Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Isaiah

Isaiah 1

Isaiah 1:1

Isaya ni nani?

Isaya alikuwa mwana wa Amozi.

Maono ya Isaya yalihusu nini?

Maono ya Isaya yalikuwa juu ya Yuda na Yerusalemu.

Isaya alipata maono yake wakati gani?

Isaya alikuwa na maono katika siku za Uzia, Yothamu, Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda.

Isaiah 1:2-3

Kwa nini mbingu zinapaswa kusikia na dunia kusikiliza?

Mbingu zinapaswa kusikia na dunia inapaswa kusikiliza kwa sababu Yahwe ametamka.

Yahwe amefanya nini?

Amewarutubisha na kuwakuza watoto

Watoto wa Yahwe wamefanya nini?

Wameasi dhidi ya Yahwe

Isaiah 1:4-6

Taifa linafafanuliwaje?

Linafafanuliwa kama wenye dhambi, watu waliojaa udhalimu, watoto wa watenda maovu na wana ambao hutenda ubaya.

Taifa limefanya nini?

Wamemtelekeza Yahwe, kujitenganisha na kumdharau Mtakatifu wa Israeli.

Isaiah 1:7-8

Hali ya nchi na miji yao ilikuaje?

Nchi yao ilikuwa na ukiwa na miji yao ilichomwa

Isaiah 1:9

Ni nini ambacho Yahwe aliwaachia?

Amewaachia waliosalia wachache sana.

Isaiah 1:10-13

Nini hakifurahi katika Yahwe?

Hafurahi katika damu ya ng'ombe dume, kondoo na mbuzi dume.

Isaiah 1:14-15

Yahwe anachukia nini?

Anachukia miezi yao mipya na sherehe zilizoteuliwa

Kwa nini Yahwe hatasikia maombi yao?

Hatasikia kwa sababu mikono yao imejaa damu.

Isaiah 1:16-18

Yahwe anawaambia kufanya nini?

Yahwe anawaambia kuacha kuwa waovu; kujifunza kufanya mema; kutafuta haki, kuwasaidia waliokandamizwa, kutoa haki kwa wasio na baba na kutetea wajane.

Isaiah 1:19-20

Wanapaswa kufanya nini ili kula mema ya nchi?

Wanatakiwa kujitoa na kutii.

Nini kitatokea kama watakataa na kuasi?

Upanga utawameza

Isaiah 1:21-23

Mji mwaminifu ulikuaje kabla haujawa kahaba?

Mji mwaminifu ulikuwa umejaa hukumu na haki.

Mji mwaminifu ulikuwa umejaa kitu gani?

Mji mwaminifu ukawa umejaa wauaji.

Isaiah 1:24-28

Yahwe atafanya nini?

Atalipa kisasi dhidi ya wapinzani wake.

Isaiah 1:29-30

Nini kitawafanya kuwa na aibu?

Watakuwa na aibu kwa mwaloni mtakatifu waliotamani na kuaibika kwa bustani ambazo walichagua

Isaiah 1:31

Nini kitatokea kwa mwanamume mwenye nguvu na kazi yake?

Wote wataungua pamoja

Isaiah 2

Isaiah 2:1-2

Neno ambalo Isaya aliliona lilikuwa linahusu nini?

Neno ambalo Isaya aliliona lilihusu Yuda na Yerusalemu.

Nini kitatokea katika siku za usoni?

Katika siku za usoni mlima wa nyumba ya Yahwe itaimarishwa.

Nani atakuja katika nyumba ya Yahwe?

Mataifa yote yatatiririka kwake.

Isaiah 2:3

Kwa nini watu wengi wataenda katika mlima wa Yahwe?

Wataenda juu kufundishwa baadhi ya njia za Yahwe.

Isaiah 2:4

Yahwe atafanya nini kwa ajili ya mataifa na watu wengi?

Yahwe atawahukumu na kutoa maamuzi.

Mataifa hayatafanya nini?

Hawatainua juu upanga dhidi ya wao wenyewe au kufanya mazoezi ya vita.

Isaiah 2:5-8

Nyumba ya Yakobo inaambiwa kufanya nini?

Wanaambiwa kutembea katika nuru ya Yahwe.

Yahwe amefanya nini?

Amewatelekeza watu wake, nyumba ya Yakobo.

Kwa nini Yahwe amewatelekeza nyumba ya Yakobo?

Amewatelekeza kwa sababu wamejaa na tamaduni kutoka mashariki na ni wasoma ishara kama Wafilisti, na wanatikisa mikono na wana wa wageni.

Isaiah 2:9-16

Kwa nini nyumba ya Yakobo inapaswa kuingia katika sehemu za mawe na kujificha ndani ya vumbi?

Wanatakiwa kujificha kwa sababu ya hofu ya Yahwe na utukufu wa enzi yake.

Nini kitatokea kwa wenye mtazamo wa kujiinua na wanamume wenye kiburi?

Wataletwa chini na kushushwa chini.

Nani atainuliwa katika siku hiyo?

Yahwe pekee atainuliwa katika siku hiyo.

Isaiah 2:17-19

Nini kitatokea kwa sanamu?

Zitapita mbali kabisa.

Watu wataenda wapi katika siku hiyo?

Wataingia katika mapango ya mawe na mashimo ya ardhi.

Isaiah 2:20-22

Nyumba ya Yakobo imeambiwa kuacha kumwamini nani?

Wanaambiwa kuacha kuamini katika mwanadamu.

Isaiah 3

Isaiah 3:1-3

Yahwe anakaribia kuondoa kitu gani kutoka Yerusalemu na Yuda?

Yahwe anakaribia kuondoa mhimili wao na fimbo.

Isaiah 3:4-7

Nani atawaongoza Yuda na Yerusalemu?

Vijana watawaongoza na watoto watatawala juu yao.

Nani atakandamiza watu?

Watu watakandamizwa wao kwa wao na kila mtu kwa jirani yake.

Isaiah 3:8-9

Kwa nini Yerusalemu imeharibiwa na Yuda kuanguka?

Imeangamizwa na kuanguka kwa sababu maneno yao na matendo yapo dhidi ya Yahwe.

Nini kinashuhudia dhidi ya Yuda na Yerusalemu?

Mtazamo katika nyuso zao hushuhudia dhidi yao.

Isaiah 3:10-12

Nini kitatokea kwa wenye haki?

Itakuwa salama kwa wenye haki.

Nini kitatokea kwa waovu?

Itakuwa vibaya kwa ajili ya waovu.

Viongozi wao wanawaongoza wapi?

Viongozi wao huwapotosha na kuchanganya upande wa njia yao.

Isaiah 3:13-15

Yahwe atafanya nini kwa viongozi na maafisa wa watu wake?

Yahwe atatangaza hukumu juu yao.

Isaiah 3:16-23

Bwana, Yahwe atafanya nini kwa binti za Sayuni?

Yahwe ataunda vigaga vya maradhi juu ya vichwa vyao na kuwafanya kuwa na upaa.

Isaiah 3:24-26

Nini kitatokea kwa wanamume?

Wanamume wataanguka kwa upanga

Isaiah 4

Isaiah 4:1-2

Kwa nini wanawake saba watakamata mwanamume mmoja?

Watataka kuchukua jina lake na kuondoa aibu yao.

Isaiah 4:3-4

Waliobaki ambao waliokoka Sayuni na Yerusalemu wataitwa kina nani?

Waliookoka ambao walibaki Sayuni na Yerusalemu wataitwa watakatifu.

Bwana atafanya nini kwa roho ya hukumu na kwa roho ya moto unaochoma?

Bwana ataosha mbali uchafu wa binti wa Sayuni na kusafisha madoa ya damu kutoka miongoni mwa Yerusalemu.

Isaiah 4:5-6

Yahwe ataumba nini juu ya eneo lote la Mlima Sayuni na juu ya sehemu yake ya kusanyiko?

Ataumba wingu na moshi mchana na moto unaong'aa usiku; kivuli kinachoning'inia juu ya utukufu wote

Isaiah 5

Isaiah 5:1-2

Mwimbaji anataka kuimba kwa nani?

Mwimbaji anataka kuimba kwa mpenzi wake

Wimbo wa mwimbaji unahusu nini?

Wimbo unahusu shamba la mizabibu la mpenzi wake.

Alifanya nini kwa shamba la mzabibu?

Alichimbua, kuondoa mawe, kupanda na mizabibu mizuri, na kujenga mnara na kishinikizo cha zabibu ndani yake.

Shamba la mzabibu lilitoa nini?

Shamba la mizabibu lilitoa mizabibu ya pori.

Isaiah 5:3-4

Wakazi wa Yerusalemu na wanamume wa Yuda wanapaswa kuhukumu nini?

Wanatakiwa kuhukumu kati ya mpenzi na shamba lake la mizabibu.

Isaiah 5:5-6

Mpenzi atafanya nini kwa shamba lake la mizabibu?

Ataondoa uzio, kugeuza shamba la mizabibu kuwa malisho, na kuvunja chini kuta zake ili liwe takataka na hakuna mvua itaanguka juu yake.

Isaiah 5:7

Nani ni shamba la mizabibu la Yahwe wa majeshi?

Shamba la mizabibu la Yahwe ni nyumba ya Israeli.

Yahwe alingojea nini?

Yahwe alingojea hukumu na haki.

Yahwe alipata nini badala ya hukumu na haki?

Yahwe alipata mauaji na vilio vya msaada.

Isaiah 5:8-12

Nini kitatokea kwa nyumba nyingi?

Nyumba nyingi zitakuwa tupu na bila wakazi.

Isaiah 5:13-14

Kwa nini watu wa Israeli na Yuda walichukuliwa mateka?

Walichukuliwa mateka kwa sababu walikosa uelewa.

Isaiah 5:15-23

Nini humwinua Yahwe wa Majeshi?

hukumu ya Yahwe huinua

Mungu Mtakatifu anatambulika kama nani?

Mungu anajulikana kwa mambo yake ya haki.

Isaiah 5:24-25

Kwa nini mzizi wa Israeli utaoza, na kuchanua kwao kupulizwa mbali kama vumbi?

Mzizi wa Israeli utaoza, na kuchanua kwao kutapulizwa kama vumbi kwa sababu walikataa sheria ya Yahwe na kukataa neno la Mtakatifu wa Israeli.

Isaiah 5:26-30

Yahwe ataliita taifa la mbali kuja kwa namna gani?

Atawaita kwa kuinua bendera ya ishara na kupiga mluzi kwa ajili yao.

Ni kwa jinsi gani taifa hilo la mbali litakuja?

Hilo taifa la mbali litakuja kwa haraka na kwa wepesi.

Isaiah 6

Isaiah 6:1-3

Ni wakati gani Isaya alimwona Bwana akikaa juu ya kiti cha enzi cha juu kilichoinuliwa?

Isaya alimwona Bwana katika mwaka ambao mfalme Uzia alikufa.

Nani alikuwa juu ya Bwana?

Maserafi walikuwa juu ya Bwana.

Isaiah 6:4-5

Nini kilitokea pale ambapo serafi walipoitana wao kwa wao?

Maserafi walipojiita wao kwa wao, milango na vizingiti vilitetemeka na nyumba ilijaa na moshi.

Isaya alisema nini alipoona vitu hivi vyote?

Isaya alisema ya kuwa ameangamia kwa sababu alikuwa na midomo michafu na aliishi miongoni mwa watu wenye midomo michafu na kwa sababu alimwona Mfalme Yahwe.

Isaiah 6:6-7

Serafi alisema nini alipogusa midomo ya Isaya kwa mkaa kutoka katika madhabahu?

Alisema, "Tazama, hii imegusa mdomo wako; hatia yako imeondolewa mbali, na dhambi yako imelipiwa"

Isaiah 6:8-10

Isaya alisikia Bwana akimuuliza nini?

Bwana alisema, "Nitamtuma nani; nani ataenda kwa ajili yetu?"

Isaya aliitikiaje kwa kile Bwana alichouliza?

Isaya alisema, "Nipo hapa; nitume".

Bwana alimwambia nini Isaya kuwaambia watu?

Bwana alimwambia Isaya kuwaambia watu kusikiliza lakini sio kuelewa; kuona, lakini sio kutambua.

Isaiah 6:11-13

Isaya alitakiwa kusema ujumbe wa Bwana kwa muda gani?

Isaya alitakiwa kuwaambia watu ujumbe wa Bwana mpaka miji iwe katika uharibifu bila wakazi na nyumba zikiwa bila watu na nchi kuanguka katika ukiwa wa kuachwa na mpaka Yahwe atume watu mbali na utulivu wa nchi ukiwa mkuu.

Isaiah 7

Isaiah 7:1-2

Ahazi alikuwa nani?

Ahazi alikuwa mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda

Wakati wa siku za Ahazi, wafalme gani walikwenda juu Yerusalemu kule Yuda kupigana vita dhidi yake?

Resini mfalme wa Ashuru na Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli alikwenda juu vitani dhidi ya Yerusalemu.

Ahazi na watu wake walichukuliaje waliposikia ya kwamba Ashuru aliungana na Efraimu?

Mioyo ya Ahazi na watu ilitetemeka waliposikia hii.

Isaiah 7:3-4

Yahwe alimwambia Isaya kufanya kazi gani?

Yahwe alimwambia Isaya kutoka nje na mwanawe na kukutana na Ahazi.

Yahwe alisema Ahazi hakutakiwa kumuogop nani?

Yahwe alisema Ahazi hatakiwi kuogopa au kutishwa na Resini na Peka.

Isaiah 7:5-6

Aramu, Efraimu na mwana wa Remalia walipanga kufanya nini?

Wanamume hawa walipanga maovu dhidi ya Ahazi na Yuda. Walipanga kushambulia na kuogofya Yuda, na kumuandaa mwana wa Tabeeli kuwa mfalme.

Isaiah 7:7-9

Yahwe alimwambia nini Ahazi kuhusu Efraimu?

Yahwe alimwambia Ahazi, "ndani ya miaka sitini na tano, Efraimu atavunjwavunjwa na hatakuwa na watu.

Yahwe anamwambia nini Ahazi kitatokea kama imani yake haipo imara?

Ahazi hatakuwa salama hadi imani yake iwe imara.

Isaiah 7:10-12

Mwitikio wa Ahazi ulikuaje Bwana alipomwambia kuomba ishara kutoka kwa Yahwe?

Ahazi alisema, "Sitamuuliza, wala sitamjaribu Yahwe".

Isaiah 7:13-15

Isaya alisema Ahabu alikuwa akifanya nini?

Isaya alisema hakuwa akijaribu tu uvumilivu wa watu lakini pia alikuwa akijaribu uvumilivu wa Mungu.

Isaiah 7:16-19

Isaya alimwambia Ahazi ya kwamba Yahwe atamletea nani dhidi yake?

Isaya alimwambia Ahazi ya kwamba Yahwe angemleta mfalme wa Ashuru dhidi yake na watu wake.

Isaiah 7:20-22

Mfalme wa Ashuru angefanya nini?

Mfalme wa Ashuru angenyoa kichwa cha Ahazi, miguu na ndevu.

Isaiah 7:23-25

Nini kitatokea kwa nchi?

Nchi itajazwa na mibigili na miiba na itakuwa sehemu ambapo kondoo na mifugo itakula.

Isaiah 8

Isaiah 8:1-2

Yahwe alimwambia Isaya kufanya nini?

Alimwambia Isaya kuchukua kibao kikubwa na kuandika juu yake, "Maher-shalal-hash-bazi"

Mashahidi waaminifu wa Yahwe wanatakiwa kuwa kina nani?

Mashahidi wa Yahwe walitakiwa kuwa Uria kuhani na Zekaria mwana wa Yeberekia.

Isaiah 8:3-10

Kwa nini Yahwe alimwambia Isaya kumuita mwana wake "Maher-shalal-hash-bazi"

Alitakwia kuitwa "Maher-shalal-hash-bazi" kwa sababu kabla hajajua namna ya kulia "Baba yangu" na "Mama yangu", mfalme wa Ashuru angekuja na kubeba utajiri wa Dameski na uporaji wa Samaria.

Isaiah 8:11-13

Ni kwa njia gani bayana za watu Isaya alionywa kutotembea?

Isaya alionywa kutoita njama chochote ambacho watu waliita njama na kutoogopa kile walichoogopa au kuwa na hofu ya hivyo vitu.

Isaya aliambiwa kumtendea nani kama mtakatifu na kumuogopa?

Isaya aliambiwa kuogopa na kuwa na hofu ya Yahwe wa majeshi na kumtendea kama mtakatifu.

Isaiah 8:14-15

Yahwe alikuja kuwa nani kwa zote nyumba ya Israeli na kwa wakazi wa Yerusalemu?

Alikwenda kuwa jiwe ambalo hufanya watu kuanguka na mwamba ambao hufanya watu kujikwaa kwa Israeli, na mtego kwa wakazi wa Yerusalemu.

Isaiah 8:16-18

Ni ushuhuda upi wa Isaya uliopatiwa kwa wanafunzi wake?

Ushuhuda wa Isaya ulikuwa kwamba angemsubiri Yahwe na kwamba Isaya na wanae walipewa na Yahwe kwa ajili ya ishara na miujiza Israeli

Isaiah 8:19-20

Kulingana na Isaya watu wa Israeli walikwenda kuwaambia nini wafuasi wa Isaya?

Walikwenda kuwaambia wanafunzi wa Isaya kutaka shauri na wasoma mizimu na wafanya mazingaombwe.

Isaya anasema ni nani watu wanapaswa kutaka shauri?

Watu wanapaswa kutaka shauri kwa Mungu wao.

Isaya anaamuru wanafunzi kuwa makini kwa kitu gani?

Wanaamuriwa kuwa makini kwa sheria na ushahidi.

Isaiah 8:21-22

Watu wa Israeli watafanya nini watakapoteseka sana na kuwa na njaa na kuwa na hasira?

Watageuza nyuso zao juu na kulaani mfalme wao na Mungu wao.

Nini kitatokea kwa watu wa Israeli?

Wataendeshwa katika nchi ya giza.

Isaiah 9

Isaiah 9:1-5

Nini kitatokea kwa yule aliyekuwa katika majonzi?

Huzuni yake itaondolewa.

Mungu aliaibisha nchi zipi katika nyakati za awali?

Mungu aliaibisha nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali.

Mungu alifanya nini kwa Zabuloni na Naftali katika muda wa baadaye?

Atawafanya kuwa na utukufu.

Ni kwa nani mwanga umeng'aa?

Mwanga umeng'aa kwa wale ambao wameishi katika nchi ya kivuli cha kifo.

Isaiah 9:6-7

Yule ambaye atabeba utawala juu ya bega lake anaitwa nani?

Jina lake ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Uwezo, Baba wa Milele, na Mfalme wa Amani.

Atatawala vikoje

Atatawala kwa hukumu na kwa haki.

Atatawala kwa muda gani?

Atatawala kutoka kipindi hiki kuendelea na milele.

Isaiah 9:8-10

Israeli alisema nini kwa kiburi na kwa moyo wa majivuno?

Israeli anasema, "Matofali yameanguka, lakini tutajenga tena kwa mawe ya kuchonga; mikuyu imekatwa chini, lakini tutaweka mikangazi katika nafasi yao.

