Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

1 Chronicles

1 Chronicles 1

1 Chronicles 1:8-16

Nani alikuwa shujua wa kwanza katika dunia?

Nimrodi, mwana wa Kushi, alikuwa shujaa wa kwanza.

1 Chronicles 1:17-42

Kwanini mmoja wa wana wa Eberi aliitwa Pelegi?

Katika siku zake, dunia iligawaniyika.

1 Chronicles 1:43-54

Nchi gani wafalme kabla wa wafalme walitawala juu ya Waisraeli?

Nchi ya Edomu wafalme kabla Israeli haijawa na wafalme.

1 Chronicles 2

1 Chronicles 2:3-4

Nini kilimtokea Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda?

Alikuwa muovu machoni pa Yahweh, hivyo Yahweh akamua.

1 Chronicles 2:5-12

Jinsi gani Akari alileta shida Israeli?

Aliiba kilicho hifadhiwa kwa Mungu.

1 Chronicles 2:13-55

Nani alikuwa mwana wa saba wa Yese?

Daudi alikuwa mwana wa saba wa Yese.

1 Chronicles 3

1 Chronicles 3:4-14

Miaka mingapi Daudi alitawala kama mfalme wa Yerusalemu?

Alitawala kwa miaka thelathini na tatu kama mfalme Yerusalemu.

1 Chronicles 3:15-24

Nani alikuwa mfalme wa mwisho wa Waisraeli?

Zedekia alikuwa mfalme wa mwisho wa Israeli.

1 Chronicles 4

1 Chronicles 4:9-26

Nini Yabesi alimuomba Mungu wa Israeli?

Aliomba Mungu ambariki, apanue mipaka yake, amlinde na alisiweze kuvumilia maumivu.

Maombi ya Yabesi yalijibiwa?

Ndio, Mungu alimjibu maombi yake.

1 Chronicles 4:27-38

Kwa nini ukoo wa Shimei na kaka zake hawaku ongezeka sana kwa idadi na watu wa Yuda waliongezeka?

Kaka zake hawakuwa na watoto wengi.

1 Chronicles 4:39-43

Kwanini baadhi ya wana wa Shimei walienda Gedori upande wa mashariki wa bonde?

Walikuwa wana tafuta majani ya mifugo yao, na wakapa mengi na mazuri.

1 Chronicles 5

1 Chronicles 5:1-3

Kwanini haki ya mzaliwa wa kwanza ya Rubeni alipewa Yusufu?

Haki ya mzaliwa wa kwanza alipewa Yusufu, mwana wa Israeli, kwasababu Rubeni alinajisi kitanda cha baba yake

Kwa mtoto yupi wa Israeli kiongozi atatoka?

Kiongozi atatoka kwa Yuda.

1 Chronicles 5:4-17

Nini kilimtokea Bera, mwana wa Baali?

Waasiria walimchukuwa matekani.

1 Chronicles 5:18-19

Wanajeshi wa ngapi wenye mafunzo Warubeni, Wagadi, na nusu kabila la Manase walikuwa nao?

Walikuwa na wanajeshi elfu arobaini na nne wenye mafunzo ya vita, waliyo beba silaha, na waliyo vuta upinde.

1 Chronicles 5:20-22

Kwanini Waagri walishindwa?

Walishinwa kwasababu Waisraeli walimlia Mungu na kumuamini, na Mungu akawajibu.

Waisraeli waliishi kwa muda gani katika nchi waliyo chukuwa kutoka kwa Waagri?

Waliishi hapo hadi mateka yao?

1 Chronicles 5:23-24

Kabila nusu la Manase liliishi wapi na familia zao?

Waliishi katika nchi ya Bashani.

1 Chronicles 5:25-26

Kwasababu Warubeni, Wagadi, na nusu kabila la Manase hawakuwa waaminifu kwa Mungu nini alichowafanyia?

Mungu alimuamsha mfalme wa Asiria na haya makabila yalipelekwa matekani na Asiria.

1 Chronicles 6

1 Chronicles 6:13-30

Kwa nani Yahweh aliwapeleka matekani Yuda na Yerusalemu?

Aliwapeleka Yuda na Yerusalemu kwa Nebukadneza mfalme wa Babilonia.

1 Chronicles 6:31-47

Kazi zipi zilikuwa za wanaume Daudi aliyo waweka wahusika wa muziki?

Walikuwa watumike kwa kuimba kataka hema la kukutania.

Nani alijenga nyumba ya Yahweh Yerusalemu?

Sulemani alijenga nyumba ya Yahweh.

1 Chronicles 6:48

Ni kabila gani la Waisraeli walipangiwa kufanya kazi katika hema la kukutania?

Walawi ndio walipangiwa kufanya hii kazi.

1 Chronicles 6:49-62

Ni sadaka zipi za maombolezo Aruni na wana wake waliwajibika nayo?

Walikuwa na wajibu wa sadaka kwenye madhabahu sadaka za kuteketeza na katika madhabahu ya uvumba.

Sadaka hizi zilikuwa kwa ajili ya nini?

Sadaka hizi zilikuwa za kufanya maombezi kwa ajili ya dhambi za Waisraeli

1 Chronicles 6:63-81

Walawi walikuwa wanaishi wapi kwa sababu hawakupewa ardhi maalumu kama makabila mengine?

Walawi walipangiwa miji kwa kura pamoja na malisho yao kutoka makabila ya Yuda, Simeoni, na Benjamini.

1 Chronicles 7

1 Chronicles 7:1-3

Ni wanaume wa aina gani walikuwa wana wa Tola?

Walikuwa wenye nguvu, wanaume wajasiri.

1 Chronicles 7:4-5

Ni idadi gani ya wanaume wa vita kutoka kabila la Isakari?

Kabila la Isakari walikuwa na wanaume wa vita 87,000.

1 Chronicles 7:6-13

Kwa yapi wana wa Bela walijulikana?

Wana wa Bela walijulikana kama maaskari na waanzilishi wa ukoo.

1 Chronicles 7:14-19

Nani alimzalia Manase mtoto wa kiume aliyeitwa Asrieli?

Suria wa Kiarami wa Manase ndiye aliyemzalia mtoto wa kiume aliyeitwa Asrieli.

1 Chronicles 7:20-22

Kwanini Efraimu alihitaji faraja kutoka kwa kaka yake wakati alipokuwa anaomboleza kwa siku nyingi?

Efraimu alihitaji faraja kutoka kwa kaka zake kwasababu wana wake Eza na Eleadi waliuwawa na wanaume wa gathi walipoenda kuiba mifugo yao.

