Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

1 Corinthians

1 Corinthians 1

1 Corinthians 1:1-3

Nani aliyemwita Paulo na alimwitwa kuwa nani?

Yesu Kristo alimwita Paulo kuwa mtume

Paulo anatamani kanisa la Korintho lipokee nini kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo?

Paulo anatamani wapate neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo

1 Corinthians 1:4-6

Mungu ametajirisha kanisa la Korintho kwa namna gani?

Mungu amewatajirisha katika namna zote, katika usemi wote na katika maarifa yote.

1 Corinthians 1:7-9

kitu gani ambacho Kanisa la Korintho halikupungukiwa?

Hawatapungukiwa karama za rohoni

Kwa nini Mungu ataliimarisha kanisa la Korintho katika nyakati za mwisho?

Mungu atawaimarisha ili wasiwe na lawama katika siku ya Bwana wetu Yesu Kristo.

1 Corinthians 1:10-11

Paulo analisihi kanisa la Korintho kufanya nini?

Paulo anawasihi wakubaliane wote na wasigawanyike katika makundi, waungane katika nia moja na kusudi moja.

Watu wa Kloe walimtaarifu nini Paulo?

Watu wa Kloe walimtaarifu Paulo kuwa kulikuwa na mgawanyiko (ugomvi) miongoni mwa watu wa kanisa la Korintho.

1 Corinthians 1:12-13

Paulo alimaanisha nini kwa kusema mgawanyiko (ugomvi)?

Paulo alimanisha hivi: Kila mmoja husema, "Mimi ni wa Paulo," au "Mimi ni wa Apolo," au "Mimi ni wa Kefa," au "Mimi ni wa Kristo."

1 Corinthians 1:14-16

Kwa nini Paulo anamshukuru Mungu kwamba hakumbatiza yeyote miongoni mwao isipokuwa Krispo na Gayo?

Paulo anamshukuru Mungu kwa hili kwa sababu hii isengeliwapa nafasi ya kusema walibatizwa katika jina la Paulo.

Kwa nini Paulo anamshukuru Mungu kwamba hakumbatiza yeyote miongoni mwao isipokuwa Krispo na Gayo?

Paulo anamshukuru Mungu kwa hili kwa sababu hii isengeliwapa nafasi ya kusema walibatizwa katika jina la Paulo.

1 Corinthians 1:17

Kristo alimtuma Paulo kufanya nini?

Kristo alimtuma Paulo kuhubiri injili.

1 Corinthians 1:18-19

ujumbe wa msalaba ni nini kwa wote wanaokufa?

Ujumbe wa msalaba ni kama ujinga(upumbavu) kwa wale wanaokufa.

ujumbe wa msalaba ni nini miongoni mwa wale wanaookolewa na Mungu?

Ni nguvu ya Mungu miongoni mwa wale wanaookolewa na Mungu.

1 Corinthians 1:20-25

Mungu ameigeuza hekima ya ulimwengu kuwa nini?

Mungu ameigeuza hekima ya ulimwengu kuwa ujinga(upumbavu)

Kwa nini ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale wanaoamini kupitia upumbavu wa kuhubiri?

Ilimpendeza Mungu kufanya hivi kwa sababu ulimwengu katika hekima yake haukumjua Mungu

1 Corinthians 1:26-27

Wanagapi Mungu aliwaita waliokuwa na hekima katika viwango vya kibinadamu, au wenye nguvu au uzao wa kifalme?

Mungu hakuwaita wengi waliokuwa katika hali hii.

Kwa nini Mungu alichagua vitu vijinga na dhaifu vya ulimwengu?

Mungu alifanya hivyo ili kuwaaibisha wenye hekima na wenye nguvu.

1 Corinthians 1:28-29

Mungu alifanya nini ili asiwepo mtu mwenye sababu ya kujivuna mbele zake?

Mungu aliwachagua walio chini na waliodharauliwa katika ulimwengu na hata vitu vile vilivyohesabiwa si kitu.

Mungu alifanya nini ili asiwepo mtu mwenye sababu ya kujisifu mbele zake?

Mungu aliwachagua walio chini na waliodharauliwa katika ulimwengu na hata vitu vile vilivyohesabiwa si kitu.

1 Corinthians 1:30-31

Kwa nini wakristo walikuwa ndani ya Kristo Yesu?

Walikuwa ndani ya Kristo Yesu kwa sababu ya kile Mungu alifanya.

Kristo Yesu amekuwaje kwa ajili yetu?

Amekuwa kwetu hekima kutoka kwa Mungu- haki yetu, utakatifu, na ukombozi.

Kama tungelijisifu, tungejisifu kwa nani?

Yeyote anayejisifu, ajisifu katika Bwana.

1 Corinthians 2

1 Corinthians 2:1-2

Katika hali ipi Paulo alikuja kwa wakorintho alipohubiri kweli ya Mungu iliyofichika?

Paulo hakuja na maneno ya ujanja au hekima alipohubiri kweli ya Mungu iliyofichika.

Paulo aliamua kujua jambo gani alipokuwa miongoni mwa Wakorintho?

Paulo aliamua asijue chochote isipokuwa Kristo na kusulubiwa kwake.

1 Corinthians 2:3-5

Kwa nini ujumbe wa Paulo na kuhubiri kwake ulikuwa katika kumdhihirisha Roho na nguvu badala ya maneno ya kushawishi yenye hekima?

Ilikuwa hivyo ili imani yao isiwe katika hekima ya kibinadamu lakini katika nguvu ya Mungu.

Kwa nini ujumbe wa Paulo na kuhubiri kwake ulikuwa katika kumdhihirisha Roho na nguvu badala ya maneno ya kushawishi yenye hekima?

Ilikuwa hivyo ili imani yao isiwe katika hekima ya kibinadamu lakini katika nguvu ya Mungu.

1 Corinthians 2:6-7

Paulo na wenzake walizungumza kuhusu hekima gani?

Walizungumza kuhusu hekima ya Mungu katika ukweli uliofichika, -hekima ya Mungu iliyofichika ambayo Mungu alitujalia kabla ya nyakati za utukufu wetu.

1 Corinthians 2:8-9

Kama watawala wa nyakati za Paulo wangelijua hekima ya Mungu jambo gani wasingefanya?

Kama wale watawala wangejua hekima ya Mungu wasingemsulubisha Bwana wa Utukufu.

1 Corinthians 2:10-11

Paulo na wale waliokuwa naye walijuaje hekima ya Mungu?

Mungu aliwafunua mambo hayo kupitia Roho.

Nani anayejua mambo yaliyoko ndani ya Mungu?

Ni Roho wa Mungu ndiye ajuaye mambo yaliyo ndani ya Mungu.

1 Corinthians 2:12-13

Sababu mojawapo ni ipi Paulo na wenzake walipokea Roho ambaye anatoka kwa Mungu?

Walipokea Roho ambaye anatoka kwa Mungu ili kwamba waweza kujua vitu kamili tulivyopewa na Mungu.

1 Corinthians 2:14-16

Kwa nini mtu asiye wa rohoni hawezi kupokea au kujua vitu vile vya Roho wa Mungu?

Mtu asiye wa rohoni hawezi kuvipokea hivyo kwa sababu ni vya upuuzi kwake na hawezi kujua vyote kwa sababu vinatambuliwa kwa namna ya Kiroho.

Paulo alisema ni mawazo(nia) ya namna gani waliyonayo watu wanaoamini katika Yesu?

Paulo alisema wana mawazo(nia) ya Kristo

1 Corinthians 3

1 Corinthians 3:3-5

Kwa nini Paulo alisema waumini wa Korintho walikuwa bado wa mwilini?

Paulo alisema walikuwa bado wa mwilini kwa sababu wivu na majivuno yalionekana miongoni mwao.

Paulo na Apolo walikuwa akina nani kwa Wakorintho?

