Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Song of Solomon

Song of Solomon 1

Song of Solomon 1:1-4

Nani ni mwandishi wa Wimbo ulio Bora?

Sulemani ni mwandishi wa Wimbo ulio Bora

Kwa ajili ya nini mwanamke mdogo alimuomba mpenzi wake afanye?

Mwanamke mdogo alimuomba mpenzi ambusu kwa mabusu ya mdomoni wake.

Ni nini mwanamke mdogo alisema ni bora kuliko mvinyo?

Mwanamke mdogo alisema upendo wa mpenzi wake ni bora kuliko mvinyo.

Mwanamke mdogo alisema jina la mpenzi wake ni kama nini?

Mwanamke mdogo alisema jina la mpenzi wake ni kama manukato yaeleayo.

Mfalme alimleta wapi mwanamke mdogo?

Mfalme alimleta mwanamke mdogo vyumbani mwake.

Song of Solomon 1:5-6

Ni vipi mwanamke mdogo alielezea ngozi yake?

Mwanamke mdogo alielezea ngozi yake kwamba ni nyeusi lakini yakupendeza kamahema la Kedari, kama mapazia ya Sulemani.

Kwanini hakutaka wanawake wengine kumshangaa?

Hakutaka wanawake wengine kumshangaa kwa sababu ngozi yake imechomeka.

Kaka wa mwanamke mdogo walifanya nini walipokuwa na hasira naye?

Kaka wa mwanamke mdogo walimfanya mtunzi wa shamba la mizabibu.

Song of Solomon 1:7

Mwanamke alimuuliza nini mpenzi wake?

Alimuuliza wapi analisha mifugo yake na wapi anapumzisha mifugo yake mchana.

Song of Solomon 1:8

Jinsi gani mpenzi wake alisema mwanamke mdogo anaweza kumpata?

Alimwambia afuate nyayo za mifugo yake hadi hema za wachungaji.

Song of Solomon 1:9-11

Kwa lipi mpenzi wa mwanamke mdogo humlinganisha nae?

Anamlinganisha na farasi mzuri wa kike miongoni mwa farasi wa magari ya farao.

Nini mpenzi wake alisema kipo juu ya mashavu yake na shingo yake?

Alisema mapambo yapo mashavuni mwake na mikufu ya madini ipo shingoni mwake.

Nini mpenzi wake alisema atamfanyia?

Alisema atamfanyia mapambo ya dhahabu yaliyochanganywa na fedha.

Song of Solomon 1:12-14

Mfalme alikuwa amelala wapi wakati mwanamke alipokuwa akiongea mwenyewe?

Mflme alikuwa amepumzika kwenye kochi wakati mwanamkealipokuwa akiongea mwenyewe.

Ni wapi mpenzi wake waliyumia usiku wake?

Mpenzi wake aliutumia usiku kulala katikati ya maziwa yake.

Mwanamke mdogo anamfananisha mpenzi wake na nani?

Mpenzi wake anamfananisha kama kifurushi cha maua katika mashamba ya mizabibu yaEni gedi.

Song of Solomon 1:15

Ni vipi mpenzi wakealielezea macho yake

Macho yake ni kama ya hua.

Song of Solomon 1:16-17

Mwanamke anasema nguzo za nyumba yao zimetengenezwa na nini?

Nguzo za nyumba yetu ni za matawi ya mierezi na dar letu ni la matawi ya miberoshi.

Song of Solomon 2

Song of Solomon 2:1-2

Ni vipimwanamke alijielezea mwenyewe?

Alijielezea mwenyewe kama ua katikati ya tambarare, nyinyiro katika bonde.

Ni nini mwanaume alisema anapenda kati ya mabinti wa wananchi wake?

Alisema anapenda nyinyoro miongoni mwa miba.

Song of Solomon 2:3-4

Kivipi mwanamke alimuelezea mpenzi wake miongoni mwa vijana wadogo?

Mwanamke alimuelezea kijana wake mdogo kama mti wa mpera miongoni mwa miti ya misituni.

Ni wapi mwanamke alikaa?

Alikaa chini ya kivuli chake kwa furaha sana.

Nini kilikuwa kitamu kwa ladha yake?

Tunda lake lilikuwa tamu kwa ladha yake.

Ni wapi mwanaume wake mdogo alimleta?

