Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Joshua

Joshua 1

Joshua 1:1-3

Yahweh alimwambia Yoshua afanye nini baada ya kifo cha Musa?

Yahew alimwambia Yoshua kuvuka Yordani na kuwaongoza watu wa Israeli katika nchi ambayo Yahweh angewapa.

Joshua 1:4-5

Kwanini Yahweh alisema kwamba hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kusimama dhidi ya Yoshua?

Yahweh alisema kuwa hapatakuwa na mtu yeyote akayesimama kinyume cha Yoshua kwasababu atakuwa pamoja na Yoshua kama vile alivyokuwa na Musa.

Joshua 1:6-7

Ni vitu gani vitatu ambavyo Yahweh alivitaka kwa Yoshua?

Yahweh alimtaka Yoshua kuwa shujaa, jasiri na kutii sheria.

Joshua 1:8-9

Ni kitu gani ambacho Yahweh alimtaka Yoshua atafakari mchana na usiku?

Yahweh alimtaka Yoshua kukitafakari kitabu cha sheria mchana na usiku

Joshua 1:10-11

Ni kitu gani ambacho Yoshua aliwaagiza viongozi wa watu wafanye?

Yoshua aliwaamuru viongozi wa watu kuwaagiza watu kuandaa vyakula kwa ajili yao kuvuka Yordani katika siku tatu.

Joshua 1:12-13

Ni vitu gani viwili ambavyo Yoshua alivisema kuwa Musa alikuwa amevisema kuwa Yahweh alikuwa amewaagiza Warubeni, Wagadi na nusu ya Manase ili wakumbuke?

vitu viwili ambavyo Yoshua alivisema kuwa Musa alikuwa amevisema kuwa Yahweh alikuwa amewaagiza Warubeni, Wagadi na nusu ya Manase ili wakumbuke ni "Yahweh Mungu wenu anawapa pumziko, na anawapeni ninyi nchi hii"

Joshua 1:14-15

Je Yoshua aliwaambia nini Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase ili wafanye?

Yoshua aliwaambia Warubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kuwaacha wake zao, watoto na mifugo katika nchi ambayo Musa alikuwa amewapa ng'ambo ya Yordani, lakini watu wa vita walitakiwa kuvuka Yordani na kuwasaidia ndugu zake.

Joshua 1:16-18

Je watu waliitikiaje agizo la Yoshua?

Watu waliitikia agizo la Yoshua kwa kusema kuwa wangelifanya kile alichokisema wakifanye na kwenda kokote alikosema waende.

Joshua 2

Joshua 2:1-3

Ni sehemu gani ambayo wapelelezi wawili kutoka Shitimu walipata mahali pa kulala wakati Yoshua alipowatuma kuipeleleza nchi?

Wapelelezi wawili walipata huduma ya malazi katika nyumba ya kahaba aliyeitwa Rahabu.

Joshua 2:4-7

Rahabu alifanya nini kwa wapelelezi wakati watu wa mfalme waliokuja kuwaangalia wapelelezi?

Rahabu aliwaficha wapelelezi wakati watu wa mfalme walipokuja kwake kwa ajili ya kuwatafuta wapelezi.

Rahabu aliwaambia nini wale watu wa mfalme?

Rahabu aliwaambia watu wa mfalme kuwa wapelezi hawapo pale, bali wameshaenda.

Joshua 2:8-9

Kwanini Rahabu aliwaambia wapelelezi sababu iliyomfanya awafiche?

Rahabu aliwaambia wapelelezi kwamba alikuwa amewaficha kwasababu anamwamini Yahweh kuwa ameshawapa nchi.

Joshua 2:10-11

Je Rahabu alisema nini juu ya sababu alizokuwa anaziamini kuwa Yahweh angewapa Waisraeli nchi?

Rahabu aliamini Yahweh alikuwa amewapa Waisraeli nchi kwasababu maji ya Bahari ya chumvi yalikuwa yamekauka kuwaruhusu watoke Misri, na ya kwamba walikuwa wamemwaangamiza mfalme wa Waamori.

Joshua 2:12-13

Rahabu aliwaomba wapelelezi wamfanyie nini?

Rahabu aliwaomba Wapelelezi wamwonee huruma na kumhifadhi yeye na familia yake wakati walipokuja kuichukua nchi.

Joshua 2:14-17

Je wapelelezi walimwahidi nini Rahabu?

Wapelelezi walimwahidi Rahabu kwamba watakuwa na huruma na waaminifu kwake kama hatasema mambo yao.

Joshua 2:18-22

Je wapelelezi walimwomba Rahabu afanye nini ili awae salama?

Wapelelezi walimwambia Rahabu afunge kamba katika dirisha la nyumba yake na kukusanya familia yake ndani ya nyumba yake.

Joshua 2:23-24

Je wapelelezi walitoa taarifa gani kwa Yoshua wakati waliporudi kutoka kwa mji wa Rahabu?

Wapelelezi walimwambia Yoshua kila kitu kilichotokea, na ya kwamba Yahweh alikuwa anawapa nchi.

Joshua 3

Joshua 3:2-4

Je maafisa walimwambia watu wafuate nini wakati makuhani wa Kilawi walipolibeba saunduku la Agano?

Maafisa waliaambia watu walifuate sanduku la Agano wakati makuhani wa Kilawi watakapolibeba.

Kwanini makuhani waliwaambia watu kubaki umbali wa dhiraa 2000 nyuma ya sanduku la Agano?

Makuhani waliwaambia watu wabaki nyuma ya sanduku ili waweze kuona njia ya kupita kwa kuwa walikuwa hawajawhi kupita njia hiyo kabla.

Joshua 3:5-6

Yoshua alisema nini juu ya kile Yahweh alikuwa anaenda kukifanya kwa watu siku ile?

Yoshua alisema kwamba Yahweh alikuwa anaenda kufanya "maajabu" miongoni mwa watu siku ile.

Joshua 3:7-11

Je Yahweh alimwambia Yoshua awaambie nini makuhani wakati watakapofika Yordani?