Walikuwa watumishi ambao kupitia wao Wakorintho walimwamini Kristo.

1 Corinthians 3:6-9

Nani anayekuza?

Mungu ndiye akuzaye.

1 Corinthians 3:10-11

Msingi ni nini?

Yesu Kristo ndiye msingi

1 Corinthians 3:12-13

Nini kitatokea katika kazi ya mtu anayejenga kwenye msingi wa Yesu Kristo?

Kazi yake itafunuliwa katika nuru na katika moto.

Nini kitatokea katika kazi ya mtu anayejenga kwenye msingi wa Yesu Kristo?

Kazi yake itafunuliwa katika nuru na katika moto.

Moto utaifanya nini kazi ya mtu?

Moto utathibitisha ubora wa kazi ya kila mtu

1 Corinthians 3:14-15

Ni nini kitatokea kama kitu chochote mtu alijenga kitabaki baada ya moto?

Mtu huyo atapokea tuzo.

Ni nini kitatokea kwa mtu ambaye kazi yake itaungua?

Mtu huyo atapata hasara, lakini yeye mwenyewe ataokolewa, kama kuopolewa kutoka motoni.

1 Corinthians 3:16-17

Sisi ni nani na nini kinaishi ndani yetu kama waumini katika Yesu Kristo?

Sisi ni Hekalu la Mungu na Roho wa Mungu anaishi ndani yetu.

Nini kitatokea kama mtu ataharibu hekalu la Mungu?

Mungu atamharibu mtu ambaye anaharibu hekalu la Mungu.

1 Corinthians 3:18-20

Paulo anasema nini kwa yule anayefikiri ni mwenye hekima katika nyakati hizi?

Paulo asema, "...awe "mjinga" ili anaweza kuwa mwenye hekima."

Bwana anajua nini kuhusu fikira za wenye hekima?

Bwana anajua kwamba fikira za wenye hekima ni ubatili.

1 Corinthians 3:21-23

Kwa nini Paulo anawaambia Waumini wa Korintho waache kujivuna kuhusu watu?

Aliwaambia kuacha majivuno, "Kwa kuwa vitu vyote ni vyenu," na kwa sababu, "...ninyi ni wa Kristo, and Kristo ni wa Mungu."

Kwa nini Paulo anawaambia Waumini wa Korintho waache kujivuna kuhusu watu?

Aliwaambia kuacha majivuno, "Kwa kuwa vitu vyote ni vyenu," na kwa sababu, "...ninyi ni wa Kristo, and Kristo ni wa Mungu."

1 Corinthians 4

1 Corinthians 4:1-2

Paulo anawaambia Wakorintho wanapaswa kuwahesabu Paulo na washirika wake kama nani?

Wakorintho wanapswa kuwahesabu wao kama watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za kweli za Mungu.

1 Corinthians 4:3-4

Paulo anasema hakimu wake ni nani?

Paulo anasema Bwana ndiye anayemhukumu.

1 Corinthians 4:5

Bwana atafanya nini atakapokuja?

Ataweka nuruni vitu vilivyofichika vya gizani na kufunua makusudi ya moyo.

1 Corinthians 4:6-7

Kwanini Paulo anaitumia kanuni hizi kwake yeye mwenyewe na kwa Apolo?

Paulo alifanya hivyo kwa ajili ya waumini wa Korintho kwamba wanaweza kujifunza maana ya usemi, "Usiende zaidi ya ilivyoandikwa." ili kwamba hakuna kati yao angeweza kufikiri kwa upendeleo kinyume na mwingine.

1 Corinthians 4:8-9

Kwa nini Paulo awatakia waumini wa Wakorintho kumiliki?

Paulo awatakia walimiliki ili kwamba Paulo na washirika wake wangeweza kumiliki pamoja nao.

1 Corinthians 4:10-11

Paulo na wenzake wanapingana na Waumini wa Korintho katika mambo matatu yapi?

Paulo asema, "Sisi tu wajinga kwa ajili ya Kristo,lakini mna busara katika Kristo. Sisi tudhaifu,lakini ninyi mna nguvu. Mnaheshimiwa, lakini sisi tunadharauliwa.

Paulo alieleza hali ya kimwili ya mitume kuwa ni ya namna gani?

Paulo alisema walikuwa na njaa na kiu, walivaa mavazi mbaya, walipingwa kikatiri na hawakuwa na makazi.

1 Corinthians 4:12-13

Kwa namna gani Paulo na washirika wenzake wanafanya wanapodharauliwa?

Wanapodharaliwa, wanabariki. Wanapoteswa, wanavumilia. Wanapotukanwa wanarudisha kwa upole.

1 Corinthians 4:14-16

Kwa nini Paulo aliandika mambo haya kwa waumini wa Korintho?

Aliawandikia kuwarekebisha kama watoto wake wapendwa.

Paulo anawaambia waumini wa Korintho wamuige nani?

Paulo anawaambia wamuige yeye mwenyewe.

1 Corinthians 4:17-18

Paulo alimtuma Timotheo kufanya kitu gani kwa waumini wa Korintho ili kuwakumbusha?

Paulo alimtuma Timotheo kwenda Korintho kuwakumbusha waumini juu ya njia za Paulo katika Kristo.

Baadhi ya waumini wa Korintho walikuwa waktenda kwa namna gani?

Baadhi yao walikuwa na majivuno, wakitenda kana kwamba Paulo hatawatembelea.

1 Corinthians 4:19-21

Ufalme wa Mungu upo katika nini?

ufalme wa Mungu upo katika nguvu.

1 Corinthians 5

1 Corinthians 5:1-2

Ni habari gani Paulo alisikia kuhusu kanisa katika Korintho?

Paulo alisikia kwamba kulikuwa na zinaa. Mmoja wao alikuwa amelala na mke wa baba yake.

Paulo alisema lazima kifanyike kitu gani kwa mtu aliyefanya dhambi na mke wa baba yake?

Yule aliyefanya dhambi na mke wa baba yake lazima aondolewe miongoni mwao.

1 Corinthians 5:3-5

Kwa namna gani na kwa nini mtu aliyefanya dhambi na mke wa baba yake angeondolewa?

Wakati kanisa la Korintho lilipokutana pamoja katika jina la Bwana Yesu walitakiwa kumkabidhi kwa shatani mtu aliyetenda dhambi ili mwili wake uharibiwe, na roho yake iweze kuokolewa katika siku ya Bwana.

Kwa namna gani na kwa nini mtu aliyefanya dhambi na mke wa baba yake angeondolewa?

Wakati kanisa la Korintho lilipokutana pamoja katika jina la Bwana Yesu walitakiwa kumkabidhi kwa shatani mtu aliyetenda dhambi ili mwili wake uharibiwe, na roho yake iweze kuokolewa katika siku ya Bwana.

1 Corinthians 5:6-8

Paulo analinganisha tabia mbaya na udhaifu na kitu gani?

Paulo anavilinganisha na hamira

paulo anatumia kitu gani kama sitiari kuhusu unyenyekevu na kweli

Anatumia mkate usiotiwa hamira kama sitiari kuhusu unyenyekevu na kweli.

1 Corinthians 5:9-10

Paulo aliwaambia waumini wa Korintho wasishirikiane na nani?

Paulo aliwaandikia wasishirikiane na watu wazinzi.

Paulo alimaanisha nini aliposema wasishirikiane na watu wazinzi?

Paulo hakumaanisha watu wazinzi wa hapa duniani. Kama ni hivyo ilipaswa kuondoka hapa duniani na kukaa mbali.

1 Corinthians 5:11-13

Paulo alimaanisha waumini wa Korintho wasishirikiane na nani?

Anamaanisha kwao wasichangamane na mtu yeyote aitwaye ndugu katika Kristo ambaye ni mzinzi, mwenye tamaa, mlevi, mtukanaji, dhalimu au mwabudu sanamu.

