Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

2 Samuel

2 Samuel 1

2 Samuel 1:1-2

Je baada ya kifo cha Sauli Daudi alifanya nini?

Baada ya kifo cha Sauli, Daudi alirudi kutoka kuwapiga Waamaleki na akakaa Siklagi kwa siku mbili.

Ni nani aliyekuja kwa Daudi siku ya tatu kutoka katika kambi ya Sauli?

Katika siku ya tatu mtu nguo zake zikiwa zimechanwa na vumbi kichwani alikuja kwa Daudi.

2 Samuel 1:3-5

Kijana alisema nini kuhusu Sauli na Yonathani?

Alisema Sauli na Yonathani wamekufa

2 Samuel 1:6-7

Kijana alisema alimwona wapi Sauli?

Alisema alimwona Sauli ameegemea mkuki wake katika Mlima wa Gilboa

2 Samuel 1:8-10

Kijana alisema Sauli alimwambia kufanya nini?

Kijana aliseama Sauli alimwambia kusimama juu yake na kumwua.

Kwa nini Sauli alimwambia kijana Mwamaleki kumwua?

Sauli alimwambia kijana Mwamaleki kumwua kwa sababu alisema, "... matatizo makubwa yamenipata kwa sababu ningali hai."

Baada ya kumwua Sauli kijana alichukua nini kutoka kwake?

Alichukua taji iliyokuwa juu ya kichwa cha Sauli na kikuku kilichokuwa mkononi mwake.

2 Samuel 1:11-13

Daudi na watu wake walifanya nini baada ya kusikia kwamba Sauli na Yonathani wamekufa.

Walichana mavazi yao na kuomboleza, kulia, na kufunga mpaka jioni.

Kwa ajili ya nani zaidi Daudi na watu wake waliomboleza, kulia, na kufunga?

Walifanya hayo yote kwa ajili ya watu wa Yahwe na nyumba ya Israeli kwa sababu walikuwa wameanguka kwa upanga.

2 Samuel 1:14-16

Kwa nini Daudi alimwua kijana Mwamaleki?

Kwa sababu alikuwa amemwua mfalme mtiwa mafuta wa Yahwe

2 Samuel 1:17-20

Ni katika kitabu gani wimbo wa maombolezo aliouimba Daudi kuhusu Sauli na Yonathani mwanawe umeandikwa?

Ni katika kitabu cha Yashari.

Nini kimekufa, kuuawa katika milima ya Israeli?

Utukufu wa Israeli umekufa.

Kwa nini Daudi alisema wasitangaze katika Gathi au katika mitaa ya Ashkeloni kwamba utukufu wa Israeli umekufa?

Alisema hivyo ili kwamba binti za Wafilisiti wasijewakafurahi, na hivyo kwamba binti wa wasiotahiliwa wasije wakasherehekea

2 Samuel 1:21-22

Ngao ya mwenye nguvu ilichafuliwa wapi?

Ilichafuliwa katika milima ya Gilboa.

2 Samuel 1:23-24

Sauli alifanya nini kwa binti wa Israeli?

Sauli aliwavika kwa mavazi ya thamani na vito vya thamani, na alitia mapambo ya dhahabu katika mavazi yao.

2 Samuel 1:25-27

Upendo wa Yonathani kwa Daudi ulikuwa wa ukubwa gani?

Daudi alisema upendo wa Yonathani kwa Daudi ulikuwa wa ajabu, kupita upendo wa wanawake.

2 Samuel 2

2 Samuel 2:1-3

Yahwe alimjibuje Daudi alipomwuliza, "Je niende katika miji ya Yuda?

Yahwe alimjibu Daudi, "Panda."

Ni kwa mji upi Yahwe alimwambia Daudi kwenda?

Yahwe alimwambia kwenda katika mji wa Hebroni.

Nani alikwenda na Daudi huko Hebroni?

Daudi alikwenda Hebroni na wake zake wawili, Ahinoamu na Abigaili. Alileta pia watu waliokuwa pamoja naye na kila mtu na familia yake.

2 Samuel 2:4-7

Watu wa Yuda walifanya nini walipokuja kwa Daudi?

Walikuja na kumtia mafuta Daudi kuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda.

2 Samuel 2:8-9

Abneri alikuwa nani?

Abneri alikuwa mwana wa Neri, jemedari wa jeshi la Sauli.

Abneri alimfanya nini Ishboshethi, mwana wa Sauli?

Alimchukua na kumleta Mahanaimu; akamfanya mfalme juu ya Gileadi, Asheri, Yezreeli, Efraimu, Benjamini, na juu ya Israeli yote.

2 Samuel 2:10-11

Ni muda gani Daudi alikuwa mfalme huko Hebroni juu ya nyumba ya Yuda?

Daudi alikuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda kwa miaka saba na miezi sita.

2 Samuel 2:12-13

Ni wapi Yoabu mwana wa Seruya na watumishi wa Daudi walipokutana na Abneri mwana wa Neri, na watumishi wa Ishboshethi?

Yoabu mwana wa Seruya na watumishi wa Daudi walikutana na Abneri mwana wa Neri, na watumishi wa Ishboshethi katika bwawa la Gibeoni.

2 Samuel 2:14-15

Ni vijana wangapi waliosimama kushindana mbele za Yoabu na Abneri?

Vijana kumi na wawili kutoka kila upande.

2 Samuel 2:16-17

Aliyeshinda vita siku hiyo ni nani?

Abneri na watu wa Israeli walishindwa mbele ya watumishi wa Daudi.

2 Samuel 2:18-21

Ni mwana yupi wa Seruya aliyemfuatia Abneri

Asaheli alimfuatia Abneri kwa karibu sana.

2 Samuel 2:22-23

Abneri alimwambia nini Asaheli ili asimfuatiliye?

Alimwambia, "kwa nini nikupige hata chini? nitauinuaje uso wangu mbele ya Yoabu, nduguyo?

Nini kilimpata Asaheli baada ya kukataa kugeuka kutoka kwa Abneri?

Abneri alimpiga kwa ncha ya mkuki wake hata ukatokea upande mwingine, na Asaheli akafa.

2 Samuel 2:24-25

Ni eneo gani Yoabu na Abishai walimfuatilia Abneri?

Walimfuatilia katika mlima wa Ama, uliopo karibu na Gia kando ya njia iendayo katika nyika ya Gibeoni.

2 Samuel 2:26-27

Abneri alisema nini kilichomfanya Yoabu na Abishai kutomfuata tena?

Alimwita Yoabu na kusema "Je upanga uangamize daima? Je haujui kwamba mwishowe utakuwa uchungu? Hata lini uwaambie watu wako wasiwafuatie ndugu zao?

2 Samuel 2:28-29

Abneri na watu wake walielekea wapi?

Walielekea Mahanaimu.

2 Samuel 2:30-32

Yoabu na watu wake walisafiri kuelekea wapi?

Yoabu na watu wake walisafiri kuelekea Hebroni.

2 Samuel 3

2 Samuel 3:1

Ni nyumba ipi iliendelea kusitawi na ni ipi ilidhoofika katika vita ndefu kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi?

Nyumba ya Daudi ilisitawi na nyumba ya Sauli ilidhoofika katika vita baina ya nyumba hizi mbili.

2 Samuel 3:2-5

Ni watoto wapi watatu wa kwanza wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni?

Ni Amnoni, Kileabu, na Absalomu.

2 Samuel 3:6-8

Ishboshi alimlaumu Abneri kwa kufanya nini?

Alimlaumu kwa kulala na suria wa baba wake.

2 Samuel 3:9-11

Baada ya Ishboshethi kumlaumu Abneri kulala na suria wa baba yake, Abneri aliaapa alikuwa anakwenda kufanya nini?

Abneri aliapa kuuamisha ufalme kutoka nyumba ya Sauli na kuuweka ufalme wa Daudi juu ya Israeli na juu ya Yuda, kutoka Dani hata Beersheba.

2 Samuel 3:12-13

Daudi alisema Abneri anapaswa kufanya nini kabla hajauona uso wa Daudi na kufanya agano naye?

Daudi aliwaambia wajumbe wa Abneri kwamba Abneri asingeuona uso wa Daudi asipomleta Mikali, binti wa Sauli, pamoja naye anapokuja kumwona Daudi.

2 Samuel 3:14-16

Daudi alikuwa amelipa gharama gani kwa ajili ya Mikali kuwa mke wake?

Daudi alikuwa amelipa mahari ya govi 100 za Wafilisiti kwa ajili ya Mikali.

2 Samuel 3:17-18

Kwa ufupi Abneri aliwambia nini wazee wa Israeli?

Abneri aliwambia wazee wa Israeli kwamba wanapaswa kumfanya Daudi mfalme wao kama walivyotaka kufanya mwanzo.

2 Samuel 3:19-20

Abneri alipofika Hebroni na wale watu wake ishirini Daudi alimfanyia nini?

Daudi aliwaandalia sherehe.

2 Samuel 3:21

Kwa ufupi Abneri alimwambia Daudi kwamba alikuwa amepanga kufanya nini?

Abneri alimwambia kwamba angewakusanya Israeli wote kwake ili wafanye agano na Daudi ili awamilki.

2 Samuel 3:22-23

Daudi na Abneri waliachanaje?

Daudi alimruhusu Abneri kuondoka, naye akaondoka kwa salama.

2 Samuel 3:24-26

Yoabu alipofika kwa Daudi, alimlaumu kwa kufanya nini?

Yoabu alimlaumu Abneri kwa kujaribu kumdanganya Daudi kwa kutambua mipango ya Daudi na kufahamu kila alichokuwa akikifanya Daudi.

2 Samuel 3:27

Yoabu alimfanya nini Abneri baada ya kumrudisha Hebroni?

Yoabu alimpiga Abneri kwa mkuki tumboni na kumwua.

Kwa nini Yoabu alimwua Abneri?

Yoabu alimwua Abneri kulipa kisasi cha damu ya Asaheli nduguye.

2 Samuel 3:28-30

Daudi alisema nini kwa Yoabu na familia yake baada ya kutambua kwamba Yoabu alikuwa amemwua Abneri?

Daudi alisema kwamba hatia ya damu ya Abneri na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na juu ya nyumba yote ya baba yake.

2 Samuel 3:31-34

Daudi alimwambia Yoabu na watu wote wafanye nini?

Aliwaambia wachane nguo zao, wavae nguo za magunia, na kuomboleza mbele ya mwili wa Abneri.

