Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Zechariah

Zechariah 1

Zechariah 1:1-3

Zekaria alitabiri wakati wa utawala wa nani?

Zekaria alitabiri wakati wa utawala wa Dario.

Zekaria alikuwa nani?

Zekaria alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Ido nabii.

Yahwe wa majeshi alisema angefanya nini ikiwa watu wangemrudia?

Yahwe wa majeshi alisema ikiwa wangemrudia, naye angewarudia.

Zechariah 1:4-6

Baba zao walifanya nini Yahwe alipowaambia kugeuka kutoka katika njia zao mbaya na matendo maovu?

Baba zao hawakusikia na hawakumjari Yahwe.

Watu walisema nini walipotubu?

Walipotubu walisema, "Mipango ya Yahwe wa majeshi imefanywa kwa kulitunza neno na matendo yake, na ameyatimiza."

Zechariah 1:7-9

Zakaria aliona nini neno la Yahwe lilipomjia usiku?

Zakaria aliona mtu amepanda farasi mwekundu kati ya miti ya mihadasi bondeni. Na nyuma yake kulikuwa na farasi mwekundu, farasi wa kijivu, na farasi mweupe

Zechariah 1:10-11

Farasi aliowaona Zakaria walikuwa ni nini?

Hawa ndiyo Yahwe aliowatuma kuzunguka katika dunia yote

Farasi waliozunguka dunia yote waliona nini?

Farasi hao waliona dunia yote imekaa na kutulia

Zechariah 1:12-15

Malaika wa Yahwe alimuuliza Yahwe swali gani kuhusu Yerusalemu na miji ya Yuda?

Malaika wa Yahwe akamuuliza Yahwe wa majeshi hata lini usiuhurumie Yerusalemu na miji ya Yuda.

Zechariah 1:16-17

Yahwe wa majeshi alisema nini kuhusu Yerusalemu na miji ya Yuda?

Yahwe wa majeshi alisema alikuwa ameimeirudia Yerusalema kwa huruma. Hivyo nyumba yake itajengwa ndani yake na kipimo kingenyoshwa juu ya Yerusalemu. Pia 'Yahwe wa majeshi alisema miji yangu kwa mara nyingine itajawa na uzuri, na Yahwe ataifariji tena Sayuni, na kuichagua Yerusalemu kwa mara nyingine tena.

Zechariah 1:18-19

Pembe nne alizoziona Zakaria zilikuwa nini?

Pembe nne walikuwa waliosababisha kutawanyika kwa Yuda, Israeli, na Yerusalemu.

Zechariah 1:20-21

Mafundi stati wanne aliowaona Zakaria walikuwa akina nani na walikuwa wakienda kufanya nini?

Mafundi stadi walikuwa watu waliokuwa wanakuja kuondoa pembe na kutupa chini pembe za mataifa yaliyoinua nguvu zao kinyume cha nchi ya Yuda na kuisambaza.

Zechariah 2

Zechariah 2:1-2

Kijana alikuwa anakwenda kupima nini na kamba ya kupimia mkononi?

Alikuwa akienda kuipima Yerusalemu, ili kutambua upana na urefu wake.

Zechariah 2:3-5

Kwa nini malaika wa pili alisema kwamba Yerusalemu ingekuwa katika nchi wazi?

Alisema hivyo kwa sababu ya wingi wa watu na wanyama ambao wangekuwa ndani yake.

Yahwe alisema angekuwa nini kwa Yerusalemu?

Yahwe alisema angekuwa ukuta wa moto kuuzunguka na angekuwa utukufu katikati yake.

Zechariah 2:6-7

Tamko la Yahwe lilikuaje kwa waliokaa na binti Babeli?

Yahwe aliwaambia wakimbilie Sayuni.

Zechariah 2:8-9

Walipaswaje kujua kwamba Yahwe wa majeshi ametuma malaika wa pili?

