Revelation
Revelation 1
Revelation 1:1-3
Ufunuo huu umetoka kwa nani kwanza, na ni kwa nani huu ufunuo unaonyeshwa?
Ufunuo wa Yesu Kristo umekuja kutoka kwa Mungu, na unaonyeshwa kwa watumishi wake.
Ni wakati gani matukio ya ufunuo yatatokea?
Matukio ya ufunuo yatatokea hivi karibuni.
Nani atabarikiwa na kitabu hiki?
Wale wasomao kwa sauti, kusikiliza, na kutii kitabu hiki watabarikiwa.
Revelation 1:4-6
Nani aliandika kitabu hiki, na aliandika kwa ajili ya nani?
Yohana aliandika kitabu hiki, na aliandika kwa makanisa saba ya Asia.
Yohana anampatia Yesu majina yapi matatu?
Yohana anampatia Yesu majina ya shahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa wafu, na mtawala wa wafalme wa nchi.
Yesu amewafanya nini waumini?
Yesu amewafanya ufalme na ukuhani kwa Mungu Baba waumini.
Revelation 1:7-8
Yesu ataonwa na nai atakaporudi?
Kila jicho litamwona Yesu atakaporudi, wakiwemo wale waliomchoma.
Kwa jinsi gani Mungu Bwana anajielezaje?
Mungu Bwana anajieleza kama Alfa na Omega, yule aliye, yule aliyekuwepo, na yule atakayekuwepo, Mwenye Nguvu.
Revelation 1:9-13
Kwa nini Yohana alikuwa katika kisiwa cha Patmo?
Yohana alikuwa katika kisiwa cha Patmo kwa sababu ya neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu.
Sauti kubwa nyuma ya Yohana ilimwambia afanye nini?
Sauti kubwa ilimwambia Yohana aandike kwenye kitabu kile alichokiona na kukituma kwa makanisa saba.
Revelation 1:14-16
Mtu ambaye Yohana alimuona alikuwa na nywele na macho ya aina gani?
Mtu ambaye Yohana alimuona alikuwa na nywele kama sufi, na macho kama mwale mkali wa moto.
Nini kilikuwa katika mkono wa kuume wa yule mtu, na nini kilikuwa kikitoka kinywani mwake?
Yule mtu alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume, na kinywani mwake kulikuwa na panga lenye makali pande mbili likimtoka.
Revelation 1:17-18
Yohana alifanya nini alipomwona yule mtu?
Yohana alianguka miguuni mwa yule mtu kama mfu.
Mtu yule alisema ana funguo zipi?
Mtu yule alisema ana funguo za Mauti na Kuzimu.
Revelation 1:19-20
Maana ya nyota saba pamoja na vinara saba vya dhahabu ilikuwa ni nini?
Nyota saba walikuwa malaika wa makanisa saba, na vinara saba vya dhahabu vilikuwa ni makanisa saba.
Revelation 2
Revelation 2:1-2
Kifungu kinachofuata cha kitabu kimeandikwa kwa malaika yupi?
Kifungu kinachofuata cha kitabu kimeandikwa kwa malaika wa kanisa la Efeso.
Kanisa la Efeso limefanya nini kuhusu wale walio waovu na kuhusu manabii wa uongo?
Kanisa la Efeso halijawavumilia wale walio waovu na limewapima manabii wa uongo.
Revelation 2:3-5
Kristo ana jambo gani dhidi ya kanisa la Efeso?
Jambo alilonalo Kristo dhidi ya kanisa la Efeso ni kwamba wameuacha upendo wao wa kwanza.
Kristo anasema atafanya nini iwapo hawatatubu?
Kristo anasema atarudi na kuondoa kinara chao kutoka pahali pake iwapo hawatatubu.
Revelation 2:6-7
Kristo anaahidi nini kwa wale watakaoshinda?
Kristo anaahidi ya kwamba wale watakaoshinda watakula kutoka kwenye mti wa uzima katika paradiso ya Mungu.
Revelation 2:8-9
Kifungu kinachofuata cha kitabu kimeandikwa kwa malaika yupi?
Kifungu kinachofuata cha kitabu kimeandikwa kwa malaika wa kanisa la Smirna.
Kanisa la Smirna limepitia nini?
Kanisa la Smirna limepitia mateso, umaskini na kashfa.
Revelation 2:10-11
Kristo anaahidi nini kwa wale walio waaminifu hadi kifo na wanaoshinda?
Kristo anaahidi kwa wale walio waaminifu hadi kifo na wanaoshinda kuwa watapata taji za uzima na hawataumizwa na kifo cha pili.
Revelation 2:12-13
Kifungu kinachofuata cha kitabu kimeandikwa kwa malaika yupi?
Kifungu kinachofuata cha kitabu kimeandikwa kwa malaika wa kanisa la Pergamo.
Kanisa la Pergamo linaishi wapi?
Kanisa la Pergamo linaishi pale ambapo kiti cha enzi cha shetani kilipo.
Kanisa la Pergamo lilifanya nini katika siku ambazo Antipa aliuawa?
Kanisa la Pergamo lilishika kwa nguvu jina la Kristo na halikukana Imani katika siku ambazo Antipa aliuawa.
Revelation 2:14-15
Ni mafundisho yapi mawili ambayo baadhi ya watu wa kanisa la Pergamo walishikilia?
Baadhi ya watu wa kanisa la Pergamo walishikilia mafundisho ya Balaamu na mafundisho ya Wanikolai.
Revelation 2:16-17
Kristo anaonya atafanya nini iwapo wale wanaoshikilia mafundisho haya ya uongo wasipotubu?
Kristo anaonya atakuja na kufanya vita dhidi ya wale wanaoshikilia mafundisho haya ya uongo.
Kristo anaahidi nini kwa wale watakaoshinda?
Kristo anawaahidi wale watakaoshinda kuwa watakula mana iliyofichwa na watapata jiwe jeupe lenye jina jipya.
Revelation 2:18-19
Kifungu kinachofuata cha kitabu kimeandikwa kwa malaika yupi?
Kifungu kinachofuata cha kitabu kimeandikwa kwa malaika wa kanisa la Thiatira.
Kristo anafahamu mambo gani mema ambayo kanisa la Thiatira limeyafanya?
Kristo anafahamu ya kwamba kanisa la Thiatira limeonyosha upendo, imani, huduma, na ustahimilivu.
Revelation 2:20-21
Kristo ana jambo gani dhidi ya kanisa la Thiatira?
Kristo ana jambo dhidi ya kanisa la Thiatira ya kwamba wamemvumilia yule mwanamke muovu nabii wa uongo Yezebeli.
Revelation 2:22-23
Kristo anaonya nini iwapo Yezebeli hatatubu?
