Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Leviticus

Leviticus 1

Leviticus 1:3-4

Aina gani ya mnyama Yahweh alimwambia Musa awaambie watu walete kama sadaka kutoka kwenye kundi la wanyama?

Yahweh alimwambia Musa awaambie watu walete sadaka ya kuteketeza kutoka kwenye kundi la wanyama wasio na doa.

Nini ambacho Yahweh alimwambia mtu afanye sadaka kukubalike kwa niaba yake kuweza kujiombea?

Yahweh alimwambia mtu kuweka mkono kwenye kichwa cha sadaka ya kutekeza ikubalike kwa niaba yake.

Leviticus 1:5-6

Nini makuhani walipaswa wafanye na damu ya ng'ombe dume?

Makuhani walipaswa kuwakilisha damu na kuimwaga juu ya madhabahu mbele ya hekalu.

Leviticus 1:7-9

Makuhani walikuwa wakina nani?

Makuhani walikuwa wana wa Aruni.

Leviticus 1:10-13

Mnyama gani Yahweh alimwambia Musa kuwaambia watu kuleta kutoka kwenye mifugo kama sadaka ya kuteketeza?

Yahweh aliwaambia watu kuleta kutoka kwenye mifugo kondoo wa kiume na mbuzi asiye na doa

Upande gani wa madhabahu kondoo wa kiume au mbuzi aliuawa?

Kondoo au mbuzi aliuliwa kaskazini wa upande wa madhabahu.

Leviticus 1:14-17

Aina gani ya ndege Yahweh alisema waletwa kama sadaka ya kuteketezwa?

Yahweh alisema ua au ua mdogo wanaweza letwa kama sadaka ya kuteketezwa.

Leviticus 2

Leviticus 2:1-3

Aina gani ya sadaka ya nafaka iliweza kuletwa kama sadaka kwa Yahweh?

Unga mzuri uliweza kuletwa kama sadaka kwa Yahweh.

Nini kilipaswa kufanywa kuanda unga mzuri kabla ya kuutoa kwa Yahweh?

Mafuta na uvumba ulipaswa kuongezwa kabla ya kutolewa kwa Yahweh.

Kwa nani sadaka ya nafaka ilibakizwa?

Sadaka ya nafaka ilibakizwa baada ya kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya wana wa Aruni.

Leviticus 2:4-10

Kama sadaka ya nafaka iliokwa na kikangio cha chuma, ina paswa kuwaje?

Kama sadaka ya nafaka ili okwa na kikangio cha chuma, ili paswa kuwa ya unga mzuri bila hamira na mafuta.

Leviticus 2:11-16

Vitu gani havikupaswa kuwa katika sadaka ya nafaka?

hamira na asali havikupaswa kuwa katika sadaka ya nafaka.

Vitu gani mara zote zilipaswa kuwa katika sadaka ya nafaka?

Chumvi ilipaswa mara zote zilipaswa kuwa katika sadaka ya nafaka.

Leviticus 3

Leviticus 3:1-2

Sadaka gani ya ushirika ili tolewa kwenye mifugo?

Sadaka ya ushrika ilitolewa kati ya dume au jike kutoka kwenye mifugo.

Wapi sadaka ya ushirika iliweza kuuliwa?

Sadaka ya ushiriki ilipaswa kuuliwa katika mlango wa hema la kukutania.

Leviticus 3:3-5

Sehemu gani za sadaka ya ushirika ili paswa kuondolewa na kuwekwa madhabahuni?

Mafuta yanayo unganisha sehemu za ndani, mrija wa ini na mapafu.

Leviticus 3:6-8

Kulikuwa na tofauti ye yote kati sadaka ya ushirika iliyo tolewa kwenye kundi la mifugo?

Hapana, hapakuwa na tofauti.

Leviticus 3:9-14

Kitu gani cha tofauti lazima kiondolewa kutoka kwenye sadaka ya ushirika inayo toka kwenye mifugo?

Mkia wa mafuta wote ilikatwa kufunga mfupa wa nyuma uliondolewa.

Leviticus 3:15-17

Kwa nani peke mafuta yalipaswa?

Mafuta yalipaswa kwa Yahweh.

Nini Yahweh aliwaambia watu wasile popote watakapo ishi?

Yahweh aliwambia wasile mafuta au damu.

Leviticus 4

Leviticus 4:1-5

Aina gani ya chakula mlango wa nne wa Mambo ya Walawi ina ongelea?

Mlango wa nne wa Mambo ya Walawi ina ongelea sadaka ya dhambi.

Leviticus 4:6-10

Mara ngapi kuhani alinyunyiza damu kutoka kwenye sadaka ya dhambi mbele ya Yahweh, mbele ya pazia la patakatifu pa patakatifu?

Kuhani alinyunyiza damu kutoka kwenye sadaka ya dhambi mbele ya Yahweh mara saba, mbele ya pazia la patakatifu pa patakatifu.

Leviticus 4:11-12

Sehemu gani za ng'ombe dume zilibebwa nje kusafishwa mbele za Yahweh na kumwaga majivu?

Ngozi ya ng'ombe dume na nyama iliyo baki, na miguu, na kichwa na sehemu za ndani, mavi vilibebwa nje kwenye majivu.

Leviticus 4:13-19

Kama kusanyiko lote la Israeli likitenda dhambi pasipo kukusudia, nani alipaswa kuweka mikono kwenye sadaka ya dhambi?

Wazee waliweka mikono kwenye sadaka ya dhambi kama kusanyiko lote la Israeli likitenda dhambi pasipo kukusudia.

Leviticus 4:20-21

Nini kingetokea kusanyiko la Israeli kama wangefuata maelekezo ya sadaka ya dhambi?

Wangesamehewa

Leviticus 4:22-26

Nyama gani angetolewa kama kiongozi angetenda dhambi?

kama kiongozi angetenda dhambi, angetoa mbuzi dume asiye na doa.

Leviticus 4:27-31

Watu wa kawaida walipaswa kuleta nini kama dhabihu wangetenda dhambi?

Watu wa kawaida walipaswa kuleta mbuzi jike asiye na doa kuwa kama sadaka ya dhambi wangetenda dhambi.

