Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Zephaniah

Zephaniah 1

Zephaniah 1:1-3

Mungu alimwambia nini Sefania atafanya kwa ndege wa mbinguni, samaki wa baharini na kwa mtu?

Mungu alisema atawaangamiza na kuwakatilia mbali.

Mungu alimwambia nini Sefania atafanya kwa ndege wa mbingini, samaki wa baharini na kwa mtu?

Mungu alisema atawaangamiza na kuwakatilia mbali.

Zephaniah 1:4-6

Nini jina la sanamu ambaye aliyemsema Mungu atamkatili mbali kila aliyebaki?

Atakatilia mbali kila baki la baali.

Hufanya nini walio darini kwenye nyumba ya ibada?

Walio darini huiabudu miili ya mbinguni

Zephaniah 1:7-9

Watu wanapaswa kufanya nini katika uwepo wa Yahweh?

Wanapaswa kuwa kimya katika uwepo wa Yahweh.

Yahweh aliwafanyia akina nani aliposema atawahukumu katika siku ya dahabihu?

Yahweh atawahukumu wakuu na watoto wa wafalme, kilammoja aliyevaa nguo za kigeni, wale ambao huruka juu kingo za mlango, na wale ambao hujaza nyumba za bwana zao ukatili na udanganyifu.

Zephaniah 1:10-11

Sauti gani itakuja kutoka Lango la Samaki na robo ya pili katika siku ile?

Kilio cha uchungu, na maombolezo yatakuja katika siku ile.

Kitatokea nini kwa wafanya biashara katika siku ile?

Wataharibiwa, na wale wote waliopima fedha watakatiliwa mbali.

Zephaniah 1:12-13

Baadhi ya wanaume wa Yerusalemu walisema nini kuhusu Yahweh?

Walisema, "Yahweh hatafanya chochote, ama kizuri au kiovu!"

Zephaniah 1:14-16

Ni siku gani itakuwa siku ya ghadhabu, siku ya uchungu, na siku ya giza?

Siku kubwa ya Yahweh itakuwa siku ya ghadhabu, uchungu, na giza.

Ni siku gani itakuwa siku ya ghadhabu, siku ya uchungu, na siku ya giza?

Siku kubwa ya Yahweh itakuwa siku ya ghadhabu, uchungu, na giza.

Zephaniah 1:17-18

Ni damu ya akina nani itamwagwa kama vumbi katika siku ya Yahweh?

Wale waliofanya dhambi dhidi ya Mungu.

Nini hakitaweza kuwaokoa katika siku ile?

Fedha zao na dhahabu zao havitaweza kuwaokoa.

Zephaniah 2

Zephaniah 2:1-3

Watu lazima wafanye nini kuiepuka hasira kali ya ghadhabu ya Yahweh?

Watu lazima watafute haki na unyenyekevu kuiepuka ghadhabu ya Yahweh.

Zephaniah 2:4-7

Kitatokea nini kwa wale ambao hawatajihadhari na maonyo ya Yahweh?

Watu wote ambao hawatajihadhari kwa maonyo ya Yahweh watang'olewa na kuharibiwa.

Kitatokea nini kwa wale ambao hawatahihadhari na maonyo ya Yahweh?

Watu wote ambao hawatajihadhari kwa maonyo ya Yahweh watang'olewa na kuharibiwa.

Zephaniah 2:8-11

Miji ya Moabu na Ammon itakuwa kama nini?

Moabu itakuwa kama Sodoma, na watu wa Ammon kama Gomorra.

Zephaniah 2:12-14

Aina gani ya ndege watafanya viota juu ya nguzo za Ashuru?

Bundi watafanya viota juu ya nguzo za Ashuru.

Zephaniah 2:15

Utakuja kuwaje mji wa kujitapa?

Mji wa kujitapa utakuwa wa heshima, sehemu watakapolala chini wanyama ndani yake.

Zephaniah 3

Zephaniah 3:3-4

Wakuu wa mji wa vurugu wako kama nini?

Wakuu wa mji wa vurugu wako kama simba waungurumao.

Zephaniah 3:5

Wakati gani Yahweh ataleta haki?

Yahweh ataleta haki kutoka asubuhi mpaka jioni.

Zephaniah 3:6-7

Yahweh anatumaini watu watafanya nini?

Yahweh alitumaini watu watamhofu yeye na kupokea masahihisho.

Zephaniah 3:8

Uamuzi gani Yahweh ameufanya kuhusu mataifa?

Yahweh ameamua kuyakusanya mataifa na kumwaga hasira yake na ghadhabu juu yao.

Zephaniah 3:9-11

Baadaye Yahweh atawaita watu kufanya nini?

Yahweh atawaita watu kumtumikia yeye wakisimama bega kwa bega.

Zephaniah 3:12-13

Jinsi gani mabaki ya Israeli yatabadilika baada ya hili?

Mabaki ya Israeli hawataendelea tena kutofanya haki na kusema uongo.

Zephaniah 3:14-18

Kwa nini Israeli wataimba na kufurahi?

Israeli wataimba na kufurahi kwa sababu Yahweh ameichukulia mbali hukumu yao.

Kwa nini Israeli wataimba na kufurahi?

Israeli wataimba na kufurahi kwa sababu Yahweh ametupilia mbali hukumu yao.

Zephaniah 3:19-20

Ni akina nani Yahweh atamwokoa kutoka kwa wale waliowanyanyasa Israeli?

Yahweh atawaokoa vilema na kuwakusanya pamoja waliotawanyika.

Kwa nini mataifa yote yatamtii na kumsifu Israeli?

Mataifa yote yatamtii na kumsifu Israeli wakati watakapona kwamba Yahweh amewarudisha.