Kristo anaonya ya kuwa atamtupa Yezebeli katika kitanda cha maradhi na kuwapiga watoto wake wafe iwapo hatatubu.
Revelation 2:24-25
Kristo anawaambia nini wale ambao hawajashikilia mafundisho ya Yezebeli?
Kristo anawaambia washikilie kwa nguvu hadi atakaporudi.
Revelation 2:26-29
Kristo anaahidi nini kwa wale watakaoshinda?
Kristo anawaahidi wale watakaoshinda mamlaka juu ya mataifa na nyota ya asubuhi.
Ni kwa lipi ambalo Kristo anasema kwa msomaji wa kitabu hiki asikilize?
Kristo anasema kwa msomaji wa kitabu hiki kuwa anapaswa asikilize kile ambacho Roho anasema kwa makanisa.
Revelation 3
Revelation 3:1-4
Kifungu kifuatacho cha kitabu kimeandikwa kwa malaika yupi?
Kifungu kifuatacho cha kitabu kimeandikwa kwa malaika wa kanisa la Sardi.
Kanisa la Sardi lina sifa gani, lakini ukweli juu yao ni upi?
Sifa ya kanisa la Sardi ni kwamba wako hai, lakini ukweli ni kwamba wamekufa.
Kristo anaonya nini kwa kanisa la Sardi kufanya?
Kristo anawaonya waamke na kuimarisha kile kilichobaki.
Revelation 3:5-6
Kristo anaahidi nini kwa wale watakaoshinda?
Wale watakaoshinda watavishwa mavazi meupe, watabaki katika kitabu cha uzima, na majina yao yatatajwa mbele ya Mungu Baba.
Revelation 3:7-8
Kifungu kifuatacho cha kitabu kimeandikwa kwa malaika yupi?
Kifungu kifuatacho cha kitabu kimeandikwa kwa malaika wa kanisa la Filadelfia.
Kanisa la Filadelfia limefanya nini ingawa lina nguvu kidogo?
Kanisa la Filadelfia limetii neno la Kristo na halijalikana jina lake.
Revelation 3:9-11
Kristo atawafanya wale wa sinagogi la Shetani wafanye nini?
Kristo atawafanya wale wa sinagogi la Shetani wasujudu mbele ya miguu ya watakatifu.
Kristo anawaambia kanisa la Filadelfia kufanya nini maana anarudi upesi?
Kristo anawaambia kushikilia sana kile walichonacho ili asiwepo mtu wa kuitwaa taji yao.
Revelation 3:12-13
Kristo anaahidi nini kwa wale watakaoshinda?
Wale watakaoshinda watakuwa nguzo katika hekalu la Mungu, watakuwa na jina la Mungu, jina la mji wa Mungu, na jina jipya la Kristo litakaloandikwa kwao.
Revelation 3:14-16
Kifungu kifuatacho cha kitabu kimeandikwa kwa malaika yupi?
Kifungu kifuatacho cha kitabu kimeandikwa kwa malaika wa kanisa la Laodikia.
Kristo anatamani kanisa la Laodikia liweje?
Kristo anatamani kanisa la Laodikia lingekuwa baridi au moto.
Kristo anataka kufanya nini kwa kanisa la Laodikia, na kwa nini?
Kristo anataka kulitapika kanisa la Laodikia kutoka kinywani mwake kwa sababu wana uvuguvugu.
Revelation 3:17-18
Kanisa la Laodikia linajisemaje lenyewe?
Kanisa la Laodikia linasema kuwa lina utajiri na halihitaji chochote.
Kristo anasema nini kuhusu kanisa la Laodikia?
Kristo anasema ya kwamba kanisa la Laodikia ni duni sana, lakuhuzunikiwa, maskini, kipofu na uchi.
Revelation 3:19-20
Kristo anafanya nini kwa wote awapendaye?
Kristo huwaelekeza na kuwafundisha kila ampendaye.
Revelation 3:21-22
Kristo anaahidi nini kwa wale watakaoshinda?
Wale watakaoshinda watakaa na Kristo katika kiti chake cha enzi.
Ni kwa nani Kristo anasema msomaji wa kitabu hiki anapaswa kumsikiliza?
Kristo anasema msomaji anapaswa kusikiliza kile ambacho Roho anayaambia makanisa.
Revelation 4
Revelation 4:1-3
Yohana aliona nini kikifunguliwa?
Yohana aliona mlango ukifunguliwa mbinguni.
Sauti ilisema itamuonyesha nini Yohana?
Sauti ilisema ya kwamba itamuonyesha Yohana yatakayotokea baada ya mambo haya.
Ni kitu gani alichokalia mmoja mbinguni?
Mmoja alikuwa amekalia kiti cha enzi.
Revelation 4:4-5
Nini kilizunguka kiti cha enzi mbinguni?
Kulikuwa na viti vya enzi ishirini na nne na wazee ishirini na wanne waliovikalia kulizunguka kile kiti cha enzi.
Zile taa saba zilizokuwa zikiwaka mbele ya kiti cha enzi zilikuwa nini?
Zile taa saba zilikuwa ni Roho saba za Mungu.
Revelation 4:6
Vitu gani vinne vilikuwa vikizunguka kiti cha enzi?
Kulikuwa na wenye uhai wanne waliozunguka kiti cha enzi.
Revelation 4:7-8
Ni maneno yapi matatu viumbe wenye uhai wanne hurudia usiku na mchana?
Usiku na mchana viumbe wenye uhai wanne hawakukoma kusema, "Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu."
Revelation 4:9-11
Wazee ishirini na wanne hufanya nini pale viumbe wenye uhai wanapotoa utukufu kwa Mungu?
Wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele ya kiti cha enzi na kusujudu, wakitupa chini taji zao.
Wazee wanasema nini juu ya wajibu wa Mungu katika uumbaji?
Wazee wanasema ya kwamba Mungu aliumba vitu vyote na kwa mapenzi yake vitu vyote vilikuwepo na viliumbwa.
Revelation 5
Revelation 5:1-2
Yohana aliona nini katika mkono wa kuume wa yule aliyekaa katika kiti cha enzi?
Yohana aliona gombo iliyotiwa mihuri saba.
Revelation 5:3-5
Nani duniani aliyestahili kufungua gombo au kuisoma?
Hakuna aliyestahili kuifungua wala kuisoma gombo.
Nani aliweza kuifungua gombo pamoja na mihuri yake saba?
Simba wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, aliweza gombo.
Revelation 5:6-7
Nani alikuwa amesimama miungoni mwa wazee mbele ya kiti cha enzi?
Mwanakondoo, ambaye alionenekana kama alikuwa ameuliwa, alisimama miungoni mwa wazee mbele za kiti cha enzi.
Pembe saba na macho saba ya Mwanakondoo vilikuwa ni nini?