Waumini walipaswa kuwahukumu kina nani?

Walipaswa kuwahukumu waliokuwa ndani ya kanisa.

Nani anawahukumu walioko nje ya kanisa?

Mungu anawahukumu walio nje.

1 Corinthians 6

1 Corinthians 6:1-3

Paulo anasema watakatifu wa Korintho wanaweza kuhukumu kitu gani?

Paulo asema wanapaswa kuwa tayari kuamua matatizo kati ya watakatifu kuhusu mambo ya maisha haya.

Watakatifu watamhukumu nani?

Watakatifu wataihukumu dunia na malaika.

Watakatifu watamhukumu nani?

Watakatifu wataihukumu dunia na malaika.

Paulo anasema watakatifu wa Korintho wanaweza kuhukumu kitu gani?

Paulo asema wanapaswa kuwa tayari kuamua matatizo kati ya watakatifu kuhusu mambo ya maisha haya.

1 Corinthians 6:4-6

Wakrito wa Korintho wanakabiliana vipi na migogoro miongoni mwao?

Muumini mmoja anakwenda kumshitaki mahakamani muumini mwenzake, na kesi yao inasuluhishwa na hakimu asiyeamini.

1 Corinthians 6:7-8

Kuwepo migogoro miongoni mwa wakristo wa Korintho hii inaonyesha nini?

hii inaonesha kwamba wameshindwa.

1 Corinthians 6:9-11

Nani hataridhi ufalme wa Mungu?

Wasio haki, waasherati, waabudu sanamu, wazinzi, walawiti, wale wanaofanya ufilaji, wevi, wenye tamaa, walevi, wadhalimu na wanyang'anyi hawatauridhi Ufalme wa Mungu.

Nani hataridhi ufalme wa Mungu?

Wasio haki, waasherati, waabudu sanamu, wazinzi, walawiti, wale wanaofanya ufilaji, wevi, wenye tamaa, walevi, wadhalimu na wanyang'anyi hawatauridhi Ufalme wa Mungu

Ilikuwaje kwa waumini Wakorintho ambao hapa kwanza hawakuwa watakatifu?

Walitakaswa na kufanywa watakatifu; wakafanywa kuwa wenye haki na Mungu katika jina la Bwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu.

1 Corinthians 6:12-13

Ni vitu gani viwili Paulo asema hataviruhusu kumtawala?

Paulo asema hawezi kutawaliwa na chakula au zinaa.

Ni vitu gani viwili Paulo asema hataviruhusu kumtawala?

Paulo asema hawezi kutawaliwa na chakula au zinaa

1 Corinthians 6:14-15

Miili ya waumini ni viungo vya nini?

Miili yao ni viungo vya Kristo

Je waumini wanapswa kuwa na muunagniko na makahaba?

Hapana. Kmwe isitokee.

1 Corinthians 6:16-17

Kinatokea nini mtu apojiunganisha kwa kahaba?

Anakuwa mwili mmoja na huyo kahaba.

Kinatokea nini mtu apojiunganisha kwa kahaba?

Anakuwa mwili mmoja na huyo kahaba.

1 Corinthians 6:18

Watu wanafany dhambi dhidi ya nani wanapofanya zinaa?

Wanafanya dhambi dhidi ya miili yao wenyewe wanapofanya zinaa.

1 Corinthians 6:19-20

Kwanini waumini wanapaswa kumtukuza Mungu kwa miili yao?

Wanapaswa kumtukuza Mungu kwa miili yao kwa sababu miili yao ni hekalu la Roho Mtakatifu na kwa sababu walinunuliwa kwa thamani.

Kwanini waumini wanapaswa kumtukuza Mungu kwa miili yao?

Wanapaswa kumtukuza Mungu kwa miili yao kwa sababu miili yao ni hekalu la Roho Mtakatifu na kwa sababu walinunuliwa kwa thamani.

1 Corinthians 7

1 Corinthians 7:1-2

kwa nini kila mwaume anapaswa kuwa na mke wake na kila mwanamke kuwa na mume wake?

Kwa sababu ya majaribu, na kuongezeka kwa matendo mengi mabaya kila mwaume anapaswa kuwa na mke wake na kila mwanamke anapaswa kuwa na mume wake.

1 Corinthians 7:3-4

Je mke au mume anamamlaka juu ya mwili wake?

Hapana. Mume anamamlaka juu ya mwili wa mke wake na vile vile mke anamamlaka juu ya mwili wa mume wake.

1 Corinthians 7:5-7

Ni wakati gani mzuri kwa mume na mke kuacha kushiriki tendo la ndoa?

Ni vyema kama wote mume na mke watakubaliana na kupanga kipindi, ili kwamba wanaweza kudumu katika maombi.

1 Corinthians 7:8-9

Paulo anasema wajane na watu ambao hawajaolewa ni jambo gani zuri kufanya?

Paulo asema ni vizuri kwao kubaki bila kuolewa.

Watu ambao hawajaolewa na wajane wanaweza kuolewa katika hali hali gani?

Wanaweza kuolewa kama watapata tamaa na kushindwa kujizuia.

1 Corinthians 7:10-11

Bwana anatoa amri gani kwa wale walioolewa?

Mke hawapaswi kutengana mume wake.Kama atatengana na mume wake asiolewe au afanye mapatano na mumewe. Pia, mume hapaswi kumpa talaka mke wake.

Bwana anatoa amri gani kwa wale walioolewa?

Mke hawapaswi kutengana mume wake.Kama atatengana na mume wake asiolewe au afanye mapatano na mumewe. Pia, mume hapaswi kumpa talaka mke wake.

1 Corinthians 7:12-14

Muumini mwanamke au mwanamke anapaswa kumpa talaka mwenzi wake asiyeamini?

Kama mwanaume au mwamke asiyeamini anaridhika kuishi na wenzi wake, Wenzi mwamini hawapaswi kumpa talaka asiyeamini.

Muumini mwanamke au mwanamke anapaswa kumpa talaka mwenzi wake asiyeamini?

Kama mwanaume au mwamke asiyeamini anaridhika kuishi na wenzi wake, Wenzi mwamini hawapaswi kumpa talaka asiyeamini.

1 Corinthians 7:15-16

Muumini anapaswa kufanya nini kama mwenzi wake asiyeamini akiondoka?

Muumini atamruhusu mwenzi wake asiyeamini aondoke...

1 Corinthians 7:17-19

Paulo aliweka taratibu gani katika makanisa yote?

Utaratibu ulikuwa: Kila mmoja aishi maisha Bwana alivyomgawia, na namna Mungu alivyomwita.

Paulo alitoa ushauri gani kwa waliotahiriwa na wasiotahiriwa?

Paulo alisema wasiotahiriwa hawapaswi kutahiriwa na waliotahiriwa wasijaribu kuondoa alama za tohara zao.

1 Corinthians 7:20-24

Paulo alisema nini juu ya watumwa?

Kama walikuwa watumwa pale Mungu alipowaita, wasijali juu ya hilo, lakini kama wanaweza kuwa huru, wafanye hivyo. Hata kama walikuwa watumwa, kwa Bwana ni watu waliohuru. Hawapaswi kuwa watumwa wa watu.

Paulo alisema nini juu ya watumwa?

Kama walikuwa watumwa pale Mungu alipowaita, wasijali juu ya hilo, lakini kama wanaweza kuwa huru, wafanye hivyo. Hata kama walikuwa watumwa, kwa Bwana ni watu waliohuru. Hawapaswi kuwa watumwa wa watu.

1 Corinthians 7:25-26

Kwa nini Paulo alifikiri ni muhimu kwa mtu ambaye hajaoa abaki bila kuoa kama Paulo alivyokuwa?

Paulo alifikiri hivy kwa sababu ya hali ya hatari ilikuwa vizuri kwa mwanaume kuacha kuoa.