Yahweh alimwambia Yoshua kuwaambia makuhani kusimama kimya katika mto Yordani.

Joshua 3:12-13

NI kitu gani ambacho Yoshua aliwaambia watu kuwa kingetokea wakati nyayo za miguu ya makuhani waliobeba sanduku itakapogusa Mto Yordani?

Yoshua aliwaambia watu kuwa maji yangetengwa wakati nyayo za miguu ya makuhani wabebao sanduku itakapogusa mto.

Joshua 3:14-16

Ni sehemu gani ambayo watu walivuka katika Mto Yordani?

Watu walivuka Mto Yordani karibu na Yeriko.

Joshua 3:17

Je makuhani waliobeba sanduku walikuwa wanafanya nini wakati watu walipokuwa wanavuka?

Makuhani waliobeba sanduku la Agano walibaki katikati ya Mto Yordani katika sehemu kavu wakati watu walipokuwa wanavuka.

Joshua 4

Joshua 4:1-5

Ni gani ambacho Yahweh alimwambia Yoshua awaagize watu kumi na wawili wachukue katika Yordani?

Yahweh alimwambia Yoshua awaagize watu kumi na wawili wachukue mawe kutoka katika sehemu kavu katikati ya Yordani sehemu ambayo makuhani walikuwa wamesimama, na kuyaleta katika sehemu ambayo wangelala usiku ule.

Joshua 4:6-7

Yoshua alisema nini juu ya sababu ya kuchukua mawe na kuyaweka sehemu watakapolala usiku?

Mawe yangekuwa kumbukumbu kwa ajili ya kuwakumbusha watu wa Israeli milele juu ya kile ambacho Yahweh alikuwa amekifanya.

Joshua 4:8-11

Ni sehemu gani ambayo Yoshua alijenga mnara wa kumbukumbu wa mawe kumi na mawili?

Yoshua alijenga mnara wa mawe kumi na mawili katika sehemu ambapo makuhani walikuwa wamesimama juu ya nchi kavu ndani ya Mto Yordani.

Joshua 4:12-16

Walikuwa ni watu wapatao wangapi walioandaliwa kwa ajili ya vita waliopitishwa na Yahweh kwa ajili ya mapigano katika uwanda wa Yeriko?

Watu wapatao 40,000 walioandaliwa kwa ajili ya vita waliopitishwa na Yahweh kwa ajili ya mapigano katika uwanda wa Yeriko.

Joshua 4:17-18

Ni kitu gani kilitokea wakati makuhani waliobeba sanduku la agano walipotoka katika Mto Yordani?

Maji ya Yordani yalirudi katika sehemu yake baada ya makuhani kutoka Yordani.

Joshua 4:19-21

Ni sehemu gani ambayo Yoshua aliyaweka mawe yaliyotolewa Yordani?

Yoshua aliyaweka Gilgali mawe yaliyotolewa Yordani.

Joshua 4:22-24

Kwanini Yoshua aliwaambia watu wawaambie watoto wao kile ambacho Yahweh alikuwa amewatendea huko Yordani?

Yoshua aliwaambia watu waambie watoto wao kile ambacho Yahweh alikuwa amewatendea huko Yordani ili mataifa/watu wote wajue kwamba mkono wa Yahweh ni wenye nguvu.

Joshua 5

Joshua 5:2-5

Yahweh alimwagiza Yoshua afanye nini na visu vya mawe?

Yahweh alimwagiza Yoshua awatahiri wanaume wote wa Israeli.

Joshua 5:6-9

Kwanini Yoshua aliagizwa kuwatahiri wanaume wote wa Israeli?

Yoshua aliagizwa kuwatahiri wanaume wote wa Israeli kwasababu wavulana waliokuwa wamezaliwa kipindi cha kuzunguka jangwani walikuwa bado hawajatahiriwa.

Joshua 5:10-12

Watu wa Israeli walitunza nini katika siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika nyanda za Yeriko?

Waisraeli waliitunza Pasaka katika siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni katika nyanda za Yeriko.

Joshua 5:13

Yoshua alikutana na nani aliyekuwa amesimama mbele yake huko Yeriko?

Yoshua alikutana na mtu aliyekuwa na upanga umechomolewa mkononi mwake.

Joshua 5:14-15

Je Yoshua alimwambia nini mtu aliyekuwa na upanga umechomolewa?

Yoshua alimwambia mtu aliyekuwa na upanga "je uko upande wetu au upande wa maadui wetu?"

Mtu mwenye upanga ulichomolewa alisema kuwa yeye ni nani?

Mtu aliyekuwa na upanga alimwambia Yoshua kuwa alikuwa ni kamanda wa jeshi la Yahweh.

Je kamanda wa jeshi la Yahweh alimwambia Yoshua afanye nini?

Kamanda wa jeshi la Yahweh alimwambia Yoshua kuondoa viatu vyake, kwa kuwa alikuwa sehemu takatifu.

Joshua 6

Joshua 6:1-2

Je Yahweh alimwahidi nini Yoshua kuhusu Yeriko?

Yahweh alimwahidi Yoshua kwamba alikuwa amempa Yeriko katika mkono wake.

Joshua 6:3-4

Ni mara ngapi watu wa Israeli walitakiwa kutembea kuzunguka ukuta wa Yerika kwa siku sita za mwanzo?

Watu wa Israeli walitakiwa kutembea kwa kuzunguka ukuta wa Yeriko mara moja kila siku kwa siku sita.

Joshua 6:5-9

Je Yahweh aliwaambia watu wafanye nini katika siku ya saba?

Yahweh aliwaambia watu watembee kwa kuizunguka Yeriko mara saba katika siku ya saba, na makuhani wapulize tarumbeta zao.

Je Yahweh alisema nini kingetokea kama watu wa Israeli na makuhani wangefanya hivyo?

Yahweh alisema kuwa kuta zilizoizunguka Yeriko zingeanguka chini kama watu na makuhani wangefanya hivyo.

