Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Luke

Luke 1

Luke 1:1-4

Nani walikuwa "mashahidi wa macho" ambao anawataja Luka?

"Mashahidi wenye kuyaona" ndio waliokuwa pamoja na Yesu tangu mwanzo wa huduma yake.

Baadhi ya mashahidi wa macho walifanya nini baada ya kuona Yesu alichofanya?

Waliandika kazi au habari ya alichofanya Yesu.

Kwanini Luka aliamua kuandika kazi yake ya kile ambacho Yesu alisema na kufanay?

Alitaka Theofilo ajue ukweli wa mambo aliyofundisha.

Luke 1:5-7

Kwanini Mungu alitazama Zakaria na Elizabeth kuwa wenye haki?

Mungu aliwatazama hao kuwa wenye haki sababu walitii amri yake.

Kwanini Zakaria na Elizabeth hawakuwa na watoto?

Hawakuwa na watoto kwasababu Elizabethi alikuwa hawezi kuzaa watoto. Kwasasa yeye na Zakaria walikuwa wazee.

Luke 1:8-10

Kazi gani ambayo Zakaria alikuwa akifanya katika hekalu la Yerusalemu?

Zakaria alikuwa akitumika kama kuhani.

Zakaria alifanya nini hekaluni?

Alichoma ubani kwa Mungu.

Watu walifanyaje wakati zakaria alikuwa hekaluni?

Watu walibaki nje katika kiwanja na walikuwa wanaomba.

Luke 1:11-15

Ambaye alionekana kwa Zakaria alipokuwa katika hekalu?

Malaika wa Bwana akamtokea Zakaria hekaluni.

Zakaria alifanya tendo gani alipomwona Malaika?

Zakaria alipomwona Malaika, aliogopo sana.

Nini alichosema Malaika kwa Zakaria?

Malaika alimwambia Zakaria asiogope na mke wake Elizabethi atakuwa na mtoto. Jina la mtoto litakuwa Yohana.

Luke 1:16-17

Je malaika alisemaje ambacho Yohana atakifanya kwa ajili ya wana wa Israeli?

malaika alisema John atawageuza tena wana wa Israeli wamwelekee Bwana Mungu wao.

Matendo yote ya Yohana yatawafanya tayari watu wa aina gani?

Watu walioandaliwa kwaajili ya Bwana watafanywa tayari.

Luke 1:18-20

Jina la Malaika lilikuwa nani na kwa kawaida alikaa wapi?

Jina la malaika lilikuwa Gabrieli na kwa kawaida alisimama katika uwepo wa Mungu.

Luke 1:21-25

Je nini malaika alisema kitatokea kwa Zakaria kwa sababu hakuamini maneno ya malaika?

Zakaria hatakuwa na uwezo wa kuzungumza mpaka mtoto atakapozaliwa.

Luke 1:26-29

Miezi sita baada ya ujauzito wa Elizabeth, nani Gabrieli alitumwa na Mungu kumwona?

Bikra aitwye Mariamu, aliyekuwa amechumbiwa na Yusufu, ukoo wa Daudi.

Luke 1:30-33

Nini alichokisema malaika kitatokea kwa Mariamu?

Malaika alisema kwamba Mariamu atakuwa mimba.

mtoto ataitwa jina gani na atafanya nini?

Mtoto ilikuwa aitwe Yesu na atatawala uzao wa Yakobo milele ufalme usio na mwisho

Luke 1:34-38

Malaika alisema haya yatatokeaje sababu sababu Mariamu alikuwa bikra?

Malaika alisema kwamba Roho Mtakatifu atakuja kwa Mariamu na nguvu zake aliye juu zitakuwa juu yake.

Malaika alisema kwamba huyu mtoto mtakatifu angekuwa mtoto wa nani?

Malaika alisema kwamba mtoto angeitwa Mwana wa Mungu.

Malaika alisema nini ambacho akiwezekani kwa kwa Mungu?

Hakuna.

Luke 1:39-41

Mariamu alipo msalimia Elizabethi, nini ambacho mtoto wa Elizabethi alifanya?

mtoto aliruka tumboni kwa furaha.

Luke 1:42-53

Nani Elizabeth alisema alikuwa amebarikiwa?

Elizabeth alisema kuwa Maria na mtoto wake walikuwa wamebarikiwa.

Luke 1:54-58

kisha Mariamu alisema kuwa matendo ya nguvu ya Mungu yatatimiza ahadi ambayo imetengenezwa na Mungu?

Wangeweza kutimiza ahadi za Mungu kwa Abrahamu na kizazi chake kuwa na huruma kwao na kuwasaidia.

Luke 1:59-61

Katika siku ya tohara, kwa kawaida wangemwitaje mwana wa Elizabeth?

Zacharia.

Luke 1:62-63

Nini alichoandika Zakaria alipoulizwa jina la mtoto atakuwa nani?

Zakaria aliandika "Jina lake Yohana."

Luke 1:64-66

Nini kilitokea kwa Zakaria gafla baada ya kuandika jina la mtoto?

ghafla baada ya kuandika jina la mtoto, Zakaria akazungumza na kusifu Mungu?

Sababu ya mtukio haya ninin ambacho kila mmoja alitambua kuhusu mtoto?

Walitambua kwamba mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.

Luke 1:67-75

Zakaria alimsifu Mungu kwa sababu Mungu amekuja kufanya njia kwa kitakachotokea?

Mungu sasa amefanya njia kuwaweka watu wake huru

Luke 1:76-79

Zakaria alitoa unabii kwamba mtoto wake atasaidia watu kujua nini?

Yohana atasaidia watu kujua jinsi watakavyo okoka kupitia msamaha wa dhambi zao.

Luke 1:80

Wapi Yohana alikulia na kuishi mpaka yeye kuanza kuonekana hadharani?

Yohana alikulia na kuishi katika maeneo ya jangwa.

Luke 2

Luke 2:1-3

watu walikwenda wapi kusajiliwa kwaajili ya sensa?

Watu walienda kwenye miji yao kusajiliwa.

Luke 2:4-5

Yusufu akaenda Bethlehemu na Mariamu kwa sababu alikuwa ukoo wa nani?

Yosefu na Maria walienda Bethlehemu kwa kuwa Yusufu alikuwa mwana wa Daudi.

Luke 2:6-7

Mariamu alipozaa mwana, alimweka wapi?

mtoto alipozaliwa, Mariamu alimweka kwenye kihori cha kulishia wanyama.

Luke 2:8-9

Malaika alioneka kwa nani?

Malaika alionekana kwa wachungaji waliokuwa wakichunga makundi yao.

Wachungaji waliitikiaje walipomona malaika?

Malaika waliogopa sana.

Luke 2:10-14

habari gani njema malaika aliwapa wachungaji?

Malaika waliwaambia wachungaji mwokozi amezaliwa, ambaye ndiye Kristo Bwana.

Luke 2:15-20

wachungaji walifanyaje baada ya malaika kuwaacha?

wachungaji wakaenda Bethelememu kumwona mtoto ambaye alikua amezaliwa.

Luke 2:21

Lini Yesu alitahiriwa?

Yesu alitahiriwa siku ya nane baada ya kuzaliwa kwake.

Luke 2:22-24

Kwa nini Yusufu na Mariamu kumleta mtoto Yesu hekaluni Yerusalemu?

Walimpeleka Yesu mpaka hekaluni ili wamweke mbele ya Bwana ili watoe sadaka, ndivyo walivyoamriwa katika sheria ya Musa.

Luke 2:25-29

Nini alichokidhihirisha Roho Mtakatifu kwa Simeoni?

Roho Mtakatifu alijidhihirisha kwa Simeoni kwamba hatakufa kabla hajamwona Bwana Kristo.

Luke 2:30-32

Nini Simeoni alisema ambavyo Yesu atakuwa?

Simeoni alisema kwamba Yesu atakuwa nuru kudhihirisha ukweli kwa wamataifa na utukufu wa watu wa Mungu Israeli.

Luke 2:33-35

Nini alikisema Simeoni kitatokea kwa Mariamu ikiwa matokeao ya Yesu?

Simeoni alisema kwamba upanga utachoma nafsi yake.

Luke 2:36-38

Nabii mke Ana alifanyaje alipokuja kwa Mariamu, Yusufu na Yesu?

Ana alianza kumshukuru Mungu na kuzungumza kuhusu mtoto kwa kila mmoja.

Luke 2:39-40

Nini kilitokea kwa mtoto Yesu baada ya kurudi Nazarethi?

Yesu alikua na akawa na nguvu, hekima ikaongezeka, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

Luke 2:41-44

kwa nini wazazi wa Yesu hawakutabua alikuwa amebaki nyuma Yerusalemu wakati wa sikukuu ya Pasaka?

Hawakutambua kwa sababu walihisi kwamba yumo kwenye kundi lililokuwa likisafiri pamoja nao.

Luke 2:45-47

Wazazi walimpata wapi Yesu na alikuwa anafanya nini?

Wazazi wake walimpata hekaluni amekaa katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.

Luke 2:48-50

Yesu alijibu nini Mariamu alipomuuliza kwamba wamekuwa na wasiwasi wakimtafuta?

"Hamkujua lazima niwe kwenye nyumba ya Baba yangu?"

Luke 2:51-52

Nini ulikua mtazamo wa Yesu kuelekea wazazi wake walipo rejea Nazareti?

Alikuwa mtiifu kwao.

Yesu akiwa anakua, alikuwa kijana wa namna gani?

Alikuwa katika hekima na kimo na aliongezeka katika fadhila kwa Mungu na watu.

Luke 3

Luke 3:3

Ni ujumbe gani Yohana alihubiri katika maeneo ya ukanda wa mto Yordani?

