Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

1 John

1 John 1

1 John 1:1-2

Je! Yohana anasema ni nini kilichokuwa tangu mwanzo?

Yohana anasema Neno la uzima lilikuwako tangu mwanzo

Ni jinsi gani Yohana aliweza kujua kuhusu Neno la uzima?

Ni kwa sababu lile Neno lilifunuliwa

Neno la uzima lilikuwa wapi kabla halijafunuliwa kwa Yohana?

Neno la Uzima lilikuwa pamoja na Baba kabla halijafunuliwa kwa Yohan

1 John 1:3-4

Kwa nini Yohana anatangaza alilolisikia na kuliona?

Yohana anatangaza alilolina na kulisikia Ili kwamba wawe na ushirika pamoja naye.

Ni pamoja na nani ambaye tayari Yohana ameshakuwa na ushirika naye?

Tayari Yohana ameshakuwa na ushirika pamoja na Baba na Mwanawe, Yesu Kristo .

1 John 1:5-7

Ni ujumbe gani kutoka kwa Mungu ambao Yohana anautanagaza kwa wasomaji wake?

Yohana anatangaza ujumbe kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hakuna giza hata kidogo

Yohana ansema nini kuhusu mtu anayesema ana ushirika na Mungu, anatmbelea gizani?

Yohana anasema kwamba mtu kama huyo ni mwongo na haenendi katika kweli.

Kwa wale wanaotembea nuruni, ni kitu gani huwatakasa kutoka dhambi zote?

Ni damu ya Yesu huwatakaza kutoka dhambi yote.

1 John 1:8-10

Yohana anasema nini kwa mtu asemaye kwamba hawana dhambi?

Tukisema kwamba hatuna dhambi twamfanya yeye kuwa mdanganyifu, na neno lake halimo ndani yetu.

1 John 2

1 John 2:1-3

Kristo ni dhabihu kwa dhambi za nani?

Yesu Kristo ni dhabihu kwa dhambi kwa ajili ya ulimwengu mzima.

Tunajuaje kama tunamjua Yesu Kristo?

Tunajua kama tunamjua Yesu Kristo kama tukizishika sheria zake

1 John 2:4-8

Ni aina gani ya mtu yule anayesema wanamjua Mungu, lakini hazishiki amri za Mungu?

Yule anayesema wanamjua Mungu, lakini hazishiki amri za Mungu, ni mwongo

aaminiye yampasa kuenenda namna gani?

Aaminiye yampasa kuenenda kama vile Yesu Kristo alivyoenenda.

1 John 2:9-11

Hali ya kiroho ya mtu asemaye yuko kwenye nuru, lakini anamchukia nduguye?

Mtu asemaye yuko nuruni, lakini anamchukia ndugu yake, yumo gizani.

Hali ya kiroho ya mtu asemaye yuko kwenye nuru, lakini anamchukia nduguye?

Mtu asemaye yuko nuruni, lakini anamchukia ndugu yake, yumo gizani.

1 John 2:12-14

Kwa nini Mungu husamehe dhambi za waaminio?

Mungu husamehe dhambi za waaminio kwa ajili ya Jina la Kristo

1 John 2:15-17

Yohana anasema tabia ya aaminiye ni lazima iweje upande wa vitu vya duniani?

Yohana anasema haimpasi mwamini kuipenda duni wala mambo ya dunia.

Ni mamb gani matatu yaliyomo dunani ambayo Yohana anataja kuwa hayatokani na Baba?

Anataja tamaa za mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima kuwa yamo ulimwenguni na siyo ya Baba.

1 John 2:18-21

Yohana anasemaje kuwa anajua kwamba ni saa ya mwisho?

Anasema anajua kuwa ni saa ya mwisho kwa sababu wapinga Kristo wamishakuja.

Ni nani ambaye Yohana anaseama kwamba anakuna?

Anasema kwamba mpinga risto anakukuja

1 John 2:22-23

Mpanga Kristo atafanya nini ambao litatuwezesha kumtambua?

Mpinga Kristo anamkataa Baba na Mwana

Je? mtu yeyote nayemkana Mwana ana Baba?