Leviticus 4:32-35

Mwanaume angeweza kuleta kondoo jike asiye na doa kama dhabihu kwa ajili ya sadaka ya dhambi?

Ndio, mwanaume angeweza kuleta kondoo jike asiye na doa kama dhabihu kwa ajili ya sadaka ya dhambi

Leviticus 5

Leviticus 5:1-4

Dhambi gani ya hiari ambayo mtu aliwajibishwa?

Kama mtu alitenda kwa kuto shuhudia kuhusu kitu alicho ona au kusikia, alipo amriwa kushuhudia, ata wajibishwa.

Mtu akishika ambacho Mungu amesema ni najisi ataitwa nani?

Kama mtu akishika chochote Mungu alicho sema ni najisi, huyo mtu ataitwa mnajisi na mwenye hatia.

Leviticus 5:5-6

Vitu gani viwili mtu mwenye hatia ya dhambi afanye?

Mtu mwenye hatia ya dhambi afanye alipaswa akiri dhambi aliyo fanya na kuleta sadaka ya hatia kwa Yahweh.

Mnyama gani alipaswa kuletwa kwa Yahweh kama sadaka ya hatia kwa Yahweh?

Mbuzi jike au kondoo angeletwa kwa Yahweh kama sadaka ya hatia.

Leviticus 5:7-10

Kama mtu angekua na uwezo wa kununua kondoo, nini angeweza leta kwa Yahweh kama sadaka ya dhambi?

Kama mtu angekua na uwezo wa kununua kondoo, angeleta kwa Yahweh ua wawili au ua wa dogo wawili.

Leviticus 5:11-13

Kama asipo kuwa na uwezo wa ua wawili wa dogo au ua wawili, nini angeleta kwa ajili ya sadaka ya dhambi yake?

Kama asipo kuwa na uwezo wa ua wawili wa dogo au ua wawili, angeleta lita mbili za efa ya unga mzuri pasipo mafuta ye yote au uvumba.

Leviticus 5:14-19

Sadaka gani iletwe kama mtu alihasi amri na kufanya dhambi kwa kutolipa chochote kilicho stahili kwa Yahweh?

Hii sadaka lazima iwe kondo dume asiye na doa kutoka kwenye mifugo yenye dhamani ya shekeli za dhahabu.

Leviticus 6

Leviticus 6:1-4

Nini mtu alipaswa kufanya kama angetenda dhambi dhidi ya jirani yake?

Kama mtu angetenda dhambi dhidi ya jirani yake alipaswa kurejesha chochote alicho chukuwa au kitu kilicho potea alicho kipata.

Leviticus 6:5-7

Nini mtu aliye danganya alipaswa kufanya kuhusu jambo lolote?

Kama mtu kadanganya kuhuku jambo lolote, alipaswa kurejesha kwa utimilifu na asilimia tano zaidi.

Leviticus 6:8-9

Kwa muda gani sadaka ya kuteketeza ilibaki madhabahuni?

sadaka ya kuteketeza ilibaki madhabahuni usiku wote mpaka asubui.

Leviticus 6:10-11

Kuhani alivaa nini kuweza kuondoa majivu madhabahuni?

Kuhani alivaa joho na vazi lingine la ndani kuweza kutoa majivu madhabahuni.

Kuhani alifanya nini kabla ya kutoa majivu nje ya kambi?

Kuhani alitoa majoho yake na kuvaa nguo zingine kabla ya kutoa majivu nje ya kambi.

Leviticus 6:12-15

Nini kilipaswa kuendelea muda wote?

Moto madhabahuni.

Leviticus 6:16-18

Nini makuhani walipaswa kufanya na nafaka iliyo baki?

Makuhani waliweza kula nafaka ya sadaka iliyo baki pasipo hamira.

Leviticus 6:19-20

Nini wana wa Aruni walipaswa kufanya wanao walipo pakwa mafuta?

Walipaswa kuleta sadaka ya nafaka ya lita mbili ya efa ya unga mzuri, nusu asubui na nusu usiku.

Leviticus 6:21-23

Hii sadaka ya nafaka ilipaswa kuandaliwaje?

Ilipaswa kuandaliwa na mafuta kwenye chombo cha kuoka, kukandwa, kisha kuokwa vipande.

Leviticus 6:24-26

Kulingana na sheria ya sadaka ya dhamb, nini kuhani alipaswa kufanya kwenye sadaka?

Alipaswa kuila sadaka ya dhambi.

Leviticus 6:27-28

Nini kilipaswa kufanywa na mtungi wa udongo ambao vazi lenye damu lilichemshwa?

Lilipaswa kuvunjwa.

Leviticus 6:29-30

Sehemu gani yasadaka ya dhambi ilipaswa kutoliwa?

Hakuna sehemu ya sadaka ya dhambi iliyo paswa kuliwa ambapo damu ililetwa kwenye hema la kukutania kufanya upatanisho kwenye mahali pa takatifu.

Leviticus 7

Leviticus 7:7-8

Sadaka gani ilikuwa kama ya sadaka ya hatia?

Sadaka ya dhambi ilikuwa kama sadaka ya hatia.

Nini kuhani alichoweza bakiza kwenye sadaka ya mtu ya kuteketeza?

Kuhani aliweza hifadhi viungo vya ndani vya hiyo sadaka.

Leviticus 7:9-16

Sadaka gani ilikuwa ya kuhani?

Sadaka ya nafaka ilikuwa ya kuhani.

Leviticus 7:17-24

Nini ilipaswa kufanywa nyama ya dhabihu ambayo haikuliwa siku ya tatu?

nyama ya dhabihu ambayo haikuliwa siku ya tatu ilichomwa.

Leviticus 7:25-30

Nini alipaswa kufanyiwa ye yote ambaye alikula mafuta kutoka kwenye mnyama au damu kutoka kwa ndege au mnyama?

e yote ambaye alikula mafuta kutoka kwenye mnyama au damu kutoka kwa ndege au mnyama alikatiliwa kutoka kwa watu wake

Leviticus 7:31-38

Nini kuhani alipewa baada ya mafuta kuchomwa madhabahuni?