2 Samuel 3:35-36

Daudi aliapaje watu waliokuja kumwambia ale kungali mchana?

Daudi aliapa, Mungu na anifanyie hivyo, na zaidi, nikionja mkate au chochote kabla jua halijazama.

2 Samuel 3:37-39

Watu na waisraeli wote walielewa nini walipoona huzuni ya Daudi juu ya Abneri?

Wote walitambua kwamba haikuwa nia ya mfalme kumwua Abneri

Mfalme aliwaambiaje watu wake kuhusu Abneri?

Aliwambia watu wake, "Je hamjui kwamba mwana wa mfalme na mtu mkubwa ameanguka leo katika Israeli?"

Daudi alitamani nini kuhusu wana wa Seruya?

Daudi alitamani Yahwe awalipe kwa mabaya kwa kuwaadhibu kwa uovu kama walivyostahili.

2 Samuel 4

2 Samuel 4:1-3

Nini kilisababisha mikono ya Ishboshethi kuwa dhaifu?

Wakati aliposikia kwamba Abneri ameuawa huko Hebroni.

Majina ya watu wawili wa Sauli waliokuwa kapteni wa makundi ya askari ni yapi?

Yalikuwa Baana na Rekabu.

2 Samuel 4:4

Jina la mwana wa Sauli aliyekuwa mlemavu lilikuwa?

Jina la mwana wa Sauli aliyekuwa mlemavu wa miguu alikuwa Mefiboshethi.

2 Samuel 4:5-7

Rekabu na Baana waliingiaje katika nyumba ya Ishiboshethi?

Rekabu na Baana waliingia katika nyumba ya Ishiboshethi kwa kutembea kwa kimya na kumpita mwanamke mlinzi aliyekuwa amelala.

Rekabu na Baana walifanya nini mara walipoingia katika nyumba ya Ishiboshethi?

Mara Rekabu na Baana walipoingia katika nyumba ya Ishiboshethi, walimwua akiwa amelala kitandani katika chumba chake.

2 Samuel 4:8-10

Rekabu na Baana walikwenda wapi baada ya kumwua Ishboshethi na kukata kichwa chake?

Walikileta kichwa kwa Daudi huko Hebroni.

2 Samuel 4:11-12

Daudi alisema nini juu ya Rekabu na Baana?

Daudi alisema Rekabu na Baana walikuwa waovu waliomwua mwenye haki.

Kwa amri ya Daudi, vijana waliwafanya nini Rekabu na Baana?

Waliwaua Rekabu na Baana na kukata vichwa, mikono na miguu yao na kisha kuwatundika kando ya bwawa huko Hebroni.

Daudi alikifanyaje kichwa cha Ishboshethi?

Aliagiza kizikwe katika kaburi la Abneri huko Hebroni.

2 Samuel 5

2 Samuel 5:1-2

Makabila yote ya Israeli yalikiri nini alichokuwa Yahwe amesema kwa Daudi?

Walikiri kwamba Yahwe alikuwa amemwambia Daudi, "Utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala juu ya Israeli."

2 Samuel 5:3-5

Ni akina nani walikwenda Hebroni, kuagana na Daudi, na kumtia mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli?

Wazee wote wa Israeli walikwenda Hebroni, wakafanya agano na Daudi na kumtia mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli.

Ni miaka mingapi Daudi alimilki juu ya Israeli na Yuda huko Yerusalemu?

Alitawala miaka thelathini na mitatu juu ya Israeli na Yuda huko Yerusalemu.

2 Samuel 5:6-7

Yerusalemu iliitwa kwa majina gani mengine?

Yerusalemu iliitwa pia ngome ya Sayuni na Mji wa Daudi.

Daudi aliitwaa ngome ya Sayuni kutoka kwa nani?

Daudi aliiteka ngome ya Sayuni kutoka kwa Wayebusi

2 Samuel 5:8-10

Kwa nini Daudi aliendelea kustawi na kustawi?

Kwa sababu Yahwe, Mungu wa majeshi alikuwa pamoja naye.

2 Samuel 5:11-12

Hiramu mfalme wa Tiro alituma nini kwa Daudi?

Hiramu alituma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, mafundi selemala, na wajenzi.

2 Samuel 5:13-16

Watoto wangapi walizaliwa kwa Daudi huko Yerusalemu?

Walikuwa watoto kumi na mmoja.

2 Samuel 5:17-18

Wafilisti walifanya nini waliposikia kwamba Daudi ametiwa mafuta mfalme juu ya Israeli.

Walikwenda kumtafuta.

2 Samuel 5:19-21

Yahwe alisema nini kwa Daudi kujibu swali la Daudi, je niwashambulia Wafilisiti? Je utanipa kuwashinda?

Yahwe alimwambia Daudi, "Washambulie, kwa maana bila shaka nitakupa ushindi juu ya Wafilisiti."

Daudi aliwashambulia wapi Wafilisiti na matokeo yalikuwaje?

Daudi aliwashambulia Baali Perazimu, na aliwashinda Wafilisiti pale.

2 Samuel 5:22-23

Wafilisiti walikuja lini mara ya pili, Yahwe alimwambiaje Daudi juu ya kuwashambulia?

Yahwe alimwambia Daudi kuwashambulia Wafilisiti kwa mbele, lakini kuwazunguka na kuwajia kupitia miti ya miforosadi.

2 Samuel 5:24-25

Yahwe alimwambia Daudi kusikiliza sauti gani kabla ya kuwashambulia Wafilisiti?

Yahwe alimwambia Daudi kuwashambulia Wafilisiti aliposikia sauti ya kwenda katika upepo uliokuwa unavuma kupitia vilele vya miti ya miforosadi.

Jibu la Daudi kwa agizo la Yahwe lilikuwa nini?

Daudi alifanya kama Yahwe alivyomwagiza.

Matokeo ya vita hii dhidi ya Wafilisiti ilikuwaje?

Matokeo ya vita hii ni kwamba Daudi aliwauwa wafilisiti kutoka Geba njia yote hadi Gezeri.

2 Samuel 6

2 Samuel 6:1-2

Kwa nini Daudi aliwakusanya tena wateuli wa Israeli?

Daudi aliwakusanya wateule wa Israeli ili kulipandisha sanduku la Mungu.

2 Samuel 6:3-5

Waliliweka sanduku la Mungu juu ya nini?

Waliliweka Sanduku la Mungu juu ya mkokoteni mpya.

Nani aliuongoza mkokoteni huo

Uza na Ahio, wana wa Abinadabu, walikuwa wakiuongoza mkokoteni.

2 Samuel 6:6-7

Kilitokea nini walipofika katika sakafu ya kupuria ya Nakoni?

Walipofika katika sakafu ya kuporia ya Nakoni, ng'ombe walikwama, Uza akanyosha mkono wake kulishikilia sanduku la Mungu, na akalikumbatia.

Yahwe alifanya nini kutokana na kitendo cha Uza.

Yahwe alikasirika na akampiga Uza kwa dhambi yake, Uza akafa palepale kando ya sanduku la Mungu.

2 Samuel 6:8-9

Daudi alijisikiaje kuhusu Yahwe alichomtendea Uza?

Daudi alikasirika kwa sababu ya Yahwe kumpiga Uza, na Daudi akamwogopa Mungu siku hiyo.

2 Samuel 6:10-11

Daudi alilifanyaje sanduku la Mungu baada ya Uza kufa?

Daudi aliliweka sanduku la Mungu kando katika nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.

2 Samuel 6:12-13

Kwa nini Daudi alilipandisha sanduku la Mungu kutoka katika nyumba ya Obedi Edomu hadi mji wa Daudi?

Ni kwa sababu Daudi aliambiwa kwamba Yahwe alikuwa ameibariki nyumba ya Obedi Edomu na kila alichokuwanacho kwa sababu ya sanduku la Mungu.

2 Samuel 6:14-15

Daudi alifanya nini wakati sanduku la Mungu linaletwa?

Daudi, alikuwa amevaa naivera ya kitani, akicheza mbele ya Bwana kwa nguvu zake zote.

2 Samuel 6:16-17

Mikali alijibu nini alipomwona Mfalme akicheza mbele za Yahwe?

Mikali alimzarau Daudi moyoni mwake.

Daudi alitoa matoleo gani kwa Yahwe, baada ya sanduku la Yahwe kuwekwa mahali pake?

Daudi alitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani.

2 Samuel 6:18-19

Daudi aliwagawia nini wanaume kwa wanawake?

Daudi aligawanya kati yao mkate, kipande cha nyama na keki ya zabibu.

2 Samuel 6:20

Mikali binti Sauli alimwambia nini Daudi?

Alisema mfalme wa Israeli alikuwa mtukufu namna gani leo, aliyejifunua yeye mwenyewe mbele ya wajakazi wake na wajoli wake, kama mtu mpumbavu ajifunuaye mwenyewe bila aibu.

2 Samuel 6:21-23

Jibu la Daudi kwa Mikali lilikuwaje?

Daudi alisema alicheza mbele za Yahwe ambaye alifurahi na kwamba angejishusha machoni pake mwenyewe lakini angeeshimiwa miongoni mwa wajakazi.

2 Samuel 7

2 Samuel 7:1-2

Yahwe alimpa nini Daudi?

Yahwe alimpa Daudi pumziko kutoka kwa adui zake wote waliokuwa wanamzinguka.

Mfalme alimwambia nini Nathani nabii?

Mfalme alimwambia Nathani nabii kwamba "Tazama, ninaishi katika nyumba ya mwerezi, lakini sanduku la Mungu linakaa katika hema.

2 Samuel 7:3-5

Nathani alimwambia nini Daudi kabla neno la Yahwe alijaja kwake?

Nathani alimwambia Daudi, "Nenda, ufanye yaliyomo moyoni mwako, maana Yahwe yupo nawe."

2 Samuel 7:6-7

Yahwe alimwuliza Daudi swali gani kuhusu viongozi wa Israeli hadi wakati huo?

Yahwe alimwuliza Daudi ikiwa alikuwa amewai kusema "Kwa nini hamjanijengea nyumba ya mwerezi? kwa kiongozi yeyote wa Israeli ambaye Yahwe alikuwa amemchagua.

2 Samuel 7:8-9

Yahwe alisema alikuwa amefanya nini kwa Daudi.

Yahwe alikuwa amemfanya mtawala juu ya watu wa Yahwe Israeli, alikuwa na Daudi popote na alikuwa amewakatilia mbali adui zake.

2 Samuel 7:10-11

Yahwe alisema alikuwa anakwenda kufanya nini kwa ajili ya Israeli?