1 Corinthians 7:27-28

Nini waumini wanapswa kufanya kama wamefungwa na mwanamke kwa viapo vya ndoa?

Hawapaswi kutafuta uhuru kutoka katika viapo vyao kwa kuoa mwanamke.

Kwa nini Paulo anawaambia walio na uhuru kutoka kwa mke na ambao hawajaolewa,"usitafute mke"?

Alisema hivyo kwa sababu alitaka awatoe katika taabu mbalimbali ambazo watazipata wanaooa katika kuishi kwao.

1 Corinthians 7:29-31

Kwa nini wanaoshughulika na dunia wanapaswa kuwa kama hawajawhi kushughulika nayo?

Wanapaswa kufanya hivyo kwa sababu mfumo wa dunia hii unaelekea mwisho.

1 Corinthians 7:32-35

Kwa nini ni vigumu wakristo waliooa kutokuwa na mgawanyiko katika kujitoa kwa Bwana?

Ni vigumu kwa sababu mume mwamini au mke hushughulika kuhusu mambo ya dunia, jinsi ya kumpendeza mke au mume wake.

Kwa nini ni vigumu wakristo waliooa kutokuwa na mgawanyiko katika kujitoa kwa Bwana?

Ni vigumu kwa sababu mume mwamini au mke hushughulika kuhusu mambo ya dunia, jinsi ya kumpendeza mke au mume wake.

1 Corinthians 7:36-38

Nani anayefanya vizuri kuliko yule mtu anayemuoa mchumba wake?

Mtu anayechagua kuacha kuoa hufanya jambo nzuri zaidi.

1 Corinthians 7:39-40

Kwa muda gani mwanamke anafungwa kwa mume wake?

Amefungwa kwa mumewe kwa muda wote anapokuwa hai.

Kama mume wa mke muumini akifa, anaweza kuolewa na nani?

Anaweza kuolewa kwa yule anayetaka, lakini tu awe mtu aliye katika Bwana.

1 Corinthians 8

1 Corinthians 8:1-3

Katika sura hii je Paulo anaanza kuzungumzia swala gani?

Paulo anazungumzia swala la chakula kilichotolewa sadaka kwa miungu.

Nini matokeo ya maarifa na Upendo?

Maarifa humfanya mtu ajivune, lakini upendo humjenga.

1 Corinthians 8:4-6

Je miungu(sanamu) ni sawa na Mungu?

Hapana. Sanamu katika dunia hii si kitu,na hapana Mungu ila mmoja.

Mungu mmoja ni yupi?

Kuna Mungu mmoja tu ambaye ni Mungu Baba.vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake.

Bwana mmoja ni yupi?

Bwana mmoja ni Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na kwa yeye sisi tupo."

1 Corinthians 8:7

Nini hutokea mtu aliyekuwa mwabudu sanamu akila chakula kana kwamba kilikuwa kimetolewa sadaka kwa sanamu?

Dhamiri zao hupotoshwa kwa kuwa ni dhaifu.

1 Corinthians 8:8-10

Je chakula tunachokula hutufanya kuwa safi zaidi au wabaya zaidi kwa Mungu?

Chakula hakiwezi kututhibitisha kwa Mungu. Hatuna ubaya kama hatuli, na hatuna uzuri kama tukila.

Tufanye nini ili tuwe makini uhuru wetu usiwe sababu ya mtu aliye dhaifu kujikwaa?

Tunapaswa kuwa makini kwamba uhuru wetu usiwe sababu ya mtu aliye dhaifu katika imani kujikwaa.

1 Corinthians 8:11-13

Nini kinaweza kutokea kwa kaka au dada mwenye dhamiri dhaifu ikiwa wale wanaofahamu ukweli kuhusu asili ya sanamu hawatakuwa makini katika kutumia uhuru wao?

Kaka au dada mwenye dhamiri dhaifu anaweza kuharibiwa.

Tunafanya dhambi dhidi ya nani ikiwa tutasababisha kwa makusudi kaka au dada katika Kristo wajikwae kwa sababu ya dhamiri za dhaifu?

Tunafanya dhambi dhidi ya kaka au dada tunayesababisha ajikwae na tunafanya dhambi dhidi ya Mungu.

Tunafanya dhambi dhidi ya nani ikiwa tutasababisha kwa makusudi kaka au dada katika Kristo wajikwae kwa sababu ya dhamiri za dhaifu?

Tunafanya dhambi dhidi ya kaka au dada tunayesababisha ajikwae na tunafanya dhambi dhidi ya Mungu.

Paulo anasema atafanya nini kama chakula kinasababisha kaka au dada yake kujikwaa?

Paulo anasema kama chakula kinasababisha kaka au dada kujikwaa, hatakula tena nyama.

1 Corinthians 9

1 Corinthians 9:1-2

Paulo alitoa kielelezo gani kuwa yeye ni mtume?

Paulo anasema kwa sababu waumini wa Wakorintho walikuwa kazi yake katika Bwana, wao wanyewe walikuwa uthibitisho wa utume wake katika Bwana.

Paulo alitoa kielelezo gani kuwa yeye ni mtume?

Paulo anasema kwa sababu waumini wa Wakorintho walikuwa kazi yake katika Bwana, wao wanyewe walikuwa uthibitisho wa utume wake katika Bwana.

1 Corinthians 9:3-6

Paulo aliorodhesha kitu gani kama haki za mitume, ndugu wa Bwana, na Kefa?

Paulo alisema walikuwa na haki ya kul na kunywa, na haki ya kuambatana na mke ambaye ni muumini.

Paulo aliorodhesha kitu gani kama haki za mitume, ndugu wa Bwana, na Kefa?

Paulo alisema walikuwa na haki ya kula na kunywa, na haki ya kuambatana na mke ambaye ni muumini.

1 Corinthians 9:7-8

Paulo alitoa mifano gani kwa wale wanaopokea faida au malipo kutoka katika kazi zao?

Paulo anataja maaskari, mtu anayepanda shamba la mizabibu, na mtu chungaye kundi kama mifano ya wale watu wanaopokea faida au malipo kutoka katika kazi zao.

1 Corinthians 9:9-11

Paulo anatoa mifano gani kutoka katika sheria ya Musa ili kutetea wazo lake la kupokea faida au malipo kutoka katika kazi?

Paulo ananukuu amri, "usimfunge ng'ombe kinywa apulapo nafaka" kutetea hoja yake.

1 Corinthians 9:12-14

Kwa nini Paulo na wenzake hawakudai haki ya kupokea vitu kutoka kwa Wakorintho?

Paulo na wenzake hawakudai haki hii ili kusuwe na kipingamizi kwa injili ya Kristo.

Bwana aliagiza nini kwa wale wanaotangaza injili?

Bwana aliagiza kwamba wale wanaotangaza injili wanapaswa kupata mahitaji yao kulingana na injili.

1 Corinthians 9:15-18

Paulo alisema hatajivuna kuhusu kitu gani, na kwa nini hakuweza kujivuna?

Paulo alisema hawezi kujivuna juu ya kuhubiri injili kwa sababu alipaswa kuhubiri injili.

1 Corinthians 9:19-20

Kwa nini Paulo alikuwa mtumishi wa wote?

Paulo alikuwa mtumishi wa wote ili awalete watu wengi kwa Mungu.

Paulo alikuwa kama nani ili kuwapata Wayahudi?

Paulo alikuwa kama Myahudi ili kuwapata Wayahudi.

1 Corinthians 9:21-23

Paulo alikuwaje ili kuwapata wale waliokuwa nje ya sheria?

Paulo alikuwa kama wale walio nje ya sheria ili kuwapata walio nje ya sheria.

Kwa nini Paulo alifanya mambo yote kwa ajili ya injili?

Alifanya hivi iliaweze kushiriki katika baraka za injili.

1 Corinthians 9:24-27

Paulo alisema kukimbia kwa namna gani?

