Hosea
Hosea 1
Hosea 1:1-2
Ni mke wa aina gani ambaye Bwana alimwambia Hosea amchukue kwa ajili yake.
Bwana alimwambia Hosea achukue mke aliyekuwa kahaba.
Hosea 1:3-5
Kwa nini Hosea alimuita mtoto wake wa kwanza Yezreeli?
Hosea alimuita mtoto wake wa kwanza Yezreeli kwa maana kwa muda mfupi Bwana ataiadhibu nyumba ya Yehu kwa sababu ya kumwaga damu huko Yezreeli.
Hosea 1:6-7
Bwana ataihurumia nyumba ya nani?
Bwana ataihurumia nyumba ya Yuda.
Hosea 1:8-9
Kwa nini Hosea alimuita mtoto wake wa pili Lo Ami?
Hosea alimuita mtoto wake wa pili Lo Ami kwa kuwa Israeli hawakuwa tena watu wake.
Hosea 1:10-11
Wataambiwa nini watu ambao mwanzo waliambiwa sio watu wa Bwana?
Wataambiwa wao ni watu wa Mungu aliye hai.
Hosea 2
Hosea 2:2-3
Bwana atafanya nini ikiwa Israeli atashindwa kuacha ukahaba wake?
Ikiwa Israeli atashindwa kuacha ukahaba wake Bwana atamvua nguo na kumuonyesha uchi wake kama siku aliyozaliwa.
Bwana atafanya nini ikiwa Israeli atashindwa kuacha ukahaba wake?
Ikiwa Israeli atashindwa kuacha ukahaba wake Bwana atamvua nguo na kumuonyesha uchi wake kama siku aliyozaliwa.
Hosea 2:4-5
Kwa nini Bwana hatakuwa na huruma juu ya watoto wa Israeli?
Bwana hatakuwa na huruma juu ya watoto wa Israeli kwa sababu ni watoto wa ukahaba.
Hosea 2:6-7
Kwa nini Israeli atarudi kwa mume wake wa kwanza?
Israeli atarudi kwa mume wake wa kwanza kwa sababu ilikuwa bora kwake zamani kuliko sasa.
Hosea 2:8-9
Nani aliziongeza fedha na dhahabu za Israeli?
Bwana aliziongeza fedha na dhahabu za Israeli.
Hosea 2:10-11
Bwana ataifanya nini Israeli mbele ya wapenzi wake?
Bwana atamvua nguo machoni pa wapenzi wake.
Hosea 2:12-13
Ni mishahara gani ambayo wapenzi wa Israeli walimpa Israeli?
Wapenzi wa Israeli waimpa mizabibu na mtini.
Hosea 2:14-15
Makahaba watamjibu nini Bwana baada ya kuwashawishi warejee?
Watamjibu kama walivyofanya katika siku za ujana wao, kama katika siku ambazo walioka katika nchi ya Misri.
Hosea 2:16-17
Katika siku hiyo Israeli atamwitaje Bwana?
Atamwita Bwana 'mume wangu' na sio tena 'Baali wangu.'
Hosea 2:18
Bwana atawafanya watu wake wafanye nini?
Bwana atawafanya watu wale walale kwa usalama.
Hosea 2:19-20
Kwa muda gani Bwana aliwaahidi watu wake kuwa mume wao?
Bwana atakuwa mume wao daima.
Hosea 2:21-22
Divai mpya na mafuta watajibu nini?
Divai mpya na mafuta watajibu Yezreeli.
Hosea 2:23
Bwana atasema nini kwa wale ambao hawakuwa watu wake?
Bwana atawaambia 'ninyi ni watu wangu.'
Hosea 3
Hosea 3:1-3
Ni kwa namna gani Hosea anatakuwa kumpenda mke wake?
Hosea anatakuwa kumpenda mke wake kama Bwana anavyowapenda wana wa Israeli.
Kwa gharama gani Bwana aliwanunua Israeli?
Bwana aliwanunua Israeli kwa vipande kumi na tano vya fedha na homeri na letheki ya shayiri.
Hosea 3:4-5
Baada ya wana wa Israeli kuishi muda mrefu bila mfalme walimtafuta nani?
Baada ya wana wa Israeli kuishi muda mrefu bila mfalme walimtafuta Bwana Mungu wao na mfalme Daudi.
Baada ya wana wa Israeli kuishi muda mrefu bila mfalme walimtafuta nani?
Baada ya wana wa Israeli kuishi muda mrefu bila mfalme walimtafuta Bwana Mungu wao na mfalme Daudi.
Hosea 4
Hosea 4:1-2
Bwana anamashitaka dhidi ya nani?
Bwana anamashitaka dhidi ya wenyeji wa nchi.
Hosea 4:3
Nini kilitokea kwa kila mtu aliyeishi kwernye nchi?
