Kiswahili: translationQuestions

Updated ? hours ago # views See on DCS Draft Material

Judges

Judges 1

Judges 1:1-3

Ni nani atakayewaongoza watu wa Israeli walipokuwa wakienda kupigana na Wakaanani"

Yuda atawaongoza watu wa Israeli kupigana dhidi ya Wakaanani.

Judges 1:4-5

Watu wa Yuda walipigana dhidi ya nani?

Watu wa Yuda walipigana dhidi yaa Adoni Bezeki.

Watu wa Yuda walipigana dhidi ya nani?

Watu wa Yuda walipigana dhidi yaa Adoni Bezeki.

Judges 1:6-7

Akina nani walikusanya chakula chini ya meza ya Adoni Bezeki?

Wafalme sabini ambao walivikata vidole gumba vyao na vidole vikubwa, walikusanya chakula chao chini ya meza ya Adoni Bezeki.

Judges 1:8-10

Ni lipi lilikuwa jina la awali la Hebroni?

Hebroni awali ilikuwa ikiitwa Kiriath Arba.

Judges 1:11-13

Kalebu alimpa nini Otinieli?

Kalebu alimpa Otinieli mtoto wake ili awe mke wa Otinieli.

Kalebu alimpa nini Otinieli?

Kalebu alimpa Otinieli mtoto wake ili awe mke wa Otinieli.

Judges 1:14-15

Kwa kuwa Aksa alikuwa Negevu, ni kitu gani alitaka baba yake ampe?

Kwa kuwa Aska alikuwa Negevu alitaka baba yake ampe chemchemi ya maji.

Judges 1:16-17

Jangwa la Yuda liko wapi?

Jangwa la Yuda lipo Negevu.

Judges 1:18-19

Kwa nini watu wa Yuda hawakuweza kuwafukuza wenyeji wa bonde?

Hawakuweza kuwafukuza wenyeji wa bonde kwa sababu wenyeji walikuwa na magari ya chuma.

Judges 1:20-24

Kwa nini Wayebusi waliishi na watu wa Benyamini huko Israeli?

Kwa sababu watu wa Benyamini hawakuwafukuza Wayebusi waliokuwa wenyeji wa Yerusalemu.

Judges 1:25-26

Nini kilitokea kwa yule mtu aliyewaonesha wapelelezi toka kwenye nyumba ya Yusufu namna ya kuingia Betheli?

Wapelelezi walimuacha yule mtu pamoja na familia yake waondoke na mtu yule akaenda katika nchi ya Wahiti, akajenga mji na akauita Luzu.

Nini kilitokea kwa yule mtu aliyewaonesha wapelelezi toka kwenye nyumba ya Yusufu namna ya kuingia Betheli?

Wapelelezi walimuacha yule mtu pamoja na familia yake waondoke na mtu yule akaenda katika nchi ya Wahiti, akajenga mji na akauita Luzu.

Judges 1:27-30

Waisraeli walipokuwa na nguvu waliwafanya nini Wakanaani?

Waisraeli walipokuwa na nguvu waliwalazimisha Wakanaani wawatumikie kwa kazi ngumu lakini hawakuwafukuza moja kwa moja.

Judges 1:31-33

Kwa nini kabila la Asheri liliishi pamoja na Wakaanani?

Kabila la Asheri liliishi pamoja na Wakaanani kwa sababu Waasheri hawakuwafukuza.

Judges 1:34-36

Nani aliwashinda Waamoni katika mlima Heresi huko Aiyaloni na Shaalbimu?

Nyumba ya Yusufu iliwashinda.

Judges 2

Judges 2:1-2

Malaika wa Bwana aliwapeleka wapi watu wa Israeli?

Malaika wa Bwana aliwapeleka wana wa Israeli katika nchi ambayo aliwaapia baba zao kuwa atawapa.

Judges 2:3-5

Malaika wa Bwana alipowaambia kuwa hatawafukuza Wakanaani mbele ya watu wa Israeli, walifanyaje?

Malaika alipowaambia kuwa hatawafukuza Wakanaani mbele ya watu Wa Israeli, walipiga kelele na kulia.

Malaika wa Bwana alipowaambia kuwa hatawafukuza Wakanaani mbele ya watu wa Israeli, walifanyaje?

Malaika alipowaambia kuwa hatawafukuza Wakanaani mbele ya watu Wa Israeli, walipiga kelele na kulia.

Judges 2:6-10

Ni kwa kipindi gani watu walimtumikia Bwana?

Watu walimtumikia Bwana kipindi cha maisha ya Yoshua na wazee walioendelea badala yake.

Judges 2:11-13

Ni miungu gani ambayo watu wa Israeli waliifata?

Watu wa Israeli waliifata miungu ya watu ambao waliwazunguka.

Judges 2:14-15

Bwana aliwaapia nini Waisraeli?

Bwana aliapa kuwa Waisraeli wakienda kupigana wakati wowote mkono wa Bwana hautakuwa pamoja nao.

Judges 2:16-17

Waamuzi walifanya nini?

Waamuzi waliwaokoa wana wa Israeli kutoka katika nguvu za wale waliokuwa wanawaibia wanachomiliki.

Judges 2:18-19

Nini kilitokea mwamuzi alipokufa?

Mwamuzi alipokufa wana wa Israeli waligeuka na kufanya mambo mabaya zaidi kuliko hata baba zao.

Judges 2:20-23

Kwa nini Bwana hakuondoa mbele ya Israeli taifa lolote ambalo Yoshua aliliacha baada ya kufa?

Bwana hakuondoa mbele ya Israeli taifa lolote ambalo Yoshua aliliacha baada ya kufa ili Bwana awajaribu Waisraeli na kujua kama watafuata njia za Bwana au hawatafuata.

Kwa nini Bwana hakuondoa mbele ya Israeli taifa lolote ambalo Yoshua aliliacha baada ya kufa?

Bwana hakuondoa mbele ya Israeli taifa lolote ambalo Yoshua aliliacha baada ya kufa ili Bwana awajaribu Waisraeli na kujua kama watafuata njia za Bwana au hawatafuata.

Judges 3

Judges 3:1-3

Kwa nini Bwana aliyaacha mataifa ili awajaribu Israeli?

Bwana aliyaacha mataifa ili kuwajaribu Israeli kwa kuwafundisha vita kizazi kipya cha Israeli ambacho hakikufahamu kabla.

Judges 3:4-6

Kwa nini Bwana alifanya hivyo kwa mataifa yaliyoachwa?

Bwana aliwajaribu Israeli kwa kuyaacha mataifa ili kuona kama watatii amri zake alizowapa babu zao kupitia Musa.

Judges 3:7-8

Waisraeli waliabudu nini?

Waisraeli waliabudu Baali na Asherah.

Judges 3:9-11

Bwana alimuinua nani ili akawasaidie wana wa Israeli?

Bwana alimuinua Othinieli mwana nwa Kehazi, ndugu mdogo wa Kalebu.

Judges 3:12-14

Nani alimpa nguvu Elgoni mfalme wa Moabu?

Bwana alimpa nguvu Elgoni mfalme wa Moabu.

Judges 3:15

Ni kipindi gani Bwana alimuinua Ehudi ili kuwasaidia wana wa Israeli?

Bwana alimuinua Ehudi kuwasaidia Waisraeli walipomuomba.