Yahwe alikuwa amesema angechagua eneo kwa ajili yao na kuwapanda pale, ili waishi mahali pao na wasisumbuliwe tena na watu waovu kama ilivyokuwa mwanzo.

2 Samuel 7:12-14

Yahwe alisema ni nani angejenga nyumba kwa ajili yake?

Yahwe alisema angeinua mzao wa Daudi, kutoka mwili wa Daudi, naye angejenga nyumba kwa jina la Yahwe.

2 Samuel 7:15-17

Yahwe alisema nini kuhusu nyumba ya Daudi na ufalme wake?

Yahwe alisema nyumba ya Daudi na ufalme wake ungethibitika milele.

2 Samuel 7:18-20

Baada ya Nathani kumwambia Daudi maneno yote Yahwe aliyokuwa amesema kuhusu ono zima, Daudi alisema nini?

Daudi aliingia akakaa mbele ya Yahwe na kuongea naye.

Daudi alisema Yahwe alikuwa amefanya nini kwake baada ya kusikia unabii wote kuhusu yeye na familia yake?

Daudi alisema Yahwe amemweshimu mtumishi wake.

2 Samuel 7:21-26

Daudi alisema sababu gani Yahwe alikuwa amefanya jambo kubwa na kulifunua?

Daudi alisema Yahwe alikuwa amefanya haya kutimiza neno lake na kusudi lake.

Daudi alisema ilikuwa ni kwa sababu gani Mungu alikwenda na kuwakomboa Israeli?

Daudi alisema Yahwe alikuwa amewakomboa Israeli ili wawe watu wa Mungu, kujifanyia jina, ili kufanya mambo makuu na ya kuogofaya kwa ajili ya nchi ya Yahwe.

2 Samuel 7:27-29

Ni kwa jinsi gani Daudi alisema alikuwa amepata ujasiri wa kuomba kwa Yahwe wa utukufu?

Daudi alisema alikuwa amepata ujasiri wa kuomba mbele ya Yahwe wa majeshi kwa sababu Yahwe wa majeshi alikuwa amemfunulia Daudi kwamba angemjengea nyumba.

Daudi alililihesabuje neno la Yahwe?

Daudi alilihesabu neno la Yahwe kuwa la kuaminika.

Daudi alitaka Yahwe afanye nini?

Daudi alitaka Yahwe kutimiza kama alivyokuwa ameahidi.

2 Samuel 8

2 Samuel 8:1

Daudi alipata nini baada ya kuwapiga Wafilisiti na kuwashinda?

Daudi aliichukua Gathi na vijiji vyake mkononi mwa utawala wa Wafilisti.

2 Samuel 8:2

Baada ya kuwashinda Moabu, aliamuaje watu wa kuua na watu wa kuacha hai?

Daudi aliamua watu gani wa Moabu waishi au wafe kwa kuwafanya walale chini juu ya ardhi na kupima mistari miwili ya kuua na mmoja mzima wa kuacha hai.

Kilifanyika nini kwa Wamoabu waliokuwa wameachwa hai?

Walifanywa watumishi wa Daudi na kuanza kumpa kodi.

2 Samuel 8:3-4

Daudi aliteka nini kutoka kwa Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba?

Daudi aliteka kutoka kwake vibandawazi elfu, wapanda farasi mia saba, na askari wa miguu elfu ishirini.

2 Samuel 8:5-8

Daudi aliwafanya nini Washami wa Damesiki walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba?

Daudi aliuwa watu ishirini elfu wa Washami.

Kwa nini Daudi alikuwa mshindi?

Yahwe alimpa Daudi kushinda kila alipokwenda.

2 Samuel 8:9-10

Tou mfalme wa Hamathi alifanya nini aliposikia kwamba Daudi alikuwa amewashinda jeshi lote la Hadadezeri?

Tou alimtuma mwanawe, Hadoramu, kwa Daudi ili kumsalimia na kumbariki, na Hadoramu alileta vitu vingi sana vya fedha, dhahabu, na shaba kwa Daudi.

2 Samuel 8:11-12

Daudi alivifanyia nini vitu alivyokuwa ameviteka kwa mataifa aliyokuwa ameyashinda?

Daudi aliweka kwa Yahwe fedha na dhahabu kutoka kwa mataifa aliyokuwa ameyateka

2 Samuel 8:13-14

Ni wapi Daudi alipowashinda Washami?

Daudi aliwashinda Washami katika Bonde la Chumvi.

2 Samuel 8:15-18

Daudi alitenda nini kwa watu wake?

Daudi alitawala kwa haki na utakatifu kwa watu wake wote.

Washauri wa Daudi walikuwa akina nani?

Wana wa Mfalme Daudi walikuwa washauri wake wakuu.

2 Samuel 9

2 Samuel 9:1-2

Kwa nini Daudi alitaka kuonesha wema kwa kila mtu aliyesalia katika familia ya Sauli?

Kwa ajili ya Yonathani.

2 Samuel 9:3-4

Siba alimjibuje mfalme alipoulizwa ikiwa kulikuwa na aliyesalia katika familia ya Sauli ambaye kwake mfalme angeonesha ukarimu wa Mungu?

Siba alimjibu mfalme, "Yonathani bado anamwana, ambaye ni mlemavu katika miguu yake."

2 Samuel 9:5-6

Nani alikuwa amesalia katika familia ya Sauli?

Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli alikuwa amesalia.

2 Samuel 9:7-8

Ni wema gani Daudi aliomwonesha Mefiboshethi kwa ajili ya Yonathani?

Alimrejeshea eneo la Sauli, babu yake, naye akala katika meza ya Daudi.

2 Samuel 9:9-10

Daudi alimwambia Siba kufanya nini kwa ajili ya Mefiboshethi?

Kulima ardhi na kuvuna mazao kwa ajili ya Mefiboshethi.

2 Samuel 9:11-13

Mefiboshethi aliishi wapi baada ya Daudi kumwonesha wema?

Mefiboshethi aliishi Yerusalemu.

Mefiboshethi alikuwa na tatizo gani kimwili?

Mefiboshethi alikuwa mlemavu wa miguu.

2 Samuel 10

2 Samuel 10:1-3

Baada ya mfalme wa kwanza wa wana wa Amoni kufa nani alifuata kuwa mfalme?

Hanuni mwana wa mfalme wa kwanza akawa mfalme mpya wa Amoni.

Daudi alifanya nini ili kuonesha wema wake kwa Hanuni?

Alituma watumishi wake kwa Hanuni kumfariji kuhusiana na baba yake.

Kwa ufupi, viongozi wa watu wa Amoni walisema nini kuhusiana na Daudi kumwonesha Hanuni wema?

Viongozi wa wana wa Amoni walimwambia Hanuni kwamba Daudi alikuwa amewatuma watumishi wake ili kuupeleleza mji na kuupindua.

2 Samuel 10:4-5

Hanuni alifanya nini kwa watumishi wa Daudi?

Aliwachukua watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao, akachana mavazi yao hadi katika viuno, na kuwaacha waende zao.

2 Samuel 10:6-8

Kwa nini watu wa Amoni waliwaajiri askari elfu ishirini wa Washami, mfalme wa Maaka mwenye watu elfu moja na watu wa Tobu wenye watu elfu kumi na mbili?

Walifanya hivyo baada ya kugundua kwamba wamenuka kwa Daudi.

Waamoni na askari walioajiriwa walikaa wapi?

Walikaa katika maingilio ya lango, wakati Washami wa Soba na wa Rehobu, na watu wa Tobu na Maaka, walisimama wenyewe katika eneo la wazi.

Daudi alifanya nini baada ya kusikia kwamba watu wa Amoni wameajiri watu maelfu ya askari?

Daudi aliposikia hivyo, alitumtuma Yoabu na jeshi lote la askari.

2 Samuel 10:9-12

Yoabu alifanya nini ili kujiandaa na vita?

Yoabu alijiandaa kwa vita kwa kuwapanga wapiganaji wazuri wa Israeli dhidi ya Washami na kumweka Abishai nduguye juu ya sehemu iliyosalia ya jeshi waliokuwa wamepangwa katika mistari ya kivita dhidi ya jeshi la Amoni.

2 Samuel 10:13-14

Jeshi la Amoni lilifanyaje lilipoona kwamba Washami wamemkimbia Yoabu na jeshi lake?

Jeshi la Amoni lilipoona kwamba Jeshi la Washami limekimbia, wao pia walikimbia mbele ya Abishai na kwenda mjini.

2 Samuel 10:15-16

Baada ya kuona kwamba wameshindwa na Waisraeli Washami walifanya nini?

Washami walijikusanya tena na Hadareza akatuma vikosi vya Kishami kutoka ng'ambo ya Mto Frati.

2 Samuel 10:17-19

Daudi alifanya nini baada ya kusikia kwamba Washami wamejikusanya tena na wametuma na kupata askari wa vikosi vingine vya Kishami kutoka ng'ambo ya pili ya Mto Frati?

Daudi alipopata habari, aliwakusanya Waisraeli wote pamoja, akavuka Yordani, na akaja Helamu kupigana na Washami.

Wafalme wote waliokuwa watumishi wa Hadareza walifanya nini walipoona kwamba wameshindwa na Israeli?

Walifanya agano la amani na Israeli na wakawa watumishi wao.

2 Samuel 11

2 Samuel 11:1

Wakati gani kwa kawaida wafalme uenda vitani

Wakati wa majira ya kipupwe.

Mfalme Daudi alikuwa wapi wakati wa majira haya?

Mfalme Daudi alikuwa amebaki Yerusalemu.

2 Samuel 11:2-3

Daudi alimwona nani wakati wa jioni alipoamuka kitandani na kutembea juu ya dali ya kasiri lake?

Alimwona Bethsheba akioga.

Mme wa Bethsheba alikuwa nani?

Alikuwa Uria Mhiti

2 Samuel 11:4-5

Daudi alifanya nini na Bethsheba?

Alilala naye na kumpa ujauzito.

2 Samuel 11:6-8

Baada ya kugundua kuwa Bethsheba ni mjamzito, Daudi alifanya nini?

Alimwambia Yoabu amtume Uria Mhiti kwake.

2 Samuel 11:9-13

Uria alifanya nini baada ya kuambiwa na Daudi kwamba aende kwake?

Uria hakwenda kwake, badala yake alilala mlangoni mwa kasiri la mfalme na watumishi wengine wa mfalme.

