Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Philemon

Philemon 1

Philemon 1:1-3

Paulo alikuwa wapi alipokuwa akiandika barua hii?

Alipokuwa akiandika barua hii Paulo alikuwa kifungoni.

Nani aliandikiwa barua hii ?

arua hii aliandikiwa Filemoni, ndugu mpendwa wake Paulo na mtenda kazi mwenzake.

Ni mahali gani Wakristo walikutana kama kanisa?

Kanisa lilikutana nyumbani.

Philemon 1:4-7

Ni tabia zipi nzuri za Filemoni ambazo Paulo alizisikia?

Paulo alisikia juu ya upendo, Imani kwa Bwana na uaminifu kwa watakatifu wote alivyokuwa navyo Filemoni.

Kwa mujibu wa Paulo, Filemoni aliwafanyia nini watakatifu?

Filemoni amekuwa akiburudisha mioyo ya watakatifu.

Philemon 1:8-9

Paulo alikuwa wapi wakati anaandika barua yake?

Paulo alikuwa gerezani wakati anaandika barua yake.

Kwa nini Paulo anamuomba jambo Filemoni badala ya kumuamuru?

Paulo anamuomba Filemoni jambo kwa sababu ya upendo.

Philemon 1:10-13

Wakati gani Paulo alimzaa Onesmo?

Paulo alimzaa Onesmo wakati akiwa kifungoni.

Paulo alimfanya nini Onesmo?

Paulo alimrudisha Onesmo kwa Filemoni.

Paulo alikuwa wapi wakati anaandika barua yake?

Paulo alikuwa gerezani wakati anaandika barua yake.

Paulo alitamani Onesmo afanye nini?

Paulo alitamani Onesmo amsaidie.

Philemon 1:14-16

Paulo alitaka Filemoni amfanyie nini Onesmo?

Paulo alitaka Filemoni asimfanye Onesmo kama mtumwa na akakubali kumrudisha Onesmo.

Paulo sasa anataka Filemoni amchukulie vipi Onesmo?

Paulo anataka Filemoni amchukulie Onesmo kama ndugu apendwaye.

Philemon 1:17-20

Paulo anataka Filemoni afanye nini kuhusu chochote ambacho Filemoni anamdai Onesmo?

Paulo anataka Filemoni abadilishe madai yote ya Onesmo yawe ya Paulo.

Paulo anamdai nini Filemoni?

Paulo anamdai Filemoni maisha yake.

Philemon 1:21-25

Je, Paulo alikuwa anategemea kuwa Filemon atamtuma Onesmo arudi?

Naam, Paulo alikuwa na ujasiri ya kwamba Filemoni atamtuma Onesmo amrudie.

Paulo ataenda wapi mara baada ya kuachiwa toka gerezani?

Paulo ataenda kumsalimia Filemoni baada ya kuachiwa toka gerezani.