Pembe saba na macho saba ni Roho saba za Mungu zilizotumwa duniani kote.
Revelation 5:8
Mabakuli ya dhahabu yaliyojaa uvumba ambayo wazee walikuwa nayo yalikuwa ni nini?
Mabakuli ya dhahabu yaliyojaa uvumba ambayo wazee walikuwa nayo yalikuwa ni maombi ya watakatifu.
Revelation 5:9-10
Kwa nini Mwanakondoo alistahili kufungua gombo?
Mwanakondoo alistahili kwa sababu aliwanunua watu wa Mungu kutoka kila kabila, lugha, watu na taifa kwa damu yake.
Makuhani wa Mungu watatawala wapi?
Makuhani wa Mungu watatawala duniani.
Revelation 5:11-12
Malaika walisema nini kuwa Mwanakondoo alistahili kupokea?
Malaika walisema kuwa Mwanakondoo alistahili kupoka uwezo, utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu, na sifa.
Revelation 5:13-14
Ni nani aliyesema kuwa yule aliye katika kiti cha enzi anapaswa kusifiwa milele na milele.
Kila kitu kilichoumbwa kilisema kuwa yule aliye katika kiti cha enzi anapaswa kusifiwa milele na milele.
Wazee walifanya nini waliposikia viumbe wenye uhai wanne wakisema "Amina!"?
Wazee walilala chini na kuabudu.
Revelation 6
Revelation 6:1-2
Mwanakondoo alifanya nini na gombo?
Mwanakondoo alifungua muhuri mmoja kati ya saba katika gombo.
Yohana aliona nini baada ya muhuri wa kwanza kufunguliwa?
Yohana aliona farasi mweupe na mpandaji akienda kushinda.
Revelation 6:3-4
Yohana aliona nini baada ya muhuri wa pili kufunguliwa?
Yohana aliona farasi mwekundu kama moto ambaye mpandaji wake alichukua amani kutoka duniani.
Revelation 6:5-6
Yohana aliona nini baada ya muhuri wa tatu kufunguliwa?
Yohana aliona farasi mweusi ambaye mpandaji wake alikuwa na mizani mikononi mwake.
Revelation 6:7-8
Yohana aliona nini baada ya muhuri wa nne kufunguliwa?
Yohana aliona farasi wa kijivu, ambaye mpandaji wake aliitwa Mauti.
Revelation 6:9-11
Yohana aliona nini baada ya muhuri wa tano kufunguliwa?
Yohana aliona roho za wale ambao waliuliwa kwa sababu ya neno la Mungu.
Roho zilikuwa chini ya madhabahu zilitaka kujua nini kutoka kwa Mungu?
Roho zilitaka kujua ni muda gani hadi pale Mungu atakapolipiza kisasi cha damu zao.
Roho ziliambiwa zitapaswa kusubri kwa muda gani?
Roho ziliambiwa zitapaswa kusubiri mpaka idadi kamili ya watumishi wenzao wauwawe.
Revelation 6:12-14
Yohana aliona nini baada ya muhuri wa sita kufunguliwa?
Yohana aliona tetemeko, jua kuwa jeusi, mwezi kuwa kama damu, na nyota kuanguka duniani.
Revelation 6:15-17
Yohana aliona wafalme, majemadari, matajiri, wenye nguvu, na wengine wote wakifanya nini?
Yohana aliwaona wakijificha kwenye mapango na kuomba mawe yawaangukie na kuwaficha.
Wafalme, majemadari, matajiri, wenye nguvu, na wengine wote walitaka kufichwa dhidi ya nini?
Walitaka kufichwa dhidi ya yule aketiye kwenye kiti cha enzi na kutoka kwa hasira ya Mwanakondoo.
Ni siku gani imewadia?
Siku kuu ya ghadhabu ya yule aketiye kwenye kiti cha enzi na ya Mwanakondoo alikuwa imewadia.
Revelation 7
Revelation 7:1-3
Malaika wanne waliokuwa wamesimama kwenye kona nne za dunia walikuwa wanafanya nini Yohana alipowaona?
Malaika wanne walikuwa wanazuia pepo nne za nchi.
Malaika wa mashariki alisema ni nini lazima kifanyike kabla dunia haijadhuriwa?
Malaika alisema kuwa muhuri lazime uwekwe kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu kabla dunia haijadhuriwa.
Revelation 7:4-8
Watu wangapi wa kabila gani waliwekwa muhuri?
Idadi ya watu waliowekwa muhuri ni 144,000 kutoka katika kila kabila la watu wa Israeli.
Revelation 7:9-10
Yohana aliona nini mbele za kiti cha enzi na mbele za Mwanakondoo?
Yohana aliona umati mkuwa kutoka kila taifa, kabila, watu, na lugha mbele ya kiti cha enzi.
Kulingana na wale walio mbele ya kiti cha enzi, wokuvu ni wa nani?
Wale walio mbele ya kiti cha enzi walisema wokovu ni wa Mungu na wa Mwanakondoo.
Revelation 7:11-12
Malaika, wazee na wenye uhai wanne walikuwa katika nafasi gani ya mwili walipomuabudu Mungu.
Walilala chini ardhini na kuweka nyuso zao juu ya ardhi wakimuabudu Mungu.
Revelation 7:13-14
Mzee alisema ni kina nani wale waliovaa kanzu nyeupe mbele ya kiti cha enzi?
Mzee alisema kuwa ni wale waliotoka kwenye dhiki kuu.
Waliokuwa mbele ya kiti cha enzi walizifanyaje kanzu zao kuwa nyeupe?
walizifanya kanzu zao kuwa nyeupe kwa kuziosha katika damu ya Mwanakondoo.
Revelation 7:15-17
Mzee alisema Mungu atawafanyia nini wale waliovaa kanzu nyeupe?
Mungu atasambaza hema lake juu yao ili wasiteseke tena.
Mzee alisema Mwanakondoo atawafanyia nini waliovaa kanzu nyeupe?
Mwanakondoo atawachunga na kuwaongoza kwenye chemichemi za maji ya uzima.
Revelation 8
Revelation 8:1-2
Nini kilisababisha kuwepo na ukimya mbinguni?
Mwanakondoo alipofungua muhuri wa saba, kulikuwa na ukimya mbinguni.
Nini kilipewa kwa malaika saba wanaosimama mbele za Mungu.
Tarumbeta saba zilipewa kwa malaika saba wanaosimama mbele za Mungu.
Revelation 8:3-5
Nini kiliinuka mbele za Mungu?
Moshi wa uvumba wa maombi ya watakatifu uliinuka mbele za Mungu.
Nini kilitokea malaika alipotupa chini duniani moto kutoka madhabahuni?
Malaika alipotupa chini moto, zilitokea ngurumo, radi na tetemeko.
