Ephesians
Ephesians 1
Ephesians 1:1-2
Vipi Paulo anaeleza watu anaandika huu waraka?
Paulo anaeleza watu anaandika huu waraka kwa waliotengwa na Mungu, na kama waaminifu wanaoaminiwa katika Kristo Yesu.
Ephesians 1:3-4
Kwa vipi Mungu Baba amewabariki waamini?
Mungu Baba amewabariki waamini kwa kila baraka za rohoni katika maeneo ya mbinguni katika Kristo
Lini Mungu baba aliwachagua wale wanao mwamini Kristo?
Mungu Baba aliwachagua wale wa mwaminio Kristo kabla ya kuumbwa ulimwengu.
Kwa kuhusudi lipi Mungu aliwachagua waamini?
Mungu Baba aliwachagua waamini ili wawe watakatifu na pasipo lawama machoni pake.
Ephesians 1:5-6
Kwa nini Mungu huwatangazia waamini ya mbeleni kabla ya kuwarithi?
Mungu aliwatangazia waamini ya mbeleni kabla ya kuwarithi kwa sababu alifurahishwa kufanya hivyo, na kwamba angetukuzwa na utukufu wa neema yake.
Ephesians 1:7-8
Ni nini waamini wanapokea kupitia damu ya Kristo,Upendo wa Mungu wa pekee?
Waamini hupokea ukombozi kupitia damu ya Kristo kwa kusamehewa dhambi.
Ephesians 1:9-12
Nini ambacho Mungu ata fanya wakati wa utimilifu wa mpango wake utakapo fika?
Mungu ata leta pamoja kila kitu mbinguni na duniani chini ya Kristo.
Ephesians 1:13-16
Ni mhuri wa namna gani waamini walipokea wakati waliposikia neno la kweli?
Waamini walipokea mhuri wa Roho Mtakatifu walioahidiwa.
Roho ni dhamana wa nini?
Roho ni dhamana wa urithi wa waamini
Ephesians 1:17-18
Kipi Paulo anacho ombea waEfeso watiwe nuru kuelewa?
Paulo anaomba waEfeso watiwe nuru kuelewa ujasiri wa wito wao.
Ephesians 1:19-21
Ni kwa Vipi Paulo anawaombea Waefeso kutiwa nuru na ufahamu?
Paulo anawaombea kwamba Waefeso watatiwa nuru na ufahamu wa ujasiri wa mwito wao,utajiri wa utukufu wa urithi wao,na ukuu wa nguvu ya Mungu ndani yao
Ephesians 1:22-23
Ni nini Mungu aliweka chini ya miguu Kristo?
Mungu aliweka vitu vyote chini ya Miguu ya Kristo
Ni nafasi ipi ya mamlaka aliyo nayo Kristo ndani ya kanisa?
Kristo ni kichwa juu ya vitu vyote ndani ya kanisa.
Kanisa ni nini?
Kanisa ni mwili wa Kristo.
Ephesians 2
Ephesians 2:1-3
Hali za kiroho za wote wasioamini zikoje?
Wote wasioamini ni wafu katika makosa na dhambi zao.
Nani anafanya kazi ndani ya wana wa kuasi?
Roho ya wa kuu waanga ina fanya kazi ndani ya wana wa kuasi.
kwa asili, wasio waamini ni nani?
Wasio amini ni wana wa gadhabu.
Ephesians 2:4-7
Kwanini Mungu aliwaleta baadhi ya watu wasioamini katika maisha mapya ndani ya Kristo?
Mungu aliwaleta baadhi ya watu wasioamini katika maisha mapya ndani ya Kristo kwa sababu ya rehema zake nyingi na pendo lake kubwa.
Kwa nini Mungu aliwaleta wasio amini katika maisha mapya na Kristo
Mungu aliwaleta wasio amini katika maisha mapya na Kristo sababu ya ukuu wa rehema zake na upendo wake mkubwa
waamini wameokolewa na nini?
waamini wameokolewa kwa neema ya Mungu.
waamini wameketishwa wapi?
waamini wameketishwa katika sehemu za mbingu na Kristo Yesu
Kwa kusudi lipi Mungu amewaokoa na kuwa kuza waamini?
Mungu amewaokoa waamini na kuwa kuza ili katika miaka ijayo awaonyeshe ukuu wa utajiri wa neema yake.