Malaika wa pili alisema Yuda na Israeli wangejua Yahwe amemtuma alipotikisa mkono wake juu ya mataifa yaliyowateka na mataifa yaliyoiteka Yuda na Israeli yalipokuwa yametekwa na watumwa wao.

Zechariah 2:10-11

Kitatokea nini Yahwe atakapokuja na kupiga hema katika Sayuni

Hilo litakapotokea mataifa makubwa yataungana yenyewe kwa Yahwe na yale ya Sayuni yatakuwa watu wake.

Zechariah 2:12-13

Kwa nini wenye mwili wote wanaambiwa wawe kimya mbele za Yahwe?

Wenye mwili wote wanaambiwa wawe kimya mbele ya Yahwe kwa sababu Yahwe ameinuka kutoka katika mbingu.

Zechariah 3

Zechariah 3:1-3

Ni nani aliyekuwa karibu na Yoshua kuhani mkuu?

Yoshua alikuwa amesimama mbele ya Yahwe na Shetani alikuwa amesimama mkono wake wa kulia.

Shetani alikuwa anafanya nini katika mkono wa kulia wa Yoshua?

Shetani alikuwa anamshitaki Yoshua kwa ajili ya dhambi.

Alipokuwa amesimama mbele ya malaika Yoshua alikuwa amevaa nini?

Yoshua alikuwa amevaa mavazi machafu.

Zechariah 3:4-5

Malaika wa Yahwe alisema alikua amefanya nini kwa Yoshua?

Malaika wa Yahwe alisema alikuwa amefanya uchafu wa Yoshua kupita kutoka kwa Yoshua.

Ni nini kilichotokea kuhusiana na vazi la Yoshua?

Malaika aliagiza mavazi machafu kuondolewa kutoka kwa Yoshua na Yoshua kuvikwa mavazi safi; kilemba safi na mavazi safi.

Zechariah 3:6-7

Yahwe alikuwa amemwahidi nini Yoshua, kuhani mkuu, ikiwa angekwenda katika njia za Yahwe na kushika maagizo yake?

Yahwe alimwahidi Yoshua kwamba angesimamia nyumba ya Yahwe na kutunza nyua zake. Yahwe alimwahidi pia kwamba angemruhusu kuja na kwenda mbele ya wale wasimamao mbele ya Yahwe.

Zechariah 3:8-9

Mtumishi aliita kwamba Yahwe alikuwa anakwenda kufanya nini yeye mwenyewe kuleta?

Mtumishi alikuwa anaitwa "Tawi."

Sehemu ya kwanza ya ujumbe kuandikwa katika sehemu saba za jiwe ulikuwa nini?

Sehemu ya kwanza ya ujumbe ulikuwa kwamba Yahwe angeondoa dhambi kutoka katika nchi hiyo kwa siku moja.

Zechariah 3:10

Kwa mjibu wa Yahwe ingekuwa lini wakati kila mtu angemkaribisha jirani yake kupumzika chini ya mzabibu na mtini wake.

Yahwe alisema hii ingefanyika "siku moja."

Zechariah 4

Zechariah 4:1-3

Zakaria alipoamshwa aliona nini?

Zakaria aliona kinara cha taa ya dhahabu na bakuri juu yake, likiwa na taa saba na miti miwili ya mizabibu kando ya bakuri.

Zechariah 4:4-5

Je! Yoshua alielewa mambo hayo katika ono yalimaanisha nini?

Hapana, Zakari alimwambia malaika aliyekuwa aliyesema naye kwamba hakufahamu maana ya mambo hayo katika ono.

Zechariah 4:6-7

Taa saba zilimaanisha nini?

Taa saba ni macho ya Yahwe yanayozunguka juu ya nchi yote.

Zechariah 4:8-11

Matawi mawili ya mzabibu ni nini?

Matawi mawili ya mzabibu ni wana wawili wa mafuta wasimamao mbele ya Bwana wa dunia yote.

Zechariah 4:12-14

Neno la Yahwe kwa Zerubabeli kuhusu mambo yalivyokuwa yanakwenda kuwa lilikuwa nini?

