Ezra
Ezra 1
Ezra 1:1-2
Ni nani aliteuliwa na Yahwe kumjengea yeye nyumba katika Yerusalem ya Yuda?
Yahwe alimteua Koreshi kumjengea yeye nyumba katika Yerusalem ya Yuda.
Ezra 1:3-6
Nani atawapa fedha na dhahabu waliosalia katika nchi?
Watu wa kila sehemu katika ufalme waliosalia katika nchi na kuishi wanapaswa kuwapa wao fedha na dhahabu.
Ezra 1:7-8
Nebukadineza aliviweka wapi vitu ambayo vilikuwa vya nyumba ya Yahwe?
Nebukadineza aliviweka kwenye nyumba ya miungu yake vitu ambavyo vilkuwa vya nyumba ya Yahwe.
Ezra 1:9-11
Vitu vingapi vya Dhahabu na fedha ambavyo Sheshbaza alivileta wakati wa uhamisho kutoka Babeli kwenda Yerusalem?
Sheshbaza akaleta fedha na dhahabu 5,400 wakati wa uhamisho kutoka Babeli kwenda Yerusalem
Ezra 2
Ezra 2:1-60
Nani aaliyewachukua watu mateka Babeli?
Mfalme Nebukadneza aliwachukua watu utumwani Babeli.
Ezra 2:61-69
Kwa nini baadhi ya wana wa kuhani kumbukumbu ya kizazi chao haikuonekana?
Wana wa kuhani hawakuweza kuona kumbukumbu ya kizazi chao kwa kuwa waliharibu ukuhani wao.
Ni wakati gani wana wa kuhani walikula vitakatifu vilivyotakaswa?
Wana wa kuhani waliweza kula baadhi vitakatifu vilivyotakaswa baada ya kuhani mwenye Urimu na Thumimu kuthibitisha.
Ezra 2:70
Watu wote wa Israel walikuwa wapi?
Watu wote katika Israel walikuwa katika miji yao.
Ezra 3
Ezra 3:1-2
Kwa nini Yeshua mwana wa Yosadaki na kaka yake kuhani, na Zerubabeli wmana wa Sheatieli na kaka yake wakainuka na kujenga madhabahu ya Mungu wa Israel?
Waliinuka na kujenga madhabahu kwa kutoa sadaka ya kuteketezwa kama ilivyoagizwa katika sheria ya Musa.
Ezra 3:3-5
Ni kwa vipindi gani Yeshua na kaka yake kuhani na Zerubabeli na kaka yake walitoa sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe?
Walitoa sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe asubuhi na jioni.
Ezra 3:6-7
Nani aliagiza miti ya mierezi kupelekwa kutoka Lebanoni mpaka Yafa kupitia baharini?
Koreshi, mfalme wa uajemi aliamuru miti ya mierezi kupelekwa kutoka Lebanoni mpaka Yafaa kwa kupitia baharini.
Ezra 3:8-9
Kazi ilianza wakati gani?
Kazi ilianza mwezi wa pili katika mwaka wa pili baada ya Israel kufika nyumba ya Mungu katika Yerusalem.
Ezra 3:10-11
Mwitikio wa watu ulikuwaje kwa sababu ya msingi wa Hekalu kuwekwa?
Watu wote walipiga kelele kwa shangwe furaha za kumtukuza Yahwe kwa sababu misingi ya Hekalu ilisimamishwa.
Ezra 3:12-13
Ulikuwaje mwitikio wa wale walioiona nyumba ya kwanza baada ya kuona kwa macho yao misingi ya nyumba imekamilika?
Wale walioiona nyumba ya kwanza walilia kwa sauti wakati misingi ilipowekwa wakaishuhudia kwa macho yao. Lakini wengi walipiga kelele za shangwe na furaha na sauti ya kushangaza.
Ezra 4
Ezra 4:1-3
Baadhi ya maadui wa Yuda na Benjamini walisikia kwamba watu waliokuwa uhamishoni walifanya nini?
Baadhi ya maadui wa Yuda na Benjamini walisikia kwamba watu waliokuwa uhamishoni walikuwa wanajenga Hekalu la Yahwe, Mungu wa Israel.
Ezra 4:4-10
Kwa kipindi gani maadui waliwazoofisha Wayahudi?
Waliwadhoofisha mikono ya wayahudi kipindi chote cha Koreshi na kipindi cha utawala wa Dario mfalme wa Uajemi.
Maadui waliandika nini wakati wa kuanza kutawala kwa Ahasuero?
