Philippians
Philippians 1
Philippians 1:1-2
Ni akina Paulo aliwaandikia waraka huu ?
Paulo aliwaaandikia watu wote waliotengwa katika Kristo wanaoishi Filipi, kujumuisha na waangalizi na wahudumu.
Philippians 1:3-6
Kwa nini Paulo anamshukuru Mungu kwa ajili ya ya Wafilipi?
Paulo alimshukuru Mungu kwa ajili ya waumini wa Wafilipi kwenye injili tangu siku ya kwanza hadi sasa.
Paulo alikuwa na uhakika gani juu ya Wafilipi?
Paulo alikuwa na uhakika kwamba aliyeanzisha kazi nzuri ndani yao ndiye atakaye hitimisha.
Philippians 1:7-8
Ni kwa mambo gani Wafilipi walikuwa washirika wenza wa Paulo?
Wafilipi walishiriki na Paulo katika kifungo chake, na katika kuitetea na kuithibitisha injili.
Philippians 1:9-11
Paulo aliomba kitu gani ambacho kingeongezeka zaidi na zaidi miongoni mwa Wafilipi?
Paulo aliomba kwamba upendo uongezeke zaidi na zaidi miongoni mwa Wafilipi.
Paulo alitamani Wafilipi wajazwe kwa nini?
Paulo alitamani Wafilipi wajazwe na matunda ya haki.
Philippians 1:12-14
Ni kwa njia gani kifungo cha Paulo kiliifanya injili ienee zaidi?
kifungo cha Paulo kwa ajili ya Kristo kilifahamika sana kwa sehemu kubwa, na ndugu wengi walikuwa sasa wakiongea kwa ujasiri habari za Yesu.
kifungo cha Paulo kiliimarishaje injili?
kifungo cha Paulo kwa ajili ya Kristo kujulikana zaidi, na ndugu wengi walianza kuhubiri kwa ujasiri.
Philippians 1:15-17
Kwa nini baadhi wanamuhubiri Krsto kwa yao na fitina?
Baadhi walimhubiri Kristo kwa faida yao na fitina walidhani wangweza kumuongezea huzuni gerezani.
Philippians 1:18-19
Paulo alijibu nini juu ya wale walikuwa wakihubiri kwa nia nzuri na wale walikuwa na nia mbaya?
Paulo alifurahia kwamba kwa njia yoyote ile Kristo anahubiriwa.
Philippians 1:20-21
kitu gani Paulo alitamani kukifanya akiwa hai au akiwa amekufa?
Paulo alitamani sana kumpa Kristo utukufu akiwa hai au akiwa amekufa.
Paulo alisema kuishi ni nini na kufa ni nini?
Paulo alisema kuishi ni Krsto, na kufa ni faida.
Philippians 1:22-24
Ni mawazo gani ambayo yalimsukuma Paulo katika mielekeo miwili tofauti?
Paulo alikuwa akisukumwa na mawazo mawili, kuwa pamoja na Kristo katika kifo au kubaki katika mwili ili aendelee na kazi yake.
Ni uchaguzi gani zilimvuta Paulo katika mwelekeo tofauti?
Paulo alivutwa na uchaguzi wa na Kristo katika kifo, au kubakia kwenye mwili kuendelea na kazi yake ngumu yenye ujira.
Philippians 1:25-27
kwa kusudi gani Paulo alikuwa na uhakika wa kubaki katika mwili pamoja na Wafilipi?
Paulo alikuwa na uhakika kwamba angeweza kubaki na Wafilipi kwa ajili ya maendeleo na furaha katika imani.
kwa vyovyote Wafilipi au mbali na wao, Paulo alitaka kusikia nini kuhusu Wafilipi?
Paulo alitaka kusikia kwamba Wafilipi wamesimama imara katika roho moja, nia moja wakishindania imani ya injili kwa pamoja.
Philippians 1:28-30
Wafilipi hawakuwaogopa watu waliokuwa wakiwapinga, jambo hili liliashiria nini?
Wafilipi hawakuogopa maadui, ilikuwa ni ishara ya uharibifu wa maadui zao, lakini ilikuwa ni ishara ya wokovu kwao.