Paulo alisema kukimbia ili kupata tuzo.

Paulo alikuwa akikimbia ili kupata tuzo ya namna gani?

Paulo alikuwa akikimbia ili kupoke tuzo isiyoharibika.

Kwa nini Paulo aliutiish mwili wake na kuufanya kama mtumwa?

Paulo alifanya hivyo baada ya kuwa amewahubiria wengine, yeye mwenyewe asije kukataliwa.

1 Corinthians 10

1 Corinthians 10:1-4

Ni mambo gani ya kufanana yaliwapata baba zao wakati wa Musa?

Wote walikuwa chini ya wingu na wakapita katika bahari. Wote walibatizwa wawe wa Musa ndani ya wingu na ndani ya bahari, na wote walikua chakula cha roho kile kile, wote walikunywa kinywaji kile kile cha roho.

Ni mambo gani ya kufanana yaliwapata baba zao wakati wa Musa?

Wote walikuwa chini ya wingu na wakapita katika bahari. Wote walibatizwa wawe wa Musa ndani ya wingu na ndani ya bahari, na wote walikua chakula cha roho kile kile, wote walikunywa kinywaji kile kile cha roho.

Mwamba wa roho uliowafuata baba zao ulikuwa nani?

Kristo alikuwa ndiyo huo mwamba uliowafuata.

1 Corinthians 10:5-8

Kwa nini Mungu hakupendezwa na baba zao wakati wa Musa?

Hakupendezwa nao kwa sababu baba zao walitamani mambo maovu.

1 Corinthians 10:9-10

Mungu aliwaharibu kwa njia gani watu ambao hawakutii?

Mungu aliwaharibu kwa nyoka, na kwa malaika wa mauti.

Mungu aliwaharibu kwa njia gani watu ambao hawakutii?

Mungu aliwaharibu kwa nyoka, na kwa malaika wa mauti.

1 Corinthians 10:11-13

Kwa nini mambo haya yalitokea na kwa nini yaliandikwa?

Yalitokea kama mifano kwetu na yaliandikwa ili kutuongoza

limetokea jaribu lolote ambalo ni la pekee kwetu?

Hakuna jaribu lilotupata ambalo si la kawaida kwa wanadamu wote.

Mungu amefanya nini kutuwezesha kuvumilia majaribu?

Ametupatia njia ya kutokea kwa hiyo tunaweza kuvumila majaribu.

1 Corinthians 10:14-19

Paulo anawaonya waumini wa Koritho kitu gani wakikimbie?

Anawaonya wakimbie kutoka katika ibada ya sanamu.

Ni kikombe gani cha baraka waumini hukibariki na mkate gani wanaumega?

Kikombe ni ushirika katika damu ya Kristo. Mkate ni ushirka katika mwili wa Kristo.

1 Corinthians 10:20-22

Wapagani wa mataifa hutoa sadaka zao kwa nani?

Wanatoa vitu vyao kwa mapepo na si kwa Mungu.

Kwa kuwa Paulo hakutaka waumini wa Korintho kushirikiana na mapepo, jambo gani anawaambia hawawezi kufanya?

Paulo anawaambia hawawezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mapepo na hawawezi kuwa na ushirika katika meza ya Bwana na katika meza ya mapepo.

Kwa kuwa Paulo hakutaka waumini wa Korintho kushirikiana na mapepo, jambo gani anawaambia hawawezi kufanya?

Paulo anawaambia hawawezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mapepo na hawawezi kuwa na ushirika katika meza ya Bwana na katika meza ya mapepo.

Sisi waumini wa Bwana tunapata hatia gani kama tukishirikiana na mapepo?

Tunapata hatia kwa kumkasirisha Bwana kwa kumtia wivu.

1 Corinthians 10:23-24

Je tunapaswa kutafuta mazuri yetu wenyewe?

Hapana. Badala yake kila mmoja atafute mazuri kwa ajili ya jirani yake.

1 Corinthians 10:25-27

Je unapaswa kufanya nini kama mtu asiyeamini atakualika kula na unataka kwenda?

Unapaswa kula chochote akupacho bila kuuliza maswali ya dhamiri.

1 Corinthians 10:28-30

kama asiyeamini atakupa chakula na unapotaka kula anakuambia kimetolewa kwenye sadaka ya wapagani kwa nini hupaswi kula?

Hupaswi kula kwa ajili ya mtu aliyekupa taarifa na kwa ajili ya dhimiri za watu wengine wengine.

kama asiyeamini atakupa chakula na unapotaka kula anakuambia kimetolewa kwenye sadaka ya wapagani kwa nini hupaswi kula?

Hupaswi kula kwa ajili ya mtu aliyekupa taarifa na kwa ajili ya dhimiri za watu wengine wengine.

1 Corinthians 10:31-33

Tunapaswa kufanya nini kwa ajili ya utukufu wa Mungu?

Tunapaswa kufanya mambo yote, ikiwa pamoja na kula na kunywa, kwa utukufu wa Mungu.

Kwa nini hatupaswi kuwa kikwazo kwa Wayahudi au Wayunani au kwa kanisa la Mungu?

Tunapaswa tusiweke kikwako chochote kwao ili waweze kuokolewa.

Kwa nini hatupaswi kuwa kikwazo kwa Wayahudi au Wayunani au kwa kanisa la Mungu?

Tunapaswa tusiweke kikwako chochote kwao ili waweze kuokolewa.

1 Corinthians 11

1 Corinthians 11:1-4

Paulo aliwaambia waumini wa Korintho wamuige nani?

Paulo aliwaambia kumuiga yeye.

Paulo alimuiga nani?

Paulo alimuiga Kristo

Kwa jambo gani Paulo aliwasifu waumini wa Korintho?

Paulo aliwasifu kwa kumkumbuka katika kila jambo na kwa kushika mapokea kama alivyowafundisha.

Kichwa cha Kristo ni nani?

Mungu ni kichwa cha Kristo

Kichwa cha mwanaume ni nani?

Kristo ni kichwa cha kila mwanaume.

Kichwa cha mwanamke ni nani?

Mwanaume ni kichwa cha mwanamke.

Hutokea nini mwanaume anaposali huku amefunika kichwa chake?

Hukiaibisha kichwa chake, kama anaomba huku amefunika chichwa.

1 Corinthians 11:5-6

Hutokea nini mwanamke anaposali huku hajafunika kichwa chake?

Mwanamke yeyote anayesali bila kufunika kichwa chake hukiaibisha kichwa chake.

1 Corinthians 11:7-8

Kwa nini mwanaume hapaswi kufunika kichwa chake?

Hapaswi kufunika kichwa chake kwa sababu yeye ni taswira na utukufu wa Mungu

1 Corinthians 11:9-10

Mwanamke aliumbwa kwa ajili ya nani?

Mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanaume

Kulikuwa na desturi gani kwa Paulo, washirika wake na makanisa ya Mungu kuhusu wanawake wanapoomba?

Ilikuwa ni desturi kwa wanawake kuomba wakiwa wamefunika vichwa vyao.

1 Corinthians 11:11-12

Kwa nini wanaume na wanawake wanategemeana?

Mwanamke anatoka kwa mwanaume na mwanaume anatoka kwa mwanamke

Kwa nini wanaume na wanawake wanategemeana?

Mwanamke anatoka kwa mwanaume na mwanaume anatoka kwa mwanamke

1 Corinthians 11:13-16

Kulikuwa na desturi gani kwa Paulo, washirika wake na makanisa ya Mungu kuhusu wanawake wanapoomba?

Ilikuwa ni desturi kwa wanawake kuomba wakiwa wamefunika vichwa vyao.

Kulikuwa na desturi gani kwa Paulo, washirika wake na makanisa ya Mungu kuhusu wanawake wanapoomba?

Ilikuwa ni desturi kwa wanawake kuomba wakiwa wamefunika vichwa vyao.