Judges 3:16-18

Ehudi alifunga wapi upanga wake?

Ehudi aliufunga upanga wake chingi ya nguo juu ya mguu wake wa kulia.

Judges 3:19-20

Nani alikuwa pamoja na Ehudi na mfalme wakati Ehudi anamwambia ujumbe?

Ehudi na mfalme tuu walikuwepo pale.

Nani alikuwa pamoja na Ehudi na mfalme wakati Ehudi anamwambia ujumbe?

Ehudi na mfalme tuu walikuwepo pale.

Judges 3:21-23

Kwa nini mafuta yalishikamana na upanga?

Mafuta yalishikamana na upanga kwa sababu Ehudi hakutoa upanga kwenye mwili wa mfalme.

Judges 3:24-25

Wakati watumishi wa mfalme walipoona milango ya chumba cha juu imefungwa, walifikiri nini?

Watumishi wa mfalme walipoona milango ya chumba cha juu imefungwa walihisi kuwa alikuwa akijitoa mwenyewe katika hali wa baridi ya chumba cha juu.

Judges 3:26-27

Ehudi alitoroka saa ngapi?

Watumishi walipokuwa wakisubiri na kuwaza wafanye nini Ehudi alitoroka.

Judges 3:28-30

Waisraeli waliwazuia kwa namna gani Wamoabu kuvuka mto?

Wana wa Israeli walivikamata vivuko vya Yordani toka kwa Wamoabu.

Judges 3:31

Shemgari aliwaua watu mia sita kwa kutumia nini?

Shemgari aliwaua Wafilisti kwa konzo la ng'ombe.

Judges 4

Judges 4:1-3

Kwa nini wana wa Israeli wamuomba Bwana msaada?

Wana wa Israeli waliomba msaada kwa Bwana kwa sababu Sisera alikuwa na magari ya farasi mia tisa na aliwashinda wana wa Israeli kwa nguvu kwa miaka ishirini.

Judges 4:4-5

Kwa nini wana wa Israeli waenda kwa Debora?

Wana wa Israeli walienda kwa Debora ili kutatua migogoro yao.

Judges 4:6-7

Mungu alisababisha Sisera akutane wapi na Baraka?

Mungu alisababisha Sisera akutane na Baraka karibu na mto Kishoni.

Judges 4:8-10

Kwa nini Bwana alisababisha mwanamke aishinde Sisera?

Bwana alisababisha mwanamke aishinde Sisera kwa sababu Baraka hakwenda bila Debora.

Kwa nini Bwana alisababisha mwanamke aishinde Sisera?

Bwana alisababisha mwanamke aishinde Sisera kwa sababu Baraka hakwenda bila Debora.

Judges 4:11-14

Mkeni alitoka kwenye uzao wa nani?

Mkeni alitoka kwenye uzao wa Hobabu, baba mkwe wa Musa.

Judges 4:15-16

Ni watu wangapi wa jeshi la Sisera waliopona?

Hakuna hata mmoja wa jeshi la Sisera aliyepona.

Judges 4:17-18

Kwa nini Sisera alienda kwenye hema ya Yaeli?

Sisera alienda kwenye hema ya Yaeli kwa sababu kulikuwa na amani kati ya Yabini mfalme wa Hazori na nyumba ya Heberi.

Judges 4:19-20

Sisera alipoomba maji Yaeli alimpa nini?

Sisera alipoomba maji Yaeli alimpa maziwa.

Judges 4:21-24

Yaeli alimuua vipi Sisera?

Yaeli alikikita kigingi cha hema upande wa kichwa chake na kikapenya kushuka chini.

Judges 5

Judges 5:3-4

Ni wakati gani nchi ilitikisika?

Nchi ilitetemeka wakati Bwana alipotoka Seiri toka Edomu.

Judges 5:5-6

Ni njia gani ambayo watu waliotembea kwa miguu walitumia?

Walitumia njia za upepo.

Judges 5:7-8

Ni kitu gani hakikuonekana kati ya watu elfu arobaini nchini Israeli?

Ngao wala mkuki havikuonekana kwa watu elfu arobaini wa Israeli.

Judges 5:9-11

Ni kitu gani kilitumika kuwekwa juu ya punda mweupe?

Mazulia yaliwekwa juu ya punda mweupe.

Judges 5:12-14

Watu wa Bwana walienda chini kwa nani?

Watu wa Bwana walienda chini kwa Debora kati ya mashujaa.

Judges 5:15-16

Isakari alifanya nini na Baraka?

Isakari alikwenda na Baraka bondeni chini ya amri yake.

Judges 5:17-18

Kit gani ambacho Zabuloni walihatarisha?

Zabuloni walihatarisha maisha yako mpaka kufikia kifo.

Judges 5:19-23

Kitu gani kilipigana na Sisera kutoka katika njia zao za mbinguni?

Nyota zilipigana na Sisera kutoka katika njia zao za mbinguni

Judges 5:24-25

Kwa nini malaika wa Bwana alimlaani Merozi?

Bwana alimlaani Merozi kwa sababu hakwenda kumsaidia Bwana.

Judges 5:26-27

Yaeli aliweka wapi mkono wake?

Yaeli aliweka mkono wake kwenye kigingi cha hema na mkono wake wa kulia katika nyundo ya mfanyakazi.

Judges 5:28-30

Mama yake Sisera aliangalia nje kupitia nini?

Mana yake na Sisera aliangalia nje kupitia dirisha lenye kamba.

Judges 5:31

Wale wanaompenda Bwana wanatakiwa wafanane na nini?

Wale wanaompenda Bwana wanatakiwa wafanane na jua linapoongezeka uwezo wake.

Judges 6

Judges 6:1-2

Wana wa Israeli walifanya nini kwa sababu ya Wamidiani?

Kwa sababu ya Wamidiani wana wa Israeli alitengeneza kwa ajili yao wenyewe kutoka kwenye mabwawa katika milima, mapago na ngome.

Judges 6:3-4

Nini kilitokea kila mara Waisraeli walipopanda mazao yao?

Kila mara Waisraeli walipopanda mazao yao Wamidiani na Waamaleki na watu kutoka mashariki waliwavamia Waisraeli.

Judges 6:5-8

Wamidiani na Waamaleki wangapi walivamia?

Haikuwezekana kuwahesabu.

Judges 6:9-10

Waisraeli waliishi kwenye nchi ya nani?

Waisraeli waliishi kwenye nchi ya Waamoni.

Judges 6:11-12

Kwa nini Gideoni alitenganisha ngano katika sakafu katika vikapu vya divai?

Gideoni alitenganisha ngano katika sakafu katika vikapu vya divai ili kuificha toka kwa Wamidiani.

Judges 6:13

Gideoni alifikiri kuwa Bwana aliwafanyia nini watu wa Israeli?

Gideoni alifikiri kuwa Bwana aliwaacha na kuwatia mikononi mwa Midiani.

Judges 6:14-15

Kwa nini Gideoni alifikiri kuwa asingeweza kuwaokoa Waisraeli?

Gideoni alifikiri kuwa asingeweza kuwaokoa Waisraeli kwa sababu familia yake ni dhaifu zaidi katika Manase na hakuwa muhimu katika nyumba ya baba yake.

Judges 6:16-18

Kwa nini Bwana alimsubiria Gideoni?