Neno la Yahwe kwa Zerubabeli lilikuwa, "Siyo kwa nguvu wala kwa uwezo, lakini ni kwa Roho wake pekee."

Ni nini kitakachosikika Zerubabeli atakaposhusha jiwe la juu?

"Neema! Neema! kwake," itasikika wakati huo.

Zechariah 5

Zechariah 5:1-2

Kitabu alichokiona Zakaria kilikuwa na ukubwa gani?

Kilikuwa na urefu wa dhiraha ishirini na upana wa dhiraha kumi.

Zechariah 5:3-4

Malaika alisema gombo lirukalo lilikuwa ni nini?

Malaika alisema gombo lililokuwa linaruka lilikuwa laana iendayo juu ya uso wa dunia yote.

Gombo lilimlaani nani?

Gombo lilikuwa laana kwa kila mfalme na kwa kila aapaye nadhiri ya uongo.

Laana ilifanya nini kwa mfalme na kwa yeye aapaye kwa uongo kwa jina la Yahwe?

Laana itaingia katika nyumba na kubaki pale na kula kila mti na mawe ya nyumba zao.

Zechariah 5:5-7

Zakaria aliona nini kilichokuwa ndani ya kikapu na malaika alisema kilikuwa nini?

Kwenye kikapu kulikuwa na efa, na malaika alisema efa hiyo ilikuwa ni uchafu katika nchi yote."

Zechariah 5:8-9

Malaika alisema mwanamke aliyekuwa ndani ya kikapu alikuwa nani?

Malaika alisema mwanamke katika kikapu, "Huu ni uovu!"

Wanawake wawili waliokuwa na mbawa kama mbawa za korongo walifanya nini na kikapu?

Wanawake wawili waliinua kikapu kati ya mbingu na nchi.

Zechariah 5:10-11

Wanawake walikuwa wakikipeleka wapi kikapu na kwa kusudi gani?

Wanawake walichukua kikapu katika kujenga hekalu huko Shinari kwa ajili yake, ili kwamba hekalu litakapokuwa tayari, kikapu kiwekwe pale katika katika msingi kilioandaliwa.

Zechariah 6

Zechariah 6:1-4

Zakaria aliona nini kikija kutoka katika milima miwili ya shaba?

Zakaria aliona vibandawazi vinne vikitoka kati ya milima miwili ya shaba.

Farasi wa vibandawazi walikuwa na rangi gani?

Kibandawazi cha kwanza kilikuwa na farasi wakundu, cha pili farasi weusi, cha tatu farasi weupe, na cha nne kilikuwa na farasi wa kijivu.

Zechariah 6:5-6

Malaika alisema vibandawazi vilikuwa nini?

Malaika alisema vibandawazi walikuwa pepo nne za mbingu.

Vibandawazi hivi vinne vilikuwa wapi?

Vilikuwa vimesimama mbele ya Bwana wa dunia yote.

Vibandawazi vitatu na farasi wausi, weupe na wa kijivu walikuwa wapi na walikuwa wakienda wapi?

Kibandawazi pamoja na farasi weusi walikwenda nchi ya kaskazini. Kibandawazi na farasi weupe walikwenda nchi ya magharibi. Kibandawazi na farasi wa kijivu walikwenda nchi ya kusini.

Zechariah 6:7-8

Kibandawazi na farasi weusi walikuwa wanakwenda kukamilisha nini katika nchi ya kaskazini.

Kibanda wazi na farasi weusi wlikuwa wanakwenda kuituliza roho ya malaika juu nchi hiyo

Zechariah 6:9-11

Zakaria alipaswa kufanya nini na sadaka iliyokuwa imekusanywa kutoka kwa Heldai, Tobiya, na Yedaya?

Zakaria aliambiwa kupeleka matoleo katika nyumba ya Yosia, mwana wa Zefania. Zakaria aliambiwa kuchukua fedha na dhahabu, kufanya taji na kuiweka juu ya kichwa cha Yoshua mwna wa Yehosadaki, kuhani mkuu.

