Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Proverbs

Proverbs 1

Proverbs 1:1-3

Ni nani alikuwa mwandishi wa mithali hizi?

Sulemani, mfalme wa Israeli, alikuwa mwandishi wa mithali hizi.

Mithali hizi zinawafundisha watu kuishi namna gani?

Mithali hizi zinawafundisha watu kuishi kwa kutenda haki, adili na usawa.

Proverbs 1:4-6

Wenye busara watapokea nini kwa kusikiliza mithali hizi?

Wenye busara wanaweza kuongeza ufahamu wao kwa kusikiliza mithali hizi.

Proverbs 1:7-9

Mwanzo wa maarifa ni nini?

Hofu ya Mungu ni chanzo cha maarifa.

Mwana anapaswa kusikiliza maelekezo ya nani?

Mwana anapaswa kusikiliza maelekezo kutoka kwa baba na mama yake.

Proverbs 1:10-11

Mwana anapaswa kufanya nini kama wenye dhambi watamshawishi?

Mwana anapaswa kukataa kuwafuata ambao wanajaribu kumshawishi kwenye dhambi.

Proverbs 1:12-14

Wale wanaotenda dhambi wanampango wa kujaza nyumba zao kwa kitu gani?

Wale wanaotenda dhambi wanampango wa kujaza nyumba zao kwa vitu waliovyowaibia wengine.

Proverbs 1:15-17

Wale wanaotenda dhambi wanaharakisha kufanya nini?

Wale wanaotenda dhambi wanaharakisha kumwaga damu.

Proverbs 1:18-19

Mapato ya udhalimu hufanya nini kwa wale wenye kushikamana nayo?

Mapato ya udhalimu huondoa uhai wa wale wanaoshikamana nayo.

Proverbs 1:20-22

Ni nani anayelia kwa sauti kwenye mitaa, sehemu za wazi na kwenye malango ya mji?

Hekima analia kwa sauti kwenye mitaa, sehemu za wazi na kwenye malango ya mji.

Proverbs 1:23-25

Wale waliopungukiwa hekima walifanya nini hekima alipowaita?

Wale waliopungukiwa hekima walikataa kusikiliza wala hawakujali wakati hekima alipowaita.

Proverbs 1:26-27

Hekima atafanya nini wakati wa msiba kwa wale waliopungukiwa hekima?

Hekima atacheka wakati wa msiba kwa wale waliopungukiwa hekima.

Proverbs 1:28-30

Hekima atafanya nini watakapomwita wenye kupungukiwa hekima?

Hekima hatajibu watakapomwita wale ambao wamepungukiwa hekima.

Proverbs 1:31-33

Wale ambao wamepungukiwa hekima watajazwa nini?

Wale ambao wamepungukiwa hekima watajazwa kwa matunda ya njama zao.

Wataishi namna gani wale ambao wanamsikiliza hekima?

Wale ambao wanamsikiliza hekima wataishi katika usalama.

Proverbs 2

Proverbs 2:1-2

Hekima anataka mwanae aweke akiba ya nini?

Hekima anataka mwanae kuweka akiba ya amri zake.

Proverbs 2:3-5

kwa namna gani mwana anapaswa kutafuta na kutafiti kwa ajili ya ufahamu?

Mwana anapaswa kutafuta ufahamu kam fedha na kuutafiti kama hazina iliyositirika.

Nini kitatokea kama mwana atatafuta na kutafiti kwa ajili ya ufahamu?

Mwana atapata maari ya Mungu.

Proverbs 2:6-8

Yahwe ni nani kwa wale wanaotembea katika uaminifu?

Yahwe ni ngao kwa wale ambao hutembea katika uaminifu.

Proverbs 2:9-10

Hekima anapokuja ndani ya moyo wa mwana, atafahamu kitu gani?

Mwana atafahamu uadilifu, haki, usawa na kila mapito mazuri.

Proverbs 2:11-13

Busara na ufahamu vitamwokoa mwana kutoka kwenye nini?

Busara na ufahamu vitamwokoa mwana kutoka kwenye njia ya uovu na kutoka kwa wale ambao hutembea katika njia za giza.

Proverbs 2:14-15

Wale ambao hutembea katika njia za giza huzificha nyayo zao kwa namna gani?

Wale ambao hutembea katika njia za giza huzificha nyayo zao kwa kutumia udanganyifu.

Proverbs 2:16-17

Ni nini ambacho mwanamke malaya huacha na kusahau?

Mwanamke malaya humwacha mwenzi wa ujana wake, na husahau agano la Mungu wake.

Proverbs 2:18-19

Mapito ya mwanamke malaya huelekea wapi?

Mapito ya mwanamke malaya huelekea kwa wale walioko kwenye kaburi.

Proverbs 2:20-22

Mwana anapaswa kutembea katika njia za nani?

Mwana anapaswa kutembea katika njia ya watu wema na wenye kutenda haki.

Kutatokea nini kwa wale watendao haki?

Wale watendao haki watajenga nyumba zao katika nchi

Kutatokea nini kwa wale ambao ni waovu?

Kwa wale ambao ni waovu wataondolewa katika nchi.

Proverbs 3

Proverbs 3:1-2

Amri na mafundisho ya Hekima yataongeza nini kwa mwanae?

Amri na mafundidho ya Hekima yataongeza miaka ya uzima na amani kwa mwanae.

Proverbs 3:3-4

Uaminifu wa kiagano na udhamini unapaswa kuandikwa wapi?

Uaminifu wa kigano na udhamini unadpaswa kuandikwa juu ya kibao cha moyo.

Proverbs 3:5-6

Mwana hapaswi kuegemea juu ya nini?

Mwana hapaswi kuegemea juu ya (kutegemea) ufahamu wake mwenyewe.

Proverbs 3:7-8

Mwana hapaswi kujiona kwa namna gani?

Mwana hapaswi kujiona kama ni mwenye busara.

Proverbs 3:9-10

Mwana anapaswa kufanya nini kwa utajiri wake?

Mwana anapaswa kumheshimu Mungu kwa utajiri wake.

Proverbs 3:11-12

Yahwe humwdibisha nani?

Yahwe huwaadibisha wale ambao anawapenda.

Proverbs 3:13-16

Hikima ni bora kuliko nini?

Hekima ni bora kuliko fedha na dhahabu.

Proverbs 3:17-18

Mapito yote ya hekima ni nini?

Mapito yote ya hekima ni amani.

Proverbs 3:19-20

Yahwe alifanya nini kwa hekima?

Kwa hekima, Yahwe aliiumba dunia.

Proverbs 3:21-22

Ni nini kitakuwa uzima kwenye moyo wa mwana?

hukumu ya kweli na ufahamu vitakuwa uzima kwenye moyo wa mwana.

Proverbs 3:23-24

Kama mwana atatembea katika hekima, nini kitatokea wakati wa kulala?

Wakati anapolala, hataogopa na usingizi wake utakuwa mtamu.

Proverbs 3:25-26

Mwana hapaswi kuogopa nini?

Mwana hapaswi kuogopa hofu ya ghafla au uhalibifu.

Proverbs 3:27-28

Mwana anapaswa kufanya nini kwa wale wanaostahili?

Mwana anapaswa kutozuia wema kwa wale ambao wanastahili.

Proverbs 3:29-30

Mwana hapaswi kufanya nini kwa jirani yake?

Mwana hapaswi kufanya mpango wa kumuumiza jirani yake.

Proverbs 3:31-32

Ni nani ambaye ni mwovu kwa Yehwe?

Mtu mwenye kudanganya ni mwovu kwa Yahwe.

Proverbs 3:33-34

Mungu hufanya nini kwa wenye dhihaka?

Mungu huwadhihaki wenye dhihaka.

Proverbs 3:35

Mwenye busara watarithi nini?

Wenye busara hurithi heshima

Proverbs 4

Proverbs 4:1-2

Wana hawapaswi kusahau kitu gani?

Wana hawapaswi kusahau mafundisho ya baba zao.

Proverbs 4:3-4

Baba alimwambia mwana aishi namna gani?

Baba alimwambia mwana aishi kwa kufuata amri za baba.

Proverbs 4:5-6

Hekima atafanya nini kwa mwana ikiwa mwana atampenda na wala asimwache?

Hekima atamlinda na kumhufadhi salama.

Proverbs 4:7-9

Hekima atafanya nini kwa mwana ikiwa mwana atamfurahia na kumkumbatia?

Hekima atamwinua, atamheshimu, atamvika kilemba kichwani, na kumpatia taji zuri.

Proverbs 4:10-12

Chini ya njia ya namna gani baba humwogoza mwana?

Baba humwongoza mwana chini ya njia nyoofu.

Proverbs 4:13-15

Mwana ni lazima ashikilie nini, kwa maana ni uzima wake?

Mwana lazima ashilie mafundisho, kwa maana ni uzima wake.