Mwanaume wake mdogo alimleta kwenye holi la maakuli.

Bendera gani ilikuwa juu yake?

bendera ya upendo ilikuwa juu yake.

Song of Solomon 2:5-6

Mwanamke alitaka nini imuuishe?

Alitaka keki za mizabibu na mapera zimuuishe.

Mikona ya kulia na ya kushoto ilikuwa wapi ya mwanaume kijana?

Mkono wake wakushuto ulikuwa chini ya kichwa chake, na mkono wake wa kulia ulimkumbatia.

Song of Solomon 2:7

Mwanamke alitaka mabinti wa wanaume wa Yerusalemu waape nini?

Mwanamke alitaka wanawake waape kwamba hawatavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe.

Song of Solomon 2:8-9

Mwanamke alisikia sauti gani?

Mwanamke alisikia sauti ya mpenzi wake.

Alisema mpenzi wake alikuwa anafanyaje?

Alikuwa akiruka ruka juu milima, akiruka vilimani.

Alisema mpenzi wake alikuwaje?

Alisema mpenzi wake alikuwa kama swala au mtoto mdogo wa paa.

Song of Solomon 2:10-11

Mpenzi wake alitaka afanye nini na yeye?

Alitaka ainuke na kwenda naye.

Nini alisema imepita na kusahaulika?

Alisema baridi imepita; mvua imeisha na kwenda.

Song of Solomon 2:12-13

Nini kilitokea kwenye nchi?

Maua yametokeza juu ya nchi.

Kilikuwa kipindi cha nini?

kupunguza matawi na kuimba kwa ndege.

Nini kilistawi na kuchipua?

Mti wa tini umepevusha tini zake za kijani, na mizabibu imestawi.

Nini mpenzi wake alikata mzuri wake afanye?

Alitaka aamke na kuja.

Song of Solomon 2:14

Mpenzi wake anamuitaje?

Mpenzi wake anamuita hua wake.

Mpenzi wake anataka kusikia nini na kuona?

Mpenzi wake alitaka kuona uso wake mzuri na kusikia sauti yake tamu.

Song of Solomon 2:15

Mwanamke alitka adake nini?

Mwanamke alitaka akamate mbwa wa mitaani.

Song of Solomon 2:16-17

Wa nani mpenzi wa mwanamke alikuwa?

Mpenzi wake alikuwa ni wake.

Mwanamke alikuwa wa nani?

Alikuwa wa mpenzi wake.

Mpenzi wake alifanya nini miongoni mwa nyinyoro?

Alikula miongoni mwa nyinyoro kwa starehe.

Alitaka mpenzi wake afanye nini?

Alitaka mpenzi wake aondoke.

Lini alitaka mpenzi wake aondoke?

Alitaka mpenzi wake kuondoka kabla ya upepo mwepesi wa asubui kupiga na vivuli kutoweka.

Alitaka aonekanaje?

Alitaka awe kama ayala au paa mdogo kwenye milima.

Song of Solomon 3

Song of Solomon 3:1-2

Mwanamke alikuwa anamtamani nani lakini hakumpata?

Mwanamke alikuwa anamtani yeye anaye mpenda lakini hakumpata.

Mwanamke alikuwa anamtafuta nani mitaani na sokoni lakini hakumpata?

Mwanamke alikuwa anamtafuta mitaani na sokoni lakini hakumpata mpenzi wake.

Song of Solomon 3:3-4

Nini mwanamke alimuuliza askari alipo mkuta?

Aliwauliza, "Mmemuona mpenzi wangu?"

Alimpata saa ngapi yeye nafsi yake iliyo mpenda?

Alimpata yeye nafsi yake inayo mpenda kidogo baada ya kuwapita walinzi.

Nini alifanya kwa mpenzi wake?

Alimkumbatia na hakumuacha kwenda mpaka alipo mleta nyumbani mwa mama yake.

Song of Solomon 3:5

Nini mwanamke alitaka mabinti wa wanaume wa Yerusalemu wa ahidi?

mwanamke alitaka mabinti wa wanaume wa Yerusalemu wa ahidi kuwa hawatavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe.

Song of Solomon 3:6-7

Nini mwanamke mdogo aliona kina kuja kutoka nyikani kilicho kimefukizwa manemane na ubani, pamoja na unga wote ?wa manukato

kitanda cha Sulemani pamoja na mashujaa sitini wamekizunguka.