Joshua 6:10-16

Je Yoshua aliwaagiza watu wasifanye nini mpaka siku ya saba?

Yoshua aliwaagiza watu wasipige kelele mpaka siku ya saba.

Joshua 6:17-19

Ni nani ambaye Yoshua aliwaambia watu wamwache hai wakati ambapo Yahweh aliwapa mji?

Yoshua aliwaambia watu wamwache hai Rahabu na watu wote katika nyumba yake kwasababu aliwaficha wapelelezi.

Ni vitu gani ambavyo Yoshua aliwaambia watu kwamba vilikuwa vitakatifu na lazima viletwe kwenye hazina?

Yoshua aliwaambia watu kwamba vitu vilivyofanywa kwa fedha, dhahabu, chuma na shaba vilikuwa vitakatifu kwa Yahweh na lazima viletwe katika hazina.

Joshua 6:20-21

Watu wa Israeli walifanya nini wakati kuta za Yeriko zilipoanguka?

Watu wa Israeli waliuteka mji na kuuharibu vyote ambavyo vilikuwa katika mji kwa ukali wa upanga.

Joshua 6:22-25

Yoshua aliwaagiza wale vijana wawili walioipeleleza nchi wafanye nini?

Yoshua aliwaagizwa wapelelezi wawili kwenda katika nyumba ya kahaba na kumtoa nje yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kama walivyokuwa wamemwapia.

Joshua 6:26-27

Je Yoshua alisema kutatokea nini kwa mtu anayetaka kuijenga tena Yeriko?

Yoshua alisema kwamba mtu atakayejaribu kuijenga Yeriko atalaaniwa.

Joshua 7

Joshua 7:1

Kwanini hasira ya Yahweh iliwaka kinyume cha watu Israeli?

Hasira ya Yahweh iliwaka dhidi ya watu wa Israeli kwasababu Akani alichukua baadhi ya vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu ili kuteketezwa kwa ajili yake mwenyewe.

Joshua 7:2-3

Je wapelelezi waliokuwa wametumwa na Yoshua kwenda Ai walitoa taarifa gani kwa Yoshua?

Wapelelezi walikuwa wametumwa kwenda Ai walitoa taarifa kwa Yoshua kwamba kulikuwa na watu wachache tu kule, hivyo jeshi dogo tu linaweza kuiteka Ai.

Joshua 7:4-5

Kulitokea nin kwa jeshi dogo la watu elfu tatu walioishambulia Ai?

Jeshi dogo lililoishambulia Ai lilifukuziwa mbali na watu wa Ai na watu thelathini na sita waliuawa.

Joshua 7:6-9

Yoshua alifanya nini baada ya kujifunza juu ya kushindwa kwa jeshi lake huko Ai?

Baada ya Yoshua kujifunza juu ya kushindwa kwa jeshi lake huko, alichana nguo zake, aliweka mavumbi kichwani, na kulala mbele ya sanduku.

Joshua 7:10-12

Yahweh alimwambia nini kuwa ilikuwa sababu ya kushindwa kwa jeshi lake huko Ai?

Yahweh alimwambia Yoshua kwamba jeshi lake lilishindwa kwasababu Israeli walikuwa wametenda dhambi kwa kuiba vitu vilivyokuwa wamewekwa wakfu ili kuteketezwa.

Joshua 7:13

Yahweh alimwambia Yoshua afanye nini?

Yahweh alimwambia Yoshua kuamka na kuwaweka wakfu watu ili wavitoe vitu vilivyokuwa vimetengwa kwa ajili ya kuteketezwa.

Joshua 7:14-18

Je Yahweh alisema kuwa ni kitu gani kingetokea kwa mtu yule ambaye alikuwa ameiba vitu vilivyokuwa vimetengwa ili kuteketezwa?

Yahweh alisema kwamba mtu yule aliyekuwa ameiba vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuteketezwa angechomwa moto na vitu vyote alivyo navyo.

Joshua 7:19-23

Je Akani alimwambia Yoshua kuwa alikuwa amechukua nini?

Akani alimwambia Yoshua kuwa alikuwa amechukua koti zuri, shekeli mia mbili za fedha, na kipande cha dhahabu.

Joshua 7:24

Yoshua na Waisraeli wote walimpeleka wapi Akani pamoja na vyote alivyokuwa navyo?

Yoshua na waisraeli walimchukua Akani na vyote ambavyo alikuwa navyo katika bonde la Akori.

Joshua 7:25-26

Ni nini kilitokea kwa Hasira ya Yahweh iliyokuwa inawaka?

Yahweh aliiachilia mbali hasira yake iliyokuwa inawaka.

Joshua 8

Joshua 8:1-2

Yahweh alimwambia Yoshua afanye nini ili kuuchukua mji wa Ai?

Yahweh alimwambia Yoshua kuchukua watu wote wa vita huko Ai na kuweka watu wa kuvizia nyuma ya mji.

Je watu walitakiwa kufanya nini na nyara walizozitoa huko Ai?

Yahweh aliwaambia watu walitakiwa kuchukua nyaara na mifugo kwa ajili yao wenyewe.

Joshua 8:3-7

Ni lini Yoshua aliwatuma watu shujaa na wenye nguvu thelathini elfu huko Ai?

Yoshua aliwatuma watu shujaa na wenye nguvu thelathini elfu kwenda Ai wakati wa usiku.

Je Yoshua alipanga kufanya nini pamoja na watu wake wakati walipoukaribia mji?

Wakati Yoshua alipoukaribia mji pamoja na watu wake, watu wa mji walitoka ili kushambulia, watu wa Yoshua wangekimbia kama mwanzo.

Joshua 8:8-14

Je watu wa Yoshua walitakiwa kufanya nini kwa mji baada ya kuutwaa?

Baada ya watu kuutwaa mji, walitakiwa kuuchoma moto.

Joshua 8:15-17

Watu wa Ai walifanya nini baada ya jeshi la Yoshua kukimbilia jangwani?