Mwana ni lazima ajiepushe na njia gani?

Mwana lazima ajiepushe katika njia ya waovu.

Proverbs 4:16-17

Waovu lazima wafanye nini kabla ya kulala?

Waovu lazima wafanye ubaya kabla ya kulala

Proverbs 4:18-21

Njia ya mwenye haki ikoje?

Njia ya wenye haki ni kama mwanga wa awali ambao hung'aa sana.

Proverbs 4:22-23

Kwa nini mwana ni lazima aulinde moyo wake kwa uangalifu wote?

mwana ni lazima aulinde moyo wake kwa uangalifu wote kwa maana ndani yake hububujika uzima.

Proverbs 4:24-27

Ni maongezi na hotuba ya namna gani mwana lazima ajitenge mbali nayo?

Mwana lazima ajitenge mbali hotuba yenye mdanganyifu na maongezi mabaya.

Proverbs 5

Proverbs 5:1-2

Mwana atajifunza nini kama atasikiliza maarifa kwa umakini?

Mwana atajifunza kuhusu busara kama anasikiliza maarifa kwa makini.

Proverbs 5:3-4

Malaya huwa kama nini mwishoni?

Mwishoni malaya huwa ni mchungu kama pakanga.

Proverbs 5:5-6

Miguu ya malaya huelekea wapi?

Miguu ya malaya huelekea kwenye mauti, njia yake yote huelekea kuzimu.

Proverbs 5:7-8

Wana wanapaswa kufuata njia gani mintarafu ya malaya na nyumba yake?

Wana wenye busara wanapaswa kufuata njia iliyombali kutoka kwa malaya na isiyokaribu na nyumba yake.

Proverbs 5:9-10

Wana watapoteza nini kama watajihusisha na malaya?

Kama watajihusisha na malaya, wana watapoteza heshima yao na miaka ya uzima wao.

Proverbs 5:11-14

Mwisho ya maisha yao kutakuwaje kama wana watajihusisha na malaya?

Kama watajihusisha na malaya nyama yao na mwili wao utaangamia.

Ni majuto gani wana watayasema mwishoni mwa maisha yao kama watajihusisha na malaya?

Kama watajihusisha na malaya mwishoni mwa maisha yao watasema kwamba wanajuta kukosa maarifa na kuyakataa masahihisho

Proverbs 5:15-17

Wana anapaswa wanywe kutoka wapi?

Wana wanapaswa wanywe maji kutoka kwenye birika lao na kwenye visima vyao.

Proverbs 5:18-19

Wana wanapaswa kufurahi pamoja na nani?

Wana wanapaswa kufurahi pamoja na mke wa ujana wao.

Wana wanapaswa kutekwa na nini?

Wana wanapaswa kutekwa kwa upendo wa mke wa ujana wao.

Proverbs 5:20-21

Yahwe huona nini?

Yahwe huona kila kitu anachofanya mtu.

Proverbs 5:22-23

Mtu mwovu tekwa na kushikwa na nini?

Dhambi yake itamteka na kumshika mtu mwovu.

Proverbs 6

Proverbs 6:1-2

Jinsi gani mwana angeweza kulaza mtego kwa ajili yake mwenyewe?

Mwana angeweza kulaza mtego kwa ajili yake mwenyewe kwa kutoa ahadi ya mkopo wa mtu mwingine asiyemfahamu?

Proverbs 6:3-5

Mwana ni lazima afanye nini ili kujiokoa mwenyewe?

Kujiokoa mwenyewe mwana lazima aende kwa jirani yake na kuomba kuondolewa ahadi yake.

Proverbs 6:6-8

Mtu mvivu lazima ajifunze nini?

Mtu mvivu lazima ajifunze kuhusu chungu

Chungu hufanya nini wakati wa jua?

Wakati wa jua, chungu huandaa na kuhifadhi chakula chake.

Proverbs 6:9-11

Nini kitatokea kwa mtu mvivu ambaye hainuki kutoka kwenye usingizi wake?

Umasikini utakuja juu ya mtu mvivu ambaye hainuki kutoka kwenye usingizi wake.

Proverbs 6:12-13

Mtu mwovu huishi kwa kitu gani?

Mtu mwovu huishi kwa udanganyifu wa kauli zake

Proverbs 6:14-15

kitu gani kitatokea kwa mtu mwovu kwa sababu ya njama zake za uovu?

mtu mwovu atakumbwa na msiba kwa ghafla.

Proverbs 6:16

Ni vitu vingapi Yahwe huvichukia na vitu vingapi ni chukizo kwake?

Kuna vitu sita ambavyo Yahwe huvichukia, saba ambavyo ni chukizo kwake.

Proverbs 6:17-21

Ni miguu ya namna gani Yahwe huichukia?

Yahwe huchukia miguu ambayo hukimbila uovu kwa haraka.

Ni shahidi wa namna gani ambaye Yahwe humchukia?

Yahwe humchukia shahidi ambaye huongea uongo.

Proverbs 6:22-25

Amri na mafundisho ni kama nini?

Amri ni kama taa na mafundisho ni kama mwanga.

Proverbs 6:26-29

Kulala na mke wa mtu mwingine kunaweza kugharimu nini kwa mwana?

Kulala na mke wa mtu mwingine kunaweza kugharimu uzima wa mwana.

Proverbs 6:30-31

Kwa nini watu wasimdharau mwizi kama akiiba?

watu wasimdharau mwizi kama akiiba ili kutimiza hitaji lake wakati akiwa na njaa.

Proverbs 6:32-33

Mtu anayefanya uasherati humharibu nani?

Mtu anayefanya uasherati hujiharibu mwenyewe

Proverbs 6:34-35

Hatakubali nini mtu mwenye kulipa kisasi dhidi ya mzinzi?

mtu mwenye kulipa kisasi dhidi ya mzinzi hatakubali fidia

Proverbs 7

Proverbs 7:1-3

Mwana ni lazima atunze na kuhifadhi nini ili kuishi?

Mwana ni lazima atunze na kuhifadhi amri za baba yake na mafundisho.

Proverbs 7:4-5

Hekima na maarifa yanamlinda mwana kutoka kwa nani?

Hekima na maarifa yanamlinda mwana dhidi ya mwanamke mshawishi.

Proverbs 7:6-9

Sulemani aliona nini alipoangalia dirishani?

Sulemani aliona vijana wengi wakiume wasiofundishwa na kati yao alikuwepo kijana aliyekuwa hana akili.

Proverbs 7:10-12

Jinsi gani mwanamke alivaa ambaye kijana alikutana naye?

Mwanamke alivaa kama kahaba

Mwanamke hufanya nini kwenye kila kona?

Mwanamke huvizia katika kila kona.

Proverbs 7:13-15

Mwanamke alikuwa amefanya nini mapema katika siku?

Mapema katika siku, mwanamke alikuwa ametoa sadaka yake ya amani.

Mwanamke amekuwa akitafuta nini kwa bidii?

Mwanamke amekuwa akitafuta uso wa kijana wa kiume kwa bidii.

Proverbs 7:16-18

Mwanamke anamkaribisha kijna wa kiume kufanya nini?

Mwanamke anamkaribisha kijana wa kiume kwenda naye kwenye kutanda chake hadi asubuhi.

Proverbs 7:19-21

Mume wa mwanamke yupo wapi

Mume wa mwanamke yupo kwenye safari ya mbali.

Proverbs 7:22-23

Kijana wa kiume anatembea kwa njia ya namna gani kumfuata huyo mwanamke.

Kijana wa kiume anatembea kumfuata huyo mwanamke kama ng'ombe anayeelekea machinjioni au kama swala aliyenaswa kwenye mtego.

Kijana wa kiume matendo yake yatamgaharimu nini?

Kijana wa kiume matendo yake yatagharimu uzima wake.

Proverbs 7:24-25

Ni maelekezo gani ya busara kijana wa kiume amepewa kuhusu mwanamke?

Kijana wa kiume amelekezwa kwa busara asipotee kuelekea katika njia ya huyo mwanamke.

Proverbs 7:26-27

Nyumba ya mwanamke ipo katika njia gani?

Nyumba ya mwanamke ipo katika njia iendayo kuzimu

Proverbs 8

Proverbs 8:1-3

Ni nani ayeita karibu na lango la mji?

Hekima anaita karibu na lango la kuingilia kwenye mji.

Proverbs 8:4-5

Hekima anamwita nani?

Hekima anawaita watoto wa wanadamu.

Proverbs 8:6-9

Hekima huongea vitu vya namna gani?

Hekima huongea vitu vya adili na vya kuaminiwa.

Proverbs 8:10-11

Hekima inathamani kuliko nini?

Hekima inathamani kuliko marijani.

Proverbs 8:12-13

Wale wenye hofu ya Yahwe huchukia nini?