Uria alimjibuje Daudi baada ya Daudi kumwuliza, "Kwa nini haukwenda nyumbani kwako?

Uria alisema asingekwenda kwake kula na kunywa na kulala na mke wake wakati sanduku na Israeli, na Yuda walikuwa katika mahema, na Yoabu na watumishi wake walikuwa wamepanga katika eneo la wazi.

2 Samuel 11:14-17

Daudi alipeleka ujumbe kwa Yoabu kwa mkono wa Uria. Ujumbe ulisemaje?

Ulisema, "Mweke uria mbele kabisa ya vita vikali, na kisha mmwache, ili apigwe na afae.

2 Samuel 11:18-20

Yoabu alimwambia mjumbe kitu gani chaweza kutokea akimpa Daudi habari ya vita?

Yoabu alimwambia mjumbe kwamba Daudi aweza kasirika akipewa habari za vita.

Yoabu alidhani ni habari gani Daudi angeweza kukasirika juu yake?

Yoabu alidhani Daudi aweza kasirika kuhusu habari kwamba jeshi liliukaribia mji ili kupigana.

2 Samuel 11:21-23

Yoabu alimwambia mjumbe kumwambia nini Daudi ikiwa angekasirika kuhusu habari ya vita?

Alimwambia ikiwa Daudi akikasirika mwambie, "Mtumishi wako Uria pia amekufa."

2 Samuel 11:24-25

Daudi alimwambia mjumbe kumwambia Yoabu afanye nini?

Alimwambia amwambie Yoabu kuzidisha mashambulizi juu ya mji na kuupindua.

2 Samuel 11:26-27

Mke wa Uria alifanya nini aliposikia kwamba mme wake amekufa?

Aliomboleza sana kwa ajili ya mme wake.

Ni nini kilichotokea kwa Bethsheba?

Baada ya uzuni yake kuisha, Daudi alimchukua kwake akawa mkewe na kumzalia mwana.

Ni nani ambaye hakupendezwa na alichokifanya Daudi?

Yahwe hakupendezwa na alichokifanya Daudi.

2 Samuel 12

2 Samuel 12:1-3

Kwa nini Nathani alikwenda kwa Daudi?

Nathani alikwenda kwa Daudi kwa sababu Yahwe alimtuma kwake.

Nathani alimwambia habari Daudi. Habari hiyo ilihusu nini?

Habari ambayo Nathani alimwambia Daudi ilikuwa inahusu tajiri aliyekuwa na kundi la kondoo na ng'ombe, na masikini aliyekuwa na kondoo mmoja pekee aliyekuwa kama binti kwake.

2 Samuel 12:4-6

Tajiri alimfanyaje masikini na kondoo wake?

Mgeni alipofika kwa tajiri, yeye alichukua kondoo wa maskini na kumwandalia mgeni wake.

Mwitikio wa Daudi ulikuwaje baada ya kusikia habari hiyo?

Daudi alikasirika sana dhidi ya tajiri na kusema tajiri anastahili kufa

2 Samuel 12:7-8

Nathani alimwambiaje Daudi baada ya yeye kumkasirikia tajiri?

Nathani alimwambia, "Mtu huyo ni wewe!"

2 Samuel 12:9-10

Yahwe alisema Daudi alikuwa amefanya nini?

Yahwe alisema Daudi alikuwa amemwua Uria kwa upanga wa jeshi la wana wa Amoni na kumchukua mkewe.

2 Samuel 12:11-13

Nathani alimwambia Daudi kitu gani kisingetokea kwake baada ya kusema, "Nimemtenda Yahwe dhambi"?

Nathani alimwambia Daudi, "Yahwe pia ameiondoa dhambi yako. Hautakufa."

2 Samuel 12:14-15

Yahwe alisema alikuwa anakwenda kufanya nini kwa sababu ya Daudi kumdharau na kuchukua mke wa Uria Mhiti kuwa mke wake?

Yahwe alimwambia Daudi upanga usingeondoka nyumbani mwake, kwamba Yahwe angeinua maafa dhidi ya Daudi kutoka katika nyumba yake mwenyewe, kwamba jirani angelala na wake wake wakati wa mchana, na kwamba mtoto ambaye angezaliwa kwa Daudi angekufa hakika.

2 Samuel 12:16-18

Baada ya mtoto aliyezaliwa na mke wa Uria kwa Daudi kuugua Daudi alifanya nini?

Daudi alimwomba Mungu kwa ajili ya mtoto naye alifunga na kuingia ndani akalala usiku wote kwenywe sakafu.

Mtoto mke wa Uria aliyemzalia Daudi alikufa lini?

Mtoto alikufa katika siku ya saba.

2 Samuel 12:19-20

Baada ya Daudi kutambua kwamba mtoto amekufa alifanya nini?

Aliinuka kutoka sakafuni, akanawa, akajipaka mafuta na kubadili nguo zake.

2 Samuel 12:21-23

Sababu ya Daudi kutokufunga baada ya mtoto kufa ilikuwa ni nini?

Daudi alisema kwamba baada ya mtoto kufa hakukuwa na sababu ya kufunga kwani asingemrudisha tena mtoto.

2 Samuel 12:24-25

Kwa nini Yahwe alituma neno kwa Nabii Nathani kumwita mtoto wa Daudi na Bethsheba Yedidia?

Kwa sababu Yahwe alimpenda.

2 Samuel 12:26-30

Wakati huo, Yoabu alikuwa anapigana na nani?

Yoabu alikuwa anapigana dhidi ya Raba, mji wa kifalme wa wana wa Amoni.

Kwa nini Yoabu alimwambia Daudi kulikusanya jeshi lililokuwa limesalia na kupiga kambi kinyume cha mji na kuutwaa?

Yoabu alimwambia Daudi kuja na kupiga kambi dhidi ya mji na kuuchukua kwa sababu Yoabu ikiwa angechukua yeye ungeitwa kwa jina lake?

2 Samuel 12:31

Mara baada ya mji wa Raba kutwaliwa, Daudi aliwafanyaje watu waliokuwa mjini?

Daudi aliwalazimisha watu wa Raba kufanya kazi ya misumeno, na kazi ya shokoa; pia aliwafanya kufanya kazi kwa shoka, pia aliwafanya wafanye kazi katika kutengeneza matofali.

2 Samuel 13

2 Samuel 13:1-2

Amnoni mwana wa Daudi alivutwa na nani?

Amnoni alimtamani sana dada yake wa kambo aliyekuwa mzuri na dada wa Absalomu, mwana mwingine wa Daudi.

2 Samuel 13:3-4

Amnoni ajibuje alipoulizwa na Yehonadabu kwa nini alikuwa akiendelea kunyong'onyea kila siku?

Amnoni alimwambia Yehonadabu kwamba alimpenda Tamari, dada wa Absalomu nduguye.

2 Samuel 13:5-9

Amnoni alifanya nini ili aweze kumwona Tamari?

Amnoni alijifanya kuwa mgonjwa na Daudi alipokuja kumwona, alimwomba Daudi kumtuma ili aandaye chakula mbele yake akile mkononi mwake na Daudi alifanya kama Amnoni alivyomwomba.

2 Samuel 13:10-12

Amnoni alifanya nini Tamari alipokuja kwake ili kumlisha?

Tamari alipokuja kumlisha Amnoni, alimshika na kumwambia, njoo ulale nami dada yangu."

2 Samuel 13:13-14

Amnoni alifanya nini Tamari alipomwambia asimlazimishe na wala asifanye jambo la aibu kama hili?

Amnoni hakumsikiliza Tamari, hivyo akambaka.

2 Samuel 13:15-17

Amnoni alijisikiaje baada ya kumbaka Tamari?

Amnoni alimchukia Tamari zaidi ya jinsi alivyokuwa amemtamani.

Amnoni alimwamru nini na kumlazimisha Tamari afanye nini?

Amnoni alimwamru Tamari "ainuke na kuondoka." na akaagiza mtumishi wake kumwondoa Tamari na kufunga mlango nyumba yake.

2 Samuel 13:18-19

Tamari alifanya nini alipoondolewa chumbani mwa Amnoni?

Aliweka majivu kichwani pake, kurarua vazi lake na kuweka mikono yake kichwani, akilia kadili alivyokuwa akienda.

2 Samuel 13:20-22

Mwitikio wa Daudi ulikuwaje aliposikia mambo haya yote?

Daudi aliposikia alikasirika sana.

Baada ya Absalomu, kaka wa Tamari, kufahamu kwamba Amnoni amembaka dada yake, alijisikiaje juu ya Amnoni?

Absalomu alimchukia Amnoni kwa sababu alikuwa amembaka dada yake.

2 Samuel 13:23-24

Absalomu aliwaarika watu gani kumtembelea huko Baali Hazori?

Alimwalika mfalme na watumishi wake na wana wote wa mfalme ili wamtembelee huko Baali Hazori.

2 Samuel 13:25-26

Mfalme alisema nini kujibu mwaliko wa Absalomu wa kutembelewa huko Baali Hazori?

Mfalme alisema kwamba wasiende wote kwa sababu watakuwa mzigo kwake.

Daudi alisemaje Absalomu alipomwomba kwamba Amnoni aende pamoja nao?

Daudi alimwuliza, "kwa nini Amnoni aende pamoja nanyi?"

2 Samuel 13:27-29

Waliokwenda na Absalomu akina nani?

Amnoni na wana wote wa Mfalme walikwenda pamoja na Absalomu.

Absalomu aliwaamru nini watumishi wake kuhusiana na Amnoni?

Absalomu aliwaamru kwamba baada ya Amnoni kuanza kulewa mvinyo na Absalomu kuwaambia "Mpigeni Amnoni," ndipo wamwue Amnoni.

Wana wa mfalme walifanya nini baada ya watumishi wa Absalomu kumwua Amnoni?

Baada ya watumishi wa Absalomu kumwua Amnoni wana wote wa mfalme waliinuka, na kila mmoja kumpanda nyumbu wake na kukumbia.

2 Samuel 13:30-31

Daudi alipata habari gani mwanzoni kuhusu tukio?

Wakati wana wa mfalme wakiwa njiani bado, habari zilimfikia Daudi kwamba Absalomu alikuwa amewauwa wana wote wa mfalme.

2 Samuel 13:32-36

Yehonadabu alisema nini kilikuwa kimetokea na kwa nini?

Yehonadabu alimwambia Daudi kwamba ni Amnoni tu ndiye aliyekuwa ameuawa, na kwamba Absalomu alikuwa amelipanga hili tangu siku Amnoni alipombaka Tamari dadaye.

