1 Timothy
1 Timothy 1
1 Timothy 1:1-2
Namna gani Paulo alifanywa kuwa mtume wa Kristo Yesu?
Paulo alifanywa kuwa mtume kutokana na amri ya Mungu.
Kulikuwa na mahusiano gani kati ya Paulo na Timotheo?
Timotheo alikuwa mtoto wa Paulo katika imani
1 Timothy 1:3-4
Timotheo alikuwa kabaki wapi?
Timotheo alikuwa amebaki katika Efeso.
Ni kitu gani Timotheo alipaswa kuwa agiza baadhi ya watu kukifanya?
Alikuwa awaamuru wasifundishe mafundisho tofauti.
1 Timothy 1:5-8
Nini ambacho Paulo alisema kilikuwa lengo la amri na mafundisho yake?
Lengo lake lilikuwa upendo utokao kwenye moyo safi, katika dhamiri njema, na kutoka imani nyoofu.
1 Timothy 1:9-11
Ni kwa ajili ya nani sheria imetengenezwa?
Sheria ni kwa ajili ya wavunja sheria, waasi, watu wasiomcha Mungu, na wenye dhambi.
Mifano ipi minne ya dhambi ambazo watu kama hao hutenda?
Wanaua, wana maadili mabaya ya kingono, watekaji, na wanadanganya.
1 Timothy 1:12-14
Ni dhambi gani ambayo Paulo alitenda hapo awali?
Paulo alikuwa mtesaji wa kanisa, mtu mwenye vurugu, na alimtukana Mungu
Nini kilimpata Paulo, kilichomfanya Paulo awe mtume wa Kristo?
Neema ya Mungu ilimjaa Paulo
1 Timothy 1:15-17
Nani ambaye Kristo Yesu alikuja duniani kumwokoa?
Yesu Kristo alikuja duniani kuokoa wenye dhambi.
Kwa nini Paulo anasema kwamba ni mfano wa rehema ya Mungu?
Paulo anasema yeye ni mfano kwa sababu alikuwa ni mtenda dhambi mbaya zaidi, lakini bado alipokea rehema ya Mungu kwanza.
1 Timothy 1:18-20
Mambo gani yalisemwa kuhusu Timotheo ambayo Paulo anayakubali?
Paulo anakubaliana na unabii uliofanywa kuhusu Timotheo, kutokana na vita vizuri vilivyofanywa na Timotheo kwa imani na dhamiri njema.
1 Timothy 2
1 Timothy 2:1-4
kwa ajili ya nani Paulo anasisitiza maombi yafanyike?
Paulo anasihi maombi yafanyike kwa ajili ya watu wote, kwa ajili ya wafalme na wote walio katika mamlaka.
Mungu anataka nini kwa ajili ya watu wote?
Mungu anatamani watu wote waokolewe na kupata maarifa ya kweli
1 Timothy 2:5-7
Nini nafasi ya Yesu Kristo kati ya Mungu na Mtu?
Yesu Kristo ni mjumbe kati ya Mungu na Mtu.
Ni kitu gani ambacho Yesu Kristo alikifanya kwa ajili ya wote?
Yesu Kristo aliyatoa maisha yake kuwa fidia ya wote
Mtume Paulo anawafundisha akina nani?
Paulo ni mwalimu wa watu wa Mataifa.
1 Timothy 2:8-10
Paulo anataka wanaume wafanye nini?
Paulo anataka wanaume kuomba na kuinua mikono iliyo mitakatifu.
1 Timothy 2:11-12
Ni kitu ambacho Paulo anawakataza wanawake wasifanye?
Paulo anawazuia wanawake kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya wanaume.
1 Timothy 2:13-15
Paulo anataka wanawake waendelee katika nini?
Paulo anataka wanawake waendelee katika imani na upendo na utakaso katika akili zote.
1 Timothy 3
1 Timothy 3:1-3
Kazi ya mwangalizi ni ya namna gani?
Kazi ya mwangalizi ni kazi njema
Mwangalizi anapaswa kuwa na uwezo gani?
Mwangalizi anapaswa kuwa na uwezo wa kufundisha
Mahusiano ya mwanganilizi juu ya fedha na pombe unapaswa kuwaje?