Wale wenye hofu ya Yahwe huchukia uovu, kiburi, majivuno na maneno ya kupotosha.

Proverbs 8:14-18

Jinsi gani wafalme na wakuu wenye hekima hutawala?

Wafalme na wakuu wenye hekima hutawala kwa haki.

Proverbs 8:19-21

Tunda la hekima ni bora kuliko nini?

Tunda la hekima ni bora kuliko dhahabu na fedha.

Hekima atawapa nini wanaompenda?

Hekima atawapa atotoa urithi kwa wale wanaompenda.

Proverbs 8:22-25

Hekima iliwekwa lini?

Hekima iliwekwa enzi za kale, tokea mwanzo.

Proverbs 8:26-29

Hekima alikuwa wapi Yahwe alipoumba dunia na mbingu?

Hekima alikuwepo pale wakati Yahwe alipoiumba dunia na mbingu.

Proverbs 8:30-34

Hekima alikuwa akifanya nini pamoja na Yahwe wakati Yahwe alipokuwa akiumba kila kitu.

Hekima alikuwa karibu na Yahwe kama fundi stadi mkuu wakati Yahwe alipoumba kila kitu.

Furaha ya Hekima ilikuwa kwenye nini?

Furaha ya Hekima ilikuwa kwa wanadamu

Proverbs 8:35-36

Mtu anayepata Hekima hupata nini pia?

Mtu anayepata Hekima pia hupata uzima na kibali cha Yahwe.

Mtu anayeshindwa kupata Hekima hupata nini pia?

Mtu anayeshindwa kupata Hekima pia hupata mauti.

Proverbs 9

Proverbs 9:1-2

Hekima amejenga nini?

Hekima amejenga nyumba yake mwenyewe.

Proverbs 9:3-4

Ukaribisho anaotuma Hekima unaelekezwa kwa nani?

Ukaribisho anaotuma Hekima unaelekezwa kwa wale wasiofunzwa, wale wasio na akili.

Proverbs 9:5-6

Hekima anasema wasiofunzwa wanapaswa kuacha nini?

Hekima anasema wasiofunzwa wanapaswa kuacha njia zao za kijinga.

Proverbs 9:7-9

Hutokea nini kwa mtu ambaye humkemea mwenye dhihaka?

Mtu anayemkemea mwenye dhihaka hukaribisha matusi na ataumizwa na kuchukiwa.

Hutokea nini kwa mtu amfundishaye mtu mwenye busara?

Mtu amfundishaye mtu mwenye busara hupendwa.

Proverbs 9:10-12

Chanzo cha hekima ni nini?

Hofu ya Yahwe ni mwanzo wa hekima

Ufahamu ni nini?

Maarifa ya Mtakatifu ni ufahamu.

Proverbs 9:13-15

Sifa za mwanamke mpumbavu ni zipi?

Mwanamke mpumbavu ni kupiga kelele, hakufunzwa, na hajui lolote.

Proverbs 9:16-18

Vitu vya wizi na vya siri vitakuwa vya namna gani mwanzoni kwa mtu anayevipata?

Vitu vya wizi na vya siri mwanzoni vinaweza kuwa vitamu na kufurahisha kwa mtu anayevipata.

Akina nani wapo katika nyumba ya mwanamke mpumbavu?

Wafu katika kina cha kuzimu wapo kwenye nyumba ya mwanamke.

Proverbs 10

Proverbs 10:1-3

Baba anahisia za jinsi gani kwa mtoto mwenye busara?

Mtoto mwenye busara humfurahisha baba yake.

Yahwe huifanya nini shauku ya waovu?

Yahwe huiharibu shauku ya waovu.

Proverbs 10:4-5

Matokeo ya mkono mlegevu ni nini?

Mkono mlegevu husababisha mtu kuwa masikini

Proverbs 10:6-7

Wale watendao haki hupokea nini kutoka kwa Mungu?

Wale watendao haki hupokea zawadi kutoka kwa Mungu.

Proverbs 10:8-11

Nini kitatokea kwa mpumbavu mwenye kuongea sana?

Mpumbavu mwenye kuongea sana ataharibikiwa

Proverbs 10:12-15

Upendo hufunika nini?

Upendo hufunika makosa yote.

Nini hupatikana kwenye midomo ya mtu wa ufahamu?

Hekima hupatikana kwenye midomo ya mtu wa ufahamu.

Proverbs 10:16-17

Hutokea nini kwa mtu anayekataa maonyo?

Mtu anayekataa maonyo huongozwa katika upotevu.

Proverbs 10:18-21

Kitu gani hakipungui wakati kukiwa na maneno mengi?

Dhambi haikosi ambapo kuna maneno mengi.

Proverbs 10:22-23

Thawabu nzuri ya Yahwe huleta nini?

Thawabu nzuri ya Yahwe hulta utajiri.

Proverbs 10:24-25

Waovu wapo kama nini?

Waovu wapo kama dhoruba ambayo hupita upesi na haipo tena.

Proverbs 10:26-27

Ni nini kinafanana na moshi kwenye macho?

Mtu mvivu ni kama moshi kwenye macho kwa mwenye kumtuma.

Miaka ya waovu itakuwaje?

Miaka ya waovu itakuwa mifupi.

Proverbs 10:28-30

Njia ya Yahwe humlinda nani?

Njia ya Yahwe huwalinda mwenye uadilifu.

Proverbs 10:31-32

Hutoka nini kwenye mdomo wa watenda haki?

Kwenye mdomo wa watenda haki hutoka tunda la hekima

Proverbs 11

Proverbs 11:1-2

Hutangulia nini kabla ya aibu?

Majivuni hutangulia kabla ya aibu.

Proverbs 11:3-4

Ni nini chenye thamani kwenye siku ya ghadhabu?

Kutenda haki kunathamani siku ya ghadhabu.

Proverbs 11:5-6

Nini huwanasa waovu?

Waovu hunaswa kwa tamaa zao wenyewe.

Proverbs 11:7-8

Nini humlinda mtu kutoka kwenye taabu?

Kutenda haki humlinda mtu mbali na taabu.

Proverbs 11:9-11

Jinsi gani mtu kafiri humharibu jirani yake?

Mtu kafiri humharibu jirani yake kwa kinywa chake.

Proverbs 11:12-14

Mtu mwaminifu hufanya nini badala kudharau?

Mtu mwaminifu hulitunza jambo kwa siri badala kudharau?

Proverbs 11:15-16

Mtu hapaswi kufanya nini kwa mgeni kwa sababu itamletea madhara yeye mwenyewe?

Mtu hapaswi kuweka dhamana ya mkopo kwa mgeni.

Proverbs 11:17-18

Jinsi gani mtu mwovu hupata mshahara wake?

Mtu mwovu huvizia ili kupata mshahara wake

Proverbs 11:19-20

Yahwe humfurahia nani?

Yahwe huwafurahia wale ambao njia zao ni kamilifu.

Proverbs 11:21-22

Kwa lipi kila mmoja anaweza kuwa na uhakika?

Kila mmoja anaweza kuwa na uhakika kuwa waovu hawatakosa adhabu.

Proverbs 11:23-24

Hutokea nini kwa mtu apandaye mbegu?

Mtu apandaye mbegu atakusanya kingi zaidi.

Proverbs 11:25-26

Mtu anayewapa maji wengine hupokea nini?

Mtu awapaye maji wengine hupokea maji kwa ajili yake mwenyewe.

Proverbs 11:27-29

Hutokea nini kwa mtu anayetegea utajiri wake?

Mtu anayetegemea utajiri wake ataanguka.

Proverbs 11:30-31

Akina nani ni kama mti wa uzima?

Wale watendao haki ni kama mti wa uzima.

Akina nani watapokea wanachositahili?

Wale watendao haki, na waovu kabisa, na watenda dhambi watapokea wanachositahili.

Proverbs 12

Proverbs 12:1-2

Mtu mpumbavu anachukia nini?

Mtu mpumbavu huchukia mafundisho.

Proverbs 12:3-4

Taji ya mume ni nini?

Mke mwema ni taji ya mume.

Proverbs 12:5-6

Waovu hutoa ushauri wa aina gani?

Waovu hutoa ushauri wa udanganyifu

Proverbs 12:7-8

Hutoke nini kwenye nyumba za wenye haki?

Nyumba za mwenye haki zitasimama

Proverbs 12:9-12

Ni nani anayejali mahitaji ya wanyama wake?

Yeye atendaye haki hujali mahitaji ya wanya wake.

Proverbs 12:13-14

Nini humnasa mtu mwovu?

Mtu mwovu hunaswa kwa uovu wa mongezi yake.

Proverbs 12:15-16

Njia ya mpumbavu ikoje machoni pake?

Njia ya mpumbavu ni sawa machoni pake.

Proverbs 12:17-18

Maneno yaliyosemwa kwa haraka ni kama nini?