2 Samuel 13:37-39

Baada ya Absalomu kumwua Amnoni alikimbilia wapi?

Absalomu alikimbilia kwa Talmai, mwana wa Amihuri mfalme wa Geshuri.

Absalomu alikaa huko Geshuri kwa muda gani?

Absalomu alikuwa Geshuri kwa miaka mitatu.

Daudi alitamani kufanya nini?

Daudi alitamani kwenda kumwona Absalomu.

2 Samuel 14

2 Samuel 14:1-3

Yoabu alifanya nini baada ya kutambua nia ya mfalme ya kumwona Absalomu?

Yoabu alituma neno Tekoa kumleta kwake mwanamke wenye busara.

Kwa ufupi Yoabu alitaka mwanamke mwenye hekima afanye nini?

Alimtaka mwanamke mwenye hekima ajifanye kuwa mwombolezaji na kwenda kuongea na mfalme maneno aliyoambiwa na Yoabu.

2 Samuel 14:4-6

Mwanamke alipoingia kwa mfalme, alimwambia mfalme kuwa yeye alikuwa nani?

Alimwambia kwamba alikuwa mjane.

Mwanamke mwenye hekima alimwambia mfalme kwamba wanawe wawili walikuwa wamefanya nini?

Alimwambia kwamba wanawe wawili walikuwa wamegombana shambani na mmoja akampiga mwingine na kumwua.

2 Samuel 14:7-9

Mwanamke mwenye hekima alimwambia mfalme kwamba alikuwa anaogopa nini kingetokea kwa mwanawe?

Alimwambia mfalme kwamba alikuwa anaogopa ukoo wote ungemwua mwanawe aliyesalia, kumwangamiza mrithi na kumwondolea mmewe uzao.

2 Samuel 14:10-11

Kwa nini mwanamke mwenye hekima alimwambia mfalme kumkumbuka Yahwe?

Alimwambia hivyo ili mlipa kisasi cha damu asimwangamize mwanaye.

Mfalme aliapa kwa nani alipomwambia mwanamke kwamba hakuna hata unywele ungeanguka chini?

Mfalme aliapa kwa Yahwe kwa kusema, "kama aishivyo Yahwe, hakuna nywele ya mwanao itakayoanguka chini."

2 Samuel 14:12-14

Kwa nini mwanamke alimwambia mfalme kwamba kwa kusema hivyo alikuwa kama mwenye hatia?

Mwanamke alisema mfalme alikuwa kama mwenye hatia kwa sababu mfalme alikuwa hajamrudisha mwanawe aliyeondoka.

Mwanamke alisema Mungu ufanya nini badala ya kuondoa uhai?

Mwanamke alisema badala ya Mungu kuondoa uhai utafuta njia ya kumrudisha aliyeko mbali naye.

2 Samuel 14:15-17

Mwanamke alisema kwa nini alikuja kuongea na mfalme?

Mwanamke alisema alikuja kuongea na mfalme kwa sababu watu walikuwa wamemwogopesha, na kwa sababu aliamini mfalme angemsikiliza.

Mwanamke alisema alimwomba nini Yahwe katika maombe yake?

Mwanamke alisema alimwomba Yahwe kuyaacha maneno ya bwana wake, mfalme, kumtuliza.

2 Samuel 14:18-20

Mfalme alimwambia nini mwanamke baada ya kumwambia asifiche neno lolote angemwuliza?

Mfalme alimwambia mwanamke, "Je siyo mkono wa Yoabu uliopamoja nawe katika haya yote?"

Kwa nini Yoabu alimwagiza mwanamke kuingia kwa mfalme na kusema maneno yote aliyokuwa amemwambia.

Yoabu alimwagiza mwanamke kufanya na kusema mambo hayo ili kubadili hali ya mambo.

2 Samuel 14:21-22

Yoabu alifanya nini baada ya mfalme kumwambia aende na kumleta Absalomu?

Yoabu aliinama uso wake chini kwa heshima na shukurani kwa mfalme.

2 Samuel 14:23-24

Ni maelekezo gani mfalme alimwambia Yoabu kuhusu Absalomu?

Mfalme alisema Absalomu arudi nyumbani kwake lakini hatamwona uso mfalme.

2 Samuel 14:25-27

Ni nini kilikuwa cha kuangaliwa katika mwonekano wa Absalomu?

Absalomu alikuwa mzuri bila mawaa na nywele zake alizozikata mwisho wa kila mwaka, zilikuwa na uzito wa shekeli mia mbili.

2 Samuel 14:28-29

Absalomu aliishi Yerusalemu kwa muda gani bila kumwona mfalme?

Absalomu aliishi Yerusalemu miaka miwili bila kumwona mfalme.

2 Samuel 14:30-31

Absalomu alisema nini kwa watumishi wake baada ya kumwita Yoabu mara mbili bila jibu lolote?

Aliwambia kulichoma shamba la shayiri la Yoabu.

2 Samuel 14:32-33

Absalomu alitaka Yoabu afanye nini?

Alitaka kumwambia Yoabu aende amwambie mfalme kwamba Absalomu alitaka kumwona mfalme.

Mfalme alifanya nini Absalomu alipoinama hata chini mbele ya mfalme?

Mfalme alimbusu Absalomu.

2 Samuel 15

2 Samuel 15:1-2

Absalomu alijiandalia nini mwenyewe?

Absalomu alijiandaliwa kibandawazi na farasi.

Nani waliokwenda mbele ya Absalomu na kibandawazi chake?

Watu hamsini walikwenda mbele ya Absalomu na kibandawazi chake.

Absalomu aliwaita watu gani aliposimama kando ya njia ya kuingia mjini?

Ikiwa mtu alikuja kwa mfalme akiwa na shitaka kwa hukumu, Absalomu alimwita.

2 Samuel 15:3-4

Absalomu angesema nini kwa watu waliokuwa wanakuja kwa mfalme kwa ajili ya mashauri yao?

Absalomu alikuwa akiwambia watu hawa kwamba mashitaka yao ni ya haki, lakini kwamba hakukuwa na mtu aliyepewa mamlaka ya kusikiliza mashitaka yao.

Absalomu alitoa sababu gani kwa kusema alitamani angefanywa mwamuzi katika nchi?

Absalomu alisema alitamani angefanywa mwamuzi katika nchi ili kila aliyekuwa na shauri au jambo angesikilizwa na kupewa haki yake kutoka kwa Absalomu.

2 Samuel 15:5-6

Absalomu alifanya nini kwa kila mtu aliyefika kumpa heshima?

Absalomu alikuwa akinyosha mkono wake kuwashika na kuwabusu waliokuja kumpa heshima.

Absalomu aliiba nini kutoka kwa watu?

Absalomu akaiiba mioyo ya watu wa Israeli.

2 Samuel 15:7-8

Absalomu alitoa sababu gani kwa mfalme kwa kwenda Hebroni?

Alimwambia mfalme kwamba alikuwa anakwenda Hebroni kutimiza nadhiri aliyokuwa ameiweka kwa Yahwe.

2 Samuel 15:9-10

Wapelelezi aliowapeleka Absalomu katika makabila yote ya Israeli walisema nini?

Wapelelezi walisema, "Mara msikiapo sauti ya tarumbeta, semeni, 'Absalomu ni mfalme katika Hebroni."

2 Samuel 15:11-12

Je wale watu mia mbili waliokwenda na Absalomu waliijua mipango yake?

Hapana, hawakuijua.

2 Samuel 15:13-15

Kwa ufupi, Daudi aliwambia nini watumishi wake baada ya mjumbe kumwambia, "Mioyo ya watu wa Israeli inaambatana na Absalomu"?

Daudi aliwambia watumishi wake waliokuwa Yerusalemu, "Inukeni tukimbie, au hakuna kati yetu atakayepona kwa Absalomu."

2 Samuel 15:16-20

Mfalme aliwaacha watu gani huko Yerusalemu kulitunza kasiri?

Mfalme aliwaacha wanawake kumi, waliokuwa masuria, kulitunza kasiri.

Watu gani walikwenda na mfalme alipokuwa akitoka Yerusalemu?

Jeshi lote la mfalme lilikwenda pamoja naye na Wakerethi, na Wapelethi, Wagiti mia sita waliokuwa wameambatana naye kutoka Gathi.

2 Samuel 15:21-23

Itai Mgiti alimwambia nini Mfalme baada ya mfalme kumwambia arudi na kubaki na mfalme Absalomu?

Itai alimwambia mfalme angekwenda popote ambapo mfalme angekwenda, kwamba kwa kuishi au kufa.

Daudi na wale aliokuwa nao walikwenda kwa njia gani walipotoka Yerusalemu?

Daudi na wale aliokuwa nao walipita Bonde la Kidroni na kuendelea katika njia ya nyikani.

2 Samuel 15:24-26

Mfalme alimwambia nini Sadoki kuhusu sanduku la agano la Mungu?

Alimwambia kulirudisha sanduku mjini.

2 Samuel 15:27-29

Kwa nini Daudi alikuwa anakwenda kusubiri katika vivuko vya Araba?

Alikuwa anakwenda kusubiri katika vivuko vya Araba ili apate habari kutoka kwa Sadoki kuhani.

2 Samuel 15:30-31

Daudi aliomba nini alipoambiwa kwamba Ahithofeli alikuwa miongoni mwa waaini waliokuwa pamoja na Absalomu?

Daudi alijibu, "Ee Yahwe, ligeuze shauri la Ahithofeli katika upumbavu."

2 Samuel 15:32-34

Daudi alipofika juu ya njia mahali Mungu alipokuwa akiabudiwa nani alikuja kumlaki?

Hushai Mwarki alikuja kumlaki Daudi.

Daudi alitaka Hushai Mwarki amfanyie nini?

Daudi alitaka Hushai Mwarki arejee mjini na kumwambia Absalomu angekuwa mtumishi wake hivyo Hushai angelibadili shauri la Ahithofeli kwa ajili ya Daudi.

2 Samuel 15:35-37

Daudi alitaka watu gani waambiwe habari na Hushai juu ya kila kitu alichokisikia katika kasiri la mfalme?

Daudi alitaka Hushai amwambie Sadoki na Abiathari makuhani habari yoyote aliyoisikia katika kasiri la mfalme.

2 Samuel 16

2 Samuel 16:1-2

Siba mtumishi wa Mefiboshethi alimletea nini Daudi?