Zechariah 6:12-13

Yahwe alisema Yoshua mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu angefanya nini?

Yahwe alisema Yoshua angekua pale alipo na kujenga hekalu kwa Yahwe, kuinua utukufu wake, na kisha kukaa na kutawala katika kiti cha enzi.

Zechariah 6:14-15

Kwa nini taji ilikuwa iwekwe katika hekalu la Yahwe?

Taji ilikuwa iwekwe katika hekalu la Yahwe kwa Heldai, Tobiya, and Yedaya na kama kumbukumbu kwa ukarimu wa mwana wa Zefania.

Watu wafanye nini kwa ajili ya matukio ya kinabii kutimia?

Yahwe alisema matukio haya yangetukia "iwapo wangesikiliza kweli kwa sauti ya Yahwe Mungu wao"

Zechariah 7

Zechariah 7:1-3

Kwa nini watu wa Betheli walimtuma Shareza, Regemu Meleki, na watu wao?

Watu wa Betheli waliwatuma kuomba upendeleo wa Yahwe.

Shareza, Regemu Meleki na watu wao waliwaomba nini kuhani na manabii.

Waliuliza, "Je! niomboleze katika mwezi wa tano kwa kufunga, kama ambavyonimekuwa nikifanya siku hizi zote?

Zechariah 7:4-7

Ni maswali gani mawili Yahwe aliwauliza watu wa nchi na makuhani kupitia Zakaria kuhusu kufunga, kula na kunywa?

Swali la kwanza Yahwe alilouliza lilikuwa, "Mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka hii sabini, je mlikuwa mnafunga kwa ajili yangu?" Swali la pili lilikuwa, "Na mlipokula na kunywa, je! hamkula na kunywa kwa ajili yenu wenyewe?

Kwa ufupi, swali la mwisho Yahwe alilowauliza makuhani na watu wa nchi lilikuwa nini?

Kwa ufupi, Yahwe aliwauliza ikiwa haya hayakuwa maneno yaleyale Yahwe aliyokuwa amewambia bado wanaishi Yerusalemu, miji ya karibu, Negebu, na vilima vya magharibi.

Zechariah 7:8-10

Yahwe kupitia Zakaria aliwambia watu wafanye nini?

Yahwe aliwaambia wahukumu kwa kweli na haki, uaminifu wa agano na rehema. Aliwaambia wasiwatese mjane, yatima na mgeni au masikini na wasitendeane ubaya.

Zechariah 7:11-12

Hitiko la watu kwa maelekezo ya Yahwe lilikuwa nini?

Watu walikataa kujari maneno ya Yahwe.

Zechariah 7:13-14

Yahwe alisema angefanya nini kama waliokataa mwanzo kumsikiliza Yahwe wangemwita?

Yahwe alisema asingesikiliza na zaidi, angewatawanya kwa upepo wa kusulisuli kwa mataifa yote wasiyoyaona bado.

Zechariah 8

Zechariah 8:1-3

Jinsi gani Yahwe anavyoonesha huruma yake kwa Sayuni?

Yahwe anaoonesha huruma yake kwa Sayuni kwa wivu na hasira kuu.

Yerusalemu na mlima wa Yahwe utaitwaje Yahwe atakaporudi kuishi katikati ya Yerusalemu?

Yerusalemu utaitwa "Mji wa Kweli" na mlima wa Yahwe utaitwa "Mlima Mtakatifu" Yahwe anapokuja kuishi katikati ya Yerusalemu.

Zechariah 8:4-5

Akina nani watakaoonekana tena kati mitaa ya Yerusalemu?

Wanaume na wanawake wazee watakuwa katika mitaa, na mitaa itajazwa pia na vijana wa kiume na kike wakicheza.

Zechariah 8:6-8

Yahwe alikuwa anakwenda kuokoa watu wake kutoka wapi?