Maneno yaliyosemwa kwa haraka ni kama makali ya upanga

Proverbs 12:19-20

Ni nini kipo katika mioyo ya wenye kupanga kutenda maovu?

Ulaghai upo kwenye mioyo ya wale wenye kupanga kutenda uovu.

Proverbs 12:21-22

Yahwe anachukia nini?

Yahwe anachukia midomo inayodanganya.

Proverbs 12:23-24

Ni nini kitawatawala wavivu?

Wavivu watatawaliwa kwa kazi za kulazimishwa.

Proverbs 12:25-26

Njia ya waovu huwaongoza kwenda wapi?

Njia ya waovu huwaongoza kwenye upotevu.

Proverbs 12:27-28

Wanaotembe katika njia ya haki hupata nini?

Wale wanaotembea katika njia ya haki hupata uzima

Proverbs 13

Proverbs 13:1-2

Mwana mwenye busara husikia nini?

Mwana mwenye busara husikia mafundisho ya baba yake.

Proverbs 13:3-6

Mtu huyandaje maisha yake?

Mtu huyalinda maisha yake kwa kulinda kinywa chake.

Nani hutamani wala asipate kitu?

Mvivu hutamani, lakini hapati kitu.

Proverbs 13:7-8

Baadhi ya utajiri wa kweli ni wa namna gani?

Baadhi ya utajiri wa kweli ni kutoa kila kitu.

Mtu masikini hata pata kitisho cha aina gani?

Mtu masikini atapata kitisho cha kupokea fidia.

Proverbs 13:9-10

Kiburi huzaa nini?

Kiburi huzaa migogoro tu.

Proverbs 13:11-12

Jinsi gani utajiri hupungua?

Utajiri hupungua wakati kunapokuwa na majivuno mengi

Proverbs 13:13-14

Msingi wa uzima ni nini?

Mafundisho yenye busara ni msingi wa uzima.

Proverbs 13:15-16

Kutoka kwenye nini mwenye busara hufanya kila uamuzi?

Mwenye busara hufanya kila maamuzi kutoka katika maarifa.

Proverbs 13:17-18

Nini kitamjia yeye ajifunzaye kutoka katika masahihisho?

Heshima itakuja kwake ambaye hujifunza kutokana na masahihisho.

Proverbs 13:19-20

Mtu anapaswa kutembea pamoja na nani ili kuwa na busara?

Ili kuwa na busara, mtu anapaswa kutembea pamoja na watu wenye busara.

Proverbs 13:21-22

Utajiri wa mwenye dhambi umehifadhiwa kwa ajili ya nani?

Utajiri wa mwenye dhambi umehifadhiwa kwa ajili ya yule atendaye haki.

Proverbs 13:23-24

Jinsi gani mzazi huonyesha upendo kwa mtoto wake?

Mzazi huonyesha upendo kwa mtoto wake kwa kuwa makini katika kumwadibisha.

Proverbs 13:25

Tumbo la mwovu lipo katika hali gani?

Tumbo la mwovu kila daima huwa na njaa.

Proverbs 14

Proverbs 14:1-4

Mwanamke mwenye busara hufanya nini?

Mwanamke mwenye busara huijenga nyumba yake mwenyewe.

Nani humdharau Yahwe?

Yule asiyemwaminifu katika njia zake humdharau Yahwe.

Proverbs 14:5-6

Shahidi mwaminifu huwa hafanyi nini?

Shahidi mwaminifu hasemi uongo

Proverbs 14:7-10

Kitu gani hakiwezi kupatikana katika midomo ya mtu mpumbavu?

Maarifa hayawezi kupatikana katika midomo ya mtu mpumbavu.

Proverbs 14:11-12

Kitu gani kitatokea kwenye nyumba ya mwovu?

Nyumba ya mwovu itaharibiwa

kitu gani kitatokea kwenye hema ya mwadilifu?

Hema ya mwadilifu itafanikiwa.

Proverbs 14:13-14

Mtu asiye mwaminifu atapata nini?

Mtu asiye mwaminifu atapata kile kinachositahili njia zake.

Proverbs 14:15-16

Mpumbavu akionywa hufanya nini?

Mpumbavu hupuuza onyo kwa ujasiri.

Proverbs 14:17-18

Mtu anayeharakisha kukasirika hufanya nini?

Mtu anayeharakisha kukasirika hufanya vitu vya kipumbavu.

Proverbs 14:19-20

Wabaya watainama kwa nani?

Wabaya watainama mbele ya wale ambao ni wema.

Proverbs 14:21-22

Wale ambao hukusudi kufanya mema hupokea nini?

Wale ambao hukusudi kufanya mema hupokea agano la uaminifu na mdhamana

Proverbs 14:23-25

Nini huja kwa kazi ngumu?

Kwa kazi ngumu huja faida.

Proverbs 14:26-27

Chemchemi ya uzima ni nini?

Hofu ya Mungu ni chemchemi ya uzima.

Proverbs 14:28-29

Nani hutukuza upumbavu?

Mwepesi wa hasira hutukuza upumbavu.

Proverbs 14:30-33

Nani humlaani Muumba wake kwa matendo yake?

Mtu ambaye humwonea masikini humlaani Muumba wake.

Proverbs 14:34-35

Ni nini huinua taifa?

Kutenda haki huinua taifa

Proverbs 15

Proverbs 15:1-2

Ni nini hugeuza ghadhabu?

Jibu la upole hugeuza ghadhabu.

Proverbs 15:3-4

Yahwe humwangalia nani?

Yahwe huwaangalia wema na wabaya.

Proverbs 15:5-6

Tabia ya mpumbavu ikoje kwenye mafundisho ya baba yake?

Mpumbavu anadharau kwenye mafundisho ya baba yake.

Proverbs 15:7-8

Sadaka ya aina gani Yahwe huchukia?

Yahwe huchukia sadaka ya waovu.

Proverbs 15:9-12

Nini humgoja kila mtu anayeiacha njia?

Adhabu kali humgoja kila mtu anayeiacha njia.

Proverbs 15:13-14

Nini hufanya uso uchangamke?

Moyo wenye furaha huufanya uso uchangamke.

Proverbs 15:15-16

Kitu gani ni bora kulio hazina kubwa pamoja na machafuko?

Kitu kidogo pamoja na hofu ya Yahwe ni bora kuliko hazina kubwa pamoja na machafuko.

Proverbs 15:17-18

Mtu wa namna gani hunyamazisha ugomvi?

Mtu mtaratibu kupata hasira hunyamazisha ugomvi.

Proverbs 15:19-20

Mwana mwenye busara huleta nini kwa baba yake?

Mwana mwenye busara huleta furaha kwa baba yake.

Proverbs 15:21-24

Nini husababisha mipango ifanikiwe?

Washauri wengi husababisha mipango ifanikiwe.

Proverbs 15:25-26

Yahwe hurarua nini?

Yahwe huurarua urithi wa wenye kiburi.

Proverbs 15:27-30

Mwenye haki hufanya nini kabla ya kujibu?

Mtu atendaye haki hufikiri kabla ya kujibu.

Proverbs 15:31-32

Mtu mwenye busara hufanya nini wakati anaposahihishwa?

Mtu mwenye busara husikiliza kwa makini wakati anaposahihishwa.

Proverbs 15:33

Ni nini huja kwanza kabla ya heshima?

Unyenyekevu huja kabla ya heshima.

Proverbs 16

Proverbs 16:1-2

Jinsi gani njia zote za mtu huonekana kwake mwenyewe?

Njia zote za mtu huonekana safi machoni kwake mwenyewe.

Proverbs 16:3-4

Kwa ajili ya nini Yahwe amefanya kila kitu?

Yahwe amefanya kila kitu kwa kusudi lake.

Proverbs 16:5-8

Dhambi husamehewa kwa kitu gani?

Kwa agano la uaminifu na dhamana dhambi husamehewa.

Proverbs 16:9-10

Mara mtu anapopanga njia yake, Yahwe hufanya nini?

Mara mtu anapopanga njia yake, Yahwe huziongoza hatua zake.

Proverbs 16:11-12

Jinsi gani kiti cha enzi imethibitishwa ?

Kiti cha enzi imethibitishwa kwa kutenda haki

Proverbs 16:13-14

Mjumbe wa mauti ni nini?

Ghadhabu ya mfalme ni mjumbe wa mauti

Proverbs 16:15-16

Nini kinapaswa kuchaguliwa zaidi kuliko fedha na dhahabu?

Hekima na ufahamu vinapaswa kuchaguliwa zaidi kuliko fedha na dhahabu.

Proverbs 16:17-18

Ni nini huja kabla ya anguko?

Roho ya majivuno huja kabla ya anguko.

Proverbs 16:19-22

Jinsi gani mtu anaweza kupata mema katika yale aliyofundishwa?