Bwana alimsubiria Gideoni ili ampe zawadi.

Judges 6:19-20

Ni wapi malaika wa Bwana alimwambia Gideoni aweke nyama na mikati isiyotiwa chachu?

Bwana alimwambia Gideoni aweke nyama na mikati isiyotiwa chachu katika mwamba.

Judges 6:21

Nini kilitokea baada yamalaika Bwana aliposhika ncha ya fimbo mkononi mwake?

Malaika wa Bwana aliposhika ncha ya fimbo mkononi mwake akagusa nyama na mikate isiyotiwa chachu; moto ukatoka nje ya mwamba, ukateketeza nyama na mikate isiyotiwa chachu.

Judges 6:22-24

Kwa nini Gideoni aliogopa alipofahamu kuwa amemuona malaika wa Bwana?

Gideoni aliogopa alipofahamu kuwa amemuona malaika wa Bwana kwa sababu alifikiri kuwa atakufa.

Kwa nini Gideoni aliogopa alipofahamu kuwa amemuona malaika wa Bwana?

Gideoni aliogopa alipofahamu kuwa amemuona malaika wa Bwana kwa sababu alifikiri kuwa atakufa.

Judges 6:25-26

Bwana alimwambia Gideoni ajenge nini juu ya mahali pa kukimbilia?

Bwana alimwambia Gideoni ajenge madhabahu nini juu ya mahali pa kukimbilia

Judges 6:27-29

Kwa nini Gideoni alifanya alichoambiwa afanye na Bwana wakati wa usiku?

Gideoni alifanya alichoambiwa afanye na Bwana wakati wa usiku kwa sababu aliogopa sana watu wa nyumba ya baba yake na watu wa mji kufanya hivyo wakati wa mchana.

Judges 6:30

Kwa nini watu wa mji walitaka kumuua Gideoni?

Kwa nini watu wa mji walitaka kumuua Gideoni kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali, na kwa sababu ameikata Ashera karibu nayo.

Judges 6:31-35

Kwa nini Gideoni aliitwa, "Yerubaali"?

Gideoni aliitwa, "Yerubaali" kwa sababu alisema, "Baali ajijitetee dhidi yake," kwa sababu Gidioni alivunja madhabahu ya Baali.

Judges 6:36-37

Gideoni alifanya nini ili kugundua kwamba Bwana alikusudia kumtumia kuikomboa Israeli?

Gideoni aliweka ngozi ya samazi kwenye sakafu na akasema kuwa Ikiwa kuna umande tu juu ya ngozi, na ni kavu duniani, basi angegundua kuwa Bwana amekusudia kumtumia kuikomboa Israeli.

Gideoni alifanya nini ili kugundua kwamba Bwana alikusudia kumtumia kuikomboa Israeli?

Gideoni aliweka ngozi ya samazi kwenye sakafu na akasema kuwa Ikiwa kuna umande tu juu ya ngozi, na ni kavu duniani, basi angegundua kuwa Bwana amekusudia kumtumia kuikomboa Israeli.

Judges 6:38-40

Gideoni alipokamua ngozi na akatoa umande kwenye ngozi ni kiasi gani cha maji kilikuwepo pale?

Gideoni alipokamua ngozi na akatoa umande kwenye ngozi kulikuwa na maji yaliyotosha kujaza bakuli.

Judges 7

Judges 7:2-3

Kwa nini Bwana aliwarudisha askari waliokuwa wanaogopa?

Bwana aliwarudisha askari waliokuwa wanaogopa ili Israeli wasijisifu juu yake wakisema, "Nguvu zetu zimetuokoa."

Kwa nini Bwana aliwarudisha askari waliokuwa wanaogopa?

wana aliwarudisha askari waliokuwa wanaogopa ili Israeli wasijisifu juu yake wakisema, "Nguvu zetu zimetuokoa."

Judges 7:4

Kwa nini Bwana alimwambia Gideoni awapeleke askari kwenye maji?

Bwana alitaka idadi ya askari iwe ndogo kwa kumwambia Gideoni ni nani wa kwenda naye.

Judges 7:5-6

Bwana alimwambia Gideoni awatenganishe vipi askari?

Bwana alimwambia Gideoni amtenganishe kila mtu atakayelamba maji kama mbwa alambavyo.

Judges 7:7-8

Askari wangapi ambao Gideoni aliwaweka?

Gideoni aliwaweka askari mia tatu na akawarudisha wengine nyumbani.

Askari wangapi ambao Gideoni aliwaweka?

Gideoni aliwaweka askari mia tatu na akawarudisha wengine nyumbani.

Judges 7:9-12

Ikiwa Gideoni ataogopa, ni kitu gani kiliimarisha ujasiri wake?

Ikiwa Gideoni ataogopa aliambiwa ashuke chini kwenye kambi na asikilize kile wanachosema na ujasiri wake utaimarishwa kushambulia kambi.

Ikiwa Gideoni ataogopa, ni kitu gani kiliimarisha ujasiri wake?

Ikiwa Gideoni ataogopa aliambiwa ashuke chini kwenye kambi na asikilize kile wanachosema na ujasiri wake utaimarishwa kushambulia kambi.

Judges 7:13-14

Mtu mmoja alipokuwa akimwambia ndoto mwenzake, mwenzake alimwambia kuwa ndoto ilikuwa inahusu nini?

Mtu mmoja alipokuwa akimwambia ndoto mwenzake, mwenzake alimwambia kuwa ndoto ilikuwa inamhusu Gideoni. Mungu amempa ushindi juu ya Wamidiani na jeshi lake.

Mtu mmoja alipokuwa akimwambia ndoto mwenzake, mwenzake alimwambia kuwa ndoto ilikuwa inahusu nini?

Mtu mmoja alipokuwa akimwambia ndoto mwenzake, mwenzake alimwambia kuwa ndoto ilikuwa inamhusu Gideoni. Mungu amempa ushindi juu ya Wamidiani na jeshi lake.

Judges 7:15-18

Gideoni aliwapa askari wake mia tatu kitu gani?

Aliwapa tarumbeta zote na mitungi tupu, na taa ndani ya kila mtungi.

Judges 7:19-21

Ni wakati gani askari wa Gideoni walipiga tarumbeta na kuvunja mitungi iliyokuwa mikononi mwao?

Wamidiani walipokuwa wakibadilidha ulinzi askari wa Gideoni walipiga tarumbeta na kuvunja mitungi iliyokuwa mikononi mwao

Judges 7:22-23

Askari walipopiga tarumbeta mia tatu Bwana alifanya nini?

Askari walipopiga tarumbeta mia tatu Bwana akaweka upanga wa kila mtu wa Midiani dhidi ya wenzake na dhidi ya jeshi lake lote.

Judges 7:24-25

Mpaka wapi watu wa Efraimu walikusanyika pamoja na kumiliki maji?

Watu wa Efraimu walikusanyika kumiliki maji mpaka Bethbara na Mto Yordani.

Judges 8

Judges 8:1-3

Kwa nini watu wa Efraimu walilumbana na Gideoni?

Watu wa Efraimu walilumbana na Gideoni kwa sababu hawakuitwa walipoenda kupigana na Midiani.

Judges 8:4-5

Gideoni aliwaomba nini watu wa Sukoti?