Revelation 8:6-7
Nini kilitokea baada ya tarumbeta ya kwanza kupulizwa?
Tarumbeta ya kwanza ilipopulizwa, theluthi moja ya nchi iliunguzwa, na theluthi moja ya miti na nyasi zote.
Revelation 8:8-9
Nini kilitokea baada ya tarumbeta ya pili kupulizwa?
Tarumbeta ya pili ilipopulizwa, theluthi moja ya bahari ikawa damu, theluthi moja ya viumbe wa baharini wakafa, na theluthi moja ya meli ziliharibiwa.
Revelation 8:10-11
Nini kilitokea baada ya tarumbeta ya tatu kupulizwa?
Tarumbeata ya tatu ilipopulizwa, theluthi moja ya maji yakawa pakanga, na watu wengi wakafa.
Revelation 8:12
Nini kilitokea baada ya tarumbeta ya nne kupulizwa?
Tarumbeta ya nne ilipopulizwa, theluthi moja ya siku na theluthi moja ya usiku hazikuwa na mwanga.
Revelation 8:13
Kwa nini tai alisema "Ole, ole, ole" kwa wale wa duniani?
Tai aslisema "Ole, ole, ole" kwa wale wa duniani kwa sababu ya milipuko ya tarumbeta tatu zilizosalia.
Revelation 9
Revelation 9:1-2
Yohana aliona nyota ya aina gani tarumbeta ya tano ilipopulizwa?
Tarumbeta ya tano ilipopulizwa, Yohana aliona nyota kutoka mbinguni iliyoanguka duniani.
Nyota ilifanya nini?
Nyota ilifungua shimo lisilo na mwisho.
Revelation 9:3-4
Nzige kutoka shimoni waliambiwa wafanye nini?
Nzige waliambiwa kutodhuru ardhi, bali watu wale ambao hawakuwa na muhuri wa Mungu.
Revelation 9:5-6
Watu walioteswa na nzige watatafuta nini lakini wasikione?
Watu walioteswa na nzige watatafuta kifo lakini hawataipata.
Revelation 9:7-9
Mabawa ya nzige yalipiga sauti ipi?
Sauti ya mabawa ya nzige ilikuwa kama sauti ya magari mengi ya vibandawazi na farasi wakimbiao kwenda vitani.
Revelation 9:10-12
Nani alikuwa mfalme juu ya nzige?
Abadoni ndiye aliyekuwa mfalme juu ya nzige, au kwa Kiyunani, Apolioni, malaika wa shimoni.
Nini kilipita baada ya tarumbeta ya tano kupulizwa?
Ole ya kwanza ilipita baada ya tarumbeta kupulizwa.
Revelation 9:13-15
Yohana alisikia sauti gani baada ya tarumbeta ya sita kupulizwa?
Tarumbeta ya sita ilipopulizwa, Yohana alisikia sauti ikitoka kwenye madhabahu ya dhahabu iliyokuwa mbele za Mungu.
Malaika wanne walifanya nini waliposikia sauti?
Malaika wanne waliachiwa kuwauwa theluthi moja ya wanadamu waliposikia sauti.
Revelation 9:16-17
Yohana aliona maaskari wangapi kwenye migongo ya farasi?
Yohana aliona maaskari 200,000,000 kwenye migongo ya farasi.
Revelation 9:18-19
Mapigo yapi yaliwauwa theluthi moja ya watu?
Mapigo ya moto, moshi, na salfa kutoka kwenye vinywa vya farasi viliwauwa theluthi moja ya watu.
Revelation 9:20-21
Watu ambao hawakuuwawa na mapigo walijibuje?
Watu ambao hawakuuwawa na mapigo hawakutubu kwa matendo yao, wala hawakuacha kuabudu mapepo.
Revelation 10
Revelation 10:1-2
Uso na miguu ya malaika mkuu ambaye Yohana alimuona ilikuaje?
Malaika alikuwa na uso kama jua na miguu kama nguzo za moto.
Malaika alisimama wapi?
Malaika alisimama na mguu wake wa kulia baharini na wa kushoto kwenye ardhi.
Revelation 10:3-4
Yohana aliaambiwa asiandike kitu gani?
Yohana aliambiwa asiandike miungurumo ya radi saba zilivyosema.
Revelation 10:5-7
Malaika mkuu aliapa kwa nani?
Malaika mkuu aliapa kwa yule anayeishi milele na milele, aliyeumba mbingu, nchi, na bahari.
Malaika mkuu alisema ni nini ambacho hakitakawizwa tena?
Malaika alisema kuwa tarumbeta ya saba itakapopulizwa, hakukuwepo kuchelewa tena, bali siri ya Mungu itatimizwa.
Revelation 10:8-9
Yohana aliaambiwa kuchukua nini kutoka kwa malaika mkuu?
Yohana aliambiwa kuchukua gombo lililofunuliwa kutoka kwa malaika.
Malaika alisema nini kitatokea Yohana atakapokula lile gombo?
Malaika alisema gombo litakuwa tamu mdomoni mwa Yohana lakini chungu tumboni.
Revelation 10:10-11
Yohana aliambiwa kutabiri kuhusu nini baada ya kula gombo?
Yohana aliambiwa kutabiri kuhusu watu wengi, mataifa, lugha na wafalme.
Revelation 11
Revelation 11:1-2
Yohana aliambiwa kupima nini?
Yohana aliambiwa kupima hekalu la Mungu na madhabahu, na wale wanaoabudu ndani yake.
Mataifa watakanyaga mji mtakatifu kwa muda gani?
Mataifa watakanyaga mji mtakatifu kwa miezi arobaini na mbili.
Revelation 11:3-7
Mashahidi wawili walipewa mamlaka ya kufanya nini kwa wale waliochagua kuwadhuru?
Mashahidi wawili walipewa mamlaka kuwaua maadui zao kwa moto.
Revelation 11:8-9
Miili ya mashahidi wawili italala wapi?
Miili yao italala kwenye mtaa wa mji ambao kimfano unaitwa Sodoma na Misri, ambapo Bwana alisulubiwa.
Revelation 11:10-12
Watu wa duniani watachukuliaje pale mashahidi wawili watakapouwawa?
Watu wa duniani watafurahi na kusherehekea pale amabapo mashahidi wawili wakiuwawa.
Nini kitatokea kwa mashahidi wawili baada ya siku tatu na nusu?
Baada ya siku tatu na nusu, mashahidi wawili watasimama kwaa miguu yao na kwenda juu mbinguni.
Revelation 11:13-14
Baada ya mashahidi wawili na tetemeko kuisha, nini kimepita?
Baada ya mashahidi wawili na tetemeko, ole ya pili imepita.