1 Chronicles 7:23-24

Kwanini Efraimu alimuita mwana wake Beria?

Efraimu alimuita mwana wake Beria kwasababu ya maafa yaliyotokea kwenye familia yake.

1 Chronicles 7:25-27

Nani alikuwa mwana wa Nuni?

Yoshua alikuwa mwana wa Nuni.

1 Chronicles 7:28-38

Wapi zilikuwa mali na makazi ya Yoshua na familia yake?

Mali zao na makazi zilikuwa ndani ya Betheli na vijiji vilivyoizunguka.

1 Chronicles 7:39-40

Ni sifa zipi walizokuwa nazo uzao wa Asheri?

Uzao wa Asheri walikuwa waanzilishi wa koo, viongozi wa familia zao, wanaume wa kipekee, wanaume wa vita, na watemi kati ya viongozi.

1 Chronicles 8

1 Chronicles 8:6-11

Wazao wa Ehudi walisukumwa kufanyaje?

Uzao wa Ehudi walisukumwa kuhamia Manahathi.

1 Chronicles 8:12-25

Wana wa Elipaali walimfukuza nani?

Wana wake waliwafukuza wenyeji wa Gathi.

1 Chronicles 8:26-31

Wana wa Yerohamu waliishi wapi?

Waliishi Yerusalemu.

1 Chronicles 8:32-37

Mikloti na familia yake waliishi wapi?

Mikloti na familia yake waliishi karibu na ndugu zao Yerusalemu.

Nani alikuwa baba waSauli?

Kishi alikuwa baba wa Sauli.

1 Chronicles 8:38-40

Wana wa Ulamu, waliokuwa uzao wa Benjamini, walijulikana kwa lipi?

Wana wa Ulamu walikuwa wanaume wa vita na wapiga mishale.

1 Chronicles 9

1 Chronicles 9:1-9

Wapi nakala za uzao wa Israeli ziliandikwa?

Nakala za ziliandikwa katika Kitabu cha Walfalme wa Israeli.

Kwanini Yuda ilipelekwa matekani na Babilonia?

Yuda ilipelekwa matekani kwasababu ya dhambi zao.

Watu gani walikuwa wa kwanza kurudi katika miji yao?

Wakwanza kurudi kuishi katika miiji yao walikuwa Waisraeli, Makuhani, Walawi, na Watumishi wa hekalu.

1 Chronicles 9:10-11

Kwa lipi Azaria alijulikana?

Azaria alikuwa na mamlaka katika nyumba ya Mungu.

1 Chronicles 9:12-16

Kwa yapi ndugu wa Adaia na Maasai walijulikani?

Walikuwa ni wanaume wenye uwezo sana wa kufanya kazi katika nyumba ya Mungu.

1 Chronicles 9:17-19

Ni majukuma gani yaliyo pita ambao walinzi wa lango walitekeleza?

Awali walisimama kulinda katika geti la mfalme upande wa mashariki wa kambi ya uzao wa Walawi.

Nini lilikuwa jukumu la Wakora?

Wakora walikuwa walinzi juu ya kazi ya hekalu na juu mwingilio wa hema Yahweh alipo ishi.

1 Chronicles 9:20-21

Lipi lilikuwa jukumu la Zekaria, mwana wa Meshelemia?

Zekaria alikuwa mlinzi kwenye mwingilio wa Hekalu, "hekalu la kuingilia"

1 Chronicles 9:22-24

Nini walinzi wa lango na watoto wao, ambao Daudi na Samweli waliwaeka katika nafasi zao, walifanya?

Walinzi wa lango na watotot wao walilinda mageti katika nyumba ya Yawehi, hema la kuabudia.

1 Chronicles 9:25-27

Kwa namna gani viongozi wa nne wa walinzi wa lango walitekeleza kazi waliyo pangiwa kulinda chumba na vyumba vya kuhifadhia katika nyumba ya Mungu

viongozi wanne wa walinzi walitumia usiku wao sehemu walizowekwa kuzunguka nyumba ya Mungu na walifungua geti kila asubuhi.

1 Chronicles 9:28-29

Kazi zipi maalumu Walawi walipangiwa kufanya?

Baadhi yao waliwajibika katika hekalu la vifaa na baadhi yao pia waliwekwa kutunza vitu vitakatifu, vifaa, na vitu , kujuisha unga safi, mvinyo, mafuta, manukato, na uvumba.

1 Chronicles 9:30-32

Upi ulikuwa waajibu wa Wakora?

Wakora waliwajibika kwa mikate ya uwepo, kuandaa kila Sabatho.

1 Chronicles 9:33-44

Kwanini waimbaji na familia za viongozi wa Walawi waliishi katika vyumba vya pahali pa takatifu walipo kuwa hawafanyi kazi?

Waimbaji na viongozi wa familia ya Walawi waliishi ndani ya vyumba katika mahali takatifu walipo kuwa hawafanyi kazi, kwa sababu wapiswa kufanya kazi walio pangiwa usiku na mchana.

1 Chronicles 10

1 Chronicles 10:1-3

Nini kiliwatokea wana wa Sauli Mlima Giliboa?

Wafilisti waliwakimbiza Sauli na wanae na kuwaua.

1 Chronicles 10:4

Kwanini Sauli alimtaka mbeba ngao amchome kwa upanga wake?

Sauli alimtaka mbeba ngao amchome kwa upanga wake ili wasio tahiriwa wasije kumtesa.

Nini Sauli alikifanya mbeba ngao wake alipo kataa kumchoma?

Sauli alichukuwa upanga wake na kuuangukia.

1 Chronicles 10:5-6

Mbeba ngao wa Sauli alivyo alifanya nini baada ya kuona Sauli kafa?

5Mbeba ngao alivyoona kuwa Sauli amekufa, naye akaangukia upanga wake na kufa.

1 Chronicles 10:7-8

Nini wanaume Waisraeli walifanya baada ya kuona jeshi limekimbia na Sauli na wanae wamekufa?

Walitelekeza miji yao na kukimbia. Kisha Wafilisti wakaja na kuishi humo

1 Chronicles 10:9-10

Nini Wafilisti walifanya mwili wa Sauli?

Wafilisti wakamvua nguo zote na ngao yake wakaeka ndani ya hekalu la miungu yao, na kichwa chake waka kining'iniza katika hekalu la Dagoni.

1 Chronicles 10:11-12

Nini wapiganaji wa Yabeshhi Gileadi walifanya miili ya Sauli na wanae?