Ephesians 2:8-10
Ni katika kipi hakuna muumini anayejisifu na ni kwa nini?
Hakuna muumini anayejisifia kazi zake, kwa sababu ameokolewa kwa neema ambayo ni zawadi ya Mungu.
Kwa kusudi lipi ambalo Mungu amewa umba waamini ndani ya Kristo Yesu?
Kusudi la Mungu ni waamini ndani ya Kristo Yesu watembee katika kutenda mema.
Ephesians 2:11-12
Ni hali gani ya kiroho kwa wamataifa wasio amini ?
Wamataifa wasio amini wametengwa na Kristo na Israeli, wageni wa agano, bila matumaini na bila Mungu.
Ephesians 2:13-16
Ni nini kilichowaleta baadhi ya watu wa mataifa wasioamini karibu na Mungu?
Baadhi ya watu wa mataifa wasioamini wameletwa karibu na Mungu kwa damu ya Kristo.
Jinsi gani Kristo aliyobadili uhusiano kati ya mataifa na waYaudi?
Kwa mwili wake, Kristo amewafanya mataifa na waYaudi watu wamoja, akiharibu upinzani uliyo watenganisha.
Kristo aliondoa ni ilikuweza kufanya amani kati ya waYaudi na wamataifa?
Kristo aliondoa sheria ya amri na masharti ilikufanya amani kati ya waYaudi na mataifa.
Ephesians 2:17-18
Kwa njia gani waamini wote wanaweza kuwasiliana na Baba?
Waamini wote wanawasiliana na Baba kwa Roho Mtakatifu.
Ephesians 2:19-22
Katika msingi upi familia ya Mungu imejengwa?
Familia ya Mungu imejengwa katika msingi wa mitume na manabii, Kristo Yesu akiwa kiwe kuu la pembeni.
Nguvu ya Yesu inafanyaje na kujengwa kwa familia Yake?
Nguvu ya Yesu ya tosha na ya ongeza kujengwa kwa familia yake.
Kujengwa kwa familia ya Mungu ni namna gani ya ujenzi?
Kujengwa kwa familia ya Mungu ni hekalu lilo tengwa kwa ajili ya Bwana.
Mungu anaishi wapi katika roho?
Mungu anakaa katika roho ndani ya mwamini.
Ephesians 3
Ephesians 3:1-2
Kwa faida ya nani Mungu kumpatia Paulo karama yake?
Mungu alimpatia Paulo karama yake kwa faida ya mataifa.
Ephesians 3:3-5
Kitu gani ambacho wanadamu wa vizazi vilivyo pita hawakufunuliwa?
Ukweli uliyo fichwa wa Yesu hauku funuliwa kwa vizazi vilivyo pita
Mungu alifunua kwa nani kile ambacho kilifichwa kwa vizazi vilivyo pita?
Mungu alifunua ukweli uliofichwa kwa mitume wake na manabii.
Ephesians 3:6-7
Ukweli upi uliofununliwa?
Ukweli uliofunuliwa ni kwamba mataifa ni warithi pamoja na waumini wa mwili, na washiriki katika ahadi ya Kristo Yesu
Paulo alipewa karama gani?
Karama ya neema ya Mungu alipewa Paulo.
Ephesians 3:8-9
Paulo alitumwa kuwasaidia nini mataifa?
Paulo alitumwa kuwasaidia mataifa kuelewa mpango wa Mungu.
Ephesians 3:10-11
Kupitia nini hekima isioelezeka ya Mungu itadhihirishwa?
Kupitia kanisa hekima isioelezeka ya Mungu itadhirishwa.
Ephesians 3:12-13
Paulo anasema waamini wana nini sababu ya imani kwa Yesu?
Paulo anasema waamini wana njia ya wazi na wana ujasiri sababu ya imani kwa Kristo.
Ephesians 3:14-16
Nini kimetajwa na kuumbwa na Baba?
Kila familia mbinguni na duniani imetajwa na kuumbwa kwa ajili ya Baba.
Paulo anaombaje waamini wa imarishwe?
Paulo anaomba waamini wa imarishwe kupitia Roho wa Mungu.
Ephesians 3:17-19
Paulo anaomba waamini waweze kuelewa nini?
Pualo anaomba waamini waweze kuelewa jinsi upana na urefu na ukubwa na undani wa upendo wa Kristo
Ephesians 3:20-21
Paulo anaomba Baba apewe nini kwa vizazi vyote?