Baada ya mafuta kuchomwa madhabhuni, paja la kulia lilipewa kuhani.

Leviticus 8

Leviticus 8:1-5

Nini Yahweh alimwambia Musa afanye kwa Aruni na wanae?

Yahweh alimwambia Musa achukue Aruni na wanae, mavazi na mafuta ya kupaka, na ng'ombe dume, kondoo dume wawili, na beseni la mkate usiotiwa chachu kwenda kwenye mwingilio wa hema la kukutania.

Leviticus 8:6-7

Nguo gani Musa alimvisha Aruni?

Musa alimvisha Aruni na kilemba, mshipi , na joho.

Leviticus 8:8-9

Nini Musa aliweka kifuani?

Musa aliweka Urimu na Thumimu kifuami.

Taji takatifu lilikuwa ni nini?

Taji takatifu lilikuwa ni sahani ya dhahabu.

Leviticus 8:10-11

Nini Musa alipaka mafuta na mafuta ya upako?

Alipaka maskani na kila kitu.

Leviticus 8:12-13

Musa alimtengaje Aruni?

Musa alimtenga Aruni kwa kumpaka mafuta.

Leviticus 8:14-17

Nini ambacho Musa alifanya na damu ya ng'ombe iliyo letwa kwa sadaka ya dhambi?

Musa alichukuwa damu na kuweka kwenye mapembe ya madhabahu na kidole chake. Kisha akamwaga damu kwenye sakafu ya madhabahu.

Leviticus 8:18-21

Nini Musa alifanya na damu ya kondoo dume iliyo tumika kwa ajili ya sadaka ya kuteketeza?

Musa alimwaga damu yake dhidi ya kila upande wa madhabahu.

Leviticus 8:22-33

Nini Musa alifanya na damu ya kondoo dume wa pili, kondoo dume wa utakasaji?

Musa alichukuwa baadhi ya damu kutoka kwa kondoo dume wa utakasaji na kuweka katika ncha ya sikio la Aruni, kidole cha mkono wa kulia, na kidole gumba cha mguu wa kulia.

Leviticus 8:34-36

Makuhani walibaki kwa muda gani katika mwingilio wa hema la kukutani?

Walibaki kwa muda wa siku saba.

Leviticus 9

Leviticus 9:1-2

Siku gani Musa alimuita Aruni na wanae na wazee wa Israeli?

Musa aliwaita katika siku ya nane.

Wanyama gani wawili Musa alimwambia Musa na wanae kuleta kwa Yahweh?

Musa alimwambia Aruni alete ndama na kondoo asiye na doa.

Leviticus 9:3-5

Wanyama gani Musa alimuuliza Aruni awambie watu wa Israeli kuleta kwa Yahweh?

Musa alimwambia Aruni awambie watu kuleta mbuzi, ndama, kondoo, na kondoo jike kutoa kwa Yahweh.

Leviticus 9:6-21

Kwanini Yahweh aliwaamuru wafanye hivi?

Yahweh aliwamuru kufanya hivi ili kwamba utukufut wake uwatokee.

Leviticus 9:22-24

Baada ya Aruni kufanya sadaka kama Musa alivyo sema, nini Aruni alifanya kwa watu?

Baada ya Aruni kufanya sadaka, alinyanyua mikono yake na kubariki watu

Leviticus 10

Leviticus 10:1-2

Nani alitoa moto usio kubalika kwa Yahweh

Nadabu na Abihu, wana wa Aruni.

Nini kiliwatokea kwa hili tendo?

Moto ulishuka kutoka kwa Yahweh na kuwateketeza.

Leviticus 10:3-4

Nani aliitwa na Musa kubeba miili nje ya maskani?

Mishaeli na Elizafani, wana wa Uzieli, mjomba wa Aruni.

Leviticus 10:5-7

Nini Musa alisema kwa Aruni na wana wake?

Musa alisema wasitoke nje ya hema la kukutani au watakufa.

Leviticus 10:8-15

Nini Yahweh alisema kwa Aruni na wana wake kuhusu nini wasinywe?

Yahweh alisema kwa Aruni na wana wake wasinywe mvinyo au kinywaji kikali kabla ya kuingia nyumba ya kukutania.

Leviticus 10:16-20

Kwanini Musa alikuwa na hasira na Eleazeri na Ithamari, wana walio baki wa Aruni?

Musa alikuwa na hasira nao kwasababu waliwacha mbuzi wa sadaka ya dhambi kuteketea.

Leviticus 11

Leviticus 11:3-8

Vitu gani vinavyo ishi duniani Yahweh alimwambia Musa na Aruni watu wa Israeli wanaweza kula?

Yahweh alimwambia Musa na Aruni kuwaambia watu wa Israeli wanaweza kula chochote kinacho ishi chenye kwato na kula nyasi.

Leviticus 11:9-12

Wanyama gani wanao ishi kwenye maji wanaweza kuliwa na watu wa Israeli?

Wanyama wanao ishi kwenye maji mkia na magamba wanaweza kula na watu wa Israeli.

Leviticus 11:13-19

Aina gani ya kipanga, mwewe, na kunguru Yahweh alisema wachukiwe na wasiliwe?

Yahweh alisema kuwa kipanga, mwewe, na kunguru Yahweh alisema wachukiwe na wasiliwe.

Leviticus 11:20-28

Aina gani ya wadudu waliweza liwa na watu?

Wadudu wanao tembea juu miguu, wanao tumia kuruka chini, wanaweza liwa na watu.

Leviticus 11:29-33

Wanyama gani wanao tambaa chini wanao hesabiwa kama najisi?

Chche, panya, kila mjusi, na kinyonga walikuwa ni najisi.

Leviticus 11:34-40

Nini kinacho tokea kitu mnyama najisi anacho kigusa?

Nacho kina kuwa najisi.

Leviticus 11:41-42

Nini Yahweh anacho sema kuhusu vitu vinavyo tambaa chini?

Yahweh anasema kuwa ni vyakuchukiwa na najisi.

Leviticus 11:43-47

Kwanini Yahweh alisema kuwa watu wa Israeli wawe watakatifu?