Walichukuwa mwili wa Sauli na hiyo ya wanae, na kuirejesha Yabeshi na kuizika mifupa yao chini ya mti .

1 Chronicles 10:13-14

Kwanini Sauli alikufa?

Sauli alikufa kwasababi hakuwa mwaminifu kwa Yahweh. Hakutii maelekezo ya Yahweh, lakini akauliza ushauri kwa mtu anaye ongea na wafu.

1 Chronicles 11

1 Chronicles 11:1-3

Kwanini Israeli yote ilikuwa tayari kumpaka mafuta Daudi awe mfalme juu ya Israeli?

Daudi alikuwa nyama na mifupa yako, aliongoza jeshi la Israeli, na Yahweh kupitia Samweli alimtangaza Daudi kuwa ata tawala Israeli.

1 Chronicles 11:4-6

Yoabu alikuwaje mkuu wa jeshi la Israeli?

Daudi alisema, yeyote atakaye washambulia Wayebusi wa kwanza atakuwa mkuu wa jeshi kwaiyo Yoabu akashambulia wa kwanza.

1 Chronicles 11:7-9

Kwanini Daudi alikuwa mkubwa na mkubwa baada ya kuanza kuishi mji wa Daudi?

Daudi alikuwa mkubwa na mkubwa Yahweh wa Majeshi alikuwa naye.

1 Chronicles 11:10-11

Kwa lipi Yashobeami alijulikana?

Aliwaua wanaume mia tatu na mkuki wake katika sehemu moja.

1 Chronicles 11:12-14

Nini ilikuwa sifa ya Eleazari Mahohi?

Baada ya jeshi la Waisraeli kukimbia, Eleazari Mahohi alisimama sehemu yake katikati ya shamba la ngano na kuwakata chini Wafilisti.

1 Chronicles 11:15-17

Ombi gani Daudi alilifanya?

Daudi alitaka maji ya kunywa kutoka kisima kilicho Bethilehemu.

1 Chronicles 11:18-19

Nini wanaume hodari wa Daudi walicho kifanya kutimiza ombi lake?

anaume hodari watatu wakatoboa kupita jeshi la Wafilisti na kuchota maji kwenye kisima cha Bethilehemu, wakachukuwa maji na kumletea Daudi.

Kwanini Daudi alikataa kunywa kutoka kisima cha Bethilehemu wakati wanaume wake hodari walihatarisha maisha yao kuyapata?

Daudi alikataa kunywa maji kwasababu wameeka maisha ya hatarini kuyapata.

1 Chronicles 11:20-21

Ipi ilikuwa sifa ya Abishai, kaka yake Yoabu?

Abishai alikuwa kiongozi wa wanaume wa tatu na mara moja aliwai kuua mia tatu kwa mkuki wake.

1 Chronicles 11:22-23

Ipi ilikuwa sifa ya Benaia, mwana wa Yehoiada?

Benaia alikuwa mwanaume mwenye nguvu aliyewai chini ya shimo kumuua simba wakati theluji ikianguka, alimuua Mmisri mkubwa kukamata mkuki wake.

1 Chronicles 11:24-25

Jukumu gani Daudi alimpa Benaia?

Benaia alisifika sana kwa Daudi, alimueka kiongozi wa walinzi wake.

1 Chronicles 11:26-47

Yupi mwanaume hodari alikuwa kaka yake Yoabu?

Asaheli alikuwa mwanaume hodari aliye kuwa kaka yake Yoabu.

1 Chronicles 12

1 Chronicles 12:1-7

Ni kipawa gani maalumu wanaume hodari walio mjia Daudi wakati akiwa amefukuzwa uweponi mwa Sauli walikuwa nacho?

Wanaume hodari walikuwa Wabenjamini waliweza kutumia mkono wa kuume na wakushoto kurusha mawe na manati na kupiga mishale kutoka kwenye upinde.

1 Chronicles 12:8-13

Ni vipaji gani vya kipekee walikuwa navyo Wagadi walio jiunga na Daudi katika ngome huko nyikani.

Wagadi walikuwa wanaume wapiganaji, waliofundishwa kwa mapambano, walioweza kumudu ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kali kama za simba. Walikuwa wepesi kwenye milima kama swala.

1 Chronicles 12:14-15

Ni nini wana wa Gadi walitimiza katika nchi walioyo pewa Waisraeli?

Wana wa Gadi hawaku katisha Yordani wakati vijito vyake vilipofurika tu, lakini pia waliwa fukuza wote wanaoishi katika mabonde.

1 Chronicles 12:16-17

Onyo gani Daudi aliwapa wanaume wa Benjamini na Yuda walipo kuja kwenye ngome yake?

Daudi aliwaambia kama wamekuja kwa amani kumsaidia, mnaweza kujiunga naye, lakini kama wakuja kumsaliti kwa maadui wake, kisha ata mwambia Mungu awakemee maana hajafanya kosa lolote.

1 Chronicles 12:18

Nini lilikuwa jibu la Amasai kwa onyo la Dauid?

Amasai alimwambia Daudi kwamba sisi sote tupo upande wake na tunataka amani kwa yeyote atakaye msaidia Daudi kwasababu Mungu anamsaidia.

1 Chronicles 12:19-20

Kwanini Wafilisti walimuondoa Daudi wakati Daudi alikuja kwa Wafilisti ili kupigana kwenye pambano dhidi ya Sauli?

Wafilisti wali hofu kuwa atamwendea Sauli na kuhatarisha maisha yao.

1 Chronicles 12:21-22

Jinsi gani wanaume wa Manase ambao baada walikuwa wakuu katika jeshi la Daudi msaidia?

Walimsaidia Daudi kupigana na kikundi cha wezi.

1 Chronicles 12:23-25

Kwanini wanajeshi wenye silaha wa vita wote walikuja kwa Daudi huko Hebroni?

Walikuja kwa Daudi Hebroni kumsaidia kuchukuwa ufalme wa Sauli ambalo lilikuwa timizo ya neno la Yahweh.

1 Chronicles 12:26-31

Kwa lipi Zadoki alijulikana?

Zadoki alikuwa kijana, wenye nguve, na mjasiri.

1 Chronicles 12:32-37

Kwa lipi viongozi mia mbili wa Isakari walijulikana?

Walikuwa na ufahamu wa nyakati na walijua nini Israeli ili paswa kufanya.

1 Chronicles 12:38-40

Kwanini wanajeshi wote walikuja Hebroni?