Ni mambo gani mawili Wafilipi walipewa na Mungu?
Wafilipi walipewa na Mungu wamwamini Kristo, lakini pia kwamba kuteswa badala yake.
Philippians 2
Philippians 2:1-2
Ni jambo gani Paulo aliwaambia Wafilipi ni lazima wafanye kukamilisha furaha yake?
Wafilipi ni lazima kuwa na fikra moja, upendo mmoja, na kuwa na kuwa wamoja katika roho na fikra.
Philippians 2:3-4
Paulo anawaelezeaje wafilipi kutenda kwa watu wengine?
Wafilipi waweze kujali watu wengine kuwa bora zaidi yao.
Philippians 2:5-8
Paulo anasema tuwe na nia kama ya nani?
Paulo anasema tuwe na nia kama ya Yesu
Kristo Yesu alijifunua katika umbo gani?
Kristo Yesu alijifunua katika umbo la Mungu
Kristo Yesu alichukua umbo gani?
Kristo Yesu alichukua umbo la mtumishi, katika mwonekano wa mwanadamu.
Ni jinsi gani Yesu alijinyenyekeza?
Yesu alijinyenyekeza kwa kutii hadi kufa msalabani.
Philippians 2:9-11
Mungu alifanya nini kwa Yesu?
Amemtukuza na kumpa jina kubwa lipitalo majina yote
Kila ulimi utakiri nini?
Kila ulimi utakiri kwamba Yesu ni Bwana.
Philippians 2:12-13
Kwa jinsi gani wafilipi wawajibike kwa wokovu?
Wafilipi wawajibike katika wokovu kwa Kuwa na hofu na kutetemeka.
Mungu anatendaje kazi na waumini?
Mungu hutenda kazi na waumini wote ili kunia na kutenda yampendendezayo.
Philippians 2:14-16
Kila jambo lifanyike bila nini?
Kila jambo lazima lifanyike bila Malalmiko na mabishano
Philippians 2:17-18
Ni kwa lengo gani Paulo anajitoa maisha yake?
Paulo anajitoa maisha yake kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na huduma ya imani ya Wafilipi
Ni jambo gani Paulo analo, pia anataka Wafilipi wawe nalo?
Paulo anawataka Wafilipi wawe na furaha kubwa kama yeye.
Philippians 2:19-21
Kwa nini Timotheo ni msaidizi wa pekee kwa Paulo?
Timotheo ni msaidizi wa pekee wa Paulo kwa sababu alikuwa na nia ya kweli kwa Wafilipi na sio kwa ajili ya mapenzi yake.
Philippians 2:22-27
Paulo anatajia kuwaona Wafilipi?
Ndio, Paulo anatarajia kuwaona Wafilipi baada ya mda mfupi
Philippians 2:28-30
Kwa nini Epafradito alikaribia kufa?
Epafratido alikaribia kufa kwa kufanya kazi ya Kristo, kumhudumia Paulo na kumpatia Paulo mahitaji.
Philippians 3
Philippians 3:1-5
Paulo aliwaonya waumini wajihadhari?
Paulo aliwaonya waamini wajihadhari na mbwa, watenda kazi wabaya, na wale wakatao miili yao.
Ni waatahiriwa wa namna gani wa kweli ambao Paulo anawasema?
Paulo anasema watahiriwa wa kweli ni wale wanaoabudu Roho wa Mungu, kumtukuza Kristo Yesu na kutokuwa na ujasiri katika mwili.
Philippians 3:6-7
Paulo anelezeaje mwenendo wake wa nyuma kwa kulinganisha na haki ya sheria?
Paulo anaelezea tabia yake ya kwanza kuwa hakuwa na hatia katika kuifuata sheria.
je, sasa Paulo analichukuliaje tumaini lake katika mwili aliokuwa nao siku za nyuma?
Sasa Paulo anahesabu yote yaliyopita katika mwili wake kama hayana maana kwa sababu ya Kristo.
Philippians 3:8-11
Ni kwa kusudi gani Paulo anayafikiria mambo yote kuwa uchafu sasa?
Paulo anafikiria mambo yote kama uchafu ili ampate Kristo.
