza kulipia kosa kwa ajili ya madhabahu.
Katika siku ya nane na kuendelea, Yahwe alitangaza angefanya nini?
Katika siku ya nane na kuendelea, Yahwe alitangaza angewapokea.
Ezekiel 44
Ezekiel 44:1-3
Yule mtu alimrudisha Ezekieli kwenda wapi?
Yule mtu alimrudisha Ezekieli kwenye patakatifu pa lango la nje lililoelekea magharibi.
Nini kilifanyika kwenye lango la magharini, na kwa nini?
Lango la magharibi lilikuwa limepigwa muhuri kufungwa, kwa sababu Yahwe Mungu wa Israeli alikuja kupitia huo.
Ezekiel 44:4-5
Ezekieli aliambiwa afikiri kuhusu nini kuhusiana na nyumba ya Yahwe?
Ezekieli aliambiwa kufikiria kuhusu lango la kuingilia la nyumba ya Yahwe na lango la dharura.
Ezekiel 44:6-7
Ni matendo gani maovu waliyokuwa wameyafanya nyumba ya Israeli kupakufuru patakatifu pa Yahwe?
Nyumba ya Israeli iliwaleta wageni pamoja na wasiotahiriwa mioyo na nyama kwenda patakatifu.
Ezekiel 44:8-9
Kwa nini nyumba ya Israeli iliwaruhu wageni kuingia patakatifu pa Yahwe?
Nyumba ya Israeli iliwaruhusu wageni patakatifu pa Yahwe kwa sababu Israeli ilitoa kazi ya kubeba patakatifu kwao.
Ezekiel 44:10-12
Waliwi waliokuwa wamepotea kutoka kwa Yahwe walifanya nini?
Walawi waliokuwa wamepotea mbali na Yahwe walifanya sadaka mbele ya sanamu zao.
Ezekiel 44:13-14
Yahwe alisema Walawi ambao waliopotea kutoka kwa Yahwe hawataruhusiwa kufanya nini?
Yahwe alitangaza kwamba Walawi ambao walipotea mbali naye wasingekuja karibu naye kutena kama makuhani wake wala kukaribia kitu chake chochote kitakatifu, vitu vitakatifu sana.
Yahwe alikuwa akienda kuwaweka wapi Walawi waliokuwa waliopotea mbali naye?
Yahwe alisema angewaweka kama watunzaji wa kazi katika nyumba, kwa ajili ya kazi zake na kila kitu ambacho kimefanyika katika hiyo.
Ezekiel 44:15-16
Kwa nini Yahwe alitangaza kwamba wana wa Zadoki wangekuja karibu naye na wangesimama mbele yake?
Wana wa Zadoki walitakiwa kuja na kusimama mbele ya Yahwe kwa sababu walimaliza kazi za patakatifu pa Yahwe wakati watu wa Israeli walipopotea.
Ezekiel 44:17-19
Ni aina gani ya mavazi makuhani walitakiwa kuvaa wakati alipokuja kwenye malango ya ua wa ndani, na kwa nini?
Makuhani walitakiwa kuvaa mavazi ya kitani wakati walipokuja kwenye malango ya ua wa ndani ili wasitoe jasho.
Ezekiel 44:20-22
Kuhani alitakiwa kumuoa nani?
Kuhani aliruhusiwa kumuoa bikira kutoka safu ya nyumba ya Israeli, au mjane ambaye aliolewa na kuhani.
Ezekiel 44:23-27
Kati ya nini makuhani wangefundisha watu utofauti?
Makuhani walifundisha watu tofauti kati ya takatifu na kufuru, najisi na isiyonajisi.
Jukumu la kuhani lilikuwa nini katika mabishano kati ya Israeli?
Makuhani walisimama na kuhukumu kati ya watu pamoja na sheria za Yahwe, na ilitakuwa kuwa haki.
Ezekiel 44:28-29
Kwa nini makuhani hawakupokea mali yoyote wala urithi katika nchi ya Israeli?