Isaiah 9:11-12

Yahwe alimwinua nani dhidi ya Israeli?

Yahwe alimwinua Resini, Waashuru na Wafilisti dhidi ya Israeli.

Baada ya haya yote, hasira ya Yahwe ilitulia?

Hapana, hasira ya Yahwe haikushuka. Mkono wake bado ulinyoshwa kupiga Israeli.

Isaiah 9:13-15

Je! watu walimgeukia Yahwe?

Watu hawakumgeukia Yahwe au kumtafuta.

Nani alikuwa "kichwa" na "mkia" ambao Yahwe alitaka kuwakata ndani ya siku moja?

Kiongozi na mtu muadilifu walikuwa kichwa na nabii ambaye alifundisha uongo alikuwa mkia.

Isaiah 9:16-17

Kwa nini Bwana hakuwa na huruma kwa wasio na baba na wajane wao?

Hakuwa na huruma juu yao kwa sababu kila mtu alikuwa sio mcha Mungu na muovu na kila mdomo ulizungumza mambo ya kipumbavu.

Baada ya haya yote, hasira ya Yahwe ilitulia?

Hapana, hasira ya Yahwe haikushuka. Mkono wake bado ulinyoshwa kupiga Israeli.

Isaiah 9:18-19

Nini kilikuwa matokeo ya kumwagikia kwa hasira ya Yahwe?

Yahwe alisababisha nchi kuchomwa na watu kuwa kama mafuta kwa ajili ya moto.

Isaiah 9:20-21

Nini kilitokea kwa Manase, Efraimu na Yuda?

Manase na Efraimu walijimeza na wote walimshambulia Yuda.

Baada ya haya yote, hasira ya Yahwe ilitulia?

Hapana, hasira ya Yahwe haikushuka. Mkono wake bado ulinyoshwa kupiga Israeli.

Isaiah 10

Isaiah 10:5-6

Rungu ya hasira ya Yahwe alikuwa nani na kiboko ambacho Yahwe alitwalia ghadhabu yake?

Ashuru alikuwa rungu ya hasira ya Yahwe na kiboko ambacho alinyoshea ghadhabu yake.

Yahwe aliamuru Ashuru kufanya nini?

Aliamuru Ashuru kuchukua mateka, kuchukua mawindo na kukanyaga Israeli kama matope katika mitaa.

Isaiah 10:7-11

Ashuru alikusudia kufanya nini?

Ilikuwa katika moyo wa Ashuru kuangamiza na kuondosha mataifa mengi.

Isaiah 10:12-14

Bwana alisema angefanya nini atakapomaliza kazi yake katika Mlima Sayuni na Yerusalemu?

Bwana alisema angeadhibu maneno ya moyo wenye majivuni ya mfalme wa Ashuru na muonekano wake wa kiburi.

Kwa nini mfalme wa Ashuru alifikiri amefanikiwa?

Mfalme wa Ashuru alifikiri alikuwa amefanikiwa kwa sababu ya nguvu yake, hekima na uelewa.

Isaiah 10:15-16

Bwana Mungu alikwenda kufanya nini miongoni mwa hodari wa juu wa Ashuru?

Bwana Mungu alikwenda kutuma udhaifu kati yao.

Isaiah 10:17-19

Yahwe alisema angeangamiza nini kule Ashuru?

Yahwe alisema angeangamiza utukufu wa msitu wake na wa nchi yake inayozaa.

Isaiah 10:20-23

Waliosalia wa Israeli wataegemea nini baada ya wao kutoroka?

Aliyesalia ambaye aliyetoroka asingetegemea tena yule ambaye aliwapiga, lakini hakika kumtegemea Yahwe.

Isaiah 10:24-25

Kwa nini Bwana Mungu aliwaambia watu ambao waliishi Sayuni kutoogopa Ashuru?

Aliwaambia kutoogopa Ashuru kwa sababu katika muda mfupi sana hasira ya Bwana dhidi yao wa Sayuni itakwisha na hasira ya Bwana itakuwa ikielekea uharibifu wa Ashuru.

Isaiah 10:26-34

Nini kilitakiwa kutokea katika siku ambapo Yahwe angenyosha mjeledi wake dhidi ya Ashuru na katika siku Yahwe angeinua kiboko chake juu ya bahari kuiinua?

Katika siku hiyo mzigo utainuliwa kutoka katika bega lao na nira kutoka katika shingo yao.

Isaiah 11

Isaiah 11:1-2

Nini kilikuwa kinakuja katika mzizi wa Yese?

Mmea na tawi litakuja kutoka katika mzizi wa Yese.

Nini kilikuwa kinakuja kutua juu yake?

Roho wa Yahwe alitakiwa kutua juu yake.

Roho wa Yahwe atampatia nini?

Roho wa Yahwe atampatia hekima na uelewa, ushauri na uwezo, maarifa na hofu ya Yahwe.

Isaiah 11:3-7

Atatumia kiwango gani kuhukumu maskini na wanyenyekevu?

Hatahukumu kwa jinsi macho yake yanavyoona au masikio yake yanavyosikia. Atahukumu kwa haki na kuamua kwa haki.

Atafanya nini kwa waovu?

Atawachinja kwa pumzi ya midomo yake.

Isaiah 11:8-9

Wanyama watafanyaje tofauti?

Hawatawadhuru wala kuwaangamiza katika mlima wake mtakatifu.

Kwa nini wanyama hawatawadhuru au kuangamiza?

Wanyama hawadhuru wala kuangamiza kwa sababu dunia itakuwa imejaa maarifa ya Yahwe.

Isaiah 11:10-11

Katika siku hiyo kwa nini Bwana atanyosha mkono wake?

Atanyosha mkono wake kuwarudisha waliosalia wa watu wake ambao wanabaki Ashru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi, na visiwa vya bahari.

Isaiah 11:12-13

Nini kitatokea kwa wale ambao wana uhasama na Yuda?

Wale ambao wana uhasama na Yuda wataondoshwa.

Nini kitatokea kati ya Efraimu na Yuda?

Efraimu hatamwonea wivu Yuda, na Yuda hatakuw na uadui tena na Efraimu.

Isaiah 11:14-16

Efraimu na Yuda watafanya nini pamoja?

Watashuka chini kwa vilima vya Wafilisti magharibi na kupora watu wa mashariki. Pia watashambulia Edomu na Moabu.

Yahwe atafanya nini kwa ghuba ya bahari ya Misri na Mto Frati?

Yahwe atagawanya ghuba ya bahari ya Misri na atagawanya mto Frati katika vijito saba.

Kwa nini Yahwe atagawanya ghuba ya bahari ya Misri na kugawa Mto Frati

Atazigawanya ili kwamba ziweze kuvukwa kwa ndara.

Isaiah 12

Isaiah 12:1-4

Katika siku hiyo, kwa nini watatoa shukrani kwa Yahwe?

Watatoa shukrani kwa sababu ingawa Yahwe alikuwa na hasira na wo, aligeuza ghadhabu yao kutoka kwao na kuwafariji.

Katika siku hiyo watu watasema Yahwe ni nani kwao?

Watu watasema Yahwe ni nguvu yao, wimbo wo, na wokovu wao.

Isaiah 12:5-6

Kwa nini watu wataambiwa kuimba kwa Yahwe?

Wataambiwa kuimba kwa Yahwe kwa maana amefanya vitu vya utukufu na kwamba ijulikane kote duniani.

Isaiah 13

Isaiah 13:1-3

Isaya alipokea ujumbe gani kutoka kwa Yahwe?

Alipokea tamko kuhusu Babeli.

Yahwe amewaita wanamume wake hodari kufanya nini?

Amewaita kutekeleza hasira yake.

Isaiah 13:4-5

Jeshi la Yahwe linatoka wapi?

Wanatoka kutoka nchi ya mbali, kutoka mbali kupita upeo wa macho.

Vyombo vya hukumu vya Yahwe vitakwenda kufanya ninii?

Vitaenda kuangamiza nchi nzima.

Isaiah 13:6-8

Watu watafanya nini pale nchi itakapoangamizwa?

Mikono yo itaning'inia kwa kulegea, na mioyo yao itayeyuka; wataogopa; maumivu makali na majonzi yatawakamata. Watakuwa na muonekano wa mshangao na nyuso zao zitawaka moto.

Isaiah 13:9-10

Kitu gani kingine kitatokea wakati wa siku ya Yahwe?

Nchi itafanywa ukiwa na wenye dhambi wataangamzwa kutoka kwake. Nyota, vilimia, jua na mwezi havitatoa mwanga wao; vitatiwa giza.

Isaiah 13:11-16

Je! patakuwa na wanamume watakaobaki?

Hapana! Yahwe atafanya wanamume kuwa adimu kuliko dhahabu safi.

Isaiah 13:17-18

Yahwe anakwenda kumwamsha nani kushambulia Wababeli?

Yahwe anakwenda kuwaamsha Wamedi kuwashambulia Wababeli.

Isaiah 13:19-20

Nini kitatokea kwa Babeli?

Mungu atawapindua kama Sodoma na Gomora na hawatakaliwa au kuishi kwa kizazi mpaka kizazi.

Isaiah 13:21-22

Nini kitalala Babeli?

Wanyama pori wa jangwani watalala pale.

Mambo haya yatafanyika lini kwa Babeli?

Muda wa Babeli umekaribia na siku zake hazitakawia.

Isaiah 14

Isaiah 14:1-2

Yahwe atafanya nini kwa Israeli?

Yahwe atawachagua tena Israeli na kuwarejesha katika nchi yao wenyewe.

Je! mtu mwingine yeyote atakwenda na Waisraeli katika nchi yao?

Wageni watajiunga nao na kujishikiza katika nyumba ya Yakobo.

Nani atawaleta Waisraeli katika nchi yao?

Mataifa yatawaleta katika sehemu yao wenyewe.

Nyumba ya Israeli itafanya nni kwa mataifa ambayo walichukua Israeli mateka.

Nyumba ya Israeli itawachukua kama watumishi wa kiume na kike. Watachukua mateka wale ambao wamewakamata na watatawala juu ya wakandamizaji wao.

Isaiah 14:3-4

Nini kitatokea katika siku ambayo Yahwe huwapa Israeli pumziko kutoka mateso yao, maumivu makali, na kazi ngumu?

Wataimba wimbo wakimsuta mfalme wa Babeli.

Nini kimetokea kwa mkandamizaji?

Mkandamizaji amefikia mwisho.

Isaiah 14:5-9

Mfalme wa Babeli alifanya nini?

Aliwapiga watu kwa ghadhabu na mapigo yasiyokoma. Alitawala mataifa kwa hasira, kwa shambulio ambalo halikuzuiliwa.

Isaiah 14:10-11

Wafalme aliyekufa wa dunia atasema nini kwa mfalme wa Babeli?

Wafalme watasema, "Umekuwa dhaifu kama sisi ..." na "Majivuno yako yamewekwa chini kuzimu ..."

Isaiah 14:12-17

Nini kimetokea kwa mwana wa asubuhi?

Ameanguka kutoka mbnguni n kukatwa chini mpaka ardhini.

Mwana wa asubuhi alisema nini moyoni mwake?

Alisema angeinua kiti chake cha enzi juu ya nyota za Mungu na kujifanya kama Aliye Juu Zaidi.

Isaiah 14:18-20

Kwa nini mfalme wa Babeli hatajiunga na wafalme wengine wa mataifa katika mazishi?

Hatajiunga nao kwa sababu aliangamiza nchi yake na kuwaua watu wake.

Isaiah 14:21-23

Nini ni tamko la Yahwe wa Majeshi dhidi ya Babeli?

Anatamka, "Nitaiinuka ju dhidi yao" na zaidi, "Nitakata kutoka Babeli jina, uzao, na watoto".

Isaiah 14:24-27

Yahwe wa Majeshi ameapa nini kuhusu Ashuru katika nchi ya Yahwe?

Alisema angevunja Ashuru katika nchi yake na juu ya milima yake kumkanyaga chini ya mguu.

Isaiah 14:28-30

Nini lilikuwa tamko dhidi ya Ufilisti?

Ilitamkwa ya kwamba Ufilisti hawatakiwi kufurahi, kwa maana Yahwe alikwenda kumuua mzizi wa Ufilisti kwa njaa ambayo itawaua Wafilisti wote waliopona.

Isaiah 14:31-32

Nani alianzisha Sayuni?

Yahwe alianzisha Sayuni.

Watu walioteswa wa Yahwe watakuta nini Sayuni?

Watu wa Yahwe walioteswa watapata kimbilio Sayuni.

Isaiah 15

Isaiah 15:1-4

Tamko linahusu nini?

Tamko ni juu ya Moabu.

Nini kitatokea kwa Ari na Kiri wa Moabu?

Kila mmoja ataangamizwa na atawekwa kama takataka katika usiku mmoja.

Isaiah 15:5-7

Wakimbizi wa Moabu watakwenda wapi?

Watakimbilia Soari mpaka Eglathi Shelishiya.

Isaiah 15:8-9

Nini kilitokea kwa maji ya Dimoni na nini kitatokea kwa Dimoni?

Maji wa Dimoni mejaa damu; lakini Yahwe ataleta zaidi juu ya Dimoni.

Nini kitatokea kwa wale ambao wanatoroka kutoka Moabu na pia wale ambao wanabaki katika nchi?

Simba atawashambulia wote ambao hutoroka kutoka Moabu na wale ambao watabaki Moabu.

Isaiah 16

Isaiah 16:1-2

Kondoo dume wanatakiwa kutumwa kwa nani?

Kondoo dume wanatakiwa kutumwa kwa mtawala wa nchi katika mlima wa binti wa Sayuni.

Wanawake wa Moabu katika vivuko vya Mto Arnoni wanalinganishwa na nini?

Wao ni kama ndege wanaotangatanga au kiota kilichotawanywa.

Isaiah 16:3-4

Yuda anatakiwa kufanya nini na wakimbizi wa Moabu?

Wanatakiwa kuwaficha na sio kuwasaliti wakimbizi na kuruhusu wakimbizi kuishi miongoni mwao; kuwa sehemu ya kujificha kutoka kwa mwangamizi.

Isaiah 16:5-10

Yule kutoka katika hema la Daudi ambaye hukaa juu ya kiti cha enzi atafanya nini?

Atahukumu huku akitafuta haki na kutenda haki.

Isaiah 16:11-12

Moabu atatimiza nini atakapoingia hekalu lake kuomba?

Moabu hatatimiza kitu kwa maombi yake.

Isaiah 16:13-14

Nini kilikwenda kutokea kwa utukufu wa Moabu?

Yahwe alisema utukufu wa Moabu utapotea ndani ya miaka mitatu.

Wangapi kutoka Moabu watabaki?

Waliosalia wa Moabu watakuwa wachache sana na kutokuwa na umuhimu.

Isaiah 17

Isaiah 17:1-3

Nini kitatokea kwa mji wa Dameski?

hautakuwa mji tena, lakini utakuwa rundo la uharibifu.

Nini kitatoweka kutoka Efraimu?

Miji iliyoimarishwa itatoweka kutoka Efraimu.

Isaiah 17:4-5

Nini kitatokea kwa utukufu wa Yakobo katika siku hiyo?

Utukufu wa Yakobo utakuwa mwembamba na unene wa nyama yake utakuwa umedhoofika katika siku hiyo.

Isaiah 17:6-7

Wanamume watatazama nini katika siku hiyo?

Wanamume watatazama kuelekea Muumba wao na macho yao yataangalia kwa Mtakatifu wa Israeli.

Isaiah 17:8-11

Katika siku hiyo miji yao imara itakuwa kama nini?

Katika siku hiyo miji yao imara itakuwa kama miteremko ya mbao iliyotelekezwa juu ya vilele vya vilima.

Isaiah 17:12-14

Nini kitatokea mataifa yakiunguruma kama kumwagika kwa maji mengi?

Mungu atakaripia mataifa na watatoroka mbali na kufukuzwa.

Fungu la wale ambai hupora Israeli ni lipi?

Fungu lao litakuwa kuona hofu kuu jioni na kutoweka kabla ya asubuhi.

Isaiah 18

Isaiah 18:1-2

Nchi yenye mabawa ya mchakarisho iko wapi?

Nchi yenye mabawa ya mchakarisho ipo ng'ambo ya pili na mito ya Kushi.

Nchi yenye mabawa ya mchakarisho ilituma mabalozi kwa nani?

Wanatuma mabalozi kwa taifa refu na laini, kwa watu wanaogopwa, taifa lenye nguvu na kushinda, ambalo hugawanya mito na nchi.

Isaiah 18:3

Wakazi wa dunia wanatakiwa kutazama na kusikiliza wakati gani?

Wanapaswa kutazama na kusikiliza pale ishara inapoinuliwa juu ya milima na pale tarumbeta inapopulizwa.

Isaiah 18:4-5

Yahwe atafanya nini kabla ya mavuno, kuchanua kunapofikia mwisho?

Yahwe atakata majani na kifaa cha kupogoa na kukata chini na kuondoa matawi yanayosambaa.

Isaiah 18:6-7

Nini kitatokea ndege wa kiangazi juu ya matawi na wanyama wote wa dunia kipindi cha baridi kikiwafikia?

Katika kipindi hicho shukrani italetwa katika Mlima Sayuni kwa ajili ya Yahwe kutoka kwa watu warefu na laini.

Isaiah 19

Isaiah 19:1-2

Tamko hili linamhusu nani?

Sura hii ni tamko kuhusu Misri.

Nani ataamsha Wamisri?

Yahwe ataamsha Wamisri.

Wamisri wataamshwa dhidi ya nani?

Wataamshwa dhidi yao wenyewe.

Isaiah 19:3-4

Yahwe atasababisha nani kuwaongoza Wamisri?

Yahwe atawapa Wamisri katika mikono ya bwana katili, na mfalme mwenye nguvu atatawala juu yao.

Isaiah 19:5-8

Nini kitatokea kwa maji ya Misri?

Maji ya bahari yatakauka na mto utakauka na kuwa tupu.

Isaiah 19:9-10

Nini kitatokea kwa watumishi wa nguo wa Misri?

Watumishi wa nguo watapondwa.

Isaiah 19:11-12

Nini kilitokea kwa ushauri wa washauri wa Farao?

Ushauri wao umekuwa hauna maana.

Isaiah 19:13-15

Kwa nini ushauri wa washauri wa Farao umekuwa hauna maana?

Ushauri wao umekuwa hauna maana kwa sababu Yahwe amechanganya roho ya kuchanganya miongoni mwa Wamisri.

Isaiah 19:16-17

Katika siku hiyo Wamisri watakuwa kama nini?

Katika siku hiyo Wamisri watakuwa kama wanawake. Watatetemeka na kuogopa.

Isaiah 19:18

Katika siku hiyo miji mitano ya Misri itafanya nini?

Itaapa utii kwa Yahwe wa Majeshi.

Isaiah 19:19-22

Katika siku hiyo nini kitakuwa katikati ya nchi ya Misri?

Katika siku hiyo kutakuwa na madhabahu kwa ajili ya Yahwe katikati ya nchi ya Misri.

Isaiah 19:23

Katika siku hiyo nani atamwabudu Yahwe kwa pamoja?