Hapana, anayemkana Mwana wawezi kuwa Baba

1 John 2:24-26

Yohana anawaambi waaminio wafanye nini ili kubaki ndani ya Mwana na Baba?

Yahana anawaambia waaminio kukaa ndani ya lile walilolisikia tangu mwanzo.

Ni ahadi gani ambayo imeahidiwa na Mungu kwa waaminio?

Mungu amewaahidi waaminio uzima wa milele.

1 John 2:27-29

Ni misimamo gani watakuwa nayo wale wanaodumu ndani ya Mwana Kristo atakapotkea siku ya majilio yake?

Wale wanaodumu ndani ya Mwana watakua na ujasiri na hawaaibika Kristo atakapotoke siku ya majilio yake.

1 John 3

1 John 3:1-3

Ni kitu gani Baba amewapa waumini kwa sababu ya pendo lake?

Baba amewapa waumini jina watoto wa Mungu.

Jambo gani litatokea kwa waaminio Kristo atakapotokea?

Kristo atakoonekana, waaminio watakuwa kama Kristo, na watamwona kama alivyo.

Kila aaminiye anayematuaini Kristo anatakiwa kufanya nini kuhusiana na yeye mwenyewe?

Kila mwamini anayetumaini katika Kristo hujitakasa mwenyewe.

1 John 3:4-6

Kristo hana nini ndani yake

Kristo hana dhambi ndani yake.

Yule anayeendelea kutenda dhambi anauhusiano gani kwa Mungu?

Yeyote anayeendelea katika dhambi hata hajamwona Kristo, wala kumfahamu.

1 John 3:7-8

Ni kwasababu gani Mwana wa Mungu alidhihirishwa?

Mwana wa Mungu alidhihirishwa kuziharibu kazi za ibilisi.

1 John 3:9-10

Ni kwa namna gani watoto wa Mungu na watoa wa ibilisi kila mmoja hufunuliwa?

Watoto wa Mungu hufunuliwa kulingana na wanavyotenda haki, na watoto wa ibilisi hufunuliwa kulingana na wanavyotenda dhambi

1 John 3:11-12

Kaini alionyeshaje kwamba alikuwa mtoto wa yule mwovu?

Kaini alionyesha kwamba alikuwa mtoto wa yule mwovu alipomuua ndugu yake.

1 John 3:13-15

Ni katika jambo gani Yohana anasema waumini wasije kushangaa?

Yohana anasema waumini wasishangae endapo kwamba ulimwengu unawachukia.

Ni tabia gani mbele ya waaminio ambayo huonyesha kuwa mtu fulani ni mtoto wa Mungu?

Tabia ya upendo mbele ya waaminio huonyesha kuwa mtu fulani ni mtoto wa Mungu

1 John 3:16-18

Jinsi gani tunaweza kuujua upendo ulivyo?

Twajua upendo nini kwa sababu Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu.

Kama kuna ndugu mwenye mahitaji, aminiye ataulionyeshaje pendo la Mungu?

Ikiwa kuna ndugu yuko kwenye uhitaj, mwamini hulionyesha pendo la Mungu kwa kumsaidia kwa mali ya duniani.

1 John 3:19-22

Mwamini anapolionyesha pendo la Mungu katika matendo na kweli, huwa anapokea nini kwa ajili yake mwenyewe?

Muumini anapolionyesha pendo la Mungu katika matendo na kweli, hupata uhakika na ujasiri mbele za Mungu kwa ajili yake mwenyewe.

1 John 3:23-24

Je, Ni amri ipi ya Mungu amboyo Yohana anawakumbusha waaminio?

Yohana anawakumbusha waaminio amri ya Mungu ya kuamini katika jina la Mwanawe Yesu Kristo na kupendana wao kwa wao.

Mungu amewapa nini waaminio ili kujua kwamba Mungu anakaa ndania yao?

Mungu amewapa waamini Roho wake ili wajue kwamba Mungu anakaa ndani yao.

1 John 4

1 John 4:1-3

Kwa nini Yohana aliwaonya waamini kutoamini kila roho?