Makuhani hawakupokea mali yoyote wala urithi katika nchi ya Israeli kwa sababu Yahwe alikuwa urithi wao na mali.
Kwa ufupi kuhani alitakiwa kula nini?
Makuhani walitakiwa kula chakula cha sadaka.
Ezekiel 44:30-31
Kuhani hakutakiwa kula nini?
Makuhani hawakutakiwa kula mzoga wala mnyama aliyejeruhiwa na mnyama, iwe ndege au mnyama.
Ezekiel 45
Ezekiel 45:1-2
Ni sadaka gani watu walitakiwa kufanya kwa Yahwe wakati wakipiga kura kugawanya nchi?
Watu walitakiwa kufanya sadaka ya sehemu takatatifu ya nchi wakati watakapopiga kura ya kugawanya nchi.
Ezekiel 45:3-5
Eneo takatifu ya nchi ilikuwa sehemu kwa ajili ya nini?
Eneo takatifu la nchi lilikuwa sehemu kwa ajili ya nyumba na miji ya makuhani.
Ezekiel 45:6-8
Eneo la mji lilikuwa mali nani?
Eneo la mji lilikuwa mali ya nyumba ya Israeli yote.
Ni nchi ya nani pande zote na mji zingekuwa za mahali patakatifu?
Nchi ya mwana wa mfalme wa Israeli pande zote za mji zilikuwa za mahali patakatifu.
Ezekiel 45:9-12
Yahwe alimwambia kuacha kufanya nini mwana wa mfalme wa Israeli?
Yahwe anamwambia mwana wa mfalme wa Israeli kuacha kuwafukuza watu wa Yahwe, na kuondoa vurugu na ugomvi.
Yahwe alisema lazima kiwekwe sawasawa?
Yahwe anasema usawa, efa, na bathi lazima vitengenezwe sawaswa.
Ezekiel 45:13-15
Je ni kiasi gani cha mafuta kutoka birika kumi zingekuwa kanuni ya kutoa mafuta?
Moja ya kumi ya birika kwa kila birika kumi ilitakiwa kuwa kanuni ya kutoa mafuta.
Ezekiel 45:16-17
Watu wa nchi walitoa mchango wao kwa nani?
Watu wa nchi wangetakiwa kutoa mchango wao kwa mwana wa mfalme wa Israeli.
Nani alitakiwa kuwajibika kutoa wanyama kwa ajili ya sadaka kwenye sikukuu ya nyumba ya Israeli?
Mwana wa mfalme katika Israeli alitakiwa kuwajibika kutoa wanyama kwa ajili ya sadaka.
Ezekiel 45:18-20
Makuhani walitakiwa kutoa wapi ng'ombe asiyekuwa na dosari kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya patakatifu?
Makuhani walitakiwa kutoa ng'ombe asiyekuwa na dosari kama sadaka ya kuteketeza siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza.
Ezekiel 45:21-24
Sikukuu ya siku ya saba ya mkate usotiwa chachu itakuwa wapi?
Katika siku ya kumi na nne ya kwanza ya mwezi kutakuwa na sikukuu ya mkate usiotiwa chachu.
Ezekiel 45:25
Ni sadaka gani ilitakiwa kutolewa siku ya kumi na sato ya mwezi wa saba?
Siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketeza, sadaka ya chakula, na sadaka ya mafuta zilitakiwa kutolewa.
Ezekiel 46
Ezekiel 46:1-2
Ni wakati gani Yahwe alisema lango la magharibi la ua wa ndani lingefunguliwa?
Yahwe alisema lango la magharibi la ua wa ndani lingefunguliwa siku ya Sabato na siku ya mwezi mchanga.
Mwana wa mfalme wa Israeli angeabudu wapi?
Mwana wa mfalme angeabudu kwenye kizingiti cha lango la ndani.
Ezekiel 46:3-5
Sadaka ya kuteketeza ya mwana wa mfalme ingekuwa siku ya Sabato?
Mwana wa mfalme angetoa wanakondoo zisizo na dosari na mwanakondoo mmoja asiye na dosari.