Wamisri na Ashuru watamwabudu Yahwe pamoja.

Isaiah 19:24-25

Nani atakuwa baraka miongoni mwa dunia katika siku hiyo ?

Israeli, Misri na Ashuru watakuwa baraka miongoni mwa dunia.

Isaiah 20

Isaiah 20:1-2

Nini kilitokea jemadari alipokuja kwa Ashdodi?

Jemadari alipigana dhidi ya Ashdodi na kuichukua.

Nani alimtuma jemadari kwa Ashdodi

Sargoni mfalme wa Ashuru alimtuma jemadari kwa Ashdodi.

Yahwe alimwambia Isaya afanye nini pale jemadari alipomchukua Ashdodi?

Yahwe alimwambia Isaya kuondoa nguo yake ya gunia na ndara na kutembea uchi na peku.

Isaiah 20:3-4

Kwa Isaya aliambiwa kutembea uchi?

Hii ilikuwa ishara ya kwamba mateka wa Misri na waliohamishwa wa Kushi walikwenda kuongozwa uchi na peku na mfalme wa Ashuru.

Isaiah 20:5-6

Nini kitatokea kwa wale ambao huweka matumaini yao kwa Kushi na Misri?

Watashangazwa na kuaibishwa.

Isaiah 21

Isaiah 21:1-2

Isaya alipewa aina gani ya maono?

Maono ya kuhuzunisha yalipewa kwake.

Maono yalihusu nini?

Maono ya Isaya ni ju ya shambulizi kwa Elamu na kuzingira kwa Media.

Isaiah 21:3-5

Maono yalimuathiri vikoje Isaya?

Yalimpa Isaya maumivu katika kiuno chake. Aliinamishwa chini na kufadhaika. Moyo wake ulidunda. Alikuwa akitetemeka.

Isaiah 21:6-7

Bwana alisema nini kwa Yahwe?

Bwana alimwambia Isaya kuweka mlinzi na kumfanya mlinzi atoe taarifa kile anachoona.

Mlinzi alipaswa kufanya nini atakapoona kibandawazi, wapanda farasi katika makundi na waendeshaji juu ya punda na ngamia?

Kisha mlinzi anatakiwa kuzingatia kwa makini na kuwa macho sana.

Isaiah 21:8-12

Dereva wa kibandawazi atakapokuja, anaita nini?

Anaita, "Babeli ameanguka, ameanguka, na maumbo yote ya miungu yamevunjwa ardhini".

Isaiah 21:13-15

Nani hukaa usiku katika nyika ya Uarabuni?

Misafara ya Wadedani hukaa usiku kule.

Misafara ya Wadedani wanaambiwa kufanya nini?

Wanaambiwa kuleta maji kwa ajili ya wenye kiu.

Wakazi wa nchi ya Tema wanaambiwa kufanya nini?

Wanaambiwa kukutana na wakimbizi na mkate.

Isaiah 21:16-17

Bwana alimwambia nini Isaya kuhusu Kedari?

Bwana alimwambia Isaya ya kwamba ndani ya mwaka utukufu wa Kedari utakwisha na wapiga mishale wachache na mahodari watabaki.

Isaiah 22

Isaiah 22:1-2

Mada ya sura ya 22 ni ipi?

Ni tamko kuhusu bonde la maono.

Watu wote wameenda wapi?

Wote wameenda juu ya dari za nyumba.

Nini kinatokea katika mji?

Mji una kelele na mji umejaa shangwe.

Je! wafu walikufa kwa upanga au vitani?

Hapana wafu hawakufa kwa upanga au kwa vita.

Isaiah 22:3-4

Nini kilitokea kwa watawala wao?

Watawala wao walitoroka pamoja na walikamatwa na kushikwa pamoja

Kwa nini Isaya alikuwa akilia kwa uchungu?

Alikuwa akilia kwa sababu ya uharibifu wa binti za watu wake.

Isaiah 22:5-7

Nani alichukua podo na ngao dhidi yao?

Elamu atachukua podo na Kiri atalaza ngao wazi.

Nini kitatokea kwa mabonde mazuri ya Yuda?

Mabonde yao yatajaa vibandawazi.

Isaiah 22:8-11

Mungu alifanya nini na ulinzi wa Yerusalemu?

Aliondoa ulinzi wao.

Isaiah 22:12-14

Yahwe wa majeshi alita nini katika siku hiyo?

Aliita kwa ajili ya kulia na kuomboleza, kwa ajili ya kunyoa vichwa na kuvaa nguo za gunia.

Watu walifanya nini badala ya kulia na kuomboleza?

Watu walishangilia na walikuwa na furaha. Waliua ng'ombe na kondoo, walikula nyama na kunywa divai.

Je! Bwana atawasamehe watu kwa jibu lao?

Bwana hatawasamehe hata watakapokufa.

Isaiah 22:15-16

Shebna, msimamizi, alifanya nini kwa ajili yake mwenyewe?

Shebna alichonga kaburi kwa ajili yake katika mwamba kama sehemu ya kupumzika.

Isaiah 22:17-19

Yahwe alisema angefanya nini kwa Shebna?

Yahwe alisema angemtupa Shebna chini, na kumuondoa katika ofisi na kituo chake.

Isaiah 22:20-24

Nanii alitakiwia kuchukua nafasi ya Shebna ya mamlaka?

Eliakimu, mwana wa Hilkia alitakiwa kuchukua nafasi ya mamlaka ya Shebna.

Isaiah 22:25

Katika siku hiyo nini kitatokea kwa kigingi kilichozamishwa katak sehemu imara?

Kigingi kilichozamishwa katika sehemu imara kitaachia, kukatika na kuanguka na uzito uliokuwa juu yake utavunjika.

Isaiah 23

Isaiah 23:1-3

Tamko katika sura ya 23 linahusu nani?

Tamko katika sura ya 23 lilikuwa juu ya Tiro.

Kwa nini meli za Tarshihi zinalia?

Wanatakiwa kulia kwa sababu hawana nyumba wala bandari.

Mji wa Tiro ulkuwa upi?

Tiro likuwa sehemu ya soko ya mataifa.

Isaiah 23:4-7

Misri atafanya nini takaposikia taarifa kuhusu Tiro?

Misri italia itakaposikia taarifa kuhusu Tiro.

Isaiah 23:8-14

Nani alipanga hili dhidi ya Tiro?

Bwana wa majeshi alipanga hili dhidi ya Tiro

Kwa nini Bwana wa Majeshi alipanga hili dhidi ya Tiro?

Amepanga hili kushusha kiburi chake na utukufu wake wote, kuaibsha wote walionuliwa wa dunani.

Isaiah 23:15-16

Tiro atasahaulika kwa muda gani?

Katika siku hiyo, Tiro atasahaulika kwa miaka sabini.

Isaiah 23:17-18

Nini kitatokea kwa Tiro baada ya kusahaulika kwa miaka sabini?

Yahwe atasaidia Tiro, na atarudi kwa kazi yake na kujifanya kuwa kahaba na falme zote za duniani.

Nini kitatokea kwa faida ya Tiro na mapato?

Faida na mapato yatatunzwa kwa ajili ya Yahwe.

Nini kitatokea kwa bidhaa ya Tiro?

Itakuwa kwa wale ambao huishi katika uwepo wa Yahwe, kwa ajili yao kula na kuwa na mavazi ya milele.

Isaiah 24

Isaiah 24:1-2

Yahwe anataka kufanya nini?

Anataka kufanya kuwa tupu dunia, kuiharibu, kuharibu sakafu yake na kutawanya wakazi wake.

Isaiah 24:3-5

Dunia ilichafuliwaje na wakazi wake?

Dunia ilichafuliwa kwa sabau wakazi wake walivuka mipaka ya sheria, kukiuka maelekezo na kuvunja agano la milele.

Isaiah 24:6-11

Nini kinatokea kwa wakazi wa dunia?

Wataungua na watu wachache watabaki.

Isaiah 24:12-13

Isaya anatumia picha gani kuonyesha itakavyokuwa katika kipindi hicho katika dunia nzima miongoni mwa mataifa?

Analinganisha hali juu ya dunia katika kipindi hicho kwa jinsi itakavyokuwa mti wa mzabibu unavyopigwa au kama makusanyo ambapo mavuno ya mizabibu yanakamilika.

Isaiah 24:14-15

Katika janga hili "watafanya" nini?

Watainua sauti zao na kupiga kelele ukuu wa Yahwe na watapiga kwa furaha kutoka baharini.

Isaiah 24:16-20

Jibu la Isaya kwa kelele na miito ya kumtukuza Yahwe, Mungu wa Israeli lilikuwa lipi?

Isaya anajibu kwa kusema, "Nimeisha, nimeisha, ole wangu! Waongo wamefanya uongo; ndio, waongo wamefanya uongo sana.

Isaiah 24:21-23

Katika siku hiyo Yahwe atamuadhibu nani?

Yahwe ataadhibu kundi la walio juu na wafalme wa dunia juu ya dunia.

Adhabu kwa ajili ya kundi la walio juu na wafalme wa dunia juu ya dunia itakuwa nini?

Watakusanywa pamoja, wafungwa katika shimo na watafungwa gerezani na baada ya siku nyingi watahukumiwa.

Kwa nini mwezi utaaibika na jua kufedheheshwa?

Hii ni kwa sababu Yahwe wa majeshi atatawala juu ya Mliima Sayuni katika Yerusalemu, na mbele za wazee wake katika utukufu.

Isaiah 25

Isaiah 25:1-5

Kwa nini Isaya alimuinua na kumsifu Yahwe?

Isaya alimwinua na kumsifu Yahwe kwa sababu alifanya mambo ya ajabu, mambo yaliyopangwa zamani, katika uaminifu timilifu.

Mambo gani ya ajabu aliyafanya Yahwe?

Yahwe alifanya mji kuwa rundo, mji ulioimarishwa, uharibifu na ngome ya wageni katika mji ambao haupo.

Nini litakuwa jibu baada ya Yahwe kufanya miji rundo, n.k.?

Watu wenye nguvu watamuinua Yahwe na mji wa mataifa yenye vurugu yatamuogopa.

Isaiah 25:6-8

Yahwe atafanya nini kwa ajili ya na kwa watu wote juu ya huo mlima?

Atafanya karamu ya vitu vinene kwa ajili ya watu wote na ataangamiza vinavyofunika watu wote, utando unaofumwa juu ya mataifa yote.

Yahwe atameza nini, kufuta mbali na kuondoa kutoka kwa watu wake?

Atameza kifo, kufuta mbali machozi kutoka katika nyuso zao na ataondoa aibu ya watu wake.

Isaiah 25:9-12

Nini kitasemwa katika siku hiyo?

Hiki kitasemwa: "Tazama, huyu ni Mungu wetu: tumesubiri kwa ajili yake naye atatuokoa. Huyu ni Yahwe; tumemsubiri. Tutakuwa na furaha na kushangilia katika wokovu wake".

Hatma ya Moabu itafananishwa na nini?

Hatma ya Moabu inalinganishwa na majani makavu ambayo yanakanyagwa chini katika shimo lililoja mbolea.

Isaiah 26

Isaiah 26:1-2

Katika siku hiyo wimbo huu utaimbwa wapi?

Wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda.

Mungu ameufanyaje mji kuwa imara?

Ameifanya na nguvu kwa kufanya wokovu kuta zake na ngome.

Malanga ya mji yatafunguliwa kwa ajili ya nani?

Malango yatafunguliwa kwa ajili ya taifa lenye haki linaloshikilia imani.

Isaiah 26:3-4

Tunatakiwa kumtumaini nani na kwa muda gani?

Tunatakiwa kumtumaini Yahwe milele.

Isaiah 26:5-6

Nini kitatokea kwa wale ambao huishi kwa kiburi; miji iliyoimarishwa?

Yahwe atailaza chini; atausambaza mji ulioimarishwa kuwa vumbi. Utakanyagwa chini kwa miguu ya maskini na kukanyagwa na wahitaji.

Isaiah 26:7-9

Shauku ya nafsi yetu ni ipi?

Jina na kumbukumbu ya Yahwe ni shauku ya nafsi yetu.

Nini hutokea hukumu itakapokuja juu ya dunia?

Hukumu itakapokuja wakazi wa uliimwengu watajifunza haki.

Isaiah 26:10

Mtu mwovu atafanya nini atakapoonyeshwa fadhila?

Hatajifunza haki.

Isaiah 26:11-12

Yahwe amefanya nini kwa ajili ya Yuda na ataleta nini kwa ajili ya Yuda?

Yahwe alitimiza kazi zetu zote kwa ajili yetu na ataleta amani kwa ajili ya Yuda.

Isaiah 26:13-15

Nini kilitokea kwa mabwna ambao walitawala juu ya Yuda?

Wamekufa, hawataishi; wamefiwa na hawatainuka. Yahwe alikuja katika hukumu na kuwaangamiza.

Isaiah 26:16-18

Yuda alimtazama Yahwe lini?

Walimtazama Yahwe walipokuwa katika shida; Yahwe alipowaadibisha.

Isaiah 26:19

Kwa nini wakazi katika vumbi wanapaswa kuinuka na kuimba kwa furaha?

Wanapaswa kuinuka na kuimba kwa furaha kwa sababu wafu wataishi, watainuka.

Isaiah 26:20-21

Kwa nini watu wanatakiwa kwenda katika vyumba vyao na kufunga milango yao?

Wanatakiwa kufanya hivi ili wajifiche mpaka hasira ipite.

Yahwe anataka kufanya nini?

Anataka kuja kutoka sehemu yake kuadhibu wakazi wa dunia kwa udhalimu wao.

Isaiah 27

Isaiah 27:1-3

Katika siku hiyo Yahwe atafanya nini na upanga wake?

Yahwe atamwadhibu lewiathani joka, na atamuua joka ambalo limo ndani ya bahari.

Katika siku hiyo Yahwe atafanya nini na shamba la mizabibu la divai?

Atailinda, kuimwagilia kil wakati na kuilina mchana na usiku.

Isaiah 27:4-5

Yahwe atafanya nini kama mibigili na miiba haishiki ulinzi wake na kufanya amani naye?

Yahwe atatembea dhidi yao na kuzichoma pamoja.

Isaiah 27:6-8

Yakobo na Israeli watafanya nini katika siku zijazo?

Yakobo atashika mzizi; Israeli atachipuka na kuota; na watajaza uso wa ardhi kwa matunda.

Isaiah 27:9

Nini litakuwa tunda kamili la Yakobo kugeuka kutoka kwa dhambi yake?

Atafanya mawe yote ya madhabahu kuwa choka na kusagwa, na hakuna ashera au dhabahu la ubani litabaki likisimama.

Isaiah 27:10-11

Kwa nini Muumba wa Israeli hatakuwa na huruma juu yao?

Kwa sababu sio watu wa kuelewa. Yahwe hatakuwa na huruma juu yao.

Isaiah 27:12-13

Katika siku hiyo watu wa Israeli watakusanyika vikoje?

Watakusanywa mmoja mmoja.

Nani atamwabudu Yahwe katika mlima mtakatifu wa Yerusalemu?

Wanaopotea katika nchi ya Ashuru na waliotengwa katika nchi ya Misri watamwabudu Yahwe katika mlima mtakatifu wa Yerusalemu.

Isaiah 28

Isaiah 28:1-2

Efraimu anajulikanaje?

Efraimu anajulikana kama mwenye kiburi na kama mlevi.

Nini kinatokea kwa uzuri wa Efraimu?

Uzuri wa Efraimu unafifia.

Bwana mwenye uwezo na mwenye nguvu analinganishwa na nini?

Analinganishwa kwa mvua ya mawe, dhoruba inayoangamiza, na tufani ya mvua yenye nguvu na kuzidi.

Mungu mwenye uwezo na mwenye nguvu watafanya nini?

Atapiga dunia kwa mkono wake.

Isaiah 28:3-4

ua linalofifia la utukufu mzuri wa Efraimu litafafanishwa na nini?

Litakuwa kama mtini wa kwanza iliyoiva kabla ya kiangazi, ambao, mtu atapouona, wakati bado upo mkononi mwake, hugugumia.

Isaiah 28:5-6

Katika siku hiyo Yahwe atakuwa nini kwa watu wake waliobaki?

Yahwe atakuwa taji zuri, roho ya hukumu kwake ambaye hukaa katika hukumu, na nguvu kw wale wanaogeuza adui zao katika malango yao.

Isaiah 28:7-10

Nanii hupepesuka kwa mvinyo na kuyumbayumba kwa kinywaji cha nguvu?

Waliobaki wa watu wa Yahwe, kuhani na nabii.

Kuhani na nabii hupepesuka na kuyumbayumba ndani ya nini?

Wanapepesuka kwa maono na kuyumbayumba kwa maamuzi.

Isaiah 28:11-12

Yahwe ataongeaje kwa watu wake?

Atazungumza kwa kwa midomo ya dhihaka na ulimi wa kigeni.

Nini kilitokea kipindi cha nyuma Yahwe alipozungumza nao?

Hawakusikia.

Isaiah 28:13

Nini sasa kitakua matokeo ya watu hawa kusiikia neno la Yahwe?

Wataondoka na kuanguka kwa nyuma na kuvunjika, kutegwa na kukamatwa.

Isaiah 28:14-15

Watawala wa watu wa Yerusalemu walisema nini?

Walisema ya kwamba walifanya agano na kifo na kufikia makubaliano na kuzimu ya kuwa hukumu itakapopita katikati haitawafikia. Walisema wamefanya uongo kimbilio lao na wamejificha ndani ya uongo.

Isaiah 28:16

Bwana Yahwe atalaza nini Sayuni?

Atalaza jiwe la msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni la thamani, msingi wa hakika.

Nini hutokea watakapoamini katika jwe la msingi?

Kama wataamini katika jiwe hili la msingi hawataaibika.

Isaiah 28:17

Nini kitatokea kwa mkimbizi wa uongo na sehemu ya kujificha?

Mvua ya mawe itamsomba mkimbizi wa udanganyifu na maji ya mafuriko yatazidi sehemu ya kujificha.

Isaiah 28:18-21

Nini kitatokea kwa agano na kifo na makubaliano na kuzimu ambayo watawala wa watu wa Yerusalemu wamefanya?

Agano hilo na makubaliano yatayeyushwa na pale mafuriko makali yatakapopita katikati watazidiwa kwake.

Isaiah 28:22-29

Isaya anasema nini itakuwa matokea ya kudhihaki?

Anawaonya kutodhihaki la sivyo kamba zao zitakazwa.

Isaiah 29

Isaiah 29:1-2

Arieli ni nini?

Arieli ni mji ambao Daudi aliweka hema.

Isaiah 29:3-4

Yahwe atafanya nini kwa Arieli?

Atazingira Arieli na atashushwa chini.

Isaiah 29:5-6

Itachukua muda gani kwa Arieli kushushwa chini?

Itatokea ghafla, mara moja.

Isaiah 29:7-8

Nani atapigana dhidi ya Arieli na ngome yake?

Kundi la mataifa yote yatapigana dhidi ya Arieli.

Isaiah 29:9-12

Yahwe alimwaga nini kwa Arieli?

Amemwaga juu yao roho ya usingizi mzito.