Katika kuanza kutawala kwake Ahasuero , maadui wakaandika mashitaka dhidi ya wenyeji wa Yuda na Yerusalem.
Ezra 4:11-13
Maadui walimwambia nini mfalme kuhusu mji wa Wayahudi?
Maadui walimwambia mfalme kwamba Wayahudi walikuwa wakijenga mji wa uasi.
Ezra 4:14-16
Kwa nini ilionekana haifahi kwa maadui kuona heshima ya mfalme inavunjwa?
Ilionekana haifai kwao kuona heshima ya mfalme inavunjwa kwa sababu walikula chumvi ya Ikulu.
Ezra 4:17-22
Baada ya barua ya maadui kutumwa kwa mfalme na kutafsiriwa na kusomwa kwake, alifanya nini?
Baada ya barua ya maadui kutumwa kwa mfalme ilitafsiriwa na kusomwa kwake, aliagizwa uchunguzi ufanywe?
Ezra 4:23-24
Kwa kipindi gani kazi ya nyumba ya Mungu Yerusalem ilisimama?
Kazi ya nyumba ya Mungu Yerusalem ilisimama mpaka kutawala kwa mwaka wa pili wa mfalme Dario wa Uajemi.
Ezra 5
Ezra 5:3-7
Walikuwa wakisubilia nini viongozi wa Wayahudi?
Viongozi wa Kiyahudi walikuwa wakisubilia amri kutoka kwa Dario
Ezra 5:8-11
Ni kwa jinsi gani Tatenai,Shetari,Bozenai na wakuu wenzao walivyotathmini kazi nyumba ya Mungu ilivyoendelea?
Waliandika kwamba kazi ilikuwa inafanywa polepole na ilikuwa inaendelea vizuri katika mikono ya Wayahudi.
Ezra 5:12-13
Kwa nini Mungu wa mbinguni aliwaweka wayahudi kwenye mikono ya Nebukadineza mfalme wa Babeli?
Mungu wa mbinguni aliwakabidhi Wayahudi katika mikono ya Nebukadineza mfalme wa Babeli kipindi watangulizi walipomchukiza yeye.
Ezra 5:14-16
Kitu gani mfalme Koreshi alirudisha kwa Sheshbaza?
Mfalme Koreshi alirudisha vitu vya fedha na dhahabu vilivyokuwa katika nyumba ya Mungu
Ezra 5:17
Wayahudi walimwomba mfalme afanye kitu gani?
Walimwomba mfalme uchunguzi ufanyike kwenye nyumba ya kumbukumbu Babeli ikiwapo hukumu ya mfalme wa Koreshi ya kujenga nyumba ya Mungu Yerusalem.
Ezra 6
Ezra 6:1-2
Kitu gani kilionekana wakati mfalme Dario alipoamuru uchunguzi ufanyike katika nyumba ya kumbukumbu Babeli?
Wakati uchunguzi unafanywa ulioagizwa na mfalme Dario chuo kilionekana katika mji wa Akmetha huko media.
Ezra 6:3-5
Kutokana na amri ya Koreshi aliyoitoa nani alipaswa kulipa kwa ajili ya nyumba kutokana na sadaka?
Gharama za nyumba ya sadaka zitalipwa na nyumba ya mfalme.
Kutokana na amri ya mfalme kitu gani kilipaswa kurudishwa kwenye nyumba ya Mungu?
Kutokana na amri ya Koreshi vitu vya dhahabu na fedha vilivyokuwa kwenye nyumba ya Mungu ambavyo Nebukadineza alivichukua kuvipeleka Babeli kutoka Hekaluni. Na avirudishe tena kwenye nyumba ya Mungu Yerusalem.
Ezra 6:6-7
Koreshi alisema ni nani atakayejenga nyumba ya Mungu?
Koreshi alisema viongozi na wazee wa Kiyahudi watajenga nyumba ya Mungu.
Ezra 6:8-10
Kwa nini Koreshi alitaka kuwapa wayahudi chochote walichotaka kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu?
Koreshi alitaka kuwapa Wayahudi chochote walichohitaji kwa ujenzi wa nyumba ya Mungu ili kwamba wataleta sadaka kwa Mungu wa mbinguni na wataomba kwa ajili yake na watoto wake.
Ezra 6:11-12
Kitu gani lazima kifanyike kwa yeyote atakayekiuka agizo la kuwasaidia wayahudi?