Gideoni aliwaomba watu wa Sukoti mikate kwa ajili ya watu waliomfuata.

Judges 8:6-10

Kwa nini Gideoni aliwaambia watu wa Penueli kuwa ataangusha mnara?

Gideoni aliwaambia watu wa Penueli kuwa ataangusha mnara kwa sababu hawakumpa jeshi lake mkate kama vile watu wa Sukothi walivyokataa.

Judges 8:11-14

Kwa nini Gideoni alilishinda jeshi la adui Noba na Yogbena?

Gideoni alilishinda jeshi la adui kwa sababu hawakutegemea shambuli.

Judges 8:15-17

Gideoni alimuonesha nani kwa watu wa Sukothi kabla hajawaadhibu?

Gideoni alimuonesha Zeba na Salmuna kwa watu wa Sukothi kabla hajawaadhibu.

Gideoni alimuonesha nani kwa watu wa Sukothi kabla hajawaadhibu?

Gideoni alimuonesha Zeba na Salmuna kwa watu wa Sukothi kabla hajawaadhibu.

Judges 8:18-19

Ni watu wa aina gani ambao Zeba na Zalmuna walimuua huko Tabori?

Zeba na Zalmuna walimuua kaka yake na Gideoni.

Ni watu wa aina gani ambao Zeba na Zalmuna walimuua huko Tabori?

Zeba na Zalmuna walimuua kaka yake na Gideoni.

Judges 8:20-21

Kwa nini Yetheri hakutoa upanga wake?

Yetheri hakutoa upanga wake kwa sababu alikuwa anaogopa kwa kuwa alikuwa kijana mdogo.

Judges 8:22-23

Ni nani ambaye Gideoni alisema ataongoza Israeli?

Gideoni alisema kuwa Bwana ataongoza watu wa Israeli.

Judges 8:24-26

Gideoni aliwaomba nini watu wa Israeli?

Gideoni aliwaomba pete za nyara zao.

Judges 8:27-31

Gideoni alitengeneza nini toka kwenye pete?

Gideoni aliytengeneza Efodi toka kwenye pete.

Israeli walifanya nini na Efodi ya dhahabu?

Waisraeli waliiandama Efodi kwa ukahaba na kuiabudu.

Judges 8:32-35

Nini kilitokea baada ya Gideoni kufa?

Baada ya Gideoni kufa, watu wa Israeli waligeuka na kujifanyia ukahaba wenyewe kwa kuabudu Baali.

Judges 9

Judges 9:1-2

Nani alikuwa baba yake na Abimeleki?

Yerubaali alikuwa baba yake na Abimeleki.

Judges 9:3-4

Kwa nini ndugu wa mama yake na Abimeleki walikubali kumfuata Abimeleki?

Walikubali kumfuata kwa sababu alikuwa ndugu yao.

Abimeleki

Abimeleki alitumia vipande sabini vya fedha kuwaajiri watu wasio na sheria na waliokuwa wajinga.

Judges 9:5-6

Kwa nini Yotamu hakuuawa?

Yotamu hakuuawa kwa sababu alijificha.

Judges 9:7-16

Ni siku ipi ambayo Yotamu aliwaambia viongozi wa Shekemu?

Yotamu aliwaambia viongozi wa Shekemu siku hiyo hiyo waliyosimama dhidi ya nyumba ya baba yake na kuwaua watoto wake, watu sabini juu ya jiwe moja.

Judges 9:17-18

Ni siku ipi ambayo Yotamu aliwaambia viongozi wa Shekemu?

Yotamu aliwaambia viongozi wa Shekemu siku hiyo hiyo waliyosimama dhidi ya nyumba ya baba yake na kuwaua watoto wake, watu sabini juu ya jiwe moja.

Judges 9:19-21

Ikiwa watu wangefanya kwa uaminifu na uelekeve kwa Yerubaali na nyumba yake nini kingetokea?

Ikiwa watu wangefanya kwa uaminifu na uelekeve kwa Yerubaali na nyumba yake moto ungeshuka toka Abimeleki na kuteketeza watu wa Shekemu na nyumba ya Milo. Moto utashuka toka kwa watu wa Shekemu na Beth Milo na kuteketeza Abimeleki.

Ni nini laana ya Yothamu?

Laana ya Yothamu ilikuwa moto ungeshuka toka Abimeleki na kuteketeza watu wa Shekemu na nyumba ya Milo. Moto utashuka toka kwa watu wa Shekemu na Beth Milo na kuteketeza Abimeleki.

Judges 9:22-24

Kwa nini Mungu alituma roho mbaya kati ya Abimeleki na viongozi wa Shekemu?

Mungu alituma roho mbaya kati ya Abimeleki na viongozi wa Shekemu ili uhalifu uliofanywa kwa wana sabini wa Yerubaali uweze kulipizwa kisasi.

Kwa nini Mungu alituma roho mbaya kati ya Abimeleki na viongozi wa Shekemu?

Mungu alituma roho mbaya kati ya Abimeleki na viongozi wa Shekemu ili uhalifu uliofanywa kwa wana sabini wa Yerubaali uweze kulipizwa kisasi.

Judges 9:25-27

Viongozi wa Shekemu walitamani kumvamia nani?

Viongozi wa Shekemu walitamani kumwangamiza Abimeleki.

Judges 9:28-29

Nani alitamani kuwaamrisha watu?

Gaali alitamani kuwaamrisha watu.

Nani alitamani kuwaamrisha watu?

Gaali alitamani kuwaamrisha watu.

Judges 9:30-35

Kwa nini hasira ya Zebuli iliwaka?

Iliwaka aliposikia maneno ya Gaali.

Kwa nini Zebuli alituma wajumbe kwa Abimeleki?

Alituma wajumbe ili wamdanganye.

Judges 9:36-37

Zebuli aliwaelezea vipi watu waliokuwa vilimani?

Zebuli alisema kuwa kulikuwa na vivuli milimani.

Judges 9:38-43

Zebuli alimwambia Gaali afanye nini?

Zebuli alimwambia Gaali apigani dhidi ya Abimeleki.

Nini kilitokea baada ya Gaali kupigana na Abimeleki?

Abimeleki alimfukuza Gaali na Gaali akakimbia mbele yake akiwa na majeraha ya mauti mbele ya miingilio ya lango la jiji.

Judges 9:44-45

Abimeleki alifanya nini baada ya kuuteka mji?

Abimeleki alibomoa kuta za mji na kueneza chunvi juu yake.

Judges 9:46-47

Viongozi wa mnara wa Shekemu waliingia wapi?

Viongozi wa mnara wa Shekemu waliingia katika ngome ya El Berithi.

Judges 9:48-51

Ni kwa namna gani Abimeleki aliwaua viongozi wa mnara wa Shekemu?

Abimeleki alikwenda mlima Aalmoni akakata matawi wakayafunga juu ya ukuta wa mnara kisha wakawasha moto.

Ni kwa namna gani Abimeleki aliwaua viongozi wa mnara wa Shekemu?

Abimeleki alikwenda mlima Aalmoni akakata matawi wakayafunga juu ya ukuta wa mnara kisha wakawasha moto.

Judges 9:52-54

Ni nini kilimtokea Abimeleki alipokaribia mlango wa mnara wa Tabezi?