Umwagaji huu wa roho ya usingizi mzito unawafanya nini wao?

Imewafunga manabii na kuwafunika watazamaji

Isaiah 29:13-16

Lalamiko la Bwana dhidi ya watu ni lipi?

Bwana alisema, "Watu hawa huja karibu na mimi kwa midomo yao na kuniheshimu kwa midomo yao, lakini moyo wao uko mbali na mimi. Kuheshimu kwao kwangu ni amri iliyofundishwa na watu.

Kwa kuwa mioyo yao iko mbali na Bwana na hawamheshimu, Bwana atafanya nini kwao?

Atasababisha hekima ya watu wenye hekima kuangamia na uelewa wa wenye busara kutoweka.

Isaiah 29:17-19

Nini kitatokea kwa Lebanoni katika muda mfupi?

Lebanoni atageuzwa kuwa shamba na shamba litakuwa msitu.

Katika siku hiyo viziwi na vipofu watafanya nini?

Viziwi watasiikia maneno ya kitabu na macho ya vipofu yataona katika giza zito.

Waliokandamizwa na maskini miongoni mwa watu watafanya nini?

Watashangilia katika Yahwe Mtakatifu wa Israeli.

Isaiah 29:20-21

Nini kitatokea kwa wale ambao hupenda kufanya maovu?

Wataondoshwa.

Isaiah 29:22-24

Nyumba ya Yakono itainua jina la Yahwe lini?

Watainua jina la Yahwe atakaona watoto wake miongoni mwo, kazi ya mikono ya Yahwe.

Nini kitatokea kwa walalamishi na wale amabo hukosea rohoni?

Walalamishi watajifunza maarifa na wale waliokosa rohoni watapata uelewa.

Isaiah 30

Isaiah 30:1-2

Yahwe alisema nini kuwa watoto wa waasi hufanya?

Alisema wanafanya mipango lakini sio kutoka kwake na kufanya utando lakini sio kwa roho wake, ili kwamba waweze kuongeza dhambi kwa dhambi.

Watoto wa waasi hutafuta nini kujilinda?

Wanatafuta ulinzi kutoka kwa Farao na kukimbilia kivuli cha Misri.

Isaiah 30:3-5

Ulinzi wa Farao na kivuli cha Misri vitakuwa nini kwa watoto waasi?

Ulinzi wa Farao utakuwa aibu yao na kivuli cha Misri kitakuwa fedheha yao.

Isaiah 30:6-7

Msaada wa Misri una thamani gani kwa watoto waasi?

Msaada wa Misri haukuwa na thamani.

Isaiah 30:8-9

Kwa nini Yahwe anamtaka Isaya kuandika katika uwepo wao juu ya kibao, na kuandika juu ya hati ya kukunja?

Yahwe anataka itunzwe kwa kipindi kijacho kama ushuhuda.

Watu waasi hawasikii kitu gani?

Hawatasikia maelekezo ya Yahwe.

Isaiah 30:10-14

Watoto waasi wanataka kusikia kitu gani?

Wanataka kusika mambo malaini na utabiri wa udanganyifu.

Isaiah 30:15-16

Yahwe anasema nini watoto waasi wanaweza kuwa na nguvu na kuokolewa?

Yahwe anasema wanaweza kuokolewa kwa kurudi na kupumzika, na kwa utulivu na imani itakuwa nguvu yao.

Jibu la Yahwe kwa kauli ya watoto waasi kuhusu kutoroka juu ya farasi na kuendesha juu farasi za haraka?

Yahwe anajibu kwa kuwaambia watoto waasi kuwa watatoroka na kwamba wale ambao huwafukuza watakuwa na kasi.

Isaiah 30:17

Yahwe alisema wangapi watatoroka kwa tishio la mmoja?

Yahwe alisema elfu moja watatoroka kwa tishio la mmoja.

Isaiah 30:18-19

Yahwe anasubiri na kuwa tayari kufanya?

Anasubiri kuwa na neema kwa watoto waasi na kuwa na rehema juu yao.

Nini kitatokea kwa wale wote wanaomsubiri Yahwe?

Watabarikiwa.

Isaiah 30:20-21

Ingawa Yahwe huwapatia mkate wa taabu na maji ya mateso, mwalimu wao hatafanya nini tena?

Mwalimu wao hatajificha tena, lakini watamwona kwa macho yao wenyewe.

Isaiah 30:22-24

Watoto waasi watafanya nini na viumbe vyao vya kuchonga na viumbe vya kuchonga vya dhahabu?

Watavikufuru na kuvitupa mbali

Isaiah 30:25-29

Yahwe atafanya nini kwa watu wake baada ya siku ya machinjo makuu ambapo minara itaanguka?

Yahwe atawafunga kufungwa kwa watu wake na kuponya vidonda vya kuwajeruhi kwake.

Isaiah 30:30

Yahwe atajidhihirishaje ufahari wa sauti yake na kuonyesha ishara ya mkono wake?

Atazidhihirisha kwa hasira ya dhoruba na miale ya moto, na upepo wa dhoruba, mvua ya dhorub na mvua ya mawe.

Isaiah 30:31-32

Sauti ya Yahwe na ishra ya mkono wake utaelekezwa kwa nani?

Wataelekezwa kuelekea Ashuru. Kwa kuwa kwa sauti ya Yahwe, Ashuru itavunjwavunjwa; atawapiga kwa fimbo.

Nini kitaambatana kila pigo cha rungu iliyoteuliwa ambayo Yahwe atailaza juu yake?

Muziki wa kigoma na vinubi vitaambatana na kila pigo wakati Yahwe akipigana vita na Ashuru

Isaiah 30:33

Nini kimeandaliwa kwa ajili ya mfalme wa Ashuru?

Sehemu ya kuchomwa imeandaliwa kwa ajili ya mfalme wa Ashuru.

Nini au nani atawasha moto ulioandaliwa kwa ajilii ya mfalme wa Ashuru?

Pumzi ya Yahwe itamuamsha.

Isaiah 31

Isaiah 31:1-2

Kwa nini ole inatangazwa kwa wale wanaokwenda chini Misri kwa ajili ya msaada?

Ole inatamkwa juu yao kwa sababu wanatumaini kwa vibandawazi na wapanda farasi lakini hawajihusishi na Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti Yahwe.

Yahwe atainuka dhidi ya nani?

Atainuka dhidi ya nyumba ovu na dhidi ya wasaidizi wa wale ambao hutenda dhambi.

Isaiah 31:3-4

Nini kitatokea kwa yule ambaye husaidia na yule ambaye anasaidiwa?

Wote wawili watatoweka pamoja.

Isaiah 31:5-9

Yahwe atafanya nini kwa ajili ya Yerusalemu?

Atailinda, ataikomboa na ataitunza.

Isaya anawaambia watu wa Israeli kufanya nini?

Anawaambia kurudi kwa Yahwe ambaye walimgeuka sana.

Baada ya Ashuru kuanguka kwa upanga, vijana wao vijana watalazimika kufanya nini?

Wanamume vijana wa Ashuru watalazimishwa kufanya kazi ngumu.

Isaiah 32

Isaiah 32:1-3

Mfalme wa haki na wakuu wa haki watakuaje?

Watakuwa kama hifadhi kutoka na upepo na kimbilio kutoka kwa dhoruba, kama vijito vya maji katika sehemu kavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi ya uchovu.

Isaiah 32:4-6

Wenye pupa na kigugumizi watafanya nini mfalme atakapotawala kwa haki na wakuu kutawala kwa haki?

Wenye pupa watafikiri kwa makini kwa uelewa na wenye kigugumizi wataongea kwa kueleweka na kwa utulivu. Mpumbavu hataitwa tena mwenye heshima, wala mdanganyifu hataitwa mwenye maadili.

Mpumbavu hufanya nini?

Anaongea upuuzi, moyo wake hupanga matendo maovu yasiyo ya Mungu na huzungumza vibaya dhidi ya Yahwe.

Isaiah 32:7-8

Mdanganyifu hufanya nini?

Anatumia njia za uovu. Huoanga mioango miovu kuharibu maskini kwa uongo.

Nini kitatokea kwa mtu mwenye heshima?

Mtu anayeheshimila atasimama kwa sabau ya matendo yake ya heshima.

Isaiah 32:9-13

Kwa nini wanawake ambao walikuwa wametulia waliiambiwa kusikiliza sauti ya Yahwe?

Waliambiwa kusikiliza sauti ya Yahwe kwa sababu katika muda mchache baada ya mwaka kujiamini kwao kutavunjwa, na mavuno ya matunda yatashindwa, na makusanyo hayatakuja.

Isaiah 32:14-15

Nini kilikwenda kutendeka kwa kasri na mji uliosongamana?

Kasri ilikwenda kuachwa na mji uliosongamana kutelekezwa.

Uharibifu utadumu muda gani?

Utadumu mpaka Roho amwagwe kutoka juu na nyika kuwa shamba linalozaa na shamba linalozaa kuchukuliwa kama msitu.

Isaiah 32:16-18

Kazi na matokeo ya wenye haki itakuwa nini?

Kazi ya wenye haki itkuwa amani na matokeo ya haki, utulivu na kujiamini milele.

Isaiah 32:19-20

Ni nani ambaye atabarikiwa?

Watabarikiwa wale ambao hupanda kando ya vijito vyote na ambao hutuma ng'ombe zao dume na punda kulisha.

Isaiah 33

Isaiah 33:1-2

Nini kitatokea kwa mwangamizaji na msaliti watakapoacha kuangamiza na kusaliti?

Mwangamizaji wataangamizwa na msaliti atasalitiwa.

Isaiah 33:3-4

Nini hutokea Yahwe anapoinuka?

Mataifa hutawanywa.

Isaiah 33:5-6

Yahwe atajaza Sayuni na nini?

Atajaza Sayuni na hukumu na haki.

Yahwe atakuwa nini katika kipindi chao?

Katika kipindi chao atakuwa uthabiti, wingi wa wokovu na hekima na maarifa

Isaiah 33:7-9

Kwa nini wajumbe wao walilia na wanadiplomasia kulia kwa uchungu?

Walilia kwa sababu njia zilitelekezwa; hapakuwa na wasafiri tena. Mikataba ilivunjwa, mashahidi walidharauliwia na miji haikuheshimwa.

Isaiah 33:10-12

Yahwe atapoinuka matokeo yake yatakuwa nini?

Yahwe atainuliwa na kutukuzwa.

Nini kitatokea kwa wale walio Sayuni ambao hushika mimba ya makapi, na kuzaa mashina ya mabua?

Pumzi yao ni moto ambao utawateketeza. Watu watachomwa kuwa majivu.

Isaiah 33:13-14

Jibu la wenye dhambi wa Sayuni ni lipi?

Wenye dhambi wa Sayuni wanaogopa; kutetemeka kumewakamata wasio na Mungu.

Isaiah 33:15-21

Nani kati ya wale wa Sayuni wanaweza kuishi na moto umezao na kuchomwa kwa milele?

Wale ambao wanaweza kuishi na moto huu na kuchomwa ni wale ambao hutembea kwa haki na kuongea ukweli; ambao hudharau ongezeko la ukanamizaj, wanaokataa kupokea rushwa, ambao hupanga uhalifu wa vurugu na kutotazama uovu.

Anayetembea kwa haki na kuzungumza ukweli atatengeneza nyumba yake wapi?

Yule anayetembea kwa haki na kuongea ukweli atajenga nyumba yake juu ya vilele.

Isaiah 33:22

Yahwe ni nani na atafanya nni?

Yahwe ni muamuzi wetu, mtoa sheria wetu na mfalme wetu; atatuokoa.

Isaiah 33:23-24

Mateka makubwa yatakapogawanywa nani atakuwa miongoni mwa watakaoivuta?

Hata vilema watakokota mateka.

Isaiah 34

Isaiah 34:1-2

Nani anatakiwa kuja karibu, kusikiliza na kuzingatia kwa makini?

Mataifa, dunia na kila kinachoijaza, ulimwengu na vitu vyote vtokavyo kwake vinatakiwa kuja karibu, kusikiliza na kuzingatia kwa makini.

Kwa nini mataifa, dunia na kila kinachoijaza, dunia na vitu vyote ambavyo hutoka kwake inatakiwa kuja karibu na kusikiliza na kuzingata kwa makini?

Vinatakiwa kufanya hivi kwa sababu Yahw amekasirika na mataifa yote na ana hasira dhidi ya majeshi yao yote.

Yahwe amefanya nini kwa mataifa na majeshi yao?

Amewaangamiza kabisa. Amewkabidhi kuchinjwa.

Isaiah 34:3-4

Nini kitatokea kwa nyota na anga?

Nyota zote za anga zitafifia na anga itakunjwa juu kama hati ya kukunja; na nyota zao zote zitafifia.

Isaiah 34:5-7

Yahwe atafanya nini baada ya upanga wake kunywa ujazo wake mbinguni?

Kisha upanga wake utashuka chni juu ya Edomu na juu ya watu waliotengwa kwa hukumu.

Yahwe ana nini Bozra na Edomu?

Yahwe ana sadaka kubwa Bozra na machinjio makubwa katika nchi ya Edomu.

Isaiah 34:8-10

Nini kitatokea katika nchi ya Edomu?

Vijito vyake vitageuzwa kuwa lami na vumbi lake kuwa salfa. Atakuwa lami nayochomwa. Itakuwa nchi ya takataka; hakuna atakayepita katikati yake.

Isaiah 34:11-15

Kwa ujumla nini kitaishi Edomu?

Ndege pori na wanyama wataishi Edomu.

Isaiah 34:16-17

Kwa muda gani ndege na wanyama watamiliki Edomu?

Watamiliki milele; kutoka kizazi kwa kizazi wataishi pale.

Isaiah 35

Isaiah 35:1-2

Nini kitatokea kwa jangwa?

Itashangilia na kuchipua kama waridi.

Nini kitatokea kwa jangwa?

Utukufu wa Lebanoni utapewa kwake, fahari ya Karmeli na Sharoni.

Nyika, Arabia na jangwa vitaona nini?

Wataona utukufu wa Yahwe, fahari ya Mungu wetu.

Isaiah 35:3-4

Kwa nini wale wenye moyo wa hofu wanatakiwa kuwa na nguvu na kutoogopa?

Kwa sababu Mungu wao anakuja na kisasi pamoja na fidia ya Mungu. Atakuja na kuwaokoa.

Isaiah 35:5-7

Baadhi ya mambo ambayo yatatokea ambapo Mungu wao atakuja ni yapi?

Vipofu wataona. Wafu watasikia. Mtu kilema ataruka. Bubu ataimba. Kutakuwa na maji katika Arabia na vijito katika nyika. Mchanga unaochoma utakuwa dimbwi na ardhi yenye kiu itatoa maji. Kutakuwa na matete ambapo mbweha waliwahi kulala.

Isaiah 35:8-9

Jina la barabara ambalo litajitokeza katika kipindi hicho litakuwa lipi?

Barabara litaitwa Njia ya Utakatifu.

Nani atakuwa na hatakuwepo juu ya barabara?

Wachafu hawatasafiri juu yake na hakuna mpumbavu atakayeenda juu yake. Hakuna simba au mnyama mkali atakuwa juu yake. Njia itakuwa kwa ajili ya yule ambaye hutembea katika njia ya utakatifu. Waliokolewa watatembea pale.

Isaiah 35:10

Nini kitatokea kwa waliolipiwa wa Yahwe watakaporudi?

Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; furaha na raha itawapita; huzuni na kushusha pumzi itatoweka.

Isaiah 36

Isaiah 36:1-5

Nini kilitokea katiika mwaka wa kumi na nne wa mfalme Hezekia?

Senakeribu, mfalme wa Ashuru, alitembea dhidi ya miji yote isiyoshindwa ya Yuda na kuikamata.

Mfalme wa Ashuru alimtuma nani kutoka Lakishi kwenda Yerusalemu kwa Hezekia?

Mfalme wa Ashuru alimtuma amiri.

Amiri alisimama wapi?

Alisimama katika mfereji wa dimbwi la juu, katika barabara kwa shamba la mwoshaji.

Nani alitoka nje kukutana na amiri?

Eliakimu mwana wa Hilkia, Shebna mwandishi na Yoa mtunza kumbukumbu, mwana wa Asafu alikwena kukutana na amiri.

Isaiah 36:6-7

Amiri alisema Farao, mfalme wa Misri, alikuwa kwa yeyote ambaye alimwamini?

Amiri alisema Farao alikuwa tete lililovunjika vunjika kama likitumika kama fiimbo ya kutembelea ingechoma mkono wake.

Isaiah 36:8

Kwa nini amiri alisema mfalme wa Ashuru angefanya kama Hezekia angefanya makubaliano na mfalme wa Ashuru.

Amiri alisema mfalme wa Ashuru angempa Hezekia farasi elfu mbili.

Isaiah 36:9-10

Amiri alisema ni nani alimwambia kutembea dhidi ya Yuda na kuiangamiza?

Amiri alisema ya kwamba Yahwe alimwambia kutembea dhidi ya Yuda na kuiangamiza.

Isaiah 36:11-12

Kwa nini Eliakimu, Shebna na Yoa walimwomba kamanda kuzungumza kwa Kiaramea.

Hawakutaka watu juu ya ukuta kusikia na kuelewa kile kilichosemwa.

Isaiah 36:13-15

Amiri alijibuje kwa ombi kwake kuzungumza kwa Eliakimu, Shebna na Yoa kwa Kiaramea?

Alijibu kwa kusimama na kupiga kelele kwa sauti kubwa katika lugha ya Kiyahudi.

Kwa ufupi amiri alisema maneno ya mfalme wa Ashuru yalikuwa ni yapi kulingana na Hezekia?

Alisema kutoruhusu Hezekia kuwadanganya kwa sababu Hezekia asingeweza kuwaokoa na alisema kutoamini ndani ya Yahwe.

Isaiah 36:16-20

Mfalme wa Ashuru alisema nini kingetokea kama Wayahudi wangefanya amani na yeye na kuja kwake?

Alisema Wayahudi wangekula kutoka kwa mizabibu yao na kutoka miti yao ya mtini, na kunywa maji kutoka kwenye vyombo vyao, hadi atakapokuja na kuchukua Wayahudi katika nchi kama nchi yao wenyewe, nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na mashamba ya zabibu.

Isaiah 36:21-22

Jibu kwa maneno ya amiri lilikuwa lipi?

Walikaa kimya na hawakujibu, kwa kuwa amri ya mfalme ilikuwa, "Usimjibu"

Eliakimu, Shebna na Yoa walifanya nini baada ya maneno ya amiri?

Walikuja kwa Hezekia kwa nguo zao zilizochanika na kutoa taarifa kwa Hezekia maneno ya amiri.

Isaiah 37

Isaiah 37:1-2

Hezekia alifanya nini aliposikia taarifa kutoka kwa Eliakimu, Shebna na Yoa?

Hezekia alichana nguo zake, akajifunika na nguo ya gunia na kwenda katika nyumba ya Yahwe. Pia akamtuma Eliakimu, Shebna na viongozi wa makuhani kwa Isaya nabii.

Isaiah 37:3-4

Hezekia alimwomba Isaya kufanya nini?