Mtu ambaye hutafakari ambacho amefundishwa hupata yaliyo mema.

Proverbs 16:23-24

Moyo wa mwenye hekima hufanya nini kwa ajili ya kinywa chake?

Moyo wa mwenye busara hutoa utambuzi kwenye kinywa chake.

Proverbs 16:25-26

Hata kama njia itaonekana sawa kwa mtu, inaweza kumwelekeza wapi?

Hata kama njia itaonekana sawa kwa mtu, inaweza kwenye mauti

Proverbs 16:27-28

Nini huwafarakanisha marafiki?

Uongo huwafarakanisha marafiki.

Proverbs 16:29-30

Mtu anayekonyeza kwa jicho hufanya nini?

Mtu anayekonyeza kwa jicho hupanga mambo maovu.

Proverbs 16:31-32

Taji ya utukufu ni nini?

Mvi ni taji ya utukufu.

Nani aliyeimara kuliko anayeuteka mji?

Mtu anayeutawala moyo wake ni imara kuliko ambaye huuteka mji.

Proverbs 16:33

Maamuzi ya kura yamefanyika namna gani?

Maamuzi ya kura yamefanywa ya Yahwe.

Proverbs 17

Proverbs 17:1-2

Mtumishi mwenye busara hufanya nini kwa mwana wenye mambo ya aibu?

Mtumishi mwenye busara hutawla juu ya mwana mwenye aibu.

Proverbs 17:3-4

Mwongo humsikiliza nani?

Mwongo huwasikiliza wale ambao husema mambo mabaya.

Proverbs 17:5-6

Hutokea nini kwa wale ambao hufurahia wakati wa msiba?

Wale ambao hufurahia wakati wa msiba hataacha kupata adhabu.

Proverbs 17:7-8

Jinsi gani rushwa ni kama jiwe la kiinimacho?

Rushwa ni kama jiwe la kiinimacho kwa sababu mtu anayetoa rushwa hufanikia kila ageukapo.

Proverbs 17:9-10

Hata kitu gani hushindwa kabisa kumgeza mpumbavu?

Hata mapigo mia hushindwa kabisa kumgeuza mpumbavu.

Proverbs 17:11-12

Nini ni kibaya kabisa kuliko kukutana na dubu aliyeibiwa watoto wake?

Kukutana na mpumbavu katika upumbavu wake ni mbaya mno kuliko kukutana na dubu aliyeibiwa watoto wake.

Proverbs 17:13-14

Mtu anapaswa kufanya nini kabla ya kutokea mabishano?

Mtu anapaswa kuondoka kabla ya mabishano hayajatokea.

Proverbs 17:15-16

Aina gani ya watu ni waovu kwa Yahwe?

Mtu ambaye huwaacha waovu au huwalaumu wale ambao hutenda haki ni mwovu kwa Yahwe.

Proverbs 17:17-18

Mtu asiye na akili hufanya nini?

Mtu asiye na akili huweka agano kwa ajili ya deni la jirani yake.

Proverbs 17:19-20

Ninia humsababisha mtu kuangukia kwenye msiba?

Ulimi wa uovu humsababisha mtu kuangukia kwenye msiba.

Proverbs 17:21-24

Dawa njema ni nini?

Moyo mchangamfu ni dawa njema

Proverbs 17:25-26

Mwana mpumbavu ni nini kwa baba na mama yake?

Mwana mpumbavu ni huzuni kwa baba yake na uchungu kwa mama yake.

Proverbs 17:27-28

Jinsi gani mpumbavu anaweza kudhaniwa ni mwenye busara?

Mpumbavu anaweza kudhaniwa ni mwenye busara kama anaponyamaza.

Proverbs 18

Proverbs 18:1-2

Mpumbavu hapati furaha katika jambo gani?

Mpumbavu hapati furaha katika ufahamu.

Proverbs 18:3-4

Nini huja pamoja na mtu mwovu?

dharau, aibu, na lawama huja pamoja na mtu mwovu.

Proverbs 18:5-6

Midomo ya mpumbavu humletea nini?

Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi.

Proverbs 18:7-8

Kitu gani ni kama chembe tamu?

Maneno ya umbeya ni kama chembe tamu.

Proverbs 18:9-10

Mnara imara ni nini?

Jina la Yahwe ni mnara imara

Proverbs 18:11-12

Tabia ya mtu ikoje kabla ya anguko lake?

Kabla ya anguko, moyo wa mtu hujivuna.

Proverbs 18:13-16

Kitu gani ni kigumu sana kustahimili?

Moyo uliovunjika ni kitu kigumu sana kustahimili.

Proverbs 18:17-18

Nani huonekana yupo sawa mwanzoni?

Wa kwanza kutetea kesi yake huonekana sawa.

Proverbs 18:19-20

Kitu gani ni vigumu zaidi kushinda kuliko mji imara?

Ndugu aliyechukizwa ni vigumu zaidi kumshawishi kuliko mji imara.

Proverbs 18:21-22

Kuna nini katika nguvu ya ulimi?

katika nguvu ya ulimi kuna mauti na uzima.

Proverbs 18:23-24

Jinsi gani mtu tajiri huwajibu wengine?

Mtu tajiri huwajibu wengine kwa ukali.

Proverbs 19

Proverbs 19:1-4

Mtu lazima awe na nyongeza ya nini kwenye shauku?

Mtu lazima awe na nyongeza ya maarifa kwenye shauku.

Proverbs 19:5-6

Kitatokea nini kwa mtu ambaye ni shahidi wa uongo?

Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa.

Proverbs 19:7-10

Hutokea nini wakati mtu masikini anapowaita rafiki zake?

Wakati mtu masikini apowaita rafiki zake, huwa hawapo.

Mtu anayeipenda nafsi yake hufanya nini?

Mtu anayeipenda nafsi yake hupata hekima.

Proverbs 19:11-12

Mtu mwenye busara hufanya nini anapokosewa?

Mtu mwenye busara husamehe kosa.

Proverbs 19:13-16

Ni nini ambacho ni kama maji yanayovuja mfululizo?

Mke mgomvi ni kama maji yanayovuja mfululizo.

Mke mwenye busara hutoka wapi?

Mke mwenye busara hutoka kwa Yahwe.

Proverbs 19:17-18

Jinsi gani mtu humkopesha Yahwe?

Mtu ambaye ni mkarimu kwa masikini humkopesha Yahwe.

Proverbs 19:19-22

Nani ataokolewa mara mbili?

Mtu mwenye hasira kali ataokolewa mara mbili.

Jinsi gani mtu anaweza kuwa mwenye busara mwishoni mwa maisha yake?

mtu anaweza kuwa mwenye busara mwishoni mwa maisha yake kwa kusikiliza ushauri na kukubali mafundisho.

Proverbs 19:23-25

Ni nini huwaongoza watu kwenye uzima?

Kumheshimu Yahwe huwaongoza watu kwenye uzima.

Mtu mvivu hawezi kufanya nini?

Mtu mvivu hawezi hata kuuleta juu mkono wake kutoka kwenye sahani kwenda mdomono mwake.

Proverbs 19:26-27

Mtoto anayemwibia baba yake na kumfukuza mama yake huleta nini?

Mtoto anayemwibia baba yake na kumfukuza mama huleta aibu na shutuma.

Proverbs 19:28-29

Ni nini huifanya haki kuwa dhihaka?

Shahidi anayepotosha huifanya haki kuwa dhihaka.

Proverbs 20

Proverbs 20:1-2

Hutokea nini kwa mtu anayemkasirisha mfalme?

Mtu anayemkasirisha mfalme huyapoteza maisha yake.

Proverbs 20:3-4

Kila mpumbavu hurukia kwenye nini?

Kila mpumbavu hurukia kwenye mabishano.

Proverbs 20:5-8

Ni vigumu kumpata mtu wa aina gani?

Mtu mwaminifu ni vigumu kumpata.

Proverbs 20:9-10

Ni kitu gani mtu yeyote hawezi kusema juu yake mwenyewe?

Mtu yeyote hawezi kusema juu yake mwenyewe kuwa "nimeuweka safi moyo wangu; Sina dhambi."

Proverbs 20:11-12

Kwa jambo gani hata kijana hujulikana?

Hata kijana hujulikana kwa matendo yake.

Proverbs 20:13-14

Kupenda nini kunamleta mtu kwenye umasikini?

Kupenda usingizi humleta mtu kwenye umasikini.

Proverbs 20:15-16

Ni nini huwa kama marijani ya thamani?

Midomo yenye maarifa ni kama marijani yenye thamani.

Proverbs 20:17-18

Mkate uliopatikana kwa uongo baadaye huwa na radha kama ya nini?

Mkate uliopatikana kwa uongo baadaye huwa na radha kama ya kokoto.