Yohana aliwonya waamini kwa sababu kuna manabii wengi wa uongo ambao wametokea duniani.

Unawezaje kujua kama Roho wa Mungu anazungumza?

Kila roho inakayokiri kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili ni ya Mungu,

Ni roho gani isiyokrisi kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili?

roho ya mpinga Kristo hakiri kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili.

1 John 4:4-6

Ni nani anayesemwa na Yohana kuwa ni Roho Mkuu

Roho Mkuu ni yule aliye ndani ya waaminio, mkuu kuliko roho zingine za duniani.

1 John 4:7-8

Waaminio wanafanya nini kinachoonyesha wanamjua Mungu na kuwa kama yeye alivyo?

Waaminio kupendana wao kwa wao, ndiko kunakoonyesha wanamjua Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo.

1 John 4:9-14

Ni kwa jinsi gani Mungu amefunua pendo lake kwetu?

Mungu amefunua pendo lake kwetu kwa kumtuma mwanawe wa pekee duniani.

Ni kwa kusudi gani Baba alimutma Mwanawe?

Baba alimtuma Mwanawe ulimwenguni ili tuishi kupitia yeye.

1 John 4:15-16

Ni kipi ambacho mwamini wa kweli hukiri kuhusu Yesu?

Mwamini wa kweli hukiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu

1 John 4:17-18

Wanaokaa ndani ya pendo na ndani ya Mungu watakauwa na msimamo gani siku ya hukumu?

Wanaokaa ndani ya pendo na ndani ya Mungu watakuwa na ujasiri katika siku ya hukumu.

1 John 4:19-21

Ni kwa jinsi gani tunaweza kupenda?

Tunapenda kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.

Anauhusiano gani na Mungu mtu anayemchukia ndugu yake?

Mtu anayemchukia ndugu yake hawezi kumpenda Mungu.

Wale wanaompenda Mungu ni lazima wampende nani pia?

Wanaompenda Mungu ni lazima wawapende ndugu zao pia.

1 John 5

1 John 5:1-3

Tunaonyeshaje kwamba tunampenda Mungu?

Tunaonyesha kwamba tunampenda Mungu tunapozishika amri zake.

1 John 5:4-5

Ni ushindi gani ambao umeushinda ulimwengu?

Ushindi ambao umeushinda ulimwengu ni imani yetu.

1 John 5:6-8

Kristo alikuja kwa mambo gani mawili?

Yesu Kristo alikuja kwa maji na kwa damu

Ni mambo gani matatu yanayomshudia Jesu Kristo?

Roho, maji, na damu yote humshuhudia Yesu Kristo.

1 John 5:9-10

Je mtu yeyote ambaye haamini ushuhuda wa Mungu juu ya Mwanawe, kufanyia nini Mungu?

Mtu yeyote ambaye haamini ushuhuda wa Mungu juu ya Mwanawe humfanya Mungu kuwa mwongo.

1 John 5:11-12

Mungu ametupa nini sisi katika mwana wake?

Mungu ametupa uzima wa milele katika mwana wake.

1 John 5:13-15

Waaaminio wanaujasiri gani mbele za Mungu?

Waaminio wana ujasiri mbele za Mungu kwamba kama wakiomba kitu chochote sawa sawa na mapenzi yake, huwasikia.

1 John 5:16-17

Mwamini anapomwaona ndugu yake natenda dhambi iisiyopelekea mauti ni lazima afanye nini?

Mwamini anamwona ndugu yake anatenda dhambi isiyopelekea kifo ni lazima kuomba kwamba Mungu atampa uzima ndugu yake.

Uasi wote ni nini?

Uasi wote ni dhambi

1 John 5:18-19

Ulimwengu wote uko wapi

Ulimwengu wote uko chini ya utawala wa yule mwovu.

1 John 5:20-21

Mungu wa kweli ni nani?

Mungu wa kweli ni Baba wa Yesu Kristo.

Ni lazima waaminio wajiepushe na nini?

Ni lazima waaminio wajiepushe na sanamu.