Song of Solomon 3:8-9

Mashujaa walikuwa wazuri katika nini?

Mashujaa walikuwa wazuri katika upanga na katika vita.

Sulemani alijitengenezea nini?

Mfalme Sulemani akajijengea kiti cha kifalme cha kubebwa na mbao za Lebanoni.

Song of Solomon 3:10-11

Kiti cha mfalme Sulemani kilikuwa namna gani?

Nguzo zake zilijengwa kwa fedha; nyuma kuliekwa dhahabu, na kiti kitambaa cha zambarau. Ndani mwake kulipambwa na upendo

Mwanamke alitaka wanawake Yerusalemu waangalie nini?

Aliwataka mwangalie mfalme Sulemani.

Mfalme Sulemani alikuwa amevaa nini siku ya arusi yake?

Alivaa taji mama yake alilo mvisha siku ya arusi yake.

Song of Solomon 4

Song of Solomon 4:1

Mpenzi wa mwanamke alielezeaje macho yake?

Macho yake ni ya hua nyuma kitamba chako cha uso.

Mpenzi wa mwanamke alielezeaje nywele zake?

Nywele zake zilikuwa kama kama kundi la mbuzi wakienda Mlima Gileadi.

Song of Solomon 4:2

Mpenzi alielezeaje meno yake?

Meno yake ni kama kondoo walio nyolewa

Song of Solomon 4:3

Mpenzi wa mwanamke alisemaje kuhusu midomo yake na mdomo wake?

Midomo yake ni kama uzi mwekendu; mdo wako wapendeza.

Mpenzi wa mwanamke aliezeaje mashavu yake?

Mashavu yake ni kama majani ya komamanga nyuma ya kitambaa chake cha uso.

Song of Solomon 4:4-5

Mpenzi wa mwanamke aliezeaje shingo yake?

Shingo yako ni kama mnara wa Daudi ukiwa umejengwa kwa mistari ya mawe, na ngao elfu moja ikining'nia juu yake.

Mpenzi wa mwanamke aliezeaje maziwa yake?

Maziwa yako mawili ni kama swala wawili, mapacha wa ayala, wakila miongoni mwa nyinyoro.

Song of Solomon 4:6-8

Wapi ambapo mpenzi wake angeenda hadi asubui kuja na vivuli kuondoka?

Angeenda kwenye mlima wa manemane na vilima vya ubani.

Kwa namnagani upendo wake ulikuwa mzuri?

Upendo wake ulikuwa mzuri kwa kila namna.

Nini ambacho upendo wake mzuri haukuwa nao?

Haukuwa na lawama ndani yake.

Song of Solomon 4:9

Sulemani alimuitaje bibi arusi wake?

Sulemani alimuira dada yake.

Sulemani alimwambia bibi arusi wake amemuibia nini?

Alimwambia amemuibia moyo wake.

Nini Sulemani alisema kilikuwa kizuri na nini kilikuwa bora zaidi?

Sulemani alisema upendo wake ulikuwa mzuri na bora kuliko mvinyo.

Song of Solomon 4:10-11

Harufu ya marashi yake yalikuwa mazuri kuliko nini?

Marashi yake yalikuwa mazuri kuliko manukato yeyote.

Nini alisema bibi arusi wake anatiririka midomoni na nini kilikuwa chini ya ulimi wake?

Alisema yatiririka asali; asali na maziwa vichini ya ulimi wako.

Nguo za mwanamke zilikuwa zanuka nini?

Harufu ya mavazi yako ni kama marashi ya Lebanoni.

Song of Solomon 4:12-14

Aina gani ya bustani na aina gani ya chemchemi Sulemani alisema dada yake, na bibi arusi, alikuwa?

Sulemani alisema ni kama bustani ilio fungwa, chemchemi iliyo fungwa kwa muhuri.

Alifananisha matawi ya mwanamke na nini?

Alifananisha matawi yake na kichaka cha miti ya komamanga yenye matunda tofauti.

Song of Solomon 4:15-16

Kwa aina gani ya maji Sulemani ana muelezea mpenzi wake?

Anamuelezea kama bustani ya chemchemi, kisima cha maji safi, mifereji inayo shuka kutoka Lebanoni.