Revelation 11:15
Nini kilizungumzwa mbinguni baada ya tarumbeta ya saba kupulizwa?
Tarumbeta ya saba ilipopulizwa, ilisemwa kuwa ufalme wa dunia umekuwa ufalme wa Bwana wetu na Kristo wake.
Revelation 11:16-17
Wazee walisema kuwa Bwana Mungu ameanza kufanya nini sasa?
Waze walisema kuwa Mungu ameanza kutawala sasa.
Revelation 11:18
Kulingana na wazee, ni muda gani ulikuwa umewasili?
Muda uliwasili wa wafu kuhukumiwa, kwa watumishi wa Mungu kupewa dhawabu, na kwa Mungu kuangamiza wale waliokuwa wakiangamiza dunia.
Revelation 11:19
Nini kilifunguliwa sasa mbinguni?
Hekalu la Mungu lilifunguliwa sasa mbinguni.
Revelation 12
Revelation 12:1-2
Ni ishara gani kuu ilionekana mbinguni?
Mbinguni alionekana mwanamke mjamzito aliyefunikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na nyota saba kichwani mwake akilia kwa maumivi ya kuzaa.
Revelation 12:3-4
Ni ishara gani kuu nyingine ilionekana mbinguni?
Mbinguni alionekana joka mwekundu mkubwa mwenye vichwa saba na pembe kumi, na taji saba kwenye vichwa vyake.
Joka alifanya nini na mkia wake?
Joka alifyeka theluthi moja ya nyota za mbinguni na kuzitupa chini duniani.
Joka alitamani kufanya nini?
Joka alitamani kumeza mtoto wa mwanamke.
Revelation 12:5-6
Mtoto wa kiume alikwenda kufanya nini?
Mtoto wa kiume alikwenda kutawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma.
Mtoto wa kiume alikwenda wapi?
Mtoto wa kiume alinyakuliwa juu kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi.
Mwanamke alikwenda wapi?
Mwanamke alikimbilia nyikani.
Revelation 12:7-10
Nani alipigana mbinguni?
Mikaeli na malaika wake walipigana na joka na malaika zake.
Baada ya mapigano, nini kilitokea kwa joka na malaika zake?
Joka na malaika zake walitupwa chini duniani.
Joka ni nani?
Joka ni yule nyoka wa zamani, ibilisi, au Shetani.
Revelation 12:11-12
Ndugu walimshindaje joka?
Ndugu walimshinda joka kwa damu ya Mwanakondoo na kwa neno la ushuhuda wao.
Ni muda kiasi gani joka anafahamu amebakiza?
Joka anafahamu ya kuwa ana muda mchache.
Revelation 12:13-14
Nini kilifanyika kwa mwanamke pale joka alipomfuata?
Mwanamke alipewa mabawa ya kuruka hadi mahali alipoandaliwa ambapo angeweza kutunzwa.
Revelation 12:15-17
Joka aliposhindwa kumgharikisha mwanamke, joka alifanya nini?
Joka aliondoka na kufanya vita na wale wanaotii amri za Mungu na kushikilia ushuhuda kuhusu Yesu.
Revelation 13
Revelation 13:1-2
Mnyama aliyemuona Yohana alitoka wapi?
Mnyama alitokeza kwenye bahari.
Joka alimpatia nini mnyama?
Joka alimpa mnyama nguvu zake, kiti cha enzi, na mamlaka ya kutawala.
Revelation 13:3-4
Kwa nini dunia nzima ilishangaa na kumfuata mnyama?
Dunia nzima ilishangaa na kumfuata mnyama kwa sababu alikuwa na jeraha kali lililokuwa limeponywa.
Revelation 13:5-6
Mnyama alizungumza maneno yapi kwa kinywa chake?
Mnyama alizungumza maneno ya kujisifu na yenye matusi dhidi ya Mungu, jina lake, na mahali anapoishi, na kwa wale wanaoishi mbinguni.
Revelation 13:7-8
Mnyama aliruhusiwa kufanya nini kwa watakatifu?
Mnyama aliruhusiwa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda.
Ni watu gani hawatamuabudu mnyama?
Wale ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima hawatamuabudu mnyama.
Revelation 13:9-10
Wito gani unatolewa kwa wale walio watakatifu?
Wale walio watakatifu wanapewa wito wa kuwa na subira ya uvumilivu na imani.
Revelation 13:11-14
Mnyama yule mwingine aliyemwona Yohana alitoka wapi?
Mnyama yule mwingine alitokeza katika nchi.
Ni pembe za aina gani na matamshi yapi mnyama mwingine alikuwa nayo?
Mnyama mwingine alikuwa na pembe kama ya kondoo na alizungumza kama joka.
Mnyama mwingine alisababisha wale wanaoishi duniani kufanya nini?
Mnyama mwingine alisababisha wale wanaoishi duniani kumuabudu mnyama wa kwanza.
Revelation 13:15-17
Nini kilifanyika kwa wale waliokataa kumuabudu mnyama?
Wale waliokataa kumuabudu mnyama waliuawa.
Ni jambo gani kila mtu alipokea kutoka kwa mnyama?
Kila mtu alipokea alama katika mkono wake wa kuume au katika paji la uso.
Revelation 13:18
Namba ya mnyama ilikuwa ipi?
Namba ya mnyama ilikuwa 666.
Revelation 14
Revelation 14:1-2
Yohana alimuona nani amesimama mbele yake?
Yohana alimuona Mwana Kondoo kasimama mbele yake juu ya Mlima Sayuni.
Revelation 14:3-5
Nani aliweza kujifunza wimbo mpya ulioimbwa mbele ya kiti cha enzi?
Ni wale 144,000 pekee waliokombolewa kutoka duniani ndio waliweza kujifunza wimbo mpya.
Nani alikombolewa kama mzawa wa kwanza kwa Mungu na kwa Mwana Kondoo?
Wale 144,000 ambao hawana hatia walikombolewa kama wazawa wa kwanza kwa Mungu na kwa Mwana Kondoo.
Revelation 14:6-7
Ni kwa nani malaika alitoa ujumbe wa milele wa habari njema?
Malaika alitoa ujumbe wa milele wa habari njema kwa kila taifa, kabila, lugha, na watu wa duniani.
Malaika aliwaambia kitu gani wale wanaoishi duniani kufanya?
Malaika aliwaambia wamuogope Mungu na kumpa utukufu.
Muda gani malaika alisema umekaribia?
Malaika alisema ya kwamba muda wa hukumu ya Mungu umekaribia.
Revelation 14:8
Malaika wa pili alitangaza nini?
Malaika wa pili alitangaza ya kwamba Babeli kuu imeanguka.
Revelation 14:9-10
Malaika wa tatu alisema kitu gani kitatokea kwa wale waliopokea alama ya mnyama?