Kwa yeyote atakayevunja amri, chuma kitolewe katika nyumba yake. Na awekwe juu ya nyumba yake. Na nyumba yake itabadilishwa kuwa takataka kwa sababu hii.
Ezra 6:13-18
Hagai na Zakaria waliwaelekezaje viongozi wa kiyahudi kuhusu kujenga?
Hagai na Zakaria waliwaelekeza viongozi wa kiyahudi kujenga kwa utabiri.
Ezra 6:19-20
Makuhani na Walawi walichinga sadaka ya Pasaka kwa ajili ya nani?
Makuhani na walawi walichinja sadaka ya Pasaka kwa ajili ya wote waliokuwa mateka wakiwemo wao wenyewe.
Ezra 6:21-22
Kwa nini wayahudi walifurahia na kusherehekea siku kuu ya mikate isiyochacha?
Wayahudi walifurahi na kushangilia siku kuu ya mikate isiyochacha, kwa kuwa Yahwe amewarejeshea furaha na amegeuza moyo wa mfalme wa Ashuru na kuwatia nguvu kwa kazi ya nyumba yake.
Ezra 7
Ezra 7:6-7
Ezra alikuwa na kazi gani?
Yeye alikuwa mtalaam mwandishi wa sheria ya Musa.
Ezra 7:8-10
Kwa nini Ezra alifika Yerusalem siku ya kwanza ya mwezi wa tano?
Siku ya kwanza ya mwezi wa tano alifika Yerusalem kwa kuwa mkono mzuri wa Mungu ulikuwa pamoja naye.
Ezra 7:11-13
Nani aliyeruhusiwa kwenda Yerusalem pamoja na Ezra?
Yeyote katika Israeli katika ufame wa Artashasta, pamoja na makuhani, na ambao wanatamani kwenda Yerusalem, wanaweza kwenda pamoja na Ezra.
Ezra 7:14-18
Kwa nini Mfalme na washauri wake saba waliwarudisha waisraeli tena Israeli?
Mfalme na washauri wake saba akawatuma wote kufahamu kuhusu Yuda na Yerusalem kuhusiana na sheria ya Mungu aliyoifahamu na kuleta Dhahabu na fedha ambazo walitoa kwa ajili ya Mungu wa Israeli ambaye makazi yake ni Yerusalem.
Ezra 7:19-20
Wayahudi wangetoa wapi chochote walichohitaji kwa ajili ya nyumba ya Mungu wao?
Wayahudi wangechukua chochote ambacho kinahitajika kwa ajili ya nyumba ya Mungu wao kutoka kwenye hazina ya Artashasta.
Ezra 7:21-24
Kwa nini watunza hazina walifanya chochote walichoamliwa na Mungu wa mbinguni kwa ajili ya utukufu wa nyumba yake?
Walipaswa kufanya chochote kilichoamliwa kutoka kwa Mungu wa mbinguni kwa utukufu wa nyumba yake, ili kwamba hasira isije kwa Artashasta na ufalme wa watoto wake.
Ezra 7:25-26
Ezra angemwazibuje mtu yeyote ambaye hakutii amri ya Mungu au amri ya Mfalme?
Ezra angetoa adhabu kwa yeyote asiyetii sheria ya Mungu au sheria ya mfalme, ikiwezekana kwa kifo,kuhamishwa,kuchukuliwa mali zake au kufungwa.
Ezra 7:27-28
Ezra alitiwaje nguvu?
Ezra alitiwa nguvu na mikono ya Yahwe Mungu wake.
Ezra 8
Ezra 8:15-16
Ezra alipochunguza watu na makuhani hakuona nini?
Ezra alipochunguza watu na makuhani, hakuwaona wana wa Levi miongoni.
Ezra 8:17
Ido na jamaa zake walikuwa na kazi gani?
Ido na jamaa zake walikuwa watumishi wa Hekalu.
Ezra 8:18-20
Ishekeli alikuwa mtu wa aina gani?
Ishekeli alikuwa mwana wa mali.
Ezra 8:21-27
Kwa nini Ezra hakumwomba mfalme majeshi au wapanda farasi kwa ajili ya kuwalinda dhidi ya maadui?
Ezra hakumwomba mfalme jeshi au wapanda farasi kwa ajili ya kumlinda dhidi ya maadui kwa sababu alikuwa amegafirika.
Ezra 8:28-30
Kwa muda gani walipaswa kuangalia fedha na dhahabu hawa watu kumi na wawili?