Yahweh alisema watu wawe watakatifu sababu yeye ni mtakatifu.

Leviticus 12

Leviticus 12:1-3

Nini Yahweh alisema kwa Musa kuhusu wanawake waliyo zaa mtoto wa kiume?

Yahweh alisema kwa Musa kwamba wanawake waliyo zaa mtoto wa kiume watakuwa najisi kwa siku saba na siku ya nane mtoto atatahiriwa.

Leviticus 12:4-5

Nini mwanamke alipaswa kufanya alipo kuwa najisi?

Alipaswa kupitia utakaso kwa siku thelathini na tatu na asiingie maskani au kugusa chochote kitakatifu kipindi hichi.

Leviticus 12:6

Nini mwanamke alipaswa kufanya mwisho wa utakaso?

mwisho wa utakaso wake, mwanamke alipaswa kuleta kwa kuhani kondoo wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketeza na ua kwa ajili ya sadaka ya dhambi.

Leviticus 12:7-8

Kama mwanamke aliye zaa mtoto hana uwezo wa kununua kondoo?

Kama mwanamke ana uwezo wa kununua kondoo, alipaswa kuleta ua mdogo kwa ajili ya sadaka ya kuteketeza.

Leviticus 13

Leviticus 13:1-2

Nini Yahweh alisema mtu afanye kama ana uvimbe kwenye ngozi yake, mchubuko, au alama inayo mdhuru?

Yahweh alisema mtu ye yote mwenye ngozi iliyo dhurika aende kwa Aruni au kwa mmoja wa wana wake.

Leviticus 13:3-4

Nini kifanyike kama kuhani akiamua kuwa uvimbe, mchubuko au alama inayo dhuru?

Mtu huyo alazima atengwe kwa wiki moja kuchunguzwa tena

Leviticus 13:5-8

Kama uvimbe, mchubuko au alama inayo dhuru ikionekana kama haidhuru?

Kuhani atamtambua kama ni msafi baada ya kuosha nguo zake.

Leviticus 13:9-11

Ni dalili gani tatu ambazo uvimbe, mchubuko, zinaweza onyesha kama itatangazwa kudhuru?

Uvimbe weupe kwenye ngozi, nywele ziwe nyeupe, na ngozi ya ndani kuonyesha.

Kama kuhani akiamua kuwa huu ni ugonjwa sugu wa ngozi, nini kuhani afanye?

Lazima amtangaze mtu huyo najisi, lakini kuhani hamtengi.

Leviticus 13:12-14

Kama ugonjwa unafunika mwili mzima na ngozi ya ndani ina onekana, mtu huyo anatangazwa kuwa nani?

Mtu anatangazwaz kuwa najisi.

Leviticus 13:15-17

Jinsi gani mtu najisi anaweza kuwa si najisi tena?

Anaweza kuwa si najisi tena kama ngozi ya ndani ikiwa nyeupe na anatangazwa si najisi na kuhani.

Leviticus 13:18-28

Nini Kuhani afanye kuchunguza mtu aliye kuwa na jipu lakini sasa ana uvimbe una onekana chini ya ngozi ambapo jipu lilikuwa na nywele hapo imekuwa nyeupe?

Kuhani atamtangaza mtu huyo najisi.

Leviticus 13:29-39

Aina gani ya ugonjwa wa kuambukiza una sababisha mtu kuwa najisi kama utapatikana kwenye kichwa au ngozi?

Kama mwanamme au mwanamke ana ugonjwa wa washwa kwenye kichwa au kwenye taya unaweza kuambukiza na kumfanya mtu najisi.

Leviticus 13:40-41

Mwanamme aliye poteza nywele zake anatangazwa nani?

Mwanamme aliye poteza nywele zake anatangazwa si najisi.

Leviticus 13:42-44

Ni hali gani ya mwanamme mwenye kichwa cha upara itamsababisha kutangazwa najisi?

Kama mwanamme kichwa chake chenye upara kikiwa na vidonda vyekundu na vyeupe ambaye kuhani aliamua kuwa ni ugonjwa ambukizi, atatangazwa najisi.

Leviticus 13:45-55

Nini mtu najisi anapaswa kufanya kuonyesha wengine kujua yeye ni najisi?

Lazima avae nguo zilizo raruliwa, nywele zizochanwa, kufunika uso wake hadi kwenye pua, na kusema "najisi, najis," katika uwepo wa wengine. Pia anapaswa kuishi peke yake nje ya kambi.

Leviticus 13:56-59

Kuhani anapaswa kufanya nini na vazi la sufu au la ngozi au chochote cha ngozi ambacho limegunduliwa kuwa najisi?

Kuhani alipaswa kuchoma moto.

Leviticus 14

Leviticus 14:3-5

Wapi kuhani alipaswa mchunguza mtu mgonjwa siku ya utakaso wake?

Kuhani alipaswa mchunguza mgonjwa nje ya kambi kuona kama amepona.

Leviticus 14:6-7

Baada ya kuhani kunyunyuza damu, maji, mti wa mierezi na hisopu kwa mgonjwa mara saba, alifanya nini na ndege aliye baki?

Aliwaruhusu ndege waliyo baki kupaa kwenye mashamba.

Leviticus 14:8-9

Nini mtu aliye takaswa anapaswa kufanya baada ya kuhani kumtangaza si najisi?

Mtu aliye takaswa lazima afue nguo zake, kunyoa nywele zote, kuoga kwenye maji, kuishi nje ya hema lake siku saba.

Leviticus 14:10-20

Katika siiku ya nane, wanyama gani mtu anaye takaswa kuleta kwa kuhani kama anaweza kununua?

Katika siiku ya nane, wanyama gani mtu anaye takaswa kuleta kwa kuhani kama anaweza kununua, kondoo dume wawili wasio na doa, kondoo jike mmoja asiye na doa, na lita mbili za efa za unga uliyo changanywa na mafuta.

Leviticus 14:21-27

Kama mtu anaye takaswa ni maskini na hawezi nunua hizi dhabihu, nini alete kama mbadala?