Wale waliopokea alama ya mnyama watateswa kwa moto na salfa.
Revelation 14:11-13
Wito gani unapewa kwa watakatifu?
Watakatifu wanapewa wito wa subira na uvumilivu.
Revelation 14:14-18
Yohana alimwona nani kaketi juu ya wingu?
Yohana alimwona mmoja mfano wa Mwana wa Mtu kaketi juu ya wingu.
Aliyeketi juu ya wingu alifanya nini?
Aliyeketi juu ya wingu aliinua mundu yake kuvuna dunia.
Revelation 14:19-20
Malaika aliyekuwa na mundu alifanya nini?
Malaika aliyekuwa na mundu alikusanya mavuno ya zabibu ya dunia na kuyarusha katika pipa la divai ya ghadhabu ya Mungu.
Nini kilitokea kwa chujio la divai la Mungu?
Chuji la divai lilipondwapondwa na damu ikamwagika kutoka kwake.
Revelation 15
Revelation 15:1
Malaika saba ambao Yohana aliwaona walikuwa na nini?
Malaika saba walikuwa na mapigo saba, ambayo ni mapigo ya mwisho.
Revelation 15:2
Nani alikuwa akisimama pembeni mwa bahari?
Wale waliokuwa washindi dhidi ya mnyama na sanamu yake walikuwa wamesimama pembeni mwa bahari
Revelation 15:3-4
Waliokuwa wamesimama pembeni mwa bahari walikuwa wakiimba wimbo wa nani?
Waliokuwa wamesimama pembeni mwaa bahari walikuwa wakiimba wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana Kondoo.
Njia za Mungu zilielezwaje katika wimbo?
Njia za Mungu zilielezwa kuwa za haki na za kweli.
Katika wimbo, nani atakuja na kumuabudu Mungu?
Mataifa yote yatakuja na kumuabudu Mungu.
Revelation 15:5-6
Kitu gani basi kilitokea katika mahali patakatifu sana?
Malaika saba wenye mapigo saba walitoka katika mahali patakatifu sana.
Revelation 15:7-8
Nini kilipewa kwa malaika saba?
Malaika saba walipewa mabakuli saba yaliyojaa ghadhabu ya Mungu.
Mpaka lini ambapo hakuna yeyote awezaye kuingia katika mahali patakatifu sana?
Hadi pale mapigo saba yatakapokamilika, hakuna mtu awezaye kuingia katika mahali patakatifu sana.
Revelation 16
Revelation 16:1
Malaika saba waliambiwa kufanya nini?
Malaika saba waliambiwa kwenda na kumwaga juu ya dunia mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu.
Revelation 16:2
Nini kilitokea baada ya bakuli la kwanza la gadhabu ya Mungu kumwagwa?
Vidonda vibaya na venye maumivu viliwajia watu waliokuwa na alama ya mnyama.
Revelation 16:3
Nini kilitokea baada ya bakuli la pili la ghadhabu ya Mungu kumwagwa?
Bahari lilikuwa kama damu ya mtu aliyekufa.
Revelation 16:4-7
Nini kilitokea baada ya bakuli la tatu la ghadhabu ya Mungu kumwagwa?
Mito na chemichemi za maji zilikuwa damu.
Kwa nini ilikuwa kweli na haki kwa Mungu kuwapa watu hawa damu kunywa?
Ilikuwa kweli na haki kwa sababu watu hawa walimwaga damu za watakatifu wa Mungu na manabii.
Revelation 16:8-9
Nini kilitokea baada ya bakuli la nne la ghadhabu ya Mungu kumwagwa?
Jua liliwachoma watu kwa moto.
Watu waliitikiaje kwa mapigo haya?
Watu hawakutubu wala kumpa Mungu utukufu.
Revelation 16:10-11
Nini kilitokea baada ya bakuli la tano la ghadhabu ya Mungu kumwagwa?
Giza lilifunika ufalme wa mnyama.
Revelation 16:12-14
Nini kilitokea baada ya bakuli la sita la ghadhabu ya Mungu kumwagwa?
Ziwa la Frati lilikauka kuandaa njia kwa ajili ya wafalme wa mashariki.
Roho chafu zilikuwa zinaenda nje kufanya nini?
Roho chafu zilikuwa zinaenda nje kuwakusanya wafalme wa dunia kwa ajili ya vita ya siku kuu ya Mungu.
Revelation 16:15-16
Sehemu ambapo wafalme wa dunia waliletwa pamoja paliitwaje?
Jina la sehemu hiyo ni Amagedoni.
Revelation 16:17-19
Nini kilitokea baada ya bakuli la saba la ghadhabu ya Mungu kumwagwa?
Sauti kubwa ilisema, "Imekwisha!" na kulikuwa na mwanga wa radi, ngurumo, na tetemeko.
Wakati huo, Mungu alikumbuka na kufanya nini?
Wakati huo, Mungu alikumbuka Babeli na kumpa Babeli kikombe kilichojaa ghadhabu yake.
Revelation 16:20-21
Watu waliitikiaje mapigo haya?
Watu walimlaani Mungu.
Revelation 17
Revelation 17:1-2
Malaika alisema atamuonesha nini Yohana?
Malaika alisema atamuonesha Yohana hukumu ya kahaba mkuu.
Revelation 17:3-5
Mwanamke alikuwa amekalia nini?
Mwanamke alikuwa amekalia mnyama mwenye vichwa saba na pembe kumi.
Nini kilikuwa kwenye kikombe ambacho mwanamke alikuwa ameshika mkononi mwake?
Kikombe kilikuwa kimejaa vitu vya kuchukiza na uchafu wa uasherati wake.
Jina la mwanamke ni nani?
Jina la mwanamke ni "Babeli Mkuu, Mama wa Makahaba na Vitu vya Kuchukiza Duniani"
Revelation 17:6-7
Mwanamke alikuwa amelewa nini?
Mwanamke alikuwa amelewa damu ya wakatifu na waliokufa kwa ajili ya Yesu.
Revelation 17:8
Mnyama aliyekuwa amekaliwa na mwanamke alitoka wapi?
Mnyama alitoka kwenye shimo refu lisilo na mwisho.
Mnyama alikuwa akienda wapi?
Mnyama alikuwa akienda kwenye maangamizo.
Revelation 17:9-10
Vichwa saba vya mnyama vilikuwa nini?
Vichwa saba vilikuwa ni milima saba ambapo mwanamke alikuwa ameketi, na pia vilikuwa ni wafalme saba.
Revelation 17:11
Mnyama alikuwa akienda wapi?
Mnyama alikuwa akienda kwenye maangamizo.
Revelation 17:12-14
Pembe kumi za mnyama zilikuwa ni nini?
Pembe kumi ni wafalme kumi.