Abimeleki alipoukaribia mlango wa mnara wa Tabezi mwanamke alitupa jiwe la juu juu ya kichwa chake na ikampasua fuvu lake.

Ni nini kilimtokea Abimeleki alipokaribia mlango wa mnara wa Tabezi?

Abimeleki alipoukaribia mlango wa mnara wa Tabezi mwanamke alitupa jiwe la juu juu ya kichwa chake na ikampasua fuvu lake.

Kwa nini Abimeleki alimwambia kijana aliyekuwa anachukua silaha achukue uoanga wake na kumuua?

Abimeleki alimwambia kijana aliyekuwa anachukua silaha achukue upanga wake na kumuua ili mtu yeyote asije akasema kuwa mwanamke alimuua Abimeleki.

Judges 9:55-57

Nini ilikuwa laana ya Yothamu?

Laana ya Yothamu ilikuwa moto ungeshuka toka Abimeleki na kuteketeza watu wa Shekemu na nyumba ya Milo. Moto utashuka toka kwa watu wa Shekemu na Beth Milo na kuteketeza Abimeleki.

Judges 10

Judges 10:1-5

Shamiri ilikuwa wapi?

Shamiri ilikuwa katika mlima wa Efraimu.

Judges 10:6-7

Kwa nini hasira ya Bwana iliwaka juu ya watu wa Israeli?

Watu wa Israeli walimuacha Bwana na hawakumwabudu tena hivyo hasira yake ikawaka juu ya Israeli.

Kwa nini hasira ya Bwana iliwaka juu ya watu wa Israeli?

Watu wa Israeli walimuacha Bwana na hawakumwabudu tena hivyo hasira yake ikawaka juu ya Israeli.

Judges 10:8-12

Kwa nini Israeli walisumbuliwa sana?

Waamoni walivuka Yordani kupigana na Yuda dhidi ya Benyamini na nyumba ua Efraimu.

Judges 10:13-14

Bwana aliwaambia watu wa Israeli wamuite nani awasaidie?

Bwana aliwaambia watu wa Israeli waiombe miungu yao wanayoiabudu iwasaidie.

Judges 10:15-18

Kwa nini Bwana alikuwa na subira juu ya taabu ya Israeli?

Israeli waliiacha miungu ya kigeni wanayoimiliki na kuiabudu hivyo Bwana akawa na subira juu ya taabu yao.

Judges 11

Judges 11:1-3

Jeftha alikuwa mtoto wa nani?

Yeftha alikuwa mtoto wa kahaba.

Judges 11:4-6

Kwa nini viongozi wa Gileadi walikwenda kumleta Yeftha kutoka nchi ya tobu?

Viongozi wa Gileadi walikwenda kumleta Yeftha kutoka nchi ya tobu ili awe kiongozi wao.

Kwa nini viongozi wa Gileadi walikwenda kumleta Yeftha kutoka nchi ya tobu?

Viongozi wa Gileadi walikwenda kumleta Yeftha kutoka nchi ya tobu ili awe kiongozi wao.

Judges 11:7-8

Kwa nini viongozi wa Gileadi waligeukia kwa Yeftha?

Viongozi wa Gileadi waligeukia kwa Yeftha kwa sababu walikuwa na shida.

Kwa nini viongozi wa Gileadi waligeukia kwa Yeftha?

Viongozi wa Gileadi waligeukia kwa Yeftha kwa sababu walikuwa na shida.

Judges 11:9-11

Ikiwa viongozi wa Gileadi walimrejesha Yeftha nyumbani tena kupigana dhidi ya askari wa Amoni na kama Bwana atawapa ushindi juu yao nini kitatokea kwa Yeftha?

iwa viongozi wa Gileadi walimrejesha Yeftha nyumbani tena kupigana dhidi ya askari wa Amoni na kama Bwana atawapa ushindi juu yao Yeftha atakuwa kiongozi wao.

Judges 11:12-16

Kwa nini watu wa Amoni walikuja kwa nguvu kuchuka ardhi ya Israeli?

Watu wa Amoni walikuja kwa nguvu kuchukua ardhi ya Israeli kwa sababu walipanda toka Misri na kuchukua nchi ya Amoni.

Kwa nini watu wa Amoni walikuja kwa nguvu kuchuka ardhi ya Israeli?

Watu wa Amoni walikuja kwa nguvu kuchukua ardhi ya Israeli kwa sababu walipanda toka Misri na kuchukua nchi ya Amoni.

Judges 11:17-20

Kina nani hawakuwa tayari kuwaacha wana wa Israeli wapite?

Mfalme wa Edomi na Moabu hawakuwa tayari kuwaacha wana wa Israeli wapite?

Kwa nini Israeli hawakwenda katika ngome ya Moabu?

Hawakwenda katika ngome ya Moabu kwa sababu Arnoni ilikuwa mpaka wa Moabu.

Judges 11:21-25

Nani aliwapa Israeli ushindi juu ya Sihoni?

Bwana Mungu wa Israeli aliwapa Israeli ushindi juu ya Sihoni.

Judges 11:26-28

Kwa muda gani Israeli iliishi Heshboni na vijiji vyake na Aroeri na vijiji vyake, na katika miji yote iliyo karibu na Arnoni?

Israeli waliishi miaka mia tatu Heshboni na vijiji vyake na Aroeri na vijiji vyake, na katika miji yote iliyo karibu na Arnoni.

Judges 11:29-31

Ikiwa Bwana atampa ushindi Yeftha juu ya watu wa Amoni, Yeftha atafanya nini?

kiwa Bwana atampa ushindi Yeftha juu ya watu wa Amoni, Yeftha atatoa chochote kinachotoka mlangoni mwa nyumba yake kumjia.

Judges 11:32-33

Yeftha alipopita kati ya watu wa Amoni kupigana nao nani alimpa ushindi?

Yeftha alipopita kati ya watu wa Amoni kupigana nao Bwana alimpa ushindi.

Judges 11:34-35

Yeftha alikuwa na watoto wangapi?

Yeftha alikuwa na mtoto mmoja tuu.

Judges 11:36-37

Binti wa Yeftha alitaka kufanya nini kabla ya kufanya yote aliyoahidi baba yake?

Alitaka wamuache pekeyake kwa miezi miwili aende kwenye vilima na kuomboleza juu ya ubikira wake.

Binti wa Yeftha alitaka kufanya nini kabla ya kufanya yote aliyoahidi baba yake?

Alitaka wamuache pekeyake kwa miezi miwili aende kwenye vilima na kuomboleza juu ya ubikira wake.

Judges 11:38-40

Yeftha alimfanyia nini binti yake?

Yeftha alimfanyia binti yake sawasawa na ahadi aliyoweka.

Judges 12

Judges 12:1-2

Watu wa Efraimu walitaka kuwafanyia nini watu wa nyumba ya Yeftha kwa sababu hawakumuita kwenda naye?

Efraimu walitaka kuchoma moto nyumba ya Yeftha kwa sababu hakuwaita kuwenda pamoja naye kupigana na watu wa Amoni.

Judges 12:3-4

Kwa nini watu wa Gileadi waliwavamia watu wa Efraimu?

Watu wa Gileadi waliwavamia watu wa Efraimu kwa sababu waliwaambia, "Ninyi Wagileadi ni wakimbizi katika Efraimu-katika Efraimu na Manase."