Song of Solomon 5

Song of Solomon 5:1

Wapi Sulemani kuja wapi?

Sulemani alikuja kwenye bustani yake.

Song of Solomon 5:2

Nini ambacho bibi arusi wake Sulemani alikuwa akikiota?

Alikuwa akiota mpenzi wake akibisha na kuongea.

Song of Solomon 5:3-4

Nini mpenzi wa Sulemani alikuwa amesha fanya?

Tayari alikuwa ameshavua vazi lake na kunawa miguu yake.

Wapi Sulemani aliweka mkono wake?

Sulemani aliweka mkono wake kwenye kitasa cha mlango.

Song of Solomon 5:5

Nini kilikuwa cha tiririka kwenye mikono ya bibi arusi alipo fungua mlango?

Mikono yake ilikuwa ya tiririka udi.

Song of Solomon 5:6

Nini bib arusi alikuta alipo fungua mlango na alijisikiaje?

Alikuta mpenzi waku aligeuka na kwenda. Moyo wake ukadidimia; nakukosa tumaini.

Song of Solomon 5:7

Nini walinzi walifanya walipo mkuta bibi arusi wa Sulemani?

Walimpiga chini na kumjeruhi na kuchukuwa vazi lake.

Song of Solomon 5:8

Nini bibi arusi aliwaambia wanawake wa Yerusalemu wa ahidi?

Aliwambia wanawake wa Yerusalemu kuwa watamwambia wakimuona.

Jinsi gani mpenzi wa mwanamke alimfanya ajisiki?

Alimfanya aumwe kwa mapenzi.

Song of Solomon 5:9

Nini wanawake walimuomba bibi arusi?

Walimuuliza kwanini mpenzi wako bora kuliko mpenzi mwengine.

Song of Solomon 5:10-11

Jinsi gani mwanamke alivyo muelezea mpenzi wake?

Alimuelezea kama amenawiri na ana ng'aa.

Jinsi gani mwanamke alivyo muelezea kichwa chake na nywele?

Kichwa chake ni dhahabu safi; nywele zake ni laini na nyeusi.

Song of Solomon 5:12

Mwanamke alielezeaje macho ya mpenzi wake?

Alielezea kama macho ya hua yameoshwa kwenye maziwa.

Song of Solomon 5:13

Bibi arusi wa Sulemani alielezeaje mashavu na midomo yake?

Mashavu yake ni kama vitanda vya manukato, Midomo yake ni nyinyoro, inayo tiririka udi.

Song of Solomon 5:14

Mwanamke alielezeaje mikono na tumbo la mpenzi wake?

Mikono yake ni ya mianzi ya dhahabu iliyo zungushiwa mikufu; tumbo lake ni pembe lililo funikwa yakuti samawi.

Song of Solomon 5:15

Mwanamke alielezeaje miguu na muonekano wa mpenzi wake?

Miguu yake ni nguzo za marimari, iliyo ekwa juu ya dhahabu safi; muonekano wake ni kama Lebanoni, mizuri kama mierezi.

Song of Solomon 5:16

Bibi arusi wa Sulemani alielezeaje mdomo wa mpenzi wake na Sulemani kwa mabinti wa Yerusalemu?

Alimuezea mdomo wake kama mtamu sana na kuwa Sulemani ni mzuri.

Song of Solomon 6

Song of Solomon 6:1

Maswali gani wanawake wa Yerusalemu wa muuliza mwanamke?

Wanamuuliza wapi mpenzi wake ameenda na njia gani aliyo enda?

Nini wanawake walitaka kutafuta?

Wanawake walitaka kumtafuta mpenzi wa mwanamke.

Song of Solomon 6:2-3

Nini mwanamke anasema mpenzi wake alikuwa anafanya?

Anasema alikuwa katika bustani yake, kwenye vitanda vya manukato, kwenda kula katika bustani na kukusanya nyinyoro.

Mwanamke na mpenzi wake walikuwa wa nani?

Mwanamke na mpenzi wake walikuwa ni wao.

Wapi mpenzi wa mwanamke alikula ?

Mpenzi wa mwanamke alikula miongoni mwa nyinyoro.

Song of Solomon 6:4

Miji gani miwili mpenzi wa mwanamke alitumia kumuelezea?

Alitumia Tirza na Yerusalemu kumuelezea.