Walikuja Hebroni kwa dhumuni madhubuti la kumfanya Daudi mfalme wa Israeli.

Wapi wanajeshi wa Israeli walipata chakula cha kutosha na kinywaji kuweza kula na kunywa kwa siku tatu kusherehekea Daudi kuwa mfalme?

Ndugu wa wanajeshi wa Israeli walituma maitaji yote kwao.

1 Chronicles 13

1 Chronicles 13:1-6

Nani Daudi alimfuata kabla ya kuzungumza na kusanyiko lote la Israeli?

Alishauriana na wakuu na viongozi wote wa Israeli.

Kwanini kusanyiko lilikubaliana na Daudi, kutuma wajumbe kila sehemu Israeli na kujiunga na Daudi kuleta sanduku la Mungu Israeli?

Kusanyiko lote liliafiki kufanya haya yote, kwa kuwa yalionekana sawa machoni pa watu wote.

1 Chronicles 13:7-8

Nini daudi na Israeli yote ilifanya walipo leta sanduku kutoka nyumbani mwa Abinadabu?

Daudi na Israeli yote walikuwa wakishangilia mbele za Mungu kwa nguvu zao zote.

1 Chronicles 13:9-11

Nini Yahweh alifanya pale Uza alipo nyoosha mkono wake kuzuia sanduku ng'ombe alipo yumba?

Hasira ya Yahweh ikawaka juu ya Uza na Yahweh akamua.

Kwanini Daudi alikuwa na hasira na Yahweh?

Daudi alipatwa na hasira kwa kuwa Yahweh alimshambulia Uza.

1 Chronicles 13:12-14

Wapi Daudi alipo eka sanduku la Mungu wakati alipo kuwa na hofu na Mungu?

Daudi aliweka sanduku la Mungu kwenye nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.

Nini Yahweh alicho fanya kwa nyumba ya Obedi Edomu?

Yahweh akabariki nyumba yake na yote aliyo miliki.

1 Chronicles 14

1 Chronicles 14:1-2

Nini Daudi alijua kwa uhakika Hiramu, mfalme wa Tire alipo tuma wajumbe, miti ya mierezi, seramala, wa jenzi kujenga nyumba ya Daudi?

Daudi alijua kuwa Yahweh alimfanya kuwa mfalme juu ya Waisraeli.

1 Chronicles 14:3-7

Nini lilikuwa tokea Daudi alipo chukuwa wake zaidi Yerusalemu?

Daudi alikuwa baba wa wana na mabinti zaidi.

1 Chronicles 14:8-9

Daudi alifanya nini alivyo sikia Wafilisti wanamtafuta?

Alienda njee dhidi yao.

1 Chronicles 14:10-12

Nini Yahweh alilmjibu Daudi alipo muuliza kama awashambulie Wafilisti?

Yahweh alimwambia Daudi shambulia kwa maana ata wakabidhi kwa Daudi.

Daudi aliagiza nini kifanyike kwa miungu Wafilisti waliyo itelekeza?

Daudi akatoa amri wateketezwe kwa moto.

1 Chronicles 14:13-14

Kutoka wapi Mungu alimwambia Daudi awashambulie Wafilisti walipo vamia bonde tena?

Mungu akamwambia Daudi lakini wazunguke kwa nyuma yao na uwajie kupitia misitu.

1 Chronicles 14:15-17

Nini Daudi paswa kusikia kabla ya kushambulia Wafilisti kwa nguvu?

Daudi alipaswa kusikia sauti ya wanajeshi wanatembea kwenye upepo uvumao kutoka juu ya miti.

Nini Yahweh alisababisha mataifa yote ya fanye umarufu wake ulipo enda nchi zote?

Yahweh akasababisha mataifa yote kumuhofia.

1 Chronicles 15

1 Chronicles 15:1-3

Nani Daudi alisema ndio watu pekee Yahweh aliyo wachagua kubeba sandaku?

Walawi pekee ndio watabeba sanduku la Mungu.

Kwa dhumuni gani Daudi alikusanya Israeli yote Yerusalemu

Daudi alikusanya wote Walawi pekee ndio watabeba sanduku la Mungu.

1 Chronicles 15:4-10

Nani Daudi alikusanya pamoja kuleta sanduku?

Daudi akakusanya uzao wa Aruni na Walawi pamoja.

1 Chronicles 15:11-12

Ni nini viongozi wa familia za Walawi walipaswa kufanya na kaka zao ili waeze kuleta sanduku la Yahweh sehemu Daudi aliyo iandaa?

Walipaswa kujiweka wakfu ilikwamba walete sanduku la Yahweh.

1 Chronicles 15:13-15

Kwanini makuhani na Walawi walijiweka wakfu?

Walijiweka wakfu iliwaweze kuleta sanduku la Yahweh, Mungu wa Israeli.

Kutoka kwa nani Musa alipata amri za kubeba sanduku kwenye mabega ya Walawi na miti yake?

Amri za kubeba sanduku zilitolewa na neno la Yahweh.

1 Chronicles 15:16-24

Nani ambaye Daudi alimpa jukumu la kusajili wana muziki?

Daudi alitoa jukumu la kusajili wana muziki kwa viongozi wa Walawi.

1 Chronicles 15:25-26

Nani aliwasaidia Walawi waliyo beba sanduku la agano la Yahweh?

Mungu aliwasaidia Walawi waliyobeba sanduku.

1 Chronicles 15:27-28

Daudi alivishwa nini na alikuwa na nini juu yake?

Daudi alivishwa na joho safi na alikuwa amevaa naivera.

Nani alileta sanduku kwa furaha za kelele, na sauti za tarumbeta, kwa upatu na vyombo vya uzi na vinubi.

Israeli yote iliyo ilileta sanduku.

1 Chronicles 15:29

Nini Mikali alimuona Daudi akifanya kilicho msababisha amdharau moyoni mwake.

Mikali alimuona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea.

1 Chronicles 16

1 Chronicles 16:1-3

Nini Waisraeli walimtolea Mungu baada ya sanduku kuwekwa katikati ya hema ambalo Daudi aliliweka?

Kisha wakatoa sadaka ya kuteketeza na sadaka ya ushirika

Nini Daudi alicho zambaza kwa kila Misraeli alipo maliza kuwabariki watu katika jina la Yahweh?

Alisambaza kwa kila mmoja kipande cha mkate, na kipande cha nyama, na keki ya mzabibu.

1 Chronicles 16:4-6

Nini Walawi walipangiwa kufanya walipo tumikia mbele za sanduku?