Alimwomba Isaya kuomba kwa Yahwe kwa ajili ya waliosalia ambao bado walipatikana kule.

Isaiah 37:5-7

Ni ujumbe gani Isaya aliwapa watumishi wa Hezekia kurudisha kwa Hezekia?

Ujumbe wa Isaya kwa Hezekia ulikuwa kutoogopa maneno ya mtumishi wa mfalme wa Ashuru. Yahwe alikwenda kuweka roho ndani ya mfalme wa Ashuru, na angesikia taariifa na kurudi katika nchi yake na atauawa kwa upanga kule.

Isaiah 37:8-13

Baada ya mfalme wa Ashuru kusikia kuwa Tirhaka, mfalme wa Kushi, alikuja kupigana dhidi yake, ni ujumbe gani mfalme wa Ashuru alituma kwa Hezekia?

Mfalme wa Ashuru alimwambia Hezekia katika barua kutoruhusu Mungu kumdanganya Hezekia kwa kusema, Yerusalemu haitatolewa kwenda kwa mkono wa mfalme wa Ashuru.

Isaiah 37:14-16

Hezekia alifanya nini baada ya kupokea barua kutoka kwa mfalme wa Ashuru na kuisoma?

Hezekia alikwenda juu kwenye nyumab ya Yahwe na kusambaza barua na kuomba kwa Yahwe.

Isaiah 37:17-18

Hezekia aliomba nini Yahwe afanye?

Kwanza, Hezekia alimwomba Yahwe kusikia na kusikiliza na kufungua macho yake na kuona maneno yote katika barua ya Senakeribu. Pili, Hezekia alimwomba Yahwe kuokoa Yerusaleu kutok kwa mkono wa Senakeribu.

Isaiah 37:19-20

Hezekia aliomba Yahwe afanye nini?

Kwanza, Hezekia alimwomba Yahwe kusikia na kusikiliza na kufungua macho yake na kuona maneno yote katika barua ya Senakeribu. Pili, Hezekia alimwomba Yahwe kuokoa Yerusaleu kutoka kwa mkono wa Senakeribu.

Hezekia alitoa sababu gani kama motisha kwa Mungu kuokoa Yerusalemu kutoka kwa Senakeribu?

Hezekia alitaka Yahwe kuokoa Yerusalemu kutoka kwa Senakeribu ili kwamba falme zote za dunia zijue ya kwamba Yahwe pekee ni Mungu.

Isaiah 37:21-25

Yahwe alijibuje kwa ombi la Hezekia?

Yahwe alijibu kwa kutuma ujumbe kwa Hezekia kupitia Isaya.

Katika ujumbe wa Yahwe kwa Hezekia, Yahwe alisema ya kuwa Senakeribu amefanya kosa gani?

Yahwe alisema Senakeribu amekataa, kukufuru, kuinua sauti yake na kuinua macho yake dhidi ya Mtakatifu wa Israeli.

Isaiah 37:26-27

Yahwe alipanga nini zamani kutatua katika nyakati za zamani?

Alipanga na kutatua kuwa Senakeribu angepunguza miji isiyoshindika kuwa rundo za uharibifu.

Isaiah 37:28-32

Jambo gani lingine Yahwe alijua kuhusu Senakeribu?

Yahwe alijua Senakeribu alipokaa chini, alipotoka, alipoingia, na hasira yake dhidi ya Yahwe.

Nini kilikuwa matokeo ya hasira ya Senakeribu dhidi ya Yahwe?

Yahwe alimgeuza Senakeribu nyuma alikotoka.

Isaiah 37:33-34

Yahwe alisema nini kuhusu mfalme wa Ashuru kuhusu Yerusalemu?

Yahwe alisema mfalme wa Ashuru hataingia Yerusalemu au kupiga mshale pale na kwamba hatamkabili kwa ngao au kujenga tuta la kuzingira dhidi yake.

Isaiah 37:35

Sababu gani Yahwe alitoa kwa kulinda na kuokoa Yerusalemu?

Alisema angelinda na kuokoa Yerusalemu kwa ajili yake na kwa ajili ya Daudi mtumishi wake.

Isaiah 37:36-37

Malaika wa Yahwe alifanya nini?

Alitoka na kupiga chini wanajesh 185,000 katika kambi ya Ashuru.

Isaiah 37:38

Nini kilitokea kwa Senakeribu baada ya kuondoka na kwenda nyumbani Ninawi?

Wakati alipokuwa akiabudu katika nyumba ya Nisroki mungu wake, wanawe, Adrameleki na Shareza, walimpiga Senakeribu kwa upanga.

Isaiah 38

Isaiah 38:1-3

Katika siku hizo nini kilitokea kwa Hezekia?

Akawa mgonjwa sana karibu ya kufa.

Isaya alimwambia nini Hezekia?

Isaya alimwambia Hezekia, "Yahwe anasema, "Weka nyumba yako sawa, kwa kuwa utakufa na hautapona".

Hezekia alifanya nini baada ya kupokea ujumbe wa Yahwe kupitia Isaya?

Aliomba kwa Yahwe kumuuliza kukumbuka jinsi alivyotembea kwa uaminifu mbele za Yahwe kwa moyo wake wote na jinsi alivyofanya mema machoni pa Yahwe. Na Hezekia alilia kwa sauti.

Isaiah 38:4-6

Yahwe alimwambia Isaya kusema nini kwa Hezekia?

Alisem kumwambia Hezekia ya kwamba alisikia maombi na machozi ya Hezekia. Yahwe alimwambia Hezekia angemwongezea miaka kumi na tano katika maisha ya Hezekia na kwa kuongeza angemuokoa Hezekia na Yerusalemu kutoka kwa mfalme wa Ashuru na angeilinda Yerusalemu.

Isaiah 38:7-8

Yahwe alisema angetoa ishara gani ili kwamba Hezekia ajue Yahwe angefanya alichosema?

Yahwe alisema angesababisha kivuli juu ya ngazi ya Ahazi kurudi nyuma hatua kumi.

Isaiah 38:9-15

Katika maombi yalioandikwa ya Hezekia, Hezekia alisema nini kingetokea katikati mwa maisha yake?

Aliisema kuwa angepita katika malango ya kuzimu.

Katika mwanzo mwa maombi yalioandikwa ya Hezekia, alisema nini kuhusu Yahwe?

Hezekia alisema kuwa asingemuona tena Yahwe katika nchi ya wanaoishi.

Isaiah 38:16-19

Hezekia alisema nini kwa Bwana kuhusu mateso yake na majonzi?

Hezekia alisema mateso ambayo Bwana ametuma yalikuwa mazuri kwake na kuwa ilikuwa kwa manufaa ya Hezekia ya kuwa apitie majonzi hayo.

Hezekia alisema Bwana amefanya nini na dhambi zake?

Hezekia alisema Bwana ametupa dhambi zote za Hezekia nyuma ya mgongo wake.

Isaiah 38:20

Hezekia alikwenda kushangilia kwa namna gani kwa kuokolewa na Yahwe?

Hezekia alisema angeshangilia kwa muziki siku zote za maisha yao katika nyumba ya Yahwe.

Isaiah 38:21-22

Isaya alisema kufanya nini ili kwamba Hezekia aweze kupona?

Alisema, "Acha wachukue mkate wa tini na kuilaza kama plasta juu ya jipu naye atapona.

Isaiah 39

Isaiah 39:1-2

Nani alituma barua na zawadi kwa Hezekia?

Merodaki-baladani mwana wa Baladani, mfalme wa Babeli alituma barua na zawadi kwa Hezekia.

Hezekia alionyesha nini kwa wale alioleta barua na zawadi kutoka kwa Merodaki-baladani?

Hezekia aliwaonyesha hazina yake - fedha, dhahabu, viungo, mafuta ya thamani, ghala ya silaha zake, na kila kitu kilichokutwa katika ghala zake. Hezekia aliwaonyesha kila kitu katika nyumba na ufalme wake.

Isaiah 39:3-4

Isaya alimuuliza Hezekia nini?

Alimuuliza Hezekia wanamume walisema nini kwake, wapi wametoka, na nini waliona katka nyumba ya Hezekia.

Isaiah 39:5-6

Isaya alisema mambo gani kwa Hezekia yatachukuliwa Babeli?

Yahwe alimwambia Hezekia ya kwamba yote ambayo yeye na mababu zake walizotunza mpaka siku hiyo itabebwa mpaka Babeli.

Isaiah 39:7-8

Kwa nini Hezekia alifikiri neno la Yahwe ambalo Isaya alizungumza lilikuwa zuri?

Alifikiri lilikuwa zuri kwa sababu alifikiri kutakuwa na amani na uthabiti katika siku zake.

Isaiah 40

Isaiah 40:1-2

Mungu anasema ni kwa jinsi gani kufariji watu wake?

Anasema kufariji kwa kuzungumza kwa upole kwa Yerusalemu, kumwambia ya kwamba vita yake imekwisha na udhalimu wake umesamehewa na kwamba amepokea mara mbili kutoka mkononi mwa Yahwe kwa dhambi zake zote.

Isaiah 40:3-5

Sauti inalia nini?

Inalia, "Katika nyika andaa njia ya Yahwe; nyosha njia katika Arabia barabara kwa ajili ya Mungu wetu"

Nini kitatokea katika nchi Israeli?

Kila bonde litainuliwa, kila mlima na kilima kusawazishwa, nchi yenye mawemawe kufanywa sawa na sehemu za kukwaruza kufanywa kuwa uwanda.

Utukufu wa Yahwe utafunuliwa kwa nani?

Utukufu wa Yahwe utaonekana na watu wote pamoja.

Isaiah 40:6-8

Nini kitasimama milele?

Neno la Mungu wetu litasimama milele.

Isaiah 40:9-14

Habari gani njema zilipaswa kutangazwa kwa Yerusalemu na miji ya Yuda?

Habari njema ilikuwa, "Huyu hapa Mungu wenu!"

Bwana Yahwe anakuja kwa namna gani?

Anakuja kama hodari mshindi.

Yahwe analeta nini pamoja naye atakapokuja?

Yahwe analeta zawadi yake pamoja naye na fidia yake huja mbele zake.

Isaiah 40:15-20

Mataifa ni kama nini kwa Yahwe?

Mataifa ni kama tone katika ndoo kwa Yahwe na huchukuliwa kama vumbi juu ya mizani.

Isaiah 40:21-22

Mungu hukaa wapi?

Mungu hukaa juu ya upeo wa macho wa dunia.

Isaiah 40:23-24

Mungu hufanya nini kwa watawala?

Mungu huwapunguza kuwa si kitu na kuwafanya watawala wa dunia kutokuwa na umuhimu.

Isaiah 40:25-26

Mungu hufanya nini na nyota?

Huongoza mpangilio wao na kuzita zote kwa jina na kwa ukubwa wa uwezo wake na nguvu yake, hakuna moja inayopotea.

Isaiah 40:27-28

Yahwe ni nani, na yukoje?

Yahwe ni Mungu wa milele, mumba wa mwisho wa unia. Hachoki na hakuna mwisho kwa uelewa wake.

Isaiah 40:29-31

Yahwe hufanya nini kwa waliochoka na kudhoofika?

Yahwe hutoa nguvu kwa waliochoka na nguvu mpya kwa waliodhoofika.

Nini kitatokea kwa wale ambao humsubiri Yahwe?

Wale ambao humsubiri Yahwe watapata nguvu mpya; watapaa juu na mabawa kama tai; watakimbia na hawatachoka; watatembea na hawatazimia.

Isaiah 41

Isaiah 41:1-2

Kwa kusudi gani Yahwe anasema, "na tuje karibu pamoja"?

Yahwe anasema kwa wle kuja karibu pamoja ili kwamba waweze kutoa hoja juu ya ugomvi.

Isaiah 41:3-4

Nani aliwaita mbele kizazi kutoka mwanzo?

Ni Yahwe ambaye amefanya mambo haya.

Isaiah 41:5-7

Jibu la visiwa ambavyo vimeona na vinaogopa na mwisho wa dunia ambao hutetemeka ni lipi?

Jibu lao ni kukaribia na kuja na wanajifariji kujenga sanamu.

Isaiah 41:8-9

Yahwe anaitaje Israeli?

Yahwe anaita Israeli mtumishi wake, watoto wa Abrahamu rafiki yake na anaita Israeli aliyechaguliwa.

Yahwe anasema anafanya nini kwa ajili ya Israeli?

Yahwe anasema anarudisha Israeli kutoka mwisho wa dunia.

Isaiah 41:10

Yahwe anaiambia Israeli kutofanya nini na kwa nini?

Yahwe anaiamba Israeli kutoogopa kwa kuwa Yahwe yupo pamoja nao na kutokuwa na wasiwasi kwa sababu yeye ni Mungu wao.

Nini cha ziada Yahwe anasema atafanya kwa ajili ya Israeli?

Yahwe anasema atawaimarisha na kuwasaidia na kuwashika kwa mkono wake wa kulia wa ushindi uliostahili.

Isaiah 41:11-15

Nini kitatokea kwa wale ambao wana hasira na hupinga Israeli?

Wataaibishwa na kufedheheshwa na hawatakuwa kitu na watatoweka.

Isaiah 41:16

Israeli atafanya nini watakapopembua wale ambao hupigana dhidi yao na kushindan nao?

Israeli atashangilia katika Yahwe, katika Mtakatifu wa Israeli.

Isaiah 41:17-20

Yahwe atafanya nini waliokandamizwa na wahitaji watakapotafuta maji?

Yahwe anasema atajibu maombi yao kwa kufanya vijito kutiririka chini ya miteremko na kufanya chemchemi katikati ya bonde, kwa kufanya jangwa kuwa dimbwi la maji na nchi kavu kuwa chemchemi ya maji. Hatawaacha.

Isaiah 41:21-22

Yahwe anasema nini kwa wale ambao hufuata sanamu?

Anasema kutoa hoja zao, kuleta mbele hoja zao nzuri kwa ajili ya sanam zao.

Ushahidi gani Yahwe anasema wale ambao hufuata sanamu wanapaswa kuleta ili tuweze kujua kama tunaweza kuwaamini au la?

Kwa ushahidi Yahwe anasema kuwaambia kile kitakachotokea, na kusema tabiri za awali ili tuweze kuwaza juu yao na kujua namna zilivyotimia.

Isaiah 41:23-24

Makadirio ya Yahwe ni yapi ya sanamu na watu wanaozichagua?

Yahwe anasema sanamu zao sio kitu na matendo yao sio kitu; yeyeambaye huzichagua ni chukizo.

Isaiah 41:25-26

Nani kati ya wale wanaoabudu sanamu walitoa amri au kutamka ya kwamba mmoja atakuja kutoka kaskazini na kukanyaga watawala kama matope, kama mfinyanzi ambaye anakanyaga udongo?

Hakuna kati ya wanaoabudu sanamu walitoa amri na hakuna aliyewasikia wakisema chochote.

Isaiah 41:27-29

Yahwe alisema nini kuhusu yule aliyemwinua kutoka kaskazini?

Alisema kwanza kwa Sayuni, "Tazama, hawa hapa', Altuma mpiga mbiu Yerusalemu.

Katika sura hii maneno ya mwisho ya Yahwe kuhusu wale wanaofuata sanamu ni yapi?

Haya hapa maneno yake: "Ninapotazama, hakuna mtu, hakuna mtu kati yao ambaye anaweza kunishauri, ambay, nitakapouliza, anawez kujiba neno. Tazama wote sio kitu, na matendo yao sio kitu; maumbo yao ya kuchonga ni upepo na tupu.

Isaiah 42

Isaiah 42:1-2

Yahwe anasema amefanya nini kwa ajili ya mtumishi wake?

Yahwe anasema amemchagua mtumishi wake, ambaye amefurahishwa naye na kuwa amemuweka roho wake juu yake.

Yahwe anasema mtumishi wake ataleta nini kwa mataifa?

Yahwe anasema mtumishi ataleta hukumu mbele kwa uaminifu kwa mataifa.

Isaiah 42:3-4

Mtumishi wa Yahwe hatafanya nini kwa tete lililopondwa au utambi unaowaka kwa kufifia?

Yahwe anasema mtumishi wake hatavunjika tete lililopondwa au kuzima utambi uwakao kwa kufifia.

Isaiah 42:5-6

Yahwe anajielezaje?

Anajielezea kama yule aliyeumba mbingu na kuzitandaza mbele; ambaye alitandaza nje dunia na kutoa uhai kwake; anayetoa pumzi kwa watu juu ya ardhi na uhai kwa wale wanaoishi juu yake.

Isaiah 42:7

Yahwe alitaka mtumishi wake aliyemteua kufanya nini kwa watu vipofu na wafungwa?

Yahwe alitaka mtumishi wake kufungua macho ya vipofu, kuachia wafungwa kutoka gerezani, na kutoka katika nyumba ya kifungo wale wanaokaa katika giza.

Isaiah 42:8-11

Yahwe anasema hatagawana nini?

Anasema hatagawana utukufu wake na mwingine wala sifa yake na sanamu za kuchonga.

Yahwe anajitofautishaje na sanamu za kuchonga?

Tofauti na sanamu za kuchonga, vitu vilikuja kuwepo Yahwe alipovitamka.

Yahwe alisema angefanya nini kuendelea kutangaza utukufu wake?

Alisema alikwenda kutangaza matukio mapya. Alikwenda kuongea juu yao kabla havijatendeka.

Isaiah 42:12-15

Yahwe atafanya nini kwa adui zake?

Atawaonyesha nguvu yake.

Isaiah 42:16

Yahwe atafanya nini kwa vipofu?

Atawaleta vipofu katika njia ambayo hawaijui; katika njia ambayo hawaijui atawaongoza. Atageuza giza kuwa nuru mbele yao na kufanya seheu zilizopinda kuwa wima na hatawatelekeza.

Isaiah 42:17

Nini kitatokea kwa wale wanaoamini sanam na kusema kwa viumbe vya kuchonga, "Nyie ni miungu yetu"?

Watageuzwa na kuaibishwa kabisa.

Isaiah 42:18-19

Viziwi na vipofu wanaamuriwa kufanya nini?

Viziwi wanaamuriwa kusikiliza na vipofu wanaamuriwa kutazama ili waweze kuona.

Isaiah 42:20-21

Kwa nini Yahwe anawaamuru kusikiliza na kutazama?

Anawaamuru kusikiliza na kutazama kwa sababu ingawa waliona mambo mengi, lakini hawakuelewa; masikio yao yalifunguliwa lakini kiukweli hakuna aliyesikia.

Isaiah 42:22

Yahwe anasema hali ya watu ikoje?

Yahwe alisema watu walinyanganywa na kuporwa; walitegwa wote katika mashimo, kushikwa mateka katika magereza; walikuwa nyara na hakuna mtu wa kuwakomboa.

Isaiah 42:23-24

Nani alimkabidhi Yakobo kwa mnyanganyi; na Israeli kwa waporaji?

Alikuwa Yahwe aliyewakabidhi.

Kwa nini Yahwe alimkabidhi Yakobo kwa mnyanganyi na Israeli kwa waporaji?

Yahwe aliwakabidhi kwa sababu walitenda dhambi dhidi ya Yahwe ambazo njia zake waliikataa kuzifuata na ambaye sheria yake walikataa kutii.