Ezekiel 46:6-8
Ni kanuni gani Yahwe alisema jinsi mwana wa mfalme anavyotakiwa kuishi baada ya kuabudu?
Yahwe alisema kanuni ilikuwa kwamba mwana wa mfalme atondoka kwa njia ile ile aliyoingilia kuabudu.
Ezekiel 46:9-10
Ni kanuni gani ambayo Yahwe alisema kuhusu jinsi ya watu kuishi baada ya kuabudu?
Yahwe alisema kanuni ilikuwa kwamba watu waingie kwa kwenda nje moja kwa moja mbele kutoka walipotokea kuingia.
Ezekiel 46:11-12
Mwana mfalme alitakiwa kutoa nini kwenye sherehe wakati atakapotoa sadaka ya hiari?
Mwana wa mfalme alipaswa kufungua lango la magharibi kwa ajili ya sadaka, na kisha kutoka nje na kufunga lango baada ya yeye.
Ezekiel 46:13-15
Kwa nini Yahwe anasema sadaka ya kuteketezwa kila asubuhi?
Yahwe alisema kondoo asiye na hatia mwenye umri wa mwaka mmoja angetolewa kama sadaka ya kutekeza kila asubuhi.
Ezekiel 46:16-18
Kutokana na Yahwe, nani angepokea urithi wa mwana wa mfalme?
Mrithi wa mwana mfalme ungepokelewa na wana wake.
Kwa nini Yahwe anasema mwana mfalme lazima auondoe urithi wa watu?
Urithi wa watu hautachukuliwa hivyo hawajatawanyika kutoka kwenye milki zao wenyewe.
Ezekiel 46:19-20
Kwa nini makuhani hawakurudisha hatia, dhambi, na sadaka za unga nje kwenye ua wa nje?
Makuhani hawakuridisha sadaka nje ya ua wa nje na hivyo kuwaweka watu wakafu.
Ezekiel 46:21-24
Nini kitakamilika katika kupika meko kwenye pembe ya ua wa nje?
Katika kupika meko kwenye pembe za ua wa nje, watumishi wa hekalu watachemsha dhabihu za watu.
Ezekiel 47
Ezekiel 47:1-2
Ni mwelekeo gani hekalu lilielekea katika maono ya Ezekieli?
Hekalu lilielekea magharibi.
Ezekieli aliona nini kwenye lango linaloelekea magaharibi?
Ezekieli aliona maji yakibubujika kutoka kwenye lango linaloelekea magharibi, upande wake wa kusini.
Ezekiel 47:3-5
Je! Ni maji marefu kiasi gani yalikuwa ambayo Ezekieli alyaona?
Maji yakawa mto ambao ulikuwa mrefu sana kupita bila kuogelea.
Ezekiel 47:6-10
Nini kilikuwa pande zote za mto?
Pande zote za mto, ukingo wa mto ulikuwa na miti mingi.
Haya maji yalibubujika kuelekea wapi, na yalifanya nini huko?
Haya maji yalibubujika kuelekea Bahari Kuu na itarudishwa kuzidi.
Ezekiel 47:11-12
Nini hakitakuwa kipya kwenye Bahari Kuu?
Kujaa maji na matope hakutaifanya mpya Bahari Kuu.
Ni aina gani ya miti itamea juu ya ukingo wa mto, na itameaje?
Miti ya chakula itamea juu ya ukingo wa mto, ikizaa matunda kila mwezi na haitanyauka.
Ezekiel 47:13-14
Nani atapokea sehemu mbili za nchi miongoni mwa makabila ya Israeli?
Yusufu atapokea sehemu mbili za nchi miongoni mwa makabila ya Israeli.
Ezekiel 47:15-17
Mpaka wa kaskazini mwa nchi utafika hata mpaka wa mji gani?
Mpaka wa magharibi mwa nchi utafikia hata mpaka wa Damaskasi.
Ezekiel 47:18-20
Nini kitakuwa mpakani mwa magharibi mwa nchi?