Kila mtu aliyeishi kwernye nchi aliangamia.
Hosea 4:4-5
Nani atajikwaa usiku?
Makuhani watajikwaa usiku.
Hosea 4:6-7
Kwa nini Bwana aliwasahau watoto wa wana wa Israeli?
Bwana aliwasahau watoto wa wana wa Israeli kwa sababu waliisahau sheria ya Mungu.
Hosea 4:8-10
Watu walifanya kama nani?
Watu walifanya kama makuhani.
Hosea 4:11-12
Ni vitu gani viliuchukua ufahamu wa watu?
Uasherati, divai, na divai mpya viliuchukua ufahamu wa watu.
Hosea 4:13-14
Kwa nini Bwana hakuwaadhibu binti za watu walipochagua kuzini?
Bwana hakuwaadhibu binti za watu walipochagua kuzini kwa maana wanaume pia walijitoa kwa makahaba, na kutoa dhabihu ili waweze kufanya vitendo vya uasherati na makahaba.
Hosea 4:15-16
Watu wahakutakiwa kwenda wapi?
Watu hawakutakiwa kwenda Gilgali au Beth Aven.
Hosea 4:17-19
Efraimu alifanya nini hata wakati ambao kileo chake kiliondoka?
Efraimu alifanya uzinzi hata wakati ambao kileo chake kiliondoka.
Hosea 5
Hosea 5:1-2
Waasi husimama wapi?
Waasi husimama sana katika mauaji.
Hosea 5:3-4
Ni kipi kitamfanya Efraimu ashindwe kurejea kwa Mungu wake?
Matendo wa Efraimu yatamfanya ashindwe kurejea kwa Mungu wake.
Hosea 5:5-7
Kwa nini Israeli, Efraimu na Yuda hawatamuona Bwana?
Israeli, Efraimu na Yuda hawatamuona Bwana kwa kuwa amejiondoa kutoka kwao.
Hosea 5:8-9
Nani alisema kuwa Efraimu itakuwa ukiwa?
Bwana alisema kuwa Efraimu itakuwa ukiwa.
Hosea 5:10-11
Bwana atamimina ghadhabu yake kwa nani?
Bwana atamimina ghadhabu yake kwa viongozi wa Yuda.
Hosea 5:12-13
Ni lini Efraimu alienda kwa Ashuru?
Efraimu alipoona ugonjwa wake alienda kwa Ashuru.
Hosea 5:14-15
Kwa muda gani Bwana atakwenda na kurudi mahali pake?
Bwana atakwenda na kurudi mahali pake mpaka watambue hatia yao na kutafuta uso wake, hata wakamtafute kwa bidii katika dhiki yao.
Hosea 6
Hosea 6:1-3
Japokuwa Bwana aliwavunja vipande vipande watu wake, je atafanya nini?
Japokuwa Bwana aliwavunja vipande vipande atawaponya.
Ni lini Bwana atawainua watu wake?
Bwana atawainua watu wake siku ya tatu.
Hosea 6:4-5
Uaminifu wa Efraimu na Yuda upo kama nini?
Uaminifu wa Efraimu na Yuda upo kama wingu la asubuhi, kama umande unaoondoka mapema.
Hosea 6:6-7
Mungu anatamani nini?
Mungu anatamani uaminifu wala si dhabihu, na kumjua yeye kuliko sadaka za kuteketezwa.
Hosea 6:8-9
Ni kwa namna gani makuhani hujiunga pamoja kufanya mauaji kwa njia ya Shekemu?
Kama makundi ya wanyang'anyi ndivyo makuhani hujiunga pamoja kufanya mauaji kwa njia ya Shekemu.
Hosea 6:10-11
Nini kilichaguliwa kwa Yuda wakati Bwana anarudisha urithi kwa watu wake?
Mavuno yalichaguliwa wakati Bwana anarudisha urithi kwa watu wake.
Hosea 7
Hosea 7:1-2
Bwana anakumbuka nini?
Bwana anakumbuka matendo yao mabaya.
Hosea 7:3-5
Ni kwa namna gani watu waliwafanya wakuu wao wafurahi?
Watu waliwafanya wakuu wao wafurahi kwa kuwadanganya.
Hosea 7:6-7
Mioyo ya watu ilikuwa kama nini?
Mioyo ya watu ilikuwa kama tanuru.
Hosea 7:8-9
Efraimu hakujua nini?
Efraimu hakujua kuwa wageni wamekula nguvu zake au mvi hunyunyuza juu yake.
Hosea 7:10-11
Ni kwa namna gani Efraimu alikuwa kama njiwa?
Efraimu alikuwa kama njiwa baradhuli na asiye na busara.
Hosea 7:12-13
Kwa nini Bwana hakuwakomboa watu?