Walawi walipangiwa kusheherekea, kushukuru na kumsifu Yahweh, Mungu wa Israeli walipo tumika mbele za sanduku la Yahweh.

1 Chronicles 16:7-9

Nini Asafu na kaka zake walipangiwa kufanya?

Walipangiwa kuimba nyimbo ya shukurani kwa Yahweh.

Nini watu walikuwa wazungumzie kuhusu kwenye nyimbo Asafu na kaka zake waliimba?

Walikuwa wazungumzie kuhusu matendo yote ya ajabu ya Yahweh.

1 Chronicles 16:10-11

Watu walikuwa wajisifu kuhusu nini na kutafuta?

Watu walikuwa wajisifu kuhusu Yahweh na kumtafute.

1 Chronicles 16:12-14

Kuhusu nini wazao wa Israeli, wateule wa Yahweh, wana paswa kukumbuka kuhusu Yahweh Mungu wao?

Wanapaswa kukumbuka matendo makuu aliyo fanya, miujiza yake na amri zake kutoka kinywa chake.

1 Chronicles 16:15-18

Nini Yahweh alichofanya na Ibrahimu ambacho Waisraeli wapaswa kuweka akilini milele?

Alifanya agano na Ibrahimu , na Waisraeli wana paswa kuweka agano la Yahweh akillini mwao milele.

Nini Yahweh aliaidi kuwapa watu wake kama urithi wao?

Yahweh aliahidi kuwapa nchi ya Kanani.

1 Chronicles 16:19-22

Yahweh alilindaje Israeli walipo kuwa wachache kiidadi na walipo kuwa wanaenda ufalme mmoja hadi mwingine?

Hakuwaruhusu yeyote awatese.

1 Chronicles 16:23-24

Nini watu wana paswa kukiri kwa mataifa wanapo imba kwa Yahweh na kutangaza wokovu wake siku hadi siku?

Wana paswa kukiri utukufu wake kwa mataifa, matendo yake makuu kwa mataifa yote.

1 Chronicles 16:25-27

Nina aliye fanya mbingu na wakusifiwa sana na wakuogopewa juu ya miungu mingine

ni Yahweh aliye umba mbingu na wakusifiwa sana, na ni wakuogopewa kuliko miungu yote.

1 Chronicles 16:28-29

Nini cha kupewa kwa Yahweh?

Utukufu na uwezo ni vya kupewa Yahweh.

1 Chronicles 16:30-31

Nini mataifa yatasema kuhusu Yahweh?

Mataifa yatasema, "Yahweh atawala"

1 Chronicles 16:32-35

Miti msituni itafanya nini mbele za Yahweh?

Miti misituni itapiga kelele mbele za Yahweh.

1 Chronicles 16:36-39

Kwa muda gani Yahweh, Mungu wa Israeli asifiwe?

Asifiwe kutoka milele na milele.

1 Chronicles 16:40-41

Nani alitoa amri na sheria zilizo andikwa kwa Israeli kwa jinsi sadaka za kuteketezwa zifanywe?

Yahweh alitoa amri na sheria ya kuandikwa kwa Israeli.

1 Chronicles 16:42-43

Sehemu gani watu na Daudi walirudi baada ya kusherehekea kuweka sanduku?

Watu wote walirudi nyumbani, na Daudi akarudi kubariki nyumba yake.

1 Chronicles 17

1 Chronicles 17:1-2

Nini kilimsumbua Daudi kuhusu wapi sanduku la agano la Yahweh lilikuwa la kaa?

Ilimsumbua Daudi kuwa sanduku la agano la Yahweh lilikuwa la kaa chini ya hema wakati Daudi alikuwa anaishi katika nyumba ya mierezi.

1 Chronicles 17:3-6

Nini Yahweh alimwambia Nathani aseme kwa Daudi kuhusu kumjengea Yahweh nyumba?

Mungu alisema Daudi hatamjengea nyumba Yahweh ya kuishi.

1 Chronicles 17:7-8

Kwanini Yahweh alimtoa Daudi kutoka malishoni na kufuata kondoo?

Alimtoa Daudi kutoka malishoni na kufuata kondoo ilikwamba awe mtawala wa watu wa Israeli.

Nini Yahweh alisema atafanya kwa ajili ya jina la Daudi?

Alisema ata mfanyia Daudi jina, kama jina la wakuu wa dunia.

1 Chronicles 17:9-10

Nani ambaye hatawatesa tena watu wa Israeli baada ya Yahweh kuwapa sehemu ya kuishi na kutosumbuliwa tena?

Watu wa ovu hawata watesa tena, kama walivyo fanya mwanzo.

1 Chronicles 17:11-12

Nini Yahweh alisema uzao wa Daudi utafanya baada ya siku za Daudi kutimia?

Uzao wa Daudi utajenga nyumba ya Yahweh.

1 Chronicles 17:13-15

Kwa muda gani Yahweh alisema kiti cha enzi cha uzao wa Daudi kitaimarishwa??

Kiti cha enzi cha uzao wa Daudi kitaimarishwa milele.

1 Chronicles 17:16-18

Nini Daudi alisema Yahweh amemfanyia kwasababu ya kile Yahweh alimuonyesha kuhusu vizazi vijavyo?

Alisema Yahweh amemheshimu na kumtambua kwa kipekee.

1 Chronicles 17:19-21

Nini Daudi anasema ni sababu Yahweh amewaokoa watu wake kutoka Misri na kujifanyia watu wake?

Yahweh aliwaokoa kutoka Misri iliwawe watu wake, kujifanyia jina lake kwa matendo makuu na yahajabu.

1 Chronicles 17:22-24

Nini Daudi anamuomba Yahweh afanye kuhusu ahadi aliyo ifanya kwa Daudi kwa habari ya kuimarisha familia ya Daudo milele?

Daudi anamuomba Yahweh afanye kama alisema.

1 Chronicles 17:25-27

Nini Yahweh aliahaidi kufanya kwa nyumba ya mtumishi wake Daudi?

Yahweh aliahaidi kubariki nyumba ya mtumishi wake Daudi na itabarikiwa milele.

1 Chronicles 18

1 Chronicles 18:1-2

Makundi gani mawili Daudi alishambulia na kuyashinda?

Alishambulia na kuwashinda Wafilisti na wa Moabu.

1 Chronicles 18:3-4

Nini Daudi alifanya kwa magari ya farasi mia yaliyo achwa baada ya kujeruhi farasi aliyo kamata kwa Hadadezeri?

Alihifadhi baadhi kwa ajili ya magari ya farasi mia moja.