Yohana alihubiri ubatizo wa toba kwa msamaha wa dhambi.

Luke 3:4-7

Ni kwaajili ya nani Yohana alisema anatayarisha njia?

Yohana alisema alikuwa akiweka tayari njia ya Bwana.

Luke 3:8

Yohana aliwaambia watu wasimani ukweli kwamba Ibrahimu alikuwa baba yao, lakini kufanya nini badala yake?

Yohana aliwaambia kuzaa matunda kwamba yatokane na toba.

Luke 3:9-11

Yohana alisema nini kinatokea kwa mti usiozaa matunda mazuri?

Yohana alisema kuwa ulikatwa na kutupwa motoni.

Luke 3:12-14

Ni nini Yohana aliwaambia watoza ushuru lazima wafanye kuonesha toba?

Yohana alisema kwamba lazima wasitoze pesa zaidi ya zile wanazopaswa.

Luke 3:15-17

Yohana aliwaambia watu kwamba anabatiza kwa maji, lakini kwamba mtu fulani alikuwa anakuja ambaye angebatiza kwa nini?

Yohana alisema mtu mmoja alikuw anakuja ambaye atabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Luke 3:18-20

Kwa nini Yohana alimkemea Herode?

Yohana alimkemea Herode kwa sababu alikuwa amemwoa mke wa kaka yake, na kwa kufanya maovu mengi.

Nani alimweka Yohana gerezani?

Herode alimweka Yohana Gerezani.

Luke 3:21-22

Ni nini kilichotokea mara moja baada ya Yohana alimbatiza Yesu?

Baada ya Yohana kumbatiza Yesu, mbingu zikafunguka na Roho Mtakatifu alishuka juu yake kama njiwa.

Nini ilichosema sauti iliyotoka mbinguni?

Sauti toka mbinguni ilisema, "wewe ni mwanangu mpendwa." Ninafurahishwa na wewe."

Luke 3:23-24

Pengine Yesu alikuwa na umri gani alipoanza kufundisha?

Yesu alikuwa na umri upatao miaka thelathini alipoanza kufundisha.

Luke 3:25-38

mwana wa Mathatia, mwana wa Amosi ... Yoda

Huu ni mwendelezo wa orodha ya wahenga wa Yesu. Tumia mfumo ule ule uliotumia kwenye mstari uliopita.

Luke 4

Luke 4:1-2

Nani alimuongoza Yesu nyikani?

Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu nyikani.

Kwa muda gani mwovu alimjaribu Yesu kule nyikani?

Shetani alimjaribu Yesu nyikani kwa siku arobaini (40).

Luke 4:3-4

Mwovu alimpa Yesu changamoto gani kuyafanya mawe juu ya ardhi?

shetani alimwambia Yesu kugeuza mawe kuwa mkate.

Mwitikio wa Yesu ulikuwa nini kwa shetani?

mtu hataishi kwa mkate pekee.

Luke 4:5-7

shetani alimwonesha nini Yesu kutoka mahali pa juu?

shetani alimwonesha Yesu falme zote za dunia.

Shetani alitaka Yesu afanye nini?

Ibilisi alitaka Yesu kuinama amwabudu.

Luke 4:8

Nini Yesu alimjibu shetani?

Ni lazima umwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye tu.

Luke 4:9-11

nini ambacho shetani alimwambia Yesu kufanya wakati alipompeleka juu ya kilele cha mnara wa hekalu?

Aliwaambia Yesu kuruka chini kutoka huko.

Luke 4:12-15

Nini mwitikio wa Yesu kwa shetani?

Usimjaribu Bwana Mungu wako.

Shetani alifanya nini baada ya Yesu kukataa kuruka kutoka hekaluni?

Ibilisi alimwacha Yesu mpaka wakati mwingine.

Luke 4:16-19

kutoka kitabu gani cha maandiko alichosoma Yesu aliposimama ndani ya sinagogi?

Yesu alisoma kutoka kwa nabii Isaya

Luke 4:20-22

Yesu alisema nini kilichokuwa kitimie siku hiyo?

Yesu alisema kwamba maandiko aliyoyasoma kutoka Isaya yalikuwa yametimia siku hiyo

Luke 4:23-24

Ni kupokelewa kupi ambako Yesu anazungumzia nabii anapata katika nchi yake?

Yesu anasema kwamba hakuna nabii anayekubaliwa katika nchi yake.

Luke 4:25-27

Katika mfano wa kwanza wa Yesu kwa watu katika sinagogi, ni wapi Mungu alimtuma Eliya kumsaidia mtu fulani?

Mungu alimtuma Eliya Sarepta, karibu na mji wa Sidoni.

Katika mfano wa pili wa Yesu kwa watu katika Sinagogi, Mungu anamtaka Elisha amsaidie mtu fulani kutoka nchi gani?

Mungu anataka Elisha amsaidie Naamani wa Siria.

Luke 4:28-32

Watu katika sinagogi walifanya nini waliposikia mifano hii kutoka kwa Yesu?

Walijawa na hasira na walitaka kumtupa juu ya mwamba.

Yesu aliepukaje kuuawa na watu katika sinagogi?

Yesu alitembea kupitia katikati yao.

Luke 4:33-34

Katika Sinagogi, pepo linazungumza nini kupitia mtu anayemjua Yesu?

Pepo lilisema kwamba alimjua Yesu alikuwa Mtakatifu wa Mungu.

Luke 4:35-39

Watu waliitikiaje baada ya Yesu kutoa pepo?

Watu walishangazwa na wakaendelea kusema hilo mmoja na mwingine

Luke 4:40-41

Yesu alifanya nini kwa wagonjwa ambao waliletwa kwake?

Yesu akaweka mikono yake juu ya kila mmoja wao, akawaponya.

Mapepo yalisema nini baada ya kufukuzwa, na kwa nini Yesu hayakuruhusu kusema?

Pepo walisema kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, na Yesu hakuruhusu waseme sababu walijua kuwa yeye ni Kristo.

Luke 4:42-44

Yesu alisema sababu gani yeye alitumwa?

Yesu alisema alitumwa kuhubiri habari njema kuhusu ufalme wa Mungu katika miji mingine mingi.

Luke 5

Luke 5:4-7

Baada ya kutumia mashua ya Simoni kama eneo la kufundishia watu, Yesu alimwambia Simon afanye nini na mashua yake?

Chukua mashua uipeleke kwenye kilindi kirefu cha maji na ushushe nyavu kwenye maji kuvua samaki.

Ingawa Petro hakupata kitu usiku uliopita, alifanya nini?

Alitii na alitupa nyavu.

Kilitokea nini walipoweka chini nyavu?

Walikusanya idadi kubwa ya samaki, nyingi sana kiasi kwamba nyavu zao zilikuwa zikikatika.

Luke 5:8-14

Simoni alitaka Yesu afanye nini?kwa nini?

Simoni alitaka Yesu aende mbali naye kwa sababu Simoni alijua kwamba (Simoni)alikuwa mtu mwenye dhambi

Yesu alisema nini kwa Simoni kuhusu kazi yake ya baadaye?

Yesu alisema kwamba tokea sasa nakuendelea atakuwa akivua watu.

Luke 5:15-19

Kwa wakati huu, watu wangapi walikwa wanakuja kusikia mafundisho ya Yesu na kuponywa magonjwa yao?

Umati mkubwa wa watu ilikuwa unakuja kwa Yesu

Luke 5:20-21

Yesu alisema nini kwa mtu aliyepooza ambaye rafiki zake walimshusha kupitia paa la nyumba?

Mwanaume, dhambi zako zimesamehewa.

Kwanini waandishi na Mafarisayo walifikiri kwamba kauli hii ilikuwa kufuru?

Kwasababu Mungu pekee anaweza kusamehe dhambi.

Luke 5:22-28

Yesu alimponya aliyepooza kwa namna hiyo kueleleza kwamba alikuwa na mamlaka juu ya nchi kufanya nini?

Yesu alimponya mtu ikiwa kielelezo kwamba alikuwa na mamlaka juu ya nchi kusamehe dhambi.

Luke 5:29-32

Yesu alipokuwa anakula na kunywa katika nyumba ya Lawi, Yesu alisema ni nini ambacho amekuja kufanya?

amekuja kuwaita wenye dhambi kutubu.

Luke 5:33-35

Yesu alisema ni lini ambapo wanafunzi wake wangefunga?

Wanafunzi wake wangefunga baada ya Yesu kuondolewa kutoka kwao.

Luke 5:36

Kwa mfano wa Yesu, nini kingetokea ikiwa kipande cha vazi jipya kingetumika kurekebisha vazi la zamani?

Nguo mpya ingechanika, na kisingefaa kwa nguo ya zamani.

Luke 5:37-39

Kwa mfano wa pili wa Yesu, nini kingetokea ikiwa divai mpya ingewekwa kwenye kiriba cha zamani?

Kiriba cha zamani kingepasuka na divai ingemwagika.

Yesu alisema nini lazima kifanyike kutunza divai mpya kwa usahihi?

Divai mpya lazima iwekwe katika kiriba kipya.

Luke 6

Luke 6:1-2

Wanafunzi wa Yesu walifanya nini siku ya sabato ambapo Mafarisayo walisema ni kinyume cha sheria?

walichuma masuke, waliyafikicha katikati ya mikono (viganja) yao, na kula nafaka.

Luke 6:3-8

Cheo gani Yesu alikikiri kwaajili yake mwenyewe kwamba kilimpa mamlaka ya kusema ambacho ni kinyume na sheria kufanyika kwenye sabato?

Cheo alichokiri Yesu, Bwana wa Sabato.