Wanaume kumi na wawili walipaswa kuviangalia fedha na dhahabu hadi watakapovipima mbele ya makuhani, walawi na viongozi watangulizi wa jamii ya Israeli katika Yerusalem ndani ya nyumba ya Mungu.
Ezra 8:31-34
Ni kwa namna gani mkono wa Mungu ulikuwa juu ya Ezra na wale kumi na wawili?
Mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nao uliwalinda na mikono ya adui na wale waliotaka kuwafanyia fujo njiani.
Ezra 8:35-36
Watu waliotoka matekani walimpa nani amri ya mfalme?
Wale waliotoka matekani wakampa amri za mfalme kwa wakuu wa mfalme na mkuu katika mji ngambo ya mto.
Ezra 9
Ezra 9:1-2
Ni kwa namna gani watu wa Israeli hawakujitenga kutokaa kwa watu wa nchi nyingine?
Watu wa Israeli hawakujitenga kutoka kwa watu wa nchi nyingine, kwa kuwa walichukua baadhi ya binti na vijana wao.
Ezra 9:3-4
Mwitikio wa Ezra ulikuwaje kwa watu wenye imani potofu?
Alichana nguo na kanzu na kunyoa nywele kichwani na ndevu na kukaa chini kutafakari.
Ezra 9:5-7
Kwa nini Ezra aliona aibu na kusononeka sana hata kuinua uso wake kwa Yahwe?
Ezra aliona aibu na kusononeka sana kuinua uso wake kwa Yahwe, kwa ajili ya kuongezeka kwa makosa ya watu wake hata kuvuka kichwani, na maovu kuongezeka hata kufika mbinguni.
Ezra 9:8-9
Kwa nini Yahwe aliongeza agano la uaminifu kwa watu wa Ezra?
Yahwe aliongeza agano la uaminifu kwa watu wa Ezra ili kuwapa nguvu mpya kuweza kujenga nyumba ya Mungu na kuondoa majuto. Alitenda hayo ili kwamba aweze kutupatia msingi wa usalama katika Yuda na Yerusalem.
Ezra 9:10-12
Nchi ilikuwa imejichanganyaje?
Nchi ilikuwa imechanganyikana na watu wasio na utaratibu wameenea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa uchafu wao.
Ezra 9:13-15
Mungu hakutazama kitu gani nyuma?
Mungu hakutazama makosa ya watu na kuadhibu kama walivyostahili.
Ezra 10
Ezra 10:1-2
Ezra alifanya nini wakati alipokuwa akiomba na kutubu?
Wakati Ezra akiomba na kutubu, akalia na kujirusha chini mbele ya nyumba ya Mungu.
Ezra 10:3-4
Agano gani Shekania aliwaambia Waisraeli waweke?
Alisema wanapaswa kuweka agano na Mungu wetu kuwaondoa wanawake wote wa kigeni na watoto wao
Ezra 10:5-6
Kwa nini Ezra hakula mkate au hata kunywa maji?
Ezra hakula mkate au kunywa maji, kwa kuwa alikuwa akiomboleza kuhusiana na wale wenye imani haba waliokuwa uhamishoni.
Ezra 10:7-8
Nini kilitokea kwa yeyote ambaye hakuja katika kipindi cha siku tatu kutokana na maagizo kutoka maofisa na viongozi?
Yeyote ambaye hakuja katika siku tatu kutokana na maelezo kutoka kwa wakuu na viongozi atachukuliwa mali zote na atatengwa na kusanyiko kuu la watu ambao walikuja kutoka uhamisho.
Ezra 10:9-11
Kwa nini watu wote ambao walisimama mbele ya nyumba ya Mungu walitetemeka?
Watu wote wakasimama mbele ya nyumba ya Mungu na wakatetemeka kwa sababu ya neno na mvua.
Ezra 10:12-15
Kwa nini Waisraeli walihitaji muda mwingi kuwaondoa na kuwatoa wanawake wa kigeni?
Walihitaji mwingi kwa sababu kulikuwa na watu wengi, na ni kipindi cjha mvua. Hawakuwa na nguvu ya kusimama nje. Kwa kuwa wamekosea katika jambo hili.
Ezra 10:16-17
Kwa muda gani viongozi walimaliza kuchunguza wanaume ambao waliishi na wanawake wa kigeni?
Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakawa wamemaliza kuchunguza wale wanaume walioishi na wanawake wa kigeni.
Ezra 10:18-44
Wanaume waliokosa walitoa nini?
Wanaume waliokosa walitoa sadaka ya kondoo kwenye mifugo kwa ajili ya makosa yao.