Watu wa Ai walilifuata jeshi la Yoshua walipokuwa wanakimbia kuelekea jangwani, mapaka kulipokuwa hakuna mtu yeyote katika mji.

Joshua 8:18-21

Ni ishara gani ambayo Yahweh alimwambia Yoshua kuwa angetoa wakati jeshi lake litakapokuwa tayari kuutwaa mji?

Yahweh alimwambia Yoshua kunyosha mkuki alioushikilia mkononi mwake kuelekea Ai.

Joshua 8:22-23

Watu wa Israeli walimshika nani akiwa hai na kumleta kwa Yoshua?

Watu wa Israeli walimteka mfalme wa Ai akiwa hai na kumleta kwa Yoshua.

Joshua 8:24-26

Je Yoshua aliteketeza akina nani katika mji Ai?

Yoshua aliwateketeza watu wote wa Ai.

Joshua 8:27-28

Waisraeli walichukua nini kutoka katika mji wa ai kabla ya kuchoma moto?

Waisraeli walichukua wanyama na nyara, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwaagiza Yoshua.

Joshua 8:29-35

Yoshua alimfanyia nini mfalme wa Ai?

Yoshua alimning'iniza mfalme wa Ai juu ya mti na kisha akautupa mwili wake mbele ya malango ya mji.

Joshua 9

Joshua 9:1-2

Je wafalme walioishi ng'ambo ya Yordani katika nchi ya milima walifanya nini ili kupigana vita dhidi ya Yoshua na Israeli?

Wafalme walioishi ng'ambo ya Yordani katika nchi ya milima waliungana pamoja chini ya amri moja ili kumshinda Yoshua na Israeli.

Joshua 9:3-5

Ni akina nani waliofanya mpango wa udanganyifu?

Wenyeji wa Gibeoni walifanya mpango wa udanganyifu

Je "wajumbe" wa Wagibeoni walijiaandaje wao wenyewe?

Walichukua magunia yaliyochakaa na kuyaweka juu ya punda. Walichukua pia viriba vilivyochakaa na kuchanika chanika na vilivyozibwa zibwa. Walivaa miguuni mwao viatu vilivyozeeka na kutoboka toboka, na walivaa nguo kuukuu, zilichanika chanika. Na mikate yote katika chombo ilikuwa mikavu na yenye uvundo

Joshua 9:6-13

Wakati Wagibeoni walipoenda kwa Yoshua walimwambia kuwa wanatoka wapi?

Wagibeoni walisema kuwa wanatoka katika nchi ya mbali.

Wagibeoni walitaka watu wa Israeli wafanye nini?

Wagibeoni waliwataka watu wa Israeli wafunge nao mkataba.

Joshua 9:14-15

Waisraeli walishindwa kufanya nini?

Waisraeli hawakumhusisha/kumshirikisha Yahweh ili awaongoze.

Yoshua aliwaahidi nini watu wa Gibeoni?

Yoshua alifanya amani pamoja nao na kuwaapia ili wawache hai.

Joshua 9:16-17

Waisraeli walijifunza nini juu ya watu kutoka Gibeoni baada ya siku chache?

Waisraeli waligundua kkuwamba watu wa Gibeoni walikuwa majirani na waliishi karudi.

Joshua 9:18-19

Kwanini waisraeli hawakuwashambulia watu wa Gibeoni?

Waisraelli hawakushambulia watu wa Gibeoni kwasababu walikuwa wameapia mbele ya Yahweh.

Joshua 9:20-23

Je Wagibeoni walifanya nini kwa Waisraeli?

Wagibeoni wakawa wakata kuni na wachota maji wa Waisraeli wote,

Joshua 9:24-25

Ni sababu gani iliwafanya Wagibeoni kujisalimisha kwa Yoshua na kwanini walikuwa wamemdanganya?

Wagibeoni walimwambia Yoshua kwamba walikuwa wameogopa kwa ajili ya maisha yao.

Joshua 9:26-27

Ni kitu gani kingetokea kwa Wagibeoni?

Yoshua aliwaondosha wasiwe na nguvu dhidi ya Waisraeli na kuwafanya kuwa wakati kuni na wachota maji kwa ajili ya jamii na madhabahu ya Yahweh.

Joshua 10

Joshua 10:1-2

kwanini watu wa Yerusalemu waliogaopa kwa kuwa watu wa Gibeoni walikuwa wamefanya amani na Israeli?c

Watu wa Yerusalem waliogopa kwasababu Gibeoni ulikuwa ni mji mkubwa, mkubwa kuliko Ai, watu wake wote walikuwa ni watu shujaa.

Joshua 10:3-4

Mfalme wa Yerusalemu aliwaomba wafalme wengine wafanye nini?

Mfalme wa Yerusalemu aliwaomba wafalme wengine waje kwake na kumsaidia kuishambulia Gibeoni..

Joshua 10:5

Wafalme walifanya nini?

Walipanda pamoja na majeshi yao yote na kuishambulia Gibeoni.

Joshua 10:6-7

Je watu wa Gibeoni walifanya nini baada ya kuwaona wafalme wote na majeshi yao?

Watu wa Gibeoni walituma ujumbe kwa Yoshua ili aje na kuwaokoa.

Joshua 10:8-10

Yahweh alimwambia nini Yoshua?

Yahweh alimwambia Yoshua kuwa wafalme wameshatiwa mkononi mwake.

Joshua 10:11

Je, Yahweh aliwauje maadui wengi?

Yahweh alitupa mawe makubwa kutoka mbinguni ambayo yaliwaua wengi kuliko wale waliouawa kwa upanga wa watu.

Joshua 10:12-14

Yoshua alimwambia nini Yahweh katika siku ile ambayo Yahweh aliwapa ushindi watu wa Israeli?

Yahweh alimwambia Yahweh, "Jua lisimame katika Gibeoni na mwezi, katika bonde la Aijaloni"

Joshua 10:15-19

Ni kitu gani kilichowatokea wafalme watano?

Wafalme watano walijificha katika pango la Makeda.