Proverbs 20:19-20

Hutokea nini kwa mtu ambaye humlaani baba yake au mama yake?

Mtu ambaye humlaani baba yake au mama yake taa yake itazimishwa.

Proverbs 20:21-24

Badala ya kujaribu kumlipa mtu kwa ajili ya kosa , mtu anapaswa kufanya nini?

Badala ya kujaribu kumlipa mtu kwa ajili ya kosa , mtu anapaswa kumsubiri Yahwe amsaidie.

Proverbs 20:25-26

Ni mtego kufanya nini kwa haraka?

Ni mtego kufanya nadhiri kwa haraka.

Proverbs 20:27-28

Nini humhifadhi mfalme?

Uaminifu wa agano na dhamana humhifadhi mfalme.

Proverbs 20:29-30

Utukufu wa vijana ni nini?

Utukufu wa vijana ni nguvu zao.

Proverbs 21

Proverbs 21:1-2

Yahwe huongoza nini popote kama apendavyo?

Yahwe huuongoza moyo wa mfalme popote apendapo.

Proverbs 21:3-4

Nini kinakubaliwa zaidi kwa Yahwe kuliko? sadaka

Kutenda haki na adili hukubaliwa zaidi kwa Yahwe kuliko sadaka.

Proverbs 21:5-6

Hutokea nini kwa mtu anayepata utajiri kwa ulimi wa uongo?

Mtu ambaye hupata utaji kwa ulimi wa uongo hufa kwa kitanzi hicho.

Proverbs 21:7-8

Kwa nini waovu huondolewa?

Waovu huondolewa kwa kuwa wanakataa kutenda adili.

Proverbs 21:9-10

Nini hakionekani kwenye macho ya waovu?

Ukarimu hauonekani kwenye macho ya waovu

Proverbs 21:11-12

Nani hujifunza hekima wakati mwenye dhihaka anapoadhibiwa?

Asiyefunzwa hujifunza hekima wakati wenye dhihaka anapoadhibiwa.

Proverbs 21:13-14

Zawadi ya siri hukamilisha nini?

Zawadi ya siri hutuliza hasira.

Proverbs 21:15-18

Mtu anayetangatanga kutoka kwenye ufahamu hupumzika wapi?

Mtu anayetangatanga kutoka kwenye ufahamu hupumzika kwenye kusanyiko la wafu

Proverbs 21:19-20

Ni bora kuishi wapi kuliko kuishi pamoja na mke mlalamishi?

Ni bora kuishi katika jangwa kuliko kuishi pamoja na mke mlalamishi.

Proverbs 21:21-22

Mtu mweye busara anaweza kuangusha chini nini?

Mtu mweye busara anaweza kuangusha chini ngome ya mji wa shujaa.

Proverbs 21:23-26

Ni nini jila la mtu wa kiburi na maringo?

Mtu wa kiburi na maringo hiitwa dhihaka.

Proverbs 21:27-29

Aina gani ya sadaka ni chukizo?

Sadaka ya mwovu ni chukizo.

Proverbs 21:30-31

Nini hakiwezi kusimama dhidi ya Yahwe?

Hakuna hekima, ufahamu au ushauri unaweza kusimama dhidi ya Yahwe?

Proverbs 22

Proverbs 22:1-2

Kitu gani masikini na tajiri wanacho?

Yahwe ni muumba wa wote masikini na tajiri.

Proverbs 22:3-4

Kwa ajili gani kuna thawabu ya utajiri, heshima na uzima?

Kwa ajili ya unyenyekevu na hofu ya Yahwe kuna thawabu ya utajiri, heshima, na uzima.

Proverbs 22:5-6

Kama mtoto amefundishwa njia ya anayopaswa kufuata, hatafanya nini hata akiwa mzee?

Kama mtoto amefundishwa njia ya anayopaswa kufuata hatayaacha mafundisho wakati akiwa mzee.

Proverbs 22:7-8

Kuna uhusiano gani kati ya yule anayekopa na yule anayekopesha?

Yule anayekopa ni mtumwa wa mtu anayemkopesha.

Proverbs 22:9-12

Ni nini kitaisha kama mwenye dhihaka atafukuzwa?

Kama mwenye dhihaka atafukuzwa ugomvi, mabishano na matusi vitaisha.

Proverbs 22:13-14

Mtu mvivu hutumia udhuru gani?

Mtu mvivu husema kuna simba mtaani kama udhuru.

Proverbs 22:15-16

Ni nini hufukuza upumbavu kutoka kwa mtoto?

Fimbo ya mafundisho hufukuza upumbavu kutoka kwa mtoto.

Proverbs 22:17-21

Mtu anapaswa kumtegemea nani?

Mtu anapaswa kumtegemea Yahwe.

Proverbs 22:22-23

Ni lazima kisifanyike kitu gani kwa masikini na wahitaji?

Masikini na wahitaji lazima wasiibiwe au kugandamizwa.

Proverbs 22:24-25

Kwa nini mtu ni lazima asifanye urafiki na mtu ambaye hutawaliwa na hasira?

Mtu ni lazima asifanye urafiki na mtu ambaye hutawaliwa na hasira kwa sababu atajifunza njia zake na kunaswa kwenye mtego.

Proverbs 22:26-27

Watu wangeweza kupoteza nini kama hawakuweza kulipa madeni yao?

Watu wangeweza kupoteza vitanda vyao kama hawakuweza kulipa madeni yao.

Proverbs 22:28-29

Ni nini hakipaswi kuondolewa?

Mpaka wa kale wenye jiwe lililowekwa na baba haupaswi kuondolewa.

Proverbs 23

Proverbs 23:1-3

Ni wakati gani mtu anapaswa kuangalia kwa makini kitu kichopo mbele yake?

Wakati mtu anapoketi kula pamoja na mtawala, anapaswa kuangalia kwa makini kile kilichopo mbele yake.

Proverbs 23:4-5

Mtu mwenye busara anajua wakati wa kuacha kufanya jambo gani?

Mtu mwenye busara anajua wakati wa kuacha kufanya kazi sana ili kupata utajiri.

Nini hutokea wakati macho ya mtu yanapotazama juu ya fedha?

Wakati macho ya mtu yanapotazama juu ya fedha huwa imeshaondoka.

Proverbs 23:6-8

Kwa nini moyo wa mtu mwovu huwa haupo pamoja na wewe anapokukaribisha kula na kunywa?

Moyo wa mtu mwovu haupo pamoja nawe kwa sababu huhesabu gharama ya chakila.

Proverbs 23:9-12

Mpumbavu huitikiaje maneno ya busara?

Mpumbavu hudharau maneno ya busara.

Ni nani atatetea kesi ya yatima?

Mteteaji wao mwenye nguvu atatetea kesi ya yatima.

Proverbs 23:13-14

Ni nini hakipaswi kuzuiliwa kwa mtoto?

Mafundisho hayapaswi kuzuiliwa kwa mtoto.

Proverbs 23:15-18

Nini hufanya uhai wa ndani sana wa baba kufurahi?

Wakati mwana anaposema haki utu wa ndani wa baba hufurahia.

Proverbs 23:19-21

Mtu hapaswi kushirikiana pamoja na nani?

Mtu hapaswi kushirikiana pamoja na walevi au walafi.

Proverbs 23:22-25

Mtu anapaswa kununua nini?

Mtu anapaswa kununua kweli, hekima, mafundisho na ufahamu.

Proverbs 23:26-28

Mwana anapaswa kutoa nini kwa baba yake?

Mwana anapaswa kutoa moyo wake kwa baba yake.

Mke wa mume mwingine huongeza nini kati ya huruma?

Mke wa mume mwingine huongeza wasaliti kati ya huruma.

Proverbs 23:29-30

Ni nani mwenye ole na mapigano?

Mtu ambaye hudumu kwenye mvinyo huwa na ole na mapigano.

Proverbs 23:31-33

Huona nini macho ya mtu anayetazama mvinyo ukiwa mwekundu?

Mtu anayetazama mvinyo ukiwa mwekundu huona mambo mageni.

Proverbs 23:34-35

Mlevi husema atafanya nini akiamka?

Mlevi husema atatafuta kinnywaji kigine anapoamka.

Proverbs 24

Proverbs 24:1-2

Mtu hapaswi kuwa na vivu kwa nani?

Mtu hapaswi kuwaonea wivu watu waovu.

Proverbs 24:3-4

Nyumba huthibitishwa kwa nini?

Nyumba huthibitishwa kwa ufahamu.

Proverbs 24:5-7

Kitu gani ni bora kuliko mtu mwenye nguvu?

Mtu mwenye maarifa ni bora kuliko mtu mwenye nguvu.

Proverbs 24:8-9

Watu humwitaje mtu ambaye hupanga kutenda uovu?

Watu humwita bwana wa fitina mtu ambaye hupanga kutenda uovu.