Jinsi gani mpenzi wake alijisikia kuhusu yeye?

Alijisikia kuwa yeye ana shanganza.

Song of Solomon 6:5

Kwanini mpenzi wa mwanamke alimtaka ageuze macho yake mbali na yeye?

Mpenzi wa mwanamke alitaka ageuze macho yake mbali kutoka kwake kwasababu macho yake yalimzidi nguvu.

Jinsi gani mpenzi wa mwanamke alielezea nywele zake?

Alielezea nywele zake kama kundi la mbuzi katika miteremko ya Mlima Gileadi.

Song of Solomon 6:6-7

Mpenzi wake alielezeaje meno yake?

Alielezea meno yake kama kundi la kondoo kutoka sehemu ya kuoshwa.

Mpenzi wake alielezeaje mashavu yake?

Alielezea mshavu yake kamamajani ya komamanga nyuma ya kitambaa chako cha uso.

Song of Solomon 6:8-9

Wanawake wangapi wengine mpenzi wa mwanamke alisema wapo?

Alisema walikuwa malikia 60, masuria 80, na wanawake wadogo wasio na idadi.

Mpenzi wa mwanamke alielezaje hua wake?

Hua wangu, asiye na doa wangu, ni yeye pekee; ni binti muhimu wa mama yake.

Nini malikia na na masuria walisema kumuhusu walipo muona?

Malikia na masuria walimsifu.

Song of Solomon 6:10

Jinsi gani mpenzi wa mwanamke alimuelezea?

Mpenzi wa mwanamke alimuelezea kama asubui, mwezi, jua, na wa kushanganza.

Song of Solomon 6:11-12

Kwanini mpenzi wa mwanamke alienda kwenye kichaka cha miti ya milozi?

Mmpenzi wa mwanamke alienda kwenye kichaka cha miti ya milozi kuona kama mizabibu imechipua, na kama mikomamanga imestawi.

Mpenzi wa mwanamke alijisikiaje?

Mpenzi wa mwanamke alijisikia kama vile alikuwa amepakia gari ya farasi la mtoto wa mfalme.

Song of Solomon 6:13

Nini mpenzi wa mwanamke alimtaka afanye?

Mpenzi wa mwanamke alimtaka amgeukie.

Kwanini mpenzi wa mwanamke alimtaka amgeukie?

Mpenzi wa mwanamke alimtaka amgeukie iliamuangalie.

Nini mwanamke alisema kuhusu yeye?

Mwanamke alijelezea kama mwanamke mkamilifu aliye onekana kucheza katika ya mistari miwili ya wachezaji.

Song of Solomon 7

Song of Solomon 7:1

Sulemani alielezeaje miguu ya mpenzi wake katika viatu na mapja yake?

Alieleza kuwa miguu yake ni mizuri kwenye viatu, binti wa mfalme! Mapaja yako ni kama mikufu.

Song of Solomon 7:2

Sulemani alielezeaje kitovu cha mpenzi wake na tumbo?

Sulemani alielezea kitovu cha mpenzi wake kama duara la bakuli; kamwe kisikose mchanganyiko wa mvinyo. Tumbo lako ni kama ngano iliyo umuka na kuzungushiwa nyinyoro.

Song of Solomon 7:3-4

Sulemani alielezeaje maziwa mawili ya mpenzi wake?

Sulemani alielezea maziwa yako mawili ni kama watoto wawili wa ayala, mapacha wa ayala.

Sulemani alielezeaje shingo, macho, na pua ya mpenzi wake?

Sulemani alielezea shingo yake kama mnara wa pembe, na pua yake kama mnara wa Lebanoni

Song of Solomon 7:5-6

Jinsi gani Sulemani alivyo eleza nywele za mpenzi wake?

Sulemani alieleza Kichwa chako ni kama Mlima Karmeli na nywele zake nyeusi.

Song of Solomon 7:7-8

Sulemani alielezaje maziwa ya mpenzi wake?

maziwa yako kama vifungu vya matunda.

Alitaka maziwa ya mpenzi wake kuwaje?

Alitaka maziwa yake kuwa kama vifungu vya mizabibu, na harufu ya pua yako yawe kama mapera.

Song of Solomon 7:9

Alitaka mdomo wa mpenzi wake kuwaje?