Judges 12:5-15

Ni kwa namna gani watu wa Gileadi walimjaribu kama mtu anatoka Efraimu?

Walimwambia aseme "Shiboleth." Na kama akisema 'Sibboleth' (kwa maana hakuweza kutamka neno hilo kwa usahihi), Wagileadi watamkamata na kumwua kwenye mabwawa ya Yordani.

Ni kwa namna gani watu wa Gileadi walimjaribu kama mtu anatoka Efraimu?

Walimwambia aseme "Shiboleth." Na kama akisema 'Sibboleth' (kwa maana hakuweza kutamka neno hilo kwa usahihi), Wagileadi watamkamata na kumwua kwenye mabwawa ya Yordani.

Judges 13

Judges 13:1-2

Kwa nini mke wa Mano hakuzaa?

Mke wa Manoa hakuzaa kwa sababu hakuwa na uwezo wa kupata mimba.

Judges 13:3-5

Kwa nini wembe haukupita kichwani wa mtoto?

Wembe haukupita kichwani kwa mtotokwa sababu mtoto alikuwa Mnaziri wa Mungu.

Judges 13:6-7

Mtu wa Mungu alionekana vipi?

Mtu wa Mungu alionekana kama malaika wa Mungu.

Judges 13:8-11

Malaika wa Mungu alipokuja mara ya pili, nani alikuwepo pale?

Malaika wa Mungu alipokuja mara ya pili mke wa Manoa alikuwepo pale.

Judges 13:12-14

Manoa alimuuliza nini malaika?

Manoa alimuuliza malaika kuhusu sheria za mtoto na kazi yake itakuwa ipi.

Judges 13:15-18

Manoa aliandaa sadaka ya kuteketezwa kwa nani?

Manoa aliandaa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.

Judges 13:19-23

Kitu gani cha kushangaza alichokifanya Bwana wakati Manoa na mke wake wanaangalia?

Manoa na mke wake walipokuwa wakiangalia wanaangalia malaika wa Bwana alitoka juu ya moto wa madhabahu na kupaa kwenda mbinguni.

Kitu gani cha kushangaza alichokifanya Bwana wakati Manoa na mke wake wanaangalia?

Manoa na mke wake walipokuwa wakiangalia wanaangalia malaika wa Bwana alitoka juu ya moto wa madhabahu na kupaa kwenda mbinguni.

Judges 13:24-25

Ni wakati gani roho wa Bwana alianza kumchochea Samsoni?

Roho wa Bwana alianza kumchochea Samsoni akiwa Mahane Dani.

Judges 14

Judges 14:1-2

Ni mtu gani ambaye Samsoni alitaka wazazi wake wamletee kama mke?

Samsoni alitaka wazazi wake wamletee kama mke mwanamke toka Timna, moja ya mabinti wa Wafilisti.

Judges 14:3-4

Kwa nini Samsoni alitaka wazazi wake wampatie mwanamke kutoka Timna kama mke wake?

Alitaka wazazi wake wampatie mwanamke kutoka Timna kama mke wake kwa sababu alimpendeza machoni pake.

Judges 14:5-6

Ni kwa namna gani Samsoni alikuwa na uwezo wa kumrarua simba?

Roho wa Bwana alikuja kwake na kumuwezesha kumrarua Simba.

Judges 14:7-11

Ni kitu gani kilikuwepo katika mzoga wa Simba?

Kulikuwa na kundi la nyuki na asali ilikuwepo kwenye mzoga wa simba.

Judges 14:12-14

Samsoni atafanya nini ikiwa thelethini hawataweza kujibu kitendawili chake?

Samsoni nguo za kitani thelathini na seti za nguo thelathini ikiwa hawataweza kujibu kitendawili chake.

Judges 14:15

Ni kipi kilitokea kwa mke wa Samsoni iwapo hatamdanganya mume wake na kupewa jibu la kitendawili?

Ikiwa mke wa Samsoni hataweza kumdanganya mume wake na kupewa jibu watamchoma moto yeye pamoja na nyumba ya baba yake.

Judges 14:16-18

Ni kwa mda gani mke wa Samsoni alilia ili kupata jibu la kitendawili?

Mke wa Samsoni alilia kwa siku saba kabla ya sikukuu yao kuisha.

Judges 14:19-20

Ni kwa namna gani Samsoni alipata seti thelathini za nguo?

Samsoni alishuka Ashkeloni na kuwaua watu thelethini na kuchukua nguo zao.

Judges 15

Judges 15:1-2

Samsoni alipokwenda kumtembelea mkewe kwa nini baba mkwe wake hamkumruhuru aingie ndani?

Alifikiri kwamba Samsoni anamchukia mke wake hivyo akamkabidhi binti yake kwa rafiki yake na Samsoni.

Judges 15:3-4

Ni kwa namna gani Samsoni hakutaka kuwa na hatia juu ya Wafilisti wakati akiwaumiza?

Samsoni hakutaka kuwa na hatia juu ya Wafilisti wakati akiwaumiza kwa kukamata Mbweha mia tatu, akawafungia taa na kuwaacha waende katika mashamba ya ngano ya Wafilisti.

Ni kwa namna gani Samsoni hakutaka kuwa na hatia juu ya Wafilisti wakati akiwaumiza?

Samsoni hakutaka kuwa na hatia juu ya Wafilisti wakati akiwaumiza kwa kukamata Mbweha mia tatu, akawafungia taa na kuwaacha waende katika mashamba ya ngano ya Wafilisti.

Judges 15:5-6

Wafilisti walipoambiwa kuwa Samsoni amechoma mashamba yao walifanya nini?

Wafilisti walipoambiwa kuwa Samsoni amechoma mashamba yao walimchoma kwa moto mke na baba yake.

Judges 15:7-8

Kwa nini Samsoni aliwakata kata Wafilisti vipande vipande, paja na mguu na kuwaua sana?

Samsoni aliwakata kata Wafilisti vipande vipande, paja na mguu na kuwaua sana ili kulipiza kisasi juu yao kwa kumuua mke na baba yake.

Kwa nini Samsoni aliwakata kata Wafilisti vipande vipande, paja na mguu na kuwaua sana?

Samsoni aliwakata kata Wafilisti vipande vipande, paja na mguu na kuwaua sana ili kulipiza kisasi juu yao kwa kumuua mke na baba yake.

Judges 15:9-11

Kwa nini wafilisti walimvamia Yuda?

Wafilisti walimvamia Yuda ili waweze kumkamata Samsoni, ili wamtendee kama alivyowatendea.

Kwa nini wafilisti walimvamia Yuda?

Wafilisti walimvamia Yuda ili waweze kumkamata Samsoni, ili wamtendee kama alivyowatendea.

Judges 15:12-14

Watu wa Yuda walipomfunga Samsoni, Samsoni aliwafanya wamuapie nini?

Watu wa Yuda walipomfunga Samsoni, Samsoni aliwafanya wamuapie kuwa hawatamuua wao wenyewe.

Judges 15:15-16

Samsoni aliwaua watu elfu kwa kutumia nini?

Samsoni aliwaua watu elfu kwa kutumia taya ya punda.

Judges 15:17-18

Baada ya Samsoni kuwaua watu elfu kwa taya ya punda alifikiri atakufa vipi?

