Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Exodus

Exodus 1

Exodus 1:1-14

Ni nchi gani ambayo wana wa Israeli walielekea pamoja na Yakobo?

Wana wa Israeli walielekea Misri na Yakobo.

Je, jamii ya Yakobo ambao waliokuwepo ni wangapi?

Wazaliwa wa Yakobo wote walikuwa na watu sabini.

Exodus 1:15-17

Je, ni nini ambayo mfalme wa Misri aliwaeleza wakunga kufanya kama mtoto angekuwa wa kiume?

Mfalme wa Misri aliwaeleza wakunga yakuwa, iwapo mtoto alikuwa wa kiume, angeuliwa.

Ni kwa nini wakunga hawakufanya jinsi mfalme wa Misri alivyowaamuru?

Wakunga walikuwa na hofu ya Mungu, ndiposa hawakufanya jinsi mfalme wa Misri alivyowaamuru.

Exodus 1:18-19

Je, wakunga walisemaje kuhusu jinsi vile wanawake wahibrania walivyokuwa na utofauti na wale wa Misri?

Wakunga walisema wanawake wahibrania walikuwa stadi kabisa, kwani walizaa kwanza, kabla mkunga awajie.

Exodus 1:20-22

Je, Farao aliwaamrisha watu wote kufanyia nini watoto wa kiume?

Farao aliwaamrisha watu wote, "Lazima mtupe kila mtoto wa kiume aliyezaliwa, mtoni"

Exodus 2

Exodus 2:1-2

Je, mwanamke wa nyumba ya Lawi alimficha mwanawe kwa muda kiasi gani?

Mwanamke wa nyumba ya Lawi alimficha mwanawe kwa miezi mitatu.

Exodus 2:3-4

Mwanamke wa nyumba ya Lawi alitumia nini kuizibisha kikapu cha manyasi?

Mwanamke wa nyumba ya Lawi aliliziba kikapu cha manyasi kutumia sifa na lami.

Exodus 2:5-6

Je, bintiye Farao alifanya nini vijakazi wake wakitembea kando ya mto?

Bintiye Farao alishuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakitembea kando ya mto.

Exodus 2:7-8

Ni nani ambaye aliletwa na msichana mdogo ili aje amlee yule mtoto kwa niaba ya binti ya Farao?

Msichana yule alienda akamleta mama mtoto ili amlee mtoto kwa niaba ya binti ya Farao

Exodus 2:9-10

Je ni nani alimpa mtoto, jina Musa?

Binti ya Farao ndiye aliyempa mtoto, jina Musa.

Exodus 2:11-12

Ni wapi Musa aliificha mwili wa Mmisri aliyemuuwa?

Musa alimuuwa Mmisri na kuuficha mwili wake chini ya changarawe.

Exodus 2:13-14

Wakati wahibrania wawili walipokuwa wakipigana, Je, ni nani Musa alimuuliza, "Mbona unampiga jamaa yako?"

Wakati wahibrania wawili walipokuwa wakipigana, Musa alimwambia aliyekuwa na makosa, "Mbona unampiga jamaa yako?"

Exodus 2:15-22

Mbona Farao hakumwua Musa?

Farao alijaribu kumwua Musa lakini Musa alikwepa kutoka kwa Farao akakaa katika nchi ya Midiani.

Ni nani aliyejaribu kuwafukuza binti wa kuhani wa Midiani?

Wachingaji walikuja wakajaribu kuwafukuza binti wa kuhani wa Midiani.

Exodus 2:23-25

Je, ni lini Mungu alilikumbuka agano lake ambalo alilofanya na Ibrahimu, Isaka na Yakobo?

Wakati Mungu alipokisikia kilio chao, alilikumbuka agano lake ambalo alilofanya na Ibrahimu, Isaka na Yakobo?

Exodus 3

Exodus 3:1-3

Je, ni nani alikuwa mkwewe Musa?

Yethro, kuhani wa Midiani, alikuwa mkwewe Musa.

Je, Malaika Wa Bwana alijitokezaje kwake Musa?

Malaika wa Yahweh alijitokeza kwake Musa kama mwali wa moto katika kijiti.

Exodus 3:4-6

Ni nani alimwita Musa kutoka katikati mwa kijiti hicho?

Mungu alimwita Musa kutoka katikati mwa kijiti hicho.

Je, Mbona Mungu alimwambia Musa azivue viatu vyake?

Mungu alisema, "Usikaribie hapa zaidi! Vua viatu vyako miguuni mwako, maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu".

Exodus 3:7-8

Mbona Yahweh alishuka chini?

Yahweh alishuka chini ili awaokoe Waisraeli kutoka kwa mikono ya Wamisri na kuwatoa kutoka nchi hiyo na kuwaleta katika nchi njema, kisha pana, nchi ijaayo maziwa na asali.

Exodus 3:9-10

Mbona Yahweh alimtuma Musa kwa Farao?

Yahweh alimtuma Musa kwa Farao ili kwamba Musa aweze kuwaleta watu wa Yahweh, wana wa Israeli, kutoka Misri.

Exodus 3:11-12

Je, ni nini ambacho kingekuwa ishara kwake Musa ya kwamba Yahweh alikuwa anamtuma?

Ishara kwake Musa ya kwamba Yahweh amemtuma ingekuwa ya kwamba wakati Musa angewatoa wana wa Israeli kutoka Misri, yeye angemwabudu Yahweh katika mlima huo.

Exodus 3:13-15

Wakati wana wa Israeli wangemuuliza Musa Jina lake Mungu, ni nini angepaswa kuwaambia?

Wakati wana wa Israeli wangemuuliza Musa Jina lake Mungu, angewaambia ni, "MIMI NIKO, AMBAYE NIKO."

Exodus 3:16-18

Je, ni muda kiasi gani wana wa Israeli wataenda jangwani ili kwamba wamtolee dhabihu, Bwana Mungu wao?

Wana wa Israeli wataenda safari ya siku tatu jangwani, ili kwamba wamtolee Bwana Mungu wao dhabihu.

Exodus 3:19-22

Mfalme wa Wamisri hangewaachilia wana wa Israeli huru waenende, sharti jambo gani lifanyike?

Mfalme wa Wamisri hangewaachilia wana wa Israeli huru waenende, sharti mkono wake ulazimishwe.

Exodus 4

Exodus 4:1-3

Ni nini iliyokuwa mkononi mwa Musa?

Fimbo ilikuwa mkononi mwa Musa.

Exodus 4:4-31

Je, fimbo ya Musa liligeuka kuwa nini wakati aliitupa chini?

Fimbo ya Musa iligeuka ikawa nyoka wakati aliitupa chini.

Musa alipaswa kuuchukua nyoka kwa njia gani?

Musa alipaswa kuuchukua nyoka kwa mkia wake.