Ni haki gani ambayo Paulo anayo?
Sasa Paulo anahaki kutoka kwa Mungu ipatikanayo katika Kristo,
Paulo anaushirika katika Kristo katika nini?
Paulo anaushirika katika mateso ya Kristo
Philippians 3:12-16
Ingawa bado hajawa kamili, Paulo anaendelea kufanya nini?
Paulo anaendelea kusonga mbele.
Ni lengo gani Paulo analotaka kufikia mbele?
Paulo anataka kufikia lengo ili apate tuzo ya juu ya wito wa Mungu katika Kristo Yesu.
Philippians 3:17-19
Paulo anawaambia Wafilipi wafanye nini kulingana na mfano wa mwenendo wake?
Paulo anawaambia Wafilipi kuungana naye na wamuige yeye katika mwenendo wake.
Nini mwisho wa wale wanaofikiri mungu wao ni tumbo lao na kufikiria kuhusu mambo ya duniani?
Wale ambao mungu wao ni tumbo lao na wanafikiria kuhusu mambo ya duniani mwisho wao ni uharibifu.
Philippians 3:20-21
Paulo anasema wenyeji au uraia wa waumini utakuwa wapi?
Paulo asema wenyeji wa waumini utakuwa kule mbinguni.
Kristo atafanya nini kwenye miili ya waamini atakapokuja kutoka mbinguni?
Kristo atabadilisha miili dhaifu ya waamini kuwa kama mwili wake wa utukufu.
Philippians 4
Philippians 4:1-3
Paulo anataka wapendwa wake huko Fiilipi wafanye nini?
Paulo anawataka Wafilipi kusimama imara katika Bwana.
Paulo anatarajia kuona nini kinatokea kwa Eudia na Sentike?
Paulo anarajia kuona Eudia na Sentike waungane katika Bwana.
Philippians 4:4-7
Paulo anawambia Wafilipi wafanye jambo gani siku zote??
Paulo anawataka kufurahi katika Bwana kila siku zote.
Badala ya kujisumbua, Paulo anasema kufanya nini?
Paulo anasema badala ya kujisumbua, mwambie Mungu kwa maombi tunachohitaji, na kumshukuru.
Kama tukifanya hivi, nini kitalinda mioyo yetu na mawazo yetu?
Kama tukifanya hivyo, amani ya Mungu italinda moyo wetu na mawazo yetu
Philippians 4:8-9
Paulo anawaambia Wafilipi kufikiria mambo gani?
Paulo anasema kufikiri mambo ambayo ni ya heshima, haki, safi yenye upendo, yenye taarifa njema, yenye busara pamoja na yale yanayohitaji sifa.
Philippians 4:10-13
Ni mambo gani ambayo wafilipi walikuwa tayari kuyafanya upya?
Wafilipi walikuwa tayari kuhuisha mambo ya yakumjali Paulo.
Ni siri gani ambayo Paulo amejifunza kuishi katika hali tofauti tofauti?
Paulo amejifunza siri ya namna ya kuridhika katika mazingira yote yaani vingi na kuwa mhitaji.
Kwa nguvu ipi Paulo anaishi kwa kuridhika?
Paulo anaweza kuishi kwa kuridhika katika hali zote kupitia Kristo amtiaye nguvu
Philippians 4:14-17
Paulo anatafuta nini kwa Wafilipi katika kutoa kwa ajili ya mahitaji yake?
Paulo anatafuta matunda yaletayo faida kkwa wafilipi.
Philippians 4:18-20
Paulo anavionaje vitu ambavyo wafilipi wametoa kwa ajili yake?
Mungu amaependezwa na sadaka za Wafilipi ambazo zimetolewa kwa ajili ya Paulo.
Paulo anasema nini Mungu atafanya kwa ajili ya Wafilipi?
Paulo anasema kwamba Mungu atawapa Wafilipi mahitaji kulingana na utajiri wake wa utukufu katika KristoYesu.
Philippians 4:21-23
Je, Paulo anasema watu wa familia ipi wawasalimie Wafilipi?
Ni wale wa familia ya Kaisari wawasalimie Wafilipi.