Luke 6:9-11

Yesu alipomponya mtu mwenye mkono wa makunyanzi siku ya sabato, jinsi gani waandishi na mafarisayo walionesha hisia zao?

Walikuwa wamejaa hasira, na walizungumzia kuhusu ambacho wangefanya kwa Yesu.

Luke 6:12-19

Lilikuwa jina gani walilopewa wanaume kumi na wawili ambao Yesu aliwachagua juu mlimani?

Yesu aliwaita hao "mitume."

Luke 6:20-21

Ni watu wa namna gani Yesu alisema wamebarikiwa?

Wote ambao ni maskini, wenye njaa, waliao, na wachukiwao kwa ajili ya Mwana wa Adamu watabarikiwa.

Luke 6:22-26

Kutokana na Yesu, kwa nini watu hao wafurahi na waruke kwa furaha?

Sababu watakuwa na zawadi kubwa mbinguni.

Luke 6:27-34

Ni kwa namna gani Yesu alisema wanafunzi wake wataweza kuwatendea adui zao na ambao waliwachukia?

Wataweza kuwapenda adui zao na kufanya mema kwa wote wawachukiao.

Luke 6:35-40

Nini mtazamo wa Baba aliye juu sana juu ya watu wasio na shukrani na waovu?

Yeye ni mkarimu na rehema juu yao.

Luke 6:41-44

Kabla ya kuondoa doa kutoka kwa ndugu yetu, Yesu alisema nini kifanyike kwanza?

Kwanza, lazima ukiondoe kipande cha mti kitoke jichoni mwako kwamba sisi si wanafiki.

Luke 6:45

Ni nini kitokacho chema kutoka hazina njema moyoni mwa mtu mwema?

Kijacho kwenye moyo wa mtu mwema ni hazina njema

Nini kitokacho kwenye hazina mbovu ya moyo wa mtu mwovu?

Kitu ambacho kinatoka kwenye moyo wa mtu mwovu ni uovu

Luke 6:46-48

Mtu anayejenga nyumba juu ya mwamba mgumu nini anachokifanya na maneno ya Yesu?

Anayasikia maneno ya Yesu na kuyatii.

Luke 6:49

Mtu ambaye hujenga nyumba yake bila msingi hufanyaje na maneno ya Yesu?

Husikia maneno ya Yesu na hayatii.

Luke 7

Luke 7:2-5

Nini ambacho Akida anamwomba Yesu kufanya alipowatumwa wazee wa Kiyahudi kwa Yesu?

Alimwomba Yesu kuja nyumbani kwake na kumponya mtumwa wake.

Luke 7:6-8

Kwa nini akida sasa anatuma marafiki kumwambia Yesu kwamba yeye hakuwa anakuja nyumbani?

Huyo ofisa alisema Yesu hakuwa anastahili aje nyumbani kwake.

Namna gani akida sasa anakwenda kwa Yesu kumponya mtumwa wake?

baadaye akida alikwenda kwa Yesu kumponya mtumwa kwa kusema neno tu.

Luke 7:9-10

Yesu alisema nini kuhusu imani ya akida?

Yesu alisema kwamba hakuna hata katika Israeli hawakuona mtu yeyote mwenye hiyo imani sana.

Luke 7:11-15

mtazamo wa Yesu nini kumwelekea mjane ambaye mtoto wake alishakufa?

Yeye kwa kina alisukumwa na huruma.

Luke 7:16-20

Nini watu walisema kuhusu Yesu baada ya kumfufua mwana wa mjane kutoka kwa wafu?

Walisema kuwa nabii mkubwa ametokea kati yao, na kwamba Mungu ameangalia watu wake.

Luke 7:21-23

Namna gani Yesu alithibitisha kwa wanafunzi wa Yohana kwamba yeye ndiye alikuwa anakuja?

Yesu aliponya vipofu, viwete, wakoma, viziwi na alifufua wafu.

Luke 7:24-28

Yesu alisema kwamba Yohana alikuwa nani?

Yesu alisema Yohana alikuwa zaidi kuliko nabii

Luke 7:29-32

Mafarisayo na mabingwa katika sheria ya Kiyahudi walijifanyia nini walipokataa kubatizwa na Yohana?

Waliukataa ushauri wa Mungu kwao wenyewe.

Luke 7:33-35

Ni mashtaka gani yalifanywa dhidi ya Yohana Mbatizaji kwa sababu hakuwa anakula mkate au kunywa mvinyo?

Walisema, "Ana roho pepo."

Mashtaka gani yalifanywa dhidi ya Yesu kwa sababu alikuja akila na kunywa?

Walisema, "Yeye ni mtu mlafi na mlevi."

Luke 7:36-45

Nini alichofanya mwanamke wa mji kwa Yesu katika nyumba ya mfarisayo?

Alilowanisha miguu ya Yesu kwa machozi yake, aliyafuta kwa nywele zake, akiibusu miguu yake na aliipaka miguu yake manukato.

Luke 7:46-47

Yesu alisema kwamba kwa sababu alisamehewa dhambi nyingi, angefanya nini?

Angependa sana.

Luke 7:48-50

wale waliokuwa wamejinyoosha mezani walionesha hisia gani pale Yesu alipomwambia mwanamke kwamba dhambi zake zimesamehewa?

Waliuliza, "Nani huyu ambaye anasamehe hata dhambi?"

Luke 8

Luke 8:1-10

Kundi kubwa la wanawake lilifanya nini kwaajili ya Yesu na wanafunzi wake?

Wanawake waliwaandalia toka katika mapato yao wenyewe.

Luke 8:11-13

Katika mifano ya Yesu, kuna mbegu gani ambayo inapandwa?

Mbegu hii ni neno la Mungu.

Mbegu zipi ambazo ziliaguka pembeni mwa njia, na nini kilitokea kwa hizo?

Ni watu ambao wanasikia neno, lakini mwovu huja na kulichukua, hivyo wasiweze kuamini na kuokoka.

Nani ambao ni mbegu zilizoanguka eneo la mwamba, na hutokea nini kwao?

Ni watu ambao hupokea neno kwa furaha, lakini huacha kuamini wakati wa majaribu.

Luke 8:14-18

Nani ni mbegu ambazo huanguka kati ya miiba, na nini kinatokea kwao?

Ni watu ambao husikia neno, lakini ni hukabiliwa na utajiri na anasa za maisha haya, nao hawazai matunda makamilifu.

Akina nani ni mbegu zilizoanguka kwenye eneo zuri, na nini kinatokea kwao?

Ni watu ambao husikia neno, hulishika na kuzaa matunda kwa ustahimilivu.

Luke 8:19-23

Nani ambao Yesu alisema ni mama yake na ndugu zake?

Ni wale watu ambao hulisikia neno la Mungu na kulitii.

Luke 8:24-27

wanafunzi walisema nini Yesu alipotuliza upepo na maji?

Walisema, "Nani huyu amabaye anaamuru hata upepo na maji, na vinamtii yeye?"

Luke 8:28-31

pepo walimsababisha mtu kutoka mkoa wa Geneserini afanye nini?

Walimfanya aishi bila nguo kwenye makaburi, walimfanya akate minyororo na pingu na daima walimwongoza jangwani.

Luke 8:32-37

Pepo walienda wapi baada ya Yesu kuwaamuru kumwacha yule mtu?

Pepo waliingia kwenye kundi la nguruwe, ambao walikimbilia kwenye ziwa na wakaza majini.

Luke 8:38-46

Yesu alimwambia nini yule mtu aende na kufanya?

Yesu alimwambia aende nyumbani kwake na akasimulie makuu yote Mungu aliyomfanya kwaajili yake.

Luke 8:47-53

Kutokana na Yesu, nini kilichosababisha mwanamke aliyetokwa damu kuponywa?

Yeye aliponywa kwasababu ya imani yake.

Luke 8:54-56

Yesu alifanya nini nyumbani kwa Yairo?

Yesu alimfufua binti Yairo kutoka kifoni.

Luke 9

Luke 9:1-6

Yesu aliwatuma wale kumi na wawili waende kufanya nini?

Yesu aliwatuma waende kuhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.

Luke 9:7-11

Herode alisikia kutoka kwa baadhi ya watu yawezekana maelezo matatu yahusuyo Yesu alikuwa nani. Yapi hayo?

Baadhi yao walisema Yesu alikuwa Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka wafu, baadhi alisema Eliya ametokea na wengine walisema nabii wa kale amefufuka.

Luke 9:12-14

Chakula gani wanafunzi wawalishe makutano?

Walikuwa na mikate mitano na samaki wawili.

wanaume wangapi walimfuata Yesu katika kundi ambapo ilikuwa jangwani?

kama wanaume elfu tano walikuwa pale.

Luke 9:15-19

Yesu alifanya nini na mikate mitano na samaki wawili?

Alitazama mbinguni, akavibariki, akamega katika vipande, na akawapa wanafunzi kuwapa makutano.

Vikapu vingapi vya mabaki ya chakula vilikuwa pale?

Vilikuwa vikapu kumi na viwili vya mabaki ya chakula.

Luke 9:20-22

Wakati Yesu aliwauliza wanafunzi yeye ni nani, Peter kujibu nini?

Alisema, "Kristo kutoka kwa Mungu."

Luke 9:23-27

Yesu alisema kwamba kama kuna mtu anataka kuja baada yake, ni lazima kufanya nini?

Lazima ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, na kumfuata Yesu.

Luke 9:28-29

Nini kilitokea katika mwonekano wa Yesu kwenye mlima?

Mwenekano wa uso wake ulibadilika na mavazi yake yakawa meupe na kung'aa.

Luke 9:30-33

Akina nani walitokea pamoja naYesu?