Anaweza kuleta kondoo dume mmoja, lita moja ya efa wa unga mzuri uliyo changanywa na mafuta, na ua wawili.

Leviticus 14:28-42

Wapi kuhani anaweka mafuta yanayo tumika kwenye utakaso?

Kuhani anaweka mafuta kwenye sikio la kulia, kidole cha kulia, kidole gumba cha kulia, na mengine kichwani mwa mtu anaye takaswa.

Leviticus 14:43-44

Nini yaweza sababisha nyumba kutangazwa najisi na kuhani?

nyumba kutangazwa najisi na kuhani kama unyevu hauwezi zuilika.

Leviticus 14:45-51

Nini yaweza kutokea kwenye nyumba kama unyevu ukisamba na hauwezi kuzuiwa?

Nyumba yaweza kuharibiwa kama unyevu ukisambaa na hauwezi kuzui.

Leviticus 14:52-57

Nyumba yawezaje kutangazwa si najisi kama unyevu ukiweza zuiliwa?

Kuhani anaweza itangaza nyumba sio najisi kama akinyunyuzia damu ya ndege na maji, mti wa mierezi, hisopu, na sufu.

Leviticus 15

Leviticus 15:1-5

Nini Yahweh alisema kwa Musa na Aruni kuwa ni dalili ya mtu aliye na mmiminiko wa maji yaliyo na uambukizo?

Yahweh alisema kwa Musa na Aruni kuwa ni dalili ya mtu aliye na mmiminiko wa maji yaliyo na uambukizo ni najisi.

Leviticus 15:6-12

Nini kinamtokea mtu ambaye ana mgusa mtu aliye najisi kwasababu ya mmiminiko wa maji yanayo ambukizika?

Mtu anaye mshika mtu najisi ni atakuwa najisi pia na atahitaji kuoga, na kufua nguo zake, na atakuwa najisi kila jioni.

Leviticus 15:13-15

Kwenye aina gani ya maji mtu anaye takaswa kuoga?

Mtu anaye takaswa anapswa kwenye maji yanayo tembea.

Leviticus 15:16-18

Hali gani ya mtu anaye au kitu kinacho kutana na manii ya mwanaume?

Lazima waoshwe na maji na atakuwa najisi hadi jioni.

Leviticus 15:19-23

Kwa muda gani mwanamke atakuwa si msafi baada ya hedhi?

Atakuwa si msafi siku saba.

Leviticus 15:24-27

Kwa muda gani mwanaume atakuwa najisi akilala na mwanamke aliye kwenye hedhi na mtiririko wake ukamgusa?

Atakuwa najisi kwa siku saba.

Leviticus 15:28-33

Nini mwanamke kuleta kama dhabihu siku ya nane baada ya mtiririko wake kukata?

Anapaswa kuleta ua wawili.

Leviticus 16

Leviticus 16:1-2

Nini Yahweh alimwambia Musa kumuonya Aruni asifanye anapo kuja kwenye patakatifu ndani pazia?

Nini Yahweh alimwambia Musa kumuonya Aruni asifanye anapo kuja kwenye patakatifu ndani pazia muda wowote.

Leviticus 16:3-7

Nini Aruni anapswa kuleta anapo ingia patakatifu?

Aruni ataleta ng'ombe dume mdogo kwa ajili ya sadaka ya dhambi na kondoo dume kama sadaka ya kuteketezwa.

Leviticus 16:8-10

Kwanini Aruni alipiga kura kwa ajili ya mbuzi?

Aruni alipiga kura kwa ajili ya mbuzi kuchagua yupi amtoe kwa Yahweh na yupi awewa kisingizio.

Leviticus 16:11

Nani ambaye Aruni analeta kwake ng'ombe dume?

Aruni anapaswa kuleta ng'ombe dume kama sadaka ya dhambi kwake na familia yake.

Leviticus 16:12-16

Nini kinapaswa kufunika kifuniko cha upatanisho ambayo ni juu amri za agano ili kwamba Aruni asife?

Wingu la uvumba mzuri.

Leviticus 16:17-19

Nani mwingine lazima awe kwenye hema na Aruni anapotoa upatanisho ndani ya patakatifu?

Hakuna mtu mwingine anapaswa kuwa naye.

Leviticus 16:20-22

Nini Aruni anapaswa kufanya anapo eka mikono yake kwenye kichwa cha mbuzi wa kisingizio?

Aruni anapaswa kukiri juu ya mbuzi wa kisingizio maovu yote ya watu wa Israeli, mahasi yao, na dhambi zao.

Leviticus 16:23-28

Nini Aruni anapaswa kufanya na mavazi ya kikuhani?

Aruni lazima avue mavazi ya kikuhani na kuyaacha kwenye hema la kukutania.

Leviticus 16:29-34

Lini Yahweh alisema siku ya upatanisho uwe?

Siku ya kumi ya mwezi wa saba, upatanisho ufanye kila mwaka.

Leviticus 17

Leviticus 17:1-4

Kama mwanaume akimua ng'ombe, kondoo, pasipo kuleta kwenye malango ya hema la kusanyiko kutoa sadaka kwa Yahweh, ana hatia ya dhambi gani?

Ana hatia ya umwagaji damu na lazima akatwe miongoni mwa watu wake.

Leviticus 17:5-6

Nini lilikuwa kusudi la hii amri?

Kusudi ya hii amri ni kufanya watu kutoa dhabihu kwa Yahweh katika malango ya hema la kukutania badala ya uwanjani.

Leviticus 17:7-9

Hii amri itazuia nini?

Hii amri itazuia watu kuto toa dhabihu kwa sanamu za mbuzi.

Leviticus 17:10-11

Nini Yahweh anasema ufanya upatanisho?

Yahweh anasema damu ufanya upatanisho.

Leviticus 17:12-14

Nini Yahweh anasema ifanyike kwa mnyama ye yote au ndege anaye uliwa kuliwa na watu wa Israeli au mgeni ye yote anaye ishi miongoni mwao?

Yahweh anasema lazima wa mwage damu yake na kufunika damu na udongo.

Leviticus 17:15-16

Nini afanye mtu aliye kula mnyama aliye kufa au kuraruliwa vipande na wanyama?