Yahwe alikuwa anakwenda kuokoa watu wake kutoka nchi ya kuchomoza na kuzama kwa jua.

Zechariah 8:9-10

Kwa nini Yahwe alitaka watu watie nguvu mikono yao?

Yahwe alitaka watu wake watie mikono yao nguvu ili kwamba hekalu liweze kujengwa.

Kilitendeka nini kabla msingi wa nyumba ya Yahwe haujawekwa.

Katika siku hizo, hakuna mazao yaliyokuwa yamekusanywa, hakukuwa na faida, na hakukuwa na amani kutoka kwa adui. Yahwe alimweka kila mtu kinyume cha jirani yake.

Zechariah 8:11-15

Yahwe alisema itakuwaje katika nyakati za Zakaria?

Yahwe alisema haitakuwa kama siku za mwanzo. Alisema mbegu za amani zitapandwa. Mizabibu ingetoa tunda lake, na nchi ingetoa mazao yake. Mbingu zingetoa umande wake. Yahwe angewafanya masalia ya watu hao kuyarithi yote haya.

Zechariah 8:16-17

Mungu anawaagiza watu waenendeje na kwa nini?

Yahwe alisema watu wote lazima wasema kweli kila mtu na jirani yake, na kuhukumu kwa kweli, haki, na amani katika malango yao. Alisema kusiwepo mwenye kupanga njama ovu moyoni mwake dhidi ya jirani yake wala kuvutwa na nadhiri za uongo. Yahwe aliagiza kwa sababu haya ni mambo aliyokuwa anayachukia.

Zechariah 8:18-19

Katika nuru ya ukweli kwamba kufunga mwezi wa nne, tano, saba na wa nane kulikuwa kunakwenda kuwa nyakati za furaha, na sherehe za kupendeza kwa nyumba ya Yuda, Yahwe aliwaambia wafanye nini?

Walikuwa wameambiwa kupenda kweli na amani.

Zechariah 8:20-22

Yahwe alisema nani atakayekuja kumtafuta na kuomba upendeleo wake?

Yahwe alisema watu wengi kutoka sehemu mbalimbali na mataifa yenye nguvu yangekuja kuomba upendeleo wake.

Zechariah 8:23

Kwa nini watu kumi kutoka kila lugha na taifa waombe kwenda Yerusalemu na watu wa Yahwe, katika siku hizo?

Wataomba kwenda Yerusalemu na watu wa Yahwe kwa kuwa watakuwa wamesikia kwamba Yahwe yupo nao.

Zechariah 9

Zechariah 9:1-2

Tamko la Yahwe linahusu nini?

Tamko la Yahwe linahusu nchi ya Hadraki na Dameski, Hamathi, na Tiro na Sidoni.

Zechariah 9:3-4

Yahwe anasema Bwana ataifanya nini Tiro?

Yahwe anasema, "Bwana atamnyang'anya na kuharibu nguvu zake juu ya bahari, hivyo atateketezwa kwa moto.

Zechariah 9:5-7

Yahwe alisema atawafanya nini Wafilisiti na kungekuwa na nini kwao?

Yahwe alisema angekata kiburi cha Wafilisti. Yahwe pia alisema wangekuwa masalia kwa Mungu kama ukoo katika Yuda.

Zechariah 9:8

Yahwe anatoa sababu gani moja ya kupiga kambi kuzunguka nchi yake?

Yahwe alisema angepiga kambi kuzunguka nchi yake dhidi ya majeshi ya adui ili kusiwepo wa kupita au kurudi, maana alisema hakuna mtesaji angeweza kupita humo tena.

Zechariah 9:9-10

Kwa nini binti Sayuni aliambiwa kupiga kelele kwa furaha kuu na binti Yerusalemu kupiga kelele kwa furaha?

Waliambiwa kufanya hivi kwa sababu mfalme wao anakuja kwao kwa utakatifu na anakwenda kuwakomboa.

Mfalme wao atakujaje kwao?