Proverbs 24:10

Jinsi gani nguvu za mtu huonyeshwa kuwa kidogo?

Mtu anapoonesha woga wake kwenye siku ya msiba, huonesha uchache wa nguvu zake.

Proverbs 24:11-14

Mungu hutoa nini kwa kila mtu?

Mungu humpa kila mtu anachostahili.

Proverbs 24:15-16

Waovu huvizia kufanya nini?

Waovu huvizia kushambulia nyumba ya wale watendao haki.

Proverbs 24:17-18

Yahwe atafanya nini kama mtu atafurahia wakati adui yake anapoanguka.

Yahwe ataona na hataridhia, na kugeuzia mbali ghadhabu kutoka kwa adui yake.

Proverbs 24:19-20

Nini hutokea kwenye taa ya waovu?

Taa ya waovu huzimika.

Proverbs 24:21-23

Mtu hapaswi kushirikiana pamoja na nani?

Mtu hapaswi kushirikiana pamoja na wale ambao huasi dhidi ya mfalme.

Proverbs 24:24-25

Kitatokea nini kwa mtu anayemwambia mtu mwenye hatia "wewe unahaki"?

Mtu huyo atalaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa.

Proverbs 24:26-27

Nini kinafanana na busu kwenye midomo?

Jibu la uaminifu ni kama busu kwenye midomo.

Proverbs 24:28-29

Mtu hapaswi kusema nini kwa jirani yake?

Mtu hapaswi kusema kuwa atalipiza kwa jirani yake kwa alichomtendea.

Proverbs 24:30-31

Shamba la mtu mvivu lilioneka vipi?

Kwenye shamba la mtu mvivu, miiba ilistawi, ardhi ilikuwa na upupu, na ukuta ulibomoka.

Proverbs 24:32-34

Nini humjia juu yake mtu mvivu kama mwivi?

Umasikini huja juu yake mtu mvivu kama mwivi.

Proverbs 25

Proverbs 25:1-3

Ni nani alikuwa mwandishi wa mithali hii?

Mfalme Sulemani alikuwa mwandishi wa mithali hii.

Ni utukufu wa Mungu hufanya nini?

Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo

Proverbs 25:4-6

Jinsi gani kiti cha enzi cha mfalme huthibitika?

kiti cha enzi cha mfalme huthibitika kwa kuwaondoa waovu kutoka kwenye uwepo wa mfalme.

Proverbs 25:7-12

Kitu gani ni bora kuliko kusimama kwenye sehemu iliyotengwa kwa wakuu?

Kumsubiri mfalme akuambie, "njoo huku," ni bora zaidi kuliko kusimama kwenye sehemu iliyotengwa kwa wakuu.

Kama umeshuhudia jambo kuhusu jirani yako, kwa nini hupaswi kuharakisha kupeleka kwenye mashtaka?

Hupaswi kuharakisha kupeleka kwenye mashtaka kwa sababu jirani yako anaweza kukuaibisha.

Proverbs 25:13-14

Mjumbe mwaminifu hufanya nini kwa mabwana zake?

Mjumbe mwaminifu huburudisha moyo wa mabwana zake?

Proverbs 25:15

Mtawala anaweza kushawishiwa kwa kitu gani?

Mtawala anaweza kushawishiwa kwa uvumilivu.

Proverbs 25:16-17

Jinsi gani jirani yako anaweza kukuchoka?

Jirani yako anaweza kukuchoka kama utaweka mguu wako nyumbani kwake mara nyingi.

Proverbs 25:18-20

Mguu unaoteleza ni kama nini?

Mtu asiyemwaminifu ambaye unamtumaini ni kama mguu unaoteleza.

Proverbs 25:21-28

Unapaswa kufanya nini kwa adui yako?

Adui yako unapaswa umpe chakula ale na kinywaji anywe.

Yahwe atafanya nini kwa mtu anayempa chakula na kinywaji adui yake?

Yahwe atampa thawabu mtu anayempa chakula na kinywaji adui yake.

Proverbs 26

Proverbs 26:1-2

Ni nini hakiwezi kutua juu ya mtu?

Laana isiyostahili huwa haitui juu mtu.

Proverbs 26:3-4

Mtu atakuwaje kama atajiunga katika upumbavu wa mpumbavu?

Mtu anayejiunga katika upumbavu wa mpumbavu atakuwa mpumbavu.

Proverbs 26:5-8

Ni nini kinafanana na mtu kujikata miguu wake mwenyewe?

Kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu ni kama kujikata miguu yako mwenyewe.

Proverbs 26:9-10

Mtu anayemwajiri mpumbavu ni kama nini?

Mtu anayemwajiri mpumbavu ni kama mpiga mshale ambaye humjeruhi kila mtu.

Proverbs 26:11-12

Kwa nini mpumbavu ni kama mbwa ambaye huyarudia matapishi yake mwenyewe?

Mpumbavu ni kama mbwa ambaye huyarudia matapishi yake mwenyewe kwa sababu mpumbavu hurudia upumbavu wake.

Proverbs 26:13-14

Mlango unaogeuka kwenye bawaba zake ni kama nini?

Mlango unaogeuka kwenye bawaba zake ni kama mtu mvivu juu ya kitanda chake.

Proverbs 26:15-17

Jinsi gani mtu mvivu huonekana machoni pake mwenyewe?

Mtu mvivu huonekana mwenye busara zaidi machoni pake wenyewe kuliko watu saba wenye ufahamu.

Proverbs 26:18-19

Mtu husema nini baada ya kumdanganya jirani yake?

Mtu husema, "Je sikuwa nafanya utani?" baada ya kumdanganya jirani yake.

Proverbs 26:20-23

Mtu mgomvi huchochea nini?

Mtu mgomvi huchochea mgogoro.

Proverbs 26:24-26

Jinsi gani mtu huficha ukweli kwamba anachuki kwa wenzake?

Mtu mwenye chuki kwa wenzake huificha kwa kwa ulimi wake.

Proverbs 26:27-28

Hutokea nini kwa mtu achimbaye shimo?

Mtu anayechimba shimo ataangukia humo.

Kinywa chenye kubembeleza huleta nini?

Kinywa chenye kubembeleza huleta uharibifu

Proverbs 27

Proverbs 27:1-2

Kwa nini mtu hapaswi kujisifu kwa ajili ya kesho?

mtu hapaswi kujisifu kwa ajili ya kesho kwa sababu hajui siku italeta nini.

Proverbs 27:3-4

Nini ni kizito kuliko uzito wa mchanga?

Uchokozi wa mpumbavu ni mzoto kuliko uzito wa mchanga

Proverbs 27:5-6

Adui anaweza kufanya nini ili kukudanganya?

Adui anaweza kukubusu kwa uzuri ili kukudanganya.

Proverbs 27:7-8

Kwa nani kila kitu kichungu huwa kitamu?

Kwa mtu mwenye njaa, kila kitu kichungu huwa kitamu.

Proverbs 27:9-10

Kitu gani ni bora kuliko ndugu aliyeko mbali?

Jirani ni bora kuliko ndugu ambaye yupo mbali.

Proverbs 27:11-12

Mtu mwenye busara anapoona mabaya?

Mtu mwenye busara hujificha anapoona mabaya.

Proverbs 27:13-14

Ni wakati gani baraka zinapotolewa kwa sauti kuu hudhaniwa kuwa laana?

Baraka zinapotolewa asubuhi sana kwa sauti kuu hudhaniwa kuwa laana.

Proverbs 27:15-16

Kitu gani ni kama kuzuia upepo?

Kumzuia mke mgovi ni kama kuuzuia upepo.

Proverbs 27:17-18

Kitu gani ni kama chuma kinachonoa chuma chenzake?

Mtu anayemnoa rafiki yake ni kama chuma ambacho kinanoa chuma chenzake.

Proverbs 27:19-20

Ni nini kisichotosheka kama mwenye kuharibu?

Macho ya mtu hayatosheki, kama mwenye kuharibu.

Proverbs 27:21-22

Hata kitu gani hakiwezi kuondoa upumbavu kwa mpumbavu?

Hata ukimtwanga mpumbavu upumbavu hauwezi kuondoka kwake.

Proverbs 27:23-25

Utajiri hudumu kwa muda?

Utajiri haudumu milele.

Proverbs 27:26-27

Kondoo hufanya nini kwa ajili ya familia?

Kondoo hutoa mavazi kwa ajili ya familia (kaya).

Proverbs 28

Proverbs 28:1-2

Akina nani hukimbia hata kama hakuna mtu anayewafukuza?

Waovu hukimbia hata kama hakuna mtu ambaye anawafukuza.

Proverbs 28:3-4

Watu gani husifiwa na wenye kuiasi sheria?

Waovu husifiwa na watu wenye kuiasi sharia.

Proverbs 28:5-6

Kipi ni muhimu zaidi, fedha, au uadilifu?