Mtu aliye kula mnyama aliye kufa au kuraruliwa na wanyama lazima afue nguo zake na kuoga kwenye maji na kubaki najisi hadi jioni

Leviticus 18

Leviticus 18:1-5

Maeneo gani mawili Yahweh aliwaambia watu hawawezi fanya kama watu huko?

Misri na Kanani.

Leviticus 18:6-18

Kundi gani la watu Mungu alikataza kuto kuwa na mahusiano ya kimapenzi nalo?

Yahweh aliwaambia hawezi kuwa na mahusiano na ndugu wa karibu.

Leviticus 18:19-20

Kwanini mwanaume asifanye mapenzi na mwanamke aliye kwenye hedhi?

mwanaume asifanye mapenzi na mwanamke aliye kwenye hedhi kwasababu muda uo ni najisi.

Leviticus 18:21

Nini watu wasitoe dhabihu kwa Moleki?

Watu wasitoe watoto wao kwa Moleki kama dhabihu.

Leviticus 18:22-25

Mahusiano gani ya kimapenzi mstari wa 22 na 23 hairuhusu?

Mstari wa 22 na 23 hairuhusu mahusiano ya kimapenzi na wanyama au wanaume.

Leviticus 18:26-28

Nini kilitokea watu waliyo ishi hapo kabla ya watu wa Israeli?

Walinajisi nchi na nchi ikawatapika.

Leviticus 18:29-30

Nini kitatokea kwa mtu ye yote au mgeni anaye ishi muda mrefu miongoni mwao anaye fanya vitu chukizo hivi?

Mtu huyo ata katwa miongoni mwa watu.

Leviticus 19

Leviticus 19:1-8

Vitu gani viwili Yahweh aliwaambia watu wafanye lazima?

Yahweh aliwaambia watu waheshimu baba zao na mama na kushika Sabato.

Leviticus 19:9-14

Kwanini Yahweh aliwaambia watu waache kona za mashamba yao bila kuvunwa na kuacha badhi ya mizabibu kwenye miti yake au iliyo anguka chini?

Nafaka zisizo vunwa na mizabibu lazima iachwe kwa ajili ya maskini na wageni.

Leviticus 19:15-16

Kwa nani watu wasionyeshe upendeleo?

watu wasionyeshe upendeleo kwa mtu kwasababu yeye ni tajiri au maskini, lakini kumuhukumu kwa haki.

Leviticus 19:17-18

Nini watu wafanye badala ya kulipa kisasi au kuwa na chuki?

Watu wanapswa kupenda jirani zao kama wenyewe.

Leviticus 19:19-22

Nini watu wafanye wanapo panda mbegu shambani?

Hawapaswi kupanda aina moja ya mbegu kwenye shamba moja.

Leviticus 19:23-31

Kwa muda gani mpandaji wa mti wa tunda asubiri kabla ya kula tunda hilo?

Lazima asubiri mwaka wa tano kabla ya kula tunda la mti.

Leviticus 19:32

Mtu gani Yahweh aliwaambia watu kuinuka kabla na kumuheshimu?

Aliwaambia watu wenye mvi na wanaume wazee.

Leviticus 19:33-37

Kwanini Yahweh alisema watu wa Israeli wapende wageni kama wanavyo jipenda?

Yahweh alisema watu wa Israeli wapende wageni kama wanavyo jipenda kwasababu watu wa Israeli walikuwa wageni nchi ya Misri.

Leviticus 20

Leviticus 20:1-2

Nini kitatokea miongoni mwa watu wanao toa watoto wao kwa Moleki?

Mtu atakaye mtoa mtoto wake kwa Moleki atauawa.

Leviticus 20:3-5

Nini Yahweh atamfanya huyo mtu kama watu wasipo muua?

Yahweh anasema atamkata kwa watu wake.

Leviticus 20:6-12

Nani Yahweh aliwaambia watu wasimgeukie?

Yahweh aliwaambia wasiongee na wao wanao ongea na wafu au roho.

Leviticus 20:13-14

Nini ilikuwa matokea ya mwanaume aliye kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine?

Alifanya kitu chukizo na wote waliuawa.

Leviticus 20:15-23

Kama mwanaume alikufanya mapenzi na mnyama, nini atafanyiwa?

Mwanaume, mwanamke, na mnyama wote watauliwa.

Leviticus 20:24-27

Namna gani Mungu alieleza nchi aliyo wapa watu wa Israeli?

Yahweh aliita "nchi ya maziwa na asali"

Leviticus 21

Leviticus 21:1-3

Kwa kifo cha nani kuhani aliruhusiwa kuwa najisi?

Kwa ndugu wa karibu sana.

Leviticus 21:4-6

Masharti gani yaliwekwa kwa makuhani kuhusu nywele zao na ndevu?

Makuhani hawaku ruhusiwa kunyoa vichwa vyao au pembeni mwa ndevu zao.

Leviticus 21:7-9

Nini kitamtokea binti wa kuhani aliye jinajisi kwa kuwa kahaba?

Binti wa kuhani aliye jinajisi kwa kuwa kahaba alichomwa.

Leviticus 21:10-12

Kuhani mkuu anapaswa kuepuka nini ata kama ni baba au mama?

Kuhani mkuu hapaswi kwenda karibu kwenye maiti, ata kama ni baba au mama.

Leviticus 21:13-17

Aina gani ya mwanamke kuhani hapaswi kuoa?

Kuhani hapaswi kuoa mjane, au mwanamke aliye achwa, au mwanamke kahaba.

Leviticus 21:18-24

Aina gani ya mwanaume Yahweh hakutaka kumfuata ataoe sadaka?

Yahweh hakutaka mwanaume mwenye mwili wa upungufu kumfuata.

Leviticus 22

Leviticus 22:1-3

Nini Yahweh anasema kitatukana jina lake takatifu?

Yahweh anasema mtu ye yote ambaye ni najisi kwasababu ye yote na anashika vitu vitakatifu atatukana jina lake takatifu.

Leviticus 22:4-6

Nini kuhani anapaswa kufanya anapo shika chochote kinajisi?