1 Corinthians 11:17-19

Kwa nini lazima iwepo migogoro miongoni mwa Wakristo wa Korintho?

Lazima iwepo migogoro kati yao ili kwamba wajulikane waliokubaliwa.

1 Corinthians 11:20-22

Nini kilikuwa kikitokea wakati Kanisa la Korintho walipokuja kula pamoja?

Walipokula pamoja kila mmoja alikula chakula chake mwenyewe kabla wengine hawajala. Mmoja alibaki njaa na mwingine alilewa.

1 Corinthians 11:23-24

Usiku ule aliposalitiwa Bwana alisema nini baada ya kuuvunja mkate?

Alisema, "Huu ndio mwili wangu, ulio kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi."

siku ule aliposalitiwa Bwana alisema nini baada ya kuuvunja mkate?

Alisema, "Huu ndio mwili wangu, ulio kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi."

1 Corinthians 11:25-26

Bwana alisema nini alipokichukua kikombe baada ya chakula cha jioni?

Alisema,"Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi mara nyingi kila mywapo, kwa kunikumbuka mimi."

Bwana alisema nini alipokichukua kikombe baada ya chakula cha jioni?

Alisema, "Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi mara nyingi kila mywapo, kwa kunikumbuka mimi."

1 Corinthians 11:27-32

Kwa mtu hapaswi kula mkate na kunywa kikombe cha Bwana kwa namna isiyostahili?

Kufanya hivy kunaleta hatia ya mwili na damu ya Bwana. Unakula na kunywa hukumu yako mwenyewe.

Kilitokea nini kwa watu wengi katika kanisa la Korintho kwa wale waliokula mkate na kunywa kikombe cha Bwana kwa namna isiyostahili?

Wengi wao walikuwa wagonjwa na dhaifu na baadhi yao walikufa.

1 Corinthians 11:33-34

Paulo anawaambia waumini Korintho wafanye nini wanapokutanika kula pamoja?

Anawaambia wasubiliane.

1 Corinthians 12

1 Corinthians 12:1-3

Paulo anataka Wakristo wa Korintho wafahamu kitu gani?

Paulo anataka wafahamu kuhusu karama za rohoni.

Mtu anayenena kwa Roho wa Mungu kitu gani hawezi kusema?

Hawezi kusema, "Yesu amelaaniwa"

Mtu anaweza kusema "Yesu ni Bwana" kwa namna gani?

Mtu anaweza kusema, "Yesu ni Bwana" kwa Roho Mtakatifu.

1 Corinthians 12:4-6

Mungu humwezesha kila muumini kufanya nini?

Mungu humwezesha kila muumini kwa karama tofauti, kwa huduma tofauti na kwa kazi mbalimbali.

Mungu humwezesha kila muumini kufanya nini?

Mungu humwezesha kila muumini kwa karama tofauti, kwa huduma tofauti na kwa kazi mbalimbali.

1 Corinthians 12:7-8

Kwa nini hupewa ufunuo wa Roho?

Hupewa ufunuo kwa faida ya wote.

1 Corinthians 12:9-11

Baadhi ya karama za Roho zinazotolewa ni zipi?

Baadhi ya karama ni imani, karama ya uponyaji, matendo ya miujiza, unabii, uwezo wa kutofautisha roho, aina tofauti za lugha na tafasiri za lugha.

Baadhi ya karama za Roho zinazotolewa ni zipi?

Baadhi ya karama ni imani, karama ya uponyaji, matendo ya miujiza, unabii, uwezo wa kutofautisha roho, aina tofauti za lugha na tafasiri za lugha.

Ni nani anayechagua karama ambazo kila mmoja hupokea?

Roho hutoa karama kwa kila mmoja kama apendavyo Yeye.

1 Corinthians 12:12-17

Katika ubatizo gani wakristo wote walibatizwa?

Tulibatizwa katika mwili mmoja na tulinyweshwa katika Roho moja.

1 Corinthians 12:18-20

Nani alibuni na kupangilia sehemu za mwili?

Mungu alipangilia kila sehemu za mwili kama alivyo buni.

1 Corinthians 12:21-24

Tunaweza kufanya bila viungo vya mwili vinavyoonekana havuna heshima sana?

Hapana. Viungo vya mwili vinavyoonekana havina heshima sana ni vya muhimu zaidi.

Mungu amefanya nini katika viungo vya mwili ikiwa ni pamoja na vile vyenye heshima kidogo?

Mungu ameviunganisha kwa pamoja viungo vyote vya mwili, na amevipa heshima zaidi vile visivyo heshimiwa.

1 Corinthians 12:25-27

Kwa nini Mungu alivipa heshima zaidi viungo vya mwili visivyo heshimiwa?

Alifanya hivi ili kusiwe na mugawanyiko katika mwili, lakini viungo vinapaswa kujaliana kila mmoja na mwezie kwa upendo sawa.

1 Corinthians 12:28-29

Mungu amemweka nani katika kanisa

Katika kanisa Mungu ameweka kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, wale wenye matendo ya miujiza, karama ya uponyaji, wale wasaidiao, viongozi, na wale wanaonena lugha mbali mbali.

1 Corinthians 12:30-31

Paulo anawaambi wakristo wa Korintho watafute nini?

Anawaambia watafute karama zilizo kuu.

1 Corinthians 13

1 Corinthians 13:1-3

Paulo angekuwaje kama atanene kwa lugha za wanadamu na malaika bila kuwa na upendo?

Anekuwa sahaba iliayo au upatu uvumao.

Paulo angekuwaje kama angekuwa na karama ya unabii, kujua siri zote na maarifa na kuwa imani kuu lakini asiwe na upendo?

Angekuwa si kitu.

Paulo angewezaje kutoa mali zake zote kuwalisha masikini na kutoa mwili wake uchomwe moto n bado asipate faida?

Kama hakuwa na upendo asingepata chochote ingawa angefanya mambo hayo yote.

1 Corinthians 13:4-7

Baadhi ya sifa za upendo ni zipi?

Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi au ukorofi. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu haraka, wala hauhesabu mabaya. Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli. Upendo huvumilia mambo yote; huamini mambo yote, una ujasiri katika mambo yote, na hustahimili mambo yote.

Baadhi ya sifa za upendo ni zipi?

Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi au ukorofi. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu haraka, wala hauhesabu mabaya. Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli. Upendo huvumilia mambo yote; huamini mambo yote, una ujasiri katika mambo yote, na hustahimili mambo yote.

1 Corinthians 13:8-10

Baadhi ya mambo yatakayo koma ni yapi?

Unabii, maarifa na kila kitu kisicho kikamilifu kitakoma na lugha zitakoma.

Kitu gani hakitakoma?

Upendo hautakoma.

Baadhi ya mambo yatakayo koma ni yapi?

Unabii, maarifa na kila kitu kisicho kikamilifu kitakoma na lugha zitakoma.

1 Corinthians 13:11-13

Paulo anasema alifanya nini alipokuwa mtu mzima?

Paulo anasema alipokuwa mtu mzima aliachana na mambo ya kitoto.

Mambo matatu yatadumu, lipi kati ya matatu ni kuu zaidi?

Imani, tumaini, na upendo vitadumu. Kuu zaidi katika haya ni upendo.

1 Corinthians 14

1 Corinthians 14:1-6

Paulo anasema tunapaswa kutamani karama gani ya kiroho?

Paulo anasema tunapaswa kutamani sana karama ya kutoa unabii.

Mtu akinena kwa lugha hunena kwa nani?

Huwa haneni na watu bali huzungumza na Mungu.

Mtu anayetoa unabii humjenga nani na mtu anayenena kwa lugha humjenga nani?

Anayetoa unabii huwajenga watu, lakini anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe.

Mtu anayetoa unabii humjenga nani na mtu anayenena kwa lugha humjenga nani?

Anayetoa unabii huwajenga watu, lakini anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe.