Joshua 10:20-25

Kilitokea nini kwa majeshi ya wafalme?

Waisraeli walichinja wengi wao. Ni watu wachache walitoroka.

Joshua 10:26-39

Kilitokea nini kwa wafalme watano walikuwa wamejificha katika pango la Makeda?

Wafalme watano waliokuwa wamejificha katika pango waliletwa kwa Yoshua, waliwashambulia na kuwaua, waliwaning'iniza juu ya miti mitano mpaka wakati wa kuzama kwa jua, na kisha walitupwa katika pango.

Joshua 10:40-41

Yoshua na jeshi la Israeli walifanya nini katika nchi yote ya milima, Negevu, nchi ya tambarare na nchi ya miteremko?

Yoshua na jeshi la Israeli waliwashinda wafalme wote bila kuacha hai hata mtu mmoja.

Joshua 10:42-43

kwanini Yoshua alifanikiwa kuwateka wafalme wote hawa na nchi zao?

Yoshua alifanikiwa kuwateka wafalme hawa na nchi zao kwasababu Yahweh, Mungu wa Israeli, aliwapigania Israeli.

Joshua 11

Joshua 11:1-3

Mfalme wa Yabini wa Hazori alifanya nini wakati aliposikia kuhusu ushindi wa Waisraeli huko Gibeoni?

Alituma ujumbe kwa wafalme wengi kutoka katika mkoa.

Joshua 11:4-5

Mwitikio wa wafalme ulikuwaje kwa ujumbe wa Yabini?

Katika kujibu ujumbe wa Yabini, majeshi yao yote yalikuja pamoja nao na walikutana kwa wakati waliokubaliana na wakapiga kambi katika maji huko Meromu ili kupigana vita na Israeli.

Je hesabu yao ilionekanaje?

Hesabu yao ilionekana kama mchanga wa pwani ya bahari.

Joshua 11:6-9

Yahweh alimwambia nini Yoshua kuwa angefanya baada ya vita?

Yahweh alimwambia Yoshua kuwa angevunja vunja miguu ya farasi zao na kuyachoma magari yao.

Joshua 11:10-11

Je Yoshua alifanya nini huko Hazori na kwa mfalme wake?

Yoshua aliuchoma moto mji na kumwua mfalme kwa upanga wake.

Joshua 11:12-13

Je Yoshua alifanya nini kwa wafalme waliosalia na miji ambayo ilipigana vita na Israeli?

Yoshua aliwateka wafalme na kuwaangamiza, lakini hakuichoma moto miji yao.

Joshua 11:14-17

Musa alikuwa amemwagiza Yoshua afanye nini?

Musa alikuwa amemwagiza Yoshua kuua kila mtu.

Je, Yoshua alifanya mambo yote ambayo Musa alikuwa amemwamuru kufanya?

Ndiyo, Yoshua aliyafanya yote ambayo Musa alikuwa amemwamuru kuyafanya.

Joshua 11:18-23

Ni mji gani pekee uliofanya amani na Israeli?

Mji peeke uliofanya amani na Israeli ulikuwa Gibea.

Joshua 12

Joshua 12:1-5

Waisraeli walifanya nini kwa nchi iliyokuwa upande wa mashariki wa Yordani?

Walichukua mali za nchi ya upande wa mashariki mwa Yordani sehemu ya mchewo ya jua.

Joshua 12:6

Ni nani aliwaongoza watu wa Isareli wakati walipowashinda watu wa upande wa mashariki mwa Yordani?

Musa, mtumishi wa Yahweh aliwaongoza kuwashinda watu wa upande wa mashariki mwa Yordani.

Joshua 12:7-20

Ni nani aliwaongoza watu wa Isareli wakati walipowashinda watu wa upande wa magharibi mwa Yordani?

Musa, mtumishi wa Yahweh aliwaongoza kuwashinda watu wa upande wa magharibi mwa Yordani.

Joshua 12:21-24

Ni wafalme wangapi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda katika nchi ambayo Yahweh alikuwa amewapa?

Yoshua na Waisraeli waliwashinda wafalme thelathini na moja katika nchi ambayo Yahweh alikuwa amewapa.

Joshua 13

Joshua 13:6-7

Yahweh alimwambia Yoshua afanye nini baada ya kuwaondoa wenyeji mbele ya jeshi la Israeli?

Yahweh alimwambia Yoshua kuwapa waisraeli nchi kama urithi kama vile Yahweh alivyokuwa ameagiza.

Ni akina walipaswa kugawana nchi?

Nchi ilipaswa kugawanywa kama urithi kwa makabila tisa na nusu ya kabila la Manase.

Joshua 13:8-13

Je makabila mengine mawili na nusu yalikuwa yamepata urithi wake wapi?

Nusu ya kabila la Manase, Warubeni na Wagadi walikuwa wamepata urithi wao upand wa mashariki mwa Yordani.

Joshua 13:14-21

Ni kabila gani moja ambalo Musa halikupa urithi?

Musa halikupa urithi kabila la Lawi.

Urithi gani kabila la Lawi lilipewa?

Musa alilipa kabila la Lawi "Matoleo ya Yahweh, Mungu wa Israeli, iliyotolewa kwa moto" kama urithi wao.

Joshua 13:22-33

Mpaka wa kabila la Rubeni ulikuwa ni nini?

Mpaka wa kabila la Rubeni ulikuwa ni Mto Yordani.

Joshua 14

Joshua 14:2-5

Ni makabila gani mawili yaliyounda kabila la Yusufu?

Makabila ya Manase na Efraimu yaliunda kabila la Yusufu.

Joshua 14:6-7

Kalebu alikuwa na umri wa miaka mingapi wakati Musa mtumishi wa Yahweh alipomtuma kuipeleleza nchi?

Alikuwa na umri wa miaka arobaini wakati ule Musa Mtumishi wa Yahweh alipomtuma kutoka Kadeshi Barnea kwenda kuipeleleza nchi.