Magharibi mwa mpaka wa nchi kutakuwa na Mto Yordani.
Ni kijito kipi cha maji kitakuwa sehemu ya mpakani kusini mwa nchi?
Kijito cha Misri kitakuwa sehemu ya mpakani kusini mwa nchi.
Nini kitakuwa mpakani magharibi mwa nchi?
Mpakani magharibi nchi kutatokea Bahari Kuu.
Ezekiel 47:21-23
Waisraeli waliainishaje urithi kwa ajili ya kila mmoja katika nchi?
Waisraeli walikuwa watupe mengi kuainisha urithi kwa kila mtu katika nchi.
Nani walitendewa mema kama mwenyeji mzaliwa na watu wa Israeli?
Wageni wanaoishi katikati mwa Waisraeli walitendewa mema kama wenyeje wazawa wa watu wa Israeli.
Ezekiel 48
Ezekiel 48:1-3
Ni kabila lipi litapewa nchi upande wa kaskazini mwa Israeli?
Kabila la Dani litapatiwa nchi upande wa mpaka wa kaskazini mwa Israeli.
Ni kabila lipi litakalokuwa kusini mwa mpaka wa kabila la Dani?
Kabila Asheri litakuwa kusini mwa mpaka wa Dani.
Ni kabila lipi litakuwa kusini mwa mpaka wa kabila la Asheri?
Kabila la Naftali litakuwa kusini mwa mpaka wa Asheri.
Ezekiel 48:4-7
Katika mpangilio, ni makabila yapi manne yangekuwa kusini mwa kabila la Naftali?
Katika mpangilio, makabila manne ya kusini mwa Naftali yatakuwa ya Manase, Efraimu, Rubeni, na Yuda.
Ezekiel 48:8-9
Itakuwaje katikati mwa nchi iliyoko karibu na mpaka pamoja na Yuda?
Hekalu litakuwa katikati ya nchi iliyokaribu na mpaka pamoja na Yuda.
Ezekiel 48:10-12
Nani angeishi kwenye inayozunguka patakatifu pa Yahwe?
Makuhani wa safu ya Zadoki wataishi kwenye nchi inayozunguka patakatifu pa Yahwe.
Ezekiel 48:13-16
Nani angeishi upande wa nchi kupakana na nchi ya kuhani?
Walawi wangeishi upande wa nchi kupakana na nchi ya kuhani.
Ezekiel 48:17-20
Kwa ajili ya nini eneo la sadaka takatifu mwa nchi lililokuwa limesalia kutumika?
Eneo la sadaka takatifu ya nchi lilikuwa limesalia kutumika kuzaa chakula kwa ajili wale wanaofanya kazi katika mji.
Ezekiel 48:21-26
Kwa ajili ya nani nchi ingekuwa mipaka ya upande wa mashariki na magharibi mwa sadaka takatifu ya nchi?
Mipaka ya upande wa magharibi na mashariki mwa sadaka ya takatifu mwa nchi itakuwa kwa ajili ya mwana wa mfalme.
Ezekiel 48:27-29
Nini kilitakiwa kuwa kwenye mpaka wa kusini mwa Gadi?
Mpaka wa kusini mwa Gani ulitakiwa kunyoshwa kutoka Tamari kwenda maji ya Meriba Kadeshi, na mbele zaidi hata kwenye kijito cha Misri, na kisha hata kwenye Bahari Kuu.
Ezekiel 48:30-32
Je! Ni malango mangapi yalitakiwa kuwa upande wa kaskazini ya mji, na yalikuwa yaitwe kwa ajili ya nini?
Kulikuwa na malango matatu upande wa kaskazini mwa mji, pamoja na mmoja ulioitwa kwa ajili ya Rubeni, mmoja kwa ajili ya Yuda, na mmoja kwa ajili ya Lawi.
Ezekiel 48:33-35
Jina la mji lingekuwaje?
Jina la mji lingekuwa "Yahwe yuko hapa".