1 Corinthians 14:7-11

Paulo anailinganish na nini hotu isiyoeleweka?

Paulo anailinganisha na chombo kama filimbi au kinubi visivyoweza kutoa sauti inatambulika, na anafananisha na tarumbeta inayotoa sauti isiyojulikana.

Paulo anailinganish na nini hotu isiyoeleweka?

Paulo anailinganisha na chombo kama filimbi au kinubi visivyoweza kutoa sauti inatambulika, na anafananisha na tarumbeta inayotoa sauti isiyojulikana.

1 Corinthians 14:12-14

Paulo anasema wakristo wa Korintho wanapaswa watamani zaidi kufanya nini?

Anasema wanapaswa kutamani zaidi kulijenga kanisa.

Anayenena kwa lugha anapaswa aombe kwa ajili ya nini?

Anapaswa aombe ili aweze kutafasiri.

Paulo anasema apoomba kwa lugha akili na roho yake zilifanya nini?

Paulo alisema kama angeomba kwa lugha, roho yake iliomba, lakini akili yake haikuwa na matunda.

1 Corinthians 14:15-16

Paulo amasema alitaka kuimba na kuomba kwa namna gani?

Paulo alisema alitaka kuomba na kuimba kwa roho na kwa akili.

1 Corinthians 14:17-21

Paulo alisema atafanya nini zaidi kuliko kunena maneno elfu kumi katika lugha?

Paulo alisema angezungumza maneno matano kwa ufahamu ili kuwafundisha wengine.

1 Corinthians 14:22-23

Kunena kwa lugha na kutoa unabii ni ishara kwa nani?

Kunena kwa lugha ni ishara kwa wasioamini na kutoa unabii ni ishar kwa waaminiao.

Wageni na wasioamini wangesema nini kama watakuja kanisani na kukuta watu wote wananena kwa lugha?

Wangesema kuwa waumini wanawazimu.

1 Corinthians 14:24-25

Paulo anasema kingetokea nini kama wote kanisani watatoa unabii na asiyeamini au mgeni akaja kanisani?

Paulo anasema asiyeamini au mgeni atashawishiwa kwa mambo yote anayoyasikia, na atahukumiwa na yote yanayosemwa.

Asiyeamini au mgeni angefanya nini kama unabii unaotolewa unafunua siri za moyo wake?

Angeanguka kufudifudi, na kumwabudu Mungu na kukiri kwamba Mungu yupo miongoni mwao.

1 Corinthians 14:26-28

Paulo anatoa mafundisho gani kwa wale wanaonena kwa lugha katika masanyiko ya waumini?

Anasema watu wawili au watu tu wanatakiwa kunena, kwa kupeana zamu. Kama hakuna mtu wa kutafasiri kila mmoja wao anatakiwa kukaa kimya ndani ya kanisa.

Paulo anatoa mafundisho gani kwa wale wanaonena kwa lugha katika masanyiko ya waumini?

Anasema watu wawili au watu tu wanatakiwa kunena, kwa kupeana zamu. Kama hakuna mtu wa kutafasiri kila mmoja wao anatakiwa kukaa kimya ndani ya kanisa.

1 Corinthians 14:29-33

Paulo anatoa mafundisho gani kwa manabii wakati kanisa linapokutanika pamoja?

Paulo anasema manabii wawili au watatu wahutubu, na wengine wasikilize kwa kupambanua kinachosemwa. kama nabii mwingine anamaono, yule aliyekuwa akinena anapaswa kunyamaza.

Paulo anatoa mafundisho gani kwa manabii wakati kanisa linapokutanika pamoja?

Paulo anasema manabii wawili au watatu wahutubu, na wengine wasikilize kwa kupambanua kinachosemwa. kama nabii mwingine anamaono, yule aliyekuwa akinena anapaswa kunyamaza.

1 Corinthians 14:34-36

Paulo alisema wanawake hawaruhusiwi kuongea sehemu gani?

Paulo alisema wanawake hawaruhusiwi kuongea kanisani.

Paulo alisema wanawake wafanye nini kama wanatamani kujifunza jambo lolote?

Paulo aliwaambia wawaulize waume zao nyumbani.

Watu walionaje kama mwanamke aliongea kanisani.

Waliona kuwa ni swala la kuleta aibu.

1 Corinthians 14:37-38

Paulo alisema wale wanaofikiri ni manabii au wa tu wa kiroho wanapaswa kukiri nini?

Paulo alisema wanapaswa kukiri kuwa mambo aliyowaandikia waumini wa Korintho yalikuwa ni amri ya Bwana.

1 Corinthians 14:39-40

Kila kitu kanisani kinapaswa kutendeka kwa namna gani?

Mambo yote yanapaswa yafanyike kwa uzuri na kaika utaratibu.

1 Corinthians 15

1 Corinthians 15:1-2

Paulo nawakumbusha nini akina kaka na akina dada?

Anawakumbusha wao kuhusu injli aliyoitangaza kwao.

Shariti gani walipaswa kulitimiza watu wa Korintho kama walitaka waokolewe kwa injili ayowahubiri Paulo?

Paulo aliwaambia wangeokolewa kama walishikilia kwa udhabiti neno alilowahibiria.

1 Corinthians 15:3-7

Sehemu gani ya injili amabayo ilikuwa kipaumblele?

Sehemu ambayo ilikwa ya muhimu kwanza ilikuwa kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na maandiko na kwamba alizikwa, na kwamba alifufuliwa siku ya tatu kulingana na maandiko.

1 Corinthians 15:8-11

Yesu alimtokea nani baada ya kuwa amefufuliwa kutoka kwa wafu?

Baada ya kuwa amefufuliwa kutoka kwa wafu, Kristo alimtokea Kefasi, wale kumi na wawili, akina kaka na akina dada zaidi ya miatano kwa mara moja, Yakobo, mitume wote na Paulo.

Kwa nini Paulo alisema alikuwa mdogo miongoni mwa mitume wengine?

Alisema hivyo kwa sababu alilitesa kanisa la Mungu.

1 Corinthians 15:12-17

Paulo alitoa dokezo gani kwa baadhi ya waumini wa Wakorintho waliokuwa wakisema kuhusu ufufuo?

Alidokeza kuwa baadhi yao walikuwa wakisema hakuna ufufuo kutoka kwa wafu.

Kama hakuna ufufuo wa wafu Paulo anasema jambo gani pia linaweza kuwa la kweli?

Paulo anasema kama ni hivyo hata Kristo pia hakufufuka katika wafu na mahubiri ya Paulo na wenzake ni ubatili na imani ya Wakorintho ni ya bure.

Kama hakuna ufufuo wa wafu Paulo anasema jambo gani pia linaweza kuwa la kweli?

Paulo anasema kama ni hivyo hata Kristo pia hakufufuka katika wafu na mahubiri ya Paulo na wenzake ni ubatili na imani ya Wakorintho ni ya bure.

1 Corinthians 15:18-19

Kama kristo hajafufuka, nini kilitokea kwa wale waliokufa katika Kristo?

Wameangamia.

Paulo anasema kama tunaujasiri katika maisha haya kwa tumaini lililo katika Kristo jambo gani lingekuwa la kweli?

Kama ndivyo, Paulo anasema hivyo kwa watu wote, sisi ni wakuhurumiwa zaidi.

1 Corinthians 15:20-21

Paulo anamuitaje Kristo?

Anamuita Kristo, "tunda la kwanza la wale ambao wamekufa".

1 Corinthians 15:22-23

Ni mtu gani ambaye kifo kilikuja duniani kupitia kwake na mtu gani ambaye ufufuo wa wafu ulikuja kupitia kwake?

Adamu alileta kifo katika dunia na kwa kupitia Kristo wote tutafanywa hai; fufuliwa.

Wakati gani wale walio katika Kristo watafanywa hai?

Hii atatokea Kristo atakapokuja.