Baada ya Samsoni kuwaua watu elfu kwa taya ya punda alifikiri atakufa kwa kiu.

Judges 15:19-20

Samsoni alipata vipi maji?

Mungu akapafungua mahali pa shimo palipo katika Lehi, na maji yakatoka.

Judges 16

Judges 16:1-2

Wagaza walipanga kumuua Samsoni saa ngapi?

Wagaza walipanga kumuua Samsoni mchana.

Judges 16:3

Samsoni aliwatorokaje Wagaza?

Samsosni akashika mlango wa jiji na miimo yake miwili, akavivuta kutoka nje, komeo na vyote.

Judges 16:4-7

Ikiwa Delila atamdanganya Samsoni, viongozi wa Wafilisti watampa nini?

Ikiwa Delila atamdanganya Samsoni, kil viongozi wa Wafilisti atampa vipande 1,100 vya fedha.

Judges 16:8-9

Delila alipomwambia Samsoni Wafilisti wako juu yako alizifanya nini kamba zilizotumika kumfunga?

Delila alipomwambia Samsoni Wafilisti wako juu yako alizikata kamba.

Judges 16:10-14

Samsoni alipozikata kama, wary walikuwa wamejificha wapi?

Samsoni alipozikata kama, wary walikuwa wamejificha ndani ya chumba cha ndani.

Judges 16:15-16

Ni kwa kiasi gani Delila alimkemea Samsoni?

Alimkemea sana kiasi kwamba alitamani kufa.

Judges 16:17

Kwa nini Samsoni hakuwahi kukata nywele zake?

Samsoni hakuwahi kukata nywele zake kwa sababu alikuwa mnaziri wa Mungu.

Judges 16:18-19

Ni kwa namna gani Delila alianza kumshinda Samsoni?

Delila alianza kumshinda Samsoni baada ya vifungo vya nywele zake kunyolewa kwa maana nguvu zake zilimwacha.

Judges 16:20-22

Wafilisti walimfanya Samsoni afanye kazi gani?

Wafilisti walimpa Samsoni kazi ya kusaga ngano katika gereza.

Judges 16:23-24

Kwa nini viongozi wa Wafilisti walikusanyika pamoja ili kutoa dhabihu kubwa kwa Dagoni mungu wao?

Viongozi wa Wafilisti walikusanyika pamoja ili kutoa dhabihu kubwa kwa Dagoni mungu wao kwa sababu walisema, "mungu wetu amemshinda Samsoni."

Judges 16:25-27

Ni nani alimsaidia Samsoni kushika nguzo zinazoshikilia nyumba?

Kijana aliyemshika mkono Samsoni ndiye aliyemsaidia kushika nguzo zinazoshikilia nyumba.

Judges 16:28-29

Kwa nini Samsoni alitaka Mungu amtie nguvu?

Samsoni alitaka Mungu amtie nguvu ili aweze kulipiza kisasi kwa Wafilisti waliochukua macho yake.

Judges 16:30-31

Samsoni aliwaua watu wangapi jengo lilipoanguka?

Samsoni aliwaua watu wengi kuliko aliowaua kipindi cha maisha yake.

Judges 17

Judges 17:1-2

Mika aliiba nini?

Mika aliiba vipande 1,100 vya fedha ambazo zilichukuliwa toka kwa mama yake.

Judges 17:3-4

Mama yake na Mika alitenga vipande vya fedha kwa ajili ya nini?

Alitenga vipande vya fedha kwa ajili ya Bwana, kwa ajili ya mtoto wake kutengeneza takwimu za chuma.

Judges 17:5-6

Mika alimfanya mmoja wa wanawe awe nani?

Mika alimfanya mmoja wa wanawe awe kuhani.

Judges 17:7-9

Kwa nini Mlawi aliondoka Bathlehemu?

Mlawi aliondoka Bethlehemu ili kwenda kutafuta mahali pa kuishi.

Judges 17:10-11

Mika alimuomba Mlawi awe nani kwake?

Mika alimuomba Mlawi awe mshauri na kuhani kwake.

Judges 17:12-13

Kwa nini Mika alifikiri kuwa Bwana atamtendea mema?

Mika alifikiri kuwa Bwana tamtendea mema kwa sababu Mlawi amekuwa kuhani wake.

Judges 18

Judges 18:1-8

Kwa nini kabila la Waadani walitafuta makazi ya kuishi?

Wadani walitafuta mahali pa kuishi kwa sababu mpaka siku hiyo hawakupokea urithi wowote toka miongoni mwa makabila ya Israeli.

Judges 18:9-12

Watu watano toka Dani walitaka kuifanyia nini ardhi ya Laisha?

Watu watano kutoka Dani walitaka kuichukua ardhi.

Judges 18:13-16

Watu watano walisema kuna ninikatika nyumbay ya Laisha?

Watu watano walisema kwenye nyumba ya Laisha kuna fodi, miungu ya kaya, sanamu zilizochongwa, na sanamu za chuma.

Judges 18:17-23

Nani alichukua sanamu za kuchongwa?

Watu watano walioenda kutembelea nchi walienda na kuchukua sanamu za kuchongwa.

Judges 18:24-26

Kwa nini Mika alikasirika?

Mika alikasirika kwa sababu Wadani waliiba miungu aliyoitengeneza, wakamchukua na kuhani wakaondoka.

Ni wakati gani Mika aliondoka na kurudi nyumbani kwake?

Mika aliondoka na kurudi nyumbani kwake baada ya kuona kuwa watu wale wana nguvu sana kushumshinda.

Judges 18:27-29

Kwa nini hakuwepo mtu wa kuwaokoa watu wa Laisha?

Hakuwepo mtu wa kuwaokoa watu wa Laisha kwa sababu palikuwa na umbali mrefu kutoka Sidoni, na hawakuwa na uhusiano na mtu yeyote.

Judges 18:30-31

Kina nani walikuwa Makuhani wa kabila la Wadani?

Yonathani mwana wa Gershomu (mwana wa Musa), yeye na wanawe walikuwa makuhani wa kabila la Wadani mpaka siku ya uhamisho wa nchi.

Judges 19

Judges 19:1-2

Mlawi alikuwa anaishi wapi?

Mlawi alikuwa akiishi kwa muda kidogo katika eneo la mbali zaidi ya nchi ya Efraimu.

Judges 19:3-4

Mwanamke wa Mlawi alimpeleka wapi Mlawi?

Mwanamke alimpeleka Mlawi kwenye nyumba ya baba yake.

Judges 19:5-6

Japokuwa Mlawi alipanga kwenda nyumbani baba mkwe wake alimtaka afanye nini?

Baba mkwe wake alimtaka abaki na ashinde usiku ule.

Japokuwa Mlawi alipanga kwenda nyumbani baba mkwe wake alimtaka afanye nini?

Baba mkwe wake alimtaka abaki na ashinde usiku ule.

Judges 19:7-8

Mlawi alifanya nini kuhusu mpango wake wa kuondoka asubuhi na kwenda nyumbani?

Mlawi alibadili mpango wake na kukaa usiku huo pamoja na baba mkwe wake.

Judges 19:9-11

Baba mkwe wa Mlawi alimuomba afanye nini siku ile ya tano?

Baba mkwe wa Mlawi alimuomba akae usiku ule na awe na wakati mzuri.