Lazima aoge na maji na kubaki najisi hadi jioni.

Leviticus 22:7-9

Nini kinaweza kutokea kuhani asiye fuata maelekezo ya Yahweh?

Watakuwa na hatia ya dhambi na wanaweza kufa kwa kumtukana Yahweh.

Leviticus 22:10-11

Watu gani wanao weza kula chochote kitakatifu?

Kuhani na familia yake ndio wanaweza kula chochote kitakatifu, na watumwa wao.

Leviticus 22:12-13

Binti wa kuhani aliye olewa na mtu asiye kuhani anaweza kula vitu vitakatifu?

Hapana, labda awe ameachika au kuwa mjane na amerudi kuishi nyumbani mwa baba yake.

Leviticus 22:14-16

Nini mtu anaye kula chakula kitakatifu pasipo kujua anapaswa kufanya?

Lazima amlipe kuhani na kuongeza theluthi tano.

Leviticus 22:17-19

Aina gani ya mnyama anaweza kubalika kama dhabihu?

Lazima awe mnyama asiyo na doa kutoka kwenye ng'ombe, kondoo, au mbuzi.

Leviticus 22:20-25

Kigezo gani muhimu cha mnyama ye yote anaye tolewa dhabihu kwa Yahweh?

Mnyama ye yote anaye tolewa kwa Yahweh lazima asiwe na doa.

Leviticus 22:26-27

Miaka mingapi ndama, kondoo, au mbuzi awe ili atolewe adhabihu kwa Yahweh?

Ndama, kondoo, au mbuzi anapaswa kuwa na sio chini ya siku nane kutolewa dhabihu kwa Yahweh.

Leviticus 22:28-33

Sadaka ya shukrani yapaswa liwa lini?

Siku hiyo hiyo iliyo tolewa dhabihu.

Leviticus 23

Leviticus 23:3

Nini Yahweh anasema kuhusu kazi na sabato?

Watu wanaweza fanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba, Sabato, ni siku ya kupumzika.

Leviticus 23:4-8

Sherehe ipi isherekewe mwezi wa kwanza wa siku ya kumi na nne?

Pasaka ya Yahweh isherekewe mwezi wa kwanza wa siku ya kumi na nne.

Leviticus 23:9-25

Nini watu walete kwa kuhani baada ya mavuno ya kwanza kwenye nchi Yahweh ana kwenda kuwapa?

Watu lazima walete kwa kuhani fondo la matunda baada ya mavuno ya kwanza.

Leviticus 23:26-29

Siku gani Yahweh aliweka kwa ajili ya Siku ya upatanisho?

Yahweh aliweka siku ya kumi ya mwezi wa saba.

Leviticus 23:30-32

Nini watu wafanye siku ya upatanisho?

Watu lazima wasifanye kazi Siku ya Upatanisho.

Leviticus 23:33-39

Sherehe ipi Yahweh alisema ifanyike siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba?

Yahweh alisema Sherehe ya Mahifadhi ya Yahweh ifanyike siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba

Leviticus 23:40-41

Nini watu watumie kusherehekea Sherehe ya Mahifadhi ya Yahweh?

Watu lazima wa tumie tunda bora kutoka mitini, matawi ya mitende.

Leviticus 23:42-44

Wapi watu wa Israeli waliishi kipindi cha Sherehe ya Mahifadhi ya Yahweh?

Watu wa Israeli walipaswa kuishi katika mahifadhi madogo kwa siku saba.

Leviticus 24

Leviticus 24:3-4

Nini Aruni afanye na mafuta safi watu wanayo mletea?

Aruni lazima na taa inawaka mbele za amri za agano katika hema la kusanyiko kutoka jioni hadi asubui kila siku.

Leviticus 24:5-6

Kuhani anapaswa kuweka nini katika mistari miwili ya sita kila Sabato?

kuhani anapaswa kuweka mikate kumi na mbili katika mistari miwili ya sita kila Sabato.

Leviticus 24:7-12

Nani ana ruhusiwa kula sadaka ya mikate hiyo kumi na mbili?

Aruni na wanae.

Leviticus 24:13-16

Watu wa Israelii walipaswa kumfanya nini mtu aliye mkufuru Yahweh?

Yahweh aliwaambia wamtoe nje ya kambi, wamueke mikono yao, na kumpiga mawe.

Leviticus 24:17-18

Nini lazima kimtokea mwanaume anaye muua mwanaume mwingine?

Lazima auawe.

Leviticus 24:19-23

Nini Yahweh alisema kifanyike kwa mtu ye yote anaye sababisha mauti au jeraha kwa mwingine?

Yahweh alisema kwa watu kwamba alicho mfanyia mtu naye afanyiwe; jicho kwa jicho, jino kwa jino.

Leviticus 25

Leviticus 25:3-7

Nini Yahweh alisema kifanyike baada ya mashamba na yale ya mizabibu kuoteshwa, kubaliliwa, na kuvunwa kwa miaka sita?

Mwaka wa saba utakuwa Sabato ya mapumziko.

Leviticus 25:8-9

Nini kifanyike mwaka wa arobaini na tisa, siku ya kumi ya mwezi wa saba?

Tarumbeta kubwa lazima lipigwe kila pande kipindi cha mwaka wa arobaini na tisa, siku ya kumi ya mwezi wa saba.

Leviticus 25:10

Mwaka wa hamsini utaitwaje?

Mwaka wa hamsini utaitwa Yubile.

Leviticus 25:11-14

Nini kiliwe kipindi cha Yubile?

Chakula kinacho ota chenyewe ndicho kiliwe kipindi cha Yubile.

Leviticus 25:15-19

Nini watu watathimini wanapo nunua au kuuza ardhi?

Miaka mingapi ipo hadi yubile ingine. Kiasi cha miaka iliyo salia ndio thamani zaidi ya ardhi kuongezeka.

Leviticus 25:20-22

Jinisi gani Yahweh atakavyo jali watu wake kipindi cha mwaka wa saba, mwaka wa Sabato, mazao yasipo limwa?