Mfalme wao atakuwa mnyenyekevu na kupanda punda, juu ya mwanapunda.

Mfalme huyu atayambia nini mataifa?

Mfalme atatamka amani kwa mataifa

Utawala wa mfalme huyo utakuwa na ukubwa gani?

Utawala wa mfalme huyo utakuwa kutoka bahari hata bahari na kutoka mto hata miisho ya nchi.

Zechariah 9:11-15

Kwa nini Yahwe amewaweka huru wafungwa wao kutoka katika shimo lisilo na maji?

Yahwe anasema amefanya hivyo kwa sababu ya damu ya agano lake nao.

Yahwe amewainua wana wa Sayuni dhidi ya nani?

Yahwe amewainua wana wa Sayuni dhidi ya wana wa Ugiriki.

Yahwe ameifanya Sayuni kuwaje?

Yahwe ameifanya Sayuni kuwa kama upanga wa shujaa.

Zechariah 9:16-17

Sayuni itakuwa kama nini katika siku hiyo Yahwe, Mungu wao, atakapowakomboa?

Katika siku hiyo, Sayuni itakuwa mapambo ya taji iliyoinuliwa juu ya nchi ya Yahwe.

Zechariah 10

Zechariah 10:1-2

Yahwe atafanya nini kwa Sayuni?

Yahwe ataandaa manyunyu ya mvua kwa Sayuni watakapomwomba, na kupanda mashamba.

Ni kitu gani kinachowafanya watu wapotee na kuangaika kama kondoo?

Watu wanatangatanga kama kondoo na kuteseka kwa sababu vinyago vinawadanganya, waganga wanasema uongo, wanasema ndoto tupu na kutoa faraja tupu. Pia watu hawana mchungaji.

Zechariah 10:3

Yahwe alisema angemwadhibu nani?

Yahwe alisema angemwadhibu beberu- viongozi.

Zechariah 10:4-5

Yahwe alisema nini kitatoka katika nyumba ya Yuda?

Yahwe alisema jiwe la pembeni, kigingi cha hema, upinde wa vita, na kila kiongozi angetoka katika nyumba ya Yuda.

Zechariah 10:6-7

Yahwe alisema angefanya nini kwa nyumba ya Yuda na Yusufu?

Yahwe alisema angeiimalisha nyumba ya Yuda na kuiokoa nyumba ya Yusufu. Yahwe alisema angezihuisha, na kuwa na rehema juu yake.

Zechariah 10:8-10

Yuda na Efraimu watafanya nini wakikumbuka Yahwe katika nchi ya mbali walipopandwa na Yahwe?

Wao na watoto wao wataishi na kurudi watakapo mkumbuka Yahwe katika nchi za mbali alipowapanda.

Zechariah 10:11-12

Yahwe alisema atafanya nini kwa Misri na Ashuru baada ya kuwakusanya wale wa nyumba ya Yuda kutoka maeneo hayo?

Yahwe alisema angeushusha utukufu wa Ashuru na kuifanya fimbo ya Misri kutoka kwa Wamisri.

Zechariah 11

Zechariah 11:1-3

Kwa nini wachungaji wanapiga yowe?

Wachungaji wanapiga yowe kwa sababu utukufu wao umeangamia.

Zechariah 11:4-6

Yahwe alimwambia Zakaria kufanya nini?

Yahwe alimwambia Zakaria, "kuchunga kondoo waliokusudiwa kuchinjwa!"

Yahwe alisema angefanya nini kwa wenyeji wa Yuda?

Yahwe alisema asingewaurumia tena lakini kila mtu kuanguka katika mikono ya wachungaji na mikono ya mfalme, nayo wangeivunja nchi.

Zechariah 11:7-9

Majina ya fimbo mbili alizozitumia Zakaria kuchunga kundi lililokusudiwa kuchinjwa ni yapi?