Bwana hakuwakomboa watu waliongea uongo dhidi yake.
Hosea 7:14-15
Watu walifanya nini ili kuendelea kuwa na nafaka na divai mpya?
Watu walijidhuru wenyewe ili kuendelea kuwa na nafaka na divai mpya.
Hosea 7:16
Kwa nini maofisa walianguka?
Maofisa walianguka kwa sababu udhalimu wa vinywa vyao.
Hosea 8
Hosea 8:1-3
Kwa nini tai anakuja katika nyumba ya Bwana?
Tai anakuja juu ya nyumba ya Bwana kwa sababu watu wamevunja agano lake na kuasi dhidi ya sheria yake.
Hosea 8:4-5
Kwa kutumia nini watu walitengeneza sanamu kwa ajili yao wenyewe?
Kwa fedha zao na dhahabu wamejifanyia sanamu wenyewe.
Hosea 8:6-7
Nini kilitokea watu walipopanda upepo?
Watu walipanda upepo na kuvuna kimbunga.
Hosea 8:8-10
Bwana atafanya nini japokuwa watu waliajiri wapenzi kati ya mataifa.
Japokuwa watu waliajiri wapenzi kati ya mataifa Bwana atawakusanya pamoja.
Hosea 8:11-12
Kama Bwana aliandika sheria zake kwao mara elfu kumi, wangeona nini?
Bwana aliandika sheria zake kwao mara elfu kumi lakini wangeiona kama kitu cha ajabu kwao.
Hosea 8:13-14
Ni kwa namna gani Bwana angewaadhibu watu watendao dhambi?
Ataadhibu dhambi zao kwa kuwarudisha Misri.
Hosea 9
Hosea 9:1-2
Israeli walipenda kulipa nini?
Israeli walipenda kulipa mshahara kwa kahaba kwenye sakafu zote za nafaka.
Hosea 9:3-4
Dhabihu za Efraimu zilikuwa kwao kama nini?
Dhabihu za Efraimu zilikuwa kwao kama chakula cha matanga.
Hosea 9:5-6
Ikiwa watu watakimbia uharibifu nini kitatokea?
Ikiwa watu watakimbia uharibifu Misri itawakusanya, na Nofu itawazika.
Hosea 9:7
Siku zipi zinakuja?
Siku za adhabu zinakuja. Siku za kulipiza kisasi zinakuja.
Hosea 9:8-9
Nini kilikuwa kwenye njia ya nabii?
Mtego wa ndege ulikuwa kwenye njia ya nabii.
Hosea 9:10
Baada ya baba kwenda kwenye Baal Peori walikuwaje?
Baada ya baba kwenda kwenye Baal Peori wakawa chukizo kama sanamu waliyoipenda.
Hosea 9:11-12
Nini kitatokea kwenye utukufu wa Efraimu?
Utukufu wa Efraimu utapaa kama ndege.
Hosea 9:13-14
Bwana atampa nini Efraimu?
Bwana atampa Efraimu umbo lenye kuharibu mimba na matiti yasiyotoa maziwa.
Hosea 9:15
Kwa nini Bwana alimfukuza Efraimu kwenye nyumba yake?
Kwa sababu ya matendo yake maovu, Bwana alimuondoa kwenye nyumba yake.
Hosea 9:16-17
Nini kitatokea kama Efraimu atakuwa na watoto?
Hata Efraimu akiwa na watoto Bwana atawaua watoto wao.
Hosea 10
Hosea 10:1-2
Nini kitatokea matunda ya Israeli yakiongezeka?
kwa kadiri matunda yake yanavyoongezeka anajenga madhabahu nyingi.
Hosea 10:3-4
Ni kwa namna gani Israeli walifanya agano?
Israeli walifanya agano kwa kuapa uongo.
Hosea 10:5-6
Kwa nini wenyeji wa Samaria watachukuliwa kwenda Ashuru?
Watachukuliwa kwenda Ashuru kama sadaka kwa mfalme mkuu.
Hosea 10:7-9
Nini kitaota juu ya madhabahu?
Miti na vichaka vitakua juu ya madhabahu zao.
Hosea 10:10-11
Kwa nini Bwana ataweka jozi juu ya shingo ya Efraimu?
Kwa sababu Efraimu alikuwa ndama mwenye mafunzo ambayo anapenda kupura nafaka, Bwana ataweka jozi juu ya shingo yake nzuri.
Hosea 10:12-13
Kwa muda gani watu watamtafuta Bwana?
Watu watamtafuta Bwana mpaka atakapokuja na kuinua haki juu yao.
Hosea 10:14-15
Nini kilitokea kwa wamama na watoto wao Shalmani alipoharibu Beth Arbeli?
Shalmani alipoharibu Beth Arbeli mama alivunjika vipande vipande na watoto wake.