Musa na Elia walitokea wakiwa Yesu

Luke 9:34-36

Sauti iliyotokea kwenye wingu lililowatia kivuli ilisema nini?

Sauti ilisema, "Huyu ni mwanangu mteule; msikilizeni yeye."

Luke 9:37-42

Kabla Yesu hajafukuza mapepo, yalimsababisha mtoto wa mtu kufanya nini?

Mapepo yalimsababisha kupiga yowe na kicheko cha kutoa povu mdomoni.

Luke 9:43-45

kauli gani Yesu aliitoa kwa wanafunzi ambao hawakuelewa?

Yeye alisema, Mwana wa mtu atatolewa kwenda mikononi mwa watu."

Luke 9:46-50

Nani ambaye Yesu alisema ni mtu mkuu kati ya wanafunzi?

Ni yule aliye mdogo kati yao ambaye ndiye mkuu.

Luke 9:51-60

Wakati siku zilikuwa zinakaribia ambapo Yesu angelikwenda juu mbinguni, yeye alifanya nini?

Yeye aliamua kuelekeza uso wake kuelekea Yerusalemu.

Luke 9:61-62

Kuwa sawa kwaajili ya ufalme wa Mungu, ni lazima mtu asifanye nini mara anapokuwa "kaweka mikono yake kulima"

Mtu lazima asitazame nyuma.

Luke 10

Luke 10:3-7

Yesu aliwaambia wasibebe nini wale sabini?

Lazima wasibebe mkoba wowote wa fedha, mfuko wowote wa safari, au malapa yoyote.

Luke 10:8-9

Yesu aliwaambia wale sabini wafanye nini katika kila mji?

Aliwaambia kuponya wagonjwa na kuwaambia watu, "Ufalme wa Mungu umekaribia kwenu."

Luke 10:10-16

Kama mji haukuwapokea wale waliotumwa na Yesu kwao, hukumu itafananaje kwa mji huo?

Itakuwa mbaya sana kuliko ile ya Sodoma.

Luke 10:17-20

Waliporudi wale sabini na kutoa taarifa kwa furaha kwamba waliweza kukemea pepo, Yesu aliwaambia nini?

Yeye alisema, "Furahini hata zaidi kwamba majina yenu yamewekwa katika kumbukumbu mbinguni."

Luke 10:21-24

Yesu alisema ilikuwa inampendeza Baba kuudhihirisha ufalme wa Mungu kwa nani?

Ilikuwa inampendeza Baba kuudhihirisha ufalme wa Mungu kwa wale wasiofunzwa, kama watoto wadogo.

Luke 10:25-30

Kutokana na Yesu, sheria ya kiyahudi inasema nini kilicho lazima mtu akifanye ili aurithi uzima wa milele?

Lazima umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa nafsi yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili yako yote na jirani yako kama wewe mwenyewe.

Luke 10:31-32

Katika mfano wa Yesu, nini kuhani Myahudi alikifanya alipoona mtu yu karibu kufa katika njia?

Alipita pembeni upande mwingine.

Malawi alifanya ninialipomwona yule mtu?

alipita pembeni upande mwingine.

Luke 10:33-35

Msamaria alifanya nini alipomuona yule mtu?

aliyafunga majeraha yake, akamweka juu ya mnyama wake, akamleta kwenye hoteli na akamtunza.

Luke 10:36-37

aliposema mfano huo, Yesu alimwambia nini yule mwalimu wa wayahudi aende akakifanye?

Nenda na ukajioneshe huruma kama ya Msamaria kwenye huu mhano.

Luke 10:38-39

Wakati ule ule Mariamu alifanya nini?

Aliketi kwenye miguu ya Yesu na akamsikiliza.

Luke 10:40-42

Martha alifanya nini Yesu alipokuja nyumbani kwake?

Alikuwa anahangaika kuandaa kuhudumia chakula.

Yesu alisema nani kachagua kufanya kitu kizuri zaidi?

Alisema kwamba Mariamu kachagua kufanya kitu kizuri zaidi.

Luke 11

Luke 11:2

Ni aina gani ya maombi Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuomba?

Aliomba, 'Baba, Jina lako litakaswe. Ufalme wako na uje. Utupe mkate wetu wa kila siku. Utusamehe dhambi zetu, Kama nasi tunavyo wasamehe wote waliotukosea. Na wala usitutie katika majaribu.

Luke 11:3-4

Maombi gani ambayo Yesun aliwafundisha wanafunzi wake kuomba?

Yeye alioma, "Baba, takasa jina lako. Ruhusu ufalme wako uje. Tupe sisi kila siku mkate wetu na tusamehe sisi makosa yetu, kwa sababu sisi husamehe kila mtu ambaye ametukosea. Na usitupeleke sisi katika majaribu."

Luke 11:5-10

Katika mfano wa Yesu, kwa nini yule mtu aliinuka na kumpa rafiki yake mkate usiku wa manane?

Kwa sababu ya huyu rafiki asiyeona aibu kung'ang'ania.

Luke 11:11-13

Baba aliye mbinguni atawapa nini wale wanaomuomba yeye.

Atawapa Roho Mtakatifu.

Luke 11:14-17

Walipomwona akifukuza mapepo, baadhi walimtuhumu Yesu anafanya nini?

Walimtuhumu anatoa mapepo kwa Beelzebuli, mkuu wa mapepo

Luke 11:18-23

Yesu alijibu anatoa pepo kwa nguvu gani?

Anatoa mapepo kwa kidole cha Mungu.

Luke 11:24-26

Kama roho chafu inamtoka mtu lakini badaye inarudi, hali ya mtu mwishowe itakuwaje?

Hali ya mtu mwishoni itakuwa mbaya sana huliko hali ya mwanzoni.

Luke 11:27-30

Wakati mwanamke akipaza sauti, akimbariki mama wa Yesu, Yesu alisema nani aliye barikiwa?

Wale ambao wanasikia neno la Mungu na kulitunza.

Luke 11:31

Yesu alisema yeye ni mkuu kuliko watu gani wawili wa Agano la kale?

Sulemani naYona

Luke 11:32-38

Yesu alisema kwamba yeye ni mkubwa kuliko watu gani wawili wa Agano la kale?

Sulemani naYona.

Luke 11:39-41

Yesu alisema Mafarisayo walijawa na nini ndani yao?

Alisema wamejaa tamaa na uovu.

Luke 11:42-44

Yesu alisema Mafarisayo walipuuza nini?

Walipuuza haki na kumpenda Mungu.

Luke 11:45-48

Yesu alisema nini wale waalimu wa sheria walikuwa wakikifanya kwa watu wengine

Walikuwa wakiwabebesha watu mizigo migumu kuibeba, lakini bila wao wenyewe kuigusa mizigo ile.

Luke 11:49-52

Yesu alisema kizazi hiki kingewajibika kwaajili ya nini?

Wangewajibika kwa damu yote iliyomwagika ya manabii tangu ulimwengu ulipoanza.

Luke 11:53-54

Waandishi na mafarisayo walifanya nini baada ya kusikia maneno ya Yesu?

Walimpinga na kubishana naye, wakijaribu kumtega kwa maneno yake mwenyewe.

Luke 12

Luke 12:2-3

Kutokana na Yesu, Kitatokea nini kwa kila kitu unachosema gizani?

Hicho kitasikika kwenye nuru.

Luke 12:4-7

Yesu alisema nani ambaye umwogope?

Unapaswa umwogope ambaye anamamlaka kukutupa jehanamu.

Luke 12:8-12

Yesu atafanya nini kwa yeyote atakaye mkiri Yesu mbele za watu?

Yesu atalikiri jina la mtu huyo mbele ya malaika wa Mungu.

Luke 12:13-15

Kutokana na Yesu, maisha yetu hayategemei nini?

Maisha yetu hayategemei katika utajiri wa mali zetu.

Luke 12:16-19

Katika mfano wa Yesu, nini ambacho mtu tajiri alikuwa anakwenda kufanya kwa sababu mashamba yake yalizaa kwa wingi?

Alikuwa anakwenda kuyaangusha chini maghala yake na kujenga makubwa zaidi, ndipo apumzike kwa urahisi, ale, anywe na afurahi.

Luke 12:20-30

Mungu alimuambia nini mtu tajiri?

ewe mtu mpumbavu, usiku wa leo wanahitaji roho ya kwako, na vitu vyote ulivyoviandaa vitakuwa vya nini?

Luke 12:31-32

Badala ya kusumbukia kuhusu mambo ya maisha haya, Yesu alisema tufanye nini?

Tuutafute ufalme wa Mungu.

Luke 12:33-36

Ni wapi Yesu amesema tuhifadhi mali zetu, na kwa nini?

Tuhifadhi mali zetu mbinguni, kwa sababu hapo wezi hawataingia na nondo haitaweza kuharibu.

Luke 12:37-38

Kulingana na Yesu, ni watumishi wapi wa Mungu wamebarikiwa?

Wamebarikiwa wale watakaokutwa wakikesha na wako tayari Yesu atakaporudi.

Luke 12:39-44

Tunajua saa ya ambayo Yesu atakuja?

Hapana.

Luke 12:45-46

Kinatokea nini kwa mtumishi ambaye anawaonea watumishi wengine na hayuko tayari kwa ujio wa bwana wake?

Bwana atamkata vipande vipande na kuteua mahali kwaajili yake pamoja na wasio waaminifu.

Luke 12:47-50

Kinahitajika nini kwa wale ambao wamepewa vingi?

Kwao vitahitajika vingi.

Luke 12:51-56

Kutokana na Yesu, aina gani ya mgawanyiko ataleta duniani?