Alileta jozi za punda wenye mzigo wa mikate mia mbili vishada mia moja vya mizeitunu, matawi vichala mia moja vya mtini na kiriba cha mvinyo.

2 Samuel 16:3-4

Kwa mjibu wa Siba, sababu ya Mefiboshethi kubaki Yerusalemu ilikuwa ni ipi?

Siba alisema sababu ya Mefiboshethi kubaki Yerusalemu ilikuwa ni kuwa aliamini kwamba nyumba ya Israeli ilikuwa inakwenda kumrudishia ufalme wa Sauli baba yeke.

Mfalme alisema nini sasa kinamilikiwa ns Siba?

Mfalme alimwambia Siba kwamba yote yaliyokuwa ya Mefiboshethi sasa yanamilikiwa na yeye Siba.

2 Samuel 16:5-6

Shimei alimtenda nini Daudi na maofisa wote wa mfalme?

Shimei alimlaani Daudi na maaofisa wote wa mfalme na akarusha mavumbi na mawe kwao.

2 Samuel 16:7-10

Shimei alimwitaje Daudi?

Shimei alimwita Daudi mwovu na mtu wa damu.

2 Samuel 16:11-14

Daudi alitumaini Yahwe angefanya nini kwa maangaiko aliyofungiwa Daudi kwa laana aliyoipata siku hiyo?

Daudi alitumaini kwamba Yahwe angemlipa kwa mema kwa laana aliyoipokea siku hiyo.

2 Samuel 16:15-16

Hushai alisema nini kwa Absalomu, Ahithofeli, na watu wote wa Israeli walipokuja Yerusalemu?

Hushai alimwambia Absalomu, "Mfalme aishi milele! Mfalme aishi milele!"

2 Samuel 16:17-19

Hushai alimwambia Absalomu atakuwa wa nani?

Hushai alimwambia Absalomu kwamba yeye, Hushai, angekuwa wa yule Yahwe na watu wake wanayemchagua.

2 Samuel 16:20-21

Shauri la Ahithofeli kwa Absalomu kuhusu jambo la Absalomu kufanya lilikuwa nini?

Ahithofeli alimshauri Absalomu kulala na masuria wa baba yake ambao Daudi alikuwa amewaacha kulitunza kasiri.

2 Samuel 16:22-23

Ushauri wa Ahithofeli ulitazamwaje na Daudi na Absalomu?

Ushauri wa Ahithofeli ulitazamwa kama mtu alikuwa amesikia kutoka katika kinywa cha Mungu.

2 Samuel 17

2 Samuel 17:1-4

Ahithofeli alimshuri nini Absalomu na wazee wote wa Israeli juu ya jinsi angepaswa kumshambulia Daudi?

Ushauri wa Ahithofeli ulikuwa ni kuwa na jeshi kubwa kufanya shambulio la ghafla juu ya Daudi usiku alipokuwa amechoka tena dhaifu, na kuwarudisha watu wote kwa utawala wao.

2 Samuel 17:5-7

Absalomu alimwuliza Hushai ushauri wake kuhusu shauri la mpango wa Ahithofeli. Ushauri wa Hushai ulikuwaje?

Hushai alisema mpango haukuwa mzuri.

2 Samuel 17:8-10

Hushai alisema sababu gani kwamba mpango haukuwa mzuri?

Kwa sababu mara ya kwanza kushambuliwa na kuuawa kwa watu wa Absalomu, hata askari jasiri sana wangeogopa kwa kuwa mauaji yangetangazwa juu ya askari wa Absalomu.

2 Samuel 17:11-12

Hushai alimshauri Absalomu kufanya nini?

Hushai alimshauri Absalomu kukusanya jeshi la Waisraeli wote na kwenda vitani ili kwamba wangeweza kumpata Daudi na kumwua yeye na watu wake wote.

2 Samuel 17:13-14

Absalomu na watu wa Israeli walilipokeaje shauri la Hushai?

Walisema lilikuwa jema kuliko lile la Ahithofeli.

2 Samuel 17:15-16

Hushai alitaka taarifa gani makuhani waende kumpa Daudi?

Ujumbe ulikuwa kwamba Daudi asipige hema katika vivuko vya Araba, lakini avuke ili kwamba yeye na watu wake wasiuawe usiku huo.

2 Samuel 17:17-18

Jishi gani taarifa za Absalomu kumshambulia mfalme Daudi zilitegemewaje?

Mtumishi wa kike angekwenda na kuwaambia watu wawili ambao wangekwenda na kumwambia Daudi kuhusu mipango ya Absalomu.

Watu wawili hawa walifanya nini baada ya hawa watatu kuonwa na Absalomu kuambiwa?

Hao watu wawili walikwenda na kushuka kisimani katika ua wa mtu mmoja.

2 Samuel 17:19-20

Hawa watu wawili walisaidiwaje?

Mke wa mtu aliwafunika katika kisima ili kuwaficha wale wawili na baada ya watu wa Absalomu kuja wanawawinda, aliwambia maaskari kwamba hao watu walikuwa wamevuka mto.

2 Samuel 17:21-22

Baada ya wtu wa Absalomu kuondoka, hao watu wawili walifanyaje?

Walitoka kisimani na kwenda kumwambia Mfalme Daudi kuvuka Yordani ili yeye na watu wake wawe salama.

2 Samuel 17:23-26

Ahithofeli alifanyaje baada ya kuona kwamba ushauri wake haukuzingatiwa?

Ahithofeli alikwenda katika mji wake, kuweka mambo yake katika utaratibu na kujinyonga.

2 Samuel 17:27-29

Daudi na watu wake walitunzwaje nyikani?

Watu watatu walikuja na mahitaji na chakula kwa Daudi na watu wake kutumia kwa kulalia, kupikia, na kula.

2 Samuel 18

2 Samuel 18:1-2

Ujumbe gani mfalme Daudi aliusema kwa jeshi?

Mfalme Daudi aliliambia jeshi kwamba angekwenda vitani pamoja nao bila shaka.

2 Samuel 18:3-4

Mwitikio wa watu katika jeshi ulikuwa ni upi kwa ujumbe wa mfalme Daudi?

Watu katika jeshi walimwambia mfalme Daudi kwamba alikuwa na thamani ya watu elfu kumi, hivyo anapaswa kubaki mjini badala ya kwenda vitani.

2 Samuel 18:5

Maagizo gani mfalme Daudi aliyowapa majemedari kuhusu Absalomu?

Mfalme aliwambia majemedari kumtendea Absalomu kwa upole kwa ajili yake.

2 Samuel 18:6-8

Matokeo ya vita katika msitu wa Efraimu yalikuwa ni yapi?

Jeshi la Israeli lilishindwa mbele ya askari wa Daudi.

2 Samuel 18:9-11

Ni nini kilichomtokea Absalomu wakati nyumbu aliyekuwa amempanda alipita chini ya matawi ya mwaloni?

Absalomu aliachwa akining'inia kwa kichwa chake katika matawi ya mti.

Kwa nini Yoabu alikasirika alipoambiwa kuhusu Absalomu?

Yoabu alikasirika kwa sababu askari alitoa taarifa kuhusu Absalomu badala ya kumpiga hata chini.

2 Samuel 18:12-13

Kwa nini yule mtu hakumwua Absalomu?

Hakuwa tiyari kumwua Absalomu hata kwa pesa kwa sababu alikuwa amemsikia mfalme akisema kwamba kusiwepo wa kumgusa huyo kijana Absalomu.

2 Samuel 18:14-15

Yoabu alimfanyaje Absalomu?

Yoabu alitupa mshale katika moyo wa Absalomu akiwa hai alipokuwa amening'inia katika mti wa mwaloni.

2 Samuel 18:16-17

Mwili wa Absalomu ulifanywaje?

Mwili wa Absalomu ulitupwa katika shimo kubwa msituni na kisha kufukiwa chini ya rundo kubwa la mawe.

2 Samuel 18:18

Kwa nini Absalomu alijenga nguzo kwa ajili yake alipokuwa yu ngali hai?

Absalomu alijenga nguzo kubwa iliyoitwa mnara wa Absalomu, kuchukua kumbukumbu ya jina lake kwa kuwa hakuwa na mwana.

2 Samuel 18:19-20

Kwa nini Ahimaasi alionywa kwenda kumpasha mfalme habari kwamba Yahwe alikuwa amemwokoa mfalme kutoka kwa adui zake?

Ahimaasi alionywa asimpelekee mfalme habari kwa sababu mwana wa mfalme alikuwa ameuawa.

2 Samuel 18:21-23

Kwa nini Ahimaasi bado alitaka kwenda kumwambia Daudi habari?

Ahimaasi alijua kwamba Yoabu alikuwa amempa Mkushi habari lakini Ahimaasi bado alitaka kuwa wa kwanza kumwambia Daudi habari njema.

2 Samuel 18:24-25

Mfalme alifikiri nini alipoambiwa kwamba kulikuwa na mtu akikimbia peke yake na kuukaribia mji?

Mfalme alijua kwamba mkimbiaji alikuwa akileta habari.

2 Samuel 18:26-27

Mfalme alifikiri nini tena aliposikia kwamba kulikuwa na mkimbiaji mwingine akikimbia peke yake?

Mfalme alijua kuwa alikuwa akileta habari.

2 Samuel 18:28-30

Ni habari gani Ahimaasi aliyoileta kwa mfalme?

Ahimaasi alimwambia mfalme kwamba Yahwe alikuwa amewatoa waliokuwa kinyume cha mfalme.

Ahimaasi alimjibuje mfalme alipoulizwa kuhusu hali ya Absalomu?

Ahimaasi alisema aliona mchafuko mkubwa, alikini hakujua ulihusu nini.

2 Samuel 18:31-33

Jibu la Mkushi lilikuwaje alipoulizwa na mfalme kuhusu hali ya Absalomu?

Mkushi alimwambia mfalme kwamba adui wa mfalme wawe kama huyo kijana.

Mfalme aliitikaje alipoambiwa habari ya kifo cha mwanawe?

Mfalme aliuzunika sana aliposikia habari na alitamani angekufa badala ya mwanawe.

2 Samuel 19

2 Samuel 19:1-2

Kwa nini ushindi uligeuzwa kuwa maombolezo kwa jeshi lote siku hiyo?

Ni kwa sababu jeshi liliambiwa kwamba mfalme alikuwa akimwombolezea mwanawe.

2 Samuel 19:3-4

Kilio cha mfalme kilikuwa kipi?

Mfalme alilia, "Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwanangu!"