Paulo anaomba utukufu wa kanisa na wa Krsito Yesu utapewa Baba kwa vizazi vyote.
Ephesians 4
Ephesians 4:1-3
Paulo anawasihi vipi waamini kuishi?
Paulo anawasihi waaminini kuishi kwa unyenyekevu, upole, na uvumilivu, wakichukuliana katika upendo.
Ephesians 4:4-6
Paulo anataja nini katika orodha ya vitu vyake ambayo ina moja tu?
Paulo anasema kuna mwili mmoja, Roho, uhakika wa taraja, Bwana, imani, ubatizo, na Mungu Baba.
Ephesians 4:7-10
Kristo aliwapa nini kwa kila muamini alipopaa?
Kristo aliwapa kila muamini karama kwa kadiri ya kipimo cha karama ya Kristo.
Ephesians 4:11-13
Karama zipi tano za Kristo kwa mwili ambazo Paulo anataja?
Kristo alitoa kwa mwili karama za mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji, na waalimu.
Hizi karama tano zina kusudi gani?
Karama tano za paswa kuwa andaa waamini kwa ajili ya kazi ya huduma, kujenga mwili.
Ephesians 4:14-16
Paulo anaelezeaje kuwa waamini wanaweza kuwa kama watoto?
Waamini wanaweza kuwa kama watoto kwa kurushwarushwa na kuchukuliwa kwa hila za watu katika ujanja wa udanganyifu.
Paulo anaelezeaje mwili ulivyo undwa?
Mwili wa waamini umeunganishwa, kwa pamoja, ili kwamba mwili wote ukue na kujijenga wenyewe katika upendo.
Ephesians 4:17-22
Paulo anasema mataifa wanatembeaje?
Mataifa wametiwa giza mawazo yao, wametengwa na Mungu, na kukabidhiwa katika matendo machafu.
Ephesians 4:23-24
Paulo anasema waamini wavae nini na wavue nini?
Waamini lazima wavue utu wa kale, na wavae utu upya.
Ephesians 4:25-27
Mwamini anawezaje kumpa shetani nafasi?
Mwamini anaweza kumpa shetani nafasi kwa kuruhusu jua lizame katika hasira yake.
Ephesians 4:28-30
Waamini wanaweza kufanya nini badala ya kuiba?
Waamini lazima wafanye kazi iliwaweze kushiriki pamoja na mwenye hitaji.
Kauli gani Paulo anasema itoke vinywani mwawaamini?
Kauli mbaya haipaswi kutoka kinywani mwamini, bali maneno yenye kujenga wengine.
Mwamini hapaswi kumuhuzunisha nani?
Mwamini hapaswi kumuhuzunisha Roho Mtakatifu.
Ephesians 4:31-32
Mwamini anapaswa kufanya nini sababu Mungu kupitia Kristo kamsamehe?
Mwamini lazima awasemehe wengine sababu Mungu kupitia Kristo kamsamehe.
Ephesians 5
Ephesians 5:1-2
Waaminio wanapaswa kumuiga nani?
Waaminio wanapaswa kumuiga Mungu Baba kama watoto wake
Ephesians 5:3-4
Nini ambacho lazima kisishuriwe kati ya waumini?
madili maovu kingono, uchafu, ulafi lazima usitajwe kati ya waumini.
Tabia gani ni ya kuonekana kwa waamini?
Waamini ni wakuonyesha tabia ya shukurani.
Ephesians 5:5-7
Nani asiye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu?
Asiye na maadili katika tendo la ndoa, mchafu, na mlafi hana urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.
Nini kinakuja kwa wana wa kuasi?
Hasira ya Mungu ya juu ya wana wa kuasi.
Ephesians 5:8-12
tunda gani la nuru la mpendeza Bwana?
Tunda la utu wema, haki, na kweli ya mpendeza Bwana.
Waamini watakiwa ku ya fanya nini matendo ya giza?
Waamini hawapaswi kushiriki, bali ku ya weka wazi.
Ephesians 5:13-14
Nini kilichofunuliwa na nuru?
Kila kitu kimefunuliwa na nuru.
Ephesians 5:15-17
Waamini wafanye nini kwa kuwa siku ni za uovu?
Waamini waokoe muda kwa kuwa siku ni za uovu.
Ephesians 5:18-21
Nini kinachopeleka kwenye uharibifu?