Judges 19:12-13

Kwa nini Mlawi hakutaka kukaa usiku ule katika Yebusi?

Mlawi hakutaka kwenda katika nchi ya wageni.

Judges 19:14-15

Kwa nini Mlawi na watumishi wake walikaa katika njia kuu ya jiji?

Walikaa katika njia kuu ya jiji kwa maana hakuna mtu aliyewaingiza nyumbani kwake usiku.

Judges 19:16-19

Watu wa kabila gani Waliishi Gibea?

Watu wa kabila la Benyamini waliishi Gibea.

Judges 19:20-21

Mzee alimmuonya Mlawi asifanye kitu gani?

Mzee alimuonya Mlawi asikae usiku katika njia kuu.

Judges 19:22-23

Kwa nini watu waovu walimtaka yule mzee amtoe nje mtu aliyekuja katika nyumba yake?

Watu waovu walimtaka mzee amtoe nje mtu aliyekuja nyumbani kwake ili wafanye naye mapenzi.

Judges 19:24-26

Mzee aliwapa nini wale watu waovu badala ya Mlawi?

Mzee aliwapa binti bikra pamoja na mwanamke wa Mlawi.

Nini kilitokea asubuhi?

Asubuhi walimruhusu yule mwanamke aende. Alienda akaanguka chini ya mlango wa nyumba ya mtu ambapo bwana wake alikuwa, na yeye akalala pale mpaka kulipokucha.

Nini kilitokea asubuhi?

Asubuhi walimruhusu yule mwanamke aende. Alienda akaanguka chini ya mlango wa nyumba ya mtu ambapo bwana wake alikuwa, na yeye akalala pale mpaka kulipokucha.

Judges 19:27-28

Mlawi alifanya nini mwanamke wake alipoacha kumjibu?

Alimuweka juu ya punda na mtu huyo akaondoka nyumbani.

Judges 19:29-30

Mlawi aliufanya nini mwili wa yule mwanamke?

Mlawi aliukata kata, mguu kwa mguu, akafanya vipande kumi na viwili, akapeleka vipande kila mahali katika Israeli.

Judges 20

Judges 20:1-4

Akina nani walikusanyika pamoja mbele ya Bwana huko Mispa?

Watu wote wa Dani toka Beersheba pamoja na nchi ya Gileadi walikusanyika pamoja mbele za Bwana huko Mispa.

Judges 20:5-7

Mlawi alisema ndugu wa Gibea walimfanya nini?

Mlawi alisema ndugu wa Gibea walimshambulia, wakaizunguka nyumba na kukusudia kumuua.

Judges 20:8-11

Ni kwa namna gani watu wataishambulia Gibea?

Wataishambulia Gibea kama kura itakavyowaongoza.

Judges 20:12-14

Kwa nini makabila ya Israeli walimwambia Benyamini awape watu hao waovu wa Gibea?

Makabila ya Israeli walimwambia Benyamini awape watu hao waovu wa Gibea ili wawaue na kuuondoa kabisa uovu huo katika Israeli.

Kwa nini watu wa Benyamini walikusanyika kutoka mijini kwenda Gibea?

Watu wa Benyamini walikusanyika kutoka mijini kwenda Gibea ili kujiandaa kupigana vita na wana wa Israeli.

Judges 20:15-16

Kitu gani cha pekee walichokuwa nacho watu mia saba waliochaguliwa?

Watu mia saba waliochaguliwa walikuwa wenye shoto na kila mmoja wao angeweza kupiga unywele kwa mawe na asikose.

Judges 20:17-25

Kwa nini Yuda alimvamia Benyamini kwanza?

Watu waliomba ushauri kwa Mungu na Bwana akasema, "Yuda atashambulia kwanza."

Judges 20:26

Baada ya Benyamini kuua Askari wengi wa Israeli, Israeli alifanya nini?

Baada ya Benyamini kuua askari wengi wa Israeli, askari walilia na kufunga mbele za Bwana hata jioni. Pia walitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana.

Judges 20:27-31

Kwa namna gani wana wa Israeli walimuuliza Bwana?

Wana wa Israeli walimuuliza Bwana kwa kutumia sanduku la agano la Mungu lililokuwepo siku hizo.

Judges 20:32-41

Askari wa Israeli walipowavuta mbali toka mjini hadi barabarani, watu wa Benyamini walidhani nini?

Askari wa Israeli walipowavuta mbali toka mjini hadi barabarani, watu wa Benyamini walidhani wanakimbia.

Judges 20:42-46

Kwa nini watu wa Benyamini hawakuweza kukimbia?

Watu wa Benyamini walikimbia toka kwa askari wa Israeli kuelekea jangwani lakini vita viliwapata.

Judges 20:47-48

Askari wangapu wa Benyamini waligeuka na kukimbilia jangwani?

Askari mia sita waligeuka na kukimbilia jangwani.

Judges 21

Judges 21:1-3

Kwa nini watu wa Israeli walikuwa na wasiwasi kuwa moja ya makabila yao linapotea?

Watu wa Israeli walikuwa na wasiwasi kuwa moja ya makabila yao linapotea kwa sababu waliahidi kutowatoa binti zao kuolewa na Wabenyamini.

Kwa nini watu wa Israeli walikuwa na wasiwasi kuwa moja ya makabila yao linapotea?

Watu wa Israeli walikuwa na wasiwasi kuwa moja ya makabila yao linapotea kwa sababu waliahidi kutowatoa binti zao kuolewa na Wabenyamini.

Judges 21:4-7

Nani atauawa?

Mtu yeyote ambaye hataenda kwa Bwana huko Mispa atauawa.

Judges 21:8-10

Ni kabila gani la Israeli halikwenda kwa Bwana huko Mispa?

Yabeshi Gileadi hakwenda kwa Bwana huko Mispa.

Judges 21:11-12

Wanaume waliwachukua akina nani toka kwa wale waliokuwa wakiishi Yabeshi Gileadi?

Wanaume waliwachukua wanawake mia nne ambao hawajalala na mwanaume.

Judges 21:13-17

Kulikuwa na tatizo gani wakati ambao Wabenyamini walirudi na kupewa wanawake wa Yabeshi Gileadi?

Wabenyamini waliporudi wakati huo na kupewa wanawake wa Yabeshi Gileadi, hawakuwepo wanawake wa kutosha kwa ajili yao wote.

Judges 21:18-19

Shilo iko wapi?

Shilo iko kaskazini mwa Betheli, mashariki ya barabara inayopanda kutoka Betheli hadi Shekemu, na kusini mwa Lebona.

Judges 21:20-21

Ni wakati gani ambao Wabenyamini walitoka nje ya mizabibu na kunyakua mke kutoka kwa wasichana wa Shilo?

Wakati wasichana wa Shilo walipotoka nje kwa ajili ya kucheza Wabenyamini walitoka nje ya mizabibu na kunyakua mke kutoka kwa wasichana wa Shilo.

Judges 21:22-24

Ni sababu gani ambayo watu wa Israeli waliwaambia watu wa Shilo kuhusu wasichana?

Watu wa Israeli waliwaambia watu wa Shilo kuwa wawaache wasichana hao wabaki kwa sababu hawakupata wake wakati wa vita.

Judges 21:25

Kila mtu alifanya nini?

Kila mtu aliifanya yaliyo sawa machoni pake mwenyewe.