Wafalme na mnyama watafanya nini wakiwa wa shauri moja.
Wakiwa wa shauri moja, watafanya vita dhidi ya Mwana kondoo.
Revelation 17:15
Maji ambayo kahaba aliyekalia yalikuwa nini?
Maji yalikuwa watu, makutano, mataifa, na lugha.
Revelation 17:16-17
Wafalme na mnyama watamfanya nini mwanamke?
Watamfanya kuwa mpweke na uchi, watamlaa mwili wake, na kumchoma kwa moto.
Revelation 17:18
Mwanamke aliyeonwa na Yohana ni nini?
Mwanamke aliyeonwa na Yohana ni mji mkuu unaotawala juu ya wafalme wa ulimwenguni.
Revelation 18
Revelation 18:1-3
Malaika mwenye mamlaka makubwa alitoa tangazo gani?
Malaika alitangaza kuwa Babeli mkuu ameanguka.
Revelation 18:4-6
Sauti kutoka mbinguni iliwaambia watu wa Mungu kufanya nini?
Sauti iliwaambia watu wa Mungu kutoka Babeli na kutokushiriki katika dhambi zake.
Mungu alimrudishia Babeli kiasi gani cha malipo kwa kile alichokifanya?
Mungu alimlipa Babeli mara mbili kwa kile alichokifanya.
Revelation 18:7-8
Mapigo gani yalimpata Babeli ndani ya siku moja?
Kifo, maombolezo, na njaa vilimpata Babeli ndani ya siku moja na aliteketezwa kwa moto.
Revelation 18:9-13
Wafalme na wafanyabiashara wa duniani waliitikiaje baada ya kuona hukumu ya Babeli?
Walipoona hukumu ya Babeli, wafalme na wafanyabiashara wa duniani walilia na kuomboleza juu yake.
Revelation 18:14
Babeli alitamani nini kilichopotea ndani ya saa moja?
Babeli alitamani starehe na fahari, zilizopotea ndani ya saa moja.
Revelation 18:15-17
Kwa nini wafalme, wafanyabiashara manahodha wa meli walisimama mbali wakati wa hukumu ya Babeli?
Walisimama mbali kwa sababu waliogopa mateso yake?
Revelation 18:18-20
Manahodha wa meli waliuliza swali gani kuhusu Babeli?
Manahodha wa meli waliuliza, "Ni mji gani kama mji mkuu?"
Watakatifu, watume na manabii waliambiwa kufanya nini wakati Babeli alipohukumiwa na Mungu?
Watakatifu, watume na manabii waliambiwa kufurahi wakati Babeli ikihukumiwa na Mungu.
Revelation 18:21-22
Babeli itaonekana lini tena baada ya hukumu yake?
Baada ya hukumu yake, Babeli hataonekana tena.
Revelation 18:23-24
Nini kilikutwa ndani ya mji mkuu Babeli ambacho alihukumiwa nacho?
Damu ya manabii, watakatifu na wote waliouliwa duniani ilikutwa.
Revelation 19
Revelation 19:1-2
Sauti kuu kutoka mbinguni ilisema nini kuhusu hukumu ya Mungu?
Sauti kuu kutoka mbinguni ilisema kwamba hukumu za Mungu ni kweli na haki.
Kwa nini Mungu alimhukumu kahaba mkuu?
Mungu alimhukumu kahaba mkuu kwa sababu aliharibu ulimwengu kwa uasherati wake na kumwaga damu za watumishi wa Mungu.
Revelation 19:3-4
Nini kitatokea kwa kahaba mkuu milele na milele?
Moshi utainuka kutoka kwa kahaba mkuu milele na milele.
Revelation 19:5-6
Watumishi wa Mungu wanaomcha waliambiwa kufanya nini?
Watumishi waliambiwa kumsifu yeye.
Revelation 19:7-8
Kwa nini sauti ilisema watumishi wa Mungu wanapaswa kushangilia na kufurahi sana?
Watumishi waliambiwa kushangilia kwa sababu sherehe ya harusi ya Mwanakondoo ilikuwa imefika.
Bibi harusi wa Mwanakondoo alivikwa nini?
Bibi harusi alivikwa kitani safi, ambayo ni matendo safi ya watakatifu wa Mungu.
Revelation 19:9-10
Malaika alisema kuwa ushuhuda wa Yesu unahusu nini?
Malaika alisema kuwa ushuhuda wa Yesu ilikuwa ni roho ya unabii.
Revelation 19:11-13
Ni nani jina la yule ambaye Yohana alimuona akipanda farasi mweupe?
Yohana aliona Neno la Mungu akipanda farasi mweupe.
Revelation 19:14-16
Neno la Mungu linawapigaje mataifa?
Kutoka katika kinywa cha Neno la Mungu kuna upanga mkali unaowapiga mataifa.
Nini kimeandikwa kwenye kanzu na paja la Neno la Mungu?
Kwenye kanzu na paja lake imeandikwa, "Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana".
Revelation 19:17-18
Ndege zilizokuwa zikipaa juu ziliitwa kula nini kwenye chakula kikuu?
Ndege waliitwa kula nyama za wafalme, majemedari, watu wakubwa, farasi na wapanda farasi, na watu wote.
Revelation 19:19-20
Mnyama na wafalme walipanga kufanya nini?
Walipanga kufanya vita na Neno la Mungu na jeshi lake.
Nini kilitokea kwa mnyama na nabii wa uongo?
Mnyama na nabii wa uongo wote walitupwa wakiwa hai kwenye ziwa la moto liwakalo salfa.
Revelation 19:21
Nini kilitokea kwa wale waliobaki waliopigana dhidi ya Neno la Mungu?
Waliobaki waliuliwa na upanga utokao kwenye kinywa cha Neno la Mungu.
Revelation 20
Revelation 20:1-3
Malaika aliyeshuka kutoka mbinguni alikuwa na kitu gani?
Malaika alikuwa na ufunguo wa shimo lisilo na mwisho na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
Shetani atabaki kifungoni kwa muda gani?
Shetani atabaki kifungoni kwa miaka elfu moja.
Malaika alifanya nini na Shetani?
Malaika alimtupa Shetani katika shimo lisilo na mwisho.
Shetani anapokuwa kifungoni hataweza kufanya nini?
Shetani hataweza kuwadanganya mataifa anapokuwa kifungoni.
Revelation 20:4
Nini kilitokea kwa wale waliokataa kupokea alama ya mnyama?
Wale waliokataa kupokea alama ya mnyama walikuja uzimani na kutawala pamoja na Kristo kwa miaka elfu moja.
Revelation 20:5-6
Wafu waliobaki watakuja uzimani wakati gani?
Wafu waliobaki watakuja uzimani baada ya miaka elfu moja kukamilika.