Pale patakuwa na watu katika nyumba moja lakini watagawanyika kila mmoja dhidi ya mwenzake

Luke 12:57-59

Kutokana na Yesu, tutafanya nini kabla sisi hatujaenda pamoja na adui wetu mbele ya hakimu?

Sisi tuwe na juhudi kuweka mambo sawa mapema.

Luke 13

Luke 13:1-7

Wagalilaya waliouawa na Pilato waliteseka kwa njia hii sababu walikuwa wenye dhambi zaidi ya wagalilaya wengine?

Hapana.

Luke 13:8-9

Katika mfano wa Yesu, ni nini kilifanyika kwa mtini ambao haukuzaa matunda baada ya miaka mitatu?

uliwekewa mbolea kama kirutubisho na mwaka mmoja zaidi uzae matunda, kama hakuna, ingekuwa kukatwa.

Luke 13:10-11

Katika Sinagogi, nini kilisababisha yule mwanamke kupindana kwa miaka kumi na nane?

Ni roho mchafu wa udhaifu kutoka kwa shetani alimpinda.

Luke 13:12-14

Kwa nini viongozi wa sinagogi waliudhika Yesu alipomponya yule mwanamke?

Sababu Yesu alimponya siku ya sabato.

Luke 13:15-17

Yesu alionesha kwa namna gani kwamba kiongozi wa sinagogi alikuwa mnafiki?

Yesu alimkumbusha kwamba angemfungua myama siku ya sabato, bado yeye alikuwa kaudhika Yesu alipomfungua yule mwanamke siku ya sabato.

Luke 13:18-21

Namna gani ufalme wa Mungu unafanana mbegu ya haradali?

Kwa sababu inaanza ndogo kama mbegu, lakini ndipo inakua nakuwa kitu kikubwa mpaka kuwa eneo la makao.

Luke 13:22-27

Wakati akiuliza kama wengi wangeokolewa, Yesu alijibu nini?

Yeye alisema, "Jitahidi kuingia kupitia mlango mwembamba, kwa sababu wengi watajaribu na hawataweza kuingia."

Luke 13:28-30

Watu watafanya nini ambao watatupwa nje, na hawawezi kuingia ufalme wa Mungu?

Watalia na kusaga meno.

Nani watakusanyanyika kupumzika wakati chakula cha jioni katika Ufalme wa Mungu?

Ibrahimu, Isaka, Yakobo, na manabii, na wengi kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini.

Luke 13:31-33

Wapi Yesu alisema kwamba lazima atauawa?

Lazima auawe katika Yerusalemu.

Luke 13:34-35

Je, Yesu alitamani kufanya nini na watu wa Yerusalemu?

Alitamani kuwakusanya kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake.

Mlejesho wa watu wa Yerusalemu ulikuwaje katika nia ya Yesu kwa ajili yao?

Walikataa.

Walakini, Yesu alitabiri nini kuhusu Yerusalemu na watu wake?

Nyuma yao iliachwa, na wasingalimuona Yesu tena mpaka walisema, "alibarikiwa anayekuja katika jina la Bwana."

Luke 14

Luke 14:1-3

Kwa mtu aliyesumbuliwa uvimbe akisimama mbele zake, Yesu aliwauliza nini wataalamu wa sheria wa Kiyahudi na Mafarisayo?

Ni kisheria kuponya siku ya sabato, au hapana?

Luke 14:4-9

Wataalam na Mafarisayo walijibu nini?

Walikaa kimya.

Alipomponya yule mtu, Yesu aliwaoneshaje wataalamu na Mafarisayo kwamba walikuwa wanafiki?

Yesu aliwakumbusha wao kwamba wangesaidia mtoto au ng'ombe wao ambaye aliangukia kwenye shimo siku ya sabato.

Luke 14:10-12

Yesu alisema kitatokea nini kwa yeyote anayejiinua mwenyewe?

Atanyenyekezwa.

Yesu alisema nini kitatokea kwa yeyote anayenyenyekea mwenyewe?

Atainuliwa.

Luke 14:13-17

Kutokana na Yesu, namna gani atazawadiwa mtu anayemkaribisha nyumbani kwake masikini, kiwete, mlemavu na kipofu?

Watalipwa siku ya ufufuo wa haki

Luke 14:18-20

Katika mfano wa Yesu wa chakula cha jioni, watu walifanya nini na nani ambao walikuwa amealikwa awali?

Wao walianza kutoa udhuru kuhusu kwa nini hawakuweza kuhudhuria kwenye chakula cha jioni.

Luke 14:21-22

Nani ambao yule bwana badaye akawakaribisha kwenye chakula cha jioni yake?

maskini, viwete, vipofu na walemavu.

Luke 14:23-27

Yule bwana alisema nini badaye kuhusu wale waliokuwa wamealikwa kwanza katika chakula chake cha jioni?

Hakuna kati yao atakionja chakula chake cha jioni.

Luke 14:28-30

Katika mfano wa Yesu kuhusu nini kinahitajika kumfuata yeye, nini lazima afanye kwanza mtu ambaye anataka kujenga mnara?

mtu lazima ahesabu gharama.

Luke 14:31-33

Kutokana na Yesu, lazima wanafunzi wake wafanye nini?

Lazima wachukie maisha na familia zao, wabebe msalaba wao, wamfuate yeye, na waachane na vyote walivyo navyo.

Luke 14:34-35

Kama chumvi ikipoteza radha yake, inafanywa nini?

Inatupwa mbali.

Luke 15

Luke 15:3-7

Katika mfano wa Yesu, mchungaji aliye poteza mmoja katika kondoo wake mia alifanya nini?

Huacha wengine tisini na tisa na kwenda kumtafuta kondoo aliyepotea, na kumleta, akifurahi.

Luke 15:8-10

Katika mfano wa Yesu, Mwanamke aliyepoteza sarafu moja kati ya shilingi zake kumi alifanya nini?

Alitafuta kwa bidii hadi alipoipata, kisha akafurahi pamoja na rafiki rafiki na majirani zake.

Nini kinatokea mbinguni mdhambi mmoja anapotubu?

Kule kunafuraha mbele ya malaika wa Mungu.

Luke 15:11-12

Katika mfano wa Yesu, mwana mdogo alifanya ombi gani kwa baba yake?

Nipe mimi sasa mali ambazo ni halali yangu kuzirithi.

Luke 15:13-14

Mwana mdogo alifanya nini na urithi wake?

Alitapanya fedha zake kwa maisha ya uasherati.

Luke 15:15-16

Baada ya fedha zake kuisha, mwana mdogo alifanya nini ili aweze kuishi?

Yeye mwenyewe alijiajiri kulisha nguruwe wa mtu mwingine.

Luke 15:17-19

alipoanza kufikiri kwa makini, mwana mdogo aliamua kufanya nini?

Aliamua kwenda na kukiri dhambi yake kwa baba yake, na kuomba kuajiriwa kama mmoja wa watumishi.

Luke 15:20-21

Baba alifanya nini alipomwona mwana mdogo akirudi nyumbani?

Alimkimbilia akamkumbatia na kumbusu.

Luke 15:22-27

Baba alifanya nini kwa haraka kwa ajili mwana mdogo?

Baba alimpa vazi, pete, viatu, na kuandaa karamu.

Luke 15:28-30

Mwana mkubwa alijisikiaje alipoambiwa kuhusu karamu ya mwana mdogo?

Alikuwa na hasira na hakutaka kwenda kwenye karamu.

Lawama ya mwana mkubwa kwa baba ilikuwa ni nini?

Mwana mkubwa alilaumu kwamba alifuata maelekezo ya baba yake, lakini hajawahi kupewa mbuzi kusherekea na rafiki zake.

Luke 15:31-32

Mwitikio wa baba kwa mwana wake mkubwa ulikuwa ni nini?

Alisema, "Mwanangu, wewe uko pamoja nami siku zote, na vyote vya kwangu ni vyako."

Kwa nini baba alisema ilikuwa sawa kufanya sherehe kwaajili ya mwana mdogo?

Kwa sababu mwana mdogo alikuwa amepotea na sasa amepatikana.

Luke 16

Luke 16:1-4

Taarifa gani tajiri aliipokea kuhusu msimamizi wake?

Alisikia kwamba msimamizi alikuwa anafuja mali zake.

Luke 16:5-7

Msimamizi alifanya nini kabla hajalazimishwa kuacha kazi yake?

Alimwita kila mdaiwa wa tajiri na kuwapunguzia madeni yao.

Luke 16:8-9

Mwitikio gani tajiri alikua nao baada ya vitendo vya msimamizi wake?

Yeye alimsifu msimamizi kwa sababu yeye alitenda kwa werevu.

Yesu aliwaambia wengine kufanya nini kuzingatia habari hii?

Alisema, "fanya marafiki kwaajili yako kwa nia ya utajiri wa duniani, ili kwamba zikishatoweka, watakukaribisha wewe kwenye makao ya milele."

Luke 16:10-12

Yesu alisema kwamba mtu ambaye ni mwaminifu kwenye kidogo pia atakuwa mwaminifu kwa kipi kingine?

Mtu huyu pia atakuwa mwaminifu katika kwa vingi.

Luke 16:13-15

Yesu alisema ni mabwana wawili wapi ambao ni lazima kuchagua kati yao kutumikia?

Ni lazima tuchagua kati ya Mungu na mali.

Luke 16:16-17

Kulingana na Yesu, ni nini kilikuwa katika athari mpaka Yohana Mbatizaji alipokuja?

Torati na manabii vilikuwapo katika athari.

Kulingana na Yesu, ni nini sasa huwa kinahubiriwa?

injili ya ufalme wa Mungu sasa huwa inahubiriwa.