Uadilifu ni muhimu zaidi kuliko fedha.

Proverbs 28:7-8

Hutokea nini kwenye utajiri mtu ambaye hupata utajiri kwa kutoza riba kubwa?

Utajiri wake hupewa mtu mwingine mwenye huruma kwa masikini.

Proverbs 28:9-10

Nani ataangukia kwenye shimo lake mwenyewe?

Mtu ambaye hupotosha mwadilifu kwenye njia mbaya ataanguka kwenye shimo lake mwenyewe.

Proverbs 28:11-12

Jinsi gani watu huitikia pale waovu wanapoinuka?

Watu hujificha wenyewe wakati waovu wanapoinuka.

Proverbs 28:13-14

Jinsi gani mwenye dhambi anaweza kupokea rehema?

Mwenye dhambi ambaye huungama na kuacha dhambi zake atapokea rehema.

Proverbs 28:15-16

Jinsi gani siku z mtawala zinaweza kuongezwa?

Mtawala anaweza kuongeza siku zake kama atachukia ukaidi.

Proverbs 28:17-18

Nini kinaweza kumfanya mtu kuwa mkimbizi hadi mauti?

Kumwaga damu ya mtu kunaweza kumsababisha mtu kuwa mkimbizi hadi mauti.

Proverbs 28:19-20

Jinsi gani mtu anaweza kujipatia umasikini mwingi?

Kama mtu atafuata vishawishi vibaya, atapata umasikini mwingi.

Proverbs 28:21-24

Jinsi gani mtu wa husuda hupata utajiri?

Mtu wa husuda huharakisha kupata utajiri.

Proverbs 28:25-26

Matokeo ya kumtumaini Yahwe yakoje?

Mtu anayemtumaini Yahwe atafanikiwa.

Proverbs 28:27-28

Mtu anayeshinswa anayepoteza macho yake kwa masikini atapokea nini?

Mtu anayeshinswa anayepoteza macho yake kwa masikini atapokea laana nyingi.

Proverbs 29

Proverbs 29:1-2

Kitokea nini kwa mtu anayefanya shingo yake kuwa ngumu baada ya maonyo mengi?

Mtu anayefanya shingo yake kuwa ngumu baada ya maonyo mengi atavunjia wala hatapona.

Proverbs 29:3-4

Ni nini huharibu utajiri wa mtu?

Kuendelea kuambatana na kahaba huharibu utadjiri wa mtu.

Proverbs 29:5-6

Ni nini husababisha mtu mbaya kukamatwa kwenye mtego?

Dhambi zake mwenyewe husababisha mtu mbaya kukamatwa kwenye mtego.

Proverbs 29:7-8

Mtu wa aina gani hugeuza ghadhabu?

Mtu mwenye busara hugeuza ghadhabu.

Proverbs 29:9-10

Wenye hamu ya kumwaga damu hutafuta kumwua nani?

Wenye hamu ya kumwaga damu hutafuta kumwua mwadilifu

Proverbs 29:11-12

Mtu mwenye hekima hufanya nini katika hasira yake?

Mtu mwenye hekima huizuia hasira yake na kujituliza mwenyewe.

Proverbs 29:13-16

Jinsi gani mfalme anaweza kuthibitisha kiti chake milele?

Mfalme anaweza kuthibitisha kiti chake cha enzi milele kwa kuwahukumu kwa kweli masikini.

Proverbs 29:17-18

Matokeo ya kumfundisha mtoto ni nini?

Kumfundisha mtoto kutawapa pumziko wazazi.

Kama watu hawafuati sheria, huwa wanafanya nini?

Kama watu hawafuati sheria, hukosa mwelekeo.

Proverbs 29:19-22

Nini ni kibaya zaidi kuliko mpumbavu?

Kuwa mtu mwenye maneno ya haraka ni vibaya zaidi kuliko kuwa mpumbavu?

Proverbs 29:23-24

Mtu wa aina gani hupewa heshima?

Mtu mwenye moyo wa unyenyekevu hupewa heshima.

Proverbs 29:25-26

Yahwe hufanya nini kwa ajili ya mtu anayemtumaini?

Yahwe humlinda mtu ambaye anamtumaini.

Proverbs 29:27

Nani ni chukizo kwa wale wenye haki?

Mtu kafiri ni chukizo kwa wale wenye kutenda haki.

Proverbs 30

Proverbs 30:1-4

Misemo ya nani imeandikwa katika mithali hii?

Misemo ya Aguri mwana wa Jakeh imeandikwa katika mithali hii.

Mwandishi hajajifunza nini?

Mwandishi hajajifunza hekima.

Proverbs 30:5-6

Kitatokea nini kwa mtu ambaye huongeza kwenye maneno ya Mungu?

Mungu atamkemea mtu ambaye huongeza kwenye maneno ya Mungu.

Proverbs 30:7-10

Mwandishi nataka awe na utajiwe wa namna gani?

Mwandishi nataka asipate umasikini wala utajiri.

Mwandishi anaogopa atafanya nini kama angekuwa tajiri?

Mwandishi anaogopa angemkaa Mungu kama angekuwa tajiri.

Proverbs 30:11-12

Akina nani hawajaoshwa uchafu wao?

Ni kizazi ambacho huwalaani baba zao na wasio barikia mama zao hawajaoshwa uchafu wao.

Proverbs 30:13-14

Kizazi chenye kiburi hufanya nini kwa masikini?

Kizazi chenye kiburi huwararu masikini

Proverbs 30:15-17

Vitu gani vinne ambavyo havisemi "imetosha"?

Vitu vinne ambavyo havisemi" imetosha" ni kuzimu, tumbo lililo tasa, ardhi yenye kiu ya maji, na moto.

Proverbs 30:18-20

Jambo gani la pili ambalo mwandishi halifahmu kwa sababu linashangaza sana?

Mwandisdhi hafahamu njia ya nyoka juu ya mwamba.

Proverbs 30:21-26

Jambo gani la kwanza amba mwandishi anasema husababisha dunia kutetemeka?

Jambo la kwanza ambalo mwandishi anasema husababisha dunia kutetemeka ni pale mtumwa anapokuwa mfalme.

Proverbs 30:27-28

Mwandishi anapata nini cha kushangaza kuhusu nzige?

Mwandishi anawashangaa nzige kwa sababu hawana mfalme, lakini wote hutembea katika safu.

Proverbs 30:29-31

Ni nini ambacho hakikwepi kitu chochote?

Simba huwa hakwepi kitu chochote.

Proverbs 30:32-33

Mtu ambaye amekuwa akitunga uovu anapaswa kufanya nini?

Mtu ambaye amekuwa akitunga uovu anapaswa kuweka mkono wake juu ya kinywa chake.

Hasira huzaa nini?

Hasira huzaa migogoro

Proverbs 31

Proverbs 31:1-3

Nani aliandika mithali hii?

Mfalme Lamueli aliandika mithali hii.

Mfalme hapaswi kumpa nani njia zake?

Hapaswi kuwapa njia zake wale ambao huwaharibu wafalme.

Proverbs 31:4-5

Watawala husahau nini wanapokunywa kinywaji kikali?

Watawala husahau sheria wakati wanapokunywa kinywaji kikali.

Proverbs 31:6-7

Wale ambao wapo katika mateso makali husahau nini wanapokunywa kinywaji kikali?

Wale ambao wapo katika mateso makali husahau taabu zao wanapokunywa kinywaji kikali

Proverbs 31:8-9

Mfalme anapaswa kutetea kesi ya nani?

Mfalme anapaswa kutetea kesi ya masikini na wahitaji.

Proverbs 31:10-12

Ni nini chenye thamani kuliko marijani?

Mke mwenye akili anathamani zaidi ya marijani.

Mke mwenye akili hufanya nini siku zote za maisha yake?

Mke mwenye akili hutenda mema kwa ajili ya mume wake na wala si mabaya siku zote za maisha yake.

Proverbs 31:13-15

Mke mwenye akili huamka wakati gani?

Huamka bado usiku.

Proverbs 31:16-19

Mke mwenye akili hujivika nini ?

Hujivika nguvu

Proverbs 31:20-21

Mke mwenye akili humfikia nani?

Humfikia masikini na wahitaji

Proverbs 31:22-25

Mume wa mke mwenye akili huketi wapi?

Mume wake huketi pamoja na wazee kwenye malango.

Proverbs 31:26-27

Kwenye ulimi wa mke mwenye akili kuna nini?

Sheria ya ukarimu ipo kwenye ulimi wa mke mwenye akili.

Proverbs 31:28-29

Watoto wa mke mwenye akili humwitaje?

Watoto wake humwita heri.

Proverbs 31:30-31

Mwanamke wa aina gani atasifiwa?

Mwanamke mwenye hofu ya Yahwe atasifiwa.