Isaiah 42:25

Je! Israeli ilitambua nani aliyewatesa kwa uharibifu wa vita na kwa nini alifanya vile?

Hapana! Iliwaka kuwazunguka, ila hawakugundua; iliwachoma, lakini hawaliweka moyoni.

Isaiah 43

Isaiah 43:1

Kwa ujumla, Yahwe alimwambia Yakobo, Israeli, kufanya nini?

Alimwambia Yakobo, Israeli, kutoogopa.

Isaiah 43:2-3

Yahwe alisema atafanya nini kwa ajili ya Israeli ili kuwalinda?

Yahwe alisema mito isingewazidi Israeli na kwamba wasingeweza kudhuriwa au kuchomwa kwa moto au miale.

Kwa nini Yahwe ametoa malipo na kubadilishana kwa ajili ya Israeli?

Amewapa Misri kama malipo na Kushi na Seba kubadilishan kwa ajili ya Israeli.

Isaiah 43:4-9

Yahwe alisema atafanya nini kwa watoto wa Israeli?

Yahwe alisema atawaleta kutoka mashariiki na kuwakusnya kutok magharibi.

Isaiah 43:10-11

Kwa nini Yahwe alitabiri kusanyiko la wanawe na binti zake kutoka mashariki na magharibi na kutangaza kwao matukio ya awali?

Yahwe alifanya hivi ili waweze kumjua yeye, kumwamini na kelewa ya kwamba yeye ni Mungu.

Je! kuna mungu mwingine au mwokozi kuliko Yahwe?

Kabla ya Yahwe hakuna mungu aliyeumbwa na hapatakuwa baada yake. Yeye ni Yahwe na hakuna mwokozi ila yeye.

Isaiah 43:12-13

Nani awezaye kutuokoa kutoka mkononi mwa Mungu?

Hakuna awezaye kutuokoa kutoka mkononi mwa Mungu.

Isaiah 43:14-15

Yahwe alimtuma Babeli kwa ajili ya nani na kuwaongoza wote chini kama wakimbizi, kuwageuza misemo yao furaha Wababeli kuwa nyimbo za maombolezo?

Yahwe alifanya hivi kwa ajili Israeli.

Isaiah 43:16-17

Ni mambo gani ya awali aliyofanya Yahwe ambayo anawaambia wao wasikumbe au kufikiria?

Yahwe alifungua njia katika bahari na barabara katika maji makuu. Aliongoza kibandawazi na farasi, jeshi na kundi lenye uwezo. Walianguka chini pamoja kutoinuka tena. Walizimwa, kupozwa kama utambi unaowaka.

Isaiah 43:18-21

Yahwe anasema jambo gani jipya alilokuwa akataka kufanya jangwani na nyikani?

Yahwe alisema angefanya njia katika jangwa na kijito cha maji katika nyika.

Isaiah 43:22-23

Watu, Israeli, ambao Mungu aliumba kwa ajili yake walishindwa kufanya nini kwa ajili ya Yahwe?

Israeli walishindwa kumwita Yahwe. Hawakumletea kondoo yeyote kama sadaka ya kuteketeza na hawakumwinua kwa sadaka zao.

Isaiah 43:24

Israeli ilifanya nini kwa Yahwe?

Israeli limpa mzigo Yahwe kwa dhambi zao na kumchosha na matendo yao maovu.

Isaiah 43:25-26

Kwa nini Yahwe anafuta makosa ya Israeli na hakumbuki dhambi zao?

Yahwe anafanya hivi kwa ajili yake mwenyewe.

Isaiah 43:27-28

Kwa nini Yahwe alikwenda kuchafua maafisa wa mahali patakatifu; kumkabidhi Yakobo katika marufuku mharibifu na Israeli kwa aibu ya uonevu.

Yahwe alikuwa akifanya hivi kwa sababu baba yao wa kwanza alitenda dhambi na wasemaji wao walikosa dhidi ya Yahwe.

Isaiah 44

Isaiah 44:3-6

Kitu gani Yahwe alimwambia Yakobo alikwenda kumwagia watoto wa Yakobo nje?

Yahwe alisema atakwenda kumwaga nje roho yake juu ya watoto wake.

Isaiah 44:7-8

Mtu angewezaje kuthibitisha kwa Yahwe ya kuwa kuna mtu mwingine kama yeye; mungu mwingine?

Kuthibitisha kwa Yahwe ulitakiwa kueleza kwake matukio ambayo yalitokea kabla Yahwe hajaanzisha watu wake wa zamani na walitakiwa kutamka matukio yatakayofuata.

Isaiah 44:9-10

Yahwe anasema nini kuhusu wale ambao huunda sanamu?

Yahwe anasema wao sio kitu na vitu ambavyo wanafurahia havina thamani na wataaibishwa.

Isaiah 44:11-13

Nini kitatokea kwa fundi stadi na washiriki wake ambao huunda mungu au kuchonga sanamu?

Mafundi stadi na washiriki wao amabo huunda mungu au kuchonga sanamu wataaibishwa.

Isaiah 44:14

Seremala anaanzaje kutengeneza sanamu?

Hukata mti wa seda, au kuchagu mvinje au mwaloni.

Isaiah 44:15-18

Mwanamume hufanya nini na mbao kutoka mtini ambao ameukata?

Mwanamume huutumia sehemu yake kwa ajili ya moto na kujipatia joto, kuoka mkate na kuchoma nyama yake juu yake na sehemu yake kutengeneza sanamu, mungu, na kuisujudia.

Isaiah 44:19-20

Kwa sababu wale ambao hutengeneza na kuabudu sanamu hawana uelewa au maarifa na macho yao ni mapofu na mioyo ya haitambui, maswali gani mawili hawajiulizi wao wenyewe?

Kwanza, hawajiulizi wenyewe kama watengeneza sehemu nyingine ya mbao kuwa kitu kichukizacho cha kuabudu. Pili, hawajiulizii kama ina maana kuinama chini kwa kipande cha mbao.

Isaiah 44:21-22

Kwa nini Yakobo na Israeli wanaambiwa kuwaza juu ya Yahwe kama Mungu pekee na sanmau kama sio kitu?

Wanatakiwa kukumbuka mambo haya kwa sababu Yahwe aliviumba, wao ni watumishi wake na hatawasahau. Pia Yahwe ameondoa nje dhambi zo na matendo yao ya uasi.

Isaiah 44:23

Kwa nini mbingu, milima, msitu na kila mti uliamriwa kuimba?

Wanaamriwa kuimba kwa sababu Yahwe amemkomboa Yakobo na ataonyesha utukufu wake Israeli.

Isaiah 44:24-25

Yahwe anafanya nini kwa wasoma ishara na kwa wale ambao huzisoma?

Yahwe huchanganya ishara wa wasemaji watupu na kuaibisha wale ambao husoma ishara.

Isaiah 44:26-27

Yahwe anafanya nini kwa mtumishi wake na wajumbe?

Yahwe hutimiza matamko ya mtumishi wake na kuleta kupita ushauri wa wajumbe wake.

Yahwe alisema nini kuhusu Yerusalemu na miji ya Yuda?

Alisema kwamba Yerusalemu atakaliwa na miji ya Yuda itajegwa tena na kwamba atainua sehemu zake zilizoachwa.

Isaiah 44:28

Yahwe anasema nini kuhusu Koreshi na kile atakachofanya?

Yahwe alisema kuhusu Koreshi, "Yeye ni mchungaji wangu, atafanya kila hitaji langu - atatamka kuhusu Yerusalemu, "Acha ajengwe tena', na kuhusu hekalu, "Acha misingi yako ilazwe"

Isaiah 45

Isaiah 45:1

Katika sura hii, mtiwa mafuta wa Bwana ni nani?

Katika sura hii, Yahwe anasema Koreshi ni mtiwa mafuta wake.

Kwa nini Yahwe anashikilia mkono wa Koreshi?

Yahwe anashikilia mkono wa Koreshi ili kushinda mataifa mbele yake, kunyanganya silaha wafalme, na kufungua milango mbele yake, li malangao yabaki wazi.

Isaiah 45:2-3

Kwa nini Yahwe ataenda mbele ya Koreshi na kusawazisha milma, kuvunja katika vipande milango ya shaba, kukata katika vipande nguzo zao za chuma na kumpa hazina ya giza na utajiri uliofichwa?

Yahwe atafanya vitu hivi ili kwamba Koreshi ajue ya kuwa ni Yahwe Mungu wa Israel ambaye alimwita.

Isaiah 45:4-6

Yahwe alimwita Koreshi kwa jina lake kwa ajli ya nani?

Yahwe amefanya hivi kwa ajili ya Yakobo mtumishi wake na Israeli aliyeichagua.

Je! Koreshi alimjua Yahwe?

Hapana, Koreshi hakumjua Yahwe.

Je! kuna Mungu mwingine kando na Yahwe?

Hapana, hakuna Mungu mwingine ila Yahwe.

Isaiah 45:7-8

Nani aliunda nuru na kuumba giza na analeta amani na kutengeneza maafa?

Yahwe ndiye ambaye hufanya vitu hivi vyote.

Nani aliumba wokovu?

Yahwe aliumba wokovu.

Isaiah 45:9-12

Yahwe analinganisha na kitu gani mtu ambaye hubishana na muumba wake?

Analinganisha mtu anayebishana na muumba wake kwa udongo ambao husema kwa mfinyanzi, "Unafanya nini?" au ?Unatengeneza nini - haukuwa na mikono ulipokuwa ukifanya?"

Isaiah 45:13

Koreshi atafanya nini kwa ajili ya Yahwe?

Atajenga mji wa Yahwe; ataruhusu watu waliohamishwa na Yahwe kwenda nyumbni na sio kwa gharama wala rushwa.

Isaiah 45:14-15

Je! kuna Mungu mwingine kando na Yahwe?

Hapana, hakuna Mungu mwingine la Yahwe.

Isaiah 45:16-17

Nani atatembea kwa aibu?

Wale ambao huchonga sanamu watatembea kwa aibu.

Wokovu wa Israeli utadumu muda gani?

Yahwe ataokoa Israeli kwa wokovu wa milele.

Isaiah 45:18-19

Je! kuna Mungu mwingine kando na Yahwe?

Hapana, hakuna Mungu mwingine la Yahwe.

Kwa nini Yahwe alibuni dunia?

Alibuni ili ikaliwe.

Isaiah 45:20

Nani ana maarifa?

Wale ambao hubeba picha za kuchonga na kuomba kwa miungu ambao hawawezi kuwaokoa, hawana maarifa.

Isaiah 45:21

Je! kuna Mungu mwingine kando na Yahwe?

Hapana, hakuna Mungu mwingine la Yahwe.

Isaiah 45:22-23

Je! kuna Mungu mwingine kando na Yahwe?

Hapana, hakuna Mungu mwingine la Yahwe.

Yahwe anaapa kwa kitu gani?

Yahwe anaapa kwake mwenyewe.

Isaiah 45:24-25

Kila ulimi utakiri nini?

Kila ulimii utakiri kwa kusema, "Ndani ya Yahwe pekee kuna ukombozi na nguvu".

Nini kitatokea kwa vizazi vyote vya Israeli?

Katika Yahwe vizazi vyote vya Israeli vitahesabiwa haki; watajisifu ndani yake.

Isaiah 46

Isaiah 46:1-2

Beli na Nebo ni kina nani?

Hawa ni sanamu

Nini hubeba Beli na Nebo?

Beli na Nebo wanabebwa na wanyama.

Isaiah 46:3-4

Nani alibeba nyumba ya Yakobo?

Yahwe alibeba nyumba ya Yakobo.

Yahwe alibeba nyumba ya Yakobo kwa muda gani na kwa muda gani atawabeba?

Yahwe aliwabeba kabla ya kuzaliwa kwao na atawebeba hata mpaka nywele kuwa mvi.

Isaiah 46:5-6

Watu hufanya nini na dhahabu na fedha?

Watu huajiri fundi wa chuma na huchukua dhahabu yao na fedha na kutengeneza kuwa mungu.

Isaiah 46:7

Je! mungu huyo anaweza kuwajibu au kuwaokoa?

Hapana hawezi kujibu wala kuokoa yeyote kutoka katika shida.

Isaiah 46:8-9

Yahwe anaweza kulinganishwa na nani? Ni nani kama yeye?

Yahwe ni Mungu na hakuna mwingine. Hakuna aliye kama yeye.

Isaiah 46:10-11

Nani humweka Yahwe, Mungu kando na sanamu?

Yahwe huwekwa kando kwa ukweli kwamba anatangaza mwisho kutoka mwanzo, na kutangaza kabla kile ambacho hakijatokea.

Isaiah 46:12-13

Yahwe anakwenda kufanya nini kwa watu wakaidi?

Yahwe analeta haki yake karibu. Atatoa ukombozi kwa Sayuni na uzuri wake kwa Israeli.

Isaiah 47

Isaiah 47:1-2

Nani hataitwa tena mrembo na wa kuvutia?

Binti bikira wa Babeli, binti wa Wakaldayo, hataitwa tena mrembo na wa kuvutia.

Isaiah 47:3-5

Binti wa Wakaldayo hawataitwa kina nani tena?

Binti wa Wakalday hawataitwa Malkia wa falme.

Isaiah 47:6-7

Kwa nini Yahwe hakufurahishwa na Wakaldayo?

Yahwe alifadhaishwa na Wakaldayo kwa sababu ingawa Yahwe aliwakabidhi watu wake katika mikono ya Wakaldayo, hawakuwaonyesha watu wa Yahwe huruma na kuweka nira nzito sana juu ya watu wazee.

Isaiah 47:8-9

Nini kitatokea kwa binti wa Wakaldayo kwa wakati mmoja katika siku moja?

Binti wa Wakaldayo atateseka kupotewa watoto na ujane kwa wakati mmoja ndani ya siku moja.

Isaiah 47:10-13

Binti wa Wakaldayo wameamini nini?

Aliuamini uovu wake.

Nini hakikulinda maafa na uharibifu ambao ulikuwa unakuja kwa mabinti wa Wakaldayo?

Tabano ya mabinti wa Wakaldayo haukuweza kuwalinda na maafa na uharibifu ambao ulikuwa unakuja juu yao.

Isaiah 47:14-15

Nini kitatokea kwa wale ambao huchunguza mbingu na kutazama nyota, wale ambao hutamka miezi mipya?

Wanamume ambao huchunguza mbingu na kutazama nyota na wale ambao hutangaza miezi mipya ndio wale ambao watakuwa kama mashina ya mabua. Moto utawachoma.

Nani ataokoa binti wa Wakaldayo?

Hapakuwa na mtu wa kuwaokoa.

Isaiah 48

Isaiah 48:1-2

Nyumba ya Yakobo inaitwaje na kutoka kwa nani wanatokana?

Wanaitwa Israeli na wanatokana kwa Yuda.

Israeli anafanya nini kwa uongo na kinyume na haki?

Israeli anaapa kwa jina la Yahwe na kumwomba Mungu wa Israeli kwa uongo na kinyume na haki.

Isaiah 48:3-8

Yahwe alifanya nini, akijua kuwa Israeli ni kaidi?

Alitamka mambo kutoka zamani na kuyafanya kujulikana, ghafla aliyafanya na yakafanyika.

Kwa kutamka mambo haya kwa Israeli kabla ya muda, Yahwe alitumaini kuzuia?

Yahwe alitaka kuzuia Israeli kusema, "Sanamu yangu imeyafanya" au "viumbe vyangu vya kuchonga, au umbo langu la chuma la kuchonga limeamuru mambo haya".

Isaiah 48:9-13

Kwa nini Yahwe atakubali kugeuza hasira yake na kujizuia kuangamiza Israeli?

Atafanya hivi kwa ajili ya jina lake.

Yahwe alitakasaje Israeli?

Aliwatakasa katika tanuu la mateso.

Isaiah 48:14-19

Yahwe alimwita nani na kwa kusudi gani?

Yahwe alimwita mshiriki wake kutekeleza kusudi lake dhidi ya Babeli.

Isaiah 48:20

Tangazo gani linatakiwa kufanywa kwenda katika mwisho wa dunia?

Tangazo ni, "Yahwe amemkomboa mtumishi wake Yakobo"

Isaiah 48:21-22

Yahwe alisema ni nani hatapokea amani?

Yahwe alisema hapakuwa na amani kwa waovu.

Isaiah 49

Isaiah 49:1-2

Yahwe alifanya nini kwa mtumishi wake Israeli?

Yahwe alimwita kwa jina toka kuzaliwa. Alifanya mdomo wa Israeli kama upanga mkali na kumficha Israeli katika kivuli ya mkono wake; alimfanya Israeli kuwa mshale uliong'arishwa; katika podo lake Yahwe alimficha.

Isaiah 49:3-4

Yahwe anakwenda kufanya nin kupitia Israeli?

Yahwe anakwena kuonyesha utukufu wake kupitia Israeli.

Israeli anamwamini Yahwe kwa ajili ya nini?

Israeli anasema haki yake ipo na Yahwe na zawadi yake ipo na Mungu wake.

Isaiah 49:5-6

Kazi ya Israeli ni ipi kama mtumishi wa Yahwe?

Kazi yake ni kumrejesha Yakobo tena kwa Yahwe na kukusanya Israeli kwake.

Jambo gani ni dogo sana kwa mtumishi wa Yahwe?

Ni jambo dogo sana kuwa mtumishi wa Yahwe kuimarisha tena makabila ya Yakobo, na kurejesha waliopona wa Israeli.

Yahwe atafanya jambo gani zaidi kwa mtumishi wake?

Atamfanya mtumishi wake mwanga kwa watu wa mataifa ambao mtumishi wake aweze kuwa wokovu wa Yahwe kwa mwisho wa dunia.

Isaiah 49:7

Nini kitatokea kwa yule ambaye anadharaulika, anayechukiwa na mataifa, mtumwa wa watawala?

Wafalme watamwona na kuinuka, na wakuu watamwona na kusujudu.

Isaiah 49:8-9

Yahwe atamsaidia na kumjibu mtumishi wake lini?

Katika kipindi Yahwe atakachoamua kuonyesha fadhila yake atamjibu mtumishi wake, na katika siku ya wokovu Yahwe atamlinda mtumishi wake.

Mtumishi wa Yahwe amepewa kusudi gani kama agano kwa watu?

Amepewa kama agano kwa ajili ya watu kujenga tena nchi, kugawa tena urithi ulioachwa.

Isaiah 49:10-11

Nani atawaongoza wafungwa?

Yule ambaye ana huruma kwa wafungwa atawaongoza.

Isaiah 49:12-13

Kwa nini mbingu, dunia na milima zinapaswa kuimba na kuwa na furaha?

Vinapaswa kuimba na kuwa na shangwe kwa sababu Yahwe hufariji watu wake, na atakuwa na huruma juu ya walioteswa.

Isaiah 49:14-15

Jibu la Yahwe kwa Sayuni lilikuwa lipi walipolalamika; "Yahwe ameniacha, na Bwana amenisahau?"

Jibu la Yahwe kwa Sayuni lilikuwa, "Je! mwanamke husahau mtoto wake, anayenyonya katika titi lake, kwa hiyo hana huruma juu ya mwanawe aliyemzaa? Ndio, wanaweza kusahau, lakini sitakusahau.