Luke 16:18-21

Kulingana na Yesu, mtu wa aina gani yule ambaye anamwacha mke wake na kuoa mwingine?

Mtu huyu ni mzinifu.

Luke 16:22-23

Katika kisa cha Yesu, ombaomba Lazaro alienda wapi baada ya alipokufa?

Ombaoma Lazaro akachukuliwa na malaika mpaka upande wa Abrahamu.

Tajiri alikwenda wapi baada ya kufa?

Kuteseka kuzimu.

Luke 16:24

Nini lilikua ombi la kwanza kutoka kwa tajiri kwa Abrahamu?

Alisema, "Tafadhali mruhusu Lazaro aje aniletee maji kidogo kwa sababu ninateswa katika moto huu."

Luke 16:25-26

Jibu la Abrahamu lilikuwa nini kwa tajiri?

Alisema, "Pale kuna shimo kubwa kati yetu kwamba hakuna anayeweza kuvuka."

Luke 16:27-28

Ombi la pili ambalo tajiri aliliomba kwa Abrahamu ni lipi?

Alisema, "Tafadhali mtume Lazaro kuwaonya ndugu zangu kuhusu mahali hapa."

Luke 16:29-31

Jibu la Abrahamu lilikuwaje kwa yule tajiri?

Alisema, "wanao Musa na manabii; waache wawasikilize hao."

Abrahamu alisema kama hangesikiliza kwa Musa na manabii, kipi kingine kisingewashwishi?

Wasingeweza kushawishiwa hata na mtu fulani aliyefufuka kutoka kwa wafu.

Luke 17

Luke 17:3-8

Yesu alisema lazima tufanye nini kama ndugu yetu anatenda dhambi dhidi yetu anarudi akisema "ninatubu?"

Lazima tumsamehe.

Luke 17:9-10

Kama watumishi, tusemeje baada ya kufanya kila kitu tulichoamriwa na Bwana wetu?

Tuseme, "Sisi ni watumishi tusio na faida; tumefanya kile tulichotakiwa kufanya."

Luke 17:11-13

Yesu alikutana na nani alipokuwa akiingia katika kijiji kilicho nchi za mipaka ya Samaria na Galilaya?

Alikutana na wakoma kumi.

Walisema nini kwa Yesu?

Walisema, "Yesu, Bwana, tuhurumie sisi."

Luke 17:14-19

Yesu aliwaambia wafanye nini?

Aliwaambia waenda na kujionyesha wenyewe kwa makuhani.

Ni nini kilichotokea kwa wenye ukoma walipokuwa wakienda?

Walitakasika.

Wakoma wangapi katika kumi walirudi kumshukuru Yesu?

Alirudi mmoja tu.

Mkoma ambaye alirudi kumshukuru Yesu alikuwa anatokea wapi?

Alikuwa anatokea Samaria.

Luke 17:20-21

Alipoulizwa kuhusu ujio wa ufalme, Yesu alisema ufalme wa Mungu uko wapi?

Ufalme wa Mungu uko ndani yako.

Luke 17:22-24

Yesu alisema itakuwa inafanana na nini siku yake, atakapo dhihirika tena?

Itakuwa kama mwako wa mwanga ghafla tokea sehemu moja ya anga kwenda nyingine.

Luke 17:25-31

Yesu alisema nini lazima kitokee kwanza?

Lazima ateseke mambo mengi na kukataliwa na kizazi hicho.

Kwa vipi siku za Mwana wa mtu zifanane na siku za Nuhu na siku za Lutu?

Wengi watakula, kunywa, Kuoana, kuuza, kupanda na kujenga wasielewe kwamba siku ya uharibifu imekuja.

Luke 17:32-33

Ni kwa jinsi gani hatupaswi kufanana na mke wa lutu?

Ni lazima tusirudi nyuma kujaribu kuweka maisha yetu hapa duniani katika siku hiyo.

Luke 17:34-36

Taswira ipi kwa asili Yesu aliitumia kujibu swali kwa wanafunzi wake, "Wapi, Bwana?"

Pale palipo mzoga, ndipo tai wanapokusanyika.

Luke 17:37

Ni picha ipi kutoka asili Yesu alitumia kujibu swali wanafunzi wake ', "Ni wapi Bwana?"

Ambapo kuna mwili, kuna mkusanyiko wa tai pamoja.

Luke 18

Luke 18:1-2

Yesu alitaka kuwafundisha nini wanafunzi wake kuhusu maombi kwenye simulizi hii?

Alitaka kuwafundisha kwamba wanatakiwa kuomba daima na wasikate tamaa.

Luke 18:3-5

Nini ambacho mjane alikuwa akiendelea kukiomba kwa hakimu dhalimu?

Aliomba kupatiwa haki dhidi ya mpinzani wake.

Baada ya muda, hakimu asiyetenda haki alisema nini kwake mwenyewe?

Alisema, "Kwa sababu mjane huyu anasababisha matatizo na hakomi kuja kwangu, nitamsaidia apate haki yake."

Luke 18:6-8

Yesu alitaka kufundisha nini kwa wanafunzi wake kuhusu jinsi Mungu ajibuvyo maombi?

Alitaka kuwafundisha kwamba Mungu ataleta haki kwa wale ambao wanamlilia.

Luke 18:9-10

Mfarisayo alifikiri vipi kuhusu haki yake mwenyewe na kuhusu watu wengine?

Alidhani kuwa na haki zaidi ya watu wengine.

Katika simulizi ya Yesu, watu gani wawili walikwenda hekaluni kuomba?

Mfarisayo na mtoza ushuru walikwenda hekaluni kuomba.

Luke 18:11-12

Mfarisayo alifikiri vipi kuhusu haki yake mwenyewe na kuhusu watu wengine?

Alidhani kuwa alikuwa na haki zaidi ya watu wengine.

Luke 18:13-14

Mtoza ushuru alimwomba Mungu nini alipokuwa hekaluni?

Aliomba, "Mungu nirehemu mimi, mwenye dhambi?

Yupi alirudi nyumbani kwake anahaki mbele za Mungu?

Mtoza ushuru alihesabiwa haki mbele za Mungu.

Luke 18:15-21

Yesu alisema kwamba ufalme wa Mungu unamilikiwa na nani?

Ni mali ya wale ambao ni kama watoto.

Luke 18:22-27

Ni kitu gani kimoja ambacho Yesu alimuomba yule kiongozi (aliyekuwa anatii amri za Mungu toka akiwa kijana) afanye?

Yesu alimuomba auze vitu vyote alivyo kuwa navyo na avigawe kwa masikini.

Mwitikio wa kiongozi ulikuwaje kwa kauli ya Yesu na kwa nini?

Alihuzunika sana, sababu alikuwa tajiri sana.

Luke 18:28-30

Yesu aliahidi nini kwa wale ambao walioacha mambo ya dunia kwa faida ya ufalme wa Mungu?

Yesu aliwaahidi vingi zaidi katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao.

Luke 18:31-37

Kutokana na Yesu, nini ambacho manabii wa agano la kale wameandika kuhusu Mwana wa mtu?

Kwamba angetolewa kwa wamataifa, alidhihakiwa na alitendewa aibu, alichapwa na alikufa lakini siku ya tatu angelifufuka tena.

Luke 18:38-41

Yule kipofu aliyekuwa njiani alilia kwa sauti akisemaje kwa Yesu?

Alisema, "Mwana wa Daudi, nihurumie."

Luke 18:42-43

Mwitikio wa watu ulikuwa namna gani baada kuona kipofu kaponywa?

Walimtukuza na kumpa utukufu Mungu.

Luke 19

Luke 19:1-4

Nani alipanda juu ya mti kumwona Yesu, na kazi yake ilikuwa ni nini na nafasi yake katika jamii?

Alikuwa Zakayo, mtoza ushuru tajiri.

Luke 19:5-7

Lawama zipi ambazo kila mtu alitoa alipomwona Yesu amekwenda nyumbani kwa Zakayo?

Walisema, "Yesu amekwenda kumtembelea mtu ambaye ni mwenye dhambi."

Luke 19:8-10

Yesu alisema nini juu ya zakayo baada ya Zakayo kutangaza zawadi zake kwa masikini?

Alisema, "Leo wokovu umekuja kwenye nyumba hii."

Luke 19:11-15

Watu walitegemea nini kitatokea Yesu akifika Yerusalemu.

Walidhani kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara moja.

Katika mfano wa Yesu, Muungwana alikuwa anasafiri kuelekea wapi?

Alikuwa anakwenda nchi ya mbali kupokea ufalme, na ndipo angerudi.

Luke 19:16-17

Yesu alifanya nini kwaajili ya mtumishi ambaye amekuwa mwaminifu na ametengeneza mafungu kumi zaidi?

Aliwapa mamlaka juu ya miji kumi.

Luke 19:18-19

Yesu alifanya nini na mtumishi ambaye amekuwa mwaminifu na ametengeneza mafungu matano zaidi?

Aliwapa mamlaka juu ya miji mitano zaidi.

Luke 19:20-23

Aina gani ya mtu ambaye yule mtuishi mwovu alifikiri alikuwa muungwana?

Alifikiri muungwana alikuwa hana huruma.

Luke 19:24-25

Afisa alimfanya nini yule mtumishi mbaya?

Alimnyang'anya yule mtumishi mbaya fungu lake.

Luke 19:26-28

Muungwana alifanya nini na wale ambao hawakutaka atawale juu yao?

Muungwana aliwauwa mbele yeake.

Luke 19:29-36

Aina gani ya mnyama ambaye Yesu alipanda juu yake akiwa anaingia Yerusalemu?

Mwanapunda ambaye hajapandwa bado.

Luke 19:37-38

Mkutano ulipaza sauti vipi wakati Yesu anashuka mlima wa mizeituni?

