Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

James

James 1

James 1:1-3

Yakobo aliandika Waraka huu kwa nani?

Yakobo aliandika Waraka huu kwa makabila kumi na mbili waliotawanyika.

Wanapopitia magumu, ni tabia gani Yakobo amewaambia wanaposwa kuwa nayo?

Yakobo amewaambia wanapaswa kuwa na furaha wanapopitia matatizo.

Kujaribiwa kwa imani kunaleta matunda gani?

Kujaribiwa kwa imani yetu kunasababisha kuvumilia.

James 1:4-5

Kujaribiwa kwa imani yetu kunaweza kuleta matokeo gani?

Kujaribiwa kwa imani yetu huleta matokeo ya uvumilivu na kukomaa.

James 1:6-8

Ni jambo gani ambalo mtu anayeomba kwa mashaka hutegemea kupokea?

Yule anayeomba kwa mashaka, asitegemee kupokea cho chote kutoka kwa Bwana.

James 1:9-11

Kwa nini mtu tajiri anatakiwa ajinyenyekeze?

Mtu tajiri anapaswa ajinyenyekeze kwa sababu atatoweka kama maua.

James 1:12-13

Wale wanaopita mtihani wa imani watapokea nini?

Wale watakaopita mtihani wa imani watapokea taji ya uzima.

James 1:14-16

Kitu gani kinasababisha mtu kujaribiwa na uovu?

Tamaa mbaya ya mtu ndiyo humsababisha kujaribiwa na uovu.

Ni nini matokeo ya dhambi iliyokomaa?

Matokeo ya kukomaa kwa dhambi ni mauti.

James 1:17-18

Ni kitu gani hushuka kutoka kwa Baba wa mianga?

Kila zawadi iliyo njema, kila zawadi iliyo kamili hushuka kutoka kwa Baba wa mianga.

Kwa njia gani Mungu alitumia kutupa maisha?

Mungu alitupa maisha kwa kyumia neno la kweli.

James 1:19-21

Nini Yakobo anatuambia kufanya juu ya kusikia, kuongea na hisia zetu?

Yakobo anatuambia tuwe wepesi wa kusikia, siyo wepesi wa kuongea wala kukasirika.

James 1:22-25

Kwa namna gani Yakobo anasema tunaweza kujidanganya wenyewe?

Yakobo anasema tunaweza kujidanganya wenyewe kwa kuwa wasikiaji wa Neno na si watendaji.

James 1:26-27

Kitu gani kinapaswa kutawaliwa ili tupate kuwa wenye dini wa kweli?

Ulimi unapaswa kutawaliwa ili tupate kuwa watu wa dini wa kweli.

Dini iliyosafi na isiyoharibiwa mbele za Mungu ni ipi?

Dini iliyo safi na isiyoharibiwa mbele za Mungu ni kuwasaidia yatima na wajane na kujilinda wenyewe na ufisadi wa dunia.

James 2

James 2:1-4

Je Yakobo anawaambia ndugu wasifanye nini wakati wanapomwona mtu akiingia katika mkutano?

Anawambia ndugu wasimpendelee mtu kwa sababu ya muonekano wake.

James 2:5-7

Je Yakobo anasema nini kuhusuuchaguzi wa Mungu kwa masikini?

Yakobo anasema Mungu aliwachagua masikini wa dunia ili wawe matajiri katika imani na kurithi ufalme aliowaahidia wampendao.

Yakobo anasema matajiri walikuwa wanafanya nini?

Yakobo anasema matajiri walikuwa wanawadharau ndugu zao na kulitukana jina la Mungu.

James 2:8-9

Ni sheria gani ya kifalme ya maandiko?

Mpende jirani yako kama unavyojipenda

James 2:10-11

Kila avunjae sheria ya Mungu anahatia kwa kitu gani?

Kila avunjae sheria moja anahatia ya kuvunja zote.

James 2:12-13

Ni kitu gani kinakuja kwa wale wasioonesha huruma?

Hukumu isiyo na huruma inakuja kwa wale wasio na huruma.

James 2:14-17

Je Yakobo anasema nini kwa wale wanaosema wanayo imani, lakini hawawasaidii wahitaji?

Yakobo anasema kuwa wale wanaosema wana imani lakini hawawasaidii wenye uhitaji, wana imani ambayo haitawasaidia.

Imani ni nini isipokuwa na matendo?

Imani pekee bila matendo imekufa.

James 2:18-20

Yakobo ansema tunapaswa kuonyesha imani yetu kwa jinsi gani?

Yakobo anasema imani yetu inapaswa iendane na matendo.

Ni kitu gani ambacho wanaamini watu wenye imani na mapepo?

Mapepo na watu wenye imani wote wanaamini kuwa kuna Mungu mmoja.

James 2:21-24

Je Ibrahimu alionyesha imani yake kwa jinsi gani?

Ibrahimu alionyesha imani yake kwa kumtoa mwanawe Isaka.

Ni maandiko gani yalitimia kutokana na imani ya Abrahamu na matendo?

Maandiko yaliyotimia yalikuwa yanasema "Abrahamu alimwamini Munguna alionekana kuwa mwenye haki."

James 2:25-26

Je Rahabu alionyesha imani yake kwa jinsi gani?

Rahabu alionyesha imani yake kwa kuwakaribisha wajumbe walikwenda kuwapeleka kwa kutumia barabara nyingine.

Jei mwili ni nini bila roho?

Mwili bila roho umekufa.

James 3

James 3:1-2

Kwa nini Yakobo husema kwamba walimu hawapaswi kuwa wengi?

Walimu hawapaswi kuwa wengi kwa sababu watapokea hukumu iliyo kuu.

Nani hujikwaa, na mara ngapi?