Isaiah 49:16-18

Yahwe anatoa nini kama kithibitisho cha kujishughulisha kwake kwa ajili ya Sayuni?

Yahwe anasema ushahidi wake ni huu: "Tazama, nimeandika jina lako katika viganja vyangu; kuta zako daima zipo mbele yangu. Watoto wako wanaharikisha kurudi, wakati wale ambao walikuangamiza wanaondoka. Tazama pembeni na uone, wote wanakusanyika na kuja kwako.

Isaiah 49:19-20

Watoto waliozaliwa katika kipindi cha unyanganyi wa Sayuni wanasemaje?

Watasema, "Sehemu imebanana mno kwa ajili yetu, tengeneza nafasi kwa ajili yetu, ili tuweze kuishi hapa.

Isaiah 49:21

Sayuni atajiulizaje?

Atauliza, "Nani amezaa watoto hawa kwa ajili yangu?" na "Nani amekuza watoto hawa?" na mwishoni, "... hawa wametoka wapi?"

Isaiah 49:22-23

Nani atawarudisha wana wa Sayuni na binti zake?

Watu wa mataifa watawarudisha.

Isaiah 49:24-25

Je! mali ya kuibiwa inaweza kuondolewa kutoka kwa hodari au mateka kuokolewa kutoka kwa mtawala katili?

Ndio, mateka watachukulia ktoka kwa hodari na mali ya kuibiwa itaokolewa; kwa kuw Yahwe atazuia wapinzani wa Sayuni na kuokoa watoto wake.

Isaiah 49:26

Yahwe atafanya nini kwa wakandamizaji wa Sayuni?

Atawalisha wakandamizaji wao kwa nyama yao wenyewe.

Binadamu wote watajua nini?

Watajua ya kuwa Yahwe ni mwokozi wa Sayuni na mkombozi, mwenye uwezo wa Yakobo.

Isaiah 50

Isaiah 50:1

Kwa nini Sayuni aliuzwa na mama yake kufukuzwa?

Sayuni aliuzwa kwa sababu ya dhambi zake, kwa sababu ya uasi wake, mama yake alifukuzwa.

Isaiah 50:2-3

Nini hutokea kwa karipio la Yahwe?

Kwa karipio la Yahwe bahari hukauka na hufanya mito kuwa jangwa. Yahwe huvisha anga na giza na kuifunika na nguo ya gunia.

Isaiah 50:4

Yahwe ametoa nini kwa mtumishi wake?

Amempatia mtumishi wake ulimi kama wale ambao walifundisha.

Mtumishi wa Yahwe alifanya nini na ulimi aliopewa na Yahwe?

Mtumishi wa Yahwe alizungumza neno la kuendeleza kwa aliyechoka.

Isaiah 50:5-6

Kwa kuwa hakuwa muasi na hakugeuka mabli, mtumishi wa Yahwe alifanya nini?

Mtumishi wa Yahwe alrudisha kwa wale ambao walimpiga na mashavu yake kwa wale ambao walinyofoa ndevu zake; Hakuficha uso wake kutoka matendo ya aibu na kutemewa.

Isaiah 50:7

Kwa nini mtumishi wa Yahwe anasema hakuaibika?

Mtumishi anasema hakuaibika kwa sababu Bwana Yahwe atamsaidia.

Isaiah 50:8-9

Nini kitatokea kwa wale ambao humshtaki mtumishi wa Yahwe na kumtamka kuwa na hatia?

Washtaki wake wote watachakaa kama mavazi; nondo itawala.

Isaiah 50:10

Yule ambaye humhofu Yahwe, ambaye hutii sauti ya mtumishi wake na yule ambaye hutembea katika giza zito bila mwanga, hufanya nini?

Anatakiwa kuamini katika jina la Yahwe na kuegemea kwa Mungu wake.

Isaiah 50:11

Mtumishi wa Yahwe atafanya nini kwa wale wanaoamsha moto, ambao huvaa miale?

Mtumishi wa Yahwe atawasababisha kulala chini katika sehemu ya maumivu.

Isaiah 51

Isaiah 51:1

Yahwe alisema nini kwa wale ambao huwakimbiza wenye haki kutazama nini?

Yahwe alisema kutazama mwamba kutoka pale walipochongwa na kwa machimbo ambapo walikatwa.

Isaiah 51:2-5

Yahwe alifanya nini kwa Abrahamu?

Yahwe alimwita, akambariki na kumfanya kuwa wengi.

Isaiah 51:6

Nini kitatokea kwa mbingu, dunia na wakazi wake?

Mbingu zitatoweka kama moshi, dunia itachakaa kama nguo; na wakazi wake watakufa kama nzi.

Nini kitaendelea milele na kutosimama kufanya kazi?

Haki ya Yahwe itaendelea milele na haki yake haitasimama kufanya kazi.

Isaiah 51:7-8

Kauli inaelekezwa kwa nani: "Usiogope fedheha ya watu, wala kuvunjwa moyo kwa matusi yao ... "?

Kauli hiyo inaelekezwa kwa wale ambao wanajua kilicho sahihi na watu ambao wana sheria ya Yahwe moyoni mwao.

Isaiah 51:9-10

Nani aliponda jitu la bahari, kukausha bahari na kufanya vilindi vya bahari kuwa njia kwa waliiokombolewa kupita katikati?

Mkono wa Yahwe ulifanya mambo haya.

Isaiah 51:11-13

Nini kitapita na nini kitatoroka mbali kutoka kwa waliolipiwa wa Yahwe watakaporudi na kuja Sayuni?

Furaha itawapita na huzuni na majonzi itatoroka mbali.

Isaiah 51:14-16

Yahwe atafanya nini kwa yule ambaye ameinama chini?

Yahwe ataharakisha kumfungua.

Isaiah 51:17-22

Yerusalemu ilikunywa nini kutoka mkononi mwa Yahwe?

Walikunywa kikombe cha hasira ya Yahwe; waliunywa bakuli, kikombe cha kupepesuka.

Nani kati ya wana wa Yerusalemu alizaliwa kumwongoza yeye?

Hakuna mtu miongoni mwa wana wote aliowazaa wa kumwongoza.

Isaiah 51:23

Baada ya Yahwe kuondoa kikombe cha kupepesuka kwa Yerusalemu atampatia nani?

Atakiweka katika mkono wa wasumbufu wa Yerusalemu.

Isaiah 52

Isaiah 52:1-3

Nini hakitatokea tena kwa Yerusalemu?

Hakuna tena ambao hawajatahiriwa au wachafu wataingia Yerusalemu.

Isaiah 52:4

Nani alimkandamiza Yerusalemu hivi karibuni?

Ashuru alimkandamiza hivi karibuni.

Isaiah 52:5-6

Katika siku hiyo kwa nini watu wa Yahwe watajua jina la Yahwe?

Watajua jina la Yahwe kwa sababu jina lake linakashfiwa daima siku nzima.

Isaiah 52:7-8

Nani ataona kurudi kwa Yahwe Sayuni?

Kila jicho la walinzi wa Sayuni litaona kurudi kwa Yahwe Sayuni.

Isaiah 52:9-10

Kwa nini uharibifu wa Yerusalemu utavunjwa mbele kwa uimbaji wa shangwe pamoja?

Wanapaswa kufanya hivi kwa sababu Yahwe amewafariji watu wake; amekomboa Yerusalemu. Yahwe amefunua mkono wake mtakatifu katika macho ya mataifa yote.

Isaiah 52:11-12

Wale ambao hubeba vyombo vya Yahwe wanapaswa kufanya nini?

Wanatakiwa kuondoka, kutogusa chochote kichafu na kujitakasa.

Kwa nini watu wa Yahwe hawahitaji kuwa na haraka au wasiwasi watakapoondoka?

Hawahitaji kuwa na haraka au wasiwasi kwa sababu Yahwe atakwenda mbele yao na Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi wao wa nyuma.

Isaiah 52:13-14

Mtumishi wa Yahwe atafanya nini?

Atatenda kwa hekima na kuwa na mafanikio; atainuliwa na kutukuzwa juu, na atainuliwa sana.

Nini kilitokea kwa muonekano wa mtumishi wa Yahwe?

Muonekano wako uliharibiwa kutoka kwa muonekano wa kibinadamu.

Isaiah 52:15

Wafalme watafanya nini kwa sabau wa mtumishi wa Yahwe?

Wafalme watafunga midomo yao kwa sababu yake.

Isaiah 53

Isaiah 53:1-2

Mtumishi wa Yahwe alikuaje?

Alikuwa mbela ya Yahwe kama asiye na nguvu, na kama chipuko katika ardhi iliyokauka.

Mtumishi wa Yahwe alionekanaje?

Hakuwa na muonekano wa ajabu au ufahari; tulipomwona, hapakuwa na uzuri kutuvutia kwake.

Isaiah 53:3

Mtumishi wa Yahwe alipokelewaje na watu?

Alidharauliwa na kukataliwa na watu na kuchukuliwa kutokuwa na maana.

Isaiah 53:4

Mtumishi wa Yahwe alifanya nini kwa ajili yetu?

Alichukua ugonjwa wetu na kubeba majonzi yetu.

Isaiah 53:5

Kwa nini mtumishi wa Yahwe alichomwa na kupondwa?

Alichomwa kwa ajili ya matendo yetu ya uasi na kupondwa kwa sababu ya dhambi zetu.

Adhabu ya mtumishi na vidonda vyake vilifanya nini kwa ajili yetu?

Adhabu yake ilituletea amani na vidonda vyake vilituponya.

Isaiah 53:6-7

Je! sisi tunakuaje kama kondoo?

Tuko kama kondoo kwa sababu wote tumepotoka njia; kila mmoja wetu njia yake mwenyewe.

Isaiah 53:8-9

Njia gani zilitumika kumshutumu mtumishi wa Yahwe?

Uonevu na hukumu zilikuwa njia zilizotumika kumshutumu.

Kwa nini mtumishi wa Yahwe alikatwa katika nchi ya walio hai?

Alikatwa kwa sababu ya makosa ya watu wake.

Je! mtumishi wa Yahwe alifanya kosa lolote?

Hapana. Hakuwa amefanya vurugu yoyote wala hapakuwa na udanganyifu katika mdomo wake.

Isaiah 53:10-11

Kwa nini yalikuwa mapenzi ya Yahwe kumponda mtumishi wake?

Yalikuwa mapenzi ya Yahwe ili kwamba kusudi la Yahwe liweze kukamilishwa kupitia yeye.

Isaiah 53:12

Kwa nini Yahwe atampa mtumishi wake fungu lake katika kundi?

Yahwe atampa mtumishi wake fungu lake kwa sababu alimwaga nje nafsi yake hadi kifo na kuhesabiwa na wakosaji. Alichukua dhambi za wengi na kuwaombea makosa.

Isaiah 54

Isaiah 54:1

Kwa nini Yahwe anasema mwanamke tasa anapaswa kuimba?

Anasema anapaswa kuimba, kwa kuwa watoto wa walioachwa ni wengi kuliko watoto wa mwanamke aliyeolewa.

Isaiah 54:2-4

Vizazi vya Sayuni vitafanya nini?

Watashinda mataifa na kukaa tena miji iliyoachwa.

Isaiah 54:5-6

Mume wa Sayuni ni nani?

Yahwe wa Majeshi, muumba waSayuni, ni mume wao.

Isaiah 54:7-8

Yahwe alifanya nini kwa Israeli?

Alimtelekeza kwa muda mfupi.

Yahwe atafanya nini kwa ajili ya Israeli?

Kwa huruma kuu Yahwe atawakusanya.

Isaiah 54:9-12

Yahwe aliapa nini kuhusu Israeli?

Aliapa hatakuwa na hasira tena nao au kuwakaripia.

Nini hakitatikiswa na nini hakitatoweka kutoka Israeli?

Agano la Yahwe la amani na Israeli halitatikiiswa na agano lake aminifu halitaondoka kutoka Israeli.

Isaiah 54:13-14

Israeli hatapitia kitu gani tena?

Israeli hatapitia tena mateso.

Isaiah 54:15-16

Nini kitatokea kwa yeyote ambaye ataanzisha shida kwa Israeli?

Yeyote ambaye ataanzisha shida kwa ajili ya Israeli ataanguka katika kushindwa.

Isaiah 54:17

Nini kitatokea kwa kila mmoja ambaye atamshtaki Israeli?

Israeli atawashutumu .

Isaiah 55

Isaiah 55:1

Wale ambao hawana pesa wanaambiwa kununua nini?

Wanaambiwa kununua divai na maziwa bila pesa na bila gharama.

Isaiah 55:2

Wale wenye kiu wanaambiwa kula nini?

Wanaambiwa kula kilicho kizuri.

Isaiah 55:3-4

Yahwe amemweka nani kama shahidi kwa mataifa na kiongozi na kamanda kwa watu?

Yahwe amemweka Daudi katika nafsi hiyo

Isaiah 55:5

Kwa nini taifa ambalo halikumjua Israeli litakimbia kwao?

Watakimbia kwa Israeli kwa sababu Yahwe Mungu wao, Mtakatifu wa sraeli amewainua.

Isaiah 55:6-7

Israeli anatakiwa kumtafuta na kumuita Yahwe wakati gani?

Wanapaswa kumtafuta wakati anaweza kupatikana; kumuita wakati yupo karibu.

Waovu na mtu mwenye dhambi anatakiwa kufanya nini?

Acha mwovu aache njia yake, na mtu wa dhambi mawazo yake.

Yahwe atafanya nini kwa yule anayerudi kwake?

Yahwe atamhurumia na atasheni kumsamehe

Isaiah 55:8-9

Kwa nini mawazo na njia za Yahwe sio mawazo n njia za Israeli?

Hii ni kwa sababu kama vile mbingu ziko juu kuliko dunia vile vile njia za Yahwe zipo juu kulko nji zao na mawazo ya Yahwe kuliko mawazo ya Waisraeli.

Isaiah 55:10-11

Nini kitatokea kwa maneno ambayo yatatoka mdomoni mwa Yahwe?

Yatatimiza kile ambacho Yahwe anatamani na yatafanikiwa kwa lile ambalo lilitumwa.

Isaiah 55:12-13

Ishara ya milele ambayo haitakatwa ni ipi?

Hii ni ishara: Israeli itatoka nje kwa furaha na kuongozwa kwa amani. Milima na vilima vitavunjika kwa kelele za furaha mbele zao. Miti yote ya mashamba itapiga makofi mikono. Badala ya vichaka vya miiba, ukijani usiokauka utaota na badala ya mibigli, mti wa mhadasi utaota.

Isaiah 56

Isaiah 56:1-2

Yahwe alisema nini kufuata kilicho sahihi na kufanya kilicho haki?

Alisema hivi kwa sababu ukombozi wake umekaribia na uthibitisho wake umekaribia kufunuliwa.

Isaiah 56:3

Mgeni na towashi ambao wamekuwa wafuasi wa Yahwe hawapaswi kusema nini?

Mgeni hapaswi kusema, "Yahwe hakika atanitenga mimi kutoka kwa watu wake" na towashi hatakiwi kusema, 'Tazama, mimi ni mti mkavu".

Isaiah 56:4-5

Yahwe atafanya nini kwa matowashi ambao hufuata sabato ya Yahwe, wanaochagua kile kinachompendeza yeye, na kushika sana agano la Yahwe?

Yahwe ataweka mnara kwake, katika nyumba ya Yahwe na ndani ya kuta zake, ambao ni bora kuliko wana na binti.

Isaiah 56:6-8

Yahwe atafanya nini kwa wageni wanaoungana kwa Yahwe kumtumikia, ambao humwabudu na kupenda jina lake, ambao hufuata sabato na kushikilia bila kuinajisi, na ambao hushika sana agano la Yahwe?

Yahwe atawaleta katika mlima wake mtakatifu na kuwafanya kuwa na furaha katika nyumba yake ya maombi; sadaka zao za kuteketeza zitakubalika juu ya mahbahu ya Yahwe.

Isaiah 56:9-10

Ni nani analinganishwa na mbwa bubu?

Walinzi wao wanalinganishwa na mbwa bubu.

Isaiah 56:11-12

Walinzi wao na wachungaji wamefanya nini?

Wote waligeuka kwa njia yao wenyewe, kila mmoja na tamaa kwa kipato kisicho haki.

Isaiah 57

Isaiah 57:1-2

Ni nini mtu huchukulia au kuelewa kuhusu wenye haki wanapotoweka?

Hawafikirii au kuelewa ya kwamba wenye haki wanakusanywa kutoka kwa uovu na kuingia katika amani.

Isaiah 57:3-4

Nani anadhihaki kwa furaha na kufungua mdomo na kutoa ulimi nje?

Wana wa wachawi wa kike, watoto wa wazinzi na mwanamke aliyekuwa kahaba wa haya mambo.

Isaiah 57:5

Jambo gani lingine hawa walioitwa watoto wa waasi na watoto wa waongo walifanya?

Walifanya ngono chini ya mwaloni, chini kila mti wa kijani. Waliwaua watoto wao katika kando ya mito iliyokauka, chini ya miamba ilitokeza juu.

Isaiah 57:6

Jambo la mapenzi yao ni lipi?

Baadhi ya vitu vilaini vya mto wa bonde ni jambo la mapenzi yao.

Isaiah 57:7-12

Hawa waasi na wadanganyifu walifanya nini kuhusu Yahwe?

Walimuacha Yahwe.

Isaiah 57:13

Yahwe atawaambia nini hawa waovu na waasi watakapolia?

Yahwe atawaambia kuacha makusanyo yao ya sanamu yawakomboe.

Nini kitatokea kwa hawa waovu na waasi?

Upepo utawabeba mbali, pumzi iitawabeba mbali.

Nini kitatokea kwa wale ambao huchukua kimbilio katika Yahwe?

Watarithi nchi na kumiliki mlima mtakatifu wa Yahwe.

Isaiah 57:14-15

Nani ataishi na Yahwe katika sehemu iliyo juu na takatifu?

Wale ambao wamepondeka na wanyenyekevu rohoni wataishi na Yahwe kule.

Isaiah 57:16-17

Nini kitatokea kama Yahwe atamshtaki mtu milele?

Roho ya mtu ingezimia mbele ya Yahwe.

Kwa nini Yahwe alimkasirikia mtu?

Yahwe alikuwa na hasira na mtu kwa sababu ya ongezeko lake la vurugu.

Isaiah 57:18-19

Ingawa Yahwe kaona njia ya mtu, Yahwe anaenda kufanya nini kwa ajili ya mtu?

Yahwe alisema atamponya.

Isaiah 57:20-21

Nani hana amani?

Mtu mwovu hana amani

Isaiah 58

Isaiah 58:1-2

Yahwe aliamuru nyumba ya Yakobo wafarijike na nini?

Aliamuru nyumba ya Yakobo kufarijiwa na uasi na dhambi zao.

Kwa nini nyumba ya Yakobo ilimtafuta Yakobo?

Walimtafuta kama taifa ambalo lilitenda haki na halikutelekeza sheria ya Mungu wao.