Joshua 14:8-9

Ni kitu gani ambacho Musa aliapa kumpa Kalebu?

Musa aliapa kumpa Kalebu nchi ambayo miguu yake imetembea juu yake kama urithi wake na kwa ajili ya watoto wake milele.

Joshua 14:10-11

Kalebu alikuwa na umri wa miaka mingapi alipomjia Yoshua?

Kalebu alikuwa na umri wa miaka themanini na tano wakati alipomjia Yoshua.

Joshua 14:12-15

Kalebu alimwomba Yoshua ampe nini?

Kalebu alimwaomba Yoshua ampe urithi wake katika nchi ya milima.

Joshua 15

Joshua 15:1-4

Sehemu ya gani ya mbali ya kusini ambako nchi ya Yuda ilifika?

Upande wa kusini ya mbali ambako ilifika ni bara la Sini.

Joshua 15:5-6

Mpaka wa upande wa Mashariki wa nchi ya Yuda ulikuwa ni nini?

Mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa ni Bahari ya Chumvi.

Joshua 15:7-10

Mji wa Wayebusi uliitwaje?

Jina la mji wa Wayebusi ni Yerusalemu.

Joshua 15:11-18

Mpaka wa Kaskazini wa ukoo Yuda ulikuwa ni nini?

Mpaka wa magharibi wa ukoo wa Yuda ulikuwa ni Bahari kuu na pwani yake.

Joshua 15:19-62

Kalebu alimpa nini binti yake, Akisa, baada ya kuwa amemwomba?

Kalebu alimpa Akisa chemichemi ya juu na ya chini ya baada ya kuwa amemwomba.

Joshua 15:63

Watu gani ambao kabila la Yuda halikuwafukuza watoke Yerusalemu?

Kabilal la Yuda halikuwafukuza Wayebusi watoke Yerusalemu.

Joshua 16

Joshua 16:3-9

Ni makabila gani ya Yusufu yaliyopokea urithi wake kwa pamoja?

Makabila ya Manase na Efraimu wana wa Yusufu walipokea urithi wao pamoja.

Joshua 16:10

Kabila la Efraimu halikuwafukuzia mbali watu gani?

Kabila la Efraimu halikuweza kuwafukuzia nje ya Gezeri Wakanaani.

Joshua 17

Joshua 17:1-2

Mzaliwa wa kwanza wa Yusufu ni nani?

Manase alikuwa ni mzaliwa wa kwanza wa Yusufu.

Makiri alikuwa ni nani?

Makiri alikuwa ni mzaliwa wa kwanza wa manase n a baba wa Gileadi.

Joshua 17:3-12

Kwanini binti Zelofehadi waliwaendea Eliazari, Yoshua na viongozi?

Binti za Zelofedadi walimwendea Eliazari, Yoshsua na viongozi kwasababu walikuwa hawana kaka ambao wangepokea urithi.

Yoshua aliwafanyia nini mabinti za Zelofehadi?

Yoshua aliwapa binti Zelofehadi urithi miongoni mwa ndugu za baba yao.

Joshua 17:13

Je Waisraeli baada ya kupata nguvu waliwafanyia nini Wakanaani?

Baada ya Israeli kupata nguvu, waliwafanya Wakanaani kuwa watumwa.

Joshua 17:14-18

Wazawa wa Yusufu walimwambia nini Yoshua?

Wazawa wa Yusufu walimwambia Yusufu kwamba nchi ya milima ilikuwa haitoshi kulingana na hesabu yao.

Yusufu aliwaambiaje wazawa wa Yusufu?

Yusufu aliwaambia wazawa wa Yusufu kupanda wao wenyewe katika msitu na kuifyeka nchi katika nchi ya Waperizi na ya Refaimu.

Joshua 18

Joshua 18:1-2

NI makabila mangapi ya watu wa Israeli yalikuwa hayajapewa urithi wakati mkutano wa watu walipokutana huko Shilo?

Wakati kusanyiko la watu wa Israeli walipokutana huko Shilo, makabila saba ya watu wa Israeli yalikuwa bado hayajapewa urithi.

Joshua 18:3-9

Yoshua alimtuma nani kwenda kuitembelea nchi juu na chini?

Yoshua aliwatuma watu watatu kutoka katika kila makabila saba ili kuitembelea nchi jjuu na chini.

Je watu watatu kutoka katika kila kabila walitakiwa kutoaje taarifa kwa Yoshua?

Watu watatu kutoka katika kila kabila walitakiwa kuandika maelezo kuhusu nchi, na maelekezo kuhusu urithi wao, na kisha watarudi kwa Yoshua.

Joshua 18:10

Yoshua alifanya nini baada ya watu kurudi kwake baada ya kuitembelea nchi?

Yoshua alipiga kura kwa ajili yao huko Shilo mbele za Yahweh baada ya watu kurudi kutoka katika kuitembelea nchi.

Joshua 18:11-28

Kabila la Benyamini lilipewa nchi katikati ya makabila gani mawili?

Kabila la Benyamini lilipewa urithi katika nchi katikati ya wazawa wa Yuda na wazawa wa Yusufu.

Joshua 19

Joshua 19:1-7

Upigaji wa kura wa mara ya pili uliangukia kwa kabila gani?

Upigaji wa kura ya pili uliangukiwa kwa Simoni.

Joshua 19:8-9

Urithi wa Simoni ulitoka katika himaya ya kabila gani?

Urithi wa Simoni ulitoka katika himaya ya kabila la Yuda.

Kwanini urithi wa Simoni ulitoka katika himaya ya Yuda?

urithi wa Simoni ulitoka katika himaya ya Yuda kwasababu himaya hiyo ilikuwa kubwa sana kwa Yuda.

Joshua 19:10-16

Upigaji wa kura wa mara ya tatu uliangukia kwa kabila gani?

Upigaji wa kura wa tatu uliangukia katika kabila la Zabuloni.

Joshua 19:17-23

Upigaji wa kura wa mara ya nne uliangukia kwa kabila gani?