2 Samuel 19:5-6

Yoabu alisema aliamini nini kingempendeza mfalme?

Yoabu alisema kwamba mfalme angependezwa kama Absalomu angeishi na wao, jeshi la mfalme, wangekuwa wamekufa.

2 Samuel 19:7-8

Yoabu alimwambia mfalme nini kingetokea kama mfalme asingeinuka, kutoka na kuongea na askari wake kwa upole?

Yoabu alisema kama mfalme asingetoka, hakuna mtu ambaye angesalia kwake usiku huo.

Watu wote walikuja wakati gani mbele ya mfalme?

Watu wote walikwenda mbele ya mfalme baada ya kuambiwa kwamba mfalme alikuwa ameketi langoni.

2 Samuel 19:9-10

Watu wote wa makabila ya Israeli walikuwa wajadiliana nini?

Walikuwa wakijadili kwamba wamlete au wasimlete mfalme tena.

2 Samuel 19:11-12

Mfalme alimtuma nani ili aongee na wazee wa Yuda kuhusu kumrudisha mfalme?

Daudi alimtuma Sadoki na kwa Abiathari makuhani ili kuongea na wazee wa Yuda.

2 Samuel 19:13-15

Daudi alisema nani atakuwa kapteni wa jeshi lake badala ya Yoabu?

Daudi alisema Amasa angekuwa kapteni mahali pa Yoabu.

Kwa nini watu wa Yuda walikuja Gilgali?

Watu wa Yuda walikuja Gilgali kumpokea mfalme na kumsindikiza kuvuka Yordani.

2 Samuel 19:16-18

Nani alivuka Yordani mbele ya Mfalme?

Shimei, watu elfu moja kutoka Benjamini pamoja naye, na Siba, mtumishi wa Sauli, wanawe kumi na watano na watumishi wake ishirini pamoja naye, walivuka Yordani mbele ya mfalme.

2 Samuel 19:19-20

Kwa nini Shimei alikuja wa kwanza kutoka familia yote ya Yusufu kumpokea mfalme?

Shimei alishuka kumpokea mfalme kwa sababu Shimei alijua kwamba alikuwa amemkosa mfalme.

2 Samuel 19:21-23

Mfalme alimwambia nini Shimei baada ya Abishai kusema kwamba Shimei anapaswa kufa?

Mfalme alimwambia Shimei hatakufa na kumwahidi kwa kiapo.

2 Samuel 19:24-25

Mefiboshethi alionekanaje alipokuja kumpokea mfalme?

Hakuwa amevalisha miguu yake, wala kunyoa ndevu zake, wala kufua nguo zake tangu mfalme alipoondoka.

2 Samuel 19:26-28

Mefiboshethi alitoa sababu gani baada ya mfalme kumwuliza, "Kwa nini haukwenda pamoja nami, Mefiboshethi?"

Mefiboshethi alimwambia mfalme kwamba Siba mtumishi wake alikuwa amemdanganya.

Ni nini zaidi Mefiboshethi alisema Siba alikuwa amemtendea?

Mefiboshethi alisema kwamba Siba alikuwa amemchongea kwa mfalme.

2 Samuel 19:29-30

Mefiboshethi alijibuje kwa mfalme wakati mfalme alipomwambia kwamba alikuwa ameamua kwamba watagawana mashamba?

Mefiboshethi alimwambia mfalme kwamba Siba achukue yote kwa kuwa mfalme alikuwa amerudi salama nyumbani kwake.

2 Samuel 19:31-33

Barzilai alikuwa amefanya nini kwa mfalme?

Barzilai alikuwa amemhudumia mfalme kwa mahitaji alipokuwa Mahanaimu.

2 Samuel 19:34-36

Kwa ufupi, kwa nini Barzilai alisema asiende Yerusalemu pamoja na mfalme?

Barzilai alisema kwamba asiende na mfalme kwa sababu alikuwa mzee sana na hakuwa na muda mrefu wa kuishi, hakuweza kuonja alichokula wala kunywa, hakuweza kusikia vema, na hakutaka kuwa mzigo kwa mfalme.

2 Samuel 19:37-39

Barzilai alimwomba nini mfalme?

Barzilai alimwomba mfalme amruhusu arudi nyumbani ili afe katika mji wake, na kumruhusu Kimhamu kuvuka pamoja na mfalme na kumtendea Kimhamu yaliyoonekana mema kwa mfalme.

2 Samuel 19:40-41

Ni nani aliyevuka kuelekea Gilgali pamoja na mfalme?

Kimhamu, jeshi lote la Yuda na nusu ya jeshi la Israeli lilivuka Gilgali pamoja na mfalme.

2 Samuel 19:42-43

Kwa nini watu wa Israeli walisema walikuwa na haki zaidi kwa Daudi kuliko watu wa Yuda?

Watu wa Israeli walisema walikuwa na haki zaidi kwa Daudi kwa sababu walikuwa makabila kumi yakihusiana na mfalme.

Kati ya watu wa Yuda na watu wa Israeli, ni wapi maneno yao yalikuwa makali zaidi?

Maneno ya watu wa Yuda yalikuwa makari zaidi kuliko maneno ya wa Israeli.

2 Samuel 20

2 Samuel 20:1-2

Kwa nini Siba alihesabiwa kuwa mfanyafujo?

Siba alihesabiwa kuwa mfanyafujo kwa sababu aliwahamasisha watu wa Israeli kutokuwa na sehemu kwa Daudi.

Ni jinsi gani mwitikio wa watu wa Yuda kwa Siba ni tofauti na mwitikio wa watu wa Israeli?

Watu wa Yuda kwa ukaribu walimfuata mfalme wao, lakini watu wa Israeli walimwacha Daudi na kumfuata Siba.

2 Samuel 20:3

Ni jinsi gani uhusiano wa Daud na wajakazi wake ulivyobadilika baada ya kuwaweka katika nyumba iliyokuwa chini ya ulinzi?

Daudi aliwapa mahitaji yao, lakini hakulala nao tena hivyo waliishi kama wajane.

2 Samuel 20:4-5

Mfalme alimwambia Amasa kufanya nini?

Mfalme alimwambia Amasa kuwaita watu wa Yuda na kwamba yeye pia awepo.

2 Samuel 20:6-8

Ni jinsi gani Daudi aliitikia taarifa ya kwamba watu wa Israeli walikuwa wamemwacha na kumfuata Siba?

Daudi alijibu kwa kumpa maelekezo Abishai kuwachukua askari wa Daudi na kumfuatia Siba kabla hajaingia katika miji wenye ngome.

2 Samuel 20:9-10

Yoabu alimtenda nini Amasa baada ya kumshika kidevu chake kwa mkono wa kuume ili ambusu?

Yoabu alimpiga Amasa kwa jambia katika mkono wake wa kushoto.

2 Samuel 20:11-13

Jinsi gani mmojawapo wa watu wa Yoabu alivyofanya baada ya kuchomwa kwa Amasa?

Mmoja wa watu wa Yoabu alimweka Amasa kando ya njia katika shamba na kumfunika kwa vazi na kisha kuwatia changamoto kila aliyependa kumfuata Yoabu na Daudi kumfuata Yoabu.

2 Samuel 20:14-16

Yoabu na watu wa Yuda walifanya nini walipompata Sheba na watu wa Israeli huko Abeli wa Bethi Maaka?

Yoabu na watu wa Yuda walijenga buruji dhidi ya ukuta wa mji na kujaribu kuugonga ili uanguke.

2 Samuel 20:17-19

Mwanamke aliulezeaje mji wa Abeli kwa Yoabu?

Mwanamke aliuelezea kama mji uliokuwa miongoni mwa miji yenye amani na mwaminifu katika Israeli na pia kama mama katika Israeli.

Kwa ufupi mwanamke alimwuliza ni Yoabu?

Mwanamke alimwuliza kwa nini alimwuliza kwa nini alikuwa anaungamiza mji wa Abeli?

2 Samuel 20:20-22

Ni sharti lipi Yoabu alilolompa mwanamke ili watu wa Yuda wauache mji?

Sharti lilikuwa kwamba ikiwa mji ungemtoa Sheba kwao, wangeondoka na kuuacha mji.

Ni jinsi gani watu wa mji pamoja na mwanamke walivyoitikia sharti la Yoabu?

Walikiondoa kichwa cha Sheba na kukirusha juu ya ukuta kwa Yoabu kama mwanamke alivyokuwa ameahidi.

2 Samuel 20:23-26

Wajibu wa Adoramu ulikuwa upi?

Wajibu wa Adoramu ulikuwa ni mkuu wa wafanya kazi ya shuruti.

2 Samuel 21

2 Samuel 21:1

Kwa nini kulikuwa na njaa katika siku za Daudi kwa miaka mitatu?

Hii ilikuwa ni kwa sababu Sauli na familia yake ya mauaji aliwauwa Wagibeoni.

2 Samuel 21:2-3

Kwa nini mfalme Daudi alitaka kufanya upatanisho kwa Wagibeoni?

Kwa sababu watu wa Israeli walikuwa wamewapia kutokuwauwa, hata hivyo Sauli aliwauwa kwa wivu wa wana wa Israeli na Yuda.

2 Samuel 21:4

Daudi alikubali kufanya nini kwa ajili ya kupatanisha kwa ajili ya maovu waliyokuwa wametendwa Wagibeoni?

Daudi alikubali kufanya chochote Wagibeoni wangemwambia.

2 Samuel 21:5-6

Wagibeoni waliomba nini kutoka kwa Daudi ili kupatanisha kwa matendo ya Sauli?

Wagibeoni waliomba wapewe watu saba waliokuwa wa uzao wa Sauli ili wawatundike mbele ya Yahwe.

2 Samuel 21:7-9

Daudi aliitikaje kwa ombi la Wagibeoni?

Daudi alijibu ombi kwa Wagibeoni kwa kumhifadhi Mefiboshethi huku akikabidhi wana wawili la Rispa na wana watano wa Mikali waliotundikwa na Wagibeoni katika mlima mbele ya Yahwe.

2 Samuel 21:10-11

Rispa alifanya nini ili kuonesha huzuni yake kwa kifo cha wanawe?

Rispa alitandaza nguo kwa ajili yake kando ya miili ya waliokufa katika mlima na hakuwaruhusu ndege wa angani au hayawani wa porini kuigusa miili.

2 Samuel 21:12-14

Daudi alichukua mifupa ya Sauli na Yonathani kutoka kwa nani?

Daudi alichukua mifupa ya Sauli na Yonathani kutoka kwa watu wa Yabeshi Gileadi.

