Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Titus

Titus 1

Titus 1:1-3

Paulo alikuwa na kusudi gani katika huduma yake kwa Mungu?

Kusudi lake lilikuwa kuanzisha na kueneza imani ya wateule wa Mungu na kueneza elimu na maarifa ya kweli.

Mungu aliwaahidi lini wateule wake uzima wa milele?

Mungu aliwaahidi uzima wa milele kabla ya nyakati zote au tangu milele iliyopita

Je Mungu anaweza kusema uongo?

Hapana.

Mungu alimtumia nani kuudhihirisha ujumbe wake kwa wakati muafaka?

Mungu alimtumia mtume Paulo.

Titus 1:4-5

Kulikuwa na mahusiano gani kati ya Tito na Paulo?

Tito alikuwa mwana wa kweli wa Paulo katika imani yao.

Titus 1:6-7

Ni mambo gani ya lazima yalitakiwa katika maisha ya kifamilia ya mzee wa kanisa?

Ni lazima awe mme wa mke mmoja, awe na watoto waaminifu wenye maadili mazuri.

Ni tabia gani ambazo mzee lazima aziepuke ili asiwe na lawama?

Ni lazima asiwe mtu mwenye kelele, asiyejizuia, asiwe mlevi, asiwe mgomvi na asiwe mchoyo.

Mwangalizi ana nafasi na wajibu gani katika nyumba ya Mungu?

Mwangalizi ni msimamizi ya nyumba ya Mungu.

Titus 1:8-9

Mzee wa kanisa anapaswa kuwa na sifa gani?

Mzee anapaswa kuwa mkaribishaji/mkarimu, mtu anayependa kufanya yaliyo mema, mwenye busara, mwenye haki, mchaji, na mwenye kiasi.

Mzee anatakiwa awe na mtazamo na msimamo gani juu ya mafundisho ya imani?

Anapaswa kushikilia (kuyasimamia) kwa nguvu mafundisho na kuyatumia katika kuwatia moyo na kuwakemea wengine.

Titus 1:10-11

Waalimu wa uongo walikuwa wanafanya nini kwa kutumia maneno yao?

Walikuwa wanadanganya watu na kuharibu familia

NI kitu gani kilikuwa kinawahamasisha Walimu wa uongo?

Walimu wa uongo walihamasishwa na faida za aibu.

Titus 1:12-13

Ni kwa namna gani Mzee anapaswa kushughulika na watu wasio na maadili ambao wanaliharibu kanisa?

Mzee anapaswa kuwasahihisha na kuwazuia kwa nguvu ili wawe katika imani ya kweli.

Titus 1:14

Paulo alisema hawapaswi kupoteza muda katika mambo gani?

Hawapaswi kuoteza muda katika hadithi za kiyahudi na maagizo ya wanadamu.

Titus 1:15-16

Ni kitu gani kilichochafuliwa katika maisha ya mtu asiyeamini?

Akili na dhamira zimeharibiwa

Ni kwa namna gani mtu mchafu/mbaya humkana Mungu ingawa hukiri kuwa anamjua?

Humkana Mungu kwa matendo yake.

Titus 2

Titus 2:1-2

Ni tabia zipi ambazo wazee hupaswa kuzionesha katika kanisa?

Wazee wanapaswa kuwa na kiasi, heshima, busara, usafi katika imani, katika upendo na katika uvumilivu.

Titus 2:3-5

Ni tabia kama zipi ambazo wanawake wazee wanapaswa kuzionesha katika kanisa?

Wanapaswa kuonesha heshima, sio usengenyaji; wanapaswa kuwa watulivu na wenye kufundisha yaliyo mazuri/mema.

Ni mambo gani wanawake wazee wanapaswa kuwafundisha wasichana?

Wanapaswa kuwafundisha kuwapenda na kuwatii waume zao, kuwapenda watoto, kuwa wenye busara, wasafi, na kuwa watunzaji wazuri wa nyumba.

Titus 2:6-8

Tito alitakiwa kufanya nini ili awe mfano kwa waumini?

Tito alitakiwa kufundisha, kuonesha usafi na heshima, na kutumia maneno yanayofaa na ya kweli yasiyohitaji kusahihishwa.

Titus 2:9-10

Ni kwa jinsi gani watumwa ambao ni waamini wanapaswa kuenenda?

Wanapaswa kuwatii mabwana zao, wasiwaibie, na wanapaswa kuonesha imani safi.

Ni athari gani itatokea kwa wengine wakati watumwa watakapoenenda kama Paulo alivyowaagiza?

Itayafanya mafundisho juu Mungu mwokozi wetu yawavutie watu wengine.

Titus 2:11-13

Ni nani atakayeokolewa na neema ya Mungu?

Neema ya Mungu inaweza kumuokoa kila mtu.

Neena ya Mungu inatufundisha kukataa nini?

Neema ya Mungu inatufundisha kukataa mambo yasiyo ya Kimungu na tamaa za kidunia.

Je waumini wanatarajia kupokea tendo gani kwa wakati ujao?

Waumini wanatarajia kupokea tumaini la mwonanekano wa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Titus 2:14-15

Kwanini Yesu alijitoa kwa ajili yetu?

Yesu alijitoa mwenyewe kwa ajili ya kulipa gharama ili kutuweka sisi huru kutoka katika dhambi (uasi) zetu, na kutufanya sisi kuwa watu wasafi wenye shauku ya kufanya mema.

Titus 3

Titus 3:1-2

Muumini anapaswa kuwa na mtazamo gani kwa watawala na wenye mamlaka?

Muumini anapaswa kuwa myenyekevu na mtiifu, kuwa tayari kwa kila kazi njema.

Titus 3:3

Ni kitu gani kinawapotosha na kuwatumikisha watu wasioaamini?

Wanapotoshwa na tamaa na anasa/starehe zao

Titus 3:4-5

Mungu hutuokoa kwa njia gani?

Mungu hutuokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa upya na kufanya upya kwa njia ya Roho Mtakatifu.

Je tumeokolewa kwasababu ya matendo mazuri tuliyokwisha kufanya au kwasababu ya huruma ya Mungu?

Tumeokolea tu kwa huruma ya Mungu.

Titus 3:6-7

Ni kitu gani Mungu alikifanya kwetu baada ya kuwa ametuhesabia haki?

Mungu alitufanya kuwa warithi wake.

Titus 3:8

Je waumini wanapaswa kuweka akili zao juu ya nini?

Waumini wanapaswa kuweka akili zao juu ya kazi nzuri ambazo Mungu ameziweka mbele yao ili wazifanye.

Titus 3:9-13

Waumini wanapaswa kuepuka nini?

Waumini wanapaswa kuepuka mijadala ya kipumbavu.

Ni nani anapaswa kukataliwa baada ya onyo moja au maonyo mawili?

Mtu yeyote anayesababisha matengano miongoni mwa waumini lazima akataliwe baada ya kuwa ameonywa mara moja au mara mbili.

Titus 3:14-15

Je waumini wanalazimika kushiriki katika jambo gani ili waweze kuzaa matunda?

Waumini wanalazimika kujifunza kushiriki wenyewe katika kufanya kazi nzuri ambazo zinagusa mahitaji ya muhimu.