Upigaji kura wa mara ya nne uliangukia kwa kabila la Isakari.

Joshua 19:24-31

Upigaji wa kura wa mara ya tano uliangukia kwa kabila gani?

Upigaji wa kura wa mara ya tano uliangukia kwa kabila la Asheri.

Joshua 19:32-37

Upigaji wa kura wa mara ya sita uliangukia kwa kabila gani?

Upigaji kura wa mara ya sita uliangukia katika kabila la Nafutali.

Joshua 19:38-39

Ni miji mingapi ilikuwa imejumuishwa katika urithi wa kabila la Nafutali?

Miji kumi na tisa ilikuwa imejumuishwa katika urithi wa kabila la Nafutali.

Joshua 19:40-48

Upigaji wa kura wa mara ya saba uliangukia kwa kabila gani?

Upigaji wa kura wa mara ya saba uliangukia kwa kabila la Dani.

Joshua 19:49-51

Watu wa Israeli walimpa Yoshua urithi gani baada ya kuwa wamemaliza kuigawa nchi?

Kwa agizo la Yahweh, watu wa Israeli walimpa Yoshua mji wa Timna Sera aliokuwa ameuomba.

Joshua 20

Joshua 20:1-3

Yahweh alimwambia Yoshua awaambie nini watu?

Yahweh alimwambia Yoshua awaambie watu hivi wanatakia kuteua miji ya makimbilio.

Joshua 20:4

Mtu aliyeua alitakiwa kueleza wapi na kwa nani juu ya kesi yake?

Mtu aliyeua mtu mwingine alitakiwa kusimama katika lango la mji na kueleza kesi yake kwa wazee wa huo mji.

Joshua 20:5-8

Baada ya mtu kukimbilia katika mji wa makimbilio na kusimama mbele ya kusanyiko kwa ajili ya hukumu, je ni kitu gani kingine kilichohitajika ili mtu huyu aruhusiwe kurudi nyumbani kwake?

Mtu huyo angeweza kuruhusiwa kuuacha mji wa makimbilio na kurudi nyumbani baada ya kifo cha kuhani mkuu.

Joshua 20:9

Je mtu anayetuhumiwa, alitakiwa afanye nini katika mji wa makimbilio ili kuepuka asije akauliwa na mtu anayetaka kulipiza kisasi cha damu iliyomwagika?

Mtu anayetuhumia alitakiwa kwanza kusimama mbele ya kusanyiko.

Joshua 21

Joshua 21:1-7

Ni akina nani waliowaomba watu wa Israeli ili wawape miji ya kuishi na maeneo ya malisho kwa ajili ya mifug yao?

Koo za Walawi waliwaomba watu wa Israeli wawape miji ya kuishi na maeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo yao.

Joshua 21:8-16

Ni kwa namna gani watu wa Israeli waliweza kuamua juu ya miji na maeneo ya malisho kwa ajili ya kuwapa Walawi?

Watu waisraeli waliweza kuamua juu kuwapa miji na maeneo ya malisho Walawi kwa kupliga kura, kama vile Yahweh alivyokuwa ameamuru.

Joshua 21:17-24

Wana wa Haruni walipewa miji mingapi?

Wana wa Haruni walipewa miji kumi na mitatu kwa jumla.

Joshua 21:25-31

Familia ya Kohathi ilipewa miji mingapi?

Familia ya Kohathi ilipewa miji kumi kwa ujumla.

Joshua 21:32-38

Koo za Gershoni zilipewa miji mingapi?

Koo za Gershoni zilipewa miji ya koo za Merari (miji kumi na tatu kwa ujumla)

Joshua 21:39-40

Koo za Merari zilipata miji mingapi?

Koo za Merari zilipata miji kumi na miwili kwa ujumla.

Joshua 21:41-42

Walawi wote walipewa miji mingapi kutoka katika sehemu ya katikati ya nchi iliyoimilikiwa na Israeli?

Walawi walipewa miji arobaini na nane pamoja na maeneo yake ya malisho kutoka katika sehemu ya kati ya nchi.

Joshua 21:43-45

Yahweh alikuwa amewaapia nini baba za Waisraeli?

Yahweh alikuwa amewaapia kuwapa nchi waliyoimiliki, na pumziko katika kila upande.

Joshua 22

Joshua 22:1-3

Ni sifa gani ambazo Yoshua aliwapa Warubeni, Wagadi na nusu kabila la Manase?

Yoshua aliwasifu kwa kusema kwamba wamefanya kila kitu ambacho Musa na Yoshua walikuwa wamewaamuru na ya kwamba hawajawaach ndugu zao bali wamemtii Yahweh Mungu wao kwa uangalifu.

Joshua 22:4-6

Yoshua aliyaambia nini makabila haya juu ya kuwa waangalifu wakati watakaporudi katika hema zao?

Yoshua aliyaambia haya makabila kuwa makini katika kuzishika amri na sheria ambazo Musa aliwaamuru.

Joshua 22:7-9

Yoshua aliwaambia nini nusu ya kabila la Manase juu ya kugawana miongoni mwa ndugu?

Yoshua aliliambia nusu kabila la Manase kugawana nyara miongoni mwa ndugu zao.

Joshua 22:10-11

je Warubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walifanya jambo gani ng'ambo ya Yordani lililowakasirisha watu wa Israeli katika nchi ya Kanaani?

Warubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walijenga madhabahu kubwa katika upande wa Yordani iliyokuwa miliki ya watu wa Israeli.

Joshua 22:12

Watu wa Israeli walifanya nini baada ya kusikia juu ya madhabahu?

Watu wa Israeli walikusanyika kwa pamoja huko Shilo ili wapande na kufanya vita dhidi ya makabila yale baada ya kusikia juu ya madhabahu.

Joshua 22:13-14

Ni wajumbe gani ambao Waisraeli waliwatuma kwa watu wa Rubeni, Gadi na nusu kabila la Manase?

Watu wa Israeli waliwatuma Finehasi, mwana wa Eliezari kuhani, na viongozi kumi kama wajumbe kwa Warubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase.