Isaiah 58:3

Ni lalamiko gani la nyumba ya Yakobo walilofanya kwa Yahwe kuhusu wao kujishusha na kufunga?

Lalamiko lao kwa Yahwe lilikuwa kwamba walipofunga na kujishusha Yahwe hakuona au kugundua.

Yahwe alisema nyumba ya Yakobo ilifanya nini katika siku ya kufunga kwo?

Yahwe alisema ya kwamba katika siku ya kufunga kwao wanatafuta starehe yao wenyewe na kukandamiza watumishi wao wote.

Isaiah 58:4-5

Yahwe alisema sababu ni ipi ya nyumba ya Yakobo kufunga?

Yahwe alisema nyumba ya Yakobo haikuwa inafunga kufanya sauti yao kusikika juu.

Isaiah 58:6-8

Ni kufunga kwa aina gani Yahwe huchagua?

Kufunga ambako Yahwe huchagua ni kuacha kamba za kiovu, kuachia kamba za nira, kuwaachi waliopondwa huru, kuvunja kila nira, kuvunja mkate wao na wenye njaa, kuleta maskini na wasio na nyumba katika nyumba zao, kuvisha walio uchi na kutojificha kwa ndugu zao wenyewe.

Isaiah 58:9-14

Yahwe angefanya nini kama nyumba ya Yakobo ingeondoa kutoka miongoni mwao nira, kidole cha kushtaki, maneno ya uovu, kama watatoa kwa ajili ya wenye njaa na kutosheleza hitaji la walioteseka?

Kama wangefanya vitu hiv basi mwanga wao ungeinuka katika giza, na giza lao litakuwa kama mchana.

Isaiah 59

Isaiah 59:1-2

Je! Yahwe anaweza kutuokoa? Anatusikia?

Mkono wa Yahwe sio mfupi sana mpaka ishindwe kuokoa; wala sikio lake kufifia sana, mpaka lishindwe kusikia.

Kwa nini Yahwe hakusikia au kuokoa nyumba ya Yakobo?

Matendo yao ya dhambi yaliwatenga na Mungu wao na dhambi zao zilimfanya Yahwe kuficha uso wake kutoka kwao na kutowasikia.

Isaiah 59:3-6

Ni zipi baadhi ya dhambi za nyumba ya Yakobo walizofanya ambazo ziliwatenga na Yahwe?

Baadhi ya dhambi ambazo ziliwatenga na Yahwe zilikuwa: Walichafua mikono yao kwa damu. Walidanganya na kuongea kwa hila. Walikuwa na hila na waongo. Walitunga shida.

Isaiah 59:7-13

Nini hutokea kwa wale ambao husafiri katika njia zilizopinda?

Wale ambao husafiri katika njia zilizopinda hawajui amani.

Isaiah 59:14-15

Nini kilitokea kwa yule ambaye aligeuka kutoka kwa uovu?

Alijifanya mwenyewe kuwa mhanga.

Nini hakikumfurahisha Yahwe?

Haikumfurahisha Yahwe alipoona hapakuwa na haki.

Isaiah 59:16

Yahwe alifanya nini alipoona hapakuwa na mtu wa kuingilia kati?

Yahwe alipoona hapakuwa na mtu wa kuingilia kati, mkono wake mwenyewe ukalet wokovu kwa ajili yake.

Isaiah 59:17-18

Kisha Yahwe alifanya nini?

Alivaa haki kama deraya ya kifua na kofia ya chuma ya wokovu juu ya kichwa chake. Alijivika mavazi ya kisasi na kuvaa ari kama joho. Aliwalipiza wote kwa yale waliyoyafanya, hukumu ya hasira kwa wapinzani wake, kisasi kwa adui zake, kwa visiwa adhabu kama zawadi yao.

Isaiah 59:19-20

Matokeo ya Yahawe kuwalipiza kwa yale waliyofanya ni yapi?

Wataogopa jina la Yahwe kutoka magharibi, na utukufu wake kutoka kwa kuchomoza kwa jua.

Mkombozi atakuja kwa nani?

Mkombozi atakuja Sayuni na wale ambao hugeuka kutoka kwa matendo yao ya uasi wa Yakobo.

Isaiah 59:21

Agano la Yahwe pamoja nao ni lipi?

Hili ndilo agano: Roho wa Yahwe ambaye yupo ju yako, na maneno yangu ambayo nimeyaweka katika mdomo wako, hayataondoka mdomoni mwako, au kutoka katika midomo ya watoto wako, au kutoka katika midomo ya watoto wa watoto wako kutoka kipindi hiki na milele.

Isaiah 60

Isaiah 60:2-3

Ingawa gza litafunika dunia, Yahwe atafanya nini kwa ajili ya Israeli?

Yahwe atainuka juu yao na utukufu wake utaonekna juu yao.

Nani atakuja kwa mwanga wa Israeli?

Mataifa na wafalme watakuja katika mwanga wao.

Isaiah 60:4-7

Kwa nini Israeli ataonekana na kung'aa na moyo wao kufurahi na kumwagikia?

Hii itakuwa kwa sababu wingi wa bahari itamwagwa kwao, na utajiri wa mataifa utakuja kwao.

Isaiah 60:8-9

Ni nani huongoza kuwaleta wana wa Israeli kutoka mbali?

Meli za Tarshishi huongoza.

Isaiah 60:10-11

Nani atajenga tena mji wa Yahwe na nani atawatumikia?

Wana wa wageni watajenga tena kuta zao na wafalme watawatumikia.

Kwa nini malango ya mji yatabaki wazi daima?

Watabaki wazi ili kwamba utajiri wa mataifa ziweze kuletwa ndani.

Isaiah 60:12-14

Nini kitatokea kwa mataifa yale na falme ambazo hawatawatumikia?

Mataifa na falme yale ambayo yatatoweka; yataangamizwa kabisa.

Isaiah 60:15-16

Yahwe atafanya nini kwa mji wa Yahwe kuwa?

Atamfanya kuwa kitu cha sifa milele, furaha kutoka kizazi mpaka kizazi.

Isaiah 60:17-18

Nini hakitasikika tena katika nchi ya Sayuni?

Vurugu haitasikika katika nchi yao, au uharibifu wala kupondwapondwa katikati ya mipaka yao.

Isaiah 60:19-20

Nini kitatoa mwanga kwa nchi?

Yahwe atakuwa mwanga wao milele.

Isaiah 60:21-22

Watu wa Yahwe watamiliki nchi kwa muda gani?

Watamiliki nchi kwa muda wote.

Yahwe atatimiza vitu hivi kwa muda gani?

Yahwe atatimiza haraka vitu hivi muda utakapowadia.

Isaiah 61

Isaiah 61:1-3

Kwa nini Roho wa Bwana Yahwe yupo juu yake?

Roho yupo juu yake kwa sababu Yahwe amemtia mafuta.

Yahwe amemtia mafuta kufanya nini?

Yahwe amemtia mafuta kutangaza habari njema kwa wanyenyekevu

Mambo gani ya kwanza matatu Yahwe amemtuma kuyafanya?

Yahwe alimtuma kuponya waliovunjika moyo, kutangaza uhuru kwa wafungwa, kufungua magereza kwa wale ambao wamefungwa.

Isaiah 61:4-5

Wageni watafanya nini Sayuni?

Watasimama na kula makundi ya wale wa Sayuni na wana wa wageni watafanya kazi katika mashamba yao na mashamba ya mizabibu.

Isaiah 61:6-7

Wale wa Sayuni wataitwa kina nani?

Wataitwa makuhani wa Yahwe; watumishi wa Mungu.

Isaiah 61:8-9

Yahwe anapenda nini na anachukia nini?

Yahwe anapenda haki na anachukia uporaji na udhalimu wa vurugu.

Isaiah 61:10-11

Yahwe amefanya nini kwa ajili yake?

Yahwe amemvisha na mavazi ya wokovu na joho la haki.

Bwana Yahwe atasababisha kitu gani kuchipua juu mbele ya mataifa yote?

Atasababisha haki na sifa kuchipua juu mbela ya mataifa yote.

Isaiah 62

Isaiah 62:1-2

Nani ataona haki na utukufu wa Sayuni?

Mataifa yataona haki ya Sayuni na wafalme wote wataona utukufu wake.

Isaiah 62:3-5

Nini hakitasemwa tena kuhusu Sayuni na nchi yake?

Sayuni haitaitwa tena "Aliyetelekezwa" na nchi yake haitajulikana tena "Yenye ukiwa"

Kwa nini Sayuni itaitwa "Furaha yangu ipo kwake" na nchi ya Sayuni "Imeolewa"?

Ataitwa vitu hivyo kwa sababu Yahwe anafurahia nayo na nchi yake itaolewa.

Isaiah 62:6-7

Kwa nini walinzi wamewekwa juu ya kuta za Yerusalemu?

Wamewekwa pale kuendelea kumkumbusha Yahwe, kumruhusu asipumzike hadi aimarishe tena Yerusalemu na kuifanya sifa ya dunia.

Isaiah 62:8-10

Yahwe ameapa nini kwa mkono wake wa kulia na kwa mkono wa nguvu yake?

Ameapa ya kwamba hatawapa tena nafaka ya Yerusalemu kama chakula adui zake, na wageni hawatakunywa divai yao mpya.

Isaiah 62:11-12

Yahwe anatangaza nini kwa mwisho wa dunia?

Hili ni tangazo la Yahwe. "Sema kwa binti wa Sayuni, 'Tazama, mkombozi wako anakuja! Tazama, dhawabu yake ipo naye, na dhawabu yake huenda mbele zake".

Isaiah 63

Isaiah 63:1-2

Anayekuja kutoka Edomu alikuwa akivaa nini na alikuwa akija kwa namna gani?

Anavaa nguo ya kifalme nyekundu na anakuja akitembea kwa kujiamini.

Kwa nini yule wa Edomu alikuwa akitembea kwa kujiamini sana?

Anatembea kwa kujiamini kwa sababu ya nguvu yake kubwa.

Huyu kutoka Edomu anasema nini juu yake mwenyewe?

Anasema anazungumza haki na kwamba anaweza kwa nguvu kuokoa.

Isaiah 63:3-4

Huyu kutoka Edomu alikuwa akitazamia kitu gani?

Alikuwa akitazamiia sik ya kisasi, na mwaka wa ukombozi kuwadia.

Isaiah 63:5-6

Je! kulikuwa na yeyote kule kumsaidia huyu kutoka kwa Edomu?

Hapana. Alitafuta lakini hapakuwa na mtu wa kusaidia.

Ni nini huyu kutoka Edomu alichofanya kwa watu?

Aliwakanyaga chini watu katika hasira yake na kuwafanya kulewa katika ghadhabu yake na kuwamwagia damu yao juu ya dunia.

Isaiah 63:7-8

Kwa nini na kwa namna gani Yahwe ameonyesha huruma kwa nyumba ya Israeli?

Amewaonyesha huruma kwa sababu ya rehema zake pamoja na matendo mengi ya agano la uaminifu.

Isaiah 63:9

Nini kilitokea nyakati za zamnai pale watu wa Yahwe walipoteseka?

Nyumba ya Israeli ilipoteseka, Yahwe aliteseka.

Katika nyakati za zamani, nani aliokoa Israeli?

Mjumbe wa uwepo wake aliwaokoa katika nyakati za zamani.

Isaiah 63:10-14

Kwa alikuja kuwa adui zao?

Alikuwa adui zao kwa sababu waliasi na kumhuzunisha Roho Mtakatifu wake.

Isaiah 63:15-16

Jina la Yahwe lilikuwa lipii tangu zamani?

Jina lake toka zamani lilikuwa "Mkombozi Wetu".

Isaiah 63:17-19

Kulikuwa na lalamiko gani au swali la nyumba ya Israeli kwa Yahwe?

Swali lao na lalamiko lilikuwa, "Yahwe, kwa nini unatufanya tutangetange kutoka katika njia zetu, na kufanya mioyo yetu migumu, ili tusikutii?

Isaiah 64

Isaiah 64:1-2

Nini kingetokea iwapo jina la Yahwe lingejulikana na wapinzani wake?

Mataifa wangetetemeka kwa uwepo wake.

Isaiah 64:3-5

Tangu nyakati za zamani kuna mtu aliyesikia au kutambua Mungu yeyote kando na Yahwe, ambaye hufanya mambo haya kwa wale ambao wanamsubiri yeye?

Hapana, hakuna aliyesikia au kutambua Mungu yeyote ambaye hufanya mambo haya kwa wale ambao humsubiri yeye.

Isaiah 64:6-7

Matendo yote ya haki ya Israeli ni kama nini?

Ni kama kitambaa cha hedhi.

Kwa nini hapakuwa na mtu wa kuliita jina la Yahwe, ambaye alifanya juhudi kumpata?

Hii ilikuwa kwa sababu Yahwe alificha uso wake kutoka kwao na kuwakabidhi kwa dhambi zao.

Isaiah 64:8-9

Mwandishi anamlinganisha Yahwe na watu wa Israeli na nini?

Yahwe analinganishwa na mfinyanzi na watu wa Israeli wanalinganishwa na udongo.

Isaiah 64:10-12

Miji mitakatifu ya Yahwe imekuje?

Miji mitakatifu ya Yahwe imekuwa nyika na Yerusalemu sehemu ya ukiwa.

Mwandishi ana maswali yapi mawili kwa ajili ya Yahwe?

Maswali mawili ni, "Unawezaje kujizuia bado, Yahwe?" na "Unawezaje kukaa kimya na kuendelea kutuaibisha?"

Isaiah 65

Isaiah 65:1-2

Yahwe alitaka nini kutoka kwa wale ambao hawakuuliza na hawakutafuta?

Alitaka kutafutwa na kupatwa kwa wale ambao hawakuuliza na hawakutafuta.

Watu hawa wasumbufu walitembea kufuata nini?

Wametembea kufuata mawazo na mipango yao wenyewe.

Isaiah 65:3-5

Baadhi ya njia ambazo watu hawa zilizokuwa makosa yanayoendelea kwa Yahwe ni zipi?

Wanaendelea kuwa na makosa kwa Yahwe kwa sababu wanatoa sadaka katika bustani na kuchoma ubani katika vigae vya tofali. Wanakaa miongoni mwa makaburi na kulinda usiku kucha na kula nguruwe pamoja na mchuzi wa nyama mbaya katika sahani zao.

Isaiah 65:6-8

Yahwe alifanya nini na atafanya nini kwa watu hawa wasumbufu?

Amewalipa na atawalipa kwa dhambi zo wenyewe na dhambi za baba zao.

Isaiah 65:9-11

Yahwe atafanya nini kwa wateule wake?

Watamiliki nchi.

Isaiah 65:12

Yahwe atafanya nini kwa wale wanaomtelekeza Yahwe?

Atawakusudia kwa upanga na wote watainama chinii kwa machinjio.

Isaiah 65:13-16

Nini kitatokea kwa watumishi wa Yahwe?

Watakula, kunywa, kushangilia na kupiga kelele na furaha.

Kitu gani kingine kitatokea kwa wale ambao humtelekeza Yahwe?

Watakuwa na njaa na kiu. Wataaibishwa na kulia kwa sababu ya maumivu ya moyo na kulia kwa sababu ya kupondwa kwa roho.

Isaiah 65:17-19

Yahwe anakwenda kuumba nini?

Yahwe anakwenda kuumba mbingu mpya na dunia mpya.

Nini litakuwa jibu la watumishi wa Yahwe kwa mbingu mpya na dunia mpya?

Watakuwa na furaha na shangwe milele kwa kile ambacho Yahwe anataka kuumba.

Isaiah 65:20-21

Watu watafanya nini katika Yerusalemu mpya?

Watajenga nyumba na kuzikaa, na watapanda shamba za mizabbu na kula matunda yao.

Isaiah 65:22-23

Watu wataishi siku ngapi?

Wataishi maisha marefu kama siku za miti.

Isaiah 65:24-25

Katika mbingu mpya na dunia mpya Yahwe atasikia na kujibu watu wake wakati gani?

Wakati bado wanazungumza Yahwe atawasikia, na kabla hawajamwta atawajibu.

Nini kitakuwa tofauti kuhusu wanyama katika milima yote mitakatifu ya Yahwe?

Wanyama hawataumia tena au kujiangamiza wao kwa wao. Mbwa mwitu na kondoo watalisha pamoja, na simba atakula nyasi kama ng'ombe.

Isaiah 66

Isaiah 66:2

Nani alitengeneza mbingu na nchi?

Yahwe alitengeneza vitu vyote kwa mkono wake.

Yahwe anakubali aina gani ya mtu?

Yahwe anakubali watu ambao wamevunjika na kupondeka rohoni na kutetemeka katika neno lake.

Isaiah 66:3-4

Mifano gani Isaya anatoa kuonyesha unafiki wa mtu?

Yahwe anasema mtu anayechinja ng'ombe pia huua mtu. Yule anayetoa sadaka ya kondoo dume pia huvunja shingo ya mbwa. Yule anayetoa sadaka ya nafaka hutoa damu ya nguruwe na yule anayetoa kumbukumbu ya ubani pia alibariki uovu.

Isaiah 66:5

Kaka wa wale ambao hutetemekea neno la Yahwe huwafanya nini wao?

Kaka zao huchukia na kuwatenga wale ambao hutetemekea neno la Yahwe.

Isaiah 66:6-9

Ni sauti gani ilitoka katika mji na hekalu?

Ilikuwa sauti ya ghasia ya vita iliyotoka kwenye mji, sauti ya Yahwe akiwalipa adui zake.

Isaiah 66:10-11

Kwa nini wote wanaopenda Yerusalemu wanatakiwa kushangilia pamoja naye na kumfurahia yeye?

Tunatakiwa kushangilia na Yerusalemu na kuwa na furaha kwa ajili yake, kwa maana utanyonya na kutosheka; kwa matiti yake utafarijiwa; kwa kuwa utakunywa kwa ujazo na kufurahia wingi wa utukufu wake.

Isaiah 66:12-14

Yahwe anataka kutandaza nini juu ya Yerusalemu?

Yahwe anataka kutandaza mafanikio juu ya Yerusalemu kama mto, na utajiri wa mataifa kama kijito kilichomwagikia.

Isaiah 66:15-17

Yahwe atatumia nini kutoa hukumu kwa binadamu?

Atatumia moto na upanga wake.

Isaiah 66:18-19

Kwa nini Yahwe atakusanya mataifa yote na lugha?

Yahwe atakusanya mataifa yote na lugha ili zije pamoja na kuona utukufu wake ili kwamba baadhi yao waliopona waweze kurudi kwa mataifa yao kutangaza utukufu wa Yahwe miongoni mwa mataifa.

Isaiah 66:20-21

Nani atatolewa kama sadaka kwa Yahwe?

Kaka wa Israeli kutoka mataifa yote watatolewa kama sadaka kwa Yahwe.

Isaiah 66:22-23

Watu watafanya nini mwezi kwa mwezi na sabato kwa sabato?

Watu wote watakuja na kusujudu chini kwa Yahwe mwezi kwa mwezi na sabato kwa sabato.

Isaiah 66:24

Nini kitatokea kwa maiti za watu ambao waliasi dhidi ya Yahwe?

Funza zitawala na moto utawaangamiza.