Hosea 11
Hosea 11:1-2
Kutoka wapi Bwana alimuita Israeli alipokuwa mdogo?
Wakati Israeli alikuwa kijana Bwana alimuita kutoka Misri.
Hosea 11:3-4
Nani alimwinua juu Efraimu kwa mikono yake?
Bwana alimwinua juu Efraimu kwa mikono yake.
Hosea 11:5-7
Ni kitu gani watu wa Mungu waliamua kufanya?
Watu wa Mungu waliamua kumuacha Mungu.
Hosea 11:8-9
Kwa nini Bwana hataiharibu tena Efraimu?
Bwana hataiharibu tena Efraimu kwa sababu yeye ni Mungu sio mwanadamu.
Hosea 11:10-11
Watu watakuja kwa namna gani?
Watu watakuja wakitetemeka toka mashariki kama ndege, kama njiwa kutoka kwenye nchi ya Ashuru.
Watu watakuja kwa namna gani?
Watu watakuja wakitetemeka toka mashariki kama ndege, kama njiwa kutoka kwenye nchi ya Ashuru.
Hosea 11:12
Nani alikuwa mwaminifu kwa Mungu?
Yuda alikuwa mwaminifu kwa Mungu.
Hosea 12
Hosea 12:1-2
Ni kitu gani Bwana anacho dhidi ya Yuda?
Bwana ana mashitaka dhidi ya Yuda.
Hosea 12:3-4
Yokobo alifanya nini tumboni?
Tumboni Yakobo alimshika ndugu yake kisigino.
Hosea 12:5-6
Watu wanatakiwa kumsubiri nani?
Watu wanatakiwa waendelee kumsubiri Mungu.
Hosea 12:7-8
Ni kitu gani ambacho hamna mtu atakayekipata kwa kazi ya Efraimu?
Katika kazi zote za Efraimu hamna mtu atakayekuta dhamboi ndani yake.
Hosea 12:9-10
Ni kwa mda gani Bwana alikuwa na watu?
Bwana alikuwa na watu tangu walipokuwa katika nchi ya Misri.
Hosea 12:11-12
Madhabahu za Gilgali zitakuwa kama nini?
Madhabahu za Gildali zitakuwa kama miundo ya jiwe katika miamba ya mashamba.
Hosea 12:13-14
Bwana alifanya nini kupitia manabii?
Bwana aliwatoa Israeli toka Misri kwa kutumia manabii na kwa manabii akawajali.
Hosea 13
Hosea 13:1-2
Kwa nini Efraimu alikuwa na hatia?
Efraimu alikuwa na hatia kwa sababu ya kuabudu Baali.
Hosea 13:3
Nini limetokea kwa makapi?
Makapi yanayotokana na upepo kutoka kwenye sakafu.
Hosea 13:4-6
Nini kilitokea watu wa Bwana waliposhiba?
Watu wa Bwana waliposhiba mioyo yao ikaunuliwa wakamsahau.
Hosea 13:7-8
Bwana atawaangamiza watu wake kama nini?
Atawaangamiza kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake.
Hosea 13:9-11
Kwa nini kuangamia kwa Israeli kulifika?
Kuangamia kwa Israeli kulifika kwa sababu walikuwa kinyume na Bwana, msaada wao.
Hosea 13:12-13
Ilipofika wakati wa Efraimu kuzaliwa nini kilitokea?
Ulipofika wakati wa Efraimu kuzaliwa hakutoka tumboni.
Hosea 13:14
Ni kitu gani Bwana alitaka kiletwe kwake?
Bwana alitaka majanga ya kigo na kaburi viletwe kwake.
Hosea 13:15
Ni kitu gani ambacho adui wa Efraimu watakipora?
Adui zakw watapora ghala lake la kila kitu cha thamani.
Hosea 13:16
Kitu gani kitatokea kwa watoto wadogo wa Israeli?
Watoto wao wadogo watavunjwa.
Hosea 14
Hosea 14:1-2
Kwa nini Israeli ilianguka?
Israeli ilianguka kwa sababu ya dhambi zao.
Hosea 14:3
Kwa nini Israeli hawataiambia kazi ya mikono yako. "ninyi ni miungu yetu"?
Israeli hawataiambia kazi ya mikono yako. "ninyi ni miungu yetu" kwa maana kwa Bwana mtu asiye na baba hupata huruma.
Hosea 14:4-6
Ni lini Bwana ataiponya Israeli?
Bwana atawaponya wakirejea kwake.
Hosea 14:7-8
Utukufu wa mtu utakuwa kama nini"
Utukufu wake utakuwa kama divai ya Lebanoni.
Hosea 14:9
Kina nani wataanguka kwenye njia za Bwana?
Waasi wataanguka ndani yake.