1 Chronicles 18:5-6

Nini Daudi aliweka kwa Aramu wa Damasko baada ya kuua wa Aramia elfu ishirini na mbili?

Daudi aliweka vikosi huko Aramu ya Damasko.

1 Chronicles 18:7-8

Nini Daudi alichukuwa kutoka kwa Hadadezeri ambacho Sulemanii alitumia badae kufanya vifaa vya hekalu?

Daudi alichukuwa shaba nyingi sana kutoka kwa Hadadezeri.

1 Chronicles 18:9-11

Nini mfalme Daudi alifanya na fedha, dhahabu na shaba ambavyo Hadoramu alileta kwa Daudi kutoka Toi, mfalme wa Hamathi na fedha na dhahabu alivyo beba kutoka kwa mataifa yote?

Daudi alivitenga hivi vitu kwa ajili ya Yahweh.

1 Chronicles 18:12-13

Nini kilitokea kwa wa Edomi wote baada ya pambano ambalo Abishai aliua wa Edomi 18,000?

Waedomi wote wakawa watumishi wa Daudi.

1 Chronicles 18:14-17

Nani alikuwa wa shauri wakuu wa Mfalme Daudi alipo tawala Israeli na kutenda haki na utaua kwa watu wake wote?

Wana wa Daudi walikuwa washauri wakuu wa mfalme.

1 Chronicles 19

1 Chronicles 19:1-3

Kwanini Daudi alitaka kuonyesha ukarimu kwa Hanuni mwana wa Nahashi, mfalme wa watu wa Amoni baada ya baba yake kufa?

Baba wa Hanuni alikuwa mkarimu kwa Daudi.

Viongozi wa Amoni waliamini kwamba Daudi alikuwa anajaribu kumfariji Hanuni wakati watumishi wa Dauidi walipo kuwa wakiingia nchini?

Viongozi walidhani watumishi wa Daudi wanakuja kutathimini na kuchunguza nchi yao ili Daudi aweze kupindua nchi yao.

1 Chronicles 19:4-5

Nini Hanuni alifanya kwa watumishi wa Daudi kusababisha watumishi wapatwe na fedhea sana?

Aliwanyoa na kukata mavazi yao kiunoni.

1 Chronicles 19:6-7

Kwanini Waamori walikodisha magari ya farasi na wapanda farasi?

Walikodisha magari ya farasi na wapanda farasi kujianda kwa vita kwasababu walikuwa kikwazo kwa Daudi.

1 Chronicles 19:8-9

Nani Daudi alimtuma alipo sikia Waamoni wanajianda kwa vita?

Daudi alimtuma Yoabu na jeshi lake lote.

1 Chronicles 19:10-11

Jinsi gani Yoabu alipanga kwa kupigana na Waamoni alipo ona misitari yao ya pambano?

Yoabu alichagua wapambanaji shupavu wa Israeli na kuwa panga dhidi ya Waaremi na kumpa amri kaka yake kupigana na Waamoni pamoja na jeshi lote.

1 Chronicles 19:12-13

Nini Yoabu alimwambia kaka yake?

Yoabu akamwambia kaka yake kuwa wasaidiane kutakapo itajika, na wawe hodari kwasababu Yahweh atafanya kilicho chema kwa watu wake.

1 Chronicles 19:14-15

Kwanini jeshi la Waamoni lilikimbia kwa mji wao?

Jeshi la Waamoni liliona kwamba Waarami limekimbia jeshi la Waisraeli, na hivyo wakambia kwa mji wao.

1 Chronicles 19:16-17

Kwanini Daudi alikusanya Israeli yote pamoja na kuwapanga kwa ajili ya vita dhidi ya Waaremi?

Daudi alisikia kwamba Waaremi wametuma usaidizi.

1 Chronicles 19:18-19

Kwanini watu wa Aramu hawakutaka tena kuwasaidia Waamoni?

hawakuwa tayari kuwasaidia Waamoni walipo ona Daudi ameua wanaume wao elfu 47 na mkuu wajeshi.

1 Chronicles 20

1 Chronicles 20:1

Nini Yoabu alifanya Daudi alipo baki Yerusalemu?

Yoabu akaongaza jeshi kwenda kupambana na kusikitisha nchi ya Waamoni, na kuishambulia Raba na kuishinda.

1 Chronicles 20:2-5

Baada ya kuchukuwa taji kutoka kwenye kichwa cha mfalme na kuweka kwake, nini Daudi aliwalazimisha watu kufanya?

Aliwalazimisha kufanya kazi ngumu.

1 Chronicles 20:6-8

Wazao wa Refaimu walipo dhihaki jeshi la Israeli nini kilitokea?

Waliuawa na Daudi na jeshi lake.

1 Chronicles 21

1 Chronicles 21:1-3

Kwanini Daudi aliamua kuhesabu watu wa Israeli?

Adui akainuka dhidi ya Israeli, na Daudi akataka kujua wangapi wapo kwenye jeshi lake.

Yoabu alijibu nini kwa ombi la Daudi la kuhesabu watu?

Alitoa sema litaleta hatia kwa Israeli.

1 Chronicles 21:4-5

Nini Yoabu alifanya mfalme alipo muamuru kwenda na kuhesabu watu?

Alienda na kurudisha idadi ya jumla ya wanaume waliyo weza kupigana.

1 Chronicles 21:6-10

Mungu alijibu nini kwa Daudi kuhesabu wanajeshi wa Israeli?

Mungu alikwazika na kushambulia Israeli.

1 Chronicles 21:11-12

Chaguzi gani tatu Yahweh alimpa Daudi?

Daudi aliweza chagua miaka mitatu ya ukame, miezi mitatu ya kutafutwa na maadui zake, au siku tatu za upanga wa Yahweh.

1 Chronicles 21:13-15

Daudi alichagua adhabu gani kati ya tatu?

Alichagua siku tatu za upanga wa Yahweh.

Nini ilikuwa matokeo ya uchaguzi wa Daudi?

Yahweh akatuma pigo Israeli, na watu wakafa. Mungu akatuma malaika Yerusalemu kuiharibu, lakini Yahweh akabadilisha nia yake.

1 Chronicles 21:16-17

Daudi alimuona malaika na upanga, alifanya nini?

Alimwambia Mungu amuadhibu yeye na familia yake, lakini asiadhibu watu wa Mungu.

1 Chronicles 21:18-20

Nini Daudi aliamuriwa kufanya eneo la kupeta la Orinani?

Alikuwa ajenge madhabahu kwa ajili ya Yahweh.