Kulewa kwa mvinyo kinapeleka kwenye uangamivu.
Kwa kipi waamini wazungume pamoja?
Waamini wazungumze kwa zaburi, sifa, na nyimbo za rohoni
Ephesians 5:22-24
Katika njia ipi wake wanapaswa kuwa watii kwa waume zao?
Wake wanapaswa kuwa watii kwa waume zao kama kwa Bwana.
Mume ni kichwa cha nani, na Kristo ni kichwa cha nani?
Mume ni kichwa cha mke, na Kristo ni kichwa cha kanisa.
Ephesians 5:25-27
Kristo analifanyaje kanisa kuwa takatifu?
Kristo analifanya kanisa kuwa takatifu kwa kuoshwa kwa maji katika neno.
Ephesians 5:28-30
Namna gani waume wapende wake zao?
Waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe.
Mtu anatendeaje mwili wake?
Mtu anautunza na kuupenda mwili wake.
Ephesians 5:31-33
Nini kinatokea mwanaume anaungana kwa mke wake?
Mwanaume anapoungana na mke wake wanakuwa mwili mmoja.
Ukweli upi uliyo sitirika waonyeshwa kwa kuungana kwa mwanaume na mke wake?
Ukweli uliyo sitirika kuhusu Kristo na Kanisa lake waonyeshwa kwa kuungana kwa mwanamume na mke wake.
Ephesians 6
Ephesians 6:1-3
Namna gani watoto wakristo wawatii wazazi wao?
Watoto wakristo wanapaswa kutii na kuwaheshimu wazazi wao.
Ephesians 6:4
Nini wafanye wababa wakristo kwa ajili ya watoto wao?
Wabab wakristo wanapaswa kuwalea watoto wao katika maonyo na maagizo ya Bwana.
Ephesians 6:5-8
Kwa Tabia zipi watumwa wakristo wanapaswa kuwatii mabwana zao?
Watumwa wakristo wanapaswa kuwatii mabwana zao kwa heshima na kwa miyo yao, na kuwahudumia kwa furaha kama kwa ajili ya Bwana.
Mwamini akumbuke nini kuhusu jema aliloli tenda?
Mwamini amini kuwa jema lolote alitendalo ataokea kutoka kwa Bwana thawabu.
Ephesians 6:9
Nini bwana mkubwa ambaye ni mkristo anapaswa kukumbuka kuhusu ubosi wake?
Bosi ambaye ni Mristo anapaswa kukumbuka kuwa yeye na mtumishi wa bwana wake yuko Mbinguni, na hakuna huruma kwake.
Ephesians 6:10-11
Kwa nini mwamini avae silaha zote za Mungu?
Mwamini lazima avae silaha zote za Mungu ili kukabiliana na hila za shetani.
Ephesians 6:12-13
Vita ya mkristo ni dhidi ya nani?
Vita vya mkiristo ni dhidi ya falme na mamlaka ya roho na watawala katika ulimwengu wa giza.
Ephesians 6:14-16
Kwa nini Mkristo lazima avae silaha zote za Mungu?
Mkristo lazima avae silaha zote za Mungu ili kusimama kinyume na mipango miouvo ya mwovu.
ni vitu gani zilizounganishwa katika silaha za Mungu?
Silaha za Mungu ni pamoja na mshipi wa kweli, drii ya haki kifuani, Viatu tayari kwa kutangaza Injili, ngao ya Imani, kofia ya wokovu, na upanga wa Roho.
Ephesians 6:17-18
Upanga wa Roho ni nini?
Upanga wa Roho ni neno la Mungu.
Ni vitu gani vilivyounganishwa katika silaha za Mungu?
Silaha za Mungu ni pamoja na mshipi wa kweli, drii ya haki kifuani, viatu tayari kwa kutangaza injili, ngao ya Imani, kofia ya wokovu, na upanga wa Roho.
Ephesians 6:19-22
Paulo alikuwa alitaka kupata nini kupitia maombi ya waefeso?
Paulo alitaka kuwa na neno alilopewa kwa ujasiri wakati anahubiri njili.
Paulo yako wapi akiandika hii barua?
Paulo yupo gerezani akiandika hii barua.
Ephesians 6:23-24
Mambo gani matatu Paulo anaomba Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo awape waamini?
Paulo anaomba Mungu awape amani, upendo, na imani, na neema kwa waamini.