2 Samuel 21:15-19

Abishai alimwokoaje Daudi alipokuwa ameshindwa na mashambulizi ya vita?

Abishai alimwokoa kwa kumwua Ishbenobu Mfilisiti aliyekuwa ameazimu kumwua Daudi.

Kwa nini watu wa Daudi walisisitiza kwamba hatakwenda nao tena vitani?

Hii ni kwa sababu waliogopa kwamba anaweza kuizima taa ya Israeli.

2 Samuel 21:20-22

Baadhi ya watu ambao watu wa Daudi na askari wake waliwauwa katika Gathi walikuwa wa uzao wa nani?

Daudi na watu wake waliwauwa wazao kadhaa wa Mrefai wa Gadhi.

2 Samuel 22

2 Samuel 22:1-2

Daudi aliimba lini wimbo kwamba Yahwe alikuwa mwamba aliyemwokoa?

Daudi aliimba wimbo huu siku Yahwe aliyomwokoa na mkono wa Sauli na adui zake.

2 Samuel 22:3-4

Daudi alisema sababu ilikuwa ipi kwa yeye kumwita Yahwe mwamba wake?

Daudi alisema ni kwa sababu Yahwe mwamba wake alikuwa anastahili kusifiwa.

2 Samuel 22:5-6

Daudi alijisikia kama nini alipokuwa mkononi mwa adui zake?

Daudi alihisi kama alikuwa amezungukwa na mawimbi ya mauti na vifungo vya kuzimu.

2 Samuel 22:7

Daudi aliitikiaje kwa hali za kuogofya zililomkabili?

Katika taabu yake, Daudi alimwita Yahwe aliyesikiliza sauti yake ya msada katika hekalu lake.

2 Samuel 22:8-9

Nini kilitendeka kwa sababu ya hasira ya Mungu?

Dunia na misingi ya anga ilitetemeka kwa sababu Mungu alikuwa na hasira, na moshi ukatoka katika pua zake na moto uwakao ukatoka katika kinywa chake.

2 Samuel 22:10-12

Mungu alishukaje kutoka mbinguni?

Yahwe alipanda katika kerubi na kuruka katika mbawa za upepo.

2 Samuel 22:13-15

Yahwe aliwatawanyaje adui zake?

Yahwe aliwatawanya adui zake kwa mishale na miale ya radi.

2 Samuel 22:16

Ni kwa jinsi gani misingi ya dunia ilivyofunuliwa?

Misingi ya dunia alifunuliwa kwa sauti ya Yahwe kwa vita na mvumo wa pumzi ya pua zake.

2 Samuel 22:17-18

Yahwe alimwokoaje Daudi kutoka kwao waliomchukia?

Yahwe alishuka chini kutoka juu na kumwinua kutoka katika maji yafurikayo.

2 Samuel 22:19-21

Kwa nini Yahwe alimwokoa Daudi?

Yahwe alimwokoa Daudi kwa sababu alipendezwa naye.

2 Samuel 22:22-23

Daudi alitunzaje njia za Yahwe?

Daudi alizitunza njia za Yahwe kwa kutunza maagizo ya Yahwe badala ya kutonda kwa uovu na kumwacha Mungu.

2 Samuel 22:24-27

Kilitokea nini baada ya Daudi kujiepusha na dhambi

Yahwe alimrudisha Daudi katika kipimo cha utakatifu wake kwa sababu alijiepusaha na uovu.

2 Samuel 22:28-29

Yahwe huwafanyaje wenye kiburi?

Yahwe huwashusha wenye kiburi.

2 Samuel 22:30-31

Yahwe ni nani kwa kila mtu anayemkimbilia?

Yahwe ni ngao yake.

2 Samuel 22:32-35

Kwa nini Daudi alimwesabu Yahwe kuwa kimbilio lake?

Hii ni kwa sababu Yahwe alikuwa mwamba wake na uwaongoza watu wasio na lawama katika njia zao.

2 Samuel 22:36-41

Kwa nini miguu ya Daudi haikuteleza?

Kwa sababu Yahwe alikuwa ni ngao ya wokovu wake na alikuwa amemtengenezea nafasi kwa miguu yake.

2 Samuel 22:42-43

Daudi alifanya nini kwa adui zake walipoomba msaada kwa Yahwe?

Baada ya adui za Daudi kuomba msaada kwa Yahwe Daudi aliwapiga katika vipande kama mavumbi juu ya nchi na kuwaponda kama mavumbi mitaani.

2 Samuel 22:44-46

Yahwe alimtendea nini Daudi?

Yahwe alimwokoa kutoka katika mashitaka ya watu wake mwenyewe na kumlinda kama kiongozi wa mataifa.

2 Samuel 22:47-49

Yahwe alitenda nini badala ya Daudi?

Yahwe alimlipia kisasi na kumweka huru mbali na adui zake.

2 Samuel 22:50-51

Kwa nini Daudi aliliimbia sifa jina la Yahwe?

Daudi aliimba sifa jina la Yahwe kwa sababu alimpa ushindi mkuu na kumwonesha uaminifu wa agano.

2 Samuel 23

2 Samuel 23:1-2

Daudi alifahamika kwa kitu gani?

Daudi alikuwa mtu aliyekuwa anaheshimiwa sana na aliyetiwa mafuta na Mungu wa Yakobo.

2 Samuel 23:3-5

Mungu wa Israeli alisema nini kwa Daudi?

Mungu wa Israeli alisema kwamba atawalaye kwa hofu ya Mungu atakuwa kama nyota ya asubuhi wakati wa jua kuchomoza.

2 Samuel 23:6-8

Kwa nini wasiofaa watakuwa kama miba kutupwa mbali?

Watakuwa kama miiba kwa sababu hawawezi kukusanywa kwa mikono.

2 Samuel 23:9-10

Elieza aliwashindaje Wafilisiti walipokutanika kwa vita?

Elieza aliwapiga Wafilisiti mpaka mkono wake ukachoka na akajitahidi kuushika upanga.

2 Samuel 23:11-14

Shama alitetea nini dhidi ya Wafilisiti?

Shama alisimama katikati ya shamba la dengu na kulitetea.

2 Samuel 23:15-17

Wale watu mashujaa watatu walifanya nini walipoambiwa Daudi alikuwa akitamani maji ya kisima cha Bethlehemu?

Mashujaa watatu walipenya katikati ya jeshi la Wafilisiti na kuleta maji kwa Daudi kutoka katika sikima cha Bethlehemu.

Kwa nini Daudi alikataa kunywa maji kutoka katika kisima cha Bethlehemu?

Alikataa kwa watu walikuwa wameyahatarisha maisha yao, hivyo aliyamwaga mbele ya Yahwe kama sadaka.

2 Samuel 23:18-19

Abishai alikuwa akifahamika kwa kitu gani?

Abishai alikuwa amefanywa kepteni juu ya askari watatu na aliua watu mia tatu kwa mkukuki wake mara moja.

2 Samuel 23:20-39

Benaya alimwuaje Mmisri aliyekuwa mtu mkubwa sana?

Benaya, ambaye alikuwa na fimbo tu, alipigana na Mmisri aliyekuwa na mkuki katika mkono wake. Benaya alishika mkuki kutoka mkono wa Mmisri na kumwua kwa huo.

2 Samuel 24

2 Samuel 24:1-2

Daudi alimwambia Ayubu kufanya nini?

Daudi alimwambia Yoabu kuhesabu watu wa makabila yote ya Israeli kuamua idadi kamili ya watu wawezao kupiga vita.

2 Samuel 24:3-7

Kwa nini Yoabu alisita kufanya kama Daudi alivyosema?

Yoabu alisita kumtii Daudi kwa sababu hakufahamu kwa nini mfalme alitaka jambo hili kutendeka.

2 Samuel 24:8-9

Ilichukua muda gani kwa Yoabu kupita katika nchi yote na kisha kurudi Yerusalemu?

Ilichukua miezi tisa na siku ishirini kwa Yoabu kupita katika nchi yote na kisha kurudi Yerusalemu.

Wapiganaji wangapi walihesabiwa na Yoabu?

Yoabu alihesabu watu laki nane mashujaa katika Israeli na laki tano katika Yuda.

2 Samuel 24:10

Kwa nini moyo wa Daudi ulimchoma baada ya Yoabu kuwahesbu watu?

Moyo wa Daudi ulimchoma kwa sababu alitambua kwamba alikuwa ametenda kwa upumbavu na kufanya dhambi kubwa.

2 Samuel 24:11-12

Yahwe alitoa ujumbe gani kwa Daudi kupitia nabii wake?

Yahwe alimwambia Daudi kuchagua kati ya machaguo matatu.

2 Samuel 24:13-14

Ni machaguo yapi matatu Yahwe aliyompa Daudi kupitia nabii Gadi?

Yahwe alimwambia achakue kati ya miaka mitatu ya njaa, au akimbie mbele ya adui zake miezi mitatu, au siku tatu ya tauni katika nchi.

2 Samuel 24:15-16

Kwa nini si zaidi ya watu elfu sabini waliokufa katika tauni?

Ni watu sabini elfu tu waliokufa katika tauni kwa sababu Yahwe alibadili nia yake na kuurudisha mkono wake.

2 Samuel 24:17

Daudi alimwomba nini Yahwe baada ya kutambua dhambi yake kuu?

Daudi alimwomba Yahwe kumwadhibu yeye na familia ya baba yake badala ya watu wa Israeli.

2 Samuel 24:18-20

Gadi alimwamia Daudi kufanya nini?

Gadi alimwambia Daudi kupanda na kujenga madhabahu kwa Yahwe katika kiwanja cha kupuria nafaka cha Arauna.

2 Samuel 24:21-23

Kusudi la Daudi kwenda kwa Arauna lilikuwa nini?

Daudi alitaka kununua uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna ili kwamba aweze kujenga madhabahu kwa Yahwe ili kuondoa tauni kwa watu.

2 Samuel 24:24-25

Kwa nini Daudi alisisitiza kununua kiwanja cha Arauna cha kupulia nafaka kwa thamani yake?

Daudi alimwambia Arauna kwamba alisisitiza kukinunua kwa thamani yake kwa sababu asingemtolea Yahwe kama sadaka ya kuteketezwa kitu chochote asichokigharimia.

Daudi alilisimamishaje pigo katika Israeli?

Daudi alilisimamisha pigo katika Israeli kwa kumjengea Yahwe madhabahu na kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani juu yake.