Mavuno ya mwaka wa sita yatazidi mavuno ya kawaida mara tatu, hivyo kutakuwa na chakula mwaka wa saba.

Leviticus 25:23-28

Nini Yahweh alisema kuhusu umiliki daima wa ardhi?

Yahweh alisema kusiuzwe ardhi daima kwa mmiliki mpya kwasababu ardhi ilikuwa yake.

Leviticus 25:29-34

Mali gani isirudishwe kipindi cha Yubile?

Nyumba ilyo nunuliwa katika mji uliyo zungushiwa ukuta utakuwa mali ya kudumu ya mwanaume aliye nunua baada ya mwaka.

Leviticus 25:35-38

Watu wanapaswa kumtendeaje mwanachi mwenzie anaye kuwa maskini na hawezi tena kujikimu?

Watu wanapaswa kumsaidia, kuto mtoza faida au kujaribu kufaidi kupitia yeye kwa vyo vyote.

Leviticus 25:39-55

Watu wanapaswa kumtendeaje mwanachi mwenzie aliye jiuza kama mtumwa?

Watu wanapaswa kumtendeaje mwanachi mwenzie aliye jiuza kama mtumwa kama mtumishi mwajiriwa, na hajafanywa kufanya kazi kama mtumwa.

Leviticus 26

Leviticus 26:1-2

Yahweh anawaambia watu wasifanye nini?

Yahweh anawaambia watu wasifanye sanamu.

Leviticus 26:3-4

Nini watu wanapaswa kufanya kuhakikisha Yahweh anatuma mvua na mavuno?

Yahweh anasema wanapaswa kutembea na amri zake na sheria, na kuzitii.

Leviticus 26:5-10

Nini Yahweh atafanya kuhakikisha watu wako salama?

Yahweh ataondoa wanyama wakali na kusababisha upanga haupiti kwenye nchi.

Leviticus 26:11-15

Kama watu wakifanya kama Yahweh anavyo waamuru kufanya, nini ana amuru kuwa fanyia?

Kama watu wanafanya kama Yahweh anavyo waambia kufanya, ana ahidi kutembea nao, kuwa Mungu wao, na watakuwa watu wake.

Leviticus 26:16-17

Aina gani ya magonjwa na homa Yahweh alisema atatuma Israeli kama wasipo tii amri zake?

Yahweh alisema atatuma magonjwa kuharibu macho yao na kudhohofisha maisha yao.

Leviticus 26:18-20

Yahweh ansema atafanya nini watu wasipo tii amri zake na sheria?

Yahweh anasema kama watu wasipo tii amri zake, wataadhibiwa mara saba kwa dhambi zao.

Leviticus 26:21-39

Yahweh alisema kama Israeli haitamsikiliza, atatuma wanyama wakali dhidi yao. Yahweh alisema ao wanyama watafanya nini?

Yahweh alisema ao wanyama wataiba watoto wao, haribu mifugo na kuwafanya wachache kiidadi.

Leviticus 26:40-43

kama watu wasipo mtii Yahweh, wamekosa matumaini yote?

Yahweh anasema kama watu wakikiri dhambi zao, dhambi za baba zao, uhasi dhidi ya Yahweh, na kwa unyenyekevu kukubali adhubu ya dhambi zao, atakumbuka agano alilo fanya na Yakobo, Isaka, na Ibrahimu.

Leviticus 26:44-46

Licha ya dhambi zao, nini Yahweh ana ahidi kufanya?

Yahweh ana ahidi kuto wakataa au kuwa chukia kabisa.

Leviticus 27

Leviticus 27:1-2

Nini dhumuni ya kiwango cha thamani?

Mtu aliye tolewa kwa Yahweh, ana weza fanya kiapo maalumu kinacho mtaka atumia kiwago cha thamani.

Leviticus 27:3-6

Nini kiwango cha thamani cha mwanaume kati ya miaka ishirini na sitini?

mwanaume kati ya miaka ishirini na sitini ana kiwango cha thamani cha shekeli hamsini za fedha.

Leviticus 27:7-10

Kama mtu anye apa kiapo hawezi kutimza kiwango cha thamani cha mtu anaye mtoa?

Kama mtu anye apa kiapo hawezi kutimza kiwango cha thamani, ata wakilishwa kwa kuhani na kuhani ata thamini huyo mtu kwa kiasi mtu anaye mfanya kiapo anaweza kulipa.

Leviticus 27:11-13

Vitu gani vingine kuhani athamini vinavyo weza kuletwa kwa Yahweh?

Kuhani anaweza thamini mnyama kutolewa kwa dhabihu, nyumba ya mtu, au badhi ya ardhi yake.

Leviticus 27:14-15

Vitu gani vingine kuhani anaweza thamini vinavyo weza kuletwa kwa Yahweh?

Kuhani anaweza thamini mnyama kutolewa kwa dhabihu, nyumba ya mtu, au badhi ya ardhi yake.

Leviticus 27:16-21

Vitu gani vingine kuhani anaweza thamini vinavyo weza kuletwa kwa Yahweh?

Kuhani anaweza thamini mnyama kutolewa kwa dhabihu, nyumba ya mtu, au badhi ya ardhi yake.

Leviticus 27:22-25

Nini mwanaume afanye na shamba alilo litoa kwa Yahweh katika mwaka wa yubile?

Wakati wanaume ametoa shamba kwa Yahweh na mwaka wa yubile ukafika, kuhani ata jua kiasi cha thamani ya shamba hadi mwaka wa yubile na mwanaume alipe thamani hiyo siku kama zawadi takatifu kwa Yahweh.

Leviticus 27:26-27

Wanyama gani ni wa Yahweh tu?

Wazaliwa wa kwanza wa wanyama wote ni wa Yahweh.

Leviticus 27:28-29

Sehemu gani ya vitu vilivyo tolewa kwa Yahweh vinaweza uzwa au kurejeshwa?

Hakuna chochote kilicho tolewa kwa Yahweh cha weza uzwa au kurejeshwa.

Leviticus 27:30-34

Mtu akirejesha sehemu ye yote ya zaka yake, nini aongeze?

Lazima ongeze theluthi tano kwa thamani yake.