Majina ya zile fimbo mbili yalikuwa ni "upendeleo" na "umoja"

Kwa nini Zakaria aliwaaribu wachungaji watatu katika mwezi mmoja?

Zakaria alifanya hivi kwa sababu alichoshwa na wachungaji hao na wao pia walimchukia.

Zechariah 11:10-12

Zakaria alilipwa kiasi gani?

Zakaria alilipwa vipande thelathini vya fedha.

Zechariah 11:13-14

Yahwe alimwambia Zakaria afanye nini na vipande vyake hivyo thelathini vya fedha?

Zakaria aliambiwa kuviweka kwenye hazina.

Kuvunja fimbo ya pili iliyoitwa "umoja,"kulifanya nini?

Kuvunja fimbo ya pili kulivunja udugu baina ya Yuda na Israeli.

Zechariah 11:15-16

Yahwe alisema atainua mchungaji katika nchi. Mchungaji huyo atafanya nini?

Mchungaji hatajari kondoo. Hatawatafuta kondoo waliopotea, wala kuwaponya wanaochechemea. Hatawalisha wanyonge, lakini atawala walionona na kupasua kwato zao.

Zechariah 11:17

Laana gani imetangazwa kwa mchungaji asiyefaa kwa kuwaacha kondoo?

Laana ni hii: "Upanga uje dhidi ya mkono wake wa kulia na jicho lake la kulia! Mkono wake wa kulia ukauke na jicho lake la kulia lipofuke!"

Zechariah 12

Zechariah 12:1-3

Yahwe ni nani afanyaye tamko hili kwa Israeli?

Yahwe ndiye azitandaye mbingu na kuweka msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mtu ndani yake.

Nani anayekwenda kujikusanya kinyume cha Yerusalemu?

Mataifa yote ya dunia yatakusanyika kinyume cha Yerusalemu.

Zechariah 12:4-5

Yahwe alisema mambo gani maalumu atakayoyafanya kwa farasi na wapanda farasi, Siku mataifa yatakapokusanyika dhidi ya Yuda?

Yahwe alisema angempiga kila farasi kwa ushangao na mpanda farasi kwa wazimu. Pia atawapofusha farasi wa majeshi.

Zechariah 12:6

Viongozi wa Yuda watakuwa kama nani katika siku hiyo?

Katika siku hiyo, viongozi watakuwa kama vyungu vya moto kati ya mti na kama miale ya moto kwa mabua yaliyosimama.

Zechariah 12:7-9

Kwa nini Yahwe atayaokoa mahema ya Yuda kwanza?

Yahwe atayaokoa mahema ya Yuda kwanza ili kwamba heshima ya nyumba ya Daudi na heshima ya nyumba ya wale waishio Yerusalemu isizidi ile ya Yuda.

Yahwe anakusudia kufanya nini siku hiyo?

Yahwe alisema kwamba siku hiyo anaazimia kuaribu mataifa yote yajayo kinyume cha Yerusalemu.

Zechariah 12:10-11

Siku hiyo, Yahwe atamimina nini katika nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu?

Yahwe atamimina roho ya huruma na maombezi.

Nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu watafanya nini watakapomwona waliyemchoma?

Watakapomwona waliyemchoma, wataomboleza kwa ajili yake kama aombolezaye kifo cha mwana wa pekee.

Zechariah 12:12-14

Nchi itaombolezaje siku hiyo?

Katika siku hiyo, kila familia itaomboleza peke yake na kila familia na kila mwanamke peke yake na mwanamme peke yake.

Zechariah 13

Zechariah 13:1-2

Kijito kilichofunguliwa kwa ajili ya nyumba ya Daudi kitakuwaje siku hiyo?

Kitakuwa kwa ajili ya dhambi zao na uchafu wao.

Yahwe ataondoa nini kutoka katika nchi na kwa nini?

Yahwe ataondoa majina ya sanamu kutoka katika nchi hata yasikumbukwe tena.

Yahwe atasababisha nini kiondoke katika nchi?