Mwangalizi hapaswi kuwa mnywaji wa pombe, na asipende fedha.
1 Timothy 3:4-5
Ni namna gani watoto wa mwangalizi waweza kumchukulia?
Watoto wa mwangalizi lazima wamtii na kumheshimu
Kuna umuhimu gani kwa mwangalizi kuweza kusimamia nyumba yake vizuri?
Ni muhimu kwa sababu kama hawezi kusimamia nyumba yake vizuri, ni wazi kwamba hawezi kulisimamia kanisa vizuri.
1 Timothy 3:6-7
Kuna hatari gani ikiwa mwangalizi ni mwamini mpya?
Hatari ni kwamba atajivuna na kuanguka katika hukumu.
Sifa ya mwangalizi inapaswa iweje kati yake na wale walio nje ya kanisa?
Mwangalizi anapaswa kuwa na sifa njema kati yake na wale walio nje ya kanisa.
1 Timothy 3:8-10
Ni jambo gani wahudumu wanapaswa kufanyiwa kabla ya kuanza utumishi wao?
Wahudumu wanapaswa kuidhinishwa kwanza kabla hawajaanza kutumika.
1 Timothy 3:11-13
Wanamke mcha Mungu ana sifa zipi?
Wanawake wacha Mungu ni wakamilifu, wasio wasingiziaji, wenye kiasi, na waaminifu katika kila kitu.
1 Timothy 3:14-15
Nyumba ya Mungu ni nini?
Nyumba ya Mungu ni Kanisa.
1 Timothy 3:16
Baada ya Yesu kutokea katika mwili, alidhibitishwa na Roho, na akaonekana na malaika, je alifanya nini?
Yesu alitangazwa kati ya mataifa, akaaminiwa na ulimwengu, na akuchukuliwa juu katika utukufu.
1 Timothy 4
1 Timothy 4:1-2
Kwa mujibu wa Roho Mtakatifu, baadhi ya watu watafanya nini nyakati zijazo?
Baadhi ya watu wataacha imani na kuwa makini kusikiliza roho zidanganyazo.
1 Timothy 4:3-5
Ni uongo gani watu hawa watafundisha?
Watakataza ndoa na baadhi ya vyakula.
Ni jinsi gani kitu chochote tunachokula kimeidhinishwa na kukubaliwa kwa ajili ya matumizi yetu?
Kila kitu tunachokula kimeidhinishwa na kuruhusiwa kupitia Neno la Mungu na maombi.
1 Timothy 4:6-10
Paulo anamhimiza Timotheo kujifunza nini?
Paulo anamhimiza Timotheo kujifunza katika utaua.
Ni kwanini kujifunza katika utaua ni muhimu kuliko kujifunza katika mwili?
Ni muhimu kwa sababu kunatunza ahadi kwa maisha ya sasa na yale yajayo.
1 Timothy 4:11-13
Paulo anamhimiza Timotheo kufanya nini kutokana na uzuri wa mafundisho yote aliyoyapokea kutoka kwa Paulo?
Paulo anamhimiza Timotheo kusema na kufundisha mambo haya kwa wengine.
Ni kwa njia zipi Timotheo anapaswa kuwa mfano kwa wengine?
Timotheo anapaswa kuwa mfano katika kunena, tabia, upendo, imani, na usafi.
1 Timothy 4:14-16
Ni kwa namna gani Timotheo alizipokea karama za kiroho alizokuwanazo?
Karama zilitolewa kwa Timotheo kwa unabii pamoja na kuwekewa mikono ya wazee.
Ikiwa Timotheo atandelea kwa uaminifu katika maisha yake na mafundisho, nani ataokolewa?
Timotheo atajiokoa mwenyewe na wale wanaomsikiliza.
1 Timothy 5
1 Timothy 5:1-2
Paulo alimwambia nini Timotheo kuhusu kumjali mzee kanisani?
Paulo alimwambia Timotheo amjali kama vile baba yake.
1 Timothy 5:3-6
Ni mambo gani ambayo watoto na wajukuu wa mjane wanapaswa kumfanyia mjane?