Walisema, "Kabarikiwa mfalme ajaye katika jina la Bwana!"

Luke 19:39-40

Yesu anasema kingetokea nini kama watu hawatapaza sauti wakifurahi?

Alisema mawe yatapaza sauti.

Luke 19:41-42

Yesu alifanya nini alipoukaribia mji?

Alilia.

Luke 19:43-46

Ndipo Yesu akatoa unabii gani ungetokea kwa watu na mji?

Alisema kwamba watu watapigwa na kwamba hakuna jiwe ilitaachwa juu ya jingine.

Luke 19:47-48

Nani walitaka kumuua Yesu alipokuwa akifundisha hekaluni?

Makuhani wakuu na waandishi na viongozi wa watu walitaka kumuua Yesu.

Kwa nini hawakuweza kumuua wakati huu?

Kwa sababu watu walikuwa wanamsikiliza kwa makini.

Luke 20

Luke 20:3-4

Viongozi wa kiyahudi walipomuuliza Yesu kwa mamlaka gani alifundisha, swali gani Yesu aliwauliza?

Aliwauliza, "Ubatizo wa Yohana ni kutoka mbinguni au kwa watu?"

Luke 20:5-10

Kama wangejibu "ilitoka mbinguni", viongozi wa Kiyahudi walidhani ni nini Yesu angesema kwao?

Viongozi wa Kiyahudi walidhani Yesu angewajibu, "sasa kwa nini hamkumwamini?"

Kama wangejibu, "kutoka kwa watu," walifikiri watu wangewafanyia nini?

Walifikiri kwamba watu wangewapiga mawe.

Luke 20:11-12

Katika mfano wa Yesu, watunza mizabibu walifanya nini bwana alipowatuma watumishi wake kuchukua matunda ya shamba la mzababu?

waliwapiga watumishi, waliwatendea vibaya, na kuwarudisha mikono mitupu.

Luke 20:13-14

Hatimaye, nani alitumwa na bwana kwenda kwa watunza mizabibu?

Alimtumwa mwanaye mpendwa.

Luke 20:15-18

Watunza mizabibu walimfanya nini yule mwana alipokuja kwenye shambani mizabibu?

Walimtupa nje ya shamba la mizabibu na kumuua.

Bwana mwenye shamba la mizabibu atafanya nini kwa watunza mizabibu?

Atawaharibu hao watunza mizabibu na kuwapa wengine shamba la mizabibu.

Luke 20:19-24

Yesu aliusema mfano huu dhidi ya nani?

Yeye aliwaambia mfano huu waandishi na wakuu wa makuhani.

Luke 20:25-26

Ni kwa namna gani Yesu alijibu swali la ni halali kulipa kodi kwa Kaisari au la?

Alisema kumpa Kaisari vitu vya kaisari, na kumpa Mungu vitu vya Mungu.

Luke 20:27-33

Tukio gani ambalo Masadukayo hawaamini?

Hawaamini ufufuo wa wafu.

Luke 20:34-36

Yesu alisema nini kuhusu ndoa katika ulimwengu huu na katika umilele?

Katika ulimwengu huu kuna kuoana, lakini katika uzima wa milele hamna kuoana.

Luke 20:37-40

Simulizi gani ya agano la kale ambayo Yesu alirejea ili kuthibitisha ukweli kuhusu ufufuo?

Alirejea simulizi ya Musa na kichaka, ambacho Musa alimwita Bwana kuwa Mungu wa Abrahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.

Luke 20:41-44

Kauli ipi ya Daudi kutoka Zabari aliyo nukuu Yesu katika swali kwa waandishi?

Alinukuu, "Bwana alisema kwa Bwana wangu, kaa kulia kwangu, mpaka niwafanye adui zako pakuwekea miguu"

Luke 20:45-47

Nyuma ya matendo yao kwa nje, mambo gano mabaya waandishi walikuwa wakifanya?

Walikuwa wakiteketeza nyumba za wajane, na kujifanya wanafanya maombi marefu.

Yesu alisema namna gani hawa waandishi watahukumiwa?

Watapokea laana kubwa sana.

Luke 21

Luke 21:1-4

Kwa nini Yesu alisema kwamba yule mjane maskini aliweka zaidi kwenye hazina kuliko zote za wengine?

Kwa sababu alitoa katika umasikini wake na wengine walitoa katika utajiri wao.

Luke 21:5-6

Yesu alisema nini kitatokea kwenye hekalu Yerusalemu?

Yeye alisema litaangushwa chini na hakuna jiwe moja litabaki juu ya lingine.

Luke 21:7-9

Maswali gani mawili ambayo watu walimuuliza Yesu kuhusu hekalu?

Waliuliza, "Mambo haya yatatokea lini, na nini itakuwa ni ishara kwamba haya mambo yako tayari kutokea?"

Yesu alionya kwamba waongo wengi watakuja. Waongo hawa watasema nini?

Watasema, "Mimi ni yeye" na "wakati umekaribia."

Luke 21:10-11

Matukio gani ya kutisha Yesu alisema yatatokea kabla ya mwisho?

Patakuwepo na vita, matetemeko ya nchi, njaa, tauni na ishara kubwa kutoka mbinguni.

Luke 21:12-15

Mateso ya waamini yatatengeneza fursa gani?

Yatatengeneza fursa kwaajili ya ushuhuda wao.

Luke 21:16-19

Nani atawachukia wafuasi wa Yesu?

Wazazi, ndugu, jamaa, marafiki, na "kila mtu" atawachukia.

Luke 21:20-22

Tukio gani ambalo litaashira kwamba uharibu wa Yerusalemu uko karibu?

Wakati Yerusalemu itakapozungukwa na majeshi, uharibifu wake unakaribia.

Yesu aliwaambia watu wafanye nini walioona kwamba uharibifu wa Yerusalemu upo karibu?

Aliwaambia wakimbilie milimani, kuuacha mji, na kutoingia mjini.

Yesu aliziitaje siku za kuharibiwa Yerusalemu?

aliziita ni siku za kisasi, kutimiza mambo yote yaliyoandikwa.

Luke 21:23-24

Mpaka lini Yerusalemu itakandamizwa na mataifa?

Yerusalemu itakandamizwa na mataifa hadi wakati mataifa yamekamilisha.

Luke 21:25-28

Ni ishara gani ambayo Yesu alisema itatangulia ujio wake wa nguvu na utukufu mkuu?

Alisema kutakuwa na ishara katika jua, mwezi, na nyota, na dhiki ya mataifa juu ya nchi.

Luke 21:29-31

Mfano gani Yesu alitoa wa jinsi wasikilizaji wake wavyojua lini majira yamekuja?

Alirejea kwenye mtini - unapoanza kumea machipukizi walijua kwamba majira ya joto yamekaribia.

Luke 21:32-33

Yesu alisema nini kitapita?

Mbingu na nchi zitapita.

Nini ambacho hakitapita kamwe?

Maneno ya Yesu hayatapita kamwe.

Luke 21:34-35

Ni nini ambacho Yesu aliwaonya wasikilizaji wake kutokufanya kwa sababu siku hiyo itakuja ghafula?

Aliwaonya wasiiache mioyo yao ikalemewa na ufisadi, ulevi na mahangaiko ya maisha haya.

Luke 21:36-38

Ni nini ambacho Yesu aliwaonya wasikilizaji wake kufanya kwa sababu siku hiyo itakuja ghafula?

Aliwaonya wawe tayari wakati wote na kuomba.

Luke 22

Luke 22:1-4

Katika wakati huu, ni sikukuu gani ya Kiyahudi iliyokuwa inakaribia?

Sikukuu ya mkate usiyotiwa chachu, iliyoitwa Pasaka.

Luke 22:5-9

Katika hali gani Yuda alikuwa anaangalia kwaajili nafasi ya kumtoa Yesu kuhani wakuu?

Alikuwa anaangalia kwenye nafasi Yesu alipokuwa mbali na mkutano.

Luke 22:10-11

Ni wapi Yesu na wanafunzi wake walikula mlo wa Pasaka?

Walikula katika chumba cha wageni Yerusalemu.

Luke 22:12-13

Ni wapi Yesu na wanafunzi wake walikula mlo wa Pasaka?

Walikula katika chumba kikubwa cha ghorofani cha wageni ambacho kilikuwa tayari kimeandaliwa huko Yerusalemu.

Luke 22:14-18

Yesu alisema lini tena atakula mlo wa Pasaka?

Atakuala mlo wa Pasaka tena pale itakapokamilika katika ufalme wa Mungu.

Luke 22:19-20

Yesu alisema nini alipoumega mkate na kuwapa wanafunzi wake?

Alisema, "Huu ni mwili wangu ambao umetolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi."

Yesu alisema nini alipowapa wanafunzi kikombe?

Alisema, "Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, iliyomwagika kwaajili yenu."

Luke 22:21-25

Ilikuwa mpango wa Mungu kwamba asalitiwe?

Ndiyo.

Wanafunzi walijua ambaye alikuwa anaelekea kumsaliti Yesu?

Hapana.

Luke 22:26-27

Nani ambaye Yesu alisema alikuwa mkubwa kati ya wanafunzi wake?

Mkubwa ni yule ambaye anatumika.

Namna gani Yesu aliishi kati ya wanafunzi wake?

Aliisha kama mtu anayetumika.

Luke 22:28-32

Yesu aliwaahidi wanafunzi wake wataketi wapi?

Alisema wataketi juu ya kiti cha enzi, wakiwahukumu wale kabila kumi na mbili za Israeli.

Luke 22:33-36

Yesu alitabiri nini ambacho Petro atafanya?