Joshua 22:15-16

Je wajumbe wa watu wa Israeli walisema nini kwa watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase?

Wajumbe wa watu wa israeli waliwaambia watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase hivi "Ni jambo gani hiili lisilo la uaminifu ambalo mmelitenda kinyume na Mungu wa israeli kwa kujijengea wenyewe madhabahu...?

Joshua 22:17-25

Watu wa Israeli walikuwa na wasiwasi na jambo gani kama watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wangeasi kinyume na Yahweh?

Watu wa israeli walikuwa na wasiwasi juu ya watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase kuwa wangeasi kinyume na Yahweh, na kisha Yahweh angekuwa na hasira na kusanyiko lote la Israeli.

Joshua 22:26-29

Je watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase waliwaambia nini wajumbe wa watu wa Israeli?

watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase waliwaambia wajumbe wa watu wa Israeli kuwa wamejenga madhabahu, si kwa sadaka za kuteketezwa wala dhabihu, bali kama ushahidi katik yao ya watu wa Israeli na ya kwamba watafanya huduma kwa Yahweh na kwa ajili ya kizazi kijacho kuona.

Joshua 22:30-31

Finehasi kuhani na wajumbe wengi waliwaambia nini juu ya maneno waliyokuwa wameyasikia kutoka kwa Warubeni, Wagadi na Manase?

Finehasi kuhani na wajumbe wengi waliwaambia kwamba maneno yaliyosemwa na Warubeni, Wagadi na Manase yalikuwa ni mazuri machoni pao.

Joshua 22:32-33

Je watu wa Israeli walifanya nini baada ya Finehasi na wajumbe kutoa taarifa kwao?

Watu wa Israeli walimbariki Mungu na hawakusema chochote zaidi kuhusu kufanya vita.

Joshua 22:34

Je Warubeni na Wagadi waliiitaje madhabahu ile?

Warubeni na Wagadi waliiita madhabahu 'ushahidi"

Joshua 23

Joshua 23:1-5

Yoshua alifanya nini baada ya Yahweh kuwapa pumziko Waisraeli kutoka katika maadui zao wote?

Baada ya Yahweh kuipa Israeli pumziko kutoka kwa maadui zao wote, Yoshua aliwaita Waisraeli wote.

Ni nani ambaye Yoshua alimsema kuwa aliwapigania?

Yoshua alisema kuwa Yahweh alikuwa akiwapigania.

Joshua 23:6-11

Yoshua aliwaambia watu wasitaje nini?

Yoshua aliwaambia watu kwamba hawapaswi kutaja majina ya miungu ya mataifa yaliyosalia miongoni mwao.

Joshua 23:12-13

Yoshua alisema Yahweh angefanya nini kama wangeoana na masalia ya mataifa waliobakia miongoni mwao?

Yoshua aliwaambia watu kwamba Yahweh angewafanya waangamie kutoka katika nchi nzuri waliyokuwa wamepewa kama wangeoana na masalia ya mataifa yaliyosalia miongoni mwao.

Joshua 23:14-15

Ni kitu ganiYoshua alisema ambacho kilikuwa kinaenda kutokea kwake?

Yoshua alisema kwamba alikuwa anaenda katika njia ya dunia yote.

Joshua 23:16

Yoshua alisema kuwa ni kitu gani ambacho kingemfanya Yahweh kuwaletea watu wa Israeli mabaya yote?

Yoshua alisema kuwa Yahweh angeleta mambo yotef mabaya juu ya watu wa Israeli kama watalivunja agano la Yahweh.

Joshua 24

Joshua 24:1-12

Yoshua alikuwa anaongea na nani na ni sehemu gani aliyokuwa akiongea nao?

Yoshua aliyakusanya makabila yote ya Israeli huko Shekemu na kuongea na wazee wa Israeli, viongozi wao, waamuzi wao, na maafisa wao.

Joshua 24:13

Ni kitu gani ambacho Yahweh alisema kuwa amewapa watu wa Israelil?

Yahweh alisema kuwa alikuwa amewapa watu wa Israeli nchi ambayo walikuwa hawajaifanyia kazi, miji ambayo hawakuijenga, mizabibu na mashamba ya mizeituni ambayo hawakuyapanda.

Joshua 24:14-15

Yoshua alisema nini juu yake na nyumba yake?

Yoshua alisema kuwa yey na nyumba yake wangemwabudu Yahweh.

Joshua 24:16-18

Watu wa Israeli walimjibuje Yoshua?

Watu wa Israeli walimjibu Yoshua kwa kumwambia kwamba wangemwabudu Yahweh.

Joshua 24:19-20

Yoshua aliwajibu vipi watu wa israeli?

Yoshua aliwaambia watu wa Israeli kwamba wangeweza kumwabudu Yahweh kwasababy ya makosa na dhambi zao.

Joshua 24:21-23

Watu wa Israeli walimwambia nini Yoshua kwa mara ya mwisho?

Watu wa Israeli kwa mara ya mwisho walimwambia Yoshua kuwa "Hapana, tutumwabudu Yahweh"

Joshua 24:24-26

Yoshua alifanya nini kutia alama ya agano walilolifanya pamoja na watu siku ile?

Yoshua aliyaandika maneno haya katika kitabu cha sheria za Mungu na kuweka jiwe kubwa chini ya mti wa mwaloni pembeni ya mahali patakatifu pa Yahweh.

Joshua 24:27-31

Yoshua alisema jiwe lingekuwa ushahidi kwa nani?

Yoshua alisema kuwa jiwe lingekuwa ushahidi dhidi ya Waisraeli kwasababu lilikuwa limeyasikia maneno yote yaliyosemwa na Yahweh na watu wa Israeli.

Joshua 24:32-33

Ni mifupa ya nani ambayo watu wa Israeli walikuwa wameileta kutoka Misri?

Watu wa Israeli walikuwa wameileta kutoka Misri mifupa ya Yusufu.