Yahwe atawafanya manabii wa uongo na roho zao chafu kutoka katika nchi.

Zechariah 13:3

Ikiwa mtu ataendelea kutabiri wazazi wake watamfanyaje?

Wazazi wake waliomzaa watamchoma akitabiri

Zechariah 13:4-6

Kwa nini anayetabiri hatavaa tena vazi la singa?

Ili aweze kuwadanganya watu.

Zechariah 13:7

Mchungaji ni nani?

"Asimamaye karibu nami"

Nini kitatokea kwa kondoo mchungaji atakapouawa?

Kondoo watatawanyika

Zechariah 13:8-9

Yahwe anatangaza nini kitatokea katika nchi yote.

Yahwe anatangaza kwamba theluthi mbili zitaondolewa. Wataangamia, theruthi tu ndiyo itakayosalia.

Ni nini kitakachotendeka kwa theruthi inayosalia pale?

Itapitishwa motoni, kusafishwa na kujaribiwa.

Theruthi iliyosalia itasemaje.

Itasema Yahwe ni Mungu wangu!"

Zechariah 14

Zechariah 14:1-2

Kwa nini mateka wa Yerusalemu wagawanywe katikati yake

Kwa sababu Yahwe atakusanya kila taifa dhidi ya Yerusalemu kwa vita, na mji utatekwa. Nyumba zitatekwa.

Zechariah 14:3-4

Nini kitatokea kwa mataifa yaliyopigana na Yerusalem?

Yahwe atatoka na kupiga vita dhidi ya mataifa hayo kama apigavyo vita katika siku ya vita.

Nini kitakachotokea katika Mlima wa Mizeituni wakati Yahwe atakaposimama juu yake?

Mlima wa Mizeituni utagawanyika katikati na kutakuwa na bonde kubwa katikati yake.

Zechariah 14:5

Yahwe na watakatifu wake watakuja lini?

Yahwe na watakatifu wake watakuja baada ya wenyeji wa Yerusalemu kukimbia chini katika bonde kati ya milima ya Yahwe.

Zechariah 14:6-8

Maji yatiririkayo kutoka Yerusalemu yatakwenda wapi?

Nusu yake yatakwenda bahari ya mashariki, na baadhi yatatiririka kuelekea upande wa magharibi.

Zechariah 14:9-11

Mfalme juuya dunia yote atakuwa nani?

Yahwe ndiye atakayekuwa mfalme juu ya dunia yote.

Je! Mungu ataiaribu Yerusalemu?

Hakutakuwa na uharibifu tena kutoka kwa Yahwe dhidi yao; Yerusalemu itakuwa salama.

Zechariah 14:12-15

Kwa pigo gani Yahwe atawashambulia watu waliopiga vita dhidi ya Yerusalemu?

Mwili, macho, na ndimi za wote waliopiga vita dhidi ya Yerusalemu itaoza.

Kitatokea nini wakati hofu kutoka kwa Yahwe itakapokuja kati yao?

Kila mtu ataukamata mkono wa jirani yake; kila mkono utainuliwa dhidi ya mkono wa jirani.

Zechariah 14:16-19

Wote wanaobaki katika mataifa yaliyokuja dhidi ya Yerusalemu watafanya nini?

Watapanda mwaka kwa mwaka kumwabudu mfalme, Yahwe wa majeshi, na kutunza sikukuu ya vibanda.

Kutotokea nini kwa mataifa yote ya dunia yasiyokwenda Yerusalemu kumwabudu mfalme Yahwe wa majeshi?

Ikiwa mtu yeyote haendi Yerusalemu, Yahwe hatawapa mvua. Mapigo yote kutoka kwa Yahwe yatawashambulia mataifa yasiyokwenda kutunza Sherehe ya Vibanda.

Zechariah 14:20-21

Akina nani hawatakuwa katika nyumba ya Yahwe katika siku hiyo?

Katika siku hiyo wafanyabiashara hawatakuwemo tena nyumbani mwa Yahwe wa majeshi.