Watoto na wajukuu wanapaswa kuwalipa wazazi wao na kuwatunza.
1 Timothy 5:7-8
Mtu ambaye hawezi kuwatunza watu wa nyumbani kwake anafanya jambo gani?
Anaikataa imani na ni mbaya zaidi kuliko asiyeamini.
1 Timothy 5:9-10
Mjane anapswa kutambulika kwa mambo gani?
Mjane anapaswa kutambulika katika matendo mema.
1 Timothy 5:11-13
Hatari gani ipo pale mjane kijana anapoamua kubakia mjane kwa maisha yake yote?
Kuna hatari yakwamba baadaye anaweza akataka kuolewa, akavunja makubaliano yake ya mwanzo.
1 Timothy 5:14-16
Paulo anataka wanawake vijana wafanye nini?
Paulo anataka wanawake vijana waolewe, wazae watoto, na wasimamie nyumba zao.
1 Timothy 5:17-18
Kitu gani kifanyike kwa wazee wanaoongoza vyema?
Wazee wanaoongoza vyema, wanatakiwa watambulike na waheshimiwe zaidi.
1 Timothy 5:19-20
Kitu gani kinapaswa kiwepo kabla ya mashitaka hayajapokelewa dhidi ya wazee?
Ni lazima kuwe na mashahidi wawili au watatu kabla ya mashitaka hayajapokelewa dhidi ya mzee.
1 Timothy 5:21-22
Paulo alimuamuru Timotheo awe makini kutunza sheria hizi kwa njia gani?
Paulo alimuamuru Timotheo awe makini kutunza sheria hizi bila ubaguzi.
1 Timothy 5:23-25
Kwa baadhi ya watu, dhambi hazijulikani mpaka lini?
dhambi zao hazijulikani mpaka siku ya hukumu
1 Timothy 6
1 Timothy 6:1-2
Je, Paulo alisema watumwa wawachukulieje mabwana zao?
Paul alisema kuwa watumwa lazima wawachukulie mabwana zao kama wanaostahili heshima.
1 Timothy 6:3-5
Ni aina gani ya mtu anayekataa maneno yenye afya na mafundisho ya Kimungu?
mtu ambaye anakataa maneno yenye afya na mafundisho ya utauwa ana majivuno na hajui kitu.
1 Timothy 6:6-8
Je, ni kitu gani ambacho Paulo anasema ni faida kubwa?
Paulo anasema kwamba utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
Kwa nini tunapaswa kuridhika kwa chakula na mavazi?
Kwa sababu hatukuja na kitu chochote duniani, na hatuwezi kuchukua chochote.
1 Timothy 6:9-10
Watu wanaotaka utajiri huanguka katika nini?
Wale wanaotaka kuwa tajiri huanguka katika majaribu na mtego.
Nini kimetajwa kuwa chanzo cha uovu wote?
Kupenda fedha ni chanzo cha uovu wote.
Nini kimetokea kwa baadhi ya watu ambao walipenda fedha?
Baadhi ya watu waliopenda fedha wameiacha imani.
1 Timothy 6:11-14
Ni vita gani ambayo Paulo anamwambia Timotheo lazima apigane?
Paulo anasema kwamba Timotheo lazima apigane vita njema ya imani.
1 Timothy 6:15-16
Ni mahali gani Mbarikiwa na nguvu pekee huishi?
Mbarikiwa anaishi katika mwanga usiofikika mahali ambapo hakuna mwanadamu awezaye kutazama.
1 Timothy 6:17-19
Kwa nini matajiri wanapaswa kuweka tumaini katika Mungu na si katika mali isiyojulikana?
Tajiri lazima awe na matumaini katika Mungu kwa kuwa ndipo unatoka utajiri wote wa kweli.
Wale walio na utajiri utokano na kazi nzuri hufanya nini kwa ajili yao?
wanajiwekea msingi mzuri, na wanapata maisha sahihi.
1 Timothy 6:20-21
Hatimaye, Paulo anamwambia Timotheo afanye nini na vitu alivyopewa?
Paulo anamwambia timotheo atunze kile alichopewa.