1 Corinthians 15:24-26

Nini kitatokea mwishoni?

Kristo atakabidhi ufalme wa mbinguni kwa Mungu Baba, pale atakapo komesha utawala zote na mamlaka na nguvu.

Kristo atatawala kwa muda gani?

Ni lazima atawale ampaka atakapowaweka chini ya miguu yake maadui wake wote.

Adui wa mwisho kuharibiwa ni nani?

Adui wa mwisho kuharibiwa ni kifo

1 Corinthians 15:27-32

Nani ambaye hajajumlishwa pale inaposema, "ameweka kila kitu chini ya miguu yake."

Ni yule anayeweka kila kitu chini ya Mwana (yeyemwenyewe) hajajumlishwa kama kuwa chini (kwa mwana).

Mwana atafanya nini ili Mungu Baba awe yote katika yote?

Mwana mwenyewe atatiishwa chini yake yeye aviwekaye chini yake vitu vyote.

1 Corinthians 15:33-34

Paulo anawaagiza Wakorintho kufanya nini?

Anawaagiza kuwa kiasi, kuishi katika haki, na wasiendelee kutenda dhambi.

Kitu gani Paulo alisema ni cha aibu kwa Wakorintho

Alisema baadhi yao hawakuwa na maarifa ya Mungu.

1 Corinthians 15:35-36

Paulo anafananisha ufufuo wa wafu na kitu gani?

Anafananisha na mbengu iliyo pandwa.

Paulo anafananisha ufufuo wa wafu na kitu gani?

Anafananisha na mbengu iliyo pandwa

Nini hutokea kabla ya mbegu kuota?

Ni lazima ife.

1 Corinthians 15:37-39

Je mbegu iliyochipuka iliyopandwa inafanana na mwili (mmea) ambao umetoka katika mbegu?

Kile ulichopanda hakifanani na vile utakavyo kuwa mwili hapo baadaye.

Je miili yote ni sawa?

Hapana. Miili yote haifanani, mwili wa mwanadamu, wanyama, ndege na samaki vyote vinatofautiana.

1 Corinthians 15:40-41

Kuna aina zingine za miili?

Kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani.

Je jua,mwezi na nyota vyote viana utukufu sawa?

Kuna utukufu mmoja wa jua, na utukufu mwingine wa mwezi, na utukufu mwingine wa nyota. Kwa kuwa nyota moja inatofautiana na nyota nyingine katika utukufu.

1 Corinthians 15:42-44

Ni kwa namna gani miili yetu iliyoharibika inapandwa?

Inapandwa kama miili ya asili, katika kutoheshimiwa na udhaifu

Hali yetu ikoje pale tunapofufuliwa kutoka kwa wafu?

Kile kinacho fufuliwa ni mwili wa kiroho usioharibika; uliofufuliwa katika utukufu na nguvu.

1 Corinthians 15:45-46

Mwanadamu wa kwanza Adamu alifanyika nini?

Alifanyika roho inayoishi.

Adamu wa mwisho alifanyika nini?

alifanyika roho itoayo uhai.

1 Corinthians 15:47-49

Mtu wa kwanza na mtu wa pili walitoka wapi?

Mtu wa kwanza ni wa dunia, alitengenezwa kwa mavumbi. Mtu wa pili ni wa mbinguni.

Tumechukua sura ya nani na tutachukua sura ya nani?

Kama vile tulivyochukua sura ya mtu anayetokana na mavumbi, pia tuatachukua sura ya mtu wa mbinguni.

1 Corinthians 15:50-51

Ni kitu gani hakiwezi kuurithi ufalme wa Mungu?

Mwili na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu.

Nini kitatokea kwetu sote?

Wote tutabadilishwa

1 Corinthians 15:52-53

Ni lini na kwa haraka kiasi gani tutabadilishwa?

Ni pale sauti ya mwisho ya mbiu itakapolia tutabadilishwa hapo hapo, katika kufumba na kufumbua.

1 Corinthians 15:54-55

Nini kitatokea wakati huu uharibifu umewekwa katika kutokuharibika na huu ubinadamu umewekwa katika milele?

Kifo kitamezwa na ushindi.

1 Corinthians 15:56-57

Uchungu wa kifo ni nini na nguvu ya dhambi ni nini?

Uchungu wa kifo ni dhambi na nguvu ya kifo ni sheria.

Mungu anatupa ushindi kupitia kwa nani?

Mungu anatupatia ushindi kupitia kwa Bwana Yesu Kristo .

1 Corinthians 15:58

Ni sababu gani Paulo anawaambia akina kaka na akina dada Wakorintho kusimama imara, wasiyumbe, kila siku kwa wingi katika kazi ya Bwana.?

Anawaambia kufanya hivi kwa sababu wanajua kuwa kazi yao katika Bwana sio bure.

1 Corinthians 16

1 Corinthians 16:1-2

Paulo alimwelekeza nani kwa njia ileile kama katika Korintho kuhusu michango kwa ajili ya watakatifu?

Paulo aliyaelekeza makanisa ya Galatia katika njia ileile kama katika kanisa la Koritho.

Paulo aliwaelekeza kanisa la Korintho wakusanye michango kwa namna gani?

Aliwaambia kuwa katika siku ya kwanza ya wiki, kila mmoja wao aweke kitu fulani kando na kukihifadhi, kama muwezavyo, ili kwamba kusiwe na michango Paulo atakapo kuja .

1 Corinthians 16:3-4

Sadaka ilikuwa inaenda kwa nani?

Ilikuwa inaenda kwa watakatifu wa Yerusalemu.

1 Corinthians 16:5-6

Ni lini Paulo alikuwa aende katika kanisa la Koritho?

Alisema atakwenda pale atakapo safiri kupitia Makedonia.

1 Corinthians 16:7-9

Kwa nini Paulo hakutaka kuwaona watakatifu wa Korintho kwa haraka katika muda mfupi?

Paulo alitaka kuwatembele na kukaa nao kwa muda mrefu, kama Bwana angeruhusu.

Kwa nini Paulo alitaka kukaa Efeso hadi Pentekoste?

Paulo alikaa Efeso kwa sababu kulikulifunguliwa mlango mpana kwa ajili yake, na kulikuwa na maadui wengi.

1 Corinthians 16:10-14

Timotheo alikuwa akifanya nini?

Alikuwa akifanya kazi ya Bwana kama Paulo.

Paulo aliamuru nini katika kanisa la Koritho kuhusu Timotheo?

Paulo aliliambia kanisa la Koritho lione kwamba Timotheo alikuwa pamoja nao pasipo kuogopa. Paulo aliwaambia wasimdharau Timotheo na pia wamsaidie katika njia yake kwa amani.

Paulo alimhimiza Apolo kufanya nini?

Paulo alimhimiza Apolo kuwatembelea watakatifu wa Korintho>

1 Corinthians 16:15-16

Wapi kati ya wakoritho walikuwa wamejiweka wenyewe kwenye huduma ya watakatifu?

Kaya ya Stefana, walijiweka wenyewe kwenye huduma ya watakatifu.

Paulo aliwaambi watakatifu wa Wakorintho wafanye nini kwa ajili ya kaya ya Stefana?

Paulo aliwaambia kuwa wanyenyekevu kwa watu hao.

1 Corinthians 16:17-18

Stefana, Fortunato, na Akiko walifanya nini kwa Paulo?

Walisimama kwa niaba ya watakatifu wa Koritho na wakaufurahisha moyo wa Paulo.

1 Corinthians 16:19-20

Nani alituma salamu zao kwa kanisa?

Makanisa ya Asia, Akila na Priska, na akina kaka wote na akina dada walituma saalamu zao kwa kanisa la Koritho.

1 Corinthians 16:21-24

Paulo anasema nini kuhusu wale wanaompenda Bwana?

Paulo alisema, "Kama yeyote hampendi Bwana, basi laana iwe juu yake."