Jinsi gani Orinani alifanya alipo muona malaika?

Yeye na wanae wa nne walijificha.

1 Chronicles 21:21-22

Orinani alipo kutana na Daudi, nini Daudi alimuomba?

Alimuomba Orinani amuuzie eneo la kupeta.

1 Chronicles 21:23-24

Nini Orinani alimpa Daudi naye akakataa?

Alimpa eneo la kupeta, ng'ombe, na ngano.

1 Chronicles 21:25-27

Baada ya Daudi kununua eneo la kupeta na kujenga madhabahu, jinsi gani Yahweh alijibu maombi yake?

Yahweh alimjibu kwa moto kutoka mbinguni kwenye madhabahu na kumuambia malaika kuweka kando upanga wake.

1 Chronicles 21:28-30

Kwanini Daudi hakwenda sehemu ya juu ya Gibeoni?

Daudi aliogopa upanga wa malaika wa Yahweh.

1 Chronicles 22

1 Chronicles 22:1-2

Baada ya Daudi kutangaza wapi nyumba ya Yahweh itajengwa, nini aliwaambia watumishi wake kufanya?

Aliwaamuru watafute wageni wanao ishi kwenye nchi ya Israeli na kuwapa kazi kama wachonga mawe wa nyumba ya Mungu.

1 Chronicles 22:3-5

Maandalizi gani Daudi alifanya ya kujenga nyumba ya Yahweh kabla ya kufa?

Alitoa kiasi kikubwa cha chuma, shaba na mierezi.

1 Chronicles 22:6-8

Kwanini Daudi alimwambia Sulemani anamuamuru ajenge nyumba ya Yahweh?

Yahweh alimwambia Daudi kwamba hatakuwa yeye wakujenga nyumba kwasababu ya umwagaji wa damu.

1 Chronicles 22:9-10

Nini Yahweh alimwambia Daudi atafanya kwa mwana wake?

Atampa pumziko na maadui zake wote kila upande, na kuimarisha ufalme wa Sulemani juu ya Israeli milele.

1 Chronicles 22:11-13

Nini Daudi alimwambia Sulemani azingatia kwa ukaribu?

Alimwambia Sulemani atii maagizo na amri Yahweh alizo mpa Musa kuhusu Israeli.

1 Chronicles 22:14-16

Nini Daudi alimwambia Sulemani afanye na vifaa vyote Daudi alivyo viandaa kwa nyumba ya Yahweh?

Alimwambia Sulemani aongeze zaidi.

1 Chronicles 22:17-19

Nini Daudi alimwambia Sulemani ainuke na kufanya?

Alimwambia Sulemani ainuke na kujenga sehemu takatifu ya Yahweh Mungu.

1 Chronicles 23

1 Chronicles 23:1-3

Nini baadhi ya vitu vya mwisho Daudi alifanya kama mfalme wa Israel?

Daudi alimfanya Sulemani mfalme kwenye sehemu yake, na akahesabu Walawi waliyo na miaka sio chini ya thelathini.

1 Chronicles 23:4-11

Kazi gani Daudi aliwapa Walawi?

Akawatenganisha kwenye vikundi kusimamia kazi ya nyumba ya Yahweh, aaskari na waamuzi, walinzi, na wengine wamsifu Yahweh kwa vyombo.

1 Chronicles 23:12-23

Nini Aruni na uzao wake walichaguliwa kufanya daima?

Aruni alichaguliwa kuandaa vitu vitakatifu, yeye na uzao wake watatoa uvumba kwa Yahweh, kumtumikia na kumpa baraka kwa jina lake.

1 Chronicles 23:24-29

Kwanini Walawi hawataitajika tena kubeba hema la kukutani?

Yahweh aliwapa sehemu ya kudumu Yerusalemu.

1 Chronicles 23:30-32

Muda gani Walawi walichukuwa kumshukuru na kumsifu Yahweh?

kila asubui wali mshukuru na kumsifu na jioni, alipo teketeza sadaka, Sabato, sherehe na siku za maakuli.

1 Chronicles 24

1 Chronicles 24:4-18

Mbinu gani walitumia kugawanya makuhani kwa huduma ya sehemu takatifu?

Waliwachaguwa kwa kura bila upendeleo.

1 Chronicles 24:19-28

Utaratibu upi uzao wa Aruni ulipaswa kuingia nyumba ya Yahweh?

Walielekezwa na Yahweh kuja nyumbani mwake kwa utaratibu maalumu.

1 Chronicles 24:29-31

Kwa utamaduni gani uzao wa Aruni ulishiriki?

Walirusha kura katika uwepo wa mfalme.

1 Chronicles 25

1 Chronicles 25:1-5

Nini wana wa Asafu, Hemani Yeduthuni walifanya na vinubi, vyombo vya uzi, na patu?

Hawa wanaume walitoa unabii kwa vinubi, vyombo vya uzi, na patu.

Kwanini wana wa Yeduthuni walicheza vinubi

Walicheza vinubi kutoa shukurani na sifa kwa Yahweh.

Nini Mungu alimpa Hemani ili kuheshimu?

Mungu alimpa wana kumi na nne na mabinti wa tatu.

1 Chronicles 25:6-31

Wana muziki gani walijumuishwa walipo rusha kura kwa kazi zao?

Wote walirusha kura kwa kazi zao, wadogo kwa wakubwa, walimu kwa wanafunzi.

1 Chronicles 26

1 Chronicles 26:7-9

Wana na ndugu wa Obedi Edomu walikuwa na uwezo wa kufanya nini?

Walikuwa wanaume wenye nguvu ya kufanya kazi zao katika huduma ya sehemu ya kukutania.

1 Chronicles 26:10-11

Shimiri alikuwaje kiongozi japo kuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza?

Japo hakuwa mzaliwa wa kwanza, baba yake alimfanya kiongozi.

1 Chronicles 26:12-14

Wapi walinzi walikuwa na wajibu wa kutumika?

Walikuwa na wajibu wa kutumika katika nyumba ya Yahweh.

1 Chronicles 26:15-19

Wana wa Obedi Edomu walipangiwa nini kuongezea lango la kusini?

Wana wake walipangiwa nyumba za ghala.

1 Chronicles 26:20-25

Nini Ahija alihusika katika nyumba ya Mungu?

alikuwa kiongozi wa hazina ya nyumba ya Mungu, na hazina ya vitu vilivyo wekwa wakfu.