Wote tunajikwaa mara nyingi.

Ni mtu gani anayeweza kuudhibiti mwili wake wote?

Mtu mkamilifu anaweza kuudhibiti mwili wake wote.

James 3:3-4

Ni mifano gani miwili ambao Yakobo anatumia ili kufafanua jinsi kitu kidogo kinavyoweza kuongoza kitu kikubwa?

Yakobo anatumia mifano ya rijamu ya farasi na usukani wa meli.

Ni mifano gani miwili ambao Yakobo anatumia ili kufafanua jinsi kitu kidogo kinavyoweza kuongoza kitu kikubwa?

Yakobo anatumia mifano ya rijamu ya farasi na usukani wa meli.

James 3:5-6

Ni kitu gani ambacho ulimi wenye dhambi unaweza kufanya kwa mwili mzima?

Ulimi wenye dhambi unaweza kuunajisi mwili wote.

James 3:7-8

Ni kitu gani ambacho binadamu hawezi kukudhibiti?

Ulimi ni kitu ambacho hamna mtu anayeweza kudhibiti.

James 3:9-12

Vitu gani viwili vinaweza kutoka katika kinywa kimoja?

Baraka na laana vyote viwili vyatoka katika kinywa kimoja.

James 3:13-14

Jinsi gani mtu anaweza kufafanua hekima na ufahamu?

Mtu hufafanua hekima na ufahamu kwa kazi anazofanya katika unyenyekevu.

James 3:15-18

Ni mtazamo gani unafanana na hekima ya duniani, isiyo ya kiroho na ya kipepo?

Mtu mwenye wivu na ubinafsi ana hekima ya duniani, isiyo ya kiroho na ya kipepo.

Ni mtazamo gani unafanana na hekima kutoka juu.

Mtu anayependa amani, mkarimu na mwenye matunda mema, asiye na upendeleo na mkweli huyo ana hekima kutoka juu.

James 4

James 4:1-3

Yakobo anasema ni nini chanzo cha ugonvi na migogoro?

Chanzo ni tamaa mbaya iliyopo ndani yao.

Kwa nini waamini hawapokei mahitaji yao toka kwa Mungu?

Kwa sababu wanaomba vitu vibaya ili vitumike kwa tamaa zao mbaya.

James 4:4-5

Kama mtu akiamua kuwa na urafiki na dunia hii, nini mahusiano ya mtu huyo na Mungu?

Mtu analiyeamua kuwa na urafiki na dunia amekuwa adui wa Mungu.

James 4:6-7

Mungu anawapinga watu gani na watu gani anawapa neema?

Mungu anawapinga wenye kiburi na kuwapa wanyenyekevu neema.

Ibilisi atafanya nini mtu anapojitoa kwa Mungu na kumpinga shetani.

Ibilisi atakimbia.

James 4:8-10

Mungu atawafanya nini wale wanaomkaribia?

Mungu atawkaribia wale wanaomkaribia.

James 4:11-14

Yakobo aliwaambia waamini wasifanye nini?

Yakobo aliwaambia waamini wasisemane wao kwa wao.

James 4:15-17

Yakobo aliwaambia waamini waseme nini juu ya mambo yatakayotokea baadae.

Yakobo aliwaambia waseme kuwa kama Mungu akiruhusu tuishi tutafanya hiki na kile.

Yakobo alisema nini juu ya wale wanaojivuna kuhusu mipango yao?

Yakobo anasema wale wanaojivuna juu ya mipango yao wanafanya uovu.

Mtu anapojua kufanya matendo mema na asifanye nini hutokea?

Mtu anapofahamu matendo mema na asifanye anakuwa ametenda dhambi.

James 5

James 5:1-3

Ni kitu gani ambacho Yakobo anakizungumzia kwa matajiri ambacho kitakuwa ushuhuda dhidi yao?

Matajiri wamekusanya hazina zao.

James 5:4-6

Matajiri wamewatendeaje watendakazi wao?

Matajiri hawa hawajawalipa watendakazi wao.

Ni kwa namna gani matajiri wanawatendea wenye haki?

Matajiri wanawahukumu na kuwauwa wenye haki.

James 5:7-8

Yakobo anasema nini kuhusu mtazamo wa muumini unavyo paswa kuwa kuhusiana na ujio wa Bwana?

Waumini wanapaswa kuungoja ujio wa Bwana kwa uvumilivu.

James 5:9-11

Ni tabia gani ambayo Yakobo anaisema tunapaswa kuiiga toka kwa manabii wa agano la kale?

Tunapaswa kuiga uvumilivu na uimara katika mateso.

James 5:12

Yakobo anasema nini juu ya uaminifu wa "ndiyo"na "hapana" ya muumini?

"Ndiyo" ya muumini inapaswa kumaanisha "ndiyo" na hapana yake inapaswa kumaanisha "hapana."

James 5:13-15

Waginjwa wanapaswa kufanya nini?

Wagonjwa wanapaswa kuwaita wazee wawaombee na kuwapaka mafuta.

James 5:16-18

Mambo gani mawili Yakobo anasema waumini wanapaswa kufanyiana ili wapate kuponywa?Yakobo anasema nini mfano wa Eliya unao tuonesha sisi juu ya maombi?

Waumini wanapaswa kuungama dhambi wao kwa wao na kuombeana. Mfano wa Eliya hutuonesha sisi kwamba maombi ya mtu mwenye haki huleta matokeo makubwa.

James 5:19-20

Ni kitu gani mtu atapata baada ya kumuongoza mwenye dhambi kutoka kwenye njia zake mbaya?

Mtu anayemuongoza mwenye dhambi toka kwenye njia zake mbaya na kumuokoa roho yake na mauti atafunika wingi wa dhambi.