Wale walioshiriki katika ufufuo wa kwanza watafanya nini?
Wale walioshiriki katika ufufuo wa kwanza watakuwa makuhani wa Mungu na Kristo na watatawala pamoja naye kwa miaka elfu moja.
Revelation 20:7-8
Mwisho mwa miaka elfu moja Shetani atafanya nini?
Mwisho mwa miaka elfu moja, Shetani ataachiwa huru kwenda kuwadanganya mataifa.
Revelation 20:9-10
Nini kilitokea pale kambi ya waumini ilipozingirwa?
Kambi ya waumini ilipozingirwa, moto ulikuja kutoka mbinguni na kuwaangamiza Gogu na Magogu.
Nini kilifanywa kwa ibilisi katika kipindi hiki?
Ibilisi alitupwa katika ziwa liwakalo moto ili ateswe milele.
Revelation 20:11-12
Wafu walihukumiwa na kitu gani mbele ya kiti kikubwa cha enzi?
Wafu walihukumiwa kwa kile kilichoandikwa ndani ya vitabu, matokeo ya kile walichofanya.
Revelation 20:13-15
Kifo cha pili ni kipi?
Kifo cha pili ni ziwa la moto
Nini kilitokea kwa wale wote ambao hawakuandikwa katika Kitabu cha Uzima?
Wote ambao hawakupatikana wameandikwa katika Kitabu cha Uzima walitupwa katika ziwa la moto.
Revelation 21
Revelation 21:1-2
Yohana aliona nini kimetokea kwa mbingu na dunia ya kwanza?
Yohana aliona mbingu na dunia ya kwanza vimekwishapita.
Kitu gani kilichukua nafasi kwa mbingu na dunia ya kwanza?
Mbingu mpya na dunia mpya ilichukua nafasi ya mbingu na dunia ya kwanza.
Kitu gani kilishuka kutoka mbinguni?
Mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, vilishuka kutoka mbinguni.
Revelation 21:3-4
Sauti kutoka kiti cha enzi kilisema ya kwamba Mungu ataishi wapi?
Sauti ilisema ya kwamba Mungu ataishi na wanadamu.
Kitu gani kimekwisha pita?
Kifo, maombolezo, kulia, na maumivu yamekwisha pita sasa.
Revelation 21:5-6
Aliyeketi juu ya kiti cha enzi alijiita jina gani?
Yule aliyeketi juu ya kiti cha enzi alijiita Alfa na Omega, mwanzo na mwisho.
Revelation 21:7-8
Nini kinatokea kwa wasioamini, wazinzi na waabudu sanamu?
Wasioamini, wazinzi na waabudu sanamu wana sehemu yao katika ziwa kali liwakalo salfa.
Revelation 21:9-10
Bibi harusi, mke wa Mwana Kondoo ndiye nani?
Bibi harusi, mke wa Mwana kondoo, ni mji mtakatifu, Yerusalemu, unaoshuka kutoka mbinguni kwa Mungu.
Revelation 21:11-13
Nini kiliandikwa katika milango ya Yerusalemu mpya?
Majina ya makabila kumi na mawili ya wana wa Israeli yaliandikwa kwenye milango ya Yerusalemu mpya.
Revelation 21:14-15
Nini kiliandikwa juu ya misingi ya Yerusalemu mpya?
Majina ya mitume kumi na wawili wa Mwana Kondoo yaliandikwa juu ya misingi ya Yerusalemu mpya.
Revelation 21:16-17
Yerusalemu mpya uliwekwa katika umbo gani?
Yerusalemu mpya uliwekwa kama mraba.
Revelation 21:18-20
Mji ulijengwa na kitu gani?
Mji ulijengwa na dhahabu safi, kama kioo safi.
Revelation 21:21-22
Hekalu ni nini katika Yerusalemu mpya?
Hekalu katika Yerusalemu mpya ni Bwana Mungu na Mwana Kondoo.
Revelation 21:23-25
Chanzo cha taa katika Yerusalemu mpya ni nini?
Chanzo cha taa katika Yerusalemu mpya ni utukufu wa Mungu na Mwana Kondoo.
Revelation 21:26-27
Kitu gani hakitaingia ndani ya Yerusalemu mpya?
Hakuna kichafu kitakachoingia ndani ya Yerusalemu mpya.
Revelation 22
Revelation 22:1-2
Yohana aliona kitu gani kikitiririka kutoka katika kiti cha enzi?
Yohana aliona mto wa maji ya uzima ukitiririka kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu.
Majani ya mti wa uzima yalikuwa kwa ajili gani?
Majani ya mti wa uzima yalikuwa kwa ajili ya uponyaji wa mataifa.
Revelation 22:3-5
Hakutakuwa na nini tena katika mji?
Hakutakuwa na laana yoyote tena, na hapatakuwa na usiku tena.
Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo vitakuwa wapi?
Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo vitakuwa ndani ya mji.
Revelation 22:6-7
Mtu anatakiwa kufanya kitu gani ili abarikiwe na kitabu hiki?
Mtu anatakiwa kutii maneno ya unabii wa kitabu hiki ili abarikiwe.
Revelation 22:8-9
Malaika alimwambia Yohana afanye kitu gani alipojiangusha katika miguu ya malaika?
Malaika alimwambia Yohana kumwabudu Mungu.
Revelation 22:10-11
Kwa nini Yohana aliambiwa asiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki?
Yohana aliambiwa asiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki kwa sababu wakati ulikaribia.
Revelation 22:12-13
Bwana alisema atakuja pamoja na kitu gani atakaporudi?
Bwana alisema atakuja pamoja na ujira wake atakaporudi.
Revelation 22:14-15
Wanaotaka haki ya kula kutoka katika mti wa uzima wanapaswa kufanya kitu gani?
Wale wanaotaka haki ya kula kutoka katika mti wa uzima wanapaswa kuosha mavazi yao
Revelation 22:16-17
Yesu anasema ana uhusiano gani na Mfalme Daudi?
Yesu anasema yeye ni mzizi na uzao Mfalme Daudi.
Revelation 22:18-19
Nini kitatokea kwa yeyote atakayeongeza katika unabii wa kitabu hiki?
Yeyote atakayeongeza katika unabii wa kitabu hiki atapokea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
Nini kitatokea kwa yeyote atakayeondoa sehemu ya unabii wa kitabu hiki?
Yeyote atakayeondoa sehemu ya unabii wa kitabu hiki sehemu yake ya mti uzima utaondolewa.
Revelation 22:20-21
Maneno ya mwisho ya Yesu ni yapi katika kitabu hiki?
Maneno ya mwisho ya Yesu ni, "Ndiyo! naja upesi."
Neno la mwisho katika kitabu hiki ni lipi?
Neno la mwisho katika kitabu hiki ni "Amina".