1 Chronicles 26:26-28

Kwa kusudi lipi baadhi ya vitu vilivyo chukuliwa vitani vili wekwa wakfu na Daudi na wakuu?

Waliweka wakfu baadhi ya vitu vilivyo chukuliwa vitani kwa kurekebisha nyumba ya Yahweh.

1 Chronicles 26:29-32

Kwa yapi Kenania na wana wake walihusika kama maafisa na waamuzi?

Walihusika kwa mambo ya ndani ya Israeli kama maafisa na waamuzi.

1 Chronicles 27

1 Chronicles 27:1-22

Wakati gani kila kikosi cha jeshi kilitumika?

Walitumika mwenzi hadi mwezi kwa mwaka mzima.

Wanaume wangapi walikuwa kwenye kila kikosi cha jeshi?

Walikuwa wanaume 24,000 kila kikosi.

1 Chronicles 27:23-24

Kwanini Daudi hakuhesabu miaka ishirni na chini?

Hakuhesabu kwasababu Yahweh aliahidi kuongeza Israeli kama nyota za mbinguni.

1 Chronicles 27:25-27

Yonathani mwana wa Uzia aliwajibika juu ya nini?

Alikuwa juu ya nyumba za ghala katika mashamba, kwenye miji, na vijijini.

1 Chronicles 27:28-31

Aina gani za miti ilikuwa maeneo ya chini?

Miti ya mizaituni na mikuyu ili kuwa maeneo ya chini.

1 Chronicles 27:32-34

Kwanini Yonathani, mjomba wake Daudi alikuwa mshauri?

Alikuwa mshauri, maana alikuwa mwenye hekima na mwandishi.

1 Chronicles 28

1 Chronicles 28:2-3

Kwanini Mungu alisema Daudi hawezi kujenga hekalu kwa jina lake?

Mungu alisema hawezi kujenga kwasababu alikuwa mwanaume wa vita na amemwaga damu.

1 Chronicles 28:4-5

Nini Yahweh alimchagua Sulemani, mwana wa Daudi, kufanya juu ya Israeli?

Alimchagua Sulemani kuketi kweye kiti cha enzi cha ufalme wa Yahweh, juu ya Israeli.

1 Chronicles 28:6-7

Nini Yahweh alisema atafanya kwa Sulemani kama ata baki kutii amri zake?

Yahweh alisema ata imarisha ufalme wake milele.

1 Chronicles 28:8

Kama watu wote wangeshika amri za Yahweh, nini kingetokea kwenye nchi nzuri walikuwa nayo?

Wange miliki nchi nzuri na kuacha kama urithi kwa watoto wao baada yao milele.

1 Chronicles 28:9-10

Nini Yahweh anaelewa kuhusu kila wazo la mtu?

Anaelewa kila amasa ya mawazo ya watu.

Nini kitatokea kama Sulemani akimuacha Yahweh?

Yahweh ata mkataa daima.

1 Chronicles 28:11-12

Nini nyumba za ghala nyumbani mwa Mungu na hazina kuhifadhi?

Nyumba za ghala na hazina zilikuwa kwa ajili ya vitu vilivyo tengwa kwa hekalu.

1 Chronicles 28:13-17

Wapi makuhani na Walawi walipangiwa wajibu wa kutumika?

Wajibu wao walio pangiwami kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Yahweh.

1 Chronicles 28:18-19

Jinsi gani Daudi aliongozwa katika vitu vyote alivyo weka katika maandishi?

Yahweh alimuongoza na kumpa kufahamu kuhusu michoro.

1 Chronicles 28:20-21

Nini Daudi alimuahidi Sulemani kuhusu uwepo wa Yahweh hadi kazi zote zitakapo kuwa zimetimia?

Yahweh hatamuacha wala kumtelekeza hadi kazi yote ya huduma ya hekalu la Yahweh itakapo kamilika.

Wasimamizi na watu wote walikuwa tayari kufanya nini?

Walikuwa tayari kufuata amri za Sulemani.

1 Chronicles 29

1 Chronicles 29:1-2

Kwanini Daudi alisema kazi ya kujenga hekalu ni kubwa?

Kazi ni kubwa, kwa kuwa hekalu sio la watu, bali la Yahweh Mungu.

1 Chronicles 29:3-5

Kwanini Daudi alitoa hazina zake binafsi kwa ajili ya nyumba ya Mungu?

Alipendezwa na nyumba ya Mungu wake.

1 Chronicles 29:6-7

Aina gani za zawadi zilifanywa na viogozi wa familia za mababu?

Walifanya sadaka za hiari.

1 Chronicles 29:8-9

Kwanini watu walifurahia sadaka za hiari?

Walifurahi kwasababu walitoa kwa moyo wote kwa Yahweh.

1 Chronicles 29:10-11

Nini Daudi anasema ni ya Yahweh?

Yote yaliko katika mbingu na duniani ni ya Yahweh, pamoja na ufalme.

1 Chronicles 29:12-13

Jinsi gani Yahweh anaeza kufanya watu wakubwa na kuwapa uweza?

Ana nguvu na uwezo na anaweza kutoa nguvu kwa yeyote.

1 Chronicles 29:14-15

Nini Daudi alisema kuhusu vitu watu walivyo mpa Yahweh?

Vitu vyote vya toka kwake, na wamerudisha kwake vilivyo vyake.

1 Chronicles 29:16-19

Katika nini Mungu anajivunia akichunguza moyo?

Yahweh anachunguza moyo na kupendezwa na unyofu.

Nini kilimfanya Daudi awangalia kwa furaha watu wa Mungu waliyo kuwa hapo?

Aliangalia kwa furaha walipo toa zawadi kwa Yahweh.

1 Chronicles 29:20-21

Jinsi gani kusanyiko lilimbariki na kumuabudu Yahweh?

Kusanyiko lote lilimbariki Yahweh, na kuinamisha vichwa vyao na kumuabudu Yahweh.

1 Chronicles 29:22-23

Kwa mamlaka ya nani walimpaka mafuta Sulemani kuwa mtawala?

Walimpaka mafuta kwa mamlaka ya Yahweh.

1 Chronicles 29:24-28

Kwa jinsi gani Yahweh allimbariki Sulemani mbele ya Israeli yote?

Kumkirimia nguvu kubwa kuliko mfalme yeyote aliyetangulia kabla yake Israeli.

1 Chronicles 29:29-30

Falme zipi zilihathirika na mafanikio ya Daudi, kwa kuongezea kwa Israeli?

Manabii walinakili mafanikio yake na matukio yaliyo hathiri falme zote za nchi nyingine.