Alitaka mdomo wake kuwa kama mvinyo.

Song of Solomon 7:10-11

Mwanamke mdogo alikuwa wa nani na alimtamani nani?

Mwanamke mdogo alikuwa wa mpenzi wake na mpenzi wake alimtamani.

Wapi mwanamke alimtaka mpenzi wake kwenda naye?

Alimtaka kwenda naye nje ya mji; tu lala usiku kwenye vijiji.

Song of Solomon 7:12

Kwanini alimtaka mpenzi wake kuinuka mapema?

Ili waende kwenye mashamba ya mizabibu; tuone kama mizabibu imemea.

Nini alisema atampa mpenzi wake watakapo fika kwenye mashamba ya mizabibu?

Alisema atampa mpenzi lake.

Song of Solomon 7:13

Nini alisema mitunguja itafanya?

Mitunguja ya toa harufu yake.

Nini alisema kipo mlangoni ambapo yeye na mpenzi wake walikuwa wanaishi?

Alisema kuna kila aina ya matunda, mpya na ya kale, aliyo muhifadhia

Song of Solomon 8

Song of Solomon 8:1

Nini mwanamke alitamani mpenzi wake awe na kwanini?

Alitamani awe kama kaka yake, aliye nyonya ziwa la mama yake. Ili kwamba kila ningekuona nje ningekubusu pasipo mtu kunidharau.

Song of Solomon 8:2-3

Wapi mwanamke angependa kumpeleka mpenzi wake?

Angependa kumpeleka kwa nyumba ya mama yake amfundishe.

Mikono ya kulia na kushoto ya mpenzi wake ilikuwa inafanya nini?

Mkono wake wa kushoto ulikuwa washikilia kichwa chake na mkono wake wa kulia wamkumbatia.

Song of Solomon 8:4

Nini mwanamke alitaka wanawake wa Yerusalemu kuahidi?

Kuape, kuwa mabinti wa wanaume wa Yerusalemu, kuwa hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe.

Song of Solomon 8:5

Wanawake wa Yerusalemu waliuliza nini?

Waliuliza nani anaye kuja kutoka nyikani, amemuegemea mpenzi wake.

Nini mwanamke alimuambia mpenzi wake alipo amka kutoka chini ya mti wa mpera?

Alimuambia kuwa mama yak alichukua mimba na kumzaa chini ya mti wa mpera.

Song of Solomon 8:6

Nini mwanamke alimuuliza mpenzi wake afanye na kwanini?

Amueke kama muhuri kwenye moyo wake kwasababu upendo wake una nguvu kama mauti na moto mkali.

Song of Solomon 8:7

Nini kisingeweza kuzuia mapenzi?

Maji yalio zuka hayawezi kuzimisha upendo.

Song of Solomon 8:8

Nini kaka zake mwanamke walisema kuhusu dada yao mdogo?

Walisema matiti yakebado hayajakua na wakajiuliza nini watafanya kwa ajli yake atakapo ahidiwa kuolewa.

Song of Solomon 8:9

Nini kaka zake mwanamke wangefanya kama angekuwa ukuta?

Kama ni ukuta, tutamjengea juu yake mnara wa fedha.

Nini kaka zake mwanamke wangefanya kama angekuwa mlango?

Kama ni mlango, tutampamba kwa mbao za mierezi.

Song of Solomon 8:10

Mwanamke alijielezeaje?

Alijielezea kama ukuta na matiti nguzo imara na amekomaa.

Song of Solomon 8:11-12

Nini mwanamke alisema kuwa Sulemani amefanya na shamba lake la mizabibu huko Baali Hamoni?

Aliwakodishia wao ambao watalitunza

Nini mwanamke anasema kuhusu shamba lake na wao walio litunza?

Alisema shekeli 1000 lilo leta zilikuwa ni za Sulemani na wao walio litunza walipata shekeli 200.

Song of Solomon 8:13

Nini mpenzi wa mwanamke alisema kwake aliye ishi kwenye bustani kuhusu marafiki zake, pamoja na yeye, walichotaka kusikia?

Alisema marafiki zake, pamoja na yeye, walitaka kuwa wa kusikia sauti yake.

Song of Solomon 8:14

Ni mwanamke alitaka mpenzi wake kufanya na kuwa?

Alitaka mwanamke kuharakisha na kuwa kama paa.