Alisema kwamba mara tatu Petro atakataa kuwa anamjua Yesu kabala jogoo hajawika.

Luke 22:37-38

Utabiri upi ulioandikwa kuhusu Yesu ambao ulitimizwa katika matukio haya?

Utabiri katika maandiko usemao, "Na alifikiriwa kama mtu ambaye anavunja sheria."

Luke 22:39-40

Katika mlima wa mizeituni, kwaajili ya nini Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuomba?

Ailitaka waombe kwamba wasiweze kuingia katika majaribu.

Luke 22:41-44

Juu ya mlima wa mzaituni, Yesu aliomba nini?

Aliomba, "Baba, kama uko tayari, ondoa kikombe hiki kwangu. Walakini siyo mapenzi yangu, bali ya kwako yafanyike."

Luke 22:45-46

Wale Wanafunzi walikuwa wakifanya nini Yesu aliporudi kutoka kuomba?

Walikuwa wakilala.

Luke 22:47-48

Namna gani Yuda alimsaliti Yesu mbele ya makutano?

Alimsaliti Yesu kwa busu.

Luke 22:49-51

Yesu alifanya nini na mtu ambaye sikio lake lilikatwa

Aliligusa sikio lake, akamponya.

Luke 22:52-53

Yesu alisema alikuwa wapi kila siku na wakuu wa makuhani?

Alikuwa hekaluni.

Luke 22:54-55

Baada ya kumkamata, walimpeleka wapi Yesu?

Walimpeleka nyumbani kwa kuhani mkuu.

Luke 22:56-58

Petro alisema nini wakati mtumishi fulani wa kike aliposema kwamba Petro alikuwa pamoja na Yesu?

Yeye alisema, "Mwanamke, mimi simjui."

Luke 22:59-60

Nini kilitokea gafla baada ya Petro kukataa hamjui Yesu kwa safari ya tatu?

Jogoo akawika.

Luke 22:61-62

Petro alifanya nini baada ya Yesu kumwangalia?

alikwenda nje na akalia kwa uchungu.

Luke 22:63-65

Watu waliokuwa wakimlinda Yesu walimfanyia nini?

Walimdhihaki na kumpiga, na walimkufuru.

Luke 22:66-68

Baraza lilipotaka kwamba Yesu awaambie kama ni Kristo, Yesu alisema kwamba kama aliwaambia, wasingelifanya nini?

Wasingeliamini.

Luke 22:69-71

Kwa nini baraza lilisema kwamba halihitaji mashahidi kuthibitisha kwamba Yesu amekiri kuwa Kristo?

Kwa sababu hilo walishasikia kutoka mdomoni mwa Yesu mwenyewe.

Luke 23

Luke 23:1-2

Mashitaka gani dhidi ya Yesu viongozi wa kiyahudi waliyafanya kwa Pilato?

Walisema Yesu alikuwa anapotosha taifa, anazuia kutoa kodi kwa kaisari, na anasema kwamba alikuwa Kristo, mfalme.

Luke 23:3-7

Baada ya kumuuliza Yesu, Pilato alisema nini kuhusu yeye?

Alisema, "Sioni kosa kwa mtu huyu."

Luke 23:8-12

Kwanini Herode alitaka kumuona Yesu?

Herode alitaka kumuona Yesu akifanya muujiza.

Yesu alijibuje swali la Herode?

Hakuna alichomjibu.

Luke 23:13-17

Yesu aliporudishwa kwa Pilato, Pilato alisema nini kuhusu Yesu kwa umma.

Alisema, "Sioni kosa kwa mtu huyu."

Luke 23:18-19

Ni nani umati walitaka afunguliwe gerezani kwa ajili ya sherehe ya pasaka?

Walimtaka Barnaba, mwahalifu.

Luke 23:20-22

Umati ulipiga kelele nini kifanyike kwa Yesu?

Walipiga kelele, Msulibishe, msulubishe.

Kwa mara tatu, Pilato aliuambia nini umati kuhusu Yesu?

Pialato alisema, "Hakuna ninachoona kinachostahili adhabu ya kifo kwake"

Luke 23:23-25

Kwa nini hatimaye Pilato anaridhia matakwa ya umma kumsulibisha Yesu?

Kwa sababu walisisitiza kwa sauti za juu.

Luke 23:26

Nani aliubeba msalaba wa Yesu, na akafuata nyuma ya Yesu.

Simoni wa Mkirene aliubeba msalaba wa Yesu.

Luke 23:27-31

Nani Yesu aliwaambia wanawake wa Yerusalemu wamlilie badala ya yeye?

Walie kwaajili yao wenyewe na watoto wao.

Luke 23:32

Ni nani alisulubiwa pamoja na Yesu?

Wahalifu wawili walisulubiwa pamoja na Yesu.

Luke 23:33-34

Kutoka msalabani, Yesu aliomba nini kwaajili ya wale wanaomsulibisha?

Yeye aliomba, "Baba, wasamehe, sababu hawajui wanachotenda"

Luke 23:35

Watu, Maaskari na mmoja wa wahalifu walimwambie Yesu afanye nini kwani Yesu alidai kuwa ni Kristo?

Walimuambia ajiokoe mwenyewe

Luke 23:36-38

Watu, Askari na yule mmoja wa wahalifu walimpa changamoto gani Yesu, kwa kuwa Yesu alikiri kuwa Kristo?

Walimkosoa ajiokoe mwenywe.

Nini kulikuwa kimeandikwa kwenye ubao juu ya Yesu?

Iliandikwa, "HUYU NI MFALME WA WAYAHUDI."

Luke 23:39-41

Watu, Maaskari, na mmoja wa wahalifu walimuambie Yesu afanye nini kwani Yesu alidai kuwa ni Kristo?

Walimwambia ajiokoe mwenyewe.

Luke 23:42-43

Ni maombi gani yule muhalifu wa pili alifanya kwa Yesu?

Alimuambia, "nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako"

Yesu aliahidi nini kwa mhalifu wa pili?

Alisema, "Leo utakuwa na paradiso."

Luke 23:44-45

Tukio gani la kimuujiza lilitokea mara kabla ya kifo cha Yesu?

Lilitokea giza juu ya nchi yote na pazia la hekalu likapasuka katikati.

Luke 23:46-51

Akida alisema nini kuhusu Yesu baada ya kifo cha Yesu?

Yeye alisema, "Hakika huyu alikuwa mtu wa haki."

Luke 23:52-53

Yusufu wa Arimathaya alifanya nini baada ya kifo cha Yesu?

"Alimuomba Pilato mwili na kuulaza katika kaburi."

Luke 23:54-56

Siku ipi ilikuwa inakaribia kuanza wakati Yesu alikuwa anazikwa?

Siku ya Sabato ilikuwa karibu kuanza.

Wanawake waliokuwa na Yesu walifanya nini siku ya sabato?

Walipumzika, kulingana na amri ya Mungu.

Luke 24

Luke 24:1-5

Wanawake walikuja lini kaburini kwa Yesu?

Walikuja mapema sana siku ya kwanza ya juma.

Wanawake walikuta nini pale kaburini?

Walikuta kwamba lile jiwe limeshavingirishwa kando, na kwamba mwili wa Yesu haukuwepo pale

Luke 24:6-10

Wale watu wawili wenye mavazi ya kung'aa (malaika) walisema kimetokea nini kwa Yesu?

Walisema kwamba amefufuka.

Luke 24:11-14

Nini ulikuwa mwitikio wa mitume wakati wale wanawake walipowaambia uzoefu wao pale kaburini?

Waliitupilia mbali taarifa kana kwamba ni maneno ya mzaha.

Petro aliona nini alipoangalia katika kaburi?

Aliona nguo za kitani peke yake.

Luke 24:15-20

Kwa nini wanafunzi waliokuwa wakienda Emau hawakumtambua Yesu alipojiunga nao?

Macho yao yalifungwa wasiweze kumtambua.

Luke 24:21-24

Wakati Yesu alipokuwa hai, mitume walitumaini angefanya nini?

Walitumaini kwamba angewaweka huru Israeli mbali na adui zake.

Luke 24:25-29

Yesu alielezea nini kwa wale watu wawili kutoka kwenye maandiko?

Alieleza kile maandiko yalisema kumhusu yeye.

Luke 24:30-32

Yesu alifanya nini walipomtambua?

Alitoweka mbele ya macho yao.

Luke 24:33-35

Wakati gani wale watu wawili hatimaye walimtambua?

Walimtambua alipobariki mkate, akaumega, na akawapa.

Luke 24:36-37

Yesu alisema nini kwanza alipowatokea wanafunzi wake huko Yerusalemu?

Alisema, "Amani iwe kwenu."

Luke 24:38-44

Yesu alithibitisha namna gani kwamba yeye siyo roho tu?

Aliwaita wanafunzi wake wamguse, na aliwaonesha mikono na miguu yake?

Luke 24:45-47

Jinsi gani wanafunzi walikuwa wanaweza kuyaelewa maandiko?

Yesu alifungua akili zao ili kwamba waweze kuelewa.

Yesu alisema nini kihubiriwe kwa mataifa yote?

Toba na msamaha wa dhambi vihubiriwe kwa mataifa yote.

Luke 24:48-49

Yesu aliwaambia kusubiri kwaajili nini wale wanafunzi?

Aliwaambia wasubiri hadi watakapo vikwa nguvu kutoka juu.

Luke 24:50-51

Kilitokea nini kwa Yesu alipowabariki wanafunzi karibu na Bethania?

Alichukuliwa juu mbinguni.

Luke 24:52-53

Wanafunzi walitumia wapi muda wao, na walifanyaje?

Walikuwa